Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109935 articles
Browse latest View live

MEMBE ARUDISHA FOMU ZA KUGOMBEA URAIS MAKAO MAKUU YA CCM DODOMA LEO

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akikaribishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Rajabu Ruhavi baada ya kuwasili katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma jana kurudisha fomu za kuomba kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho, baada ya kupata wadhamini wanaohitajika. 
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (katikati), akikabidhi fomu za kuomba kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Rajabu Luhavi alipozirejesha katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma jana, baada ya kupata wadhamini wanaohitajika. Kulia ni Mkewe Mama Dorcas Membe.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (katikati), akikabidhi fomu za kuomba kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Rajabu Luhavi alipozirejesha katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma jana, baada ya kupata wadhamini wanaohitajika. Kulia ni Mkewe Mama Dorcas Membe.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (katikati), akizungumza na wanaCCM baada ya kurejesha fomu za kuomba kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), mjini Dodoma jana, baada ya kupata wadhamini wanaohitajika. Kulia ni Mkewe Mama Dorcas Membe na (kushoto) ni Kada wa CCM, Kapteni mstaafu Alhaj Mohamed Ligola. Picha na John Badi

DK.Shein Arejesha Fomu za kugombea Urais wa Zanzibar leo mjini Unguja

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akirejesha Fomu za kuomba ridhaa ya Chama kumchagua kuwa Mgombe Urais wa Zanzibar kupitia Chama Chake kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akitia saini kitabu maalum wakati wa kurejesha Fomu za kuomba ridhaa ya Chama kumchagua kuwa Mgombe Urais wa Zanzibar kupitia Chama Chake  CCM  katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akitia saini kitabu maalum wakati wa kurejesha Fomu za kuomba ridhaa ya Chama kumchagua kuwa Mgombe Urais wa Zanzibar kupitia Chama Chake  CCM  katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo akiwa na familia yake waliomsindikiza
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipeana mkono na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idii baada ya kurejesha Fomu za kuomba ridhaa ya Chama kumchagua kuwa Mgombe Urais wa Zanzibar kupitia Chama Chake  CCM  katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akitoka nje ya Jengo la Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja akifuatana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar mara aliporejesha Fomu za kuomba ridhaa ya Chama kumchagua kuwa Mgombe Urais wa Zanzibar kupitia Chama Chake  CCM  katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Viongozi mbali mbali waliomsindikiza nje ya Jengo la Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja   mara aliporejesha Fomu za kuomba ridhaa ya Chama kumchagua kuwa Mgombe Urais wa Zanzibar kupitia Chama Chake  CCM  katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo. Picha na Ikulu, ZNZ.

KESI YA MIRATHI YA MALI ZA MWANDISHI WA HABARI MKONGWE NCHINI YAUNGURUMA JIJINI ARUSHA

$
0
0
KESI ya kugombea  mirathi ya mwandishi wa habari mkongwe nchini marehemu Betty Luzuka (pichani) imeibua mapya  mahakamani mara baada ya ushahidi wa njia ya video kumuonyesha mke wa aliyekuwa ofisa mwandamizi wa  jumuiya ya  Afrika Mashariki ,Phil Makini Kleruu aitwaye Hilda Kleruu akichukua fedha za marehemu kabla na baada ya marehemu kuaga dunia.

Hilda, ambaye amefunguliwa kesi na kaka wa marehemu, Ssarongo Luzuka akimtuhumu kujimilikisha mali za marehemu bila kufuata utaratibu wa kifamilia na kimahakama mara baada ya marehemu kuaga dunia Agosti mwaka 2013 katika hospitali ya Shreee Hindu ya jijini Arusha baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kesi hiyo ya mirathi inayovuta hisia za watu mbalimbali jijini Arusha  ipo katika mahakama ya mwanzo ya Maromboso  yenye nambari 222 ya mwaka 2013 inaitaka mahakama hiyo ipitie hukumu yake iliyotolewa Septemba 27 mwaka 2013  na hakimu Prince Gideon iliyompa  ushindi kaka wa marehemu. Kwa habari kamili BOFYA HAPA

UTT-PID na SUMA JKT kujenga nyumba za kisasa za kuuza kwa askari na maofisa wa jeshi na umma

$
0
0
2015-06-26 15.13.03Mtendaji Mkuu wa UTT-PID, Dr. Gration Kamugisha (kushoto) akipeana mikono na Mkurugenzi Mkuu Lt-Colonel, Felix Samillan baada ya kutiliana saini ya mkataba wa kujenga nyumba za kisasa za kuuza kwa askari na maofisa wa jeshi na umma mradi unaotarajiwa kujengwa Chalinze

Na Mwandishi Wetu
Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT-PID) kwa kushirikiana na Taasisi ya SUMA JKT imesainiana mkataba wa makubaliano wa ujenzi wa nyumba za kisasa za kuuza kwa askari na maofisa wa jeshi na Umma, tukio lililofanyika Juni 26, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Katika tukio hilo, Taasisi ya UTT PID iliwakilishwa na Afisa Mtendaji Mkuu Dr. Gration Kamugisha na Taasisi ya SUMA JKT iliwakilishwa na Mkurugenzi Mkuu Lt-Colonel, Felix Samillan huku mradi huo ukitegemea kuanza katika kipindi cha mwaka mpya wa fedha wa serikali Julai mwaka huu.
Aidha, nyumba zinazotarajiwa kujengwa zitakuwa ni za vyumba viwili na vitatu katika miundo mbalimbali na za kuvutia ambazo zitakuwa za mfumo wa kisasa kwa kuishi kifamilia pia.
Katika mkataba huo utatanguliwa na ujenzi wa nyumba za mfano katika eneo la Chalinze na mara baada ya ujenzi huo kukamilika, Nyumba za mradi zitajengwa kwa walengwa wote watakaokuwa wameomba na kukidhi vigezo muhimu vya kupata nyumba hizo.
UTT-PID inafanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na Utoaji huduma za ushahuri katika maeneo ya upembuzi yakinifu wa miradi mbalimbali, Uratibu wa fedha na huduma zinazohusiana katika maandalizi ya mapendekezo ya miradi kwa benki au taasisi za fedha, uteuzi wa watoa huduma kuhusiana na maandalizi ya zabuni na usimamizi wa majengo na mali ambao ni utoaji wa huduma fanisi za usimamizi wa majengo yaliyochini ya uangalizi thabiti wa taasisi.
Pia wanaendesha miradi ya viwanja maeneo mbalimbali nchini ikwemo Bagamoyo, Chalinze Mkoa wa Pwani, Lindi, Kagera, Korogoro na mikoa mingine mingi.

Mhandisi Edwin Amandus Ngonyani ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico)

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mhandisi Edwin Amandus Ngonyani (pichani) kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico). Uteuzi huo umeanza Jumapili iliyopita, Juni 28, 2015. 
Taarifa ya kuthibitisha uteuzi huo iliyotolewa Ikulu, Dar es salaam na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) leo, Jumanne, Juni 30, 2015, inasema kuwa kabla ya uteuzi  wake Mhandisi Ngonyani alikuwa Mkaguzi Mkuu wa Migodi na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Stamico. 
Mhandisi Edwin Ngonyani ni mhandisi wa migodini mwenye uzoefu wa muda mrefu wa sekta ya madini. Anayo shahada ya kwanza ya fani hiyo kutoka Chuo Kikuu cha Zambia na shahada ya uzamili (MSC) kwenye fani hiyo hiyo kutoka Chuo Kikuu cha Exeter, Camborne School, Uingereza. 
Mhandisi Ngonyani amefanya  kazi  nzuri wakati anakaimu nafasi ya Ukurugenzi Mtendaji na kwa kumteua, Rais Kikwete ana imani kubwa kuwa ataendeleza kazi hiyo nzuri ya kuimarisha uwekezaji wa umma katika sekta hiyo ya madini kupitia Stamico.


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu – Dar es Salaam.


30 Juni, 2015

UJUMBE WA WAFANYABIASHARA KUTOKA KOREA WATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA NISHATI NA MADINI KWENYE MAONESHO YA SABASABA

$
0
0
 Mmoja wa wafanyabishara wa nishati kutoka Korea akiangalia  vinyago kwenye banda la  Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC) kwenye Maonesho  ya Kimataifa ya  Sabasaba (Dar es Salaam International  Trade Fair; DITF) yanayoendelea katika  viwanja  vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam

 Afisa wa Huduma kwa Wateja kutoka Shirika la  Umeme Nchini (TANESCO)  Lucas Kusare ( wa pili kutoka kulia) akiwaonesha  wafanyabiashara wa nishati kutoka Korea mfano wa mtambo wa kuzalisha umeme kwa njia ya maji katika  Banda la  TANESCO kwenye Maonesho  ya Kimataifa ya  Sabasaba (Dar es Salaam International  Trade Fair; DITF) yanayoendelea katika  viwanja  vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam

 Mtaalam kutoka Idara ya Madini Mhandisi Rayson Nkya (Katikati) akimwonesha  Makamu wa Rais wa Kampuni  ya  Energy and Minerals  Resources Development  Association ya Korea,  Dk. Song Jae Ki (Kulia) moja ya machapisho  ya Wizara ya Nishati na Madini kwenye Maonesho  ya Kimataifa ya  Sabasaba (Dar es Salaam International  Trade Fair; DITF) yanayoendelea katika  viwanja  vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni   Godfrey Fweni kutoka  Idara ya Madini ya Wizara hiyo. 
 Mmoja wa wafanyabiashara kutoka Korea (Kulia) akiangalia vinyago katika banda la Kituo cha Jimolojia  Tanzania (TGC) Kushoto ni Afisa Utawala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Matiko Sanawa.

Washirki kutoka Wizara ya Nishati na Madini, wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Maonesho  ya Kimataifa ya  Sabasaba (Dar es Salaam International  Trade Fair; DITF) yanayoendelea katika  viwanja  vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI , UTALII NA MICHEZO ZANZIBAR AZINDUA HOTELI TAUSI Palace, MJI MKONGWE ZANZIBAR

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk (kulia) akiwa na mwenyeji wake Mwenyekiti wa Makampuni ya Hoteli ya Mark and High Class Group Tanzania Rustam Merani wakingia katika Hoteli yao mpya ya Tausi Palace iliyopo Shangani Mjini Zanzibar.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk  akikata utepe akiwa na mwenyekiti wa Makampuni ya Hoteli ya Mark and High Class Group Tanzania Rustam Merani.
 Mwenyekiti wa Makampuni ya Hoteli ya Mark and High Class Group Tanzania Rustam Merani akimuonesha moja ya vyumba cha Hoteli hiyo Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk mara baada ya kuizundua rasmi.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk akizungumza na Wadau mbalimbali mara baada ya kuzinduliwa Hoteli ijulikanayo kama ‘TAUSI Palace’ iliyopo Shangani, Mji Mkongwe Zanzibar. 
Mwenyekiti wa Makampuni ya Hoteli ya Mark and High Class Group Tanzania Rustam Merani akizungumza na Wageni na Wadau mbalimbali (hawapo pichani) mara baada ya kuzinduliwa Hoteli ijulikanayo kama ‘TAUSI Palace’ iliyopo Shangani, Mji Mkongwe Zanzibar. Picha zote na Makame Mshenga. Picha zote na Makame Mshenga.
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

MAHAKAMA YA TANZANIA YASHIRIKI KATIKA MAONESHO YA 39 YA BIASHARA YA KIMATAIFA ‘SABASABA’ 2015

$
0
0
 Muonekano wa Banda la Mahakama ya Tanzania likiwa katika Viwanja vya Julius Nyerere maarufu kama Viwanja vya Sabasaba, Mahakama ya Tanzania inashiriki katika Maonesho haya lengo likiwa ni kutoa fursa kwa wananchi kupata elimu juu ya taratibu mbalimbali za Mahakama ikiwa ni pamoja na kutoa Malalamiko pamoja na kupokea maoni ya jinsi ya kuboresha huduma ya utoaji haki nchini. Banda la Mahakama lipo mkabala na Banda la Zanzibar ndani ya viwanja vya Sabasaba. Katika Maonesho ya mwaka huu, Mahakama ya Tanzania imepanua wigo wa kutoa huduma zake ambapo katika banda hilo kuna uwakilishi wa kila ngazi ya Mahakama kuanzia Mahakama za Mwanzo, Mahakama za Wilaya/Hakimu Mkazi, Mahakama Kuu pamoja na Divisheni zake ikiwa ni Divisheni ya Ardhi, Biashara na Kazi na Mahakama ya Rufani (T).
Vilevile katika banda hilo pia kuna elimu inatolewa kuhusiana na taratibu mbalimbali za ufunguaji wa kesi za mirathi na kadhalika, wananchi wote wanakaribishwa kutembelea banda hilo. 

 Bi. Wanyenda Kutta, Mkurugenzi Msaidizi wa Utumishi, Mahakama akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yahusuyo Mahakama kwa vijana wa scout waliotembelea banda hilo
 Vijana wa scout wakipata maelezo kuhusu mahakama

 Mhe. Eva Nkya, Naibu Msajili Mwandamizi, Mahakama Kuu ya Tanzania akifafanua jambo kwa moja ya wateja waliotembelea banda la Mahakama 
 

Mhe. Frank Mahimbali, Naibu Msajili- Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi akisisitiza jambo kwa wateja waliokuja kupata elimu ya Mahakama.  
Picha na Mary Gwera, Mahakama.

WASHINDI WA TUZO ZA TANAPA 2014 WAKABIDHIWA TUZO JIJINI MWANZA

$
0
0
Meneja Mawasiliano wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) ,Pascal Shelutete akitoa neno la ukaribisho katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanahabari waliofanya vizuri katika uandishi wa masuala ya Uhifadhi.Hafla iliyofanyika katika Hotel ya Gorden Crest jijini Mwanza. 
Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa ,Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza katika hafla hiyo juu ya lengo la kuanzishwa kwa tuzo hizo kwa wanahabari nchini.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akitoa ,Ngao,Vyeti pamoja na mfano wa Hundi kwa washindi wa tuzo za TANAPA 2014 zitolewazo kwa wanahabari.
Mkuu wa Majeshi Mstaafu,Meja Jenerali ,Mirisho Sarakikya akizungumza katika hafla hiyo zaii akizungumzia historia ya namna alivyoshiriki zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro zaidi ya mara 38.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Dkt. Magufuli akagua ujenzi wa Daraja la Kigamboni-Kukamilika mwezi wa Tisa mwaka huu

$
0
0
 Kazi za Ujenzi wa Daraja la Kigamboni ukiendelea kwa kasi

 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akikagua moja ya nguzo za barabara za juu flyovers katika maingilio ya Daraja la Kigamboni. Katika eneo hilo kutajengwa barabara za juu ili kuruhusu magari kupita kwa urahisi wakati wa kuingia na kutoka katika daraja hilo.
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (wakwanza kulia) akifanya ukaguzi katika mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mfuko wa Hifadhii ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhan Dau. Mradi wa Ujenzi wa Daraja hilo umefikia Asilimia 85, na unatarajiwa kukamilika mwezi wa tisa mwaka huu.

Ankal ajionea huduma mpya ya TTCL ya kupata matangazo ya Televisheni kwa njia ya internet viwanja vya sabasaba jijini Dar es salaam

$
0
0
Ofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania Bw. Karim Bablia aelezea huduma mpya ya TTCL ya kupata matangazo ya Televisheni kwa njia ya internet katika banda lao kwenye maonesho ya SabaSaba jijini Dar es salaam Juni 30, 2015.
Pichani Ankal akiwa na wadau wa TTCL alipotembelea banda lao na kupata maelezo ya huduma mpya ya IPTV,

MCHUMI WA BOT AELEZA SABABU ZA KUSHUKA NA KUPANDA GHAFLA KWA THAMANI YA SHILINGI YA TANZANIA

$
0
0
Mchumi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Lusajo Mwankemwa akielezea sababu za kushuka na kupanda ghafla kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania katika banda la BOT viwanja vya SabaSaba jijjini Dar es salaam Juni 30, 2015

TAARIFA MBALIMBALI ZA MICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA ( TFF)

$
0
0
Rais wa Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, Leodgar Tenga leo ametangaza kuanza kwa michuano ya kombe la Kagame itakayoanza kutimua vumbi Julai 18, 2015 na kumalizika Agosti 2 mwaka huu jijii Dar es salaam.

CECAFA YATOA RATIBA YA KAGAME 2015.

Rais wa Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, Leodgar Tenga leo ametangaza kuanza kwa michuano ya kombe la Kagame itakayoanza kutimua vumbi Julai 18, 2015 na kumalizika Agosti 2 mwaka huu jijii Dar es salaam.

Akiongea na waandishi wa habari leo katika ofisi za TFF zilizopo Karume, Tenga ameishukuru serikali ya Tanzania na TFF kwa kukubali kuwa wenyeji wa michuano hiyo mikubwa, vyombo vya habari na wapenzi wa mpira wa miguu nchini kwa sapoti yao na kuipokea kwa mikono miwili michuano hiyo.

Lengo la CECAFA ni kuona vilabu vya ukanda huu vinapata nafasi ya kucheza michezo mingi na kujiandaa kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Naye Rais wa TFF, Jamal Malinzi amewashukuru CECFA kwa kuipa Tanzania uenyeji huo na kuahidi TFF itahakikisha michuano hiyo inafanya nchini katika hali ya amani na usalama toka mwanzo mpaka mwisho wa michuano hiyo.

Timu zilizothibtisha kushiriki michuano hiyo ni Yanga, Azam (Tanzania), APR (Rwanda), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djibout), KMKM (Zanzibar), Khartoum-N (Sudan), Al Shandy (Sudan) LLB AFC (Burundi), Heegan FC (Somalia), Malakia (Sudani Kusini), Adama City (Ethipia) na KCCA (Uganda).

Wakati huo Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye ametangza ratiba ya michuano ya Kombe la Kagame itakayoanza kutimua vumbi Julai 18, 2015 jijini Dar es salaam ikishirikisha timu 13 kutoka nchi wanachama wa CECAFA.

Mechi ya ufunguzi tarehe 18 Julai, 2015 Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam itashuhudia wenyeji Yanga SC wakicheza na Gor Mahia ya Kenya, huku APR ya Rwanda ikicheza na Al Shandy ya Sudan na KMKM ya Zanzibar wakifungua dimba na Telecom ya Somalia.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

LOWASSA ARUDISHA FOMU LEO MJINI DODOMA, ATEMA CHECHE KWA WANAOMTUHUMU

$
0
0



WAZIRI Mkuu Mstafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa, amerejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwania kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.

 Mh. Lowassa ambaye alikuwa amesindikizwa na Wenyeviti wa CCM wa mikoa 12 kutoka bara na visiwani, aliwasili makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma majira ya saa 8:30 mchana wa leo Julai 1, 2015, na kupokewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Tanzania Bara), Rajabu Luhavi. 

Baada ya kukabidhi fomu hizo, Mh. Lowassa, alikutana na waandishi wa habari na kusoma taarifa yake fupi, ambapo alionya wale wote wanaoeneza habari potofu kuwa yeye ni mla rusha, watoe ushahidi, wapi amekula rushwa, na ni  kiasi gani, za nani na wapi, Awataka Watanzania kupuuza habari hizo na kwani yeye ni muadilifu na hana shaka na hilo. Alisema, yeye ana fedha kiasi gani za kuwapa Wana CCM 874,297, waliojitokeza kumdhamini.

 "Maneno hayo sasa basi, natoa changamoto kwa yeyote mwenye ushahidi huo autoe hadharani vinginevyo waache kueneza uvumi na uongo" Alisema Mh. Lowassa.  Alisema yeye anachukia umasikini, na kwamba endapo chama kitamteua na hatimaye Watanzania kumchagua kuwa Rais wa awamu ya Tano, atahakikisha anatimiza dhamira yake ya kuwaondolea Watanzania umasikini.


 Mh. Lowassa, ambaye alisindikizwa na Vigogo wa chama hicho akiwemo, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, na Mzee Pankrans Ndejembi wakiwemo wenyeviti wa CCM 12 kutoka Tanzania Bara na Visiwani, amehitimisha zoezi hilo baada ya kuzunguka mikoa 31 ya Tanzania Bara na Visiwani, na mara zote amekuwa akipata idadi kubwa ya wana CCM na wananchi waliojitokeza kwenye ofisi za CCM mahala alikopita, ikiwa ni pamoja na wengine kujipanga barabarani na kumpungia mikono
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa (katikati) akizipanga vyema fomu zake ili azikabidhi kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Rajab Luhavi (kushoto), wakati alipofika kwenye Ofisi ya CCM Makao Makuu, Mjini Dodoma leo Julai 1, 2015. Mh. Lowassa amerudisha fomu hizo, baada ya ziara yake ya nchi nzima kutafuta saini za WanaCCM wa kumdhamini ili apate ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015, ambapo jumla ya WanaCCM 874,297 walimdhamini.Kushoto kwa Mh. Lowassa ni Mkewe, Mama Regina Lowassa.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa (katikati) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Rajab Luhavi fomu za wanaCCM waliomdhamini ili aweze kuwania Uteuzi wa CCM wa kugombea urais kwenye kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Rajab Luhavi wakionyesha fomu hizo kwa wanahabari wakati wakikabidhiana, kwenye Ofisi ya CCM Makao Makuu, Mjini Dodoma leo Julai 1, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kurudisha fomu za wanaCCM waliomdhamini ili apare baada ya ziara yake ya nchi nzima kutafuta saini za WanaCCM wa kumdhamini ili aweze kuwania Uteuzi wa CCM wa kugombea urais kwenye kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.

watu wanne wafariki na 25 kujeruhiwa baada ya Gari kugonga Treni mkoani Morogoro

$
0
0
Taarifa ya ajali gari kugonga treni tarehe 01/07/2015 majira ya 0730 gari no T. 837 CTM aina ya ISUZU Jouney mali ya FEISAL s/o HUWEL ikitokea Tindiga kwenda Morogoro ikiendeshwa na Bakari s/o Seleman 35yrs mkazi wa kilosa iligonga treni no 88u03 treni iliyokuwa ikitoka Morogoro kwenda Dodoma ikiendeshwa na Inea s/o Chipindula 48yrs  mkazi wa Morogoro 
Ajali hiyo imesababisha vifo vya watu 4, (01)Salehe s/o Gombaike 35yrs mkutu, (02)Mama Husna 33yrs mzaramo mkazi mamoyo, (03)Sulat Mwajiri 06yrs, (04)Mwajiri 38yrs mkazi wa Pugu dar es salaam, majeruhi 25 wote wamelazwa hospitali ya wilaya Kilosa. 

Imetolewa na KAIMU RPC MOROGORO


MRATIBU MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA TANZANIA ATEMBELEA BANDA LA MODEWJIBLOG MAONYESHO YA SABASABA LEO

$
0
0
IMG_6278
Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akisalimiana na Mwandishi mwandamizi wa mtandao wa habari wa Modewjiblog, Andrew Chale alipotembelea katika banda la mtandao huo ambao mwaka huu mwezi Septemba unatimiza miaka 7 tangu kuanzishwa ambapo wametumia fursa ya maonyesho ya saba saba kukutana na wadau mbalimbali wanaotumia mtandao huo kupata habari mbalimbali sambamba na kubadilishana mawazo na ushauri wa maboresho ya kazi. Kushoto aliyefuatana naye ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu. Kulia ni mdau wa karibu na mshauri wa mtandao wa habari Modewjiblog, Lemmy Hipolite.
IMG_6282
Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, aliyeambatana na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akiangalia moja ya documentary ya TV katika banda hilo minayoonyesha wadau mbalimbali wanaotumia mtandao huu ambao walipata kuhojiwa.
DSC_0646
Mmoja wa wadau wa Modewjiblog, Rehema Pascal akiuzungumzia mtandao wa habari wa Modewjiblog alipotembelewa ofisini kwake wakati wa kurekodi 'documentary' hiyo.

President Kikwete Unvelis a Cornerstone for MICT Premises in Arusha

$
0
0
The Mechanism for International Criminal Tribunals President (MICT) Judge Theodor Meron welcomes President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete to Lakilaki village in Arusha to officiate the cornerstone unveiling signaling the commencement of construction of MICT premises. Looking on second left is the Chief Justice Mohamed Chande Othman and third left is Mr. Stephen Mathias who is Assistant Secretary General Office of Legal Affairs.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete unveils a cornerstone to signal the commencement of construction of MICT Premises at Lakilaki village in the outskirts of Arusha town this afternoon. Third Left is MICT President Judge Theodor Meron,Second Left is Chief Justice Mohamed Chande Othman,fourth left clapping is Mr.Stephen Cutts,Assitant Secretary General Central Support Services and behind the President is Mr.Stephen Mathias,Assistant Secretary General-Office of Legal Affairs.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete delivers his keynote speech during Cornerstone unveiling ceremony for construction of Mechanism for International Criminal Tribunals MICT Premises at Lakilaki village in Arusha.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete with MICT President Judge Theodor Meron during the ceremony in Arusha. (photos by Freddy Maro)

BENKI YA CRDB YAVUTIA WATU WENGI KATIKA MAONYESHO YA SABASABA

$
0
0
BENKI ya CRDB imewataka Watanzania kutembelea banda lao ili kupata huduma mbalimbali za Fedha.

Akizungumza katika Maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama sabasaba yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba, Ofisa wa benki hiyo, John Titus amesema kuwa banda lao linashughulika na kufungua akaunti na kumuhudumia mteja.


Aliongeza kuwa Benki ya CRDB pia imeweka Mobile  Branch ambayo hufanya kazi zote zinazofanywa na benki hiyo ikiwemo huduma za kuweka fedha na kutoa.


Titus alisema pia wanahuduma ya Jumbo ambayo ni akaunti kwa ajili ya watoto.


Alisema akaunti hiyo huwapa watoto fursa ya kuwekezewa fedha zitakazowasaidia katika masomo na maisha yao ya baadae.

Wateja wa Benki ya CRDB wakipata huduma za Fedha katika Mobile Branch katika maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba Barabara ya Kilwa.
Wateja wa Benki ya CRDB wakipata huduma za Fedha katika Mobile Branch katika maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba Barabara ya Kilwa.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA MITANO KUSAJILIWA NA KUPEWA VYETI BURE MKOANI MWANZA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mhe Zainab Rajabu Telack akiwahutubia Wananchi waliojitokeza katika Sherehe za uzinduzi wa Mkakati wa Uasajili na kutoa Vyeti vya kuzaliwa bure kwa Watoto wenye Umri chini ya miaka Mitano kwa kifupi (U5BRI) hafla iliyofanyika katika viwanja vya Kituo cha Afya Project wilayani Sengerema.

Mkuu wa wilaya hiyo akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Magesa Stanslaus Mulongo kama Mgeni rasmi katika Uzinduzi huo ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika kampeni ya siku saba kuanzia Tarehe 30 juni 2015 hadi 6 julai 2015 katika vituo vyote vya Tiba vinavyotoa huduma ya Mama na Mtoto kwenye wilaya zote za Mkoa wa Mwanza.

Tayari Mkakati kama huu ulizinduliwa mwaka 2013 na kutekelezwa katika Wilaya zote za Mkoa wa Mbeya na kuonesha mafanikio makubwa kwani hadi sasa zaidi ya Watoto laki mbili wamesajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa bure.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bi Emmy Hudson akiwahutubia Wananchi waliojitokeza katika Sherehe za uzinduzi wa Mkakati wa Uasajili na kutoa Vyeti vya kuzaliwa bure kwa Watoto wenye Umri chini ya miaka Mitano katika viwanja vya Kituo cha Afya Project wilayani Sengerema.
Wafanyakazi wa RITA wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe Zainab Rajabu Telack (katikati) walioketi.

DIAMOND PLATNUMZ KUITINGISHA MOSHI JULY 24, 2015 KWENYE MISS KILIMANJARO AMBASSADOR

Viewing all 109935 articles
Browse latest View live




Latest Images