Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 879 | 880 | (Page 881) | 882 | 883 | .... | 3278 | newer

  0 0


  BARAZA LA ULAMAA LIME KUTANA MUDA HU 

  NA KWA KAULI  MOJA WAME  MTEUA SHEIKH ABUBAKARI ZUBERI KUWA KAIMUMUFTI WA TANZANIA 

  KWA KURA ZOOTE 8 

  MUNGU AMBARIKIE NA 

  AMREHEM MUFTI ALIE TANGULIA MBELE YA HAQI

  0 0

    Marehemu Bibi Fatma Moh’d Othman Mjumbe wa Bodi ya
  Utumishi Serikalini ambae pia ni Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Mkoani

  Pemba aliyefariki dunia Hospitali ya Muhimbili na kuzikwa Kijijini
  kwao Kiwani Mkoa wa Kusini Pemba.

   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akijumuika pamoja na waumini wa Dini ya Kiislamu katika kumsalia Bibi Fatma Moh’d Othman aliyefariki Da es salaam juzi na kuzikwa Kijijini kwao Kiwani Wilaya na Mkoani Pemba.

  Balozi Seif pamoja na baadhi ya viongozi 
  wakiwasili makaburini kwa ajili ya Mazishi ya Bibi Fatma Moh’d Othman 
  hapo Kiwani Mkoa wa Kusini Pemba.

   Mwili wa Marehemu Bibi Fatma ukichukuliwa na 
   wananchi mbali mbali tayari kuupeleka makaburini mahali alipotengewa  maalum kwa kuzikwa.

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0
 • 06/22/15--05:30: Article 19


 • 0 0


   Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue (mwenye tisheti) akiangalia Tuzo iliyopata Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali  (CAG) iliyoshinda katika utoaji wa huduma za ukaguzi kwa nchi zinazotumia Kiarabu,Kingereza na Kifaransa (Afroasae) alipopita katika banda la CAG katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma  katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo  kushoto ni CAG,Profesa Juma  Assad .
   Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akisaini Kitabu cha wageni katika banda la CAG katika maonesho ya Wiki ya Utumishi  katika Viwanja vya Mnazi Mmoja  leo jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Kiongozi ,Balozi Ombeni Sefue (mwenyetisheti) akiwa kwenye picha ya pamoja kushoto ni CAG, Profesa Juma Assad  katika maoenesho ya Wiki ya Utumishi  Umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. 

  0 0

   Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali,Profesa Juma Assad akisaini katika kitabu cha wageni katika banda la Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa (TFDA) katika viwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo  anayeshuhudia ni Meneja wa Mawasiliano TFDA,Gaudensia Simwanza.
    Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa (TFDA).Hitt Sirro akimpa maelezo katibu Mkuu Kiongozi ,Balozi Ombeni Sefue (mwenye Kofia) katika Manonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Jijini Dar es Salaam nyuma ya Katibu Mkuu Kiongozi ni Meneja wa Mawasiliano,Gaudensia Simwaza.
   Katibu Mkuu Kiongozi ,Balozi Ombeni Sefue (Mwenyekofia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa (TFDA).Hitt Sirro katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma  katika viwanja vya Mnazi Mmoja ,jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue( katikati )akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula la Dawa (TFDA) (Picha na Emmanuel Massaka)

  0 0

   Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (wa pili kulia ), akimkabidhi zawadi ya mashine ya kushonea 'cherehani', kwa Betha Benedict (wa pili kushoto), mkazi wa Bunju Jijini Dar es Salaam baada ya kuwezeshwa na mpango wa Airtel Fursa “Tunakwezesha”. Kushoto ni mama yake Betha na kulia ni Meneja wa Airtel, Fadhili Mwasijeba.
  Bertha Benedict (watatu Kulia) akionyeshwa na meneja Huduma wa jamii wa Airtel Hawa Bayumi (wapili Kulia) vifaa alivyokabidhi na Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa. Kushoto ni   Irene Paul balozi wa Airtel kupitia mpango wa Airtel Fursa,  mama yake Betha na kulia ni Meneja mauzo wa Airtel kanda ya kusini, Fadhili Mwasijeba.
   Bertha Benedict (Kulia) akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Airtel mara baada ya kuwasili nyumbani kwake kwaajili ya kukabidhi zawadi kupitia mpango wa Airtel Fursa  (katikati), Meneja Huduma kwa jamii wa Airtel Tanzania Hawa Bayumi.
  Wafanyakazi wa Airtel wakishusha zawadi  zilizokabidhiwa kwa Bertha Benedict (hayupo pichani)  mkazi wa Bunju Jijini Dar es Salaam baada ya kuwezeshwa na mpango wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha”.
  Wafanyakazi  wa Airtel wakiwa katika picha ya pamoja na Bertha Benedict (wapili Kulia) mara baada ya kuwezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa. Kutoka kushoto ni Irene Paul balozi wa Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa, mama yake Bertha, Hawa Bayumi na Meneja mauzo wa Airtel  kanda ya kusini , Fadhili Mwasijeba


  KAMPUNI  ya Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel Fursa ambao umelenga kuwawezesha vijana wajasiliamali wadogo wadogo nchini umetoa msaada mwingine tena jijini Dar es salaam kwa msichana mjasiriamali Bertha Benedicto.

  Bertha ambaye amelelewa katika Kituo cha Kulea watoto cha Dogodogo Center Kilichopo Bunju Jijini Dar es Salaam na kuhitimu mafunzo ya mwaka mmoja ya ufundi wa kushona nguo kituoni hapo amepatiwa vifaa mbalimbali pamoja na cherehani ya kisasa ili kuendeleza ujuzi wake.

  Akiongea wakati wa makabithiano Meneja wa mahusiano ya jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi alisema  “ Airtel tumeona ni vyema kupitia mpango wetu wa Airtel Fursa kumpatia vifaa na mashine hii ya kisasa ya kushonea Bi Bertha Benedecto  kwa lengo la kumwezesha kuendesha shughuli zake za kiuchumi kwa ufanisi zaidi.  Sambamba na hilo  tumeweza kumpeleka kwenye mafunzo ya kumsaidia  kujijenga, kuweka mahesabu yake na kuendesha biashara yake ili aweze kukuza biashara na kuisaidia familia yake”.

  Tunaamini hii ni nafasi ya pekee kwa vijana wadogo kati ya umri wa miaka 17 mpaka 24 walioko katika maeneo mbalimbali ya nchi kuweza kufaidika na mpango huu wa Airtel Fursa wenye lengo la kuwawezesha vijana wajasiriamali wadogo wadogo kukuza mitaji na biashara zao kwa ujumla. Aliongeza Bayumi”

  Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Bertha amesema vifaa hivyo vitamwezesha kuendesha maisha yake na familia kwa ujumla huku Mama yake Immaculate Makinda akiishukuru Airtel kwa kuwa mkombozi kwao.

  Bertha alisema, “nawashukuru sana Airtel kwa kuweza kufanikisha ndoto zangu. Kwa kuweza kunipatia vifaa hivi vya kisasa. Nimekuwa nikipata ugumu wa kupata wateja kwani sikuwa na vitendea kazi vya kutosha vitakavyoweza kukidhi mahitaji ya wateja wangu lakini sasa naamini nitapata wateja wengi sana na kuinua biashara yangu”

  Kwa upande wake Mratibu wa Dogodogo Centre, bw.Issa Buzohela alisema, anaiomba kampuni ya Simu ya Airtel  kuendelea kukisaidia kituo hicho na kuinua vipaji vya vijana kwani nchi yetu imezungukwa na vijana wenye vipaji mbalimbali lakini hawana uwezo wa kuendeleza vipaji vyao.

  Mpaka sasa Airtel Fursa  imeshawawezesha vijana mbalimbali na kuboresha shughuli zao za kiuchumi kwa kuwapatia vitendea kazi  na kuwaingiza katika warsha za mfunzo ya Airtel Fursa ili waweze kutimiza ndoto zao.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiriano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya akimkaribisha Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kwenye Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati wa maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Habu Mkwizu.
  Balozi Sefue akisaini Kitabu cha Wageni katika Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
  Balozi Sefue akisoma Kitabu cha Sera ya Mambo ya Nje huku akisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Yahya.
  Katibu Mkuu Kiongozi,  Balozi Sefue (katikati), Naibu Katibu Mkuu Balozi Simba Yahya (kushoto) wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Manejimenti ya Utumishi wa Umma,  Bw. Habu Mkwizu alipokuwa akiwaelezea jambo.
  Picha na Reginald Philip

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akimvisha cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza Mhitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Magereza Daraja la Pili ambaye amefanya vizuri kwa upande wa Gwaride, Stafu Sajini Boniphace Felix. Mhitimu huyo amevishwa cheo hicho kwa niaba ya Wahitimu 216 wa Mafunzo hayo.
  Maafisa wa Jeshi la Magereza wakionyesha umahiri mkubwa wa mbinu mbalimbali za kujihami  na adui kama wanavyoonekana kikakamavu katika picha wakati wa hafla fupi ya kufunga Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili.
   Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufunga Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza.
   Kikundi cha kwaya kinachoundwa na Maafisa wa Jeshi la Magereza wa Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga kikitumbuza mbele ya Mgeni rasmi, IGP Ernest Mangu(hayupo pichani)katika sherehe za kufunga Mafunzo hayo ya Uongozi Daraja la Pili, Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga.


  0 0

   Bank M Dy.CEO Jacqueline Woiso talking to the audience during the AMCHAM's Daraja la Mafanikio event yesterday.
   From left: Janeth Reuben-Lekshingo-Gen.Manager,Organisatio Effectiveness,Acacia Mining Jacqueline WoisoPetro Kapembwa-HR Manager Cocacola Kwanza Miranda Naiman-Founder and managing director-Empower Kelvin Twissa-Head of Dept, Brand and Communications Vodacom Zuhura Muro-MD Kazi Services Hally Mahler-Director of HIV Programs & Senior Regions HIV Technical Advisor for Jhpiego Tanzania Sameer Gupta-Director Kamal Steel.
  From left: Janeth Reuben-Lekshingo-Gen.Manager,Organisatio Effectiveness,Acacia Mining Jacqueline Woiso Petro Kapembwa-HR Manager Cocacola Kwanza Miranda Naiman-Founder and managing director Empower Kelvin Twissa-Head of Dept, Brand and Communications Vodacom

  Zuhura Muro-MD Kazi Services Hally Mahler-Director of HIV Programs & Senior Regions HIV Technical Advisor for Jhpiego Tanzania Sameer Gupta-Director Kamal Steel


  0 0

     Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akipitia taarifa ya huduma zinazotolewa na Mfuko aliyokabidhibiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Michael Mhando baada ya kutembelea banda hilo katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
       Katibu Mkuu Kiongozi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa NHIF katika banda la maonesho ya wiki ya Utumishi.
    Picha ya pamoja ya watumishi wa NHIF wanaoshiriki maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma.PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.


  0 0

  Simba Sports Club leo hii imezindua tovuti yake Ili kukuza  mawasiliano  na  wadau wake mbalimbali  hususani; wanachama, wapenzi, vyombo  vya  habari na wadau wengine muhimu. 

  Akizungumza  wakati  wauzinduzi  huo  Rais  wa  Simba Evans Aveva  alisema ‘’Katika dunia na zama  za  utandawazi  tovuti  ndio  na  mitandao   ya   jamii   ndio  njia  kuu ya mawasiliano. Sisi  tuliliona  hili  na  leo  hii  nafurahi  kuwa  Simba Sports Club itazindua  rasmi  tovuti  yake  ambayo  itakuwa  jukwaa  kuu la mawasiliano  na utoaji wa taarifa zake za  club ya   Simba. Natarajia wengi wenu mtaitumia kikamilifu na muhimu zaidi mtatupa mrejesho chanya kuhusu  tovuti yetu’’. 

  AfisaMtendajiMkuuwa EAG Group Imani Kajula ambao ni washauri watekeleza ji wa Masokona Biashara wa Simba alisema ‘’Tovuti hii sio tuitaiwezesha Simba kuwapa wadau wake taarifa mbalimbalibali pia  itatumika  kwa  ajili  ya uuzaji  wa  vifaa  vya  Simba, Bidhaa  mbalimbali  mpya  na  muhimu  zaidi  kuwaunganisha   wanachama, mashabiki  na wapenzi wa  Simba  kutumia   mitandao  ya  jamii  iliyo   rasmi  ya  Simba Sports Club’’. 

  Mkutano   huo  wa  wandishi  wa  habari   ulitumika  kutaarifu   Wanachama, Wapenzina  Vyombo   vya   habari   juu   ya  kocha   mpya   wa   Simba. 

  Alizungumza  wakati  wakumtambulisha   kocha   mpya   wa   Simba, Rais   Aveva   alisema ‘’Baada ya kupitia  vyeti  na  maombi   ya  makocha   mbalimbali, Napenda  kuwa taarifu kuwa Klabu ya Simba imeingia  kwenye  mkataba  wa   kuifundisha   na   kocha Dylan Kerr raia   wa   Uingereza. Ni kocha   mwenye    uzoefu   wa   zaidi   ya   miaka 30, akiwa  amefanya  kazi  Nchi  mbalimbali  zikiwemo    Uingereza, Scotland, Vietnam   na    AfrikayaKusini’’. 

  Aliendelea  kusema ‘’Tunaamini   ujuzi   na   uzoefu wake wa  ukocha na pia kama mchezaji wa kiwango cha juu  utakuwa   chachu   ya   kuifanya   Simba    ifanye    vizuri’’.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group Imani Kajula Akimwelezea Jambo Rais wa Simba Sport Club, Evans Aveva (Aliyekaa) Wakati wa Uzinduzi wa Tovuti ya Club Hiyo Anayeshuhudia ni Makamu wa Rais wa Club ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu.

  0 0

   Watui wakifanya mazoezi katika siku ya yoga duniani iliyofanyika katika viwanja vaya kokobichi jijini Dar es Salaam jana.
  Baadhi ya wananchi wakifurahiya mazoezi yaliyokuwa yakiendelea katika fukwe za kokobichi jijini Dar es Salaam jana.PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.

  0 0


  0 0

   KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, (aliyekaa), akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (kushoto), alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye wa Maonyesho ya Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam Juni 22, 2015
   Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, (CAG), Profesa Mussa J. Assad, (kushoto), akipatiwa maelezo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (kulia), wakati alipotembelea banda la PPF kwenye Maonyesho yanayoendelea ya Wiki ya Utumishi wa Umma, kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Juni 22, 2015

  0 0

  BARAZA la Mchele nchini (RCT) kwa kushirikiana na taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na masuala ya kilimo (ANSAF), wameishauri serikali kutekeleza na kuendeleza sheria ya tozo ya ushuru wa forodha ya asilimia 75 kwa mchele unaotoka nje ya Shirikisho la Afrika Mashariki ili kuwaboreshea bei wakulima wa hapa nchini.


  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kwenye mkutano wa kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima wa mchele, Mkurugenzi Mtendaji wa Ansaf, Audax Rukonge, alisema kwa kufanya hivyo kutasaidia mkulima wa hapa nchini aweze kupata bei inayoendana na uhalisia wa zao hilo.


  Rukonge alisema mchele mwingi unaoingizwa hapa nchini umekuwa haulipiwi kodi, jambo linalosababisha madhara makubwa kwa mkulima, ikiwemo kushindwa kujiendeleza katika kilimo hicho na kuongeza kwamba kwa sasa mawaziri wa shirikisho hilo wapo mbioni kutaka kubadilisha ushuru huo uwe chini ya asilmia 75, jambo ambalo halikubaliki.


  Naye Mwenyekiti wa Baraza la Mchele Tanzania (RCT), Julius Wambura, alisema serikali inatakiwa kupanua wigo wa ukusanyaji wa takwimu za bei ya mchele ili kila mwananchi aweze kupata taarifa sahihi na kwa wakati.  Kama vile haitoshi, Wambura aliomba serikali kuwezesha bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko ianze kazi ili iweze kutekeleza majukumu yake pamoja na kuweka madaraja na viwango vya ubora vinavyotakiwa kwa walaji wa mchele wa ndani na masoko ya nje.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Ansaf, Audax Rukonge akizungumza na waandishi wa habairi jijini Dar es Salaam, kwenye mkutano wa kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima wa mchele,
  Mwenyekiti wa Baraza la Mchele Tanzania, Julius wambura akifungua semina  hiyo
  Mkurugenzi Mtendaji wa Ansaf, Audax Rukonge akizungumza na waandishi wa habairi jijini Dar es Salaam, kwenye mkutano wa kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima wa mchele.

  0 0

     Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifafanua jambo alipokuwa akihutubia umati wa watu waliofurika kumsikiliza  katika uwanja wa CCM Wilaya ya Sengerema ambapo aliwaambia wakazi hao Chama Cha Mapinduzi kitasimamia haki na misingi kwani ndio chama pekee kinachojali watu.

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wapo kwenye ziara ya Kukagua na kuimarisha uhai wa chama,Kukagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010,katika Mikoa ya Kagera,Geita na sasa mkoani Mwanza.
   Mbunge wa Jimbo la Sengerema Ndugu William Ngeleja akihutubia wakazi wa Sengerema mjini kwenye mkutano wa hadhara ambao Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alikuwa mgeni rasmi.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Sengerema mjini kwenye uwanja wa CCM wilaya ambapo aliwaambia moja ya sababu kubwa ya kuporomoka kwa vyama vya upinzani nchini ni kutotaka kubadili viongozi na kubaki na viongozi wale wale ambao tangia 1995 mpaka leo wameshindwa kuleta mabadiliko kwenye vyama vyao na kuendelea kushindwa kwenye chaguzi.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Nyamazugo kutoka kwa Mhandisi wa Maji mkoa wa Mwanza Ndugu Antony Sanga. Mradi huo mpaka kukamilika utakuwa na uwezo wa kutoa lita milioni 15 hivyo kuzidi mahitaji ya Sengerema ambayo ni lita milioni 8 kwa sasa,awamu ya kwanza ya mradi huo unategemewa kukamilika mwezi wa 8 mwaka huu na awamu nyingine inategemewa kukamilika mapema mwaka 2016.Pichani kushoto ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
   kivuko kipya cha SUMAR III kitakachokuwa kinatoa huduma kati ya Sengerema na Mwanza kupitia feri ya Kamanga.
    Mbunge wa Jimbo la Sengerema Ndugu William Ngeleja akizungumza jambo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana (pichani kati) wakati wa uzinduzi wa kivuko kipya cha SUMAR III kitakachokuwa kinatoa huduma kati ya Sengerema na Mwanza kupitia feri ya Kamanga. 
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa kivuko kipya cha SUMAR III kitakachokuwa kinatoa huduma kati ya Sengerema na Mwanza.  0 0

  Kitambi  ni  ile  hali  ya  tumbo  kuwa kubwa  na  kuchomoza  kwa  mbele  na  wakati mwingine  kufikia  hatua  ya  kunin’ginia.
  JINSI  KITAMBI  KINAVYO  PATIKANA
  Kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kitaalamu, mwili wa binadamu una seli kati  ya bilioni 50  hadi 200 za mafuta zilizogawanyika katika  sehemu  mbalimbali  za  mwili wa binadamu.
   Kwa wanawake  seli hizo  zipo sana katika maeneo ya matiti, kwenye  nyonga, kiunoni na kwenye makalio.

  Kwa upande  wa  wanaume seli  hizo zinapatikana  sana kwenye kifua, tumboni na kwenye makalio pia.
  Mafuta ya tumbo yanayofanya kitambi hukusanywa kwa njia kuu mbili:
  i.                    Njia  ya kwanza ni mafuta kutoka kwenye tishu zilizo chini ya ngozi
  ii.                  Na  njia  ya pili ni kutoka kwenye ogani za ndani kama moyo, kongosho n.k

  0 0

  Taasisi ya John Mashaka Foundation pamoja na American Engineering Group (AEG) hatimaye imeweza kuwasaidia wanakijiji 3,500 katika kijiji cha Manila wilayani Rorya kupata maji safi na Salama. Mradi huu umegharimu kiasi cha Shilling Billioni moja. Kabla ya huu mradi, wananchi wa hiki kijiji walikuwa wakitembea kilometa 24 kwenda ziwani na kurudi. Kazi ambayo ilikuwa ikifanywa na watoto pamoja na Wanawake.

  Huu ni mradi wa aina yake, kwani unatoa maji safi na salama. Na ina uwezo wa kusafisha kiasi cha lita 100,000 kwa siku ambayo inakuwa safi na salama kwa kiwancho cha 99.9%. Mitambo hii imeagizwa moja kwa moja kutoka Marekani, ambako ilibuniwa katika chuo kikuu cha Massachussets Institute of Technology, kwani haihudumiwa kwa namna yoyote ile ile. Inajitegemea na kujiendesha kwa kutumia nishati ya jua. Pampu ya maji ina uwezo wa kufanya kazi kwa miaka 20.
  Mafundi Wakichota maji kwenye kisima cha Zamani, ambayo ilikuwa ni ya Msimu.
  Mafundi Wakishauriana Jambo. Huu mtambo ni wa aina yake. Unatumia solar na inaweza kupandisha maji kiasi cha lita 20,000 kwa saa. Na inachuja maji kwa ubora wa 99.9% ambayo ni safi na salama.
  Mkuu wa mkoa wa Mara, Col. (Rtd) Aseri Msangi akiongea na wanakijiji kuhusu manufaa ya huu mradi wa maji kwenye maisha yao.
  Wakina Mama watakaosimamia mradi wa maji wakipiga picha ya Pamoja mbele ya Matenki ya Maji.

  0 0

   Katika kutambua na kudhamini juhudi za Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulahman  Kinana katika kukuiimarisha chama Mbunge wa Viti Maalumu  Mhe. Vicky Kamata amejitolea kutoa baiskel 500  kwa wanawake wa Umoja wa Wanawake wa mkoa mzima wa Geita ambapo  Wanawake hao watatumia baiskel hizo kukuiimarisha chama. Pichani Mhe Kamata akipongezwa kwa moyo wake huo
   Baiskeli alizotoa Mhe Vick Kamata mkoani Geita
   Mhe. Vicky Kamata akihutubia umati wa wananchi kwenye mkutano huo wa hadhara mkoani Geita
  Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulahman  Kinana  akifurahia jinsi Mbunge wa Viti Maalumu  Mhe. Vicky Kamata alivyojitolea kuwainua kinamama wenzake wa Geita

  0 0

  Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (katikati) akifafanua jambo wakati wa semina ya Daraja la Mafanikio iliyoandaliwa na American Chamber of Commerce (AMCHAM) kwa udhamini wa Vodacom Tanzania iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kupitia semina hiyo, mamia ya vijana kutoka sehemu mbalimbali (pichani) walipatiwa ujuzi wa jinsi ya kuandika CV, barua za maombi ya kazi pamoja na ujuzi utakaowasaidia kutafuta kazi katika makampuni makubwa na yale ya kimataifa. Kushoto ni Mkurugenzi wa Empower, Miranda Naiman na kulia ni Mkurugenzi wa Kazi Services, Zuhura Muro.
  Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (kushoto) akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya American Chamber of Commerce (AMCHAM) Bakhti Shah alipohudhuria semina ya Daraja la Mafanikio iliyoandaliwa AMCHAM kwa udhamini wa Vodacom Tanzania jijini Dar es Salaam leo. Kupitia semina hiyo, mamia ya vijana kutoka sehemu mbalimbali (pichani) walipatiwa ujuzi wa jinsi ya kuandika CV, barua za maombi ya kazi pamoja na ujuzi utakaowasaidia kutafuta kazi katika makampuni makubwa na yale ya kimataifa. Kulia ni Mkurugenzi wa Compass Communication Maria Sarungi Teshai.
  Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (wa pili kutoka kulia) akifuatilia semina ya Daraja la Mafanikio iliyoandaliwa na American Chamber of Commerce (AMCHAM) kwa udhamini wa Vodacom Tanzania iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kupitia semina hiyo, mamia ya vijana kutoka sehemu mbalimbali (pichani) walipatiwa ujuzi wa jinsi ya kuandika CV, barua za maombi ya kazi pamoja na ujuzi utakaowasaidia kutafuta kazi katika makampuni makubwa na yale ya kimataifa.

older | 1 | .... | 879 | 880 | (Page 881) | 882 | 883 | .... | 3278 | newer