Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel Catalog



Channel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 88 | 89 | (Page 90) | 91 | 92 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Na Mwandishi Wetu

  NAIBU Spika, Job Ndugai (pichani) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Pasaka Jumamosi Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

  Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa maandalizi kuhusiana na tamasha hilo la Dodoma yamekamilika na kwamba wasanii wanatarajiwa kuwasili mkoani humo leo wakitokea Iringa.

  “Waliohudhuria matamasha ya Dar es Salaam na Mbeya wameona mambo mazuri na leo (jana) tunafanya vitu Iringa, hivyo tumempa heshima Naibu Spika kubariki tamasha letu la Dodoma, naamini mambo yatakuwa mazuri sana,” alisema Msama.

  “Ni matumaini yetu kwamba tamasha litakuwa zuri na kila mtu atafika kuja kuona kile ambacho wasanii wametuandalia,” alisema Msama na kuyataja makundi yatakayotumbuiza kutoka nje ya Tanzania kuwa ni kundi la Ambassadors of Christ ‘Kwetu Pazuri’ la Kigali, Rwanda.

  Wasanii wengine wa nje ya Tanzania watakaotumbuiza tamasha hilo ni Sipho Makhabane wa Afrika Kusini, Ephraim Sekeleti wa Zambia na Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya.

  Msama aliwataja wasanii wa Tanzania watakaopanda jukwaani leo kuwa ni Rose Muhando, Upendo Nkone, Bonny Mwaitege, Upendo Kilahiro, John Lissu, kwaya ya Kinondoni Revival na kundi la Glorious Celebration.

  “Kila msanii amepanga mambo yake kuwafurahisha Watanzania, naamini wengi watajitokeza na kushirikiana katika tamasha letu linalozidi kupanda chati mwaka hadi mwaka,” alisema Msama na kuongeza kuwa tamasha hilo litakamilika Jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

  0 0
 • 04/03/13--02:13: Kinyozi kazini


 • 0 0


  0 0
 • 04/03/13--02:24: SHUKRANI
 • Marehemu Peter Cuthbert Samatta

  Familia ya Mheshimiwa Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas A. Samatta wa Oyster Bay, Dar Es Salaam na Bibi Trinita Samatta wa Singida tunatoa shukrani zetu kwa wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kutufariji katika msiba wa mpendwa wetu Peter Cuthbert Samatta aliyefariki katika Hospital Kuu ya Taifa Muhimbili tarehe 11 Frebruari, 2013 na kuzikwa kwenye Makaburi ya Kinondoni hapa Dar Es Salaam tarehe 14 February 2013.

  Shukrani za pekee ziwafikie wafutao. Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete; Mheshimiwa Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman; Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu; Waheshimiwa Majaji wastaafu; Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe na Mama Membe; Mheshimiwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta na Mama Sitta.

  Menejimenti na Watumishi wa Shirika la Taifa la Bima; Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe; Profesa Mkude; Makamu Mkuu wa Chuo Cha Mzumbe Profesa Joseph Kuzilwa na Makamu wake Maprofesa F. kamuzora na J. S. Itika.

  Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) Bwana Majid Abdo; Menejimenti na Watumishi wa MDH (Management Development for Health); Menejimenti na Watumishi wa ESOS. Madaktari na Manesi wa Mwaisela Wodi Number 08 Hospital Kuu ya Taifa ya Muhimbili na wale Hospital ya Misheni ya Makiungu, Singida.

  Wanachama wa Green Women Group na waume zao; Majirani wa Mtaa wa Bongoyo Oyster Bay na Mitaa inayopakana na Mtaa huo; Majirani wa Oyster Bay Neighborhood Association (CONA); Bibi Elizabeth Mwella; Majirani wa Familia ya Marehemu Mjini Singida; Walimu wenzie wa Mjane wa Marehemu Trinita; Viongozi wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano, Upanga, Dar Es Salaam; Kwaya ya Kanisa hilo; Wanajumuia wa Jumuia ya Mtakatifu Agostino wa Hippo; Ndugu, Jamaa na Marafiki.

  Ibada ya Shukrani itafanyika katika Kanisa la Mtakatifu Albano siku ya Jumamosi tarehe 6 April, 2013, kuanzia saa mbili asubuhi. Karibuni.

  “MPENDWA WETU PETER MIKONONI MWA MWENYEZI MUNGU PUMZIKA, MIOYONI MWETU ISHI DAIMA”

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi Mdogo wa China aneyeishi Zanzibar,Bibi Chen Qiman,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar jana.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Balozi Mdogo wa China aneyeishi Zanzibar,Bibi Chen Qiman,(kushoto) mara baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar jana.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia washiriki wa mkutano wakati akifungua ramsi mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa meza kuu na baadhi ya viongozi, wakati akifungua ramsi mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba, akichangia wakati wa mkutano mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umefunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
  Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakiwa ukumbini humo wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua ramsi mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Kunduchi Beach, kufungua ramsi mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wa mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, baada ya kuufungua mkutano huo ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, baada ya kuufungua mkutano hio, ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. Picha na OMR.

  0 0


  Tanzania this week became the newest developing country partner to join the Global Partnership for Education (GPE), including mainland Tanzania and Zanzibar, a semi-autonomous island.
  “We welcome Tanzania to the Global Partnership for Education and look forward to working with the Tanzanian and Zanzibar governments and a wide range of development partners to ensure access and improve the quality of learning for all children in Tanzania and Zanzibar,” said Alice Albright, GPE’s Chief Executive Officer.
  As a member of the Global Partnership, Tanzania is now eligible to apply for a Program Implementation Grant in the amount of US$ 100 million. Based on indicators such as the size of the school population and available donor funding, this will be divided into US$94.8 million for Mainland Tanzania and US$ 5.2 million for Zanzibar.
  Tanzania will join the Africa 1 constituency of the GPE Board of Directors. Mainland Tanzania’s and Zanzibar’s current Education Sector Plans cover the periods 2008-2017 and 2008-2016, respectively.
  The Global Partnership for Education is made up of nearly 60 developing country governments, as well as donor governments, civil society organizations/NGOs, teacher organizations, international organizations, and private sector organizations and foundations, whose joint mission is to galvanize and coordinate a global effort to provide a good quality education to children, prioritizing the poorest and most vulnerable.

  0 0


  Petition to prevent any building on "ground zero" area where the shocking incident took place on 29th March 2013 which took away so many innocent lives.
  Parents lost their beloved kids playing near the mosque. Some families lost their sole bread earners in the construction works. Some were just on the road, going to church on Good Friday.
  The area should be preserved as a reminder of the tragic loss we have all suffered.
  Additionally, the nearby building of the same owner should also be taken down ASAP to prevent any further casualties.
  By signing, you let the concerned authorities know your displeasure at the act and ask them to do their best to attain this goal.


  0 0


  Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa TTCL Bw. Peter Ngota akionyesha simu mpya na ya kisasa (smart phone) zinazopatikana katika vituo vyote vya huduma kwa wateje nchini kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya BANDO NA TTCL pamoja kampeni ya BASTI iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.kulia ni mkuu wa Mauzo Bw. Kisamba Tambwe.
  Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa maendeleo ya bidhaa wa TTCL Ernest Isaya, afisa mkuu wa mauzo na masoko Peter Ngota na Mkurugenzi wa Mauzo Bw. Kisamba Tambwe.
  Afisa mkuu wa mauzo na masoko wa TTCL Bw. Peter Ngota akionesha bango lenye punguzo kubwa la bei ya Intanet wakati wa uzinduzi wa kampeni ya BASTI uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Mauzo wa TTCL, Kisamba Tambwe. 

  BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI

  0 0

  Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda leo amekutana na Makamu wa Raisi na Mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya BG Group ya Afrika mashariki Bwana Sam Iskander yeye na maofisa aliokuwa anawaongoza walikuwa na mazungumzo ya kikazi na waziri mkuu ofisini kwake Magogoni Dar es salaam.Picha na Chris Mfinanga


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013 na mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa mwaka wa Fedha 2013/2014 kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (hawapo pichani) inayoongozwa na Mhe. Edward N. Lowassa (Mb.) (kulia). Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam leo 
  Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Mhe. Waziri Membe (hayupo pichani).


  Waheshimiwa Wabunge na Wajumbe wengine wa Kamati hiyo wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikino wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) (kulia-mstari wa kwanza), akimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa kikao kati ya Uongozi wa Wizara na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Wengine katika picha ni Bw. John  Haule (katikati), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Balozi Rajabu Gamaha (kushoto), Naibu Katibu Mkuu.

  Baadhi ya Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa kikao kati ya Uongozi wa Wizara na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

  Wakurugenzi wengine kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani).

  Wakurugenzi na Wajumbe wengine kutoka Idara, Vitengo na Taasisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Waziri Membe (hayupo pichani) wakati wa kikao kati ya uongozi wa Wizara na Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

  0 0

  Evans Bukuku upo hapo??

  0 0
  0 0

  KUNA HALI YA HATARI SANA KATIKA ENEO LA KITUO CHA POLISI KAWE JIJINI DAR ES SALAAM HIVI SASA BAADA YA WANANCHI KUAMUA KUKIVAMIA KITUO HICHO KUTOKANA NA DEREVA MMOJA WA BAJAJI KUDAIWA KUUWAWA NA ASKARI WA JESHI LA WANANCHI AMBAYE ANASHIKILIWA NA POLISI.

  KIUKWELI HALI NI MBAYA SANA ENEO HILI HIVI SASA KWANI MABOMU YA MACHOZI NA MILIO YA RISASI VIMETAWALA KATIKA ENEO HILI IKIWA NI KATIKA HALI YA KUWATAWANYA WANANCHI HAO AMBAPO WANANCHI HAO WANAENDELEA KURUSHA MAWE.
   BARABARA YA IMEFUNGWA NA HAKUNA SHUGHULI ZINAZOWEZA ENDELEA KUFANYIKA KATIKA ENEO HILO.
   MOSHI WA MABOMU YA MACHOZI UKIONEKANA KWA MBALI WAKATI POLISI WAKIENDELEA KUWATAWANYA WANANCHI HAO.



  WANANCHI WAKIWA WAMEJIKUSANYA PEMBENI WAKITAFAKARI KINACHOENDELEA.

  0 0
 • 04/03/13--09:50: VURUGU ZAIBUKA TUNDUMA LEO
 • Kamanda  wa polisi  wa mkoa  wa Mbeya  Diwani Athuman
  .............................................................

  Taarifa  kutoka Tunduma mkoani Mbeya zinadai  kuwa hali  si shwari katika eneo hilo kutokana na kuzuka kwa  vurugu kubwa zinazodaiwa kusababishwa na masuala ya  kiimani ya nani achinje kati ya mkristo na Muislam .

  Habari zinasema vurugu  hizo zimeanza  majira ya saa nne asubuhi  kwa makundi  ya vijana  kuandamana mitaani na kuvutana  kuhusu uamuzi  wa viongozi  wa dini ya kikristo Tunduma  kuandika barua kwa mkuu  wa wilaya  kutaka  kuruhusiwa kuchinja  wakati wa Pasaka.

  Insemekana kuwa kabla ya  Ijumaa kuu  viongozi hao  wa dini ya Kikristo  walikutana na mkuu  wa  wilaya  Mhe. Momba Abuud Saidea ambae  aliwataka kuwasilisha barua rasmi ya  kufanya hivyo .

  Hata hivyo inaelezwa  kuwa  vurugu  hizo za  leo hazina mahusiamo ya moja kwa moja na masuala ya dini kwani  wanaoshiriki katika  vurugu  hizo ni vijana  wapiga debe ambao baadhi yao  wamechanganyika na  vibaka  kwa lengo la kuchafua hali ya hewa, kwani  suala la uchinjaji ambalo lilifanyika  siku ya Pasaka  halikuwa na mvutano  wowote baada ya wakristo kuchinja katika bucha zao na  waislamu hao  kuchinja katika mabucha yao na kila mmoja  kufanya biashara  kwa kupata  wateja wake kama kawaida .

  Ila katika hali ya kushangaza ni baada ya  leo kuibuka  kundi hilo la  vijana  wanaofanya kazi katika stendi na vijiwe mbali mbali kuanzisha vurugu kiasi cha  polisi  kuingilia kati kwa kutumia mabomu ya machozi na kuwatawanya  wananchi  waliokuwa wamekusanyika maeneo mbali mbali .

  Kutokana na vurugu  hizo mpaka  wa Tunduma  ambao unaingia nchi  za kusini  wa Tanzania  ulifungwa  pamoja na magari yaliyokuwa yakitoka  Sumbawanga  pia  kuzuiwa  kuendelea na  safari hadi hali  hiyo  ilipotulia mida hii saa 8 mchana baada ya kamanda wa polisi wa mkoa  wa Mbeya  Diwani Athuman  kufika  eneo hilo.



  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan akifafanua Jambo wakati alipotembelea Mradimpunga wa Umwagiliaji kwenye Bonde la Mpunga la Jendele kulia Mwenyekiti wa Tasaf Jendele Ali Mussa waziri alifanya Ziara ya Wilaya ya Kati Unguja kukutembelea Mradi Uliofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Mratibu wa wa Programu ya kuimarisha huduma za kilimo Bw Zaki Khamis Juma akimueleza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan kuhusu wakulima wa kuzalisha Mbegu za Mpunga kwenye Bonde la Kinyasini -kisongoni Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakati wa Ziara ya kutembelea Miradi ya Tasaf na Assp inayofadhiliwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan akipita kwenye shamba la mpunga la kuzalishia Mbegu la kinyasini-kisongoni Walaya ya Kaskazini A Unguja Waziri akiwa katika Ziara ya kutembelea Miradi iliyofadhiliwa na ASSP [Picha na Ali Meja ]

  0 0

  Ndugu  Michuzi,
   
  Shirika la ndege la kisiwa cha  Samoa, Samoan airline wameanzisha utaratibu wa kulipia nauli ya ndege kulingana na uzito wa mtu na mizigo. Wenyewe wameiita ' Fare weight'  system.The lighter the passenger the lighter the fare. Yaani jinsi unavyokuwa  na uzito  mdogo  ndivyo unavyolipa   nauli ndogo. Utaratibu huu umeanza  kuanzia mwezi november mwaka jana na watu wamependezwa nao, hata wale  wenye  uzito mkubwa wameona  ni sahihi kufanya  hivyo, ingawa wanalipa  zaidi kuliko watu wenye  mzito mdogo. 
  Watanzania mnaionaje hii kitu tukii copy & paste? Nadhani  ni jambo zuri ambalo vile vile linaweza kuchangia watu kuchunga  afya  zao  hasa swala la kuongeza  uzito bila mpango.
   
  Mdau  Ruger
  Ughaibuni

  0 0

  This week, Kali TV attended Face Africa clean water Gala in New York City. Face Africa organization works on solving the issue of clean water availability to everyone in Liberia. Kali TV also was at the Afrikana ball night in Washington DC. Afrikana Ball is an event where Africans came together and show their culture through African attire and fashion. In the small town of Gettysburg Pennyslvania, Africans and friends of Africa joined together inside Trinity United Church of Christ to connect, enjoy African food music and drums.

  0 0

  GenBanner
  sp flag
    
  Dear Smart Partner Invitees,
   
  Countdown for your Engagement-Registration in Global 2013
  For those of you yet to respond to the invitation, this is a special last Countdown for your engagement in Global 2013, Dar es Salaam.

  The deadline for registration/engagement is Friday the 5th April
    
  Therefore you now only have 2 days remaining to register  your interest.

  You may do this by sending us an email to  

  0 0
 • 04/03/13--20:00: Ngoma Azipendazo ankal
 • Kaka Fresh Jumbe anatamba hadi aliko huko Japan na ngoma yake ya 'Ama zake ama zangu' aliyoimwaga na Dar International enzi hizo.

older | 1 | .... | 88 | 89 | (Page 90) | 91 | 92 | .... | 3285 | newer