Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 895 | 896 | (Page 897) | 898 | 899 | .... | 3285 | newer

  0 0

  MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, akipongezwa  na Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal wakati wa Kikao cha Kamati Maalum ya CCM Zanzibar ilokutana ukumbi wa Mkutano Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui kwa ajili ya kupitisha Jina la Mgombea Nafasi ya Urais wa Zanzibar Dk. Shein.
   VIONGOZI wa Meza Kuu wakiwa katika ukumbi wa Mkutano Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui kwa ajili ya kupitisha Jina la Mgombea Nafasi ya Urais wa Zanzibar Dk. Shein.

  NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali, akitoa maelezo ya kikao hicho cha Kamati Maalumu ya CCM Zanzibar. 
   MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wajumbe wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar baada ya jina lake kupitishwa kuwa  Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM. 
  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwa  na Wajumbe wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar baada ya jina lake kupitishwa kuwa  Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM. 

  0 0

   Mwenyekiti wa Kariakoo Family Foundation Development (KFFD) Mohamed Bhinda akimkabidhi mlezi wa  kituo cha Yatima cha Al Madina Tandale jijini Dar es salaam leo. KFFD ni jumuiya ya watu wanaoishi ama waliopata kuishi eneo la Kariakoo ambao wameunda jumuiya hiyo  kudumisha umoja wao pamoja na kusaidiana katika shida na raha.
   Ujumbe wa KFFD ukiwa na mlezi wa  kituo cha Yatima cha Al Madina Tandale jijini Dar es salaam baada ya kukabidhi misaada leo. 
   Ujumbe wa KFFD ukiwa na watoto wanaolelewa katika  kituo cha Yatima cha Al Madina Tandale jijini Dar es salaam baada ya kukabidhi misaada leo. 

  0 0
 • 07/05/15--04:51: Article 13


 • 0 0


  Baadhi ya Wanalyalamo wakijumuika na watoto wa 
  kituo cha Yatima Group Trust Fund kilichopo Chanika, Dar es Salaam
  .

  baadhi ya wanalyamo family katika picha ya pamoja na mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho, Winfrida Lubanza(mwenye miwani na blauzi nyeusi)

  WITO umetolewa kwa Watanzania nchini kujitolea kwa hali na mali usaidia watu wenye uhitaji ikiwemo watoto yatima wanaolelewa kwenye vituo mbalimbali. Wito huo umetolewa jana na mkurugenzi mtendaji wa kituo cha Yatima Group Trust Fund kilichopo Chanika, jijini Dar es Salaam, Winfrida Lubanza wakati akizungumza na wanafalia wa Lyalamo.

  Alisema jamii inapaswa kuwakumbuka na watoto wakuopo katika vituo hivyo kwani wanastahili kupata mahitaji muhimu ya kibinadamu kama ilivyo kwa watoto waliopo majumbani. "watoto yatima ni watoto km wengine nao wana uhitaji sawa hivyo jamii isiwasahau na kwani nao wanapata furaja na kupata matumaini zaidi,"alisema.

  Aidha, aliongeza kuwa kituo chake kinakabiliwa na chsnggamoto mbalimbali ikiwemo chakula, madawa, sabuni na ada kwa wanafunzi sambamba na mtaji wa kuwezesha kuanzisha biashara ambayo itaweza kuwapatia pesa za kujikimu.
  "tunachangamoto nyingi mfano kuna mwanafunzi yupo kidato cha nne amerudishwa kituoni sababh hatujakamilisha ada,"alisema.
  Naye kiongozi wa Lyalamo family, Aziza Kibwana alisema wamefarijika kufika kituoni hapo na kuona vhangamoto hivyo watajitahidi kuchangia walichojaaliwa.Pia amesisitiza wadau kujitokeza kusaidia. " Sisi tumesoma shule ya msingi boarding tukiwa wadogo na tulikuwa na watoto kutoka katika vituo kama hivi hivyo tunaguswa sana na hali zao ndio maana tuko hapa," alisema.Aziza aliongeza kwamba kupitia umoja wao watajitahidi kadiri wawezavyo kuvifikia vituo mbambali na kutoa misaada.
  " Humu kuna marais, kuna mawaziri, wabunge, wanasoka, wasanii, wafanyabiashara, madaktari, wahasibu n.k sasa ni muhimu kuwakumbuka na watoto waliopo huku ili kuwajengea misingi mizuri ya kutimiza ndoto zao," aliongeza .Katika ziara yao Lyalamo family walikabidhi kituoni hapo vyakula, mafuta, dawa, madaftari, sabuni na vitu vinginevyo ambapo watoto waliopo kituoni hapo walifurahi na kushukuru.
  Kituo hicho kilichoanzishwa mwaka 2001 kinalea watoto kati ya 150 hadi 300 wenye umri wa kuanzia 0 hadi miaka 18.

  0 0

  Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb.) akifungua Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki ambao pamoja na mambo mengine utapokea na kujadili taarifa ya ziara ya Mawaziri nchini Burundi kuhusu hali ya kisisasa nchini humo. Mkutano huo ambao ni maandalizi ya Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi utakaofanyika tarehe 06 Julai, 2015, umefanyika kwenye Hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Julai, 2015.
  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Dkt. Richard Sezibera naye akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Joyce Mapunjo wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
  Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nao wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa Mkutano huo.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Mwenyekiti wa Kikundi cha Tujiajiri Group cha Tarafa ya Nyasa wilaya ya Nzega Bw.Fanuel Kifunyu(waKwanza kulia)akiongea na kuonyesha ujumbe kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo kuhusu Bidhaa mbalimbali wanazotengeneza zikiwamo Sabuni,matofali ya kufungamana,na karanga baada ya kupata mafunzo ya mfuko wa Maendeleo ya Vijana,Stadi za Maisha,Ujasiriamali na Uongozi Bora.Wengine pichani ni Afisa Vijana Laurean Masele(wa pili kutoka kulia),Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana Uratibu na Uhamasishaji(katikati) na Afisa Vijana Amina Sanga(Mwenye kiremba cha Njano.

   Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana Uratibu na Uhamasishaji Bi.Esther Riwa akimwuliza maswali Mwanakikundi cha Ushonaji na utengenezaji wa Viatu Bw.Chepe changamoto gani wanazokutana nazo katika ufanyaji wao wa kazi za ushonaji uku mwanakikundi uyo akibainisha kutopatikana wa mashine za kutengenezea viatu ivyo mpaka nchi jirani ya kenya.

  Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana Uratibu na Uhamasishaji Bi.Esther Riwa(wa Kwanza kushoto) akipita katika shamba la nyanya la kikundi cha Nserema kinacholima Nyanya,Matikiti,na Kabeji kutoka  kijiji cha Iyombo Tarafa ya Nyasa.kikundi icho kinategemea kuomba mkopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ili kuboresha kilimo chao kwa kununua pembejeo za kilimo,kununua mbegu bora na madawa ya kuulia wadudu.katikati mwenye shatu jekundu ni Mwenyekiti wa kikundi icho Bw. Stephen Ndikamara.

  0 0

   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akielekea viwanja vya Ole Kanambe kwa ajili ya kushiriki sala ya aliyekuwa Sheikh maarufu wa Ole marehemu sheikh Alawy bin Omar bin Salim Baalawy, aliyefariki jana usiku.
   Mamia ya waombolezaji kisiwani Pemba wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa sheikh maarufu wa Ole Kanambe marehemu sheikh Alawy bin Omar bin Salim Baalawy, aliyefariki jana usiku.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, pamoja na waumini wa dini ya Kiislamu Kisiwani Pemba, wakiitikia dua baada ya kuusalia mwili wa  aliyekuwa Sheikh maarufu wa Ole Kanambe, marehemu sheikh Alawy bin Omar bin Salim Baalawy.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiweka udongo kwenye kaburi la aliyekuwa Sheikh maarufu wa Ole marehemu sheikh Alawy bin Omar bin Salim Baalawy, aliyefariki jana usiku.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, pamoja na waumini wa dini ya Kiislamu Kisiwani Pemba, wakiomba dua baada ya kuuzika mwili wa  aliyekuwa Sheikh maarufu wa Ole Kanambe, marehemu sheikh Alawy bin Omar bin Salim Baalawy. (picha na Salmin Said, OMKR)

  0 0

  Klabu ya Kimondo Super Sports inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania yenye maskani yake wilayani Mbozi mkoani Mbeya inapenda kutoa tamko juu ya mkanganganyiko wa taarifa za kuptosha za usajili wa mchezaji wake Geofrey Bahati Mwashiuya.


  Klabu inasikitishwa saana na habari/taarifa zenye mkanganyiko zinazotolewa na msemaji wa timu ya Yanga,Katibu wa timu ya Yanga na mchezaji wetu Geofrey Mwashiuya katika vyombo mbalimbali vya habari;

  Jerry Muro alisikika katika vyombo vya habari akijinadi kuwa klabu ya soka ya Yanga imemsajili Geofrey Mwashiuya tangu Oktoba,2014 kwa kandarasi ya miaka mitatu,wakati huohuo Katibu wa Yanga Dkt,Jonas Tiboroha alidai mchezaji huyu alisajiliwa na klabu ya Yanga tangu mwezi Februari,2015.

  Klabu ya KIMONDO inasikitishwa na taarifa hizi zenye mkanganyiko mkubwa kuhusu suala la mchezaji huyu,na kwa kauli hizo mbili zinazokinzana Watanzania wanaweza kuona ukweli wa mambo ukoje.


  Taarifa sahihi ni kwamba mchezaji Geofrey Mwashiuya ana mkataba wa miaka minne na timu yetu ya KIMONDO  na ndio muda sahihi ulioandikwa katika TMS na uliopo katika mkataba wa maandishi. Zaidi klabu ya KIMONDO inasikitishwa na taarifa hizi za upotoshwaji zinazofanywa na YANGA kwa makusudi kabisa kuwa mchezaji wetu hana mkataba na sisi.


  0 0
 • 07/05/15--12:24: TAARIFA KUTOKA TFF MUDA HUU

 • Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi anashiriki katika kongamano la Fainali za Dunia kwa Wanawake zinazofanyika Vancouver- Canada kwa siku tatu kuanzia tarehe 3 - 5 Julai mwaka huu.
  Katika kongamano hilo Malinzi ameambatana na katibu mkuu wa Chama cha Soka la Wanawake Tanzania (TWFA), Amina Karuma.
  Kongamano hilo la soka la Wanawake linahudhuriwa na nchi 209 wanachama wa FIFA, ambapo hufanyika kila baada ya miaka minne, pindi zinapofanyika fainali za Dunia kwa wanawake.
  Miongoni mwa wachangiaji wa kongamano hilo ni mjumbe wa kamati ya Utendaji ya FIFA, ambaye pia aliwahi kuwa Rais wa chama cha soka cha nchini Burundi, Lydia Nskera.

   

  STARS YAALIKWA CHAKULA CHA JIONI UBALOZINI
  Wakati huo huo Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager jioni ya leo ilialikwa chakula cha jioni na ofisi ya Ubalozi wa Tanzania iliyopo jijini Kampala.
  Katika hafla hiyo ya chakula cha jioni, wenyeji wakiwemo maofisa wa ubalozi , watanzania waishio nchini Uganda waliwapongeza wachezaji, viongozi kwa mchezo mzuri dhidi ya Uganda na kuwatakia kila la kheri katika safari ya jumatatu ya kurejea jijini Dar es salaam.
  Stats inatarajiwa kuwasili Dar es salaam uwanja wa Mwl. JK Nyerere jumatatu saa 10 kamili jioni kwa shirika la ndege la Rwanda.

  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA 

  MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0
 • 07/05/15--12:27: Opportunity of a Lifetime:
 • Watch this video on a lifetime opportunity that will get you to financial freedom and good retirement plans if you are an employee. Also it will offer you a very low barriers into entrepreneurship, providing training, support, and ample encouragement along the way.

  0 0


  0 0

  Na Bashir Yakub
  Kwa wale ambao tayari wana hati za majumba au viwanja wanajua wazi kuwa hati hizo zimeandikwa muda maalum, tofauti na wengi wanavyofikiria hasa wale ambao pengine hawajamiliki ardhi au wanamiliki ardhi lakini hawamiliki nyaraka hii.

   Hati unayopewa ina muda maalum wa kuishi. Sio kweli kwamba ukishapata hati basi ndio umemaliza, hapana. 
  Kama ilivyo kwa bidhaa nyingine au nyaraka nyingine kwa mfano leseni za kuendeshea vipando vya moto ambazo huisha muda (expire) ndivyo ilivyo kwa hati za nyumba/viwanja pia ambazo nazo huisha muda wake ( expire).

  0 0

  KAMPUNI ya Msama Promotions chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama, jana ilikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa vituo 10 vya kulea yatima ikiwa ni mwendelezo wa kusaidia makundi maalumu katika jamii.

  Akikabidhi misaada hiyo katika ofisi zake zilizopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam, Msama alisema misaada hiyo ni sehemu ya fedha za mauzo ya DVD za Tamasha la Pasaka la mwaka huu.

  Msama alisema kupitia mauzo ya DVD za Tamasha hilo ambalo lilifanyika April 6 katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, wameona ni vema kuwafariji watoto yatima.

  “Msama Promotions kama kawaida yetu, tumekuwa tukiyakumbuka makundi maalum katika jamii kama yatima, walemavu na wajane, hivyo leo hii tumewasaidia vitu mbalimbali watoto,” alisema Msama.

  Alisema kampuni yake imekuwa ikifanya hivyo sio tu kwa kutambua wajibu wake katika kusaidia jamii, pia kuguswa na mazingira ya watoto hao wanahitaji sapoti ya jamii nzima.

  “Watoto hawa ni kama wengine wanaokula, kunywa na kusaza katika familia zao, hivyo wanahitaji kusaidiwa na jamii nzima
  si jukumu la wenye vituo vya kuwalea tu,” alisisitiza Msama.

  Vituo vilivyonufaika na msaada huo wa jana, ni Chakuama, Maunga Centre, Mwandaliwa, Malaika, Honoratha, Zaidia, Mujahidin, Arahman na Almadina cha Tandale.

  Miongoni mwa vitu hivyo vilivyopokewa jana na viongozi wao, ni unga, sukari, mafuta ya kupikia, sabuni na vingine vingi kwa kila kituo.

  Msama alisema mwendelezo wa msaada wa kampuni yake utafanyika pia mikoani baada ya uzinduzi wa albamu tatu za mwimbaji wa injili, Bonny Mwaitege utakaofanyika Agosti 2.
                       
  Alisema sehemu ya mapato ya uzinduzi huo utakaofanyika katika Ukumbi wa Diambond Jubilee, jijini Dar es Salaam, yatanunua baiskeli 100 kwa ajili ya walemavu.

  Aliitaja baadhi ya mikoa itakayokumbukwa safari hii ni Iringa, Morogoro, Tabora, Dodoma, Tabora, Pwani, Mwanza, Mbeya na Singida.
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akimkabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula mtoto Haid Edwin (5) wa kituo cha Yatima cha Honorata cha jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akimkabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula watoto wa kituo cha Yatima cha Al Madina cha jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wanahabari wakijadiliana jambo kwenye tukio hilo

  0 0

   Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Askofu Mkuu Wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Dkt.Stephen Munga wakati wa maadhimisho ya Jubilei ya miaka 125 ya dayosisi hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Mbuyukenda mjini Tanga leo. Picha na Freddy Maro.
  ------------------------------------
  Sehemu ya hotuba ya Rais Kikwete juu ya 
  Dhima ya Viongozi wa Dini na Uchaguzi Mkuu
   Huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu ambao pia una umuhimu wa aina yake katika historia ya nchi yetu.  Tunaiaga Awamu ya Nne na kuikaribisha Awamu ya Tano ya uongozi wa nchi yetu. Niruhusuni nitumie fursa hii kuwaomba viongozi wa dini muiombee nchi yetu ipite kipindi hiki kwa salama na amani.  
  Uzoefu wa nchi nyingi za Afrika, chaguzi hutoa mwanya kwa uvunjifu wa amani. Haijawa hivyo kwetu, lakini haina maana kuwa tunayo kinga ya milele. Hata na sisi tunaweza kuwa kama wale iwapo yale yaliyowafikisha wenzetu hapo hatutayaepuka.

  Mafanikio yetu ya  kuendesha uchaguzi kwa amani na usalama yametokana na tahadhari ambazo Serikali na viongozi wa dini tumekuwa tukizichukua.  Tuendelee kufanya hivyo. Tusiwape mwanya wanasiasa wenye dhamira ovu kuwafarakanisha Watanzania.  

  Tuendelee kukemea matumizi mabaya ya fedha,  rushwa, hila, ghilba na hujuma katika chaguzi.  Tunapaswa kufanya hivyo tena zaidi sasa, wakati wa michakato ya ndani ya vyama vya siasa na baadae wakati wa uchaguzi.  

  Tuwakemee wanasiasa  wapenda madaraka kwa gharama yoyote, ambao watataka kutumia fedha kununua ushindi au  ubaguzi wa rangi, kabila, dini na kadhalika, kuwabagua wapinzani wao na kujijenga kisiasa.  

  Nawaomba msiwasikilize wala kuwaendekeza kwani mchezo wao ni mauti yetu.   Wakatalieni kwa macho makavu na kwa kweli. 

  Hatupaswi kukaa kimya dhidi ya watu wanaokiuka maadili na kuchochea mifarakano katika taifa letu. Hawa si watu wema watatufikisha pabaya. Hawaitakii mema nchi yetu.  Kamwe tusiruhusu wachezee dini zetu ambazo ni mhimili muhimu sana wa amani yetu. 

  Tofauti na ukabila ambao pamoja na ubaya wake, lakini unaweza kuhusisha eneo dogo, dini unahusisha nchi nzima.  Hakuna mtu, dini wala eneo litakalonusurika. Tutapoteza ile sifa yetu ya kihistoria ya kuwa lulu na mfano wa amani katika Afrika.  

  Tusikubali kumchukiza Mungu  akatukasirikia na kutuadhibu kwa jambo ambalo liko ndani ya uwezo wetu kulizuia lisitokee.  Kwa kweli mambo yakiharibika,  hatuwezi kumlaumu mtu mwingine yeyote bali  sisi wenyewe.  Katu hatuwezi kusema ni mapenzi ya Mungu bali itakuwa ni makosa yetu wenyewe.

  Nawaomba viongozi wa dini mlisaidie taifa letu.  Limeni mraba wenu vizuri nasi tulime wetu. Msiwape nafasi viongozi wa siasa na hata wa dini kutumia majukwaa ya dini kuendeleza maslahi yao ya kisiasa na  hasa kupandikiza chuki katika jamii.  

  Tunawategemea  viongozi wa dini msiwe sehemu ya makundi ya wagombea au vyama vya siasa. Mnatakiwa msiwe na upande bali  muwe juu ya pande zote. Hapo ndipo mtakapofanya vizuri kazi yenu ya ulezi na kuponya  taifa iwapo kutatokea matatizo.

  Hatuwategemei viongozi wa dini muwapangie waumini wenu vyama au viongozi wa kuwachagua. Tunawategemea kuwahimiza na kuwakumbusha kuutumia  haki na wajibu wao  vizuri, muwahimize na kuwakumbusha kuwa watatakiwa kufanya mambo matatu muhimu. 

  Kwanza, kujiandikisha, pili, kujitokeza kwenda kupiga kura na tatu kuchagua viongozi wazuri, wasiokuwa waovu, wasiofanana na uovu na kuukaribia uovu, watakaosukuma mbele gurudumu la maendeleo na kujali maslahi mapana ya jamii husika na nchi yetu.


  Kusoma hotuba yote BOFYA HAPA
  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Anthony Mavunde akizungumza wakati wa tamasha la kupinga na kukataa vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, lililofanyika katika viwanja vya mnara wa Mashujaa Mpwapwa.
  Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Anthony Mavunde (kushoto) akizungumza jambo na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Jacob Erasto Chimeledya wakati wa maadhimisho hayo ya kupinga na kukataa vitendo vcya ukatili kwa watoto.


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wizara yake katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne. Chikawe alisema kupitia taasisi zake yakiwemo Majeshi ya Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na Uokoaji, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Idara ya Wakimbizi pamoja na Idara zingine zilizoko chini ya wizara hiyo, imepata mafanikio makubwa hususani katika jukumu la msingi la ulinzi na usalama wa nchi jambo ambalo limewezesha nchi kuwa na amani na utulivu. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wizara yake katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne. Chikawe alisema kupitia taasisi zake yakiwemo Majeshi ya Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na Uokoaji, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Idara ya Wakimbizi pamoja na Idara zingine zilizoko chini ya wizara hiyo, imepata mafanikio makubwa hususani katika jukumu la msingi la ulinzi na usalama wa nchi jambo ambalo limewezesha nchi kuwa na amani na utulivu. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza (CGP), John Minja.
  Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (D-IGP), Abdulharman Kaniki akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu uwepo wa vituo vidogo vya polisi nchini (Police Posts) pamoja na majukumu yake. Kwa mujibu wa D-IGP, vituo hivyo vipo kwa mujibu wa sheria na haviruhusiwi kuwa na silaha za moto, na endapo askari wa vituo hivyo vidogo wakimkamata mtuhumiwa watampeleka katika vituo vikubwa vya polisi ili utaratibu mwingine wa kisheria uweze kufanyika. Kiongozi huyo wa Polisi alipewa nafasi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe ili kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu vituo hivyo, wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelezea mafanikio ya wizara katika Serikali ya Awamu ya Nne, uliofanyika katika Ukumbi wa wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athuman. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam. Benki ya CRDB inatoa huduma za kibenki katika maonyesho hayo ikiwa ni pamoja na kufungua akaunti kwa wateja wapya na kutoa huduma za kuweka na kutoa fedha katika tawi linalotembea iliyopo katika viwanja vya Sabasaba. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma (Na Mpiga Picha Wetu) 
    Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam.
  Wateja wa Benki ya CRDB wakipata huduma za kibenki katika tawi linalotembea lililopo katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Balozi wa Tanzania Ubelgiji, Luxembourg na Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu wa Taasisi ya Afrika Rise baada ya kikao kilichofanyaka Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Ubeligiji kuwasilisha taarifa za Tanzania kuteuliwa kuwa Nchi ya Heshima katika Kongamano la Biashara Kati ya Afrika na Ubelgiji litakalofanyika Aprili 2016. Makampuni zaidi ya 1000 kutoka Taanzania, Ubeligiji, Luxembourg, Afrika, Canada, Switzerland na Dubai yanatarajiwa kushiriki katika Kongamano hilo litakalofanyika Ubelgiji.

  0 0  0 0older | 1 | .... | 895 | 896 | (Page 897) | 898 | 899 | .... | 3285 | newer