Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 904 | 905 | (Page 906) | 907 | 908 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Mwenyekiti wa Afya Sacos Othman Mussa Juma akitoa hutuba ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Ushirika huo uliofanyika Ukumbi wa Ecrotanal Mjini Zanzibar. Wajumbe wa Mkutano huo walizimia kuongeza Akiba ya shilingi elfu 30 kutoka elfu 10 kwa mwezi ili kuzidi kujikwamua na Umaskini.
   Mgeni Rasmi wa Mkutano huo ambaye ni Mkurugenzi wa Bohari kuu ya Madawa Zanzibar Zahran Ali Hamad akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Ushirika wa Afya Sacos. Katika Mkutano huo aliwaomba kuzidisha mashirikiano miongoni mwao.
   Baadhi ya Wanachama wa Ushirika wa Afya Sacos wakisikiliza hutuba ya ufunguzi ya mgeni rasmi(hayupo pichani) katika Mkutano wa mwaka wa Ushirika huo.
   Katibu Mkuu wa Ushirika wa Afya Sacos Kassim Issa Kirobo akitoa nasaha zake katika Mkutano huo ambapo aliwaahidi kusimamia vyema Ushirika huo ili utimize lengo la kujikwamua na Umaskini.
  Mmoja wa wanachama wa AFYA SACOS Makame Mussa akichangia katika mkutano huo ambapo aliwasihi Viongozi wake kuwa waadilifu ili Ushirika wao uweze kuwaletea maendeleo. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0

  Shindano la Miss Kilimanjoro Ambassador 2015 limepamba moto kwa kuchukua sura mpya kwenye vyombo vya habari likiwa na mvuto wa aina yake.

  Warembo wanaowania taji hilo wako kambini kwa sasa wakinolewa vilivyo ikiwa ni maandalizi ya fainali za shindano hilo litakalofanyika julai 24 katika ukumbi Kili Home mjini Moshi.

  Habari za kuamianika toka kamati ya maandalizi imesema kuwa kamati imejipanga kisawasawa kuhakikisha wanakidhi kiu ya wapenzi wa tasnia ya urembo katika mikoa ya kaskazini  ikiwemo Arusha ,manyara na Kilimanjaro kwa ujumla.

  Pamoja na burudani toka kwa washiriki hao kutakuwa na burudani ya wasanii wa bongo flava,ngoma za asili na saplaizi amabAyo haijawahi kutokea katika mkoa wa Kilimanjaro katika anga za burudani.

  Kiingilio cha siku hiyo V.I.P(A) ni Tsh 200,000/= ikijumuisha chakula na vinywaji, V/I.P(B) ni Tsh 100,000/= pamoja na vinywaji, SILVER ni Tsh 50,000/= na REGULAR ni 30,000/=


  0 0

  digna ft maromboso

  0 0


  0 0

  Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel leo imezindua promosheni kwa wateja wake yenye lengo la kuboresha uhusiano pamoja na kuwazawadia wateja wake nchi nzima kila wiki kwa muda wa siku 120.

  Promosheni hiyo ijulikananyo kama " Jiongeze na Mshiko" ni ya kipekee kwani inampatia mteja kujiunga na kushiriki bure kwa kujibu maswali na kujishinda shilingi milioni 1 kila wiki na mwisho wa promosheni kujishindia shilingi milioni 2. Na ikiwa mteja atapenda kujishindia zawadi kubwa zaidi ataweza kujiunga na ngazi ya Premium kwa kuchajiwa shilingi 300 kwa siku na kupata nafasi ya kujishindia shilingi milion 3 kila wiki na mwisho wa promosheni kujishindia shilingi milioni 50.

  Akiongea wakati wa Uzinduzi wa promosheni hiyo, Meneja huduma za ziada wa Airtel, Bi Prisca Tembo, alisema" promosheni hii inathihirisha lengo letu la kuwawezesha watanzania kufikia ndoto zao na huku tukiendelea kutoa huduma bora za kibunifu zinazokithi mahitaji yao.

  Promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" itawawezesha watanzania wengi kujishindia mamilioni ya pesa kila wiki na kuwawezesha kupata fedha kwaajili ya kuendesha shughuli zao za kijamii na kiuchumi pindi watakapoibuka washindi kwa muda wa wote wa mienzi minne.

  Mteja atatakiwa kujibu maswali na kujikusanyia pointi zitakazomwongezea nafasi ya ushindi na kuweza kujishindia zawadi ya pesa taslimia kupitia promosheni hii ya " Jiongeze na Mshiko" natoa wito kwa watanzania kujiunga na kupata nafasi ya kujishidia pesa taslimu kila wiki.

  Akiongea jinsi ya kujiunga na kushiriki , Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde alisema "wateja wataweza kujinga na promosheni hii bure kwa kutuma ujumbe wenye neno "BURE" kwenda namba 15470, na kisha kuanza kupokea maswali kwenye simu zao na kujibu maswali bure bila gharama yoyote na kujikusanyia pointi. Mteja atakapomaliza kujibu maswali ya bure atapata ujumbe utakaomuuliza kama angependa kujiunga na ngazi ya premier, ili kuwezeshwa kufunguliwa maswali zaidi na kujikusanyia pointi nyingi kwa zawadi zenye thamani kubwa.

  Aliongeza kwa kusema maswali yatakayoulizwa ni ya kawaida hivyo tunategemea wateja wetu watafurahia kuyajibu na kupata nafasi ya kujishindia shilingi milioni 108 ikiwa ni moja ya njia ya kuwazawadia kwa kutumia huduma zetu.

  Alitoa wito kwa Tanzania kuwa waangalifu na kuhakiki taarifa zozote wanazopewa kuhusu Ushindi kwa kupiga 100, namba yetu ya huduma kwa wateja.
  Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (kulia), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa promosheni mpya ya Airtel 'Jiongeze na Mshiko' itakayomwezesha mteja wa mtandao huo kujishindia mamilioni ya pesa kwa njia ya sms. Katikati ni Meneja wa Huduma za Ziada wa Airtel, Prisca Tembo na Afisa Huduma za Ziada, Fabian Felician.
  Meneja wa Huduma za Ziada wa Airtel, Prisca Tembo (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa promosheni mpya ya Airtel 'Jiongeze na Mshiko' itakayomwezesha mteja wa mtandao huo kujishindia mamilioni ya pesa kwa njia ya sms. Kushoto ni na Afisa Huduma za Ziada, Fabian Felician na Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde.

  0 0


  0 0

  Mdau Saida Yunus Chui akiwa ni mwenye furaha sana muda mfupi baada ya kula Nondozz yake ya Master School of Improvement and Education Leadership katika Chuo Kikuu cha Birmingham University, kule kwa Bibi (Uk).
  Mdau Saida Yunus Chui akiwa akiwa ndani ya ukumbi wa Chuo Kikuu cha Birmingham University, tayari kwa kula Nondozz yake ya Master School of Improvement and Education Leadership.
  Mdau Saida Yunus Chui akiwa na hazbendi wake,Ahmed Mashaka (kulia) pamoja na Dada yake mada baada ya kula Nondozz yake ya Master School of Improvement and Education Leadership.

  0 0

   Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha hiyo jijini Arusha
   Picha ya pamoja ya washiriki pamoja 
  na mgeni rasmi Mh. Godbless Lema.

  0 0

  Mkutano wa Mkubwa watatu wa  Kimataifa,  unaojadili Ufadhili wa Maendeleo (FFD3) , umeanza leo Jumatatu  jijini  Adds Ababa, Ethiopia.

  Ujumbe  Tanzania katika mkutano huu ambao   utakafanyika kwa siku tatu unaongozwa na  Waziri wa   Fedha  Mhe. Saada Mkuya  Salum (pichani) akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe.  Jakaya Mrisho Kikwete. 
  Mhe.  Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum atauhutubia mkutano huo  siku ya  Jumanne Julai 14, 2015. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0
  0 0


  0 0


  0 0

   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, akiweka saini kwenye Kitabu cha Wageni Ofisini kwa Balozi wa Tanzania, Uingereza, jijini London mwishoni mwa juma.
   Katibu Mkuu Kiongozi, Mheshimiwa Ombeni Sefue, akizungumza na Maafisa wa Ubalozi, alipotembelea Ubalozini hapo. Mheshimiwa Katibu Kiongozi alikuwa nchini Uingereza katika Ziara yake ya kikazi ambayo iliandaliwa na Taasisi ya ESAMI kuhudhuria semina ambayo ilikuwa na lengo la kuwakutanisha Viongozi wa Vyama vya Siasa na Watendaji wa Serikali, kuangalia changamoto mbalimbali ambazo wanakumbana nazo na muingilio wake katika utendaji wa kazi zao za kila siku.
   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiwa pamoja na Balozi wa Tanzania, Uingereza, Mhe. Balozi Peter Kallaghe, kwenye Ofisi za Ubalozi Tanzania London, Uingereza.
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (waliokaa-kushoto) na Balozi wa Tanzania Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe (waliokaa-kulia), wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa wa Ubalozi. Mheshimiwa Katibu Mkuu Kiongozi alitembelea ofisi hizo za Ubalozi na kupata nafasi ya kuzungumza na Maafisa hao mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi nchini Uingereza. Picha na Rashid Dilunga


  0 0

  Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015. Katika kipindi hiki utasikia mahojiano yetu na watu mbalimbali akiwemo Katibu Uenezi na Itikadi wa CCM Ndg. Nape Nnauye kuhusu DEMOKRASIA kuelekea uchaguzi nchini Tanzania
  KARIBU


  0 0

  Na Khamis Haji, Milan Italy Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amefungua milango kwa wafanyabiashra na wawekezaji wa Ulaya kutumia fursa nzuri za uzalishaji wa biashara za viungo na utalii nchini ili kuweza kufungua miradi yao. 
  Amesema kwa miaka mingi Zanzibar imejulikana kama visiwa vya viungo (Spice Islands) kutokana na utajiri mkubwa wa mazao hayo, hali ambayo imechangia kukua kwa soko la utalii na kuimarisha uchumi wake. 
  Maalim Seif amesema hayo alipokuwa akihutubia katika maadhimisho ya siku ya Tanzania, kwenye maonyesho ya kibiashara ya kimataifa yanayofanyika mjini Milan Italy, ambapo zaidi ya nchi 140 zinashiriki. 
  Amesema sekta ya kilimo cha viungo kama karafuu na bidhaa nyengine zinazozalishwa Zanzibar na Tanzania Bara, ni eneo linaloweza kupewa kipaumbele na wafanyabiashara hao na kuweza kuwanufaisha wananchi wa Tanzania ambao wengi wao ni wakulima. 
  Katika sekta ya utalii Maalim Seif ambaye anamuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwenye maonyesho hayo amesema, vivutio vilivyopo Tanzania ikiwemo Mji Mkongwe wa Zanzibar, Mlima Kilimanjaro, mbuga za wanayama na fukwe, imeifanya Tanzania kuwa nchi ya kipekee. 
  “Tanzania tuna utajiri mkubwa wa rasilimali, tunayo gesi na mafuta, madini mbali mbali ikiwemo Tanzanite, mazingira bora kwa kilimo na vivutio vya utalii. Nakuombeni tumieni fursa hizi kuja kuwekeza”, amesema Maalim Seif. Ameishukuru Serikali ya Italy kwa kuandaa maonyesho hayo na kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi washiriki, na kwamba kitendo hicho kinadhihirisha uhusiano mwema uliopo kati ya Italii na Tanzania. 
  Mapema akizungumza kwenye maonyesho hayo, Mkurugenzi Mkuu wa maonyesho hayo ya Milan 2015 Bw. Bruno Antonio Pasquino ameelezea kuridhishwa na ushiriki wa Tanzania kwenye maonyesho hayo, pamoja mazingira mazuri ya uwekezaji. 
  Amesema ushiriki huo ni fursa nzuri kwa Tanzania kuweza kujitangaza kwa mataifa mbali mbali yanayoshiriki maonyesho hayo, ili hatimaye wawekezaji waweze kuvutika na kuelekeza miradi yao nchini Tanzania. 
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa maonyesho hayo ya Milan 2015 Bw. Bruno Antonio Pasquino mara alipowasili.
   Maalim Seif na ujumbe wake pamoja na wenyeji wake wakijiandaa kuelekea kwenye maonyesho ya kimataifa ya biashara Mjini Milan Italy

   Maalim Seif na wenyeji wake akielekea kwenye maonyesho ya kimataifa ya biashara Mjini Milan Italy
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia washiriki wa maonyesho hayo wakati wa kuadhimisho siku ya Tanzania kwenye maonyesho hayo mjini Milan Italy. Picha zote na Salmin Said, Italy

  0 0  By Dr. N. T. Jiwaji,

  ntjiwaji@yahoo.com

   This month once again thousands of eyes will be turned upwards in the west horizon looking for a sacred celestial body.  The Moon is the closest celestial body and continually in our eyes at night shifting position and changing shape as it orbits the Earth. 
  The sight of one particular shape, the First Crescent marks the beginning of the month in many cultures that use the lunar calendar. Muslims will be awaiting the First Crescent to mark the end of Ramdhan fasting and celebrate Idd the following day.  
  This month the First Crescent is expected to occur on either Thursday 17th or Friday 18th July.  
  There is uncertainty in our ability to see the First Crescent because it is a very thin crescent that appears very close to the west horizon within the glowing atmosphere around the just set Sun. To read more CLICK HERE

  0 0


  0 0

   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akipeana mikono  na mmoja kati ya wafanyabiashara wa Italia huku baadhi ya wajumbe wa Tanzania wakishuhudia.
    Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, akiwasilisha taarifa inayohusu fursa za uwekezaji nchini Tanzania kwenye kongamano la wafanyabiashara na wawekezaji nchini Italia.
   Baadhi ya washiriki wa kongamano la wafanyabiashara na wawekezaji kwenye maonyesho la biashara ya Milan Italia lililofunguliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, wakifuatilia ufunguzi huo.

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza kwenye ufunguzi wa kongamano la wafanyabiashara na wawekezaji mjini Milan Italia. 
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyabiashara na wawekezaji wa Italia. Kushoto ni balozi wa Tanzania nchini Italia Dkt. James Alex  Msekela na kulia ni waziri wa biashara wa Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akibadilishana mawazo na mmoja kati ya wafanyabiashara wa Italia pamoja na ujumbe aliofuatana nao, baada ya kufungua kongamano la wafanyabiashara na wawekezaji, kwenye maonyesho ya biashara ya Milan nchini Italia. Picha na Salmin Said, OMKR Italy

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media group Joseph Kussaga akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tanzania Breweries Limited Roberto Jarrin wakati alipotembelea ofisi za Clouds zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tanzania Breweries Limited, Roberto Jarrin (kushoto) katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa clouds Media group Joseph Kussaga (katikati kwa waliokaa) kulia kwake ni Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Ruge Mutahaba na kushoto ni Mkurugenzi wa Media wa kampuni ya Aggrey&Clifford wakati alipofanya ziara kwenye ofisi za Clouds zilizopo Mikocheni ijini Dar es Salaam.
   Ujumbe wa kampuni ya TBL ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Robert Jarrin ukipkelewa atika ofisi za ITV eneo la Mikocheni jijini Dar es Saaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya The Guardian Limited Richard Mgamba (Kushoto) akisalimana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) Roberto Jarrin (kulia) wakati alipotembelea ofisi za kampuni ya The Guardian zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Je. Unasumbuliwa  na  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu wa  nguvu  za  kiume ?
   Unahitaji     tiba   ya  uhakika    kwa  ajili   ya  tatizo  lako  ?

  KAMA   JIBU  LAKO  NI  NDIO  BASI  HII  NI  
  HABARI   NJEMA  SANA  KWAKO.

  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL   FOODS  CLINIC   ni  duka  la   kuuza  dawa  mbalimbali  za  asili.

  Tunakujulisha  kuwa tunayo  dawa  asilia  iitwayo   JIKO  ambayo  inatibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la  UKOSEFU  NA  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME  .

  Dawa  ni  ya  asilia  kabisa  ( PURE  HERBAL ), isiyo  na  kemikali  za  viwandani   na  
  INATIBU  NA  KUPONYESHA  KABISA  
  tatizo  la ukosefu  na  upungufu  wa  
  nguvu  za kiume  ndani  ya  siku  thelathini.
  BEI  YA  DAWA  HII  NI  TSHS.80,000/= tu.

  Tunapatikana  jijini  DAR  ES  SALAAM  katika  eneo  la  
  TABATA  MAKOKA  karibu  na  Shule  ya  
  Sekondari  ya  Mtakatifu  Annuarite.

  Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini, tunayo  huduma  ya  kuwafikishia  dawa  mahali  walipo ( FREE  DELIVERY  )  .  
  Kwa  wateja  waliopo  Zanzibar, tunatumia  dawa  kwa njia  ya  usafiri  wa  
  boti  na  kwa  wateja  waliopo  ughaibuni  (DIASPORA)  
  tunawatumia  dawa  kwa  
  njia  ya  POSTA  au  DHL.

  KUFAHAMU  JINSI   NA  NAMNA  
  DAWA  YA  JIKO  INAVYO  FANYA  
  KAZI, TAFADHALI  TEMBELEA :


  NA  KWA  MAHITAJI  YA  DAWA  YA  JIKO, WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  0766  53  83  84.

older | 1 | .... | 904 | 905 | (Page 906) | 907 | 908 | .... | 3272 | newer