Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 896 | 897 | (Page 898) | 899 | 900 | .... | 3284 | newer

  0 0
 • 07/06/15--07:47: Airtel Fursa - Episode 3
 • Airtel Fursa ni mradi wa kijamii wenye dhumuni la kuhamasisha vijana, kuwapa nafasi ya kujiendeleza kibiashara na ujuzi utakoawawezesha kuimarisha biashara zao.
  Bofya hapa: goo.gl/ECdVkc na wewe ukamate fursa na Airtel

  0 0

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha na kufanya mazungumzo na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakati wa mkutano wa dharura wa wakuu wan chi za jumuiya hiyo uliofanyika ikulu jijini Dar es salaam leo.(picha na Freddy Maro).
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Liberata Mulamula kwa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati kiongozi huyo wa Uganda alipowasili ikulu jijini Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa wakuu wan chi za Jumuiya ya Afrika Mashariki leo. 


  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akifuturu pamoja na wageni waalikwa kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC yeye mwenyewe.
  Waandazi wa futari hiyo iliyofuturiwa jijini Dar es Salaam wakiendelea na maandalizi siku ya tukio.
  Baadhi ya washiriki wa futari iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo.


  0 0
 • 07/06/15--11:51: KUMBUKUMBU
 •   Leo [06 Juni, 2015] ni mwaka mmoja tangu ututoke ghafla katika dunia hii. Mama yetu mpenzi Jasmin Salum Saadallah.

  Sisi tulikupenda lakini Mola alikupenda zaidi. Mapenzi ya Allah Yatimizwe.Unakumbukwa siku zote na watoto, wajukuu, ndugu, jamaa na marafiki zako.

  Tunamuomba Mwenyezi Mungu  
  ailaze roho yako mahali pema peponi.

   AMIN
    

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Laurean Rugambwa Bwanakunu (pichani) kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bohari ya Dawa (MSD). 


  Taarifa iliyotolewa Dar es salaam leo, Jumatatu, Julai 6, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi wa Ndugu Bwanakunu unaanzia Juni 23, mwaka huu, 2015. 

  Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Bwanakunu alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Ariel Glaser Paediatric AIDS Healthcare Initiative.


   Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu – Dar es Salaam.


  6 Julai,2015


  0 0

  International Conference on Literacy and Numeracy from July 9-10th 2015, the Conference will be held at the Nkrumah Hall-UDSM and is organized by School of Education-UDSM. Please circulate this advert widely.

  0 0

  Kocha Abdulghani Msoma akifuatilia michezo ya Bonaza katika uwanja wa mnazi mmoja kushoto Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Hamad Masauni na kulia Mchezaji wa Zamani wa timu ya Nyuki. iliokuwa na makazi yake kikwajuni  Zanzibar. 
                  Kizazaa katika goli la Kilimani Mashariki hakuna madhara yaliotokea
  Miss the ball get the man....
   Kipa wa timu ya Kilimani Mashariki akidaka mpira wakati wa mchezo wao na timu ya Kisimajongoo. 

  0 0

  NA NASIBU MGOSSO.

   Awali ya yote nichukue fulsa hii kuomba radhi kwa makosa ya kiuandishi yaliyo jitokeza katika makala iliyopita  ambayo  mwanzoni  mwa paragrafu  ya kwanza nilianza kueleza moto nikitugani,  lakini katika maelezo kulitokea mkanganyiko,  Sehemu hiyo ilipaswa isomeke hivi:

  Moto ni mgongano endelevu  wa  kikemikali ambao uzaa joto na mwanga.  Mgongano  huo  endelevu   utasababisha muwako  ambao  utaendelea   kukua  endapo  utapata  vitu vikuu  vitatu  ambavyo  ni joto,  hewa  ya  oksijeni  na kuni(vitu  vinavyoungua).   Vituhivyo  kitaalam  tunaviita  ’fire element’.

  Oksijeni nimiongoni mwa  vitu vinavyo  saidio moto kuwaka  haizalishwi na moto kamailivyo someka  katika  makala iliyo pita.
  Baada ya marekebisho hayo  sasa tuendelee na  kinga na taadhari dhidi  ya moto.

  Kunavyanzo vingi vya moto  lakini chanzo kikubwa ni  sisi  Binadamu  kwa sababu  ya asili na alakati za maisha ya kila siku  kuhusisha matumizi ya moto kwa   maana ya mwako,  nishati ya umeme pamoja na vyombo vya usafiri na usafirishaji.  Katika mahitaji hayo inatulazimu kujenga urafiki na moto bila kujali hatari iliyopo.

  Aina ubishi kwamba moto ni nyenzo muhimu katika  maisha yetu ya kila siku,   na niadui yetu mkubwa  sana anaye penda kutu shambulia  akitokea ndani ya jengo au chombo .  


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Arusha kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kidiplomasia la Utekelezaji wa Itifaki ya Rasimu ya Aripo inayolenga kulinda aina mbalimbali mpya za mimea, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha leo Julai 6, 2015.
  'WAGOMBEA WANAPOKUTANA', Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, ambaye ni mmoja kati ya wagombea wa Urais kupitia CCM, akizungumza jambo na mgombea mwenzake, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Arusha kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kidiplomasia la Utekelezaji wa Itifaki ya Rasimu ya Aripo inayolenga kulinda aina mbalimbali mpya za mimea, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Kidiplomasia la Utekelezaji wa Itifaki ya Rasimu ya Aripo inayolenga kulinda aina mbalimbali mpya za mimea, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha leo Julai 6, 2015.


  0 0

  Waziri wa zamani Daniel Yona akiituliza familia yake mara baada ya hukumu kutolewa leo katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es salaam.
  Waziri wa zamani Basi Mramba akiteta na mawakili wake baada ya kuhukumiwa leo mahakamani Kisutu.


  Mawaziri wa zamani Basil Mramba  na Daniel Yona  leo wamekutwa na hatia na katika kesi iliyokuwa inawakabili kifungo cha kwenda jela miaka mitatu kila mmoja kwa kukutwa na makosa 10 ya matumizi mabaya ya madaraka. 

   Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi Grey Mngonja (kushoto)  ameachiwa huru bada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha makosa dhidi yake. 

  Pia Mahakama hiyo imewahukumu kulipa faini ya shilingi milioni 5  au kwenda jela miaka 2 zaidi baada ya kukutwa na hatia ya kuisababishia serikali hasara ya shilini bilioni 11.7. 

  Washitakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 11.7 kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni iliyopata zabuni ya ukaguzi wa madini ya dhahabu nchini.
  Hukumu hiyo imetolewa chini ya jopo la mahakimu watatu ambao ni Hakimu Saul Kinemela, Jaji Sam Rumanyika na Jaji John Utamwa aliyekuwa mwenyekiti wa jopo hilo baada ya kupitia ushahidi pamoja na vielelezo vilivyowasilishwa na pande zote mbili katika kesi hiyo.
  Kwa mara ya kwanza washitakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo mwaka 2008 wakikabiliwa na mashitaka ya kuisababishia serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya kukagua madini ya dhahabu ya M/S Alex Stewart ya Uingereza.


  0 0

  Taarifa ya makubaliano toka kwa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki imetolewa leo Ikulu Dar es Salaam wakati wa kuhitimisha Mkutano wa siku mbili wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya hiyo ambapo baadhi ya maadhimio waliyokubaliana ni kwamba Rais Museveni wa Uganda awe msimamizi wa juhudi za upatanishi wa makundi nchini Humo.

  Akizungumza wakati wa Mkutano huo, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Dkt. Richard Sezibera alisema kuwa Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Museveni apewe jukumu la usimamizi katika kupatanisha makundi nchini Burundi, pia  Serikali ya Burundi iwanyang'anye silaha kikundi cha vijana cha Imbonerakure pamoja na makundi mengine ya vyama vya siasa ambayo yanamiliki silaha hizo, Umoja wa Afrika (AU) ipeleke waangalizi wa kijeshi kuhakikisha kuwa vikundi hivyo vinanyang'anywa silaha hizo, Jumuiya ya Nchi za Maziwa Makuu kutuma Timu ya Wakaguzi na Wataalam wa mambo ya intelijensia kujua kama FDLR wapo nchini Burundi.

  Sezibera aliongeza kuwa Upande wowote utakaoshinda uchaguzi unapaswa kuunda Serikali ya Kitaifa ambayo itashirikisha Vyama vilivyoshiriki pamoja na vile visivyoshiriki uchaguzi nchini humo, pia upande wowote utakaoshinda uchaguzi uheshimu makubaliano ya Arusha na kuhakikisha kuwa hautobadili Katiba ya nchi hiyo.


  0 0
  0 0

  Je wewe ni Chef wa Kitanzania? Basi jiunge na Whatsapp  group la Tanzania Chef's Club ambalo unaweza jiunga kwa kutuma request mobile no +46709297384 Lengo likiwa ni kukutana,  kufahamiana,  na kusaidiana ki-taaluma popote ulipo duniani - KARIBUNI SANA -  Chef Issa

  0 0

    Habari na picha 
  na John Nditi
  MKUU wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe, Julai 6, 2015, amefanya ziara ya kikazi katika wilaya ya Ulanga, ambapo moja ya jukumu kubwa lilikuwa ni kulihutubia baraza la madiwani wa halmashauri hiyo , ambalo lilikuwa na jukumu la kupitia majibu ya hoja za ukaguzi kwa mwaka 2013/2014.
  Hata hivyo katika hotuba yake kwa madiwani hao kabla ya kuvunjwa kwa baraza hilo kupisha uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, Mkuu huyo wa mkoa alitumia fursa hiyo kuwapongeza madiwani na watendaji wa halmashauri kwa kuiwezesha kupata hati safi kwa kipindi cha miaka minne mfululizo.
  Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa huyo, hati safi hizo zilipatikana katika mwaka wa fedha wa 2010/2011. 2011/2012,2012/2013 na 2013/2014.
  Mkuu huyo wa mkoa alisema , mafanikio hayo hawakutokea kwa kubahatisha ila yanatokana na kufanya kazi kwa ushirikiano, uadilifu na bidii, baina ya madiwani , watendaji wa halmashauri na wananchi wa wilaya ya Ulanga.
  Hata hivyo aliwaambia madiwani hao na watendaji wa halmashauri hiyo , kuwa pamoja na mafanikio ya kupata hati safi , wasiridhike ama kutosheka na mafanikio na kuanza kubweteka.
  “Lazima muendelee kufanya kazi kwa bidii zaidi ili kudumisha na kulinda mafanikio hawa na kufikia kiwango cha juu kabisa cha mafanikio katika hesabu za halmashauri na kuendelea kupata hati safi isiyokuwa na msisitizo” alisema Mkuu wa mkoa.
  Alisema , lengo ni kuifanya halmashauri hiyo kuwa ya mfano wa kuigwa na halmashauri nyingine za mkoa wa Morogoro na Tanzania nzima.
  Hata hivyo alisema , kwa mwaka huo wa 2013/2014, halmashauri zote saba za mkoa pamoja na Ofisi ya Mkuu wa mkoa zimepata hati safi na kutaka kila halmashauri kufata misingi ya sheria za ukaguzi wa hesabu za serikali.

  Mabaraza ya madiwani , kwa mujibu wa sheria na tangazo la serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi , anapaswa kuwa yamefikia ukomo wake kuanzia Julai 6 hadi 8, mwaka huu ili kupisha uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu. 
   Sehmu ya majengo ya Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro.
   Madiwani wa Ulanga wakifurahia jambo wakati MKUU wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe akiwahutubia
  MKUU wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe akiwahutubia madiwani wa Ulanga
  MKUU wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe, katika picha ya pamoja na madiwani wa Halmashauri ya Ulanga  0 0

   Mafundi na wahandisi ujenzi wakiendelea na kazi ya kusuka nguzo kuu katika daraja la mto Kilombero kama walivyokutwa eneo la Kivukoni, mjini Ifakara. 
  Daraja hilo linajengwa na mkandarasi M/S China Railway 15 Group Corparation ya China na lina lenye  urefu wa mita 384  ambapo gharama yake ni Sh bilioni 56 ikiwa na kuweka lami  ya kilometa 9.142 fedha  zilizotolewa na Serikali ya Tanzania  Picha na John Nditi


  0 0


  Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. 
  Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ?
  Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu
  HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME
  Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo :
  Hatua  ya  kwanza, ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na  kuwa  mgumu  kama  msumari.
  Na  hatua  ya  pili  ni  lazima, uume  wake  uendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa  STRONGER  AND  LONGER  ERECTION.


  0 0

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  Baadhi ya vyombo vya habari katika taarifa zao zilizochapishwa katika matoleo yao ya Jumatatu tarehe 6 Julai, 2015 vimechapisha taarifa zinazohusu utafiti uliofanywa na REDET juu ya Maoni ya Wananchi Kuhusu Uchaguzi Mkuu Utakaofanyika Oktoba 2015. Taarifa hizi zimesababisha wadau wengi hapa nchini kutaka ufafanuzi kutoka REDET. Kama ilivyo kawaida yake REDET imejijengea heshima na utamaduni wa kufanya kazi zake kwa misingi ya uwazi na ukweli. Kwa hali hii tunapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:

  i. REDET ilifanya utafiti juu ya maoni ya wananchi kuhusu hali ya siasa Tanzania na uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2015 kuanzia tarehe 23 hadi 26 Juni 2015. Utafiti ulikusudiwa kufanyika katika mikoa yote 30 Tanzania Bara na Zanzibar. Kwa bahati mbaya kibali cha kufanya utafiti Zanzibar hakikutolewa kwa wakati. Hivyo taarifa za utafiti zilipatikana kutoka mikoa 25 ya Tanzania Bara tu. Badala ya kupokea taarifa za mahojiano 1,500, zilipokelewa 1,250 sawa na takribian asilimia 83. Rasimu ya taarifa ya awali iliandaliwa kutoka mikoa hiyo tu;

  ii. Tarehe 2 Julai, 2015 REDET ilitoa mwaliko wa Mkutano wa Wanahabari ili kuwawezesha Watanzania kupitia vyombo vya habari kupokea matokeo ya utafiti Jumapili tarehe 5 Julai, 2015 saa 5.00 asubuhi;

  iii. Baada ya kutafakari kwa kina na kwa kuzingatia ukweli kwamba rasimu ya taarifa ya utafiti haikuhusisha mikoa yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Uongozi wa REDET uliazimia kufanya juhudi zaidi ili kuwezesha mamlaka husika katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuridhia utafiti huu uhusishe pia mikoa ya Zanzibar, ili ripoti itakayotolewa iwe kamilifu na yenye sura ya Kitaifa;

  iv. Tarehe 4 Julai, 2015, REDET ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu kuhairishwa kwa mkutano wa wanahabari uliokuwa ufanyike tarehe 5 Julai, 2015 kutokana na kutokamilika kwa taarifa kamili ya utafiti;

  v. REDET imewasilisha maombi kwa uongozi wa juu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuomba uwasiliane na mamlaka husika Zanzibar ili ruhusa iweze kutolewa kufanya utafiti huu katika mikoa mitano ya Zanzibar;

  vi. REDET itatoa taarifa kamili ya utafiti kuhusu Maoni ya Wananchi Kuhusu Uchaguzi Mkuu Utakaofanyika Oktoba 2015, mara tu taarifa yake itakapokamilika; na

  vii. Mwisho, uongozi wa REDET unaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

  Imetolewa na:
  Menejimenti, Mpango wa Utafiti
   na Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET)

  0 0

  MSTAHIKI Meya wa manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda amesema kuwa soko jipya la SIMU 2000 litaweza kuchukua wafanyabiashara 512 kutoka kila pembe ya manispaa ya kinondoni. 
  Mstahiki  Mwenda amewatoa hofu wafanyabiashara wa soko jipya la kituo cha basi cha Simu2000 mawasiliano kuwa watafanya biashara bila ya kuwa na matatizo yoyote kwa kuwa soko hilo lipo katika mfumo wa kisasa. 
  Meya  Mwenda alisema hayo alipokuwa akikabidhi vizimba vya soko hilo kwa wafanya biashara ndondogo waishio katika wilaya ya Kinondoni tu, na sio mtu kutoka eneo la nje ya manispaa hiyo hivyo kuwataka kulitunza soko hilo kama mali yao. 
  “Tumeamua kulifanya soko hili ili liweze kuanza kazi kabla ya uzinduzi rasmi utakaofanywa baadae hili kuweza kuwapa fursa wafanya biashara kuliko kuacha jingo limeisha na kuonekana kama picha hivyo nawaomba mfanye biashara hili muweze kujiongeza kipato” alisema Mwenda. 
   Alitoa wito kwa wafanyabiashara hao kutokata tama kwani mwanzo ni mgumu kwnai eneo lenyewe ni jipya hivyo sio rahisi kuona biashara ikichanganya kwa haraka kama wanavyofikiri.
  Meya wa manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda akitoa maelekezo kwa  watendaji wa soko hilo  wakati akagua vizmba kabla ya kuwakabidhi wafanya biashara.
  Meya wa manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda akiwa na watendaji wa soko hio wakikagua vizmba kabla ya kuwakabidhi wafanya biashara.

  0 0

   Mwandikishaji Msaidizi katika kituo cha kupiga kura kituo cha Afya Msoga Bi.Happyness Thomas Misana akimkabidhi fomu Mbunge wa Chalinze Mh.Ridhiwani Kikwete wakati mbunge huyo alipojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura leo.
  Afisa TEHAMA kutoka Tume ya Taisa Ya Uchaguzi Bwana SAnif Khalfan akimkabidhi Mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete kutambulisho chake cha mpiga kura baada ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la kupiga kura leo

  0 0

  Viongozi wa meza kuu wakifuatiliac mchezo huo kati ya Muembeladu na Kisimajongoo katika Bonaza la kukuza Vipaji kwa Vijana lililodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Masauni. na kutoa Ofa kwa mchezaji Bora kupata fursa ya kusoma Kozi ya Computer katika Kituo cha Vija cha TAYI  
                 Mchezaji wa timu ya Muembeladu akimpita mchezaji wa timu ya Kisimajongoo.timu ya Muembeladu imeshinda mabao 4--1
         Mchezaji aliyeibuka mchezaji Bora Amour Janja akiwapita wachezaji wa timu ya Kisimajongoo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 896 | 897 | (Page 898) | 899 | 900 | .... | 3284 | newer