Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

NEWS UPDATES: NEC YA CCM Inapiga kura sasa kupata tatu bora. Saa tatu usiku mkutano unakaa kuamua jina moja

0
0
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari jioni hii juu ya kilichofanyika kwenye Mkutano wa Hamlashauri Kuu ya CCM, ambapo amesema kuwa sasa NEC inapiga kura kupata majina matatu yatakayopelekwa kwenye Mkutano Mkuu unaotarajiwa kufanyika Usiku wa leo majira ya saa tatu, kwenye Ukumbi wa Dodoma Convition Centre.

NEWS UPDATES KUTOKA DODOMA JIONI HII;NI DKT ASHA ROSE MIGIRO,BALOZI AMINA SALUM ALI NA DKT JOHN POMBE MAGUFULI

0
0
 Balozi Amina Salum Ali
 Dkt John Pombe Magufuli
Dkt Asha Rose Migiro.

Pichani ni majina matatu ya wagombea kiti cha Urais kwa chama cha CCM,yaliyopitishwa jioni ya leo na Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM,ambapo kati ya hayo majina matatu kupitia Mkutano Mkuu wa CCM unaotarajiwa kufanyika usiku huu utaibua jina la mtu mmoja tu ambaye  atatambulika kuwa ndiye mgombea kiti cha Urais kupitia chama hicho cha CCM

UKOSEFU WA CHAKULA MASHULENI WACHANGIA UTORO

0
0

 
Na Woinde Shizza,Arusha
Ukosefu wa Chakula sheleni hususan zile zinazomilikiwa na serikali
umetajwa kuwa chanzo kikubwa kinasababisha wanafunzi kutoroka
mashuleni na kwenda kujitafutia chakula hali inayoathiri taaluma na
maendeleo ya elimu nchini.



Mwanakijiji wa kijiji cha Arkata  Kipara Ngine amesema kuwa watoto
wengi wamekua wakitoroka shuleni kwa kukosa chakula hivyo kupelekea
idadi ndogo ya mahudhurio  mashuleni.

Kipara ameihasa saerikali kwa kushirikiana na mashirika binafsi pamoja
na wazazi kuhakikisha upatikanaji wa chakula  katika sahule ya msingi
Arkata iliyopo wilaya ya Monduli mkoani hapa.

Mwenyekiti wa Kamati ya  Shule Kipi Alarosi  amesema kuwa licha ya
changamoto ya utoro bado shule hiyo inakabiliwa na uchakavu wa majengo
na upungufu wa madarasa hivyo ameiomba jamii na wapenda maendeleo
wajitokeze kuiwezesha shule hiyo iweze kufanya vizuri kitaaluma.

“Shule haina madirisha na majengo yamechakaa mvua ikinyesha inaingia
mpaka darasani watoto hawasomi vizuri hata kipindi cha jua vumbi
linajaa darasani “ Alisema Mwenyekiti.

Mkurugenzi wa Shirika la wafugaji Monduli Pastoralist Development
(MPDI) Erasto Sanare  amesema kuwa baada ya kupokea ombi la shule hiyo
watatua fedha za ukarabati wa  madarasa ya shule hiyo ili kuwajengea
watoto mazingira bora.

Alisema mwamko wa jamii ya wafugaji katika masomo umekua kwa kiasi
kikubwa  mashirika na watu binafsi yakijitoa kusaidia kutatua
changamoto zao ili watoto wa wafugaji wapate elimu bora.

FUATILIA MKUTANO MKUU WA CCM LIVE KUPITIA HAPA HAPA GLOBU YA JAMII

TASWIRA MBALIMBALI KUTOKA KWENYE MKUTANO MKUU WA CCM MJINI DODOMA USIKU HUU

0
0
 Meza Kuu ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete tayari kwa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi unaoendelea usiku huu kwenye Ukumbi wa Mikutano wa CCM wa Dodoma Convetion Centre, uliopo njia ya Kuelekea Chuo Kikuu cha UDOM, Mjini Dodoma.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Aliekuwa Mgombea Urais na Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa wakati alipowasili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa CCM wa Dodoma Convition Centre, uliopo njia ya Kuelekea Chuo Kikuu cha UDOM, Mjini Dodoma.
 Baadhi ya Wake wa Viongozi wakiwa kwenye Mkutano huo.
 Mmoja wa Wagombea Urais alieingia kwenye hatua ya tatu bora, Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya wajumbe wa Mkutano huo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na Aliekuwa Mgombea Urais na Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM unaofanyika usiku huu kwenye Ukumbi wa Dodoma Convition Centre, uliopo njia ya Kuelekea Chuo Kikuu cha UDOM, Mjini Dodoma.
 Mmoja wa Wagombea Urais alieingia kwenye hatua ya tatu bora, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya Mabalozi walioalikwa kwenye Mkutano huo.

SPORTS XTRA NDONDO CUP YAZINDULIWA RASMI, ABAJALO, FC KAUZU MUZIKI WAO..OGOPA SANA!

0
0
3Baada ya kuisubiri kwa muda mrefu burudani hii adimu! Sasa utamu umewadia!!

Msimu wa pili wa mashindano ya Sports Xtra Ndondo Cup chini ya udhamini wa Dr. Mwaka, Daktari bingwa wa masuala ya Afya ya uzazi na Tiba asilia kutoka kituo cha Foreplan Clinic, kilichopo Bungoni, Ilala, Dar es salaam umezinduliwa rasmi katika uwanja wa Bandari, Tandika, jijini Dar es salaam.

Mechi ya ufunguzi yenye mvuto wa aina yake imepigwa jana ikiwakutanisha mabingwa watetezi, Abajalo FC ya Sinza Dar es salaam dhidi ya timu iliyojizolea Umaarufu ya wauza mitumba wa Tandika, FC Kauzu na hadi dakika 90 zinamalizika wanaume hao wa ‘Shoka’ walitoka suluhu (0-0).
5Sports Xtra Ndondo Cup ni mashindano yenye heshima kubwa kwa sasa na kwa kulitambulia hilo, Mgeni rasmi alialikwa kufungua pazia ambaye ni Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF anayewakilisha mkoa wa Dar es salaam, Wilfred Kidau akiambatana na mwenyekiti wa chama cha soka cha Dar es salaam (DRFA), Almas Kasongo pamoja na mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya Temeke (TEFA), Peter Muhinzi.
4
2Kwa wale ambao hawakushuhudia!, hakika mechi ya ufunguzi ilikuwa nzuri mno ikichagizwa na wachezaji wa ligi kuu wanaokipiga katika michuano hayo, mfano FC Kauzu walimtumia mshambuliaji hatari wa Kagera Sugar, Atupele Green na ngome ya ulinzi iliongozwa na beki wa Mbeya City, Juma Said Nyosso.
7Cha kufurahisha! FC Kauzu wanatumia jezi za Zambarao kama ilivyo kwa Mbeya City FC, hivyo Nyosso alionekana kama anakipiga katika kikosi hicho cha Juma Mwambusi. Abajalo FC wao walikuwa na mtu kama Paul Maona na nahodha wao George Kavila wanaokipiga Kagera.
8
Mashabiki zaidi ya Elfu tano walihudhuria mechi hiyo iliyojaa vitimbwi, mbembwe za kila aina na nimekuwekea baadhi ya picha zikionesha shamrashamra za mashabiki wa Sports Xtra Ndondo Cup Chini ya udhamini wa Dr. Mwaka.
6

Dkt Shein awashukuru wana CCM kwa kumchagua tena kuwa mgombea wa urais Zanzibar na aahidi ushindi wa kishindo.

MWENYEKITI WA CCM RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AFUNGA MKUTANO MKUU WA CCM DODOMA

0
0

Sikiliza hotuba mbalimbali kwenye mkutano 
mkuu wa CCM kwa hisani ya Kwanza Productions.
Bofya link ya buluu chini ya kila kichwa cha habari...

Hotuba Ya Dr Ali Mohamed Shein kukubali kuwa mgombea wa CCM Zanzibar 2015

--------------------------------------------
Hotuba Ya Dr Asha - Rose Migiro kukubali yatokeo ya mkutano Mkuu wa CCM 2015
----------------------------------------------
Hotuba Ya Balozi Amina Salum Ali kukubali matokeo ya mkutano mkuu wa CCM 2015
------------------------------------------------
Hotuba Ya Dr John Pombe Magufuli kukubali kuwa mgombea wa CCM 2015
----------------------------------------------
Hotuba Ya Mwenyekiti Wa CCM Taifa Mhe. Jakaya Kikwete kufunga mkutano mkuu wa chama 2015

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

OPPORTUNITIES ABOUND TO PRODUCE MORE AFRICAN SCIENTISTS IN BAGAMOYO

0
0


Rector of AIMS Tanzania,
Mark Roberts
 The scope for producing more African Scientists will be broadened with the introduction of a highly specialized African Institute for Mathematical Sciences (AIMS) in Tanzania, to be specific in the historic town of Bagamoyo.
Tanzania will be the fifth country in Africa to benefit from the AIMS expertise in delivering postgraduate training to talented students and conducting research on applications of the mathematical sciences. 
Next year, a sixth centre will be established in neighboring Rwanda. The masterplan of the organization, the AIMS Next Einstein Initiative (NEI), is to establish fifteen such institutes across Africa, all nurturing highly trained scientists in a range of specialisms.

AIMS NEI centres are currently also operational in South Africa, Senegal, Ghana and Cameroon. So far 731 high caliber African Scientists from 41 African nations have graduated to take up further academic options, such as PhDs, and to pursue careers in professions such as education, IT and business. 

NEW, GOOD QUALITY PORTABLE ICE CUBES MAKER FOR SALE

0
0
 CALL  O717 4441… OR 0766 0067…

CCM DMV, MAREKANI, YAMPONGEZA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI

0
0
CCM DMV TUNATOA PONGEZI KWA MWENYEKITI WATAIFA NA WAJUMBE WOTE TOKA KAMATI KUU HALMASHAURI KUU MKUTANO MKUU KWA KUTUPATIA MGOMBEA MCHAPAKAZI MAKINI AMBAYE ATAPEPERUSHA BENDERA YA CHAMA CHA, MAPINDUZI OCTOBER MWAKA HUU NA CHAMA KITAPATA USHINDI MKUBWA TUNA IMANI NAYE KUBWA MH JOHN POMBE MAGUFULI HONGERA SANA

Ofisi ya Kambi ya Upinzani Bungeni yaandaa futari wakati wa kikao cha ukawa jijini Dar es salaam

0
0
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Willibroad Slaa akishiriki futari iliyoandaliwa na Ofisi ya Kambi ya Upinzani Bungeni wakati wa kikao cha Viongozi Wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na wabunge wa umoja huo kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam kujadili mikakati mbalimbali ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu. Kushoto kwake ni Mbunge wa CUF, Ali Khamis Seif (Mkoani) na kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa NLD Zanzibar, Ahmad Hemed. 
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe akijadiliana jambo na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Said Issa Mohamed (katikati) pamoja na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Ndelakindo Kessy (kushoto) huku wakishiriki futari iliyoandaliwa na Ofisi ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni wakati wa kikao cha Viongozi Wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na wabunge wa vyama vinavyounda umoja huo kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam kujadili mikakati mbalimbali ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu.
Baadhi ya Wabunge wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kutoka kushoto, Naomi Kaihula (Viti Maalum CHADEMA), Salum Baruan (CUF- Lindi Mjini) na Mohamed Habib Mnyaa wakishiriki futari iliyoandaliwa jana jijini Dar es Salaam na Ofisi ya Kambi ya Upinzani Bungeni, wakati wabunge wa vyama vinavyounda umoja huo waliposhiriki kikao cha Viongozi Wakuu wa UKAWA (Summit) kilichojadili mikakati mbalimbali ya maandalizi ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu




Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar Said Issa Mohamed akijiandaa kuwamiminia uji baadhi ya wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakati wa kula futari. Wabunge hao walikuwa wakihudhuria kikao cha Viongozi Wakuu wa UKAWA kilichofanyika juzi jijini Dar es Salaam kujadili mikakati mbalimbali ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu. Walioketi kutoka kushoto ni Seleman Bungala Bwege (CUF- Kilwa Kusini),Mohamed Habib Mnyaa (CUF-Mkanyageni) na Mama Riziki.

Wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakati wa kula futari. 

WAKAZI WA KWAMTOGOLE-TANDALE JIJINI DAR WANUFAIKA NA KAPU LA PAMOJA NA VODACOM RAMADHANI

0
0
  Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Renatus Rwehikiza (kushoto) akimkabidhi Fatuma Khamis mkazi wa Kwamtogole – Tandale jijini Dar es Salaam (wa tatu toka kushoto) mfuko wa maharage ikiwa ni moja kati ya vyakula mbalimbali alivyokabidhiwa ikiwa ni msaada ulitolewa na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom kwa ushirikiano na Doris Foundation. Wanaoshuhudia Grace Lyon (kulia) na Doris Mollel (wa pili toka kushoto).
 Baadhi ya wakazi wa Kwamtogole – Tandale jijini Dar es salaam wakiwa wanasubiria kugawiwa vyakula mbalimbali vikiwa kwenye vikapu maalum vilivyotolewa msaada na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom kwa ushirikiano na Doris Mollel Foundation kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
 Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Renatus Rwehikiza (kushoto) akiongozana na baadhi ya washirika wenza kutoa msaada wa vyakula mbalimbali  kwa baadhi ya wakazi wa Kwamtogole –Tandale jijini Dar es Salaam kwa ajilli ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Msaada huo ulitolewa na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom kwa ushirikiano na Doris Mollel Foundation.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania pamoja na Doris Mollel  Foundation wakiwa wamebeba vikapu vyenye vyakula mbalimbali kwa ajili ya kutoa msaada kwa wakazi wa Kwamtogole – Tandale jijini Dar es Salaam. Msaada huo ulitolewa na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom kwa kushirikiana na Doris Mollel Foundation kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mkazi wa Kwamtogole –Tandale jijini Dar es Salaam Bi.Taabu Abdallah (kushoto) akikabidhiwa msaada wa vyakula mbalimbali na  Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Renatus Rwehikiza. Msaada huo ulitolewa na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom kwa ushirikiano wa Doris Mollel Foundation kwa ajilli ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

SALASALA VISION GROUP WAKABIDHIWA HATI ZA HEKARI 250 HUKO FUKAYOSI BAGAMOYO PIA YAZINDUA TOVUTI

0
0
Afisa Mtendaji Mkuu EAG Group Iman Kajula (wa pili kulia) akipokea hati ya Kimila ya eneo walilolonunua eneo la Fukayosi, Bagamoyo,  kwa ajili ya Jumuiya hiyo iliyoasisiwa na wakazi wa Kilimahewa Salasala jijini Dar es salaam likiwa na malengo ya kijamii na kiuchumi. Tangu kuasisisiwa SVG imetekeleza miradi Mingi kwenye eneo la Salasala ikiwemo kupanda miti zaidi ya 5,000, kutengeneza barabara, kutengeneza viwanja vya michezo na kulinda maeneo ya wazi, Ulinzi, kutengeneza gari la polisi na misaada ya miradi mbalimbali endelevu ikiwamo kujenga ofisi ya Serikali ya Mtaa Salasala
 
SVG haikuishia hapo, imeamua kwa dhati kuchochea maendeleo ya Wanachama wake. Mradi mkubwa uliotekelezwa ni pamoja na kununua hekari 250 huko Fukayosi Bagamoyo. Baada ya ununuzi huu mchakato wakupata hati ulifanywa na kufanikiwa kupata hati za kimila na kukabidhiwa kwa wanachama wa SVG ili kuanza kuendeleza maeneno hayo.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Afisa Aridhi wa Wilaya ya Bagamoyo Bw.Kibona aliipongeza SVG kwa kuwa kikundi kilicho makini na kutumia dhima ya umoja ni nguvu, alisema hati za kimila zina faida nyingi sana ikiwamo kutokuwa na kipindi cha ukomo ikilinganishwa na hati za kawaida.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa SVG Yahaya Banka alisema ‘’ SVG inalenga kuendelea kuwa chachu ya maendeleo kwa wanachama wake na familia zao. Tunaamini kwa kutumia nguvu ya umoja tunaweza kuleta maendeleo makubwa katika eneo letu tunaloishi pia kwa familia za wanachama’’

African in New York Episode 16

0
0
The Executive Director of the African in New York TV show interviewed Mr. Kenneth Goodwin Jr. the Japanese and Chinese Financial Capital Markets specialist who also talked about the difference between the Chinese and Japanese aid strategies and objectives. 
As Tanzania is one of the major recipients of the Chinese and Japanese foreign aid, this interview teaches something about the difference between the two aid packages. Do you want to know about what Tanzania should expect from these types of Aid? Then watch this interview. 
 Deogratius Mhella 
The Executive Director and Producer 
African in New York

news alert: Mchekeshaji wa Kenya Mzee Ojwanga afariki dunia

0
0

Mwigizaji wa filamu za vichekesho wa Kenya Benson Wanjau maarufu kama Mzee Ojwang (pichani) amefariki dunia Jumapili jioni katika hospitali ya Taifa ya  Kenyatta National alikokuwa amelazwa kwa matibabu. Taarifa kutoka NAirobi zinasema alikuwa anaumwa "Nimonia" (Pneumonia). 
Marehemu Mzee Ojwang alijipatia umaarufu mkubwa Afrika Mashariki kwa vituko vyake kwenye filamu za Vitimbi, Vioja Mahakami, Vituko na  Kinyonga. Alikuwa haonekani kwa muda mrefu kwenye televisheni za Kenya na mashabiki wake wakiwemo wa Tanzania walikuwa hawaishi kumuulizia aliko bila kupata jibu. 
Mola aiweke Mahali pema roho 
ya Mzee Ojwang - Amin.

Maalim Seif Ziarani Italy

0
0
Na Hassan Hamad, Milan, Italy 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amewasili Mjini Milan nchini Italy kwa ajili ya kuanza ziara rasmi ya kiserikali. Katika uwanja wa ndege wa Milan, Maalim Seif amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Italy Dkt. James Msekela. 
Akiwa nchini Italy, Maalim Seif ambaye anamuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa yanayofanyika Mjini Milan, pamoja na mambo mengine atatembelea mabanda ya maonyesho ya Tanzania. 
Aidha anategemewa kufungua kongamano la bishara za Kitanzania litakalotanguliwa na burudani ya kikundi cha sanaa cha Bagamoyo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiongozana na balozi wa Tanzania nchini Italy Dkt. James Msekela, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Milan nchini Italy kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi nchini humo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa na balozi wa Tanzania nchini Italy Dkt. James Msekela, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Milan nchini Italy kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi nchini humo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, na balozi wa Tanzania nchini Italy Dkt. James Msekela, wakiwa pamoja na baadhi ya wajumbe wa ziara hiyo. (Picha na Salmin Said, OMKR, Milan)

Kiota Kipya cha maraha ndani ya Bunju, jijini Dar es salaam

0
0
Posto Bella Resort, Kiota Kipya cha maraha pande za  ya Bunju jijini  Dar es salaam.

Chimbo jipya kwa jina La Posto Bella Resort limefunguliwa nje kidogo ya mji wa Dar. Kwa wale wanaopenda maeneo private, utulivu na salama, hakuna haja ya kuumiza kichwa. 

Kama inavyoonekana kwenye picha, pana garden nzuri iliyotengenezwa kwenye miinuko ya Bunju A, 1.2km toka Bagamoyo road, njia ya kuingia DogoDogo Centre, ikipata upepo baridiii unaotokea bahari ya Hindi. 
Ni mazingira ya kiutu-uzima na kimahaba, hakuna kelele za aina yoyote isipokuwa ndege wanaoruka mitini tuu, hakuna boda boda wala honi za magari. Kwa mazingira ya chimbo hili, anayekutafuta lazima atumie GPS!
Ni muafaka kwa ajili ya watu wanaotafuta privacy kama wapendanao, mikusanyiko ya kifamilia (family gatherings), harusi za watu wachache, sherehe za kiofisi (corporate parties), birthdays, mitoko ya ki-group cha kazini, engagement parties, kitchen parties, na mengineyo mengi. Ukumbi (garden yetu) ni bure, hatutozi hela yoyote. Pia ni mahali muafaka kwa mitoko ya familia kwa ajili ya lunch na dinner siku za weekend.
Bei zetu za vinywaji na chakula ni za kawaida sana. Kwa maelezo zaidi tupigie 0655123695 au email: postobellaresort@gmail.com

Picha zaidi tucheki kwenye facebook page yetu www.facebook.com/PostoBellaResort na kwenye Instagram: @posto_bella. Tafadhali tu-follow kwenye instagram uweze kupata habari za matukio mbali mbali kila mwezi.
Posto Bella is like Nowhere in Dar!
Kijani ya kupendeza yatawala eneo la kiota hicho.

SPORTS HEADQUATER: KIPINDI KIREFU NA MAARUFU CHA MICHEZO KULIKO VYOTE NCHINI

Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images