Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live

MAHAKAMA YASHIRIKI KATIKA MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

$
0
0
 Baadhi ya wananchi waliotembelea katika banda la Mahakama ya Tanzania lililopo katika maonesho ya Utumishi wa umma yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakipata maelezo/ufafanuzi kutoka kwa Afisa wa Mahakama juu ya taratibu mbalimbali za kimahakama.

 Wananchi wakipata maelezo/ufafanuzi kutoka kwa Afisa wa Mahakama juu ya taratibu mbalimbali za kimahakama.
 1.   Mhe. Hussein Kattanga (aliyesimama ndani ya banda katikati), Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Mhe. John Kahyoza, Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania (wa kwanza kushoto, ndani ya banda) na Mhe. Warsha Ngh’umbu, Mkurugenzi Msaidizi wa Ukaguzi, Mahakama ya Tanzania (wa kwanza kulia) wakibadilishana mawazo na baadhi ya wananchi waliotembelea katika banda la Mahakama ya Tanzania lililopo katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Mnazi Mmoja. Mahakama ni moja ya Taasisi iliyoshiriki katika Maonesho hayo muhimu lengo likiwa ni kutoa elimu kwa wananchi na pia kutoa nafasi kwa wananchi kutoa malalamiko yako pamoja na maoni katika uboreshaji wa utoaji huduma za Mahakama.


1.   Mhe. Hussein Kattanga, Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Katiba na Sheria alipotembelea katika banda lao. Maonesho haya ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanatarajiwa kumalizika rasmi tarehe. 23.06.2015. Picha na Mahakama


MKOA WA MARA WAJITOKEZA KWA WINGI KUMDHAMINI WAZIRI BERNARD MEMBE

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (mwenye miwani) akilakiwa na umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mara, waliofika katika Ofisi ya CCM ya mkoa huo mjini Musoma Jana, kwa ajili ya kumdhamini iliaweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 1,800 mkoani humo
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akizungumza na umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mara, waliofika katika Ofisi ya CCM ya mkoa huo mjini Musoma Jana, kwa ajili ya kumdhamini iliaweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 1,800 mkoani humo
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akipongezwa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliofurika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Geita Juni 21.2015, kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akipongezwa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliofurika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Geita Juni 21.2015, kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho. Picha zaidi BOFYA HAPA

Introducing "ALBINO" by Wakubwa wa Jiji from Mwanza

YOGA DAY LIVE FROM THE UN HEADQUATERS IN NEW YORK

HII NDIO SABABU YA LOWASSA KUWANIA URAIS WA TANZANIA

Yaliyojiri katika ziara ya Rais Jakaya Kikwete nchini India kwa muhtasari

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AANZA ZIARA MKOANI MWANZA,AMALIZANA NA KAGERA NA GEITA

$
0
0
 
  Katibu Mkuu wa CCM ndugu Kinana (kulia) akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya  katika Kata ya Nyehunge Kijiji cha Isaka, Jimbo la Buchosa, wilayani Sengerema, Mwanza leo.
  Katibu Mkuu wa CCM ndugu Kinana  akitoka akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya  katika Kata ya Nyehunge Kijiji cha Isaka, Jimbo la Buchosa, wilayaniSengerema, Mwanza leo. 
  Kinana akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji  katika Kijiji cha Kalebezo, Kata ya Nyehunge, Jimbo la Buchosa.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama wa Kijiji cha Kalebezo, Kata ya Nyehunge, Buchosa baada ya kuzindua mradi wa maji.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara iliofanyika kwenye kijiji cha Nyehunge jimbo la Buchosa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza mmoja wa wakazi wa kijiji cha Nyehunge wilayani Sengerema katika jimbo la Buchosa,alipokuwa akiuliza swali .

Ndugu Kinana ambaye yupo katika ziara hiyo ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ameanza ziara mkoani Mwanza, baada ya kumaliza ziara katika mikoa ya Kagera na jana Mkoa wa Geita.

Akiwa mkoani Mwanza atafanya kazi ya kuimarisha uhai wa chama, kusimamia, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi  ya CCM, pamoja na kusilikiza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Nyehunge wilayani Sengerema katika jimbo la Buchosa,Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

UHALIFU MTANDAO KUELEKEA UCHAGUZI 2015

$
0
0

Nianze makala hii kwa kupongeza jitihada za dhati za serikali ya awamu ya Nne katika uwekezaji wake kwenye sekta ya TEHAMA Nchini. Ni wazi kabisa nchi yetu imepiga hatua kubwa katika maswala ya TEHAMA kulinganisha nan chi nyingi Afrika. Mifano michache ni pamoja na kuhama kutoka analogia kulekea Digitali, Mkonge wa taifa, Kupatikana kwa Khala Mtandao la taifa, kuaandikisha upigaji kura kimtandao na mengineyo mengi.


Aidha, Jitihada kama vile kupatikana kwa sharia mtandao, kupatikana kwa vitengo vinavyo shughulikia uhalifu mtandao,  wakala za serikali mtandao na mengineyo yamekua ni hatua ya kipekee iliyoweza kutoa matumaini kwa watanzania kutoka kwa serikali ya awamu hii ya Nne inayo ongozwa na Dk. Jakaya Kikwete.
Jitihada hizi njema naona bado kuna ya kufanyika zionyeshe matunda na zibaki salama kwa muda mrefu. Nimeyasema hayo kufuatia kauli yangu niliyoitoa, Nilipo sema serikali ina jukumu la kuwekeza zaidi katika maswala ya usalama mitandao ili kuweza kubakisha salama jiihada hizi za TEHAMA kwani isipo fanywa hivyo kuna hatari kubwa mbele yetu kimtandao iyakayo pelekea jitihada hizi kuingia dosari kubwa.

Hatari za kimtandao zitakazo pelekea kuathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wetu, siasa zetu, tamaduni na jamii yetu kwa kwa ujumla wake. Napo zungumzia uchumi nipamoja na upotevu mkubwa wa fedha unaosababishwa na uhalifu mtandao ulio athiri taasisi za fedha na mawasiliano nchini. Kumekua na wimbi kubwa la wizi wa fedha kimtandao hii ni mjumuisho wa pesa kutoka mabenki pamoja na pesa zinazo potea kutokea kwenye miamala ya simu. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

LOWASSA AZIDI KUPATA MAPOKEZI MAKUBWA KILA ANAKOKWENDA, SONGEA ALAZIMIKA KUKAA JUU YA PAA LA NYUMBA

$
0
0
WAZIRI Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa amesema hana shaka na swala la kukatwa jina lake katika vikao vya Chama cha Mapinduzi(CCM), kwani anaamini Chama chao kitatenda haki kwa kurudisha jina lake kuwa mgombea urais wa Tanzania.

Lowassa ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wa Mkoa wa Ruvuma katika ofisi kuu za CCM Mkoani humo, wakati akitoa shukrani baada ya kudhaminini na wanaCCM zaidi ya elfu 52.

"Nimekuwa mwanaCCM tangu mwaka 1977 nilipomaliza chuo kikuu, sijawahi kufanya kazi nje ya CCM hivyo nakijua chama na hakuna mgombea atakayeweza kuvunja rekodi ya utendaji wangu katika chama, sasa leo anayetaka kukata jina langu anatoka wapi? anakata kwa sababu gani? Sioni kosa la kukatwa jina na Watanzania hawaoni, kwa hiyo msiwe na wasiwasi jina litarudi tu". alisema Lowassa.

 Lowassa aliwasili Mkoani Ruvuma mapema mchana wa leo akitokea Mkoani Iringa kwaajili ya kusaka wadhamini katika mbio zake za kusaka urais kwa tiketi ya chama hicho, ambapo umati wa watu ulifurika kumlaki na kupelekea kufunga barabara kuu ya mjini, hali iliyompelekea Lowassa kupanda juu ya kibambaza cha jengo la ofisi ya CCM Mkoa ili aweze kuzungumza hao.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, akizungumza na Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma waliokuwa wamesimama nje ya Ofisi za CCM Mkoa huo, mjini Songea leo Juni 21, 2015, wakati alipofika kwa ajili ya kupata udhamini utakaomuwezesha kupata ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Chifu wa Kabila ya Wangoni, Chifu Ally Yussuf Songea (97). Chifu huyo alikwendwa kwenye uwanja wa Ndege wa Songea kumpokea Mh. Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono wanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.

MEMBE AHUDHURIA MSIBA WA MTOTO WA JENERALI MSUGURI NA KUHANI MSIBA WA JOHN NYERERE BUTIAMA MKOANI MARA

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia) akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya Serikali wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa Luteni mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Marehemu Martin David Msuguri wakati wa ibada ya kumuaga na mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Baba yake, Jenerali mstaafu David Msuguri, Butihama mkoani Mara Juni 21.2015. Marehemu Martin alifariki Juni 19 mwaka huu katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam baada ya kuugua.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia) na Mama Maria Nyerere wakiwa katika shughuli ya kuaga mwili wa Luteni mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Marehemu Martin David Msuguri wakati wa ibada ya kumuaga na mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Baba yake, Jenerali mstaafu David Msuguri (wa tatu kulia), Butihama mkoani Mara Juni 21.2015. Marehemu Martin alifariki Juni 19 mwaka huu katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam baada ya kuugua.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akijadiliana jambo na Mama Maria Nyerere baada ya  shughuli ya kuaga mwili wa Luteni mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Marehemu Martin David Msuguri, katika ibada ya kumuaga na mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Baba yake, Jenerali mstaafu David Msuguri, Butihama mkoani Mara Juni 21.2015. Marehemu Martin alifariki Juni 19 mwaka huu katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam baada ya kuugua. Kulia ni Mbunge wa Mchinga (CCM), Saidi Mtanda.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiweka shada la maua kwenye kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati alipokwenda nyumbani hapo kuhani msiba wa mtoto wa Baba wa taifa, Marehemu John Guido Nyerere, wilayani Butihama mkoani Mara Juni 21.2015. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiweka shada la maua kwenye kaburi la mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Bw. John Guido Nyerere aliyefariki Mei 9 mwaka huu, wakati alipokwenda kuhani msiba, wilayani Butihama mkoani Mara Juni 21.2015.
Picha na John Badi

maalim seif afariji wagonjwa na wafiwa katika Mkoa wa Kusini Unguja.

$
0
0
Na Hassan Hamad, OMKR. 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amefanya ziara ya kuwatembelea na kuwafariji wagonjwa na wafiwa katika Mkoa wa Kusini Unguja. 
Katika ziara hiyo Maalim Seif amewaombea wagonjwa hao kuweza kupona haraka, ili waweze kuungana na wananchi wengine katika shughuli za kimaisha, sambamba na kuwataka wale waliofiwa kuwa na subra katika kipindi hiki kigumu cha msiba. 
Miongoni mwa vijiji alivyotembelea katika mkoa huo ni pamoja na Muyuni, Kizimkazi, Kajengwa, Uroa, Binguni na Kiboje. Hii ni ziara yake ya kwanza ya kutembelea wagonjwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhan, katika utaratibu wake wa kutembelea wagonjwa na wafiwa kila ifikapo mwezi wa Ramadhan, ziara ambazo huzifanya katika Wilaya zote za Unguja na Pemba.
 Wakati huo huo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amejumuika na wananchi mbali mbali katika futari ya pamoja nyumbani kwake Mbweni, aliyoiandaa kwa ajili ya watendaji wa vyama vya siasa. 
Amewashukuru wananchi hao kwa kuamua kushirikiana nae katika futari hiyo, jambo ambalo amesema linaonesha mapenzi na mshikamano miongoni kwa waislamu. 
Maalim Seif ametoa wito kwa waislamu nchini kuendeleza utamaduni wa kualikana na kufutari kwa pamoja, kitendo ambacho hukuza na kuendeleza umoja na maelewano kwa wananchi.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akitoka katika moja ya nyumba wakati  akiwa katika ziara ya kutembelea wagonjwa na wafiwa katika Mkoa wa Kusini Unguja.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akishiriki katika dua katika ziara ya kutembelea wagonjwa na wafiwa katika Mkoa wa Kusini Unguja.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na mmoja wa wagonkwa wakati akiwa katika ziara ya kutembelea wagonjwa na wafiwa katika Mkoa wa Kusini Unguja.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika ziara ya kutembelea wagonjwa na wafiwa katika Mkoa wa Kusini Unguja.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na wananchi akiwa katika ziara ya kutembelea wagonjwa na wafiwa katika Mkoa wa Kusini Unguja. Picha na Salmin Said, OMKR

UTT AMIS ILIVYOSHIRIKI MAONYESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2015

$
0
0
Ofisa Mafunzo Idara ya Masoko UTT AMIS, Waziri Ramadhani (kulia) akitoa maelezo ya namna ya kujiunga na Mfuko wa Umoja wakati wa maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Ofisa Mafunzo Idara ya Masoko UTT AMIS, Waziri Ramadhani (kulia) akitoa maelezo ya namna ya kujiunga na Mfuko wa Umoja wakati wa maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa wa Mafunzo wa UTT AMIS, Doris Malenge.
Mmoja wa Wateja waliotembelea banda la UTT AMIS akijaza fomu kwa ajili ya Mfuko wa Watoto kwenye maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Msaidizi wa Huduma kwa Wateja, Saidi Mkomwa.
Maofisa wa UTT AMIS wakiwa katika picha ya pamoja. Wa pili kulia ni Ofisa Masoko Mwandamizi, Martha Mashiku, kulia ni  Ofisa Msaidizi wa Huduma kwa Wateja, Saidi Mkomwa, Ofisa Uendeshaji UTT AMIS, Justine Joseph (kushoto) na Ofisa Mafunzo, Doris Mlenge (wa pili kushoto) na Ofisa Mafunzo Idara ya Masoko, Waziri Ramadhani (katikati).
------------------------
Kampuni ya Uwekezaji ya UTT Asset Management and Inventor Services Plc (UTT AMIS) ni mrithi wa taasisi ambayo hapo awali ilijulikana  kama Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT), ambayoiliundwa  Juni 19, 2003.
UTT AMIS ni taasisi ya serikali chini ya Wizara ya Fedha ambayo kuanzia mwezi Julai 2013 imechukua na kusimamia kazi zote za iliyokuwa UTT.
Dhumuni kuu ni kuazisha na kuendesha mifuko ya uwekezaji wa pamoja ili kuwawezesha wananchi kujiwekea akiba huku wakiwekeza katika Masoko ya Mitaji na Fedha. 
Hadi sasa UTT AMIS inaendesha mifuko mitano, ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi.

MBUNGE WA KIGAMBONI DK.FAUSTINE NDUGULILE AZINDUA MASHINDANO YA DIWANI CUP KATA YA KISARAWE TWO MANISPAA YA TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mbunge wa Kigamboni, Dk.Faustine Ndugulile (wa pili kulia), akizungumza na wachezaji wa timu za Dubu na Tumaini (hawapo pichani), wakati akifungua mashindano ya  kombe la umoja na mshikamano maarufu kama Diwani Cup yaliyoanza uwanja wa Kibamande eneo la Mwasonga Manispaa ya Temeke Dar es Salaam jana. Kulia ni mlezi wa mashindano hayo,  Diwani wa Kata ya Kisarawe II,  Issa Zahoro.
Mlezi wa mashindano hayo Diwani wa Kata ya Kisarawe II,  Issa Zahoro, akikagua timu ya Dubu kutoka eneo la Mwasonga.
 Mlezi wa mashindano hayo Diwani wa Kata ya Kisarawe II,  Issa Zahoro, akikagua timu ya Tumaini kutoka katika kata hiyo.
Mbunge wa Kigamboni, Dk.Faustine Ndugulile
Mbunge wa Kigamboni, Dk.Faustine Ndugulile, akiwasalimia mashabiki wakati akiwasili kufungua mashindano hao. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

WAISLAM WAJUMUIKA NA WATANZANIA WENZAO KATIKA FUTARI YA PAMOJA STOCKHOLM, SWEDEN

$
0
0
 Shekhe akitowa mawaidha katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Jumuiya ya Waislamu jijini Stockholm, Sweden, leo 
 Sehemu ya waumini wakiwa katika hafla hiyo jijini Stockholm
 Mgeni rasmi katika hafla ya futari hiyo, Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe Dorah Msechu (wa pili kulia) akiwa na sehemu ya waumini waliohudhuria
Mgeni rasmi katika hafla ya futari hiyo, Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe Dorah Msechu, akitoa salamu na shukurani kwa Jumuiya ya Waislamu nchini humo kuandaa futari y pamoja na kudumisha undugu na umoja wa Watanzania katika Diaspora
Baadhi ya wanajumuiya wakifuturu. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MATOKEO YA KUFUTIWA HATI YA ARDHI.

$
0
0
Na Bashir Yakub
Makala  zilizopita  nilieleza   mazingira ya  kisheria  ambapo  mtu  anaweza   kunyanganywa  ardhi  yake  na  kufutiwa  hati  miliki  na  hatimye  ardhi  kupewa  mtu  mwingine  au  kukabidhiwa  mikononi  mwa  serikali. Nilieleza  mambo  mengi  ikiwemo   sababu  ambazo  zinaweza  kupelekea mamlaka  za  ardhi  kufuta  hati  miliki  ya mtu.  
Pia  nilionya  kuwa unapomiliki  ardhi  sio  kwamba  umemaliza,  hapana,  isipokuwa  kuna umuhimu  mkubwa wa  kuzingatia  na  kufuata masharti  yaliyo  katika  hati  miliki. Hii  ni  kwasababu  Sheria ya  Ardhi  imeweka  bayana  na  kutoa  mamlaka  kwa  ofisi  kuu  za ardhi  kufuta  umiliki  wa mtu  iwapo  unakiuka  masharti  ya  hati.


Pia  nikaeleza  kuwa  yawezekana  maafisa  ardhi  kutumia  mwanya huo   kuchukua  ardhi  yako  kwa  manufaa fulani  au  kwakuwa  yupo  mtu nyuma  ya  mchezo  huo  ambaye   anaitaka  ardhi  yako. 
Utatumika  mwanya  wa  kutotekeleza  masharti  kukunyanganya  ardhi ili  apewe  huyo  aliyesimamia  mchezo  huo. Na  mwisho  nikasema  kuwa  huwezi  kujua  kama  haya  yapo  mpaka  yakutokee  vinginevyo  unaweza  kudhani   tunaongea  vitu  ambavyo  havijawahi  kutokea. Waliofikwa  na  haya  wanajua  nazungumza  nini. 

Mkurabita yaendelea na Urasimishaji biashara na Rasilimali za Wanyonge katika mikoa ya Mbeya, iringa na morogoro

$
0
0
 Mkurugenzi wa Liganga Blacksmith Group,akizungumza na wanahabari na kuwaonyesha bidhaa zinazotengenezwana kampuni hiyo walipoanzia na sasa walipo baada ya kupata mafunzo na kuwa wakopaji wazuri kwenye taasisi za fedha za mkoa huo.
 Kemy Kiula, Mwenyekiti wa Kikundi cha wanaushirika cha trust deed of the regegistered of Tanzania, akipanga biashara na mwanaushirika mwenzake biashara zao zimerasimishwa na wameanza kujipatia mikopo. 
 wananchi wa morogoro eneo la kihondana viongozi wa manispaa ya morogoro wakiwa katika mikutano ya kuzungumzia elimu inayotolewa na uwasilishaji wa maombi ya mikopo katika mabenki baada ya kupimiwa mameneo yao na biashara zao.
Mzee Raphael Bundala, akiwaomba mkurabita washirikiane na mabenki kuunda chombo cha kuwa na akaunti yao ili mikopo wanapohitaji pasiwepo na usumbufu kama ilivyozoeleka kwa masikini hakopesheki.


Chef Issa aanzisha whatsapp group la Ma-Chef wa Kitanzania popote walipo duniani

$
0
0
Chef Issa ameanzisha group la Whatsapp kwa ajili ya Tanzanian chef's popote duniani ambalo anasema kama wewe ni Chef unaweza jiunga kwa kutuma request mobile No. +46709297384 
Lengo likiwa ni kukutana,  kufahamiana,  na kusaidiana kitaaluma. Ma-Chef wote wa Kitanzania mnakaribishwa.

MWENGE KUZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA SH. MILIONI 1.2 MUFINDI

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - RELEASE NO. 15
JUMLA ya miradi 13 yenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni 1.2 inatarajiwa kuzinduliwa pamoja na kuwekwa mawe ya msingi na Mwenge wa uhuru utakapokimbizwa katika Halmashauri ya wilaya ya Mufindi mapema alhamisi ya tarehe 25 mwezi huu.
Taarifa ya Ofisi ya habari na mawasiliano ya halmashauri ya Mufindi kwa vyombo vya habari imefafanua kuwa, vyanzo vya fedha zilizotumika kukamilisha miradi hiyo  vimegawanyika katika sehemu kuu nne, ambapo asilimia 10 ya fedha hizo ni kutoka serikali kuu, asilimia 12 ni Fedha za Halmashauri, wakati asilimia 13 ni  fedha za wahisani huku wananchi wakichangia  asilimia 65.
 Taarifa hiyo imeendelea kubainisha kuwa miradi hiyo 13 imegawanyika katika vijiji vya Mtili, Lugolofu, Mabaoni, Idetelo, Lugongo na kata ya Kinyanambo huku miradi mikubwa Zaidi ni pamoja na mradi wa sakosi ya Faraja wenye gharama ya Zaidi ya sh milioni 478 utakaozinduliwa katika kata ya Kinyanambo sanjari na mradi wa msitu ulioghalim Zaidi ya Sh. Milioni 180 utakao kaguliwa katika kijiji cha Lugongo.
Aidha, Mwenge wa uhuru utakabidhiwa kwa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi, katika hafla itakayo fanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari Kinyanambo majira ya saa mbili asubuhi, ukitokea Manispaa ya Iringa na badaye jioni utakesha katika kijiji cha Mabaoni Mgololo kata ya Makungu. 
Mwenge wa uhuru uliasisiwa rasmi mnamo mwaka 1960 na hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, ukiwa na shabaha ya kuleta matumaini, upendo, heshima na kuchochea maendele katika jamii za kitanzania.

MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE AKISHIRIKI KAMPENI YA MAZINGIRA KATIKA SOKO LA MASAMA-MULA

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai (Mwenye kofia katikati) akishirikiana na wananchi wa Lukeni, Kata ya Masama-Mashariki kufanya usafi katika Soko la Masama-Mula mwishoni mwa juma, katika kampeni ya kutunza mazingira kwenye jimbo hilo iliyopewa jina la 'Keep Hai Clean' ikitumia gari maalum la kukusanyia taka lenye uwezo wa kubeba tani 32 za taka ambalo Mbunge huyo alitoa msaada kwa wananchi wake hivi karibuni.

Asili na historia ya neno la picha ya mnato ya "SELFIE"

$
0
0

Na Sultani Kipingo 
wa Globu ya Jamii
Karibu kila mtu duniani leo hii analijua neno “Selfie” ambalo maana yake ni picha ya mnato ya kujipiga mwenyewe kwa kujielekeza Camera, lakini ni wachache wanaojua kwamba neno hilo lilianza kuvuma muda wa mwaka juzi tu, pale watunzi wa kamusi za Oxford walipoliweka kwenye kamusi zao na kulitaja kuwa ndilo neno la mwaka 2013 na kulipa maana hiyo ya kujipiga picha mwenyewe na kutundikwa kwenye mitando ya kijamii.

Ingawa matumizi ya neno “Selfie” linaonekana ni la kileo, lakini tendo la mtu kujipiga picha mwenyewe si  geni kabisa kwani tangia miaka ya awali ya sayansi ya picha za mnato aghalabu watafiti na waendelezaji wa sayansi hii walizoea kujipiga picha wenyewe katika kufanikisha tafiti zao. 
Hapo elewa kwamba sayansi hii ilianza tokea miaka ya 1800 mwanzoni na katikati ya miaka hiyo na kuendelea

Hiyo hapo juu ndiyo “Selfie” inayoaminika kuwa ni ya kwanza kabisa kupigwa duniani na kuwepo katika kumbukumbu iliyopigwa mwaka 1839 na mkemia na mtafiti wa picha za mnato aitwaye Robert Cornelius wa jiji la Philadelphia nchini Marekani (BOFYA HAPA) .

 Akitumia mbinu zilizotumia wakati huo, huyu bwana alijipiga picha hii kwa kufunua lensi (zamani hakukuwa na kitufe cha kubofyea, ilikuwa unafunua lensi kwa muda maalumu na kisha kuiziba) na akaenda mbele ya Camera ambako alikaa kwa muda unaotakiwa lensi kuwa wazi, kisha akarudi na kuiziba. Nyuma ya hii picha akaandika  “The first light Picture ever taken. 1839.” Yaani “Picha ya mwanga ya kwanza kabisa kuchukuliwa. 1839”


Globu ya jamii imefanya utafiti huu wa kubaini picha moja ya mnato ya watu wanne wanaojipiga "Selfie" mwaka 1920  (kulia) inayozunguka kwenye mitandao ya kijamii   na kudaiwa kuwa ndiyo “Selfie”  ya  awali kabisa (BOFYA HAPA). Hivyo ukweli ndio huo hapo juu.


Viewing all 110089 articles
Browse latest View live




Latest Images