Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

UN SECRETARY-GENERAL MESSAGE ON WORLD YOUTH SKILLS DAY 15 July 2015

$
0
0
            I welcome this first-ever commemoration of World Youth Skills Day.  On July 15th each year, the international community will underscore the value of helping young people to upgrade their own abilities to contribute to our common future. 
            While overall more young people have greater educational opportunities than in the past, there are still some 75 million adolescents who are out of school, denied the quality education they deserve and unable to acquire the skills they need. 
            We may see an understandably frustrated youth population – but that picture is incomplete.  With the right skills, these young people are exactly the force we need to drive progress across the global agenda and build more inclusive and vibrant societies. 
            Skills development reduces poverty and better equips young people to find decent jobs. It triggers a process of empowerment and self-esteem that benefits everyone. And it strengthens youth capacity to help address the many challenges facing society, moving us closer to ending poverty hunger, injustice and environmental degradation. 
            On this Day, I call for investing politically and financially in developing the skills of young people so that they can help build a more just and sustainable future for all.


THREE DAYS OF REVIVAL AT UMOJA CHURCH IN DALLAS, TEXAS

Rais Kikwete akutana na Koffi Annan Geneva

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na kufanya mazungmzo na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan mjini Geneva leo.Watau kushoto ni Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Geneva Mh.Modesti Mero.Koffi Annan alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kati ya mwaka 1997 na 2006. Picha na Freddy Maro
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan mjini Geneva baada ya mazungumzo yao leo jijini Geneva

SIMU TV: Habari kutoka vituo vya Television mbalimbali

JUMUIYA YA KUINUA VIPAJI VYA KUHIFADHI QURAN JIMBO LA KIKWAJUNI YANDAA MASHINDANO MADOGO YA KUHIFADHI QURAN

$
0
0
 M.C. wa shughuli  Ustaadh Khamis Ameir akisoma utaratibu wa mashindano madoga ya kuinua vipaji ya kuhifadhi Quran ya Jimbo la Kikwajuni yaliyofanyika uwanja wa Alabama Michenzani Mjini Zanzibar.
 Mwafunzi Ramla Khamsin Jafar wa madrasati Nurul-iman akionyesha jitihada zake katika mashindano ya kuhifadhi yaliyofanyika ya Jimbo la Kwahani.
  Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa kina mashindano hayo.
 Jaji kiongozi Abushayth Daud Mohudhar akitoa matokeo ya mashindano hayo.
 Mgeni rasmin Mbunge wa Kikwajuni Mh. Hamad Yussuf Masauni akimkabidhi zawadi mshindi wa juzuu tano Fauzia Said Ali wa Madrasat Akhlaq, pesa taslim shiling laki moja
 Mgeni rasmin, ambae pia ni mdhamini  wa Mashindano madogo ya kuinua vipaji vya kuhifandi Quran Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mh. Hamad Yussuf Masauni akitoa nasaha zake mara baada ya kushuhudia mandano ya kuhifandi Quran yaliyoshirikisha wanafunzi kutoka vyuo vinane vya jimbo la kikwajuni. (kulia) Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Nassor Salim (Aljazira) na kushoto ni Mwenyekiti wa mashindano hayo Khamis Said Ali

TIMU YA WIZARA YA AFYA YAANZA MAZOEZI YA MAANDALIZI YA MASHINDANO YA SHIMIWI KATIKA UWANJA WA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Kocha wa timu ya Wizara ya Afya na  Ustawi wa Jamii, Ally Lidengi, akitoa maelekezo kwa wachezaji wa mchezo wa kamba  wakati wa Maandalizi ya Mashindano ya Shimiwi katika uwanja wa Taifa Muhimbili Dar es Salaam yanayotarajiwa kuanza 15 Septembar 2015  Jijini Morogoro.

Kocha wa timu ya Wizara ya Afya na  Ustawi wa Jamii, Ally Lidengi, akitoa maelekezo kwa wachezaji hao wakati wa Maandalizi ya Mashindano ya Shimiwi katika uwanja wa Taifa Muhimbili Dar es Salaam yanayotarajiwa kuanza 15 Septembar 2015  Jijini Morogoro.
PICHA ZOTE  NA KHAMISI MUSSA

Bodi ya Mikopo yaongeza muda wa kuwasilisha maombi

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu 
(HESLB) Bw. George Nyatega
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeongeza muda wa waombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kuwasilisha maombi yao hadi mwishoni mwa mwezi huu (31 Julai, 2015). 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo (Jumatano, Julai 15, 2015) na Mkurugenzi Mtendaji wa (HESLB) Bw. George Nyatega, hatua hiyo imechukuliwa ili
kuwapa fursa wombaji ambao hawajakamilisha kufanya hivyo. 
“Hatua hii imechukuliwa ili kuwapa fursa wale ambao kwa sababu mbalimbali hawakuweza kufanya maombi ya mikopo katika  muda uliopangwa,” amesema Bw. Nyatega katika taarifa yake iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari. 
Itakumbukwa kuwa awali Bodi ilianza kupokea maombi kwa njia ya mtandao (www.olas.heslb.go.tz) tarehe 4 Mei, 2015 na mwisho wa kuwasilisha maombi ulipangwa kuwa tarehe 30 Juni, 2015. 
Kupitia taarifa yake, HESLB imewataka waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 ambao hawajakamilisha maombi yao kukamilisha na kuwasilisha maombi yao ya mikopo ndani ya muda ulioongezwa na kusisitiza kuwa hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza baada ya tarehe 31 Julai, 2015. 
HESLB ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu.

JINSI YA KUANDAA NA KUTAYARISHA DAWA-LISHE NA KUNENEPESHA, KURUTUBISHA NA KUONGEZA MWILI.

$
0
0
Dawa-lishe  ya  kuongeza, kurutubisha  na  kunenepesha  mwili, ni  dawa  maalumu  kwa  watu  wenye  uzito  wa  chini  (  Under weight ) ambao  wanataka  kuongeza  mwili  na  uzito.
Dawa  hii  huwasaidia  watu  ambao  miili  yao  imedhoofu  kutokana  na  sababu  mbalimbali  kama  vile  kuugua  magonjwa  na  maradhi  mbalimbali.
Na  kwa  wale  watu  wembamba  ambao  wanataka  kuongeza  miili  yao, dawa  hii  huwasaidia  vizuri  sana. 
Kusoma zaidi makala hii BOFYA HAPA

Kiongozi wa Kundi la TMK wanaume kugombea udiwani kata yake ya Kilungule, wilayani Temeke

$
0
0
Kiongozi wa Kundi la TMK wanaume na Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe kinachosimamia bendi ya vijana machachari wa Yamoto, Saidi Fella leo amechukua fomu ya kuomba kugombea udiwani katika kata yake ya Kilungule, wilayani Temeke, jijini Dar es salam.
Saidi Fella ameamua kuchukua fomu hiyo na kugombea nafasi hiyo ili aweze kutatua kero za wakazi wa kata ya Kilungule na kuleta maendeleo katika Kata hiyo.
 "Nimeamua kuchukua nafasi hii ili kutatua kero za kata yangu, hapa kuna shida ya maji na barara naamini nikiwa Diwana nitaweza kuonana na wakubwa wa nchi uso kwa uso.

Katibu wa Siasa na Uenezi kata ya Kilungule, Juma Ally Kilindo Akimkabidhi fomu ya Kuomba kugombea udiwani  Saidi Fella.

Saidi Fella akisaini kitabu cha wageni mara alipofika katika Ofisi za Kata ya Kilungule wilaya ya Temeke.

UNAKARIBISHWA KWENYE SHEREHE ZA EID EL FITR ZA PAMOJA DMV

$
0
0

Assalamu Alaykum Wa Rahmatullaahi wa Barakaatuhu

Uongozi wa Tanzanian Muslims Community of Washington DC Metro (TAMCO) Una Furaha Kuwakaribisha  WaTanzania Wote katika Sherehe za Eid El Fitr, kuadhimisha Kumaliza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Zitakazo Fanyika (Inategemea Kuandama kwa Mwezi)

Friday July 17, 2015

1.     Chai ya Asubuhi ya Pamoja, Baada ya Salat El Eid
Kuanzia Saa Tatu Asubuhi – Saa Nane Mchana 9AM-2PM

Wheaton Claridge Park Activity Building
11901 Claridge Road
Wheaton,  MD 20902

2.     Sherehe za Eid za Jioni  
Kuanzia Saa Kumi na Moja Jioni Mpaka Saa Nne Usiku 5PM-10PM

Meadowbrook Park Activity Building
7901 Meadowbrook Lane
Chevy Chase, MD 20815

Kwa Taarifa Zaidi Wasiliana na :
Ali Mohamed  301-500-9792
Asha Hariz 703-624-2409
Shamis 202-509-1355 

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 15/07/2015

Watanzania kuendelea kuula viwanja vya Bayport

$
0
0
Meneja Biashara wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kushoto, akizungumza jambo wakati akitangaza taasisi yao kuendelea kutoa huduma ya mradi wa viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, ulioanza Mei 22, mwaka huu na kupokewa vizuri na Watanzania wengi. Kulia ni IT Meneja wa Taasisi hiyo, Daud Mavule.

WATANZANIA wenye nia ya kumiliki ardhi, wataendelea kuipata fursa hiyo baada ya Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, kuwapatia nafasi wateja wao katika mradi huo ulioanza rasmi Mei 22 mwaka huu na kuzinduliwa katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Hayo yamesemwa na Meneja Biashara wa Taasisi hiyo, Thabit Mndeme, alipokuwa akizungumza jijini Dar es Salaam, juu ya huduma hiyo ya viwanja vinavyotolewa kwa watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali.

Kwa mujibu wa Mndeme, wameamua kuendelea kutoa huduma hiyo ya viwanja katika eneo ya Vikuruti, baada ya kufanya tathmini kwa kuangalia umuhimu wa Watanzania kuweza kumiliki viwanja ili kujenga nyumba za kuishi, nyumba za biashara na mahitaji mengineyo wapendayo.
Mbali na huduma hiyo ya viwanja, Bayport ni taasisi ya kifedha inayojihusisha na mambo ya mikopo ya fedha, mikopo ya bidhaa bila kusahau bima ya elimu kwa uwapendao, huku huduma zote hizo zikifanikisha maisha bora kwa wateja wao na Watanzania kwa ujumla.

Meneja Biashara wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kushoto, akizungumza jambo wakati akitangaza taasisi yao kuendelea kutoa huduma ya mradi wa viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, ulioanza Mei 22, mwaka huu na kupokewa vizuri na Watanzania wengi. Kulia ni IT Meneja wa Taasisi hiyo, Daud Mavule.

“Bayport Financial Services ni taasisi yenye kutoa huduma bora kwa wateja wetu na Watanzania kwa ujumla, hivyo tunaamini huduma yetu ya mikopo ya viwanja kuwa endelevu ni sehemu ya kuhakikisha kwamba watu wote wanakuwa na uwezo wa kumiliki ardhi kwa ajili ya matumizi yao mbalimbali. 

 “Hii ni huduma endelevu na muhimu inayotolewa kwa watu wote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo mteja kutoka mahali popote anaweza kumiliki kiwanja hicho kwa kuchukua fomu za kuomba viwanja hivyo kupitia ofisi zetu zilizoenea nchi nzima, bila kusahau kwa wakala wetu Bank Of Africa (BOA),” alisema.


Mndeme alisema kwamba sasa wateja wao watazidi kunufaika kununua viwanja vilivyopo Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, huku wakivipata kwa njia ya mkopo au kwa fedha taslimu.

WATANZANIA WAISHIO BOTSWANA KUANZA KUFAIDIKA NA MFUKO WA GEPF KUPITIA MPANGO WA ‘GEPF DIASPORA SCHEME’ (GDS)

$
0
0
Ujumbe wa Mfuko wa GEPF nchini Tanzania na Mwenyekiti wa Watanzania waishio nchini Botswana wakiongozwa na Meneja Mahusiano wa Benki ya FNB Botswana, Bibi Patricia Mpelega (wa pili kushoto) wakati wakielekea kwenye tawi (Branch) la benki hiyo kwaajili ya uzinduzi wa akaunti maalum ya kuwasilisha michango kwa Watanzania wainshio nchini humo, kwa kujiwekea akiba zao za baadae.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko kutoka Mfuko wa GEPF, Aloyce Ntukamazina (wa tatu kulia) akimpa maelezo mafupi juu ya mpango huo wa GDS Meneja Mahusiano wa Benki ya FNB Botswana, Patricia Mpelega, muda mfupi kabla ya kuzindua akaunti maalum.Wengine pichani ni Mwenyekiti wa watanzania waishio Botswana, Nieman Kissasi (kulia) na Meneja wa Mkoa wa Ilala Bw Jafari Meraji .
Bi Patricia Mpelega akimpongeza Mwenyekiti wa watanzania waishio Botswana, Nieman Kissasi baada ya kukamilisha zoezi la ufunguzi rasmi wa akaunti ya Diaspora Botswana
Mwenyekiti wa Watanzania waishio Botswana Bw Nieman Kissasi akikamilisha utaratibu wa kuwasilisha michango yake kama ishara ya uzinduzi rasmi wa akaunti hiyo kulia kwake ni Meneja wa Mkoa wa Ilala Bw Jafari Meraji .

SAMAKI SAMAKI PRESENT MUSIC PLANET AT LEADERS CLUB JULY 18, 2015

TIMU YA WATU 39 KUTOKA AFRIKA KUSINI WAPNDA MLIMA KILIMANJARO KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA KUSAIDIA KUNUNUA TAULO MAALUMU KWA WASICHANA WALIOPO MASHULENI PINDI WAWAPO KATIKA HEDHI

$
0
0
Mwanzilishi wa taasisi ya Imbumba Foundation ,Richard Mabaso akizungumza lengo la safari hiyo ya kupanda Mlima Kilimanjaro ijulikanao kama Trek4 Mandela ambayo ni mahususi kwa ajili ya kuchangisha fedha zausaidia wasichana walioko mashuleni.
Mkurugenzi mkuu wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Washiriki wa Changamoto hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Tanzania,Allan Kijazi.
Katika timu hiyo wamo wakurugenzi wa taasisi mbalimbali za nchini Afrika Kusini ,watu maarufu ,watangazaji katika vituo vya Luninga,wachezaji filamu n.k. katikati hapo ni Ofisa Uhusiano wa nje wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom nchini Afrika kusini,Maya Makanjee.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WELCOME TO 6th INTERN. AFRICAN FESTIVAL TUEBINGEN,GERMANY FROM 23-26 JULY 2015

$
0
0
Dear Africans, friends and well-wishers of Africa, 
Summer is around the corner! It’s time to relax and spend quality time with friends, family and well-wisher at the largest extravaganza African Diaspora festival taking place for the 6th time in Down-town Tübingen in Germany from the 23 to the 26h of July 2015 at the African Village (Festplatz). www.ngoma-africa.com

IN LOVING MEMORY

$
0
0
ANDREW MINANI FATUKUBONYE

It is 10 years now since you departed. Your untimely departure clouded our hearts with untold sadness and grief. As we pray for you on this day for eternal peace and comfort, you are fondly remembered by your beloved wife, daughters, grandchildren, relatives and your friends.
John 5:28-29, “Rest in God’s loving Embrace”
Memorial services will be held at his residence Buhororo- Ngara on 18th July 2015 at 1400hrs.

KAMPUNI YA MSAMA PROMOTIONS YAGAWA ZAWADI ZA EIDD EL FITR KWA VITUO VYA WATOTO YATIMA JIJINI DAR

$
0
0

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akimkabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali kwa mtoto Sophia Said wa kituo cha Yatima cha Maunga cha Kinondoni jijini Dar es Salaam ikiwa ni masandalizi ya Sikukuu ya Idd El Fitr.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwakabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali watoto, Gatson Edward na Bonny Mayanga wa kituo cha Yatima cha Tuwakomboe cha Temeke jijini Dar es Salaam ikiwa ni masandalizi ya Sikukuu ya Idd El Fitir. Jumla ya vituo 10 vilinufaika na msaadahuo ambao umetokana na mapato ya Tamasha la Pasaka la mwaka huu.
Sehemu ya misaada hiyo ikishushwa

KAMPUNI ya Msama Promotions chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama, jana iligawa misaada ya vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi mil 9.5 kwa vituo 10 vya kulea yatima vya jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi misaada hiyo kwa viongozi na wawakilishi wa vituo hivyo, Msama mwasisi wa matamasha ya Injili nchini tangu mwaka 2000, alisema ametoa vitu hivyo kuwapa faraja watoto wa vituo hivyo.


Msama ambaye hivi karibuni alitoa msaada kama huo wenye thamani ya shilingi mil 7.5, alisema msaada huo wa jana ni kuwapa faraja watoto hao kufurahia sikukuu ya Idd el Fitr inayoweza kuangukia kati ya Julai 18 au 19.


“Nimeguswa kuendelea kusaidia watoto hawa, najisikia faraja na amani ya moyo ninapofanya hivi nikikumbuka mbali mno, ikiwemo hata maisha niliyowahi kuishi na kuyapitia, hivyo si kutaka sifa wala umaarufu,” alisema.


Msama ametoa wito kwa jamii kutambua watoto wanaolelewa katika vituo hivyo si kupenda kwao, bali ni kutokana na changamoto za kimaisha zilizowapata hadi ku kila mtoto angependa kulelewa na wazazi wake.


Vituo vilivyopewa msaada wa vitu mbalimbali kama unga, mchele, sukari, sabuni na juisi, ni Honoratha, Mwana, Umra, Mujahidina, Zaidi, Hairat, Sifa, Mwandaliwa na Chakuwama.


Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Alhaji Mzee ambaye ni mmoja wa watoto wa kituo cha Alhaji Mzee wa kituo cha Mwandaliwa, alisema ni furaha kubwa kwao kupata msaada huo kuelekea sikukuu hiyo.


Msama alisema fedha zilizotumika kununua vitu hivyo ni kutoka katika mfuko wa Tamasha la Pasaka ambalo hufanyika kila mwaka tangu 2000 chini ya uratibu wa kampuni ya Msama Promotions.


Msama ni mtu aliyejipambanua kama mdau mkubwa katika kusaidia jamii kupitia makundi maalumu kama yatima, walemavu na wajane kwa lengo la kuwapa faraja ya kufurahia maisha kama wengine.


Mbali ya kutoa misaada mbalimbali kwa makundi hayo kabla au baada ya tamasha la Pasaka kila mwaka, Msama amewahi kusaidia waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto, mwaka 2011

DAVIS MOSHA ATANGAZA RASMI NIA YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MOSHI MJINI

$
0
0
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Davis Mosha akisalimiana na wakazi wa Moshi waliofika katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa.
Davis Mosha akizungumza na waandishi wa habari marabaada ya mkutano wake wa kutangaza nia.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

SIMU TV: UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETI JULY 16

$
0
0
STAR TV: Shule za binafsi na za Serikali ngoma droo katika matokeo ya kidato cha sita.Pata habari kamili katika magazeti ya leo July 16; https://youtu.be/rSp5Fl0nhGQ
CH 10:Kingunge ajilipua tena,atofautiana na jaji Warioba, atoa shutuma nzito, ambeba Lowasa. Ni katika dondoo za magazeti ya leo July 16; https://youtu.be/Htt-qLCcQ2c

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images