Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 86 | 87 | (Page 88) | 89 | 90 | .... | 3285 | newer

  0 0

  .....MPAMBANO TMK Halisi Vs TMK Family.......
  Sir Kassim Juma Nature, kinara wa kundi la TMK Wanaume Halisi akiwanyooshea Mike mashabiki wake usiku wa kuamkia leo katika mchuano wa NANI MFALME ambapo mashabiki walimkubali kuwa Mfalme wao dhidi ya mahasimu wao, TMK Wanaume Family.
  Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa mashabiki wa TMK Halisi, wakati wote vidole juu...TATU BILA, hata walipopagawishwa na nyimbo kali za TMK Family.
  Mhe. Temba akicheza na mashabiki katika mpambano huo wa kukata na shoka
  JB wa TMK Halisi akicheza na mashabiki wake pia
  Sir Nature (kulia) na Doro..kazini
  Mhe. Temba na Chege,,,kazini
  ..Inspector Haroun akiwa jukwaani akiwakilisha Gangwe Mob kivyake
  ..Inspector anapoamua kuvua viatu na kupiga shoo peku...
  ..Chezea Dar Live wewe!
  Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa akionesha manjonjo yake mbele ya mpiga gitaa wake!
  ...dogo Lila kutoka kundi la Nature, akiwa ni member mpya wa kundi, akichana mistari vibaya mno....
  ...dogo Aslay wa TMK Family akiwaimbisha mashabiki
  ...Profesa jay nae alikuwepo kuwakilisha vilivyo game ya Hip Hop
  DJ Jd alikuwepo kwenye mashine kucheza nyimbo za Prof jay na pia kuwaonesha Ma DJ chipukizi jinsi ngoma inavyochezwa!
  ........shooo wa Wanaume Family ikipamba moto
  DJ JD alikuwa kama jaji pia, hapa akimtangaza Nature ndiye Mfalame kama mashabiki walivyoitikia.
  ...Nature akipungia mkono mara baada ya kutangazwa mfalme.
  PICHA: Richard Bukos na Issa Mnally - GPL

  0 0

   Na Abdulaziz video,Lindi
  Baraza kuu la Waislam Mkoa wa Lindi limetoa msaada wa Vifaa vya Ujenzi kwa ajili ya kuunga jitihada za waislamu wa Kata ya Nachingwea na Jamhuri,Manispaa ya Lindi baada ya kujitolea kuchangia ujenzi huo ili
  kuimarisha elimu ya Dini.
   Vifaa hivyo ikiwemo Bati,saruji,rangi na gjharama za ufundi vyenye thamani ya Tshs Milioni 2 laki tatu(2,300,000/) vimekabidhiwa na Katibu wa Bakwata mkoa,Alhaj Abdillah Salum kwa maalim wa Madrasa hiyo ya Al Rijala Musalam,Ustadh Abdulwahab Manzi.
   Akikabidhi Vifaa hivyo,Alhaj Abdillah aliwataka waislamu mkoani humo kujitoa na kuchangia ukuaji wa elimu ya Dini ya Kiislam kwa vijana na watoto ili wakue katika maadili yaliyo mema.
  '' Waislam tujitoe kushangia elimu hii kwa muskabali wa maisha yajayo mambo mengi yanatokea kutokana na jamii nyingi kutofuata maadili na mafundisho ya dini ni lazima tuamke na tushikamane katika ibada kuombea Nchi yetu Amani''alisema Alhaj.
   Sambamba na msaada huo pia aliiomba serikali kurudisha na kutenga katika mipango yake ya elimu kwa kutoa fursa kwa elimu ya dini kufundishwa mashuleni kutokana na muda mchache anaopata mtoto katika kupata elimu ya Dini kwa siku za jumamosi na jumapili.
   Akipokea msaada huo Ustadh Abdulwahab Manzi aliishukuru Baraza hilo baada ya kuona juhudi za waislam kuchangia ujenzi huo ambapo alibainisha kuwa msaada huo utakamilisha kazi ya Ujenzi huo huku
  akitoa wito kwa waislamu wengine nchini ambao wamejaliwa kupata uwezo kuimarisha elimu ya Dini ikiwa pamoja na kujitolea kuchangia madrasa pamoja na Misikiti ili Waumini wapate fursa ya kusoma na kuabudu
   Katibu wa Baraza kuu la waislamu mkoa wa Lindi,Alhaj Abdillah Salum akikabidhi msaada wa kumalizia ujenzi  wa Madrasat Al Rijala Musalam kwa Maalim wa chuo Hicho,Ustaadh Abdulwahab Manzi 
  katika eneo la ujenzi Manispaa ya Lindi

  Madrasat Al Rijal ikiwa katika hatua za ujenzi na kazi itakamilika baada ya kutolewa msaada na Baraza kuu la waislam mkoa wa Lindi 
  0 0


  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la Mto Rufiji (RUBADA) Bw. Aloyce Masanja akiwaonyesha wadau kutoka katika taasisi na Idara mbalimbali za serikali ripoti ya awali iliyotayarishwa na Kampuni ya Odebretch International ya Brazili ikiwa ni hatua ya awali ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa uzalishaji umeme wa maji wa Stierglers Gorge, ripoti hiyo imewasilishwa kwa wadau hao ili kuijadili na kuangalia kama moja ya hatua za utekelezaji mradi huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la Mto Rufiji (RUBADA) Bw. Aloyce Masanja akiwaonyesha wadau kutoka katika taasisi na Idara mbalimbali za serikali ripoti ya awali iliyotayarishwa na Kampuni ya Odebretch International ya Brazili ikiwa ni hatua ya awali ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa uzalishaji umeme wa maji wa Stierglers Gorge, ripoti hiyo imewasilishwa kwa wadau hao ili kuijadili na kuangalia kama moja ya hatua za utekelezaji mradi huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka hiyo, Profesa Raphael Mwalyosi.

  0 0

  Watoto wakibembea katika bembea mpya iliyozinduliwa Pasaka katika uwanja wa Dar Live jana
  ...wakiwa tayari 'ku take off'
  ..kama kawaida, licha ya mvua kunyesha mara kwa mara, watoto waliogelea kwenye pool yao.
  ...wengine waliforahia michezo ya baskeli
  ...wengine walipanda ndege ya Dar Live
  ..mandhari ya Dar Live mchana
  ....Merry Go Round!
  Dar Live at Night!
  PICHA: Abdul Mohamed/GPL

  0 0

   Hali inavyojionyesha sasa ni kuwa filamu za kiswahili miaka michache ijayo zitakuja kuteka soko katika nchi nyingi duniani kuliko ilivyo sasa hivyo hakuna haja yoyote ya kutumia kiingereza katika filamu zetu sisi kama waafrika tunaopaswa kuendeleza na kukuza mila na tamaduni zetu ikiwemo lugha ya kiswahili ambayo ni lugha inayozungumzwa na mataifa mbalimbali. 

  Watengenezaji wa filamu nchini Denmark ni kama wanatupa ishara kuwa filamu za kiswahili ni lulu huko ulaya hivyo tufanye juu chini kuongeza ubora katika filamu zetu ili kuteka soko la dunia. 

  Tantine ambaye jina lake halisi ni Tatu Daniel Musa ni actress anayekubalika nchini Denmark akiwa tayari amecheza filamu chache tu huku filamu yake ya JABUKA ikiwa imemfanya akubalike vizuri kwa mashabiki. Filamu hiyo imetumia lugha ya kiswahili hivyo kuonyesha kuwa kiswahili kinatuunganisha watu wengi Afrika, ulaya na marekani.

  Tantine muigizaji aliyejaaliwa mvuto wa aina yake ana asili ya Tanzania na Congo. SWP ilipomuuliza anavutiwa na kazi za actors gani katika nchi za africa mashariki alijibu kuwa anapenda kazi za Irene Uwoya and Wema Sepetu.


   Actress huyu anayezungumza kiswahili, kidanish na kiingereza anasema kuwa filamu za kiswahili zinapendwa katika nchi za scandnavia lakini tatizo ni kuwa hazifiki huko hivyo wadau kukosa filamu hizo pengine ikiwa sababu kubwa kwa wao kuanza kutengeneza filamu kwa kiswahili ili kuwapa wadau kitu wanachotaka.


   "Kwakweli filamu za kiswahili zina pendwa sana apa Scandinavia Kuna wadau wengi wanatamani movie za kiswahili ila wanakosa sehemu za kuzinunulia ili wazione".

  Hilo linatokea hasa kutokana na nchi nyngi za scandinavia kuwa na ushirikiano wa karibu na nchi za africa mashariki na pia mara nyingi wanamuziki wa Tanzania wakialikwa kufanya show katika nchi hizo. Hata hivyo subtile ya kiingereza bado ni muhimu ili kuzidi kuwavutia wasiojua kiswahili ili kukuza soko zaidi. 

  Hili linatakiwa kuchukuliwa seriously kwa wasambazaji na watengenezaji wa filamu za kiswahili katika kusambaza filamu katika nchi ambazo kazi zao zinakubalika hii ndivyo inavyofanyika hata Hollywood na Bollywood kutoa kipaumbele na kufanya utafiti wa soko katika nchi wanazohisi kazi zao zinakubalika. 

  Serikali yetu nayo kupitia kwa rais Kikwete isikie kilio hiki cha wasanii wa filamu maana kama serikali ikiwa serious itakusanya mapato mengi sana kupitia filamu na wasanii kuwa na kipato kizuri zaidi kuliko ilivyo sasa. Pichani ni muigizaji Tantine anayeishi Denmark

  0 0


  Rais Mstaafu Mzee Benjamin William Mkapa alipotembelea majengo ya Ofisi za Halmashauri na za Serikali zilizochomwa moto wakati wa vurugu za wahuni zilizotokea Masasi hivi karibuni.


  0 0

  Michuzi, Wakumbushe wabongo historia ya Kazeh (Nowadays Tabora). Picha ya kwanza ni Nyamwezi people 1914, picha ilipigwa na wajerumani. Je hapo kuna mtu alikuwa na Cholesterol au Blood Pressure? Picha ya pili ni Tabora 1906.
  Mdau Ujerumani


  0 0
 • 04/01/13--13:01: mambo ya gado leo

 • President Uhuru Kenyatta, EU, US, the West and China


  0 0
 • 04/01/13--13:10: Article 21


 • 0 0
 • 04/01/13--13:24: nyama choma orijino
 •  Mjomba Ankal!
  Nikiwa safari kirudi Bombii hii, nyumbii hii (Songea) baada ya kutoka Stendi ya Msamvu mjini Morogoro kama kilometa 30 hivi mara Basi la letu la Super Feo likasimama, nikakutana na mambo yetu ya nyama choma ya wamasai wa Moro. Mshikaki mmoja buku tatu, yaani lainiiiiii!!!!!!!!
  Mdau Gerson Msigwa  0 0

  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akisalimiana na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akisalimiana na Mama Rachel Chebet, mke wa Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akiongea na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akimuongoza kuelekea kwenye chakula cha mchana Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto na mkewe Rachel Chebet katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akipozi na familia ya Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka. PICHA NA IKULU

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete April 1, 2013 amekutana na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto ambaye alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.

  Akiongea na mgeni huyo katika hoteli ya Seronera iliyoko katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara, Rais Kikwete amempongeza Mhe Ruto na Rais mteule wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta, kwa ushindi wao kwenye uchaguzi mkuu nchini Kenya.

  Mhe Rais pia alimueleza Mhe Rutto furaha yake pamoja na kuridhishwa na jinsi uchaguzi ulivyofanyika kwa amani katika nchi hiyo.

  Alielelezea matumaini yake ya kuwa urafiki uliopo kati ya Tanzania na Kenya utadumishwa pamoja na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Mhe Rutto, ambaye aliwasili mkoani Mara wiki iliyopita akiwa na mke wake na watoto, ameondoka leo baada ya chakula cha mchana alichoandaliwa na mwenyeji wake.

  0 0


  Mwili wa dereva wa lori moja kubwa lenye ujazo wa tani 18 ukiwa umeopolewa na askari jeshi, tayari kupelekwa mochwari ya Hospitali ya Mt Meru. Dereva huyu ametambulika kwa jina moja tu la Alex amefikwa na mauti akiwa ndani ya gari hilo wakati vijana wengine wakiendelea kupakia moram asubuhi ya leo
  Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema akiwasili eneo la ajali mapema asubuhi.
  Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia ajali hiyo mbaya wakishangaa zoezi la uokoaji na wengine wakisubiri kutambua ndugu zao, jambo ambalo halikupata nafasi.
  Mwananchi huyu aliishiwa nguvu baada ya kushuhudia mwili wa rafiki yake ukiopolewa kutoka kwenye kifusi
  Hali ilivyo machimboni hapo
  Kina mama wakilia kwa uchungu wakihofu kuondokewa na wapendwa wao
  Vikosi vya Jeshi la Wananchi na Polisi vikiwa kazini
  Sehemu ndogo ya Fuso ikionekana huku gari nyingine ikiwa haionekani kabisa.


  Inakadiliwa watu zaidi ya watu 18 wamepoteza maisha kufuatia kufukiwa na gema la mchanga/moram wakati wakichimba na kupakia kwenye malori eneo la Moshono jijini Arusha.  Ajali hiyo mbaya imetokea katika machimbo ya moram nje kidogo ya jiji eneo jirani na Moshono-Kiserian ambapo vijana hao wanaokadiriwa kufikia idadi hiyo walikuwa wakipakia moram kwenye magari mawili, moja ni Fuso na lingine kubwa zaidi (tani 18) na yote mawili yamefukiwa kabisa na kifusi.  Shuhuda mmoja wa ajali ambae pia ni mchimbaji ameieleza Blog hii kwamba kwa kawaida gari ndogo kama Fuso hupakiwa na watu 7, na hiyo kubwa huwa na watu 12 bila kuhesabu dereva na utingo.  Miongoni wa waliofikwa na mauti ni pamoja na madereva wa magari hayo. Katika eneo la ajali hali ni ya simanzi na vilio toka kwa kina mama huku baadhi wa wababa na marafiki na ndugu wa jamaa waliofukiwa wakishindwa kujizuia na kuangua kilio.  Meya wa Manispaa Mh Gaudence Lyimo pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema ni miongoni mwa viongozi wakubwa waliofika eneo la ajali kusaidiana na kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania kufanya uokozi.  Wachina wakipeleka moja ya mashine zao (Excavator) kuongeza nguvu katika kusaidia kufukua miili ya watu hao iliyonaswa na kifusi hicho. 
  HABARI KWA HISANI: ARUSHA255 BLOG

  0 0
 • 04/01/13--20:00: Ngoma azipendazo Ankal

 • Zaita Muzica na Freddy Supreme Ndala Kasheba na wenzake walichangamsha sana enzi hizo na ngoma yao ya 'Umbea'

  0 0
 • 04/01/13--20:04: msaada tutani....
 • Salaam Ankal,

  Natafuta mwanamume wa kitanzania mwenye umri usio chini ya miaka 55 mpaka 65 aishiye Eropeanzone hususani Holland( Netherland,Belgium, Germany,and scaninaviacountries like Sweden ,Norway and Denmark , mimi ni mtanzania ninaiyeishi zaidi ya miaka 30 Ulaya hususani Ujerumani, Natafuta mwanamume Mtz awezaje kuongea Kiswahili,kiingereza lakini sio lazima!!!

  Nina binti wawili, wameolewa na nina wajukuu watatu, naishi kwa kujitegemea, nina umri wa miaka 57, naishi Hamburg na Berlin kikazi lakini makao yangu kimaisha ni Berlin

  Naaomba majibu kwa Email: nganashe@gmail.com yaambatanishwe na picha na email adress, bila picha hakuna majibu!!!!!!

  Asante Michu kwa kazi yako na Kazi njema

  0 0


  SERIKALI     kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema haitabidili kamwe  maamuzi iliyotoa kuhusu Pori Tengefu la Loliondo, mkoani Arusha na kuwataka wanaharakati wanaochochea mgogoro wa ardhi katika eneo
  hilo kuacha mara moja.

  Tamko hilo la serikali, limekuja muda mfupi baada ya watu mbalimbali kutoa maoni yao kwenye mitandao na vyombo vya habari kwamba uamuzi wa serikali kuhusu pori tengefu si sahihi.

  Tamko la serikali lilitangazwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki hivi karibuni kwamba, wameacha  kilomita za mraba 25,000 kwa ajili ya wananchi na serikali imechukua kilomita za mraba 15,00 kwa ajili ya kutunza rasilimali za nchi.

  Alifanya hivyo kwa kwa mujibu wa Sheria ya Wanyamapori Namba 5 ya Mwaka 2009, Sehemu ya 16 Vifungu Na. 4, 5 na 6 na kwamba muda mrefu viongozi wa wizara wamekuwa wakikutana na wananchi na viongozi wa mkoa
  wa Arusha na Wilaya ya Ngorongoro kujua kero zilizopo ili zitatuliwe na ndio imewezesha serikali kufanya uamuzi alioufanya.

  "Ukweli ni kuwa Waziri Kagasheki alifuata sheria alipotoa tamko kuhusu kupunguza eneo la pori tengefu la Loliondo kwa mujibu wa sheria inayompatia waziri mwenye dhamana uwezo wa kupitia upya mapori tengefu
  na kufanya marekebisho mbalimbali muhimu kwa manufaa ya wananchi bila kuathiri uhifadhi,"alisema George Matiko, ambaye ni msemaji wa wizara.

  Katika taarifa kwa vyombo vya habari jana, Matiko alisema tamko lilizingatia tafiti mbalimbali ikiwemo utafiti wa  Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) na mapendekezo ya tume mbalimbali zilizoundwa kuchunguza mgogoro wa Loliondo ikiwemo ya Waziri Mkuu iliyoundwa mwaka juzi.

  Aliongeza kuwa eneo la kilomita za mraba 1,500 litaendelea kumilikiwa na wizara kwa mujibu wa sheria na kwa kutambua kuwa ni sehemu ya mazalia ya wanyamapori, mapito ya wanyamapori na vyanzo vikuu  vya
  maji kwa hifadhi mbalimbali ikiwemo Serengeti.

  Alisisitiza ardhi iliyobaki baada ya kuondoa eneo la pori tengefu la Loliondo itasimamiwa na vijiji kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya Vijiji Namba 5 ya Mwaka 1999 na wananchi watawezeshwa ili waanzishe Eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) katika ardhi hiyo kwa manufaa yao.

  "Tanzania inajali uhifadhi lakini pia inajali maslahi ya wananchi, ndiyo maana asilimia 25 ya eneo la nchi hii limehifadhiwa bila kuwepo migogoro. Hakuna migogoro kati ya wananchi na Serikali, kwa kuwa wananchi wanatambua umuhimu wa uhifadhi kwao na kwa vizazi vijavyo. Ndiyo maana wananchi wanachangia kwa kiwango kikubwa katika kufanikisha uhifadhi,"alimaliza Matiko.

  0 0

  Wakati ulimwengu ukiyumba kwa sababu ya matatizo ya kiuchumi, wajasirimali wanatafuta uchumi mbadala ambao wanaweza kuuamini kwa ajili ya kuhifadhi na kuzalisha pesa zao.

  Ktk mazingira hayo kuna sababu nyingi za kuamini kwamba uchumi unaofuata sheria za ki-Islam unajiuza, na hilo limetokana na misingi yake ktk kukataa riba, kukataa kitu kinachijulikana kama ‘short selling na baadhi ya miamala ya kibiashara inayoendelea duniani.

   Ni kwa sababu kama hizo ambapo ulimwengu uliingia ktk matatizo makubwa ya kiuchumi na kuwafanya wajasirimali kutafuta uchumi mbadala ambao unaongozwa kwa misingi madhubuti na kwa umakini wa hali ya juu imefahamika.

  Kufuatia mazingira hayo kiongozi wa Dubai Sheikh Mohammad Bin Rashid Al Maktoum mapema mwaka huu ametangaza kwamba ana mpango wa kuifanya Dubai kuwa makao makuu ya uchumi unaofuata sheria za ki-Islam.

  Kama hatua ya kulifanikisha hilo, Sheikh Mohammad alitangaza mkakati ya kuibadilisha Dubai kua makao makuu ya Sukuk (Islamic bonds) ambazo zitahamasisha mashirika na nchi mbalimbali kutoa Islamic bonds badala ya zile zile zisizokua za ki-Islam.

  Ktk hatua nyingine ni kuundwa kwa jopo la kisheria la pamoja ambalo litashughulia na maswala ya viwango. Kwa maelezo zaidi kuhusu benki zinazofuata sheria za ki-Islam tembelea http://ijuebankyakiislam.blogspot.com

  0 0

  Ambassador Mohamed Maharage Juma is the New Chief of Protocol in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation. 

  According to a statement released by the ministry, the appointment became effective on March 23, 2013. Before the appointment, Ambassador Juma was Tanzania's Ambassador in Abu Dhabi, UAE.
  President Jakaya Mrisho Kikwete introduces the First Lady Salma Kikwete to  Ambassador Mohamed Maharage Juma, the new Chief of Protocol
  President Kikwete, Vice President Dr Mohamed Ghalib Bilal, Prime Minister Mizengo Pinda and Ambassador Mohamed Maharage Juma chat as they await the arrival of Chinese President at the Julius Nyerere International Airport in Dar es salaam
  Ambassador Mohamed Maharage Juma  ready to undertake his first major assignment as the new Chief of Protocol during the two-day visit of Chinese President Xi Jinping

  0 0

  Ladies and Gentlemen, You'r busy.You haven't got time to listen to every note of every song that comes across your desk.That why we've made it easy for you to enjoy a few-minute of some of our best songs at www.ngoma-africa.com . That all takes.Few minutes.And you're done. If you like what you hear,please contact Us for our full-length CDs.... Or you wanna book the band for concert,Festival national and International tour,please contact@ngoma-africa.com website at http://www.ngoma-africa.com

  0 0


  Pichani kushoto ni Meneja Mahusiano wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel-Tanzania,Jackson Mmbando akimkabidhi fulana ya Airtel Yatosha pamoja na Muda wa maongezi kwa mmoja wa watumiaji wa huduma hiyo mara baada ya kueilezea vyema,kulia ni Meneja Mauzo wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel-Morogoro,Aluta Kweka.
  Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya wa hip hop, kutoka kundi la Tip Top Conection ajulikanae kwa jina la Madee a.k.a Rais wa Manzese akiwarusha vilivyo wakazi wa mji wa Morogoro na wimbo wake wa “NANI KAMWAGA POMBE YANGU”,wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel  Yatosha ndani ya mji huo.Huduma hiyo itatambulishwa tena  hivi karibuni  kwa wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake.
  Sehemu ya Umati wa watu waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha ndani ya mkoa wa Morogoro.
  Wakazi wa morogoro walijitokeza kwa wingi jukwaani kujiunga na huduma ya Airtel yatosha kwa Kupiga *149*99#.

  Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Ney wa Mitego akitumbuiza mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Morogoro waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel  Yatosha ndani ya mji huo.Huduma hiyo itatambulishwa tena  hivi karibuni  kwa wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake.

  Pichani kulia ni Meneja Mahusiano wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel-Tanzania,Jackson Mmbando akimkabidhi fulana ya Airtel Yatosha mmoja wa watumiaji wa huduma hiyo mara baada ya kueilezea vyema huduma hiyo mbele ya  wakazi wa mji  huo na vitongoji vyke,Katikati ni Msanii Nguli wa muziki wa kizazi kipya wa hip hop Fid Q akishuhudia tukio hilo.
  Msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Juma Nature akiwa sambamba na baadhi ya wasanii wenzake wanaounda kundi la Wanaume TMK-Halisi wakiwarusha vilivyo wakazi wa mji wa Morogoro na Vitongoji vyake wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya  Airtel Yatosha ndani ya mji wa Morogoro jana jioni kwenye viwanja vya shule ya msingi Sabasaba.

  Sehemu ya umati wa wakazi wa morogoro uliofurika kwenye uwanja wa shule ya msingi Sabasaba wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel  Yatosha wakishangilia,huduma hiyo itatambulishwa tena  hivi karibuni  kwa wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake.


older | 1 | .... | 86 | 87 | (Page 88) | 89 | 90 | .... | 3285 | newer