Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

JESHI LA MAGEREZA LAIBUKA MSHINDI WA KWANZA KATIKA UTENGENEZAJI WA SAMANI MAONESHO YA 39 YA BIASHARA KIMATAIFA, "SABASABA", MWAKA 2015

$
0
0

Muonekano wa Samani za Ofisi ambazo hutengenezwa kwa Ustadi mkubwa katika Viwanda mbalimbali vinavyoendeshwa na Jeshi la Magereza zikiwa tayari zimekamilika kwa matumizi ya kiofisi 


Na Lucas Mboje wa 

Jeshi la Magereza
Jeshi la Magereza limeibuka Mshindi wa kwanza kwa upande wa Utengenezaji bidhaa za Samani kwenye Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Jijini, Dar es Salaam Maarufu "SABASABA" kwa Mwaka huu 2015.
Akizungumzia ushindi huo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja amesema kuwa anajivunia ushindi huo kwani kulikuwa na ushindani mkubwa wa Makampuni mengi yanayoshiriki katika Maonesho haya ya Kibiashara yanayoendelea.

"Nachukua fursa hii kwa dhati kuwapongeza sana Maafisa wote washiriki katika Banda letu la Jeshi la Maonesho kwa kazi nzuri iliyowezesha ushindi huo wa kwanza kwa upande wa Utengenezaji wa Samani Bora", alisema Jenerali Minja.

Aidha, Jenerali Minja amewaomba Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Jiji la Dar es Salaam watembelee Banda la Jeshi la Magereza ili waweze kujipatia bidhaa bora pia kuona na kujifunza namna bora ya utengenezaji wa bidhaa mbalimbali.
Kwa upande wao Maofisa wa Jeshi la Magereza wanaoshiriki katika Maonesho haya wameushukru Uongozi wa Jeshi la Magereza kwa kuwawezesha kushiriki kikamilifu hususani kufanikisha maandalizi yote muhimu ya kushiriki katika Maonesho haya ya Biashara yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Jeshi la Magereza Tanzania limepiga hatua kubwa ya Maboresho juu ya utengenezaji wa bidhaa bora za Samani hivyo kupelekea kuibuka mara kwa mara Mshindi wa kwanza katika Maonesho mbalimbali ya Kibiashara hapa nchini.

The executive council of Tanzania Freight Forwarders association - TAFFA

DIRA YA DUNIA YA IDHAA YA KISWAHILI YA BBC, LONDON

YANGA YAPANIA KUBAKI NA KOMBE LA KAGAME

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein Afutarisha Mkanyageni, Pemba

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mkoani  Mkoa wa Kusini Pemba Bw. Hemed Suleiman wakati alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni katika futari iliyoitayarisha kwa Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni  Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini  Pemba
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba Bi Hanuna Ibrahim Masoud wakati alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni katika futari iliyoitayarisha kwa Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni  Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini  Pemba 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akishiriki katika swala ya magharibi iliyoswalishwa na Sheikh Chumu Salim  kabla ya futari iliyoitayarisha kwa Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni  Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini  Pemba jana  katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni
 Akinamama wa Vijiji tofauti vya  Mkoa wa Kusini Pemba wakiwa katika futari iliyotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein jana  katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni
 Wananchi na Waislamu wa  Kijiji cha  Mkanyageni Wilaya ya Mkoani  Mkoa wa Kusini  Pemba wakiwa katika  futari iliyotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein jana katikaviwanja vya Skuli ya Mkanyageni
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Viongozi wengine wakiitikia dua iliyoombwa baada ya kufutari pamoja na Wananchi wa Kijiji cha  Mkanyageni Wilaya ya Mkoani  Mkoa wa Kusini  Pemba jana katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni

MAGUFULI AKIJIBU MASWALI YA BUNGE KWA UMAHIRI MKUBWA - JUNE 2015

JOTO LA ASUBUHI LA 93.7 EFM JUMATATU JULY 6, 2015

Kikao cha Kamati Maalum ya CCM Zanzibar kufanyika kesho


WAZIRI KOMBANI AFUNGUA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU

$
0
0
Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Selina Kombani akiwahutubia wajumbe waliohudhuria Kikao cha Pili cha Baraza la Nne la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu lililofanyika jana katika ukumbi wa Hazina Ndogo mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akielezea machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa Kikao cha Pili cha Baraza la Nne la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo lililofanyika jana katika ukumbi wa Hazina Ndogo mkoani Dodoma.
Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Selina Kombani akimkabidhi hundi mmoja wa wastaafu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ibrahimu Masanja mara baada ya kufungua Kikao cha Pili cha Baraza la Nne la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo lililofanyika jana katika ukumbi wa Hazina Ndogo mkoani Dodoma.

TTCL Yakuza Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Waziri Mkuu Atembelea Banda Lao

$
0
0
Waziri Mkuu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Peter Pinda akiwapongeza washiriki kwa kubuni  huduma mbalimbali katika Maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba. Wa pili kutoka kulia ni Kaimu mkuu wa Biashara Kanda ya Dar es Salaam Bw. Karim Bablia. Waziri Mkuu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Peter Pinda akiwapongeza washiriki kwa kubuni huduma mbalimbali katika Maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba. Wa pili kutoka kulia ni Kaimu mkuu wa Biashara Kanda ya Dar es Salaam Bw. Karim Bablia.Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Veronica Ngusaru (kushoto) kuhusu faida mbalimbali za kutumia mtandao wa TTCL ndani ya banda la kampuni hiyo alipotembelea Maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba. Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Veronica Ngusaru (kushoto) kuhusu faida mbalimbali za kutumia mtandao wa TTCL ndani ya banda la kampuni hiyo alipotembelea Maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba.Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Jotham Lujava (katikati) akipata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazooneshwa na kampuni hiyo. Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Jotham Lujava (katikati) akipata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazooneshwa na kampuni hiyo.Picha ya pamoja ya maofisa wa kampuni ya TTCL wanaoshiriki Maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba. Picha ya pamoja ya maofisa wa kampuni ya TTCL wanaoshiriki Maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba.

IGP MANGU AFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOANI PWANI

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini ,IGP Ernest Mangu akikagua gwaride lililo andaliwa kwa ajili yake wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Pwani .IGP alikuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo ambapo alizungumza na Maofisa, Wakaguzi na Askari wa mkoa huo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGPErnest Mangu akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe.Evarest Ndikilo wakati alipomtembelea ofisini kwake wakati alipokuwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Pwani .IGP alikuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo ambapo alizungumza pia na na Maofisa, Wakaguzi na Askari wa mkoa huo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akizungumza na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama Mkoani Singida Bw.Bravo Ryapambile (katikati) wakati alipokuwa katika ziara yake ya kikazi katika wilaya hiyo ambapo alikagua baadhi ya vituo vya polisi vilivyopo katika wilaya hiyo.Kushoto ni Mkuu wa Polisi Wilayani Mkalama, Mrakibu wa Polisi Michael Marwa.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

Angalia Kipindi Chote Cha ' Nyumbani Na Diaspora' Kwenye TBC1.

TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services yafutulisha wadau wake

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Hemedi Mgaza, kushoto, akitembelea katika ofisi ya Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services katika futuru iliyoandaliwa na taasisi hiyo. Pichani ni wadau wengine walioalikwa katika futari hiyo.

TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services, jana imefuturisha wadau wake wanaoendelea na mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, huku ikiwataka kudumisha amani, umoja, upendo na mshikamano kwa Watanzania wote. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Utawala wa Bayport Financial Services, Evelyine Hall, katika futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wadau wake mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
Viongozi wa Taasisi ya Bayport Financial Services na wageni waalikwa wakijadiliana jambo katika futari ya Bayport iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Mwenye koti jeusi na kofia ni Haruna Mbeyu, akifurahia jambo.

Akizungumza katika futari hiyo, Evelyine alisema ni vyema Watanzania wote, hususan Waislamu kuutumia vyema mwezi huo, ikiwa ni nguzo muhimu katika Dini ya Uislamu Tanzania na duniani kwa ujumla. Alisema Bayport inaheshimu misingi ya dini zote, hivyo kwakuwa mwezi wa Ramadhan ni sehemu ya ibada kwa Waislamu, vyema wakautumia vizuri, sanjari na kulinda Amani, upendo, umoja, mshikamano, bila kusahau jamii kuishi kwa kuheshimiana ili nchi yetu iweze kupiga hatua. 
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Hemedi Mgaza wa tatu kutoka kulia, akipiga picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, mara baada ya kumaliza kufuturu katika futari iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, huku ikiandaliwa na Bayport.
Wakati wanatembelea katika ofisi ya taasisi hiyo baada ya kumaliza kupata futuru, jijini Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Abdallah Ulega, mwenye kanzu akizungumza jambo katika futuru iliyoandaliwa na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, iliyofanyika Makao Makuu ya Taasisi hiyo, mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa DC ni Meneja Utawala wa Bayport, Evelyine Hall na anayemuhoji DC ni Mwandishi wa Habari, Phillip Daudi, aliyeshika kipaza sauti. Picha na Mpiga Picha Wetu.

“Bayport Financial Services inajivunia kutoa huduma kwa Watanzania wote, ambao leo baadhi yao wapo katika ibada ya mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, hivyo tunaamini mwezi huu utakuwa na tija, endapo utatumiwa vyema,” alisema Evelyine. 

Naye Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kuwa Watanzania wamekuwa wakiishi kwa kuheshimiana, hivyo wanaamini wataendelea kutoa huduma bora ya mikopo ya fedha, mikopo ya viwanja, mikopo ya bidhaa mbalimbali kama vile injini ya boti, vifaa vya ujenzi, ambapo huduma zote hizo zinapatikana kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz na kupitia mawakala na ofisi zao zilizoenea sehemu mbalimbali za Tanzania Bara.
Mkuu wa Wilaya Kilwa, DC Abdallah Ulega kulia, akipiga picha na Meneja Utawala wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Evelyine Hall na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo kushoto. DC alikuwa miongoni mwa wadau walioalikwa katika tukio la futari lililofanyika jana jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na taasisi hiyo inayojihusisha na mambo ya mikopo.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya Kilwa, Abdallah Ulega, aliipongeza Bayport kwa kitendo chao cha kiungwana cha kuamua kuandaa futari hiyo kwa wadau wao. “Sisi serikali tutaendelea kuwaunga mkono wadau mbalimbali wenye kuamua kuanzisha mambo mazuri kama haya, hivyo tunawapongeza kwa dhati juu ya jambo hili muhimu linalojenga kuheshimiana kwa namna moja ama nyingine,” alisema Ulega.

Bayport Financial Services ni miongoni mwa taasisi za kifedha zinazojihusisha na mambo ya mikopo, ikiwa na mchango mkubwa kwa Watanzania wote wanaoamua kukopa ili kujikwamua kiuchumi, ambapo watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni zilizoidhinishwa wamekuwa wakinufaika kwa kiasi kikubwa tangu taasisi hiyo ilipoanzishwa nchini.

Balozi wa Tanzania nchini Oman aandaa futari mjini Muscat

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Oman Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh aliandaa hafla ya Futari kwa ajili ya Wawakilishi mbalimbali kutoka serikali ya Oman, Mabalozi, Jumuiya ya wafanya biashara, watanzania na wageni mbalimbali iliyofanyika nyumbani kwa Mheshimiwa Balozi maeneo ya Shatti Al Qurum. 
 Mgeni rasmi katika Hafla hii alikuwa Sayyid (His Highness) Mohamed bin Salim Al Said , Mkuu wa Itifaki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Oman, halfla hii pia ilihudhuriwa na Nasser Al Busaidy, Afisa Mwandamizi katika Idara ya Itifaki ya Ofisi ya Mfalme (Royal Court ) mabaloz mbalimbali akiwemo Balozi wa Afrika Kusini Mheshimiwa Jenerali Chris Pepani, Balozi wa Palestina Ahmed Abbas Ramadhan, Bolozi wa Pakistan Mheshimiwa Ayaz Hussain na Balozi wa Indonesia Mheshimiwa Sukanto pamoja na wawakilishi wa Jumuiya ya wafanya biashara, Marafiki wa Tanzania (Friends of Tanzania) na watanzania wanaoishi Oman.
Wageni waalikwa kinamama wakipata Futari
Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh, wa pili kulia Balozi wa Tanzania nchini Oman akiongea na wageni wake wakati wakipata futari

Wageni waalikwa wakipata Futari
wageni waalikwa wakubwa kwa wadogo wakipata Futari
Waliokaa kutoka kushoto ni Nasser Al Busaidy , Afisa Mwandamizi katika Idara ya Itifaki ya Ofisi ya Mfalme (Royal Court ) , Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman  katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi His Highness Mohamed bin Salim Al Said Mheshimwa Chris Pepani, Balozi wa Afrika Kusini na  Sheikh Abdallah Al Zakwan, Mwakilishi wa Jumuiya ya wafanyabiashara

PLEASE VOTE FOR VANESSA MDEE IN MTV AFRICA MUSIC AWARDS 2015


TAIFA STARS YATOKA SARE YA 1-1 NA UGANDA CRANES JIJINI KAMPALA LEO

$
0
0
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)  imetoka sare ya bao 1- 1 dhidi ya wenyeji Uganda (The Cranes) katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN mwaka 2017 nchini Rwanda uliofanyika uwanja wa Nakivubo.
Stars ambayo leo imeonekana kubadilika katika mchezo wa leo, ilicheza soka la kuvutia tangu mwanzo mpaka mwisho wa mchezo hali iliyowaduwaza wenyeji Uganda.
Mpaka dakika 45 za mchezo za kipindi cha kwanza zinamalizika, Uganda 0 - 0 Tanzania. Kipindi cha pili kilianza kwa Stars kufanya mashambulizi mfululizo kupitia kwa washambuliaji wake John bocco na Rashid Mandawa.
Dakika ya 58, John Bocco aliipatia Tanznaia bao la kwanza kwa mkwaju wa penayi kufuatia mlinzi wa Uganda Bakaki Shafik kuunawa mpira wa ndani ya eneo la hatari.
Mara baada ya bao hilo Uganda walifanya mashambulizi mfululizo langoni mwa Stars na kufanikiwa kupata bao la kusawzisha dakika ya 82, kupitia kwa mchezaji Kizito Hezron.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika Uganda 1 - 1 Tanzania. Kwa matokeo hayo Uganda wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 4 - 1 na sasa watakutana na Sudan.
Mara baada ya mchezo huo kochaa mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema anashukuru vijana wake wamejitahidi kucheza vizuri, mchezo ulikua mzuri timu ilitengeneza nafasi chache na kuweza kutumia nafasi moja iliyopatikana.
Mkwasa amewaomba watanzania kuendelea kuwapa sapoti, wamekaa na timu kwa muda mfupi wa wiki moja tu lakini katika mchezo wa leo mabadiliko yameonekana, hivyo wanahitaji muda kidogo kuweza kukaa na vijana kwa muda mrefu ili kujenga timu bora.
Stars inatarajiwa kurejea Tanzania siku ya jumatatu mchana kwa usafiri wa shirika la ndege la Rwanda Air.
Taifa Stars: Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Haji Mngwali, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Frank Domayo,/Said Ndemla John Bocco, Rashid Mandawa/Salum Telela, Saimon Msuva/Ramadhan Singano.
The Cranes: James Alitho, Muzamiru Mutyaba, Brian Ochwo, Hassan Waswa, Denis Oola, Faruk Miya, John Shemazi/Robert Sentongo, Bakaki Shafik, Tekkwo Derick/Kizito Hezron/Kalanda Frank.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA 
MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Kongamano la PENUEL 2015 lilivyofana

$
0
0
Mwenyeji wa Kongamano la PENUEL 2015  Apostle Onesmo Ndegi na Kiongozi wa huduma ya Living Water Centre Kawe jijini Dar es salaam akiongea wakati wa Kongamano hilo lililofana sana.
 Apostle Onesmo Ndegi akizungumza na waamini.
Watumishi wa Mungu kutoka nchi mbalimbali waliohudumu katika PENUEL 2015 wakiwa na wake zao katika picha ya pamoja.
Kwa taarifa kamili na picha zaidi BOFYA HAPA


MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MH. SAID MECK SADICK ASHIRIKI KAMPENI YA MEDIA CAR WASH FOR CANCER LEADERS CLUB LEO

$
0
0


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Said Meck Sadick akizindua kampeni ya kuosha Magari katika viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya kuchangia Fedha kwa waandishi wa habari ambao wanamatatizo ya Kiafya ikiwemo Saratani ( MEDIA CAR WASH FOR CANCER).
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), BW. Assah Mwambene (kulia) akikabidhi kiasi cha fedha kwa Mmoja wa Waratibu wa MEDIA CAR WASH FOR CANCER Bw. Benjamin Thomson, zilizochangwa na Idara hiyo kupitia chama chao cha Maofisa Habari wa Serikali  ambao walichanga kiasi cha shilingi Milioni 1,680,000=. Katikati ni  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda.

Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na michezo pia imechangia shilingi 1,350,000/= baada ya kuguswa na  kampeni  hiyo adhimu ya kuwachangia waandishi wa Habari wenye Matatizo mbalimbali yakiwemo ya Saratani.

Kampeni hiyo imefanyika leo katika viwanja vya Leaders  Club  Kinondoni jijini Dar es salaam ambapo viongozi mbalimbali wakiwemo na wadau wa habari walishiriki zoezi la kuosha magari kwa kuchangia kiasi chochote cha fedha, Mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa Dar Es Salaam Mhe. Said Meck  Sadick.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda akishiriki kuosha moja ya Magari yaliyofika kuoshwa katika MEDIA CAR WASH FOR CANCER  kuchangia waandishi wa habari wenye magonjwa mbalimbali ikiwemo Saratani.
 Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe akiosha Gari wakati wa  Shughuli hiyo maalum kwa ajili ya Kuchangia waandishi wenye udhoofu wa afya zao (MEDIA CAR WASH FOR CANCER).
Ankali akiosha Moja ya Magari kwa ajili ya kuchangia waandishi wa habari ambao wana maradhi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Saratani
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Bw. Assah Mwambene akimshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda mara baada ya kushiriki zoezi la kuwachangia waandishi wa Habari wenye Matatizo mbalimbali yakiwemo ya Saratani (MEDIA CAR WASH FOR CANCER).
 Picha ya pamoja ya waandishi wa 
Habari pamoja na Baadhi ya Viongozi.

Unaweza Changia pia kupitia M-Pesa 0766 970240
au Tigo Pesa 0653 155 808.

KAMPENI YA MEDIA CAR WASH FOR CANCER NDANI YA VIWANJA VYA LEADERS CLUB JIJINI DAR LEO.

DIT yaongeza muda wa udahili wa wanafunzi wa kozi mbalimbali

$
0
0
Chuo cha Teknolojia cha Dar es Salam (DIT), imeongeza muda wa udahili wa wanafunzi wa kozi tofauti kutoka Agosti mwaka huu hadi kufikia Oktoba, lengo likiwa kutoa fura zaidi kwa waombaji kukamilisha taratibu. 
Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, Mkuu wa Uhusiano wa chuo hicho, Amaan Kakana alisema, wamesogeza muda kwa waombaji wa kozi hizo ambazo zitaanza rasmi Novemba ili kutoa fursa kwa wanafunzi wengi zaidi kupata fursa hiyo. 
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live


Latest Images