Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 885 | 886 | (Page 887) | 888 | 889 | .... | 3348 | newer

  0 0


   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere  wakati alipokwenda kijijini  Butiama mkoani Mara kumsalimia akiwa njiani kuelekea Mwanza  akitoka Musoma Ijumaa.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na mtoto wa Baba wa Taifa Madaraka Nyerere wakati alipokwenda kijijini  Butiama mkoani Mara kumsalimia akiwa njiani kuelekea Mwanza  akitoka Musoma

  Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda akiwasha mshumaa kwenye kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere  wakati alipomtembelea mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere kijijini Butiama akiwa njiani kuelekea Mwanza akitoka Musoma
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akitazama kifimbo alichozawadiwa  na Mtoto wa Baba wa Taifa, Madaraka Nyerere  (kulia) wakati alipomtembelea mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere kijijini Butiama akiwa njiani kuelekea Mwanza akitoka Musoma  Juni 26, 2015.  Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma  Zelote Stephen
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana  katika futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  Magesa Mulongo kwenye hoteli ya Malaika mjini Mwanza. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

  0 0


  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wameongoza makundi ya vijana kutoka Shirikisho la Vyuo Vikuu pamoja na Machinga wa mjini Mwanza kukimbia mchakamchaka (jogging) kwa umbali wa zaidi ya kilometa 2,kuanzia Barabara ya Stesheni,kupitia barabara ya Posta,Kenyatta, Karuta,Lumumba maeneo ya Soko Kuu mpaka Stendi ya zamani Tanganyika.

  Viongozi mbali mbali walishiriki mchakamchaka huo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Magessa Mulongo,Mbunge wa Jimbo la Kwimba Mhe. Shanif Masoor na Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Ndugu Miraji Mtaturu.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana akikimbia  mchaka mchaka (jogging)katika mitaa ya jiji la Mwanza ,wengine pichani ni Katibu wa CCM wilaya ya Nyamagana Mpanda(kushoto),Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Ndugu Miraji Mtaturu na wa mwisho kulia ni Mwenezi wa CCM mkoa wa Mwanza Magelepa.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na vijana walioshiriki mchakamchaka (jogging) na kuwataka kuendelea kufanya mazoezi kwani yanasaidia kuimarisha afya na kujenga mwili.

  PICHA NA MICHUZI JR-MWANZA

  0 0

   Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad na  Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi wakiwa katika viwanja vya Ikulu Zanzibar kujumuika katika futari ya pamoja iliyoandaliwa kwa viongozi mbali mbali wakiwemo , Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pandu Ameir Kificho na Wawakilishi wa CCM. Hafla imefanyika punde baada ya kuvunjwa Baraza la Wawakilishi jana jioni
   Sehemu ya waalikwa katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein ikijumuisha viongozi mbali mbali wakiwemo   Wawakilishi wa CCM. Hafla imefanyika punde baada ya kuvunjwa Baraza la Wawakilishi jana jioni
   Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiagana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad Futari ya pamoja iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein ikijumuisha viongozi mbali mbali wakiwemo   Wawakilishi wa CCM. Hafla imefanyika punde baada ya kuvunjwa Baraza la Wawakilishi jana jioni. 
  Picha na IKULU, ZNZ

  0 0  TBC
  SIMUtv: Habari kadhaa zimepewa uzito wa hali ya juu katika Magazeti ya Leo. Wajua ni habari gani? Tazama hapa.      https://www.youtube.com/watch?v=0AJAUR8HoPI
   STAR TV
   Unajua leo June 27 kuna habari gani kuu katika magazeti ? Kuwa wa kwanza kufahamu kwa kuangalia uchambuzi hapa. SIMUtv                   https://www.youtube.com/watch?v=Oa-5Qa2Mse0

  0 0

  Watu wenye silaha wameshambulia hoteli moja ya kitalii iliyoko kwenye pwani ya Tunisia na kuwauwa watu 37.
  Maafisa wa serikali ya Tunisia wamesema kuwa mmoja wa washambuliaji hao aliuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa ulinzi na kuwa waliosalia bado wanasakwa na polisi.
  Shambulio hilo lilitokea katika mji wa Sousse, ambao huwavutia maelfu ya watalii kutoka bara Ulaya na Afrika ya Kaskazini.
  Hili lilikuwa shambulizi la pili dhidi ya hoteli ya watalii nchini Tunisia katika kipindi cha miezi michache iliyopita.
  Inaaminika kuwa washambuliaji hao waliwavamia watalii ufukweni.
  Mnamo mwezi Machi mwaka huu, wanamgambo wa Kiislamu waliokuwa wamejihami kwa bunduki waliwauawa zaidi ya watu 26 katika makavazi ya Bardo, iliyoko katika mji mkuu wa nchi hiyo Tunis.Makavazi hayo ya Bardo hilo lilikuwa maarufu sana kwa watalii.
  October mwaka wa 2013, mlipuaji wa kujitoa, alijilipua nje ya nyumba moja mjini Sousse, baada ya maafisa wa polisi kutibua jaribio lake la kutaka kuingia ndani na kuishambulia.
  Chanzo BBC Swahili.

  0 0

  Mifuko ya saruji  220 yenye thamani ya Zaidi Tsh milioni 3.
  Meneja wa kanda ya nyanda za juu kusini wa PPF Bw. Ephrahim Mwaikenda  akimkabidhi msaada wa saruji mifuko 220 yenye thamani ya Zaidi Tsh milioni 3 kwa  Mkuu wa shule ya Sekondari Idodi, Christopher Mwasomola  kwaajili ya kujengea majengo yaliyoungua moto katika shule ya Sekondari Idodi iliyopo tarafa ya Idodi mkoani Iringa.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
   TANGAZO KUHUSU USHIRIKI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII  KWENYE MAONYESHO YA 39 YA  BIASHARA YA KIMATAIFA YA DARES SALAAM
  1. Wizara ya Maliasili na Utalii inashiriki kwenye Maonyesho ya 39 ya  Biashara ya Kimataifa ya Dares Salaam (Saba Saba) yatakayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius.K.Nyerere,  Barabara ya Kilwa kuanzia tarehe 28 Juni hadi 8 Julai, 2015.
  2. Karibu kwenye Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii ujionee na kuelimika kuhusu shughuli za Utalii,  Ufugaji Nyuki, Uhifadhi wa Misitu, Malikale na Wanyamapori.
  3. Safari za kutembelea Hifadhi za Mikumi na Saadani kwa gharama nafuu zitakuwepo
  4. Aidha, Wizara itachezesha bahati nasibu ambapo mshindi atazawadiwa safari ya kwenda kutembelea Hifadhi ya Mikumi au Saadani.
  5. Pia, Utapata fursa ya kuwaona wanyamapori hai kama vile Chui, Mamba, Nyoka, Ndege wa aina mbalimbali pamoja na mfalme wa pori SIMBA.
  Karibuni Wote
  “Unganisha Uzalishaji    na Masoko ”

  0 0

   Watoto wakiwa katika moja ya michezo wakiwa na hatari ya katatwa na vitu vyenye nnja kali kwakuwa wanatembea bila kuvaa viatu.
  Watoto wakijaribu kuruka ukuta bila mafanikio.
   Hali si shwari kwa watoto hawa ambao walikua wakitaka kujaribu kuruka ukuta na kutokufanikisha lengo lao.

  0 0
 • 06/27/15--03:06: KILICHO BORAA ZAIDI
 •  Hali hapa itakuwa ngumu katikati ya barabara na  ni eneo la mistari ya pundamilia nani avuke na asivuke naona sasa wote wameona wavuke.
   Wazee wa kuchagua chagua wakiwa katika harakati za kupata kilicho boraaaa zaidi na ni saizi yake.
  Magari yakiwa katika hospitali yake na madaktari wakiwa katika shughuri ya kuyaweka sawa ili yaweze jongea kama mengine.(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA GLOBU YA JAMII.)

  0 0

  Mashindano ya Kombe la Meya Shinyanga 2015 (Pepsi Meya Cup 2015) yamezinduliwa rasmi leo na mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine Matiro katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga.

  Mashindano hayo ambayo yameandaliwa na mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam na kudhaminiwa na kampuni ya Vinywaji baridi ya  Pepsi (SBC Tanzania Ltd) yanashirikisha timu 17 za kata zote za manispaa hiyo na timu ya polisi Shinyanga.

  Mashindano ya Kombe la Meya Shinyanga yakihusisha mpira wa miguu yataendelea kufanyika hadi tarehe 25,Julai 2015 na yatakuwa yanafanyika siku tatu kwa wiki yaani Ijumaa,Jumamosi na Jumapili.

  Mshindi wa kwanza katika mashindano hayo ataondoka na kitita cha shilingi milioni moja na laki tano,kombe na medali ya dhahabu,wa pili shilingi milioni moja,kombe dogo na medali ya fedha na wa tatu shilingi laki tano,kombe dogo na medali ya shaba.

  Malunde1 blog ilikuwepo wakati wa uzinduzi huo,Kadama Malunde,ametuletea picha kutoka eneo la tukio....
  Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam akizungumza wakati wa ufunguzi wa Pepsi Meya Cup Shinyanga 2015,ambapo alisema lengo la mashindano hayo ya mpira miguu kwa vijana yatakayoshirikisha timu 18 za manispaa ya Shinyanga ni kwa ajili ya burudani,ajira na kusaka vipaji kutoka kwa vijana katika manispaa ya Shinyanga.

  Waamuzi wa mchezo wa ufunguzi wakikagua wachezaji wa timu ya Masekelo FC na Ngokol0 FC.

  Mgeni rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine akikagua timu ya Ngokolo fc kabla ya mechi ya ufunguzi kati ya Masekelo fc na Ngokolo fc haijaanza katika uwanja wa mpira wa Shycom Mjini Shinyanga.
  Mechi kati ya Masekelo fc na Ngokolo fc ukiendelea ambapo hadi mwisho wa mchezo,Masekelo fc bao 2,na Ngokolo fc bao 2.

  Wengine walipaki na baiskeli zao uwanjani kujionea kilichokuwa kinajiri uwanjani.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

   Mjumbe wa Bodi ya Filamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bi.Vicensia Shule(wa kwanza kutoka kushoto) akimwuliza  jambo Mwenyekiti wa makampuni ya Proin Bw,Johnson Lukaza(hayupo pichani) leo jijini Dar es salaam walipotembelea kujionea  miundombinu ya kampuni hiyo.Kutoka kulia ni Makamu mwenyekiti wa  wa Bodi iyo Bw.Sylvester Sengerema na katikati ni  Bw.Bishop Hiluka.
   Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi,Joyce Fissoo akichangia jambo wakati walipotembelea miundombinu ya Filamu ya Makampuni ya Proin.Bi Fissoo ametoa wito kwa makampuni yanayotengeneza Filamu Tanzania kuendelea kushirikiana na Serikali ili kuimarisha Tasnia ya Filamu na kusaidia katika kupambana na Changamoto mbalimbali.
  Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Bw,Johnson Lukaza akimwonyesha Katibu mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi,Joyce Fissoo  moja ya Kazi walizotengeneza na kuingia Sokoni,Pia aliiomba Serikali kusaidia kuweka sheria kali zitakazo zuia wizi wa Filamu nchini.
  Wajumbe wa Bodi ya Filamu Tanzania wakifurahia jambo na Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin Bw,Johnson Lukaza(wa tatu kutoka kushoto) walipotembelea miundombinu ya kutengenezea filamu ya Kampuni iyo eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam.Wajumbe hao walijionea jinsi Filamu inavyotengenezwa na pia walitembelea eneo kampuni iyo wanapojenga Studio ya kutengenezea Filamu.

  0 0

  Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii
  MAMIA wamejitokeza katika kuaga mwili wa aliyekuwa Mhariri wa Mawio na Mwanahalisi online  ,Edson Kamukara aliyefariki mwishoni wiki na anatarajiwa kuzikwa  Juni 29 mkoani Kagera.
  Wakizungumza wakati wa kuaga kwa aliyekuwa Mhariri wa Mawio na Mwanahalisi online  ,Edson Kamukara  wamesema ni pigo kwa tasnia ya habari kutokana na kuwa na kusimamia kitu anachoamini kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari .

  Akizungumza juu ya kifo chake ,Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amesema kifo cha kamukara ni pigo kutokana na kuwa na msimamo wa bila kuyumbusha na bahasha.
  “ Ni bora kuishi kwa kusimama kwa muda mrefu kuliko kuishi kwa kupiga magoti kwa muda mfupi hiyo ikiwa ni kuangalia kutumia kalamu kwa wanyonge bila masilahi ya wanasiasa”amesema Mbowe
  Kwa upande wa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP.Reginard Mengi amesema Kamukara alikuwa jasiri katika kufanya mbambo yake kwa kusimamia misingi ya habari na alikuwa hangalii fedha.
  “Fedha angekuwa Kamukara anaiangalia basi angekuwa tajiri kwani alikuwa ni mtu kusimamia misingi ya habari kwa ajili ya wanyonge”amesema Mengi.
  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema), Freeman  Mbowe akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama hicho,Dk.Wilbroad Slaa wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara  katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
   Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Hamis Kagasheki (katikati)akiwa na viongozi wa Chadema ,Kushoto ni  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema), Freeman  Mbowe na Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama hicho,Dk.Wilbroad Slaa wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara  katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
   Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Reginard Mengi akipeana mkono Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema) ,Freeman  Mbowe wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara  katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam. 
  Safari ya kuelekea Kagera kwaajili ya maziko ya  Mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara  katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.) 


  0 0


  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa nchini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla kwenye sherehe za kuadhimisha miaka miwili ya kutawazwa Papa Francis kuwa Kiongozi wa kanisa katoliki nchini jana jioni kwenye makazi ya balozi huyo jijini Dar es salaam
  Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa nchini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla qkihutubia kwenye sherehe za kuadhimisha miaka miwili ya kutawazwa Papa Francis kuwa Kiongozi wa kanisa katoliki nchini jana jioni kwenye makazi ya balozi huyo jijini Dar es salaam
  Rais Kikwete akigonganisha glasi na Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa nchini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla na Muadhama kardinali Polycarp Pengo kwenye sherehe za kuadhimisha miaka miwili ya kutawazwa Papa Francis kuwa Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani  jana jioni kwenye makazi ya balozi huyo jijini Dar es salaam

  Meza Kuu wakati wa hafla hiyo.
  rais Kikwete, Waziri Membe,  Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa nchini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla na  Kaimu Mufti wa Tanzania Sheikh abubakar Zubeiry kwenye sherehe hizo.
  0 0

  Mwanasiasa Mkongwe hapa nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akisani fomu ya udhamini mbele ya Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono mgombea huyo. zoezi hili limefanyika jioni ya leo Juni 27, 2015 kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Kinondoni, Mkwajuni Jijini Dar. ambapo kwa wilaya ya Kinondoni amepata udhamini wa wanaCCM 95, 251 na kufanya jumla kuu kuwa 212, 150 na kuifanya Dar es salaam kuwa Mkoa wa kwanza kuwa na idadi kubwa ya WanaCCM waliomdhamini Mh. Lowassa. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza na kuwashukuru wanaCCM wa Wilaya ya Kinondini Jijini Dar es Salaam kwa kumdhamini ili apate ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Jumla ya WanaCCM 212, 150 wamdhamini Mh. Lowassa jijini Dar.
  Katibu wa CCM Wilaya ya Temeke, Robert Kerenge akikabidhi fomu za Wadhamini kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa leo Juni 27, 2015. Jumla ya WanaCCM 72, 100 wa Wilaya ya Temeke Wamemdhamini Mh. Lowassa ili apate ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza na kuwashukuru wanaCCM wa Wilaya ya Ilala waliomdhamini ili apate ridhaa ya Chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Juni 27, 2015.
  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Ramadhan Madabida akizungumza jambo kumuhusu, Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa (kulia), wakati alipofika kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Dar es Salaam kusaini kitabu leo Juni 27, 2015, wakati akiwa katika ziara yake ya kutafuta saini za WanaCCM wakumdhamini ili apate ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 212, 150 kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
  0 0

   Wananchi wakiwa wamesimama juu ya daraja la zamani, wakati Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipokagua ujenzi wa daraja jipya la Isegenge katika Kata ya Mahina, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza leo.Ndugu Kinana kesho atahutubia katika mkutano wa hadhara utakaofanyika kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza,mkutano huo utarushwa moja kwa moja na televisheni mbalimbali ikiwa ni sehemu ya hitimisho ziara yake ya Mikoa mitatu,kuanzia Mkoa Kagera,Geita na Jijini Mwanza.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua ujenzi wa  daraja jipya la Isegenge katika Kata ya Mahina, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza leo.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika eneo la soko la Igoma, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza leo.
    Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na msafara wake wakiondoka katika eneo la mradi wa maji mara baada ya kuukagua na kupata maelezo mafupi juu ya mradi huo wa maji wa Fumagila katika Kata ya Kishiri, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji ilani ya CCM na uhai wa Chama katika jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza leo.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza katika mkutano wa hadhara aliofanya baada ya kuzindua Ofisi ya CCM  Kata ya Buhongwa, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza leo.
    Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, wakati wa uzinduzi  Ofisi ya CCM  Kata ya Buhongwa, Kinana akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza leo.  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Makamu wa Dkt. Bilal, wakati walipokuwa katika shughuli za kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max, zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Vangimembe Lukuvi ameanza ziara ya siku tatu Mkoani Iringa ambapo aliongea na watendaji wa Mkoa wa Iringa kuhusiana na migogoro ya ardhi inayoukumba Mkoa huo . Aidha, Waziri Lukuvi alipata fursa ya kukagua shughuli za Shirika la Nyumba la Taifa na kusikiliza migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi wa Manispaa ya Iringa na wilaya za jirani za Kilolo na Mufindi. 
   Katika ziara hiyo, Waziri Lukuvi amerejea kauli yake aliyoitoa katika mikoa aliyokwishafanya ziara kwa kuwaonya na kuwaagiza Maafisa ardhi, wapima, wathamini na maafisa mipango miji kuacha mara moja kujinufaisha kwa kuwadhulumu wananchi haki zao za ardhi. 
   Aidha ameutaka Uongozi wa Mkoa wa Iringa kuharakisha upimaji wa ardhi ya wananchi na utoaji wa hati na kutenga muda wao ili kuweza kusikiliza kero za wananchi ili kupunguza migogoro ya ardhi.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi akiwasili kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Iringa na kupokelewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayoub huku Meya wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi akishuhudia. Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayoub (kushoto) akitoa taarifa migogoro ya ardhi inayoukumba Mkoa huo na utekelezaji wake. Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayoub akitoa taarifa migogoro ya ardhi inayoukumba Mkoa huo na utekelezaji wake. Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa mkoa wa Iringa wakifuatilia kwa kina taarifa ya migogoro iliyokuwa ikisomwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayoub (hayupo pichani).
    Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi akizungumza katika kikao hicho kilichowashirikisha watendaji wa mkoa wa Iringa.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  CHANNEL 10.
  SIMUtv:  Hatimaye serikali ya Tanzania imekubali mapendekezo ya kuwaingiza mabaharia katika utafiti kwenye sekta ya mafuta na gesi.   https://www.youtube.com/watch?v=MwReNguQ3G4

  SIMUtv:  Kiongozi wa ACT Zitto Kabwe amewashauri Wakazi wa mikoa ya kusini Kuwashauri Wabunge wao kuhusu Mswaada wa Gesi kutojadiliwa.     https://youtu.be/2fQQbAGvuts

  SIMUtv:  CHADEMA Maendeleo CHADEMA kimetoa rai kwa Mwanachama yeyote kuchukuliwa hatua endapo atabainika kukigawa chama hicho.      https://youtu.be/XiTciGXx8jg

  SIMUtv:  Kiongozi Mkuu wa NCCR Mageuzi Mhe. James Mbatia akanusha uvumi juu ya chama hicho kujitoa katika Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA.  https://youtu.be/9I-neurG_xQ

  SIMUtv:  Wamiliki wa Vyombo vya habari wamekusanyika kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwandishi wa habari Edson Kamukara aliyekuwa akifanya kazi katika vyombo vya Mwanahalisi.    https://youtu.be/bbKDpjI55rI

  SIMUtv:  Waziri Mkuu wa Zamani Edward Lowassa amejizolea wadhamini zaidi ya laki 2 katika Jiji la Dar es salaam na kukanusha uvumi wa kuwa ananunua wadhamini.  https://youtu.be/VXLxVM-eM3E

  SIMUtv:  Rais Jakaya Kikwete ameliambia Jeshi la Magereza kuwafunza wahalifu waliopo magerezani ili watoke wakiwa na nidhamu njema pamoja na stadi za maisha.     https://youtu.be/DwzfYW6F0wY

  AZAM TV.
  SIMUtv:  Harakati za kusaka Urais zimeendelea kuzua gumzo kutokana na kila mmoja kuwa na sera za kipekee ndani ya chama kimoja. https://youtu.be/KF2e2QqHdZM

  SIMUtv:  Hatimaye Mwalimu Antony Khalfani Chalamila amejitokeza mjini Dodoma na kuchukua fomu ya kuwania urais na kufikisha idadi ya watangaza nia 41. https://youtu.be/wmXa9h0G0P4

  SIMUtv:  Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia amewaasa UKAWA kuwa umoja huo si CHADEMA bali ni nguvu ya pamoja ya kupigania haki na katiba mpya.        https://youtu.be/OA_1ADJ66GY
  SIMUtv:  Hali ya wasiwasi imetanda Mkoani Morogoro baada ya magaidi kuvamia na kumuua mkulima kwa kumkata na majambia.     https://youtu.be/yaC1mYxy3CE
    
  TBC.
  TBC: Hii ndiyo kauli ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kufuatia Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka nje kususia kikao hapo jana.      https://youtu.be/H3cCx7PzRYw

  TBC: Rais Jakaya Kikwete amelitaka Jeshi la Magereza kuwafunza wahalifu waliopo magerezani ili watoke wakiwa na nidhamu njema pamoja na stadi za maisha.     https://youtu.be/QjYYUnqB0DI

  TBC:  RAIS Jakay Kikwete aongoza waombolezaji kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita marehemu  Kelvin Max .     https://youtu.be/QjYYUnqB0DI

  TBC: Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani akiongozana na Amina Salum Leo wamerudisha fomu za kuwania urais Mjini Dodoma.   https://youtu.be/b8mPfOHGlRY

  STAR TV
  Katibu mkuu wa Maliasili na utalii Dk. Adelhem Meru atoa rai katika kuendeleza sekta ya utall ili Taifa liweze kunufaika na rasilimali zilizopo kusaidia kukuza uchumi wa nchi.  https://youtu.be/pMH8iJa_yt0

  Kilimo cha mpunga kimewanufaisha wakulima zaidi ya 1,200 mkoani Tabora kufuatia kuboreshwa kwa miundombinu ya skimu ya umwagiliaji Dudumo.    https://youtu.be/gD11tIvC-KA

  Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linawashikilia vijana 6 kati ya 50 wanaosadikiwa kuwa ni magaidi waliokutwa na silaha za moto.     https://youtu.be/FHBzpaZlxW8

  Mwenyekiti wa CHADEMA avitaka vyombo vya habari kuwawekea bima ya maisha Waandishi wa habari  wakati akiuaga mwili wa Mwandishi wa habari jijini Dar es salaam.    https://youtu.be/zSHwiJBLk4Q

  Watu 3 wamefariki Dunia na wengine kujeruhiwa kutokana na ajali iliyohusisha magari mawili ya mizigo kugongana Nje kidogo ya Dar es salaam.   https://youtu.be/RHYHwdYVqpQ

older | 1 | .... | 885 | 886 | (Page 887) | 888 | 889 | .... | 3348 | newer