Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 87 | 88 | (Page 89) | 90 | 91 | .... | 3286 | newer

  0 0   Waziri wa Kazi Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi na Ushirika wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Haruna Ali Suleiman akisalimiana na wachezaji wa ZSSF kabla ya mchezo wao na NSSF.
   Waziri wa Kazi Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi na Ushirika wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Haruna Ali Suleiman akisalimiana na wachezaji wa NSSF kabla ya mchezo wao na ZSSF.
   Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume akisalimiana na wachezaji wa timu ya NSSF.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Chiku Matesa akisalimiana na wachezaji wa NSSF.
    Mshambuliaji wa timu ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ally Chuo akitafuta mbinu za kumtoka beki wa ZSSF, Hamadi Nyange katika mchezo wa Tamasha la Pasaka uliofanyika kwenye Uwanja wa Amani mjini Zanzibar.
   Baadhi ya maofisa wa NSSF wakiongozwa na Juma Kintu (kushoto)
    Waziri wa Kazi Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi na Ushirika wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Haruna Ali Suleiman (kati) akifuatilia mchezo wa soka katika tamasha Pasaka lililofanyika kwenye uwanja wa Amaan mjini Zanzibar. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Chiku Matesa na Mkurugenzi Uendeshaji ZSSF, Abdulwakil Haji Hafidh. 
   Benchi la ufundi la ZSSF.
   Benchi la ufundi la timu ya NSSF.
  Waziri wa Kazi Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi na Ushirika wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Haruna Ali Suleiman akimkabidhi ngao ya ubingwa wa michuano ya tamasha la Pasaka, nahodha wa timu ya Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), Mohamed Hamad 'Loto' baada kuifunga timu ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa penati 4-2 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Aman mjini Zanzibar, mwishoni mwa wiki. 

  0 0
 • 04/02/13--01:57: KIJIWE CHA UGHAIBUNI

 • 0 0

  WAZIRI wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye bonanza la vyombo vya habari linaloandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).

  Bonanza hilo litafanyika Jumamosi wiki hii viwanja vya Sigara, Chang’ombe, Dar es Salaam kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa moja usiku likidhaminiwa na na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

  Pamoja na mambo mengine, Waziri Mwakyembe atakabidhi zawadi za vikombe na medali kwa washindi mbalimbali watakaoibuka siku hiyo, pia atapata fursa ya kuzungumza na washiriki wa bonanza hilo.

  Lengo la bonanza ni kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari bila kujali ni wa siasa, michezo, uchumi, afya na mambo mengine, ili kubadilishana mawazo na kufurahi pamoja na huwa linafanyika mara moja kwa mwaka, likiandaliwa na TASWA.

  Bonanza hilo ambalo litahusisha wadau 1,500 kutoka vyombo mbalimbali vya habari litaambatana na michezo mbalimbali itakayohusisha vyombo vyote vitakavyoshiriki na pia kutakuwa na burudani ya muziki.

  Tunataka bonanza la mwaka huu liwe la aina yake kuanzia mgeni rasmi, burudani, michezo na mambo mengine yawe ya kuvutia, ambapo Alhamisi Aprili 4,2013 saa tano asubuhi kutakuwa na mkutano na wanahabari mgahawa wa City Sports Lounge, Posta Dar es Salaam ambao ni maalum kutangaza makundi yatakayotumbuiza kwenye Media Day na tunatarajia makundi hayo nayo yatakuwepo kwenye mkutano huo.

  Tunaomba vyombo vya habari ambavyo havijathibitisha ushiriki wao kwa njia ya maandishi vifanye hivyo kama vilivyoagizwa kwenye barua zao za mialiko, vinginevyo ushiriki wao hautathaminika.

  Bonanza litaanza saa tatu asubuhi, ambapo baadhi ya michezo itakayoshindaniwa ni soka ya ufukweni, netiboli, wavu, mbio za magunia, mbio meta 100, kuruka kichura, kuvuta kamba, kucheza muziki na kuimba.

  Nawasilisha.

  Juma Pinto
  Mwenyekiti TASWA
  02/04/203

  0 0

  Mkuu wa Shughuli za Biashara za Kibenki wa Benki ya Afrika Tanzania, Bw.Wasia Mushi (kushoto) akigawa chakula kwa wagonjwa wa hospitali ya Walemavu ya CCBRT ya jijini Dar es Salaam Jumatatu ya Pasaka. Wafanyakazi wa benki hiyo waliungana na wagonjwa katika hospitali hiyo na kula chakula cha mchana pamoja katika sikukuu hiyo.
  Mkuu wa Shughuli za Biashara za Kibenki wa Benki ya Afrika Tanzania, Bw.Wasia Mushi (kushoto) akiongea na wagonjwa wa hospitali ya Walemavu ya CCBRT ya jijini Dar es Salaam Jumatatu ya Pasaka. Wafanyakazi wa benki hiyo waliungana na wagonjwa katika hospitali hiyo na kula chakula cha mchana pamoja katika sikukuu hiyo.
  Mkuu wa Shughuli za Biashara za Kibenki wa Benki ya Afrika Tanzania, Bw.Wasia Mushi (kulia) akigawa zawadi kwa wagonjwa wa hospitali ya Walemavu ya CCBRT ya jijini Dar es Salaam Jumatatu ya Pasaka. Wafanyakazi wa benki hiyo waliungana na wagonjwa katika hospitali hiyo na kula chakula cha mchana pamoja katika sikukuu hiyo.

  0 0

  Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof; Makame Mbarawa akipokea kutoka kwa Mkuu wa Mfuko wa Vodacom wa Kusaidia Jamii - Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule mfano wa hundi yenye thamani ya Sh 30 Milioni. Fedha hizo zimetolewa kumalizia ujenzi wa jengo la kituo cha afya cha Michenzani Mkoa wa Kusini Pemba.
  Mkuu wa Mfuko wa Vodacom wa Kusaidia Jamii - Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule akikabdhi kwa mmoja wa wazee wa shehia ya Michenzani Mkoa wa Kusini Pemba mfano wa hundi yenye thamani ya Sh 30 Milioni. Fedha hizo zimetolewa kumalizia ujenzi wa jengo la kituo cha afya cha Michenzani ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya katika eneo hilo. Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof; Makame Mbarawa(wa pili kushoto) na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim wakishudia.
  Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof; Makame Mbarawa akielezea ukwa Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule na Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni ya Vodacom Salum Mwalim(mwenye fulana nyekundu) ujenzi wa jengo jipya la kituo cha Afya cha Michenzani Mkoa wa Kusini Pemba muda mfupi kabla ya Vodacom Foundation kukabidhi hundi yenye thamani ya Sh 30 Milioni kumalizia ujenzi wa jengo hilo.
  Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof; Makame Mbarawa akiongoza kikundi cha ngoma ya kibati kutoka Chokochoko Mkoa wa Kusini Pemba kucheza ngoma hiyo wakati wa haflka ya kupokea hundi yenye thamani ya Sh 30 Milioni kumalizia ujenzi wa kituo cha Afya cha Michenzani Kisiwani humo zilizotolewa na Mfuko wa Vodacom wa kusaidia Jamii - Vodacom Foundation. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mfuko huo Yessaya Mwakifulefule akifurahia burudani hiyo.

  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Ndugu Leonard Thadeo katikati akizungumza na washiriki wa mafunzo ya siku mbili ya Sayansi ya Michezo yanayoendeshwa na wataalam wa Michezo kutoka katika Chuo cha Newman University Uingereza.Kulia ni Dkt. Iman Silver Kyaruzi na kushoto ni Dkt. Tony Myers. Semina hiyo inafanyika jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini Ndugu Leonard Thadeo( hayupo pichani) kuhusu Semina ya siku mbili ya Sayansi ya Michezo inayoendeshwa na wataalam wa Michezo kutoka katika Chuo cha Newman University cha London
  Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Ndugu Leonard Thadeo (Kushoto waliosimama) akitoa maelezo mafupi kwa mtaalamu wa michezo kutoka Newman University cha London Dkt.Tony Myers( kulia aliyesimama) katika Semina ya siku mbili ya Sayansi ya Michezo inayofanyika Jijini Dar es Salaam.( Picha zote na Benjamin Sawe wa WHVUM).

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja, akikata utepe kuzindua rasmi jukumu la kuwasafirisha Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani kwa Mkoa wa Arusha. Katikati ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aisha Nyerere akipongeza uzinduzi huo. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Arusha.
  Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kushoto) akisalimiana na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aisha Nyerere baada ya kutoa hotuba ya uzinduzi wa mabasi manne na gari ndogo moja (pick-up) kwa ajili ya kuwasafirishia mahabusu toka gerezani kwenda mahakamani na kurudi gerezani kwa mkoa wa Arusha. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Arusha.
  Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba yake kabla ya kuzindua mabasi manne na gari ndogo moja (pick-up) kwa ajili ya kuwasafirishia mahabusu toka gerezani kwenda mahakamani na kurudi gerezani kwa Mkoa wa Arusha. Katika hotuba yake mkuu wa jeshi hilo aliwataka maofisa magereza wa mkoa huo wawe makini kuyatunza magari hayo. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Arusha.
  Sehemu ya magari matano ya kuwasafirisha Mahabusu yaliyozinduliwa na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja, katika hafla iliyofanyika Gereza Kuu la Arusha.

  0 0  0 0


  0 0
 • 04/02/13--06:24: DEATH ANNOUCEMENT • 0 0

  Airtel Niger’s Regulatory Director, Mr. Karimou Salifou, receives the award from Salifou Labo Bouche, Minister of Communication and New Technologies.

  Bharti Airtel (“Airtel”), a leading telecommunications services provider with operations in 20 countries across Asia and Africa, has been named the Most Socially Responsible Company in Niger at the 3rd Edition of the National Excellence Awards Ceremony.

  Airtel Niger was awarded by the independent organization for Management Excellence that rates organizations and individuals distinguishing themselves for exceptional achievements during the year.

  Airtel Niger’s Regulatory Director Mr. Karimou Salifou, received the award on behalf of the Managing Director from Niger’s Minister of Telecommunications in the presence of government officials, corporate officials and civil society representatives.

  Speaking after the ceremony, Mr Salifou said “This is in recognition of the tremendous contribution Airtel has made through its corporate responsibility in Niger, through the adoption and refurbishment of schools in underprivileged and remote areas of the country. We believe these investments, as with others we have made to better the lives of the communities in Niger, will help support some of the infrastructure needs in schools.”

  He added: “We are also extremely humbled because this award recognizes what Airtel is doing in the 17 countries that we operate in across Africa, especially in the area of education. We believe this will go a long way in raising the literacy levels across the continent; we encourage more corporate organisations to join hands to help young students who we depend on for our future economic growth and development. ”

  In awarding Airtel, it was noted that the company’s contribution to underprivileged children was highly appreciated by communities, government and the civil society.

  According to the United Nation’s Development Programme (UNDP) index covering the years between 1980 and 2012, only 48 percent of the children in Niger are completing primary education, indicating a need for public-private partnerships in alleviating the challenge.

  Tiemoko Coulibaly, CEO for the Francophone Africa Region at Bharti Airtel said : “ Our community engagement in the Francophone countries that we operate in appreciates that there are unique socio-economic challenges. This distinction recognizes Airtel’s efforts in trying to touch the hearts of the communities that we serve.”

  0 0


  Familia ya Kanumba inawakaribisha katika kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo cha marehemu Steven Kanumba itakayofanyika Leaders Club  Jumapili hii tarehe 7 /04/  2013 kuanzia saa 8 mchana.

  Kutakuwa na uzinduzi wa muvi ya mwisho kufanywa na marehemu. Pia itaoneshwa kwa mara ya kwanza preview ya muvi iitwayo After death(Never happened before) iliyoandaliwa na Jackline Wolper kwa ajili ya kumuenzi marehemu Kanumba.Kutasindikizwa na Twanga Pepeta na wachekeshaji maarufu Tanzania.KIINGILIO NI BURE. MSIKOSE TUMUENZI NDUGU YETU.

  0 0
 • 04/02/13--11:20: Article 23


 • 0 0


  Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imekamilisha mchakato na kuridhia viwango vipya vya nauli kwa ajili ya usafiri wa mijini na usafiri wa kwenda mikoani. 

  Viwango hivi vipya vimefikiwa baada ya kufuata taratibu za kisheria na za kiutendaji ambazo SUMATRA kama msimamizi na mdhibiti wa sekta ya usafiri wa barabara inapaswa kuzifuata kabla ya kuridhia viwango hivyo. 


  Viwango vipya vya nauli vitaanza kutumika kuanzia tarehe 12 Aprili, 2013.


  0 0


  Na Abdulaziz,Lindi
  MKUU wa wilaya Kilwa Mkoani Lindi Mhe Abdallah Ulega (pichani juu)  ameeleza  kuwa wakati umefika sasa kwa watendaji na viongozi wa umma  kufanya kazi ya kuwahudumia  wananchi  bila ya kuwapangia muda maalumu wa kuonana nao. Aliyasema hayo katika  ziara mbalimbali za kukagua miradi ya maendeleo katika kata mbalimbali za Wilaya hiyo .

  Mhe Ulega akiongea na baadhi ya watendaji amewaasa kuacha urasimu wa utoaji  wa huduma kwa  jamii  na kubainisha kuwa Watendaji na watoa huduma mbalimbali za jamii kuwa vikwazo hali inayochangia wananchi kukosa imani na serikali yao kutokana na  vitendo/taratibu za kuwahudumia wananchi  ikiwemo kuwapangia muda maalumu wa kuonana nao kupata huduma stahiki  hali ambayo ni moja ya vikwazo vinavyolalamikiwa sana Wilayani Humo .

  ‘Mtumishi wa umma ni Yule aliyetayari kuwahudumia wananchi  kwa misingi ya haki, unyenyekevu nidhamu na uadilifu asiyekuwa tayari kufanya hivyo aamue kuacha kazi na kabla ya watu  kuichukia  na kuisema vibaya serikali yao wale wote watakao fanya kazi kwa  mazoea na kutotenda haki  kwa katika kutoa huduma kwa wakati wawajibike kabla hawajawajibishwa kwa sababu Hatuwezi kukubali kuona serikali ikitukanwa  na kupakwa matope kwa uzembe na makosa ya mtendaji  mmoja ambaye hataki kuwajibika”  alisema Ulega.

  Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo, Mhe Addo Mapunda (picha ndogo) akiongea na Globu ya Jamii  alibainisha kuwa ofisi yake imejipanga kuhakikisha Jamii zinapata huduma stahiki zinazotolewa na Halmashauri hiyo na kuahidi kueleza kuwa kipo kitengo cha kupokea Kero na Malalamiko ili kutafutiwa ufumbuzi.

   ‘Mwandishi nakuhakikishia Maagizo ya Mkuu wa Wilaya kuhusu watendaji ninayashughulikia ipasavyo na ndio maana naalika watendaji wa kata wote na maafisa Tarafa wote kila kukiwa na Baraza la Madiwani ili nao wafikishe ujumbe kwa wananchi wao maazimio  yote yanayotolewa na kupitishwa na Madiwani’

  Aidha Mapunda alisisitiza kuwa Ofisi yake imejipanga kuhakikisha Elimu inayotolewa wilayani humo Inaboreka ili kuondoka na aibu ya Wilaya hiyo kuwa ya mwisho na kutoa wito kwa jamii kushirikiana vema na Walimu waliopangwa katika shule zao ikiwa pamoja na kuanza kujenga nyumba bora kusaidia watumishi wanaoletwa kwa Kushirikiana ili walimu hao wafurahie kuishi


  0 0
 • 04/02/13--19:30: Ngoma Azipendazo Ankal
 • Kataa ama kubali lakini ngoma ya 'Georgina' ya Marijani Rajabu wakati huo akiwa na wana Sokomoko Safari Trippers ndio wiimbo wa Taifa wa maraha kwa watanzania.

  0 0


  Na Mwandishi Maalum

   Hatimaye, Mkataba wa Kimataifa wa kudhibiti Biashara ya Silaha, (ATT) ambao  wiki  iliyopita ulishindikana kupitishwa kwa kauli  moja baada ya Ujumbe wa  Syria,  Korea ya Kaskazini  ( DPRK)na Iran kutia ngumu,  umepitishwa  na Baraza Kuu la  67 la Umoja wa Mataifa kwa kupigwa kura.
   Mkataba huo umepitishwa kwa kura 154 za ndiyo,  huku Syria,  Iran na  Korea ya Kaskazini ( DPRK) zikipiga kura ya hapana na nchi 23 zikapiga  kura ya kutofungamana na upande wowote.

  Baraza hilo lilihitaji kura 97 tu kuupitisha  Mkataba tofauti na wiki iliyopita ambapo wajumbe  kutoka nchi 193 walioshiriki majadiliano ya wiki mbili  wakati wa MKutano wa  Mwisho wa Mkataba wa Silaha  walitakiwa kuupitisha  kwa kuunga mkono kwa kauli  moja badala ya kupiga kura.

  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kati ya mataifa yaliyopiga kura ya ndiyo, na hasa ikizingatiwa kwamba katika miaka yote ya majadiliano ya kuandaa  Mkataba huu, Tanzania imesimama kidete kwa kutaka   silaha ndogo na nyepesi ziwe sehemu ya mkataba pamoja na  risasi kwa kile ambacho Tanzania imekuwa ikisisitiza kwamba   silaha hizo zimekuwa tatizo kubwa na tishio la amani na usalama katika eneo la nchi za Maziwa Makuu.

  Baada ya kuona kwamba usiku ule wa  Marchi 28, Mkataba ulikuwa umekwama kupitshwa kwa kauli moja,  nchi moja ilitoa pendekezo la kutaka liandaliwe Azimio ambalo lingepelekea  Mkataba huo uwasilishwe   katika Baraza Kuu ili ukaamuliwe kwa  kupigiwa kura.

   Mkataba  utaanza kufanya kazi ndani ya siku 90 baada ya kuwa umeridhiwa kwa sahihi zipatazo   50.

  Kupitishwa kwa  Mkataba huo  kwa kwanza na wa aina yake na Baraza Kuu,   kuna andika historia  ya aina yake katika Umoja wa Mataifa, na hasa ikizingatiwa kwamba biashara ya silaha ni biashara nyeti na yenye faida kubwa kuliko hata biashara ya madawa ya binadamu.

  Lakini pamoja na faida kubwa inayopatika kutokana na biashara hiyo,   maisha ya mamilioni ya watu wasiokuwa na  hatia  yanapotea kila mwaka kutokana na  matumizi yasiyo halali ya sihala hasa zile nyepesi na ndogo ndogo.

  Dhumuni kuu la  Mkatana huu pamoja na mambo mengine ni  kusimamia na kuratibu Biashara  ya silaha zikiwamo,  mizinga ya kivita, magari ya kivita,  ndege za kivita,  helkpota za mashambuli, meli za kivita, makombora , silaha ndogo na  nyepesi.

  Aidha Mkataba  pamoja na masuala mengine hautaingiali uhuru wa nchi kununua silaha kwa matumizi yake ya ndani na haki ya kujilinda na kulinda mipaka yake, vile vile mkataba hauzui kufanya biashara au  kusafirisha aina yoyote ile ya silaha wala kuingilia taratibu ambazo nchi itakuwa   tayari imejiweka katika kudhibiti masuala ya silaha.

  Inatarajiwa kwamba utekelezaji wa mkataba huu  utasaidia sana kudhibiti silaha zisiangukie kwa makundi mbalimbali yakiwamo ya kigaidi na hivyo kujenga na kuimarisha amani na usalama wa jumuiya ya kimataifa.
  0 0

  Meneja uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu akiongea kwenye simu na mmoja wa washindi aliejishindia shilingi Milioni moja katika Promosheni ya”MAHELA”inayoendeshwa na kampuni hiyo,wanaoshuhudia katikati ni Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo,Bw.Benjamin Michael na Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini Abdallah Hemedy. Zaidi ya shilingi Milioni 152 bado zinaendelea kushindaniwa, Mteja anatakiwa kutoma neno MAHELA kwenda namba 15544 ili aweze kujinyakulia fedha taslimu.
  Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini Abdallah Hemedy, akionesha moja ya namba ya simu ya mshindi wa Promosheni ya”MAHELA”aliejishindia kitita cha shilingi Milioni moja, katikati ni Meneja wa huduma za ziada wa Vodacom Tanzania,Bw.Benjamin Michael na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Bw.Matina Nkurlu. Zaidi ya shilingi Milion 152 bado zinaendelea kushindaniwa,Mteja anatakiwa kutoma neno MAHELA kwenda namba 15544 ili aweze kujishindia fedha taslimu.

  0 0

  Kamishna wa Idara ya Sera ya manunuzi ya umma kutoka wizara ya Fedha Dk. Frederick Mwakibinga (kulia) akiongea jambo na Clemence Tesha ambaye ni mjumbe wa kamati ya sera ya manunuzi wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya sera ya manunuzi ya umma lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja lilihudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi.
  Emmanuel Maliganya ambaye ni Afisa Ugavi kutoka Benki Kuu ya Tanzania akichangia mada kuhusu utendaji kazi wa maafisa ugavi wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya sera ya manunuzi ya umma lililofanyoka hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma kuhudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi.
  Juma Fimbo kutoka Umoja wa wataalamu wa Manunuzi na Ugavi Tanzania akielezea jinsi maafisa ugavi wanavyotakiwa kufanya kazi zao kwa kutumia taaluma ya uchumi wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya sera ya manunuzi ya umma lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma na kuhudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi.
  Mkurugenzi wa Ugavi kutoka Akaunti ya Changamoto za Milinia (Millenium Challange Account) Marieth Ngaida akichangia mada wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya sera ya manunuzi ya umma lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma.
  Prof. Gaspar Munishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala akielezea kuhusu umuhimu wa kuboresha rasimu ya Sera ya manunuzi wakati wa kongamano la kujadili rasimu hiyo lililofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa JB jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma. Kulia ni Dk. Godfrey Sansa kutoka Chuo hicho.
  Khamisi Tikka kutoka Mamlaka ya Rufaa za zabuni akichangia mada wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya Sera ya manunuzi ya Umma lililofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa JB jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma na kuhudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi.
  Baadhi ya wajumbe kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi wakimsikiliza Prof. Gaspar Munishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala (hayupo pichani) wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya Sera ya manunuzi ya Umma lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma.Picha na Anna Nkinda – Maelezo

  0 0


   Mpishi wa Bia wa kampuni hiyo, Kelvin Nkya, akiwapatia maelezo maofisa wa majeshi ya Rwanda na Ghana, kuhusu idara mbalimbali za uzalishaji walipotembelea kiwanda cha bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam hivi karibuni. Maofisa hao waliongozwa na maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

  Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Oriyo akiwapatia maelezo ya awali maofisa hao wa kijeshi kutoka nchi hizo mbili.
   Mpishi wa Bia wa TBL, Kelvin Nkya akiwapatia maelezo maofisa hao namna bia inavyopikwa kwa kutumia kompyuta.


older | 1 | .... | 87 | 88 | (Page 89) | 90 | 91 | .... | 3286 | newer