Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

MDAU JOHN CHACHA AMPONGEZA DKT JOHN MAGUFULI KWA USHINDI WA KUIPEPERESHA BENDERA YA CCM KUWANIA URAIS 2015

0
0

Mgombea uraisi kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi -CCM Dkt John Magufuli akipongezwa na mwandishi mwandamizi wa kituo cha ITV na Radio one John Chacha siku chache kabla ya Dkt Magufuli kuchukuwa fomu ya kutia nia kugombea nafasi ya Urais kupitia chama cha CCM,ambapo aliagana na mwandishi huyo akiwa njiani kuelekea mikoa ya Geita,Mwanza na Kagera.

Pichani ilikuwa ni nje ya ofisi za CCM makao makuu mjini Dodoma,John Chacha anamtakia kila lakheri na afya njema katika safari yake ya kuipeperusha bendera ya chama chake katika kuwania nafasi ya Urais katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika hapo baadae mwaka huu 2015.


VACANCIES @ International Engineering Company based in Dar-es-salaam

0
0
An International Engineering Company based in Dar-es-salaam is seeking local talents to fill four sales position of which two are in Renewable Energy and two in Industrial Engineering.  All applicants will be going through a series of interviews. Qualified candidates should forward their CV’s to hr@aeg.co.tz 

COMMISSION BASED SALES POSITIONS:
·       To research sources for developing prospective customers and for information to determine their potential.
·       To establish, to develop and to maintain business relationships with current customers and prospective customers and to generate new business for the organization’s products/services.
·       To make telephone calls and in-person visits and presentations to existing and prospective customers.
·       To Develop clear and effective written proposals/quotations for current and prospective customers.
·       To expedite the resolution of customer problems and complaints.
·       To coordinate sales efforts with marketing, sales management, accounting, logistics and technical service
·       To demonstrate products and services to existing/potential customers and assists them in selecting those best suited to their needs.
·       Must be able to meet set sales targets

QUALIFICATIONS AND REQUIREMENTS:
·       Must posses at least one year experience in the sales and marketing. Solar sales or industrial experiences preferred
·       Engineering/Marketing degrees preferred
·       Possession of a post-secondary is a Must. University degree or equivalent
·       MUST demonstrate aptitude for problem solving; ability to determine solutions for customers is preferred
·       Must be result-orientated and able to work both independently and within a team environment.
·       Must posses’ excellent verbal and written communication skills.
·       Proficiency in using Microsoft Office Suite applications is preferred
·       Must be proficient in both English and Kiswahili
Must be authorized to work in Tanzania

Timu ya Jimbo la Mkunazini Yaingia Nusu Fainali Kombe la Bonaza la Masauni Cup Unguja

0
0
Kikosi cha timu ya Mwembeladu kilicho shindwa kumaliza mchezo wao wa mwisho na timu ya Mkunazini timu hii ilihitaji ushindi wa mabao 3--0 ili kuweza kusonga mbele ya Bonaza hilo kuingia nusu fainali, mchezo huo umemalizi kabla ya wakati wake zikiwa zimebaki dakika 4 mchezo kumalizika.  
Kikosi cha timu ya Mkunazini kinachotinga Nusu Fainali  usiku wa kuamkia leo  katika viwanja vya Mnazi Mmoja na Timu ya Kikwajuni Juu. Picha zaidi BOFYA HAPA

Priscus Tarimo atangaza rasmi nia ya kugombea udiwani jimbo la Moshi mjini

0
0
Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Priscus Tarimo akizungumza wakati wa mkutano wake wa na wakazi wa kata ya Kilimanjaro, katika Manispaa ya Moshi akieleza mambo mbalimbali aliyotekeleza wakati wa kipindi chake cha Udiwani na kutumia nafasi hiyo kutangaza nia ya kugombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini.

MWENYEKITI WA BAVICHA AMVAA MCHUNGAJI MSIGWA UBUNGE IRINGA MJINI

0
0
MWENYEKITI wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), Leonce Marto amechukua fomu ya kuwania ubunge katika jimbo la Iringa kupitia chama chake hicho.
Amechukua fomu hiyo siku moja tu baada ya Rais Jakaya Kikwete kulihutubia  bunge la 10 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo uhai wake utakoma Agosti 20, mwaka huu.
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, jimbo la Iringa Mjini limekuwa likiongozwa na Mchungaji Peter Msigwa ambaye pia alichaguliwa kupitia Chadema katika uchaguzi wa 2010.
Kwa kupitia taarifa yake aliyoisambaza kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii jana, Marto alisema;  “nawasalimu nyote wenye mapenzi mema na Taifa letu la Tanzania na wapenda mabadiliko na demokrasia za ushindani ndani ya vyama vya siasa kwa minajili ya katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 .”

MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM, EDMUND RUTARAKA ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MOSHI MJIN

0
0
Naibu Kamanda wa Vijana wa CCM Manispaa ya Moshi na mjumbe wa NEC ,Edmund Rutaraka akizungumza na wajumbe wa Halmshauri kuu  CCM ya wilaya ya Moshi mjini wakati wa kutangaza nia kugombea ubunge jimboni humo.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Magavilla on UBISHI Episode 4 - Mwananchi/ The Composition Challenge

0
0
The ‘composition’ challenge discussed on ‘UBISHI’
One of the great opportunities that we have in accelerating the fortunes of this great country is addressing, what I like to refer to as, our ‘composition’ challenge; what kind of people make up our populous, in particular our youth, in terms of skills, competencies and values.
If you are making strides in life and form part of the top echelons of society, the plight of the bottom of the food chain may not be of particular interest to you – think again!
Irrespective of its composition, the broad bottom will always carry the narrow top.  The masses, at large, are either consumers of the products that keep our companies running and or are the ones casting the votes that inform who will lead our country.
Are you still not interested in the plight of broad bottom?
I reflect briefly on this in this week’s Ubishi Talk Show series

For more visit www.magavilla.com/videos  
 Regards, Magavilla, Costantine aka Kifimbo 
 Twitter/Instagram: cmagavilla FB/Linkedin: costantine magavilla

DKT. JOHN POMBE MAGUFULI NDIE MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM, MH. SAMIA SULUHU KUWA MGOMBEA MWENZA

0
0
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikumbatiana na Dkt. John Pombe Magufuli, mara baada ya kutangazwa kuwa ndiye Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, mchana huu hapa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Dodoma Convition Centre, Mjini Dodoma. Dkt. Magufuli ameibuka kidedea kwa jumla ya kura 2104, wakati wapinzani wake Amina Salum Ally, akiibuka na kura 253 na Dkt. Asha-Rose Migiro, akipata kura 59. Viongozi wakuu wameenda kwenye kikao hivi sasa cha kujua nani atakuwa Mgombea Mwenza wa Urais. hivyo tutaendelea kuwajuza zaidi, endelea kuwa jirani na Libeneke lako pendwa la Globu ya Jamii.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Dkt. John Pombe Magufuli kuwa ndie Mgombea Urais wa CCM.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgombea Mwenza wake, Mh. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kumtangaza, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Dodoma Convetion Centre, Mjini Dodoma mchana huu.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Mgombea Mwenza wake, Mh. Samia Suluhu Hassan wakati akimtambuliasha kwa wanaCCM na Watanzania.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mh. Samia Suluhu Hassan akipongezwa na Spika wa Bunge, Mh. Anne Makinda pamoja na viongozi wengine. Kushoto ni Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda.

NEWS ALERT: WATU KADHAA WAUWAWA, SILAHA ZAPORWA BAADA YA MAJAMBAZI KUVAMIA KITUO KIDOGO CHA POLISI CHA SITAKISHARI, UKONGA, JIJINI DAR ES SALAAM USIKU HUU

0
0
Habari zilizotufikia chumba cha habari  zinasema kwamba watu kadhaa wameuwawa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, baada ya kuvamia kituo kidogo cha Polisi cha Sitakishari, Ukonga jijini Dar es salaam usiku huu.

Habari ambazo hazijathibitishwa zinasema kwamba askari polisi kadhaa kituoni hapo pamoja na raia mmoja wameuwawa. Silaha kadhaa pia inasemekana zimeporwa na askari wako eneo la tukio hivi sasa.

Tunaendelea kufuatilia taarifa hii na tutawajuza maendeleo yake kadri tutapopata fununu zaidi.


MKUTANO WA 12 WA WAKUU WA UTUMISHI WA UMMA WA NCHI ZA AFRIKA WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA KUFUNGULIWA LEO DAR ES SALAAM

0
0
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue akiongoza kikao cha maandalizi ya Mkutano wa  kumi na mbili (12) wa Wakuu wa Utumishi wa Umma wa nchi za Afrika Wanachama wa Jumuiya ya Madola  utakaofunguliwa leo katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre jijini  Dar es salaam
 Katibu Wakuu na watendaji mbalimbali wakijadili wakati wa kikao: kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu . Dkt. Florens Turuka, akifuatiwa na Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimneti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu na Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhem James Meru
Taswira ya moja ya eneo mkutano wa Wakuu wa Utumishi Barani Afrika utakapofanyika.

SIMU TV: MAGAZETINI LEO

ASKARI WANNE WA JESHI LA POLISI NA RAIA WATATU WAPOTEZA MAISHA KATIKA TUKIO LA UJAMBAZI JIJINI DAR

0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu akizungumza na waandishi wa habari leo katika kituo cha Stakishari Ukonga jijini Dar es Salaam, kutokana na Askari wa Jeshi la Polisi  na raia wa eneo hilo kuuwawa na majambazi waliovamia katika kituo hicho usiku wa kuamkia leo. 
Viongozi wa Jeshi la Polisi nchini wakiongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu, wakitembelea maeneo mbalimbali ambayo majambazi walidhuru, katika kituo cha Stakishari Ukonga jijini Dar es Salaam leo.

Na Bakari Issa
ASKARI wa nne wa Jeshi la Polisi na raia watatu wamefariki dunia  katika tukio la ujambazi lililotokea katika kituo cha Polisi cha Stakishari kilichopo Ukonga jijini Dar es Salaam.

Katika tukio hilo watu wapatao nane wamesadikika kuingia katika kituo hicho cha Polisi eneo la Stakishari majira ya saa 4 usiku wa kuamkia leo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu amesema lengo la la watu hao ni kutaka kuiba silaha zilizokuwa katika kituo hicho cha Stakishari.

Aidha, amesema wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa zinazohusu uharifu kwa Jeshi la Polisi.

Pia, kuhusu uvamizi wa Majambazi, Mangu amesema watajitahidi kuanza kuimarisha ulinzi kwa upande wao hususani katika vituo vya Polisi ndiyo baadae kwenda kuimarisha usalama wa  wananchi.

MICHUANO YA KAGAME KUANZA JUMAMOSI

0
0
 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - RELEASE NO. 121
TAREHE 13 JULAI 2015
Michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa Kagame Cup) inatarajiwa kuanza kutimua vumbi siku ya Jumamosi tarehe 18 Julai 2015 jijini Dar es salaam, kwa kushirikisha timu 13 kutoka nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka kwa Nchi za Afrika Mashariki na kati.

Mashindano ya CECAFA Kagame Cup ni mashindano makongwe barani Afrika ambayo yalianza mwaka 1967 kwa kushirikisha timu za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, na mwaka huu ni mashindano ya 40 tangu kuanza kwa michuano hiyo

Klabu ya Simba ndio timu inayoongzoa kwa kutwaa ubingwa huo mara sita (6) ikifuatiwa na Yanga, Gor Mahia zilizotwa mara (5), APR ya Rwanda ikiwa imetwaa ubingwa huo mara tatu (3). Yanga na Gor Mahia zina nafasi ya kufikia Simba SC endapo zitafanikiwa kutwaa Ubingwa msimu huu.

Mechi ya ufunguzi ufunguzi siku ya jumamosi uwanja wa Taifa itawaktanisha APR ya Rwanda dhidi ya Al Shandy ya Sudan saa 8 kamili mchana, KMKM kutoka Visiwani Zanzibar watacheza dhidi ya Telecom ya Djibout  uwanja wa Karume saa 10 jioni, huku wenyeji timu ya Yanga wakiwakaribisha Gor Mahia kutoka Kenya saa 10 jioni.

Kuelekea kwenye mashindano hayo, waandaji wa michuano hiyo CECAFA kwa kushirikiana na wenyeji Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza viingilio vya michezo hiyo, ambapo Uwanja wa Karume kiingilio kitakua shilingi elfu mbili (2,000) na uwanja wa Taifa kiingilio cha chini kitakua ni shilingi elfu tano (5,000) na kiingilio cha juu ni elfu 20,000 (20,000).

Timu zinazoshiriki michuano hiyo
Kundi A: Yanga (Tanzania Bara), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djibout), KMKM (Zanzibar), Khartoum-N (Sudan).
Kundi B: APR (Rwanda), Al-Shandy (Sudan),LLB AFC (Burundi), Heegan  FC (Somalia).
Kundi C: Azam FC (Tanzania), Malakia (Sudan Kusini), Adama City (Ethiopia) na KCCA (Uganda).

Michuano hiyo ya CECAFA Kagame Cup itaonyeshwa moja kwa moja na kituo cha luninga cha Supersport.

UCHAGUZI TWFA
Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Soka cha Wanawake chini (TWFA) inatangaza kuwa wafuatao wamepita katika mchujo wa awali katika nafasi walizoomba kama ifuatavyo:
1.   Amina Ali Karuma  - Mwenyekiti
2.   Devotha John Marwa – Mwenyekiti
3.   Cecilia Makafu – Katibu Msaidizi
4.   Somoe Roberst Ng’itu – Katibu Msaidizi
5.   Debora Ernest Mkemwa – Mjumbe Kamati ya Utendaji
6.   Mwanaheri Kalolo – Mjumbe Kamati ya Utendaji
7.   Theresia Reginald – Mjumbe Kaamti ya Utendaji

Hivyo mtu yeyote mwenye pingamizi anaombwa aliwasilishe katika ofisi za TFF – Karume kuanzia tarehe 15/07/2015  mpaka 20/07/2015.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

UCHAKAVU WA MAJENGO YA SHULE TISHIO KWA WANAFUNZI

0
0

 Jengo la shule ya msingi Donyonaado.

 Na Woinde Shizza,Monduli
Wakati shule nyingi nchini zinafunguliwa baada kumalizika kwa likizo
Wanakijiji wa kijiji cha Donyonaado kilichopo wilaya ya Monduli mkoani
Arusha wameeleza wasi wasi juu ya uchakavu wa jengo la shule ya Msingi
Idonyonaado huenda linaweza kuanguka na kusababisha maafa kwa
wanafunzi.

Shule hiyo iliyoko umbali wa kilomita 64  kutoka Monduli mjini
iliyojengwa kwa udongo na mawe na wanakijiji waliojitoa haina milango
na madirisha hivyo wanafunzi kupata adha ya vumbi na baridi  kali hasa
kipindi cha mvua.

Wanakijiji hao wamesema kuwa  hali mbaya  ya miundombinu ya shule hiyo
imewafanya wazazi wengi kusita  kuwapeleka watoto mashuleni  hivyo
ameiomba serikali na mashirika binafsi yajitokeze kusaidia kutatua
changamoto hizo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Donyonaado ,Malulu Kutetei amesema kuwa licha
ya changamoto za shule hiyo bado wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa
nyumba bora za walimu pamoja na uhaba wa maji jambo linalokwamisha
maendeleo ya taaluma shuni hapo.

Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Wafugaji la Monduli
Pastodalist Development Initiative (MPDI) ,Erasto Sanare ameeleza
kusikitishwa na changamoto zinazoikabili shule hiyo hivyo kushiriki
katika  ujenzi wa shule ya kudumu ,ameieomba serikali isaidia shule
hiyo ambayo ni tegemeo kwa wafugaji.

Licha ya Jamii ya Wafugaji kuamka katika masuala ya elimu tofauti na
miaka iliyopita bado kuna mazingira duni ya elimu ikiwemo kukosekana
kwa shule za kutosha,miundombinu mibovu,uhaba wa maji na vifaa vya
kufundishia na nyumba za walimu

WATAKWIMU WA NCHI ZA AFRIKA WASISITIZWA KUZINGATIA WELEDI NA UWAZI

0
0
 Mwakilishi wa Benki ya Afrika (ADB) nchini Tanzania Tonia Kandiero akizungumza na washiriki wa Warsha  ya Kimataifa ya Watakwimu kutoka nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya kiingereza juu ya ushiriki wa ADB katika masuala ya Takwimu katika Bara la Afrika leo jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. albina Chuwa akiwakaribisha nchini Tanzania washiriki wa mkutano wa kimataifa wa Watakwimu kutoka nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya kiingereza leo jijini.Washiriki wa Warsha hiyo wanajadili na kubadilishana uzoefu kuhusu Pato la Taifa.
 Naibu Mkuu, Wizara ya Fedha Prof.  Adolf Nkenda akifungua warsha ya siku 5 ya watakwimu kutoka nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya kiingereza uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Washiriki wa Warsha hiyo ya kimataifa ya Watakwimu kutoka nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya kiingereza wakiwa katika picha ya pamoja leo jijini Dar es salaam.


Na.Veronica Kazimoto- Dar es salaam.
SERIKALI imesema kuwa itaendelea kuongeza uwazi katika matumizi ya takwimu zinazokusanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini ili kukidhi vigezo na malengo ya mfumo mpya uliowekwa na Umoja wa Mataifa wa mwaka 2008 wa upataji wa takwimu za pato la Taifa.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Warsha ya kimataifa ya siku 5 ya watakwimu kutoka nchi za Afrika zinazozungumza Kiingereza, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha Prof. Adolf Nkenda amesema kuwa Tanzania inaendelea kukusanya takwimu mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya watunga Sera na wananchi.

Amesema kwa kutambua na kuthamini mchango wa takwimu katika maendeleo, Serikali imeamua kuingiza takwimu za ubora wa mazingira na takwimu za matumizi ya simu za mkononi kwenye Pato la Taifa.

Amefafanua kuwa, mabadiliko hayo yataiwezesha Tanzania kuwa na takwimu zenye uhalisia kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanyika nchini na mchango wake katika Pato la Taifa.

Prof. Nkenda ametoa wito kwa washiriki wa warsha hiyo kuendelea kuzingatia weledi katika utekeleaji wa majukumu yao ili waweze kutoa takwimu sahihi zinazoonesha hali halisi ya tafiti zinazofanyika katika nchi zao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)   Dkt. Albina Chuwa  akizungumza na washiriki wa Mkutano huo wa Kimataifa amesema kuwa Nchi za Afrika zinahitaji Takwimu sahihi ili ziweze kuendelea.

Amesema Tanzania imepiga hatua kwa kuweka kipaumbele katika shughuli mbalimbali za Takwimu ikiwemo kusaini mkataba wa Takwimu wa Afrika kuhusu kuongeza uwazi katika upatikanaji na matumizi ya takwimu  zilizopo kwa Maendeleo ya Taifa.

Ameeleza kuwa kupitia Mfumo mpya wa Umoja wa Mataifa wa kutengeneza Pato la Taifa wa mwaka 2008, Tanzania imefanikiwa kuingiza shughuli mbalimbali katika Pato la Taifa ambazo hapo awali hazikuwemo, zikihusisha shughuli za kitaalam za Sayansi na Teknolojia pamoja na sanaa.

Ili kufanikisha shughuli za takwimu Barani Afrika Dkt. Chuwa ameziomba Serikali zote za Afrika kuutumia na kuheshimu Mkataba wa Afrika wa Takwimu wa mwaka 2008 unaotoa kipaumbele katika uboreshaji wa shughuli za Takwimu.

"Napenda kutumia fursa hii kuziomba Serikali za Afrika kuzijengea uwezo Ofisi za Takwimu ili ziwe na uwezo wa kuzalisha takwimu za masuala mbalimbali kwa muda mfupi maana Takwimu ni sasa kwa ajili ya kukidhi mahitaji na matarajio ya wananchi", amesisitiza Dkt. Chuwa.

Aidha, ameongeza kuwa warsha hiyo ya siku 5 ambayo imewajumuisha watakwimu kutoka nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na baadhi ya nchi za Afrika Magharibi zikiwemo Ghana na Nigeria inalenga kuwajengea uwezo washiriki hao kwa kuwa na uelewa wa pamoja katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za Takwimu katika nchi zao.

Naye Mwakilishi wa Benki ya Afrika (ADB) nchini Tanzania Bi.Tonia Kandiero amewataka washiriki wa warsha hiyo kuzingatia mfumo uliowekwa wa upataji wa takwimu za Pato la Taifa ili kuwezesha uwepo wa takwimu sahihi za maendeleo ya nchi husika.

Amesema kuwa wingi wa washiriki wa warsha hiyo waliohudhuria kutoka nchi mbalimbali za Afrika ni ishara tosha kuwa nchi zao zinathamini mchango wa Takwimu katika kuleta maendeleo.

Amesema Benki ya Afrika ambayo yeye ni mwakilishi wake itaendelea kushirikiana na nchi za Afrika ili kuhakikisha kuwa Takwimu mbalimbali zikiwemo za Watu na Makazi, Pato la Taifa na nyinginezo zinapatikana kwa wakati na kuchangia maendeleo ya Afrika.

Article 20

0
0
First Secretary from the Embassy of the People’s Republic of China, XU Jingchun (r) handing over a checque amounted to USD 10,000 to Newala district for the construction of a ward at Kitangari hospital in Newala district in Mtwara yesterday.

MKUTANO WA 12 WA WAKUU WA UTUMISHI WA UMMA WA NCHI ZA AFRIKA WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA K U FUNGULIWA LEO

0
0
om1
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue akiongoza kikao cha maandalizi ya Mkutano wa  kumi na mbili (12) wa Wakuu wa Utumishi wa Umma wa nchi za Afrika Wanachama wa Jumuiya ya Madola  utakaofunguliwa leo
om2
Taswira ya moja ya eneo mkutano wa Wakuu wa Utumishi Barani Afrika utakapofanyika
om3

Katibu Wakuu na watendaji mbalimbali wakijadili wakati wa kikao: kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu . Dkt. Florens Turuka, akifuatiwa na Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimneti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu na Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhem James Meru

Danny Bulenge: Naweza kumsindikiza Mwaitege

0
0
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama
 
MUIMBAJI wa Muziki wa Injili anayekuja kasi katika muziki huo, Danny Bulenge amesema anakidhi kuwa mmoja wa watakaomsindikiza mwenzake Bonni Mwaitege uzinduzi unaotarajia kufanyika Agosti 2 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Bulenge anakidhi kumsindikiza Mwaitege anayetarajia kuzindua albamu tatu ambazo ni moto wa kuotea mbali katika muziki huo.
Bulenge alisema hivi sasa anaendelea na mazoezi kwa lengo la kufikisha ujumbe wa neno la Mungu na kuahidi kusindikiza vilivyo albamu hizo tatu kwa staili ya aina yake.
 
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama, Bulenge ni mmoja wa wataungana na Mwaitege katika uzinduzi huo.“Uzinduzi  wa  albamu tatu za Bonny Mwaitege unatakiwa kufanyika kwa maandalizi ya hali ya juu ambayo yanafanyika kwa mfumo  wa kisasa,” alisema Msama na kuongeza.
 
“Uzinduzi wa Mwaitege utakuwa ni wa aina yake kwa sababu maandalizi yake kwa yamefanywa kwa ustadi mkubwa  hasa hatua za mwisho za rekodi ya albamu hizo inayomaliziwa  jijini Mwanza na baadaye Nairobi,” alisema Msama.
 

Msama alisema sambamba na muimbaji huyo, mikoa mbalimbali imeonesha nia ya kutaka uzinduzi wa albamu hizo. Aidha Msama alitoa wito kwa mashabiki wa muziki wa Injili Tanzania kujiandaa kupata neno la Mungu kupitia muimbaji huyo. Bonny Mwaitege anatamba na nyimbo mbalimbali kama Mama ni Mama, Mke mwema, Wakusamehe, fungua moyo wako na njoo uombewe na Yesu yupo.

GGM Kili Challenge takes 38 Climbers to Uhuru Peak in the Fight Against HIV/AIDS

0
0
 Executive Chairperson from TACAIDS, Dr. Fatma Mrisho, addressing the media (not in picture) at the Reception of the 39 Heroes who climbed Mt. Kilimanjaro at Mweka Gate in Moshi, Tanzania for the 14th year of Kilimanjaro Challenge which has this year raised about TZS 1.2B funds to fight against HIV/AIDS in Tanzania.
 13 year old Susan Elias, from Moyo wa Huruma Orphanage centre in Geita reached Uhuru Peak thus receiving her certificate from the Regional Administrative Secretary Hon. Severine Kahitwa joined by Vice President Geita Gold Mine (GGM), Simon Shayo and Executive Chairperson from TACAIDS, Dr. Fatma Mrisho during the Reception of the 39 Heroes who climbed Mt. Kilimanjaro at Mweka Gate in Moshi, Tanzania for the 14th year of Kilimanjaro Challenge which has this year raised about TZS 1.2B funds to fight against HIV/AIDS in Tanzania.
 Kili Challenge Ambassador from South Africa's Rugby team Mr. Krynauw Otto reached Uhuru Peak thus receiving his certificate from the Regional Administrative Secretary Hon. Severine Kahitwa joined by Vice President Geita Gold Mine (GGM), Simon Shayo and Executive Chairperson from TACAIDS, Dr. Fatma Mrisho during the Reception of the 39 Heroes who climbed Mt. Kilimanjaro at Mweka Gate in Moshi, Tanzania for the 14th year of Kilimanjaro Challenge which has this year raised about TZS 1.2B funds to fight against HIV/AIDS in Tanzania.
 13 year old Michael Lomo, from Moyo wa Huruma Orphanage centre in Geita reached Uhuru Peak thus receiving him certificate from the Regional Administrative Secretary Hon. Severine Kahitwa joined by Vice President Geita Gold Mine (GGM), Simon Shayo and Executive Chairperson from TACAIDS, Dr. Fatma Mrisho during the Reception of the 39 Heroes who climbed Mt. Kilimanjaro at Mweka Gate in Moshi, Tanzania for the 14th year of Kilimanjaro Challenge which has this year raised about TZS 1.2B funds to fight against HIV/AIDS in Tanzania.
  A team of 38 Heroes who reached Uhuru Peak arrived safely at the foot of Mweka Gate in Moshi, Tanzania for the 14th year of Kilimanjaro Challenge which has this year raised about TZS 1.2B funds to fight against HIV/AIDS in Tanzania.

TAMASHA LA NCHI ZA JAHAZI 2015 KUFANYIKA NGOME KONGWE ZANZIBAR KUANZIA JULAI 18 HADI 26

0
0
 Mjumbe wa bodi wa Tamasha la Jahazi, Fatma Allo (kulia), akizungumza katika mkutano na wadau wa filamu na wanahabari Dar es Salaam leo jioni kuhusu tamasha la nchi za jahazi litakalofanyika kuanzia Julai 18 hadi 26 mwaka huu Ngome Kongwe mjini Zanzibar.Kutoka kushoto ni Meneja wa Tamasha, Daniel Nyalusy na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tamasha la Jahazi, Martin Mhando.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tamasha la Jahazi, Martin Mhando (kushoto), akizungumza kuhusu tamasha hilo kubwa la jahazi. Kulia ni  Mjumbe wa bodi wa Tamasha la Jahazi, Fatma Allo.
 Meza Kuu. Kutoka kushoto ni Mratibu John Mchaina 'Simple', Mratibu Rehema Jonas, Mjumbe wa Bodi, Mahabobo Champs, Daniel Nyalusy, Ofisa Mtendaji Mkuu, Martin Mhando na Mjumbe wa Bodi, Fatma Allo.
HABARI ZAIDI INGIA HAPA
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images