Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 89 | 90 | (Page 91) | 92 | 93 | .... | 3284 | newer

  0 0


  Mtuhumiwa namba moja wa mashitaka 24 ya kuua bila kukusudia Raza Hussein Ladha (kushoto) akiwa chini ya ulinzi wakati alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam pamoja na watuhumiwa wenzake kumi. Mtuhumiwa namba moja wa mashitaka 24 ya kuua bila kukusudia Raza Hussein Ladha (kulia) na watuhumiwa wenzake kumi wakisubiri kupandishwa kizimbani, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es SalaamMtuhumiwa namba moja wa mashitaka 24 ya kuua bila kukusudia Raza Hussein Ladha (aliyevaa kanzu nyuma) akiwa na watuhumiwa wenzake mara baada ya kupandishwa kizimbani na watuhumiwa wenzake kumi, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.  Picha na Francis Dande


   Mfanyabiashara Radha Hussein Ladha wa jijini Dar es Salaam, Diwani katika Manispaa ya Kinondoni, Ibrahim Mohamed maarufu kama Kisoki (59) na wenzao 9, jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 24 ya kuua bila ya kukusudia.
  Katika kundi hilo pia wamo wafanyakazi wa Manispaa ya Ilala ambao ni Mhandisi Mkuu, Mhandisi Charles Salu (48), Mhandisi wa Majengo Godluck Sylivester (35) Mbaga na Mkurugenzi Mkuu wa Mkaguzi wa Majengo, Willibrod Wilbard (42).
  Washtakiwa wengine ni Mhandisi Mohamed Swaburi (61), Mhandisi Mshauri, Zonazea Oushoudada (60), Mkadiriaji Majenzi, Vedasto Nziko (59), Msanifu Majengo, Michael Hema (59), Msajili Msaidizi AQRB, Albert Mnuo na Ofisa Mkuu Mtekelezaji OQRB, Joseph Ringo.
  Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi, Devotha Kisoka, Wakili wa Serikali, Tumain Kweka akisaidiana na mawakili wenzake watano, alidai kuwa washtakiwa walifanya makosa kinyume na kifungu cha 195 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho 2002.
  Kweka anasadiana na wenzake Benard Kongora, Ladslaus Komanya, Neema Haule, Joseph Maugo na Mutalemwa Kishenyi.Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao kwa pamoja Machi 29, mwaka huu katika Mtaa wa Indira Gandhi, Wilaya ya Ilala waliwaua bila ya kukusudia Yusuph Mohamed, Kulwa Khalfan na Hamada Mussa.
  Mbali na watu hao, pia wanadaiwa kuwaua bila ya kukusudia Kessy Manjapa, Khamis Mkomwa, Boniface Benard, Suhail Ally, Salmani Akbar, Seleman Haji, Seleman Mtego, Sikudhani Mohamed, Ahmed Milambo, Salum Mapunda, Suleiman Rashid na John Majewa.
  Wengine ni Mussa Mnyamani, David Severin Herman, William Joackim, Abdulrahman Mwiha, Emmanuel Christian, Mmanyi Ngadula, Adivai Desiki, Emmanuel Greyson na Augustino Kasiri.
  Washtakiwa wote hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mashtaka yanayowakabili Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza hadi Mahakama Kuu.
  Mawakili wa utetezi wakiongozwa na Wakili wa Kujitegemea, Jerome Msemwa waliiomba mahakama kutoa dhamana kwa wateja wao kwa sababu mashtaka ya kuua bila ya kukusudia yanayowakabili yanadhaminika.
  Wakili wa Serikali, Kongora alipinga maombi hayo, huku wakili mwenzake Komanya akisema kuwa wakati huu si wa kutoa dhamana kwa kuzingatia mazingira ya tukio lililosababisha kuwepo kwa kesi hiyo.
  Kutokana na hoja hizo, Hakimu Kisoka aliiahirisha kesi hiyo hadi Aprili 16, mwaka huu atakapotoa uamuzi iwapo washtakiwa wapate dhamana ama la.

  0 0
 • 04/03/13--23:15: TAARIFA YA MSIBA

 • MDAU Said Mdoe amefiwana dada yao kipenzi Fatma Mdoe (pichani) aliyefariki ghafla jana (Jumatano) saa 10 jioni. Msiba uko nyumbani kwa marehemu Mbezi Beach, Dar es salaam, jirani na Dr Hizza.

  Mazishini yatakuwa leo Alhamisi saa 10 Alasiri katika makaburi ya Kisutu, jijini Dar es salaam.  Msafara wa kutoka Mbezi kuelekea makaburini utaanza saa 8.30 mchana ili kukabiliana na adha ya foleni.

  Mungu amlaze mahali pema Peponi
  AMINA.
   

  0 0  0 0

  Mabondia Issa Omar na Shaban Madilu ambao wanacheza pambano lao la raundi kumi ubingwa wa UBO international, wakisindikizwa na wakongwe wa masumbwi nchini Joseph Marwa atakaezipiga na amour mzungu katika pambano la kisasi ,baada ya mzungu kupigwa na marwa miaka saba iliyopita jumapili hii ndani ya ccm mwinjuma anataka ajiulize ilikuwaje na amepata uzoefu wa kutosha wa kulipa kisasi.

  Mabondia wote hao pamoja na uzito wa juu Ramadhan kido na musa mbabe wanategemea kupima afya zao na uzito siku ya jumamosi saa nne asubui hapohapo ukumbini CCM Mwinjuma – mwananyamala zoezi zima la upimaji litaongozwa na dr donard Madono akisaidiwa na Emanuel mlundwa.

  Mpambano huo ulioandaliwa na bigright promotion na kusimamiwa na PST kama mwakilishi wa UBO nchini unategemea kuwakutanisha mabondia mbalimbali wenye uwezo mzuri na kuwavutia washabiki wa mchezo huo kwa kushuhudia mapambano zaidi ya tisa kwa wakati mmoja na mabondia wanaotegemea kupima siku ya jumamosi ni Ide mnali toka mtwara atakaezipiga na zumba kukwe wa dare s salaam, Husein Mbonde atazipiga na mwaite juma,Martin Richard atapigana na Faraji Sayuni, Salum Chandonga atazipiga na mdogo wake amour mzungu ,Mohamed mzungu. Herman Richard na kade hamis, kani west na Nasor Hatibu,james Edmond na julias anastaz .pia kutakuwa na maonesho ya ngumi za watoto wenye vipaji.

  Mpaka leo hii haijaripotiwa kama kuna tatizo lolote na mabondia karibu wote wapo katika hali nzuri na wapo tayari kwa mpambano

  0 0

  Kijiji cha Ndulamo wilayani Makete kimepewa mradi feki wa maji,ambapo mabomba mapya ya maji hayo yamefunguliwa muda mchache baada ya kuwekwa lakini yote yamefumuka kwa wakati mmoja na kuvijisha maji kama ionekanavyo pichani hapa, uchunguzi nilioufanya umebaiini kuwa mabomba hayo ni feki,yaliyo chini ya kiwango na hayana uwezo wa kupitisha maji mengi na yenye presha kubwa,hadi hivi sasa kijiji hakina maji kwa sababu yamefungwa kwenye chanzo.Mamlaka ya maji inatakiwa kulifuatilia swala hili kwa ukaribu na kufanikisha kutatua tatizo la Maji kijijini hapa.Picha na Edwin Moshi wa Globu ya Jamii,Makete.

  0 0
 • 04/04/13--00:40: daladala limenasa
 • Vijana wakichimba udongo wakati wakijaribu kuliondoa daladala linalofanya safari zake kati ya Ubungo na Kariakoo lililonasa kwenye matope viwanja vya Jangwani Dar es Salaam.

  0 0  Wanawake na wasichana wa Dar es salaam na mikoa ya jirani Kitchen party gala ipo on tayari.

  Mwaka jana ile ya mwisho ya mwezi wa kumi tulifanyia Diamond jubelee VIP hall na ukumbi ulishona sana sana.Kulikuwa na mapungufu kadhaa ambayo sitapenda yajirudie
   this time.Najua ni mara chache shughuli kukosa upungufu fulani lakini kulirudia kosa ndio kosa zaidi.

  Sasa mwaka huu tumepata ukumbi mpya kabisa upo ndani ya jengo la GOLDEN JUBELEE.Hili jengo ni jipya lipo pembeni ya jengo la PPF Tower mjini kabisaaa.

  Ukumbi huo unaingiza watu 1000 tu na ndio idadi tunayoitaka siku hiyo.
  Service zao ni za kihoteli kabisa na wao ndio wataserve kila kitu.Ukumbi huu uko chini ya JB Belmonte hotel hivyo wao ndio watatoa huduma za chakula.Chakula chetu kitakuwa kwenye hadhi ya starter,main course na desert.
  Hivyo tumeona tuadvance ili kukidhi mahitaji yako ya kihuduma,mazungumzo yetu ya siku hiyo na burudani.

  Na kwasababu tumeadvance kihuduma na shughuli kwa ujumla  kiingilio chetu this time kitapanda kitakuwa Tsh 40,000/= Ukumbi una vyoo vingi vipya na visafi na wa hadhi ya kimataifa.Pia najua kina mama ndio waandaaji wa shughuli mbalimbali za kifamilia,marafiki,ukoo mje muone ukumbi huu mpya.Hawa wana kumbi 4 katika jengo hili hili.Unaoingiza watu 1000,600,400 na 150 mkuje muone maana tunapata taabu sana ya kumbi  hasa kama unataka maeneo ya town.
  Tutakuwa na wasemaji wa ndani na nje ya Tanzania.
  DRESS CODE:Tusisahau dress code yetu ya siku hiyo imekuwa inspired na bendera ya nchi yetuTanzania.

  TAREHE:Kparty gala itakuwa jumamosi ya tarehe 27 april 2013.Kuanzia saa tano asubuhi mpaka kumi na mbili jioni.
   Kwa lolote piga namba hii 0787583132 na 0657442255.

  ASANTENI

  Ognaniser
  Dina Marios
  !

  0 0
 • 04/04/13--00:56: NYUMBA / KIWANJA KINAUZWA
 • Nyumba iko Mwananyamala "B" inatazamana kabisa na ofisi ya Posta. Bei: 
  Shilingi za kitanzania Milioni mia moja na Themanin(180,000,000/= ). Kwa maelewano zaidi tafadhali wasiliana na Ndugu Ramadhani Said Sululu kwa namba 0754-380571. Au 0715-380571 Au 0783-380571. 

  Karibuni sana.


  0 0


  0 0

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayofanya kazi pamoja na kampuni ya Samsung zimesaini makubaliano ya kushirikiana kudhamini mashindano makubwa Afrika kwa vijana wa chini ya miaka 17. 

  Katika mkataba huo wa mamilioni ya dola, Samsung pia itakuwa mtoaji rasmi wa vifaa vya mawasiliano kwenye mpango huo wa mashindano maarufu kama Airtel Raising Star (ARS) unaoendeshwa na Airtel. 

  Airtel inatoa huduma za mawasiliano kwa simu za mkononi kwenye nchi 20 barani Asia na Africa huku Samsung ikiwa ni miongoni mwa makampuni makubwa ya vifaa vya kisasa vya elektoniki. 

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam leo, Airtel imefanya kazi kwa karibu sana na taasisi za elimu kwenye nchi 17 zinazozungumza Kiingereza na Kifaransa ambapo kwa kupitia mashindano hayo ya soka ya Airtel Rising Stars yamefanikiwa kushirikisha zaidi ya timu 18,000. ambapo vijana wa kike na wa kiume wapatao 400,000 barani Afrika walishiriki katika mashindano hayo ya Airtel Rising Star. 

   Mwaka jana mashindano haya ya Airtel Rising Stars yalionekana kukua kwa asiliamia 65 na kuna kila dalili kwa mwaka huu kukua zaidi,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa na Airtel Makao Makuu. 

  Mkakati huo wa kukuza soka barani Afrika unaungwa mkono kwa dhati na klabu kubwa za England; Arsenal FC na Manchester United ukiwa na lengo la kuibua na kukuza vipaji vipya vya vijana wa Kiafrika. “ARS imefikia kuwa chanzo kizuri cha wachezaji wapya wa timu za mataifa mbalimbali huku pia wengine wakijiunga na klabu zinazoshiriki ligi kuu barani humu. Afrika ina vijana wengi zaidi duniani. 

  Uwiano wa vijana barani humu ni mkubwa kuliko mabara yote kwani takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 60 ya Waafrika zaidi ya bilioni moja ni vijana,” alisema George Ferreira, Makamu wa Rais wa Samsung Electronics, Africa. 

  Akizungumzia ushirikiano huo, Andre Beyers, Ofisa Masoko Mkuu wa Airtel Africa alisema: "Ushirikiano huu utapanua wigo wa biashara na kuyawezesha mashindano ya ARS kufikia malengo yake.” 

  Msimu ujao wa Airtel Rising Stars ukiwa ni wa tatu tangu kuanzishwa kwake utaanza mwishoni mwa mwezi huu. Moja kati ya matunda ya mashindano haya ya Airtel ni Priscilla Okyere, binti aliyeibuka kutoka ARS na sasa ni nahodha wa timu ya taifa ya wasichana chini ya miaka 17 ya Ghana. Aliiongoza timu hiyo kunyakua medali ya fedha kwenye mashindano ya Dunia ya FIFA Under-17 kwa wanawake mwaka jana huko Azerbaijan.

  0 0

  Kamanda wa vyuo vikuu nchini Moses Katabalo (pichani) akitoa maoni yake kwa waandishi wa habari ( hawapo pichani ) ofisini kwake jijini Dar es Salam jana kuhusu hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa , hivyo amewataka wanafunzi kutojiingiza kwenye migogoro ya masuala ya udini na kiushi vizuri kwani wanategemeana katika masomo na maisha, iwapo watafarakana athari zake ni kubwa.
  Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Taifa na Mwenyekiti wa tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( UDSM )Seki Kasuga pichani akitoa maoni yake kuhusu hotuba ya mwisho wa mwezi aliyoitoa Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni, Seki amewashauri wanavyuo nchini kutobaguana, kushikamana ili kuendelea vizuri kwenye masomo yao pamoja na kujiepusha vitendo vitakavyoleta migogoro.
  Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam anaechukua masomo ya sayansi Halima Ahmad (pichani) akichangia hotuba ya mwisho wa mwezi aliyoitoa Rais Kikwete kuhusu amani na utulivu nchini , amesema wanavyuo wasikubali kutumiwa katika kuleta migogoro isiyokuwa na manuafaa kwa taifa letu, bali waendelee kutafuta elimu kwa faida yao pamoja na maendeleo nchini.Picha na Mwanakombo Jumaa- (MAELEZO).

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilkimo (IITA) yenye Makao Makuu nchini Kongo Dk.Nteranya Sangiinga,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar na ujumbe wake leo.
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilkimo (IITA) yenye Makao Makuu nchini Kongo Dk.Nteranya Sangiinga,(aliyesimama) akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakati wa mazungumzo akiwa na Ujumbe wake Ikulu Mjini Zanzibar leo. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

  0 0

   Na Mwandishi Wetu

  BENDI ya muziki wa dansi ya Extra Bongo na kundi la taarabu la Jahazi Modern ndiyo burudani zitakazonogesha tamasha la vyombo vya habari litakalofanyika Dar es Salaam kesho (Jumamosi).

  Akizungumza Dar es Salaam jana, wakati wa kutambulisha burudani hizo, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinachoandaa bonanza hilo, Juma Pinto alisema maandalizi kuhusiana na tamasha hilo linalojulikana kama Media Day Bonanza yamekamilika.

  Alisema wameichukua Extra Bongo inayoongozwa na Ally Choki na Jahazi Modern inayoongozwa na Mzee Yusuph kutokana na makundi hayo kuwa juu hivi sasa katika muziki kwa maeneo yao.


  “Tunaamini watakaokuja kwenye tamasha watakuwa na furaha ya aina yake na tumejiandaa vya kutosha,” alisema Pinto na kueleza kuwa bonanza hilo litafanyika viwanja vya Sigara Chang’ombe, Dar es Salaam na mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe.


  Pia Pinto alisema bendi ya Msondo Ngoma Music itapiga kwenye viwanja hivyo kuanzia saa moja usiku baada ya bendi za Extra Bongo na Jahazi kumaliza kutumbuiza Media Day na kwamba imetoa ofa kwa wanahabari watakaotaka kubaki kuendelea kupata burudani mpaka usiku wa manane.

  “Msondo wana bonanza lao kila Jumamosi, sasa wamekubali kwamba wanahabari watakaotaka kubaki baada ya bonanza kumalizika jioni wabaki wajiunge na Msondo Ngoma,” alisema Pinto. Bonanza hilo la TASWA linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) likiwa na lengo la kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari bila kujali ni wa siasa, michezo, uchumi, afya na mambo mengine pamoja na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari ili kubadilishana mawazo na kufurahi pamoja.

  Kwa upande wake Ofisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu alisema wamejipanga vya kutosha na kwamba wadau wafike kwa wingi kuhakikisha mambo yanaenda kama yalivyopangwa.  “TBL ni mdau mkubwa wa wanahabari, tumewaandalia mambo mazuri, naomba msikose,” alisema Malulu na kuongeza kuwa wanaamini wadau 1,500 kutoka vyombo mbalimbali vya habari wanaotarajiwa kushiriki bonanza hilo watafurahi vya kutosha siku hiyo.

  Naye Choki akizungumza kwenye mkutano huo, alisema vijana wake wamejipanga vya kutosha kushambulia na kuwa dhamira yao ni kuona wana habari wanafurahi vya kutosha na kuwa mambo waliyowaandalia kila mtu atafurahi kuiona Extra Bongo.

  0 0  0 0

  On April 4, United States Ambassador Alfonso E. Lenhardt, (center); bestowed the 2013 Tanzanian Women of Courage award to Minister of State of the First Vice President's Office, Zanzibar Government of National Unity, the Honorable Fatma Abdulhabib Fereji, (4th from left); and the Director of the Maasai Women's Development Organization (MWEDO), Ms. Ndinini Kimesera Sikar (3rd from right); and their family members. The awardees were honored for their efforts to promote equality, opportunity, participation in public life, and access to health care and education for Tanzanian women and girls. They become the sixth and seventh recipients of the Tanzanian Women of Courage Award since the U.S. Embassy began this recognition in 2008. The ceremony was held at the U.S. Embassy in Dar es Salaam and was attended by over 175 guests, including senior government officials and leaders from Tanzania's civic and media sectors.

  0 0


  Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Tanzania Bw. Philipe Poinsot (kulia),Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Sophia Simba (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa UN-Women Kanda ya Afrika Mashariki na Pembe ya Pwani,Bi. Christine Musisi wakiwa katika Kikao kazi cha Ushirikiano kuhusu kuandaa Mkakati wa Pamoja wa namna ya kushughulikia masuala ya Jinsia katika Sekta ya Madini,kilichofanyika jijini Dar.
  Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Tanzania Bw.Phillipe Poinsot akiongea wakati wa ufunguzi Kikao kazi cha Ushirikiano kuhusu kuandaa Mkakati wa Pamoja wa namna ya kushughulikia masuala ya Jinsia katika Sekta ya Madini,jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Washiriki wa kikao hicho wakifuatilia ufunguzi rasmi wa Kikao kazi cha Ushirikiano kuhusu kuandaa Mkakati wa Pamoja wa namna ya kushughulikia masuala ya Jinsia katika Sekta ya Madini.

  0 0

  Kutokana na umamuzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kupandisha nauli za usafiri wa mabasi,treni na gharama za bandari zitakazoanza kutumika April 12 mwaka huu, usafiri wa daladala jijini umeanza kuonekana wa shida, hasa nyakati za jioni ,kwani baadhi ya wenye mabasi ya daladala jijini Dar es Salaam wameanza kutumia mwanya huo na kuongeza nauli kinyemela hivyo kusababisha wananchi kutaabika na kusongama katika vituo vya usafiri.

  abiria wakisubiria usafiri kwenye kituo cha Akiba,jijin Dar.
   Baadhi ya wakazi jijini Dar es Salaam jana wakisubiri usafiri katika maeneo ya shule ya Sekondari ya Azania.
  Baadhi ya wanachi katika maeneo ya Jangwani jana wakitembea kwa miguu.baada ya kuona tatizo la kususbiri usafiri.Picha na Mwanakombo Jumaa -Idara ya Habari (MAELEZO).

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk.Charles Kimei (katikati) akifafanua jambo wakati alipokuwa akiwasilisha matokeo ya utendaji wa Benki ya CRDB kwa mwaka 2012.
  Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Benki ya CRDB Bi.Tully Mwambapa aliwakaribisha wageni waalikwa katika hafla ya kutangaza matokeo ya kifedha ya mwaka 2012 ya Benki ya CRDB.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk.Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari kwa kufurahi na wajumbe wa Bodi ya Benki hiyo Bi.Joyce Nyanza(Kushoto) na Bwana Ally Laay(Kulia).Wengine ni mchambuzi wa masuala ya Fedha Dkt.Mohamed Warsame (Kulia) na Mkurugenzi wa Ujasiriamali watu Bi.Dorah Ngaliga(Kushoto).
  Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakifuatilia jambo.


  0 0


  For more Click Here http://vodacom.co.tz/welcome/

  0 0

  Hello brother, 
   Kwanza kabisa napenda kukupongeza kwa kazi kubwa na nzuri ya kutuhabarisha,Ubarikiwe sana! 

  Brother,Nina aunt yangu mmoja ambaye kwa sasa ni zaidi ya miaka mitatu amekuwa akiishi kwa shida mateso na maumivu makali kupita maelezo, Huyu aunt amepatwa na uvimbe wa ajabu mguuni ambao ulianza kama uvimbe wa kawaida mfano wa mtu unapokuwa umekaa kwa muda mrefu ukiwa safarini.

  Baada ya miezi kazaa mguu uliendelea kujaa kwa kasi ndipo akabidi aende KCMC HOSPITAL kwa ajili ya vipimo,ma daktari walifanya vipimo pamoja na elephantiasis(matende) lakini vipimo vyote vikaja negative ikabidi aanzishiwe dozi za anti biotic.

   Baada ya kutumia hizo anti biotic, mguu uliendelea kujaa na kuaanza kutoa usaa mwingi sana,ukiambatana na maumivu makali, Hali ilivyoendelea kuwa siyo ya kuridhisha ikabidi afike Muhimbili Hospital kwa ajili ya vipimo tena, hapo alichukuliwa vipimo ikiwa pamoja na kucheki ini na figo, kukata kiasi cha ngozi ili kubaini kama ni cancer au tumor lakini majibu talivyotoka pia yakaonyesha negative.

  Sasa tatizo tunashindwa kuelewa inakuaje mguu uko katika hali hiyo lakini hospitalini tunashidwa kuambiwa nini tatizo/chanzo! Chakusikitisha zaidi amejitahidi sana kwenda hapa na pale ili apate kutibiwa lakini sasa imefika hata akirudi hospitali anakuta na kauli za ma nurse" umerudi tena mama mwenye mguu usiotibika" nakubaki akitokwa na machozi bila kujua mwisho wake nini na lini.

  Brother,Naomba unipostie hii ili kama kuna mdau yeyote anaeweza kutusaidia kwa ushauri au njia yeyote yakupata ufumbuzi juu ya hili na zaidi kutibiwa tutashukuru sana, Nimeambatanisha picha za mguu jinsi ulivyo fikia kwa sasa. 
   Natanguliza shukran zangu za dhati

  Mdau  Shomari Mob: +255 779970000

older | 1 | .... | 89 | 90 | (Page 91) | 92 | 93 | .... | 3284 | newer