Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 907 | 908 | (Page 909) | 910 | 911 | .... | 3286 | newer

  0 0


  #NewSongAlert
  #supportgoodmusic
  Cc @rossiempangala_ @johmakini

  0 0

    Mbunge wa Jimbo la Kinondoni anayemaliza muda wake, Mhe. Idd Azzan, akionesha fomu ya kuomba kuwania tena ubunge wa Jimbo la Kinondoni aliyokabidhiwa jana jijini Dar es Salaam, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)

  Kada wa Chama Cha Mapinduzi, Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Jamii UVCCM Dar es Salaam na Kamanda mstaafu wa wa UVCCM Wilaya ya Kinondoni, na Wakili wa Mahakama kuu, Jumaa Mhina 'Pijei' akikabidhiwa fomu ya kuomba kuwania Ubunge Jimbo la Kawe,jana jijini Dar es Salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Pijei amejipanga kulikomboa jimbo hilo lililo mikononi mwa wapinzani wao.


  0 0
  Sikinde
  MAGWIJI wa muziki wa dansi nchini, Msondo Ngoma na Mlimani Park Orchestra ‘Wana Sikinde Ngoma ya Ukae’, wataonyeshakana kazi katika Sikukuu ya Iddi Mosi kwenye viwanja vya TCC Club, Chang’ombe.
  Msondo
  Mpambano huo ujulikanao kama ‘Nani Mtani Jembe’ umeandaliwa na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi.
  Mratibu wa mchuano huo, Joseph Kapinga ‘Kaps’, amesema pambano hilo litakuwa la kusherekea sikukuu ya Idd el Fitr.
  Kapinga alisema kuwa pia pambano hilo litaamua ni bendi gani kali kati ya magwiji hao.
  “Ni mchuano ambao pia utaamua ni muumbaji yupi bora kati ya Shabaan Dede wa Msondo Ngoma na Hassan Rehani Bichuka wa Sikinde,” alisema Kapinga.
  Mratibu huyo alisema kila bendi itapiga kwenye jukwaa lake kama kawaida ili kuondoa malamiko ya kuhujumiwa.
  “Pia kutakuwa na michezo aina mbalimbali ya watoto,” alisema Kapinga.
  Alisema mchuano huo utaanza saa nane mchana hadi ‘liamba’.
  Wadhamini wengine wa shindano hilo ni Saluti5.


  0 0

  This year’s Cecafa Kagame Cup will be live on your world of champions from July 18 to August 2.
  All matches will be live on SuperSport as the broadcaster reaffirms its commitment to East Africa’s premier club competition with two live matches every day from the national stadium in Dar es Salaam.

  There will be great prizes for the stand out performers with the player of the tournament, top goal scorer, best goalkeeper, defender and midfielder each getting a DStv Explora.

  The man of the match in each game will get a Zappa box. 

  Commentary will be in two languages with Bernard Otieno, Jacob Mulee and Mark Ssali in English commentary while Ali Salim Mmanga, Cliff Ndimbo and Michael Were will be in Swahili.  East Africa’s popular Simba Soccer show hosted by Chiko Lawi will be live in Dar es Salaam on July, 2015 at 8.00 pm.

  On the pitch, Five-time winners and home side Yanga have been drawn in group A with Kenyan Premier League champions Gor Mahia, Khartoum of Sudan, Somalia’s Telecom and KMKM of Zanzibar.

  Last year’s finalists APR of Rwanda are pooled in group B with Al Ahly Shandy of Tanzania, LLB of Burundi and Somalia’s Elman.

  Ugandan side KCC headline group C with Malakia of South Sudan, Azam (Tanzania) and Adama City of Ethiopia.


  The winners will get Ksh3million cash prize with the runners up Sh2million while third placed side will pocket Ksh1m.  0 0

   Zahara Muhidin Michuzi akiweka sahihi katika kitabu cha wageni alipowasili katika ofisi za CCM mkoa wa Tabora ili kuchukua form ya kugombea viti maalum kwa vijana.
  Binti huyo wa Michuzi mara baada ya kuhitimu elimu yake ya shahada yake ya uchumi UDOM ameona ni vyema akawatumikia wananchi wa nyumbani kwake mkoani Tabora kwa kutangaza nia ya kugombea ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.
   Zahara Michuzi (kushoto) na Mwasham Hashim (kulia) karani wa UVCCM Tabora akitoa maelekezo ya uchukuaji wa form hizo.
   Zahara Michuzi akikabidhiwa form yake leo katika ofisi za UVCCM mkoa-Tabora
   Zahara akiifurahia form yake ya Ubunge wa viti maalum Tabora.
   Zahara (kushoto) akilipia fedha  ya form hiyo huku mama yake mlezi, Rehema Saidi (katikati),  akishuhudia kitendo hicho. Picha na Aloyson Blog wa TBN kanda ya Magharibi.

  0 0

  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets with South Centre Executive Director Martin Khor in Geneva this afternoon .President Kikwete is in Geneva to attend the High Level Panel on the Global Response to Health crises.
  The Chairman of the High Level Panel on the Global Response to Health crises President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with Celso Amorim a panel member from Brazil during one of the consultative sessions held at World Health Organization(WHO) Headquarters in Geneva this morning. (photos by Freddy Maro)

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dkt. Ibrahim Mzengi wakati aliposoma taarifa fupi ya mkoa huo baada ya Waziri Mkuu kuwasili Mpanda mkoani Katavi kwa mapumziko mafupi Julai 15, 2015. Kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Mhandisi Emmanuel Kalobelo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Mkuu wa Matawi wa Benki ya Exim, Bi Elizabeth Mayengo (wa pili kulia) na Meneja Mahusiano wa benki hiyo, Bi. Violet Bikoche (wa pili kushoto) wakibadilishana mawazo na baadhi ya wateja wa benki hiyo wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
   Baadhi ya wateja wa Benki ya Exim wakishiriki futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan jijini Dar es Salaam  hivi karibuni.
  Mkuu wa Matawi wa Benki ya Exim, Bi Elizabeth Mayengo (kulia) akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

  0 0

  1
  Naibu katibu Mkuu wa Chadema tawi la zanzibar Salum Mwalim akielezea maswala mbalimbali kuhusiana na hali ya Usalama kuelekea katika Uchaguzi mkuu katika hafla ya utiaji Saini waraka wa maadili ya Uchaguzi kwa vyama vya Siasa Grand Palas Zanzibar
  2
  Baadhi ya Wajumbe wa vyama vya Siasa waliohudhuria katika hafla ya utiaji Saini waraka wa maadili ya Uchaguzi kwa vyama vya Siasa Grand Palas Zanzibar. 
  3
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya ZEC Nassor Khamis Mohammed akifafanua baadhi ya mambo katika hafla ya utiaji Saini waraka wa maadili ya Uchaguzi kwa vyama vya Siasa Grand Palas Zanzibar.
  4
  Naibu Katibu Mkuu wa ATC-Wazalendo Juma Said Sanani akitia saini waraka wa maadili ya Uchaguzi kwa vyama vya Siasa Grand Palas Zanzibar.
  5
  Mwakilishi wa CCM Hafidh Ali akitia saini waraka wa maadili ya Uchaguzi kwa vyama vya Siasa Grand Palas Zanzibar. 
  6

  Naibu katibu Mkuu wa Chadema tawi la zanzibar Salum Mwalimakitia saini waraka wa maadili ya Uchaguzi kwa vyama vya Siasa Grand Palas Zanzibar. 

  0 0

  download
  Tunaelekekea kipindi hiki cha kusherehekea sikukuu ya Eid-El-Fitr na ambapo wananchi wenye imani ya kiislam na hata madhehebu mengine hutumia muda huo kwenda kuabudu pamoja na muendelezo wa sherehe hizo kwenye maeneo mbalimbali ya starehe, Jeshi la Polisi nchini linatoa wito kwa wananchi wote kuwa makini na kusheherekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu pasipo vitendo ama viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.

  Jeshi la Polisi nchini linapenda kuwaondoa hofu wananchi kuwa, limejipanga vizuri kuhakikisha wananchi wanasherehekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu. Ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine yote.

  Aidha,  tahadhali zichukuliwe kwa wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara ikiwemo maderera na watembea kwa miguu, kuwa makini kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na hasa kwa madereva wa magari na pikipiki kuepuka kwenda mwendo kasi na kutumia vilevi wawapo kazini.

  Jeshi la Polisi linaendelea kuwasisitiza wananchi kutoa taarifa haraka kwenye vyombo vya dola juu ya kitu chochote ama mienendo ya watu watakaowatilia shaka mahali popote kwani taarifa hizo za haraka zitasaidia kuzuia uhalifu kabla haujatokea.

  Vilevile wananchi wachukue tahadhari watokapo kwenye makazi yao, wasiache nyumba wazi ama bila mtu na endapo italazimika basi ni vema watoe taarifa kwa majirani zao kwa ajili ya usalama.

  TUNAWATAKIA WATANZANIA WOTE SIKUKUU NJEMA YA EID –EL-FITR 
  Imetolewa na: Advera John Bulimba-SSP
  Msemaji wa Jeshi la Polisi

  Makao Makuu ya Polisi.

  0 0


  1

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania, Lennarth Hjelmaker, wakati Balozi huyo alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 16, 2015 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
  2

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania, Lennarth Hjelmaker, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 16, 2015 alipofika kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.

  0 0

  Homa ya michuano ya Kagame inazidi kupamba moto kufuatia vilabu mbalimbali zinazoshirki michuano hiyo kuanza kuwasili jijini Dar es salaam zikiwa na vikosi vyao kamili kwa lengo la kusaka Ubingwa wa michuano hiyo.

  APR ya Rwanda tayari imeshawasili jijjini Dar es salaam, pamoja na timu za Al Shandy ya Sudan, KMKM ya Visiwani Znzibar, huku timu za Al Malakia ya Sudan Kusini na mabingwa mara tano wa michuano hiyo Gor Mahia wakitarajiwa kuwasili leo saa saa 10 jioni kwa ndege ya Kenya (KQ).

  Kueleka mchezo wa ufunguzi kati ya Yanga dhidi ya Gor Mahia, wenyeji timu ya Yanga (watoto wa Jangwani) wameendelea kujifua katika uwanja wa Polisi Ufundi chini ya kocha wake mholanzi Hans Van der Pluijm na msaidizi wake Mkwasa kuhakikisha wanafanya vizuri katika mechi hiyo.

  Gor Mahia ambayo inafundishwa na kocha Frank Nutal raia Skotilandi, inawasili ikiwa na kikosi chake cha kwanza kamili kilichocheza michezo 17 ya Ligi Kuu nchini Kenya bila kufungwa, ikishinda michezo minne na sare michezo mitatu.

  Wasifu wa Azam:
  Klabu ya Azam ilishiriki kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya kombe la Kagame mwaka 2012 lakini walishangaza wengi kwa kumaliza kama washindi wa pili baada ya kufungwa na Yanga mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainali.


  0 0

  Dhima ya Simba Sports Club ya kuendeleza mabadiliko ndani ya Simba bado inaendelea kushika kasi, Katika kipindi cha miezi mitatu sasa, mmekuwa mashuhuda wa Simba inayolenga kuleta mapinduzi makubwa katika jinsi mpira unavyoendeshwa, kujali wanachama, wapenzi wake na kukuza vyanzo vya mapato.

  Akizungumza wakati wa kutangaza rasmi Simba Week 2015 Rais wa Simba Evans Aveva alisema ‘’Kila mwaka timu yetu ya Simba imekuwa na utaratibu wa kuwa na siku maalum kwa ajili ya kufurahi, kuwatambulisha rasmi wachezaji, jezi za timu na kujiandaa kwa msimu mpya, siku hii imekuwa maarufu kama Simba Day. 

  Tangu ianzishwe imekua ikiboreka siku hadi siku, mwaka huu tumeona ni muhimu kuiboresha zaidi na hususani kuangalia mchango wa timu yetu kwa jamii inayoizunguka’’.

  Aliongeza kusema ‘’Hivyo basi mwaka huu tunaanzisha Simba Week ambayo lengo lake kuu ni kuwa wiki ya Simba Sports Club kufanya kazi za jamii, kukuza vipaji vya soka vya vijana, kutembelea wadau wa maendeleo na pia shughuli nyingine zenye tija kwa timu yetu na jamii kwa ujumla. Wiki hii itahitimishwa siku ya Simba Day ambapo mambo mengi mazuri yatafanyika. Tofauti na miaka mingine, tutatengeneza program ambayo itawashirikisha wana Simba Nchi nzima.

  Tunategemea kuwa na siku za kujitolea kwa jamii, wapenzi wote wa Simba Nchi nzima watajitokeza kufanya shughuli za kijamii kwenye maeneo yao. Simba inaamini kwa dhati tukiunganisha Nguvu zetu tunaweza kuleta madabiliko makubwa sana Nchini kwetu’’.

  Pia Rais huyo wa simba Alisema, Napenda kuwataarifu rasmi kuwa siku ya Simba Day, Simba Sports Club itacheza mechi na AFC Leopards ya Kenya kwenye mechi hii wachezaji wetu wapya wataonekana rasmi baada ya maandalizi ya kutosha, kabla ya mechi hii kutakuwa na mechi kali ya utangulizi kati ya Viongozi wa Simba na Bongo movie ambao watachanganyika na Bongo Flava, mechi hii nina uhakika itakuwa burudani tosha. 

  Jambo jema na jipya ni kuwa Kiingilio cha siku hii ni BURE!. BURE kwa wanachama wa Simba ambao watakuwa na kadi mpya za Simba hivyo nawaomba wanachama wachangamkie fursa hii kwa kuchukua kadi mpya!. Simba itaendelea kujali wanachama wake mara zote!

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa EAG Group amabo ni washauri na watekelezaji wa Masoko na Biashara wa Simba, Imani Kajula alisema ‘’ Siku ya Simba Day jezi mpya za Simba zitaanza kuuzwa rasmi, napenda kutumia jukwaa hili kutahadharisha wauza jezi feki kuwa mkono wa dora utawafikia.


  Kwa wale wanaotaka kuwa mawakala au wauzaji wa jezi za Simba milango iko wazi wawasiliane nasi kwa anuani zilizopo kwenye tovuti ya klabu www.simbasports.co.tz au kufika kwenye klabu ya Simba. Pia wapenzi wanaotaka kuwa wanachama wanaweza kujiunga kupitia tovuti ya klabu na mawakala kwani kwa kuwa mwanachama wa Simba Sports Club mwanachama anapata faida nyingi ikiwemo bima ya maisha hadi 250,000 ikiwa mwanachama atafiwa na mwenza, mtoto au yeye mwenyewe akifariki’’
  SIMBA DAY 2015 Simba Kucheza na AFC Leopards, Kiingilio bure.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group Imani kajula Akiwa Pamoja na Rais Wa Simba Sport Club Evans Aveva wakati wa Uzinduzi wa Simba Day.

  0 0


  0 0

  The Vice President, H.E Dr. Mohamed Gharib Bilal, (2nd left) listens to a client of Standard Chartered Bank Tanzania Limited at an Iftar event hosted by the Bank in Dar es salaamrecently. 3rd right is the Bank’s CEO, Liz Lloyd.

  0 0


  0 0


   Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Ally Yahaya Simba(Kushoto) akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili ofisini kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akimueleza Dkt. Ally Yahaya Simba (Kushoto) umuhimu wa kuendelea kufanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya mawasiliano,alipomtembelea leo ofisini kwake.

    Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Ally Yahaya Simba akiongea na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga na kumhakikishia kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi ya Taifa hasa katika kuiendeleza Sekta ya Mawasiliano Nchini.

   1-    Watendaji wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (mwenye suti nyekundu) alipotembelewa na Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Ally Yahaya Simba (kulia kwa Katibu Mkuu) aliyeteuliwa kushika nafasi ya Prof. John Nkoma aliyemaliza Muda wake.

  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiwaeleza jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (Hawapo pichani), walipotembelewa na Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Ally Yahaya Simba.Kulia kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Raphael Hokororo

   Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiagana na Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Ally Yahaya Simba(kushoto) Picha na Hassan Silayo-MAELEZO

  0 0


  0 0

   The United Nations High Commissioner for Refugees UNHCR Mr.Antonio Guterres welcomes to his Geneva office President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete The President paid a courtesy call on him today and held talks on the influx of Refugees in Tanzania
    The United Nations High Commissioner for Refugees UNHCR Mr.Antonio Guterres introduces President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete to him some of his senior staff members.
  The United Nations High Commissioner for Refugees UNHCR Mr.Antonio Guterres and President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete shake hands when the nlatter paid a courtesy call on him today and held talks on the influx of Refugees in Tanzania. Photos by Freddy Maro

  0 0

older | 1 | .... | 907 | 908 | (Page 909) | 910 | 911 | .... | 3286 | newer