Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

NEWS ALERT: BANZA STONE AFARIKI DUNIA MCHANA HUU

$
0
0
Taarifa iliyotufikia chumba cha habari cha Globu ya Jamii hivi punde, inaeleza kuwa Mwanamuziki wa siku nyingi wa Muziki wa Dansi hapa nchini, Ramadhan Masanja "Banza Stone" amefariki dunia mchana huu nyumbani kwao Sinza karibu na Lion Hotel jijini Dar es salaam.

TAARIFA ZAIDI ZITAWAJIA BAADAE KIDOGO.

Chato, Biharamulo kupata umeme wa uhakika kuanzia Jumapili

$
0
0
Na Teresia Mhagama Imeelezwa kuwa Wilaya za Chato na Biharamulo zitaanza tena kupata umeme wa uhakika ifikapo Jumapili ya tarehe 19 Julai, 2015 baada ya kukamilika kwa ukarabati wa mtambo wa umeme wa kilowati 650 unaohudumia wilaya hizo. 
 Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Kagera na kujionea maendeleo ya ufungaji wa mtambo huo wa pili uliofungwa wilayani Biharamulo ambao ulianza kufanya kazi mwanzoni mwa mwezi Juni mwaka huu. 
Mwijage amesema kuwa mtambo huo ulipata hitilafu ambapo kifaa kijulikanacho kama crankshaft kilikatika hivyo wataalam kutoka Shirika la Umeme nchini (TANESCO) wanaendelea kufunga crankshaft nyingine ambayo imetolewa katika mtambo wa umeme ulioko mkoani Kigoma ambao hautumiki kwa sasa. 
Alisema kuwa mtambo huo wa kilowati 650 umeongeza kiasi cha umeme uliokuwa ukipatikana katika wilaya hizo mbili hivyo hivi sasa upo uhakika wa upatikanaji wa umeme wa kutosha tofauti na ilivyokuwa hapo awali. 
"Tuliamua kuongeza mtambo wa pili kwa kuwa ule wa kwanza ulikuwa haukidhi mahitaji ya wakazi wa wilaya hizi mbili na hii ni kwa sababu mtambo huo ulikuwa ukizalisha umeme wa kiasi cha kilowati 800 wakati mahitaji ya umeme katika wilaya hizi ni kilowati 1300," alisema Mwijage. 
Alieleza kuwa kukamilika kwa mtambo huo wa kilowati 650 kumezifanya wilaya hizo kuwa na umeme wa kiasi cha kilowati 1450 na hivyo kuwa na ziada ya umeme wa kiasi cha kilowati 150. 
Alisema kuwa awali mtambo huo wa kilowati 650 uliofungwa katika wilaya ya Biharamulo, ulikuwa ukitumika mkoani Kigoma na uamuzi wa kuupeleka mtambo husika wilayani Biharamulo ulifanyika baada ya mkoa wa Kigoma kupata mitambo mipya ya uzalishaji umeme. 
“Baada ya kuuleta mtambo huu wilayani Biharamulo, Serikali ilinunua baadhi ya vipuri vipya kwani vile vya awali vilichakaa na kusababisha mtambo huu kutokufanya kazi kwa ufanisi. Wataalam wetu wa TANESCO walibadilisha vifaa chakavu na kufunga vifaa vipya ili mtambo huu uanze kuhudumia wilaya hizi mbili,” alisema Mwijage.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa kwanza kushoto) akizungumza na  na wataalam kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)  ambao wanakarabati  kifaa kilichopata hitilafu (crankshaft) katika mtambo wa kuzalisha umeme wa kilowati 650  uliofungwa wilayani Bharamulo ambao unatarajia kuanza tena kuzalisha umeme siku ya Jumapili.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa kwanza kushoto)  akiangalia housing  ya kifaa kilichopata hitilafu (crankshaft) katika mtambo wa kuzalisha umeme wa kilowati 650 uliofungwa wilayani Bharamulo ambao unatarajia kuanza tena kuzalisha umeme siku ya Jumapili. Anayetoa maelezo ni  mtaalam kutoka Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Mhandisi John Magembe.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (katikati)  akiweka saini katika Kitabu cha Wageni mara baada ya kufika katika Ofisi za  Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wilayani Biharamulo kukagua maendeleo ya ukarabati wa   kifaa kilichopata hitilafu (crankshaft) katika mtambo wa kuzalisha umeme wa kilowati 650  uliofungwa wilayani Bharamulo ambao unatarajia kuanza tena kuzalisha umeme siku ya Jumapili.

Haji Sunday Manara amlilia Rafiki yake Ramadhani Masanja Banza Stone

$
0
0


Oooh Rama Mate...! Nilipenda kumwita hvyo. Ni kijana wa mjini hasa. ilianza nae standard one shule ya msingi darasa moja pale Mnazi Mmoja Primary school  iliyopo mkabala na iliopozaliwa TANU (ofisi ndogo ya CCM ) New street (Lumumba) na tulikuwa sote kwa miaka miwili kabla ya wazazi kunihamishia Bunge Orimary iliopo Ohio street mkabala na ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa miaka hiyo tulikuwa na uswahiba mkubwa wa kitoto. Nikikumbuka halftime mbio zetu kwenda kwa muuza mihogo mkongwe Mzee Said na kuisukumizia na juice yake tamu ya ukwaju. 
Kipindi hcho kila tupatapo upenyo wa mapumziko, tofauti na watoto wengi wa zama zile kupenda kucheza soka. kutwa Mate alikuwa anapenda kupiga ngoma zilizokuwa ndani ya hall la shule hyo maarufu jijini. 
Sikuwa najua kuwa ndio kipaji chake. Ila kiukweli Mate alikuja kuwa mwanamuziki maarufu sana nchini na katika  moja ya tungo zake maridhawa ni wimbo wa "Mtaji wa masikini" na ule wimbo wa "Aungurumapo simba" ambao kwa miaka mingi sasa umekuwa kama wimbo rasmi wa klabu kubwa kabisa Tanzania Simba SC. 
Mate alinizidi kidogo umri,  hvyo shule alikuwa ananikingia kifua na watoto watundu waliojaribu hata kunigusa na hakuacha kunitania tulipokuwa tukikutana enzi za ukubwani. Alikuwa haishi kunitambia kuwa yeye ni mbabe wangu na mimi  nikimwambia ilikuwa lazma unilinde kwa kuwa shule ulikuwa unaniigizia.
Kwa kweli utani ndio maongezi yaliyotawala pindi tulipokuwa tukikutana. Naandika ujumbe huu huku nikijikaza kudondosha chozi langu. Ninajua Mate...namna ulivyopigania uhai wako. Walimwengu nao hawakuacha kukuzushia kifo. Ila muumba aliamua kwa makusudi yake akuchukue leo ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kama lilivyo jina lako!
Umeacha alama Mate. Na wimbo wa "Aunguramapo Simba" naona ipo haja ya kuutukuza, hasa  hasa siku ya Simba gala mwanzoni mwa mwezi ujao. Nisiandike sana maana najijua nilivyo na uswahiba na machozi kama nilivyokuwa na uswahiba na wewe Mate. 
Kapumzike kaka 
 Inna lillah wa inna ilaihi raajiun...
Ni mimi nduguyo, rafikiyo, classmate wako
Haji Sunday Manara

UP DATES: MAREHEMU BANZA STONE KUZIKWA KESHO SAA 10 JIONI MAKABURI YA SINZA

$
0
0
 Baadhi ya ndugu na jamaa wa Marehemu Ramadhan Massanja "Banza Stone" wakijadiliana jambo mchana huu, nyumbani kwao Sinza Lion, Jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa kaka wa Marehemu, Hamisi Masanja, Banza Stone atazikwa kesho saa kumi jioni katika makaburi ya Sinza jijini Dar es salaam. Mola aiweke mahali pema roho ya marehemu - AMINA.

Mawasiliano yakiendelea kupeana taarifa na ndugu wengine.

Amini Salimini Amour Awania Ubunge Jimbo la Mkwajuni Zanzibar Kupitia Tiketi ya CCM

$
0
0
Mtoto wa Komando Dk Salmin Amour Juma Amini Salimini achukua Fomu kugombea Jimbo la Mkwajuni Zanzibar akiwasili katika Ofisi za CCM Wilaya ya Kaskazini A Gamba kwa ajili ya kuchukua Fomu kogombea Jimbo hilo, akisalimiana na Wananchi waliopo hapo. 
Mama wa Amini Salimi Bi Khadija Kasimi akisalimiana na Katibu Msaidi wa Ofisi ya CCM Wilaya Kaskazini A Unguja alipofika katika Ofisi hizo kumshindikiza Mtoto wake kuchukua Fomu ya Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni Zanzibar. 
Katibu Msaidizi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Kaskazini Unguja Ndg Shafi Hamad akitowa maelezo kwa Mgombea kabla ya kumkabidhi fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Jimbo la Mkwajuni
Katibu Msaidi Ofisi ya CCM Wilaya ya Kaskazini a Unguja Ndg Shafi Hamad akimkabidhi Fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Mkwajuni Amini Salimini, baada ya kukamilisha taratibu zote za malipo na kutimiza masharti ya Chama cha Mapinduzi. Picha zaidi BOFYA HAPA

Tabora Stand Up; Eid Mosi Wasanii Wafurika Hapatoshi

$
0
0
Shangwe na burudani za kutosha zinatarajiwa kufanyika katika sikukuu ya Eid hapo kesho mkoani Tabora panapo majaaliwa ya Mwenyezi Mungu. Mashabiki  mjini Tabora watarajiwa kufurahia onesho hilo katika maeneo mawili tofauti ambapo mchana itakuwa Bwalo la Polisi kuanzia saa 8 mchana na Usiku katika viwanja vya Muungano Mesi kuanzia saa 2 usiku.
Wasanii wa kila nyanja wametua mjini hapo na kufanya mahojiano CG Fm Redio leo mchana; wasanii hao ni Kassim Mganga a.k.a tajiri wa mahaba, Ommy Dimpoz, Mkude Simba (Kitale) na rafiki yake Stan Bakora, Young Killer, na Baraka Da Prince.
Eid_Tabora (8)
Kassim Mganga akiwa CG Fm Redio, 89.5 The point of no Return
Eid_Tabora (11)
Ommy Dimpoz

DIASPORA CONFERENCE TO BE HELD IN DAR ES SALAAM NEXT MONTH

Vijana wazidi kuchukua fomu za Ubunge, sasa ni Dkt. Walter Nnko

$
0
0
JOTO la Uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, limepanda kwa kila rika la wazee, vijana , na akina mama, ambapo kila mmoja amekuwa anatazama Jimbo la kugombea kupitia chama anachokiamini katika ngazi ya Udiwani na Ubunge. Walter Nnko ni Daktari mzalendo na kamanda wa vijana kondo/kunduchi.

 Dr. Walter Nnko amechukuwa fomu ya ubunge jimbo la kawe na muda ukifika atawaomba wanachama wa CCM wampe ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi utakaofanyika mwezi wa kumi MWAKA huu. 

Anaamini kuwa amesheheni majawabu ya kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Kawe. Akizungumza nasi Jumatano amesema, ni wakati wa vijana wasomi kuonyesha elimu zao kwa vitendo, na kurejesha faida ya fedha za umma zilizowasomesha wakiwa vyuoni kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo. "Nataka nilipe fadhila za wananchi wa Jimbo la KAWE kwa kuwatumikia kuyafikia maendeleo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)" amesema Dk.Nnko.

 Anabainisha kuwa kiu yake ni kuhakikisha wananchi wa Jimbo la KAWE wanapata huduma nzuri za afya, elimu bora, ajira na bila kusahau miundo mbinu. "Naheshimu kampeni ya Mwenyekiti wa taifa wa chama chetu ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuamsha ari ya kuboresha elimu ya sekondari kwa kuhakikisha maabara zinajengwa" anasema Nnko. 

Anasema endapo atapata nafasi hiyo ya kupeperusha bendera ya CCM katika jimbo ilo atahakikisha anafanya mbinu zote kuongeza shule za kata, zahanati kwenye kila kata, atasimamia ujenzi unaoendelea wa Hospitali ya rufaa inayojengwa mji mpya, kata ya Mabwepande ili kuhakikisha jimbo la Kawe lina huduma nzuri za afya, kupata vifaa vya maabara na kujenga maabara za kutosha, anadai kuwa majengo bila vifaa yanapoteza maana.

Washindi wa Kopa Bayport wakabidhiwa fedha zao

$
0
0
Meneja wa Bayport Mkoani Lindi, Jovin Mapunda, kulia, akimkabidhi kiasi cha Shilingi Milioni moja mshindi wa Kopa Bayport, Said Mkinda, katika droo iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Fedha hizo alikabidhiwa juzi. Jovin Mapunda. Picha zote kwa hisani ya Bayport Financial Services.

Washindi wanne wa Kopa Bayport wakabidhiwa fedha zao
Na Mwandishi Wetu, Dar es SalaamWATEJA wanne wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, walioshinda Sh Milioni Moja kila mmoja katika bahati nasibu ya Kopa Bayport, wataisherehekea vizuri Sikukuu ya Eid el Fitr, baada ya kukabidhiwa fedha zao jana. Wateja hao ambao ni Simion Ngassa (Iringa), Sisco Haule (Kigoma), Phelis Nziku (Arusha) na Said Mkinda (Lindi), ambao washindi wote hawa walikabidhiwa fedha zao kwa kupitia Ofisi za Mkoa za Taasisi ya Bayport zilizoenea nchi nzima.
Mteja wa Bayport Phelis Nziku wa Arusha kushoto akikabidhiwa kiasi cha Sh Milioni moja baada ya kushinda bahati nasibu ya Kopa Bayport.

Akizungumzia hatua ya makabidhiano hayo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkuu wa Mauzo wa Bayport Financial Services, Charles Mgeta, alisema kwamba ni furaha yao kuona washindi wao wote wamepata haki zao kutokana na kushinda kwenye shindano la Kopa Bayport.
Mteja wa Bayport akipewa fedha zake
Alisema wanaamini wateja hao wataendelea kufurahia huduma za Bayport zinazotoa picha halisi ya namna gani taasisi yao ina lengo la kuwakomboa na kuwakwamua pia kwa kutoa huduma bora kwa ajili ya maendeleo ya watanzania wote. “Kama tulivyotangaza hapo awali kwamba tulikuwa na washindi wanne waliokopa Bayport na kushinda Sh Milioni Moja kila mmoja, hivyo tumekabidhi kwa kupitia mameneja watu katika maeneo waliyoshinda wateja hawa.

“Tunawaomba wateja wetu na Watanzania kwa ujumla kuendelea kutuunga mkono ili tuwapatie huduma bora kama vile mikopo ya bidhaa, mikopo ya fedha taslimu bila kusahau Bima ya Elimu kwa Uwapendao, huku huduma ya ukopaji kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz ukiwarahishia wateja wetu kukopa kwa njia ya haraka popote walipokuwapo,” alisema Mgeta.

Kwa mujibu wa Mgeta, promosheni ya Kopa Bayport imeanzishwa kwa lengo la kuwashukuru wote wanaokopa kwenye taasisi yao, huku wahusika wakuu wakiwa ni wale wanaokopa kwenye taasisi yao inayoongoza kwa huduma bora za kifedha.%

MKONO WA IDDI TOKA KWA AFANDE MSANGI RPC WA MBEYA

$
0
0
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED ZAHORO MSANGI ANAWATAKIA EID MUBARAK WAANDISHI WOTE WA HABARI WA NDANI NA NJE YA MKOA WA MBEYA.
 PIA WA VYOMBO MBALIMBALI KAMA VILE REDIO, TELEVISHENI, MAGAZETI, BLOGS NA MITANDAO MINGINE YA KIJAMII.
WITO: TUSHEREHEKEE KWA AMANI NA UTULIVU BILA KUWEPO NA HALI/VIASHIRIA VYOVYOTE VYA UVUNJIFU WA AMANI
MBEYA BILA UHALIFU INAWEZEKANA, ULINZI NA USALAMA UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE!
"EID MUBARAK"

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 17/07/2015

AMON MPANJU AJITOSA KUGOMBEA JIMBO LA KAWE

$
0
0
Mwenyekiti  wa Shirikisho la vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Amon Anastaz Mpanju ambaye pia alikuwa Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba Mpya amejitokeza hii leo sambamba na wana CCM wengine katika safari ya kuwania Ubunge katika Jimbo la Kawe Wilaya ya Kinondoni.
Akizungumza na Father Kidevu Blog, katika ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni, Mpanju amesema huu ni wakati muafa kwake kuwatumiakia wana Kawe.
Mpanju ambaye kitaaluma ni Mwanasheria, amesema wanakawe wananafasi sasa ya kuandika historia  ya aina yake si tu kumchagua mtu mlemavu bali kumchagua, kijana na mchapakazi mwenye uwezo wa kutetea na kuwasilisha hoja za kuleta maslahi kwa kawe na taifa.

“Huu ni wakati wa wananchi wa Kawe kuandika historia ya aina yake, sit u kwa kumchagua mtu mwenye ulemavu kuwaongoza bali kijana mwenye uwezo wa kutetea hoja na maslahi yua wananchi na taifa kwa ujumla,”alisema Mpanju.

Mpanju amekuwa ni mwananchi wa 16 kujitokeza kugombea jimbo la Kawe na ni mwana CCM wa 39 kujitokeza kuomba ridhaa ya chama kuteuliwa kugombea Ubunge kwa tiketi ya chama hicho.

Mwenyekiti wa wa Shirikisho la vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Amon Mpanju akizungumza na wanahabari . Kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe.
 Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe akimsaidia kutia saini ya dole gumba Mpanji.
Mwenyekiti wa wa Shirikisho la vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Amon Mpanju akipokea fomu kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe, kwaajili ya  kuomba ridhaa ya wana CCM Kinondoni kumteua kugombea Ubunge Jimbo la Uchaguzi la Kawe katika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.
Nae Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athumani Sheshe (pichani), amempongeza Mpanju kwa uamuzi wake huo na kusema kuwa anatekeleza moja ya kanuzi na sheria za Chama kuwa watu wote ni sawa na walemavu wanahaki ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa vipongozi.

“Mimi nitoe wito kwa watu wote wenye ulemavu nchini ambao wanasifa na vigezo vinavyotakikana kugombea nafasi mbalimbali za uongozi nchini wajitokeze na kufanya hivyo na watatendewa sawa sawa na wengine bila ubaguzi au unyanyapaa,”alisema Sheshe.

Elimu ya utambuzi wa fursa kwa vijana inahitajika - Ridhiwani Kikwete

$
0
0


Ridhiwani Kikiwete wakati wa mahojiano na Joseph Msami.(Picha:UM/Idhaa ya Kiswahili)
Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya ujuzi kwa vijana inashangaza kuona kuwa baadhi ya vijana wanajishughulisha katika kujikwamua kiuchumi lakini wengi hawafahamu  kuhusu malengo ya maendelo ya milenia amesema mbunge kijana kutoka Tanzania Mhe. Ridhiwani Kikwete.
Katika mahojiano na Joseph Msami alipotembelea makao makuu ya Umoja wa Mataifa hivi karibuni, mbunge huyo wa Chalinze mkoani Pwani anasema licha ya fursa lukuki za kimaendeleo ajira ni changamoto kubwa kwa vijana katika  nchi zinazoendelea.
(SAUTI MAHOJIANO)
KUSIKILIZA BONYEZA HAPA

2015 Eid Greetings from CRDB BANK

Steven Nyerere achukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la kinondoni na kurudisha leo

$
0
0
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni, Athumani Sheshe, akimkabidhi fomu ya kugombea ubunge jimbo la Kinondoni, Muigizaji, Steven Mengere (kulia) katika ofisi za chama hizo eneo la Mkwajuni, Jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni mke wa mgombea Dk. Sarah Makene. Picha na Elisa Shunda
Muigizaji, Steven Mengere, akionyesha fomu ya kugombea ubunge jimbo la kinondoni kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kukabidhiwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni, Athumani Sheshe (kushoto) katika ofisi za chama hicho zilizopo eneo la Mkwajuni, jijini Dar es Salaam jana. 
akiwa kwenye picha ya pamoja na wasanii wa filamu nchini na baadhi ya ndugu zake baada ya kurudisha fomu ya kugombesa ubunge jimbo la kinondoni

MKUU WA MKOA WA MTWARA AFUNGUA MKUTANO WA MAENDELEO YA MISITU

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Halima Dendego akizungumza wakati wa uzinduzi wa mkutano wa nne wa wadau wa sekta ya misitu unaolenga kuangazia masuala ya usimamizi shirikishi ya misitu vijijini ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI mjini Mtwara. Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Fatma Ally, Kaimu Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki Bi. Gladness Mkamba na Mkuu wa Utafiti na Sera wa Taasisi ya UONGOZI Bw. Denis Rweyemamu.
Kaimu Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki Bi. Gladness Mkamba akitoa mada kuhusu hali ya utunzwaji wa misitu wakati wa mkutano wa nne wa wadau wa sekta ya misitu unaolenga kuangazia masuala ya usimamizi wa shirikishi ya misitu vijijini ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI mjini Mtwara.
Mkuu wa Idara ya Utafiti na Sera wa Taasisi ya UONGOZI Institute Bw. Denis Rweyemamu akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliolenga kuunganisha wadau mbali mbali wa sekta ya misitu ili kuweza kuzungumzia changamoto na fursa zilizopo katika masuala ya usimamizi wa misitu vijijini kupitia vikundi shirikishi vya kijamii.
Viongozi wa serikali wakiwa na wadau mbali mbali wa sekta ya misitu katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa mkutano wa nne wa wadau wa sekta ya misitu uliolenga kuangazia masuala ya usimamizi shirikishi ya misitu vijijini ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI mjini Mtwara.

KWETU HOUSE 2015 MSIMU WA PILI YATUA JIJINI MWANZA KUSAKA VIPAJI KWA MASHABIKI WA SOKA, MSHINDI KULAMBA MILIONI 15

$
0
0
Msimu wa pili wa Kwetu House - “kwetu house, kipaji zaidi ya soka” hili shindano ambalo hujumuisha zaidi wapenzi wa soka wenye Kipaji, jumla ya mikoa mitano (Arusha, Zanzibar, Dodoma, Mbeya na Mwanza) kutoa washiriki zaidi kwa ajili ya kunogesha na kuleta upinzani wa kutosha msimu huu mshindi ataondoka na kitita cha shilingi milioni 15, tofauti na msimu uliopita ambao ilikuwa Sh milioni 10.

Baada ya Kwetu House kusaka Shabiki mwenye Kipaji Kwenye Mikoa ya Arusha, Zanzibar,Dodoma na Mbeya sasa ni zamu ya ROCK CITY *Mwanza kwa Mashabiki wote wa Soka wenye Vipaji tofauti (Mwimbaji,Mchekeshaji,mbunifu wa mavazi,mchoraji n.k) kuonyesha vipaji vyao na hatimye Kupata washiriki watakao iwakilisha Jiji la Mbeya kwenye Jumba la (Kwetu House ) jumla ya washiriki 20 kutoka Mikoa Mitano kukaa kwenye Nyumba ya Kwetu House
Team ya Kwetu House 2015 Msimu wa Pili wakiwa Studio za Jembe FM 93.7 Mwanza Mara Baada ya Mahojiano kuhusiana na KWETU HOUSE 2015 Kwa Jiji la Mwanza.
Mkuu wa Channels Azam TV Madam Stellah Adam akizungumzia KWETU HOUSE 2015 kwa Mwaka huu ambapo Kauli mbiu ni "Kipaji na Soka" Stellah aliongezea Zawadi ya Mshindi wa Mwaka huu imeongezeka kutoka milioni 10 Msimu uliopita Hadi Milioni 15 Kwa Msimu huu wa Pili.

Coastal Union kukipiga na Friends Corner kesho Iddi Pili

$
0
0
MABINGWA wa Ligi kuu soka Tanzania bara mwaka 1988 Coastal Union ya Tanga kesho Iddi Pili inatarajia kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Friends Corner ikiwa ni maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa Ligi kuu soka Tanzania bara.

Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa Iddi Pili kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani ikiwa ni muendelezo wa mechi za kujipima nguvu kwa ajili ya kukiimarisha kikosi hicho kwa ajili ya mashindano ya Ligi kuu yajayo.

Maandalizi ya kuelekea mechi hiyo yamekamilika kwa asilimia kubwa na hivyo Friends Corner watatua mkoani siku hiyo hiyo ya mchezo huo tayari kwa ajili ya mchezo huo.

Taarifa inaeleza baada ya kumalizika mechi hiyo tutaangalie uwezekano wa kucheza mechi nyengine za majaribio ili kuweza kukipa makali kikosi cha timu hiyo ambacho msimu ujao kimedhamiria kuleta mapinduzi kwenye michuano hiyo.

Na mtambue kuwa dhamira ya timu yetu ni kuhakikisha inafanya maandalizi kabambe ili kuweza kurejesha heshima yao ya miaka ya nyuma walipochukua ubingwa wa ligi kuu.

Hata hivyo tunawataka wanachama, wapenzi na mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye mechi hiyo ili kuweza kuona viwango vya wachezaji wapya waliosajiliwa kabla ya kuanza msimu mpya wa Ligi kuu.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Coastal Union.
OSCAR ASSENGA.

DIAMOND PLATNUMZ KUINOGESHA MISS KILIMANJARO AMBASSADOR 2015

MAELFU WAJITOKEZA KUMLAKI KWA SHANGWE DKT MAGUFULI JIJINI MWANZA LEO.

Viewing all 109996 articles
Browse latest View live


Latest Images