Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 877 | 878 | (Page 879) | 880 | 881 | .... | 3278 | newer

  0 0


   Mchakato wa Udhamini ukiendelea katika kijiji cha Sagara Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
   Dkt. Magufuli akiagana na Wanachama wa CCM katika Kijiji cha Sagara waliojitokeza kumdhamini katika harakati za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea Urais kupitia Tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao.

  Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mkoani Geita Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kulia  akikabidhiwa fomu yenye orodha ya Wadhamini kutoka Kijiji cha Sagara Wilayani Kongwa waliojitokeza kumdhamini katika  mbio za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama hicho kutoka kwa Katibu wa CCM Wilayani Kongwa 
   Dkt. Magufuli akisalimiana na wana Kongwa mara baada ya kupata wadhamini katika Wilaya hiyo Mkoani Dodoma. 
  Dkt. Magufuli akisalimiana na wana Kongwa mara baada ya kupata wadhamini katika Wilaya hiyo Mkoani Dodoma.


  0 0


  Mh January Makamba Akipokea Fomu ya Wazamini katika jiji la  Mwanza kutoka kwa Katibu wa CCM wilaya ya Ilemela Loth Olemeint.
  Mbunge wa Bumbuli January Makamba ambaye anazunguuka mikoani kwa sasa kusaka wadhamini, leo alikua katika Jiji la Mwanza huku mamia ya wanachama na wakazi wa Mwanza walifulika katika ukumbi wa Nyanza kumsikiliza Mh January.
  Makamba ametoa ahadi kwa wakazi wa Mwanza kuwa hataka kama hatofanikiwa katika Mchakato huu hatokua na kinyongo wala Chuki kwa atakae Teuliwa.
  Kwa upande mwingine Mh January amesema kuwa anamajibu ya kiuchumi katika Jiji la Mwanza na endapo akifanikiwa kupata nafasi hiyo atabadilisha uchumi wa jiji la Mwanza kwa kutumia lasiri Mali za jiji hilo la Mwanza. Picha zote na John Sambila

  Msafara wa Pikipiki ukimpokea January Makamba Kuelekea Ukumbi wa Nyanza.  Mh January Makamba akimshukuru Katibu wa CCM wilaya ya Nyamagana Elius Mpanda baada ya kupata wadhamini wa kutosha mkoani Mwanza.

  0 0

   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Chifu wa Wahehe Adam Abdu  Sapi Mkwawa baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Iringa 
   Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu  wakizungumza na  Chifu wa Wahehe Adam Abdu  Sapi Mkwawa baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Iringa leo
  Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na  Chifu wa Wahehe Adam Abdu  Sapi Mkwawa baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Iringa Juni 20, 2015 
  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0


  By Dr. Noorali T. Jiwaji
  The Open University of Tanzania
  Faculty of Science Technology and Environmental Studies
  Lecturer in Physics
  Head of Department of Physical Sciences

  0 0

  Hamisi Mrisho Mohamedi mzawa wa Kariakoo ambaye pia ana makazi yake kule Segerea Jijini Dar, siku ya Ijumaa, 19 Juni 2015 alifunga ndoa na Bi. Rehema Joachim Milanzi mkazi wa Segerea, Dar. Mohamedi kuachana kabisa na klabu ya makapera aka Bado nipo nipo Club na kufanikiwa kupata mama mwenye nyumba Bi. Rehema. Harusi ilifanyika Masjid Kubah iliyopo Segerea Mwisho, Dar es Salaam. Tuwatakie maisha mema maharusi.
  Maharusi wakiwa wamekumbatiana kwa furaha baada ya kumeremeta 
  Maharusi wakisindikizwa 
  Maharusi wakiwa na furaha na hati zao za ndoa

  0 0


  0 0


  Nembo ya UM
  Kila mwaka, Umoja wa Mataifa hutafuta vijana waliobobea katika fani mbali mbali, ambao wapo tayari kuanza huduma ya kitaaluma kama wahudumu wa kimataifa wa umma. Mpango wa Vijana Waliobobea Kitaaluma, yaani YPP, huleta vipaji vipya kwa Umoja wa Mataifa kupitia kwa mtihani wa kila mwaka.
  Mwaka huu wa 2015, mtihani utafanyika mnamo tarehe 4 Disemba katika fani za Usimamizi, Masuala ya fedha, Mifumo ya takwimu, habari, masuala ya kijamii na Masuala ya Sheria.
  Ili kushiriki mtihani huu, ni lazima uwe unatoka nchi zilizoorodheshwa kushiriki mwaka 2014, uwe na shahada ya kwanza, uwe unaongea Kiingereza au Kifaransa sanifu, na uwe na umri wa miaka 32 kabla ya mwisho wa mwaka huu. Utatakiwa kufanya ombi la kushiriki mtihani huu kati ya tarehe zifuatazo:
  Mei 20 hadi Julai 19 -     Usimamizi
  Mei 27 hadi Julai 26 -      Fedha
  Juni 03 hadi Agosti 02 – Takwimu
  Juni 10 hadi Agosti 09 – Habari
  Juni 17 hadi Agosti 16– Masuala ya Kijamii
  Juni 24 hadi Agosti 23– Masuala ya Sheria
  Kumbuka, itakuwa vyema ikiwa utakamilisha na kuwasilisha maelezo yote kwa njia sahihi na nadhifu kwani hicho kitakuwa kigezo cha kupima uwezo wa wako kukubaliwa kuufanya mtihani.
  Kumbuka pia kuwa, maombi ambayo hayatakamilishwa vyema au yatakayochelewa kuwasilishwa hayatakubaliwa, kwa hiyo ni lazima uwasilishe ombi lako kabla ya tarehe ya ukomo.
  Kuona kama nchi yako inashiriki,  na maelezo zaidi, tembelea tovuti:
  Mtihani
  Mtihani umegawika katika sehemu mbili: sehemu ya kwanza ambayo ni kwa kuandika, itatahini upana wa ujuzi wako, uwezo wa kutathmini mambo, na uwezo wa kuandika nakala muhimu.
  Sehemu ya pili ni kwa wale wanaopita ule wa kwanza pakee, na ni aina ya mahojiano

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Peter Malebo Mjumbe wa Kamati ya Mgusu Miners Co. Oparative Society Limited jinsi mchanga unavyosafishwa.

  Katibu Mkuu wa CCM Ndug Kinana leo amehitimisha ziara yake ndani ya mkoa wa Geita kwa kutembea kilometa 1680 kwa Gari,ametembelea Majimbo sita na Wilaya zake sita,huku akiwa amehutubia mikutano 78,mikutano 72 ya hadhara na mikutano 6 ya ndania.Ndugu Kinana ametembelea miradi 53 ya Maendeleo,miradi mitano ya CCM.Kama vile haitoshi Ndgu Kinana amejizolea Wanachama wapya 6816,Wapinzani wakiwa 640 hasa kutoka CHADEMA.

  Ndugu Kinana akiwa na msafara wake kesho anaanza ziara Mkoani Mwanza ya Kuimarisha uhai wa chama,kuhimiza na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2010-15,sambamba na kusikiliza matatizo ya Wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.
   Baadhi ya Wachimbaji wadogo wadogo wakiendelea na shughuli zao za kusaka Dhahabu katika eneo waliloachiwa wachimbaji hao eneo la Mgusu,wilayani Geita mkoani Geita.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyeshwa dhahabu ambayo tayari imeshapatikana baada ya kupitia hatua zote hizo kutoka kwa  Mjumbe wa Bodi ya Mgusu Miners Co Oparative Society Limited Bw.Abdul Jumbe.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Geita Mh. Vick Kamata wakinyanyua mikono juu wakati wakikabidhi baiskeli za viongozi wa kata wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) zilizonunuliwa na Mbunge huyo, katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Nyankumbu.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Shule ya Msingi, Nyankumbu, katika Kata ya Kalangalala, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama mkoani Geita leo.

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akipokea baadhi ya wafuasi wa chama  cha CHADEMA,waliokuwa wakirudisha kadi na kujiunga na chama cha CCM,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Nyakumbu,mkoani Geita.

    Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha wachimbaji dhahabu wadogo wadogo,Mkoani Geita.

  PICHA NA MICHUZI JR-GEITA.


  0 0

  Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake cha leo pamoja na mambo mengine kilipitia mwenendo wa timu ya Taifa (Taifa Stars) ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mchezo kati ya Tanzania na Uganda, kama sehemu ya tathmini ya mwenendo wa timu.

  Kamati ya Utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo;
  1. Ajira ya Kocha Mkuu Maart Nooij inasitishwa mara moja kuanzia Juni 21, 2015.
  2. Benchi lote la ufundi la Taifa Stars limevunjwa kuanzia Juni 21, 2015.
  3. Uongozi wa TFF utatangaza punde benchi jipya la ufundi la timu ya Taifa.

  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA 
  MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
  Juni 20, 2015

  Kocha Mkuu wa Taifa Stars Maart Nooij akisindikizwa na ulinzi mkali usiku huu baada ya kumalizika kwa mchezo wa Tanzania na Uganda wa kuwania kufuzu fainali za CHAN katika Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar ambapo Taifa Stars ilichapwa 3-0.


  0 0

  Rais wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiwa katika mazungumzo na Wakuu wa Makampuni makubwa ya India. 
  Aliwahimiza kuchangamkia fursa za uwekezaji nchini Tanzania. kushoto kwa Mhe. Rais ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Abdallah Kigoda (Mb) na kulia ni kiongozi wa Chama cha Wafanyabiashara nchini India. Mazungumzo hayo yakifanyika katika Hoteli ya Taj Palace jijini Delhi 
  
  Wakuu wa Makampuni Makubwa ya India wakimsikiliza Rais Kikwete. Baadhi ya Makampuni hayo tayari yalishawekeza nchini Tanzania na Makampuni mengine yalionesha dhamira ya kuja kuwekeza.
  Kiongozi wa Chama cha Wafanyabiashara wa India akimkabidhi, Mhe. Rais zawadi.
  Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Abdallah Kigoda (Mb) kulia akizungumza jambo na mmoja wa Wakuu wa Makampuni ya India. Mwingine kushoto ni Waziri wa Maji, Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (Mb). Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Dear friends and supporters, 
   I am very please to be able to share a brand new song and video with you. Twajiachia was recorded at Tao Studio in Hamburg, together with German producer Flo Bauer during the Mzungu Kichaa and Malfred tour at the end of 2014. 
  Their Tanzanian backing band Bongo Beat also joined them for the recording session. 
  All musicians are featured in the music video, which was directed and shot on location in Hamburg by Zeki Oguz Teoman. 
  The video represents the journey of 6 musicians from Tanzania, who during their tour, do a quick visit for a one day studio session, and record from the heart and from the fingertips.
  Twajiachia literally means ‘we are letting go’ but in slang it would translate more towards ‘we are having fun’. The chorus ends with the line ‘ngoma likipigwa tuna pata raha tele’ which means ‘when the drum beats, we are filled with joy’. ‘At times we all face hardships and music can be an important tool to help bring back the joy and purpose in life. Twajiachia is meant to do exactly this!’ – Mzungu Kichaa. 
   The song is an example of the globalization of urban club music: an upbeat fusion between European electronic sounds, Bongo Flava and Jamaican dancehall. 
   Please tag @mzungukichaa,
   @malfred and hashtag #twajiachia when posting your comments or links to social media so that we can repost and share your thoughts and comments with our followers.
  Espen Sorensen
   - Mzungu Kichaa

  0 0
 • 06/20/15--14:06: welcome to safaribudget.com
 • Safaribudget.com is a result of collaboration and innovative efforts of dedicated people and companies to offer customers best value, right price, and convenient service. It’s time to make a reservation for a safari of a lifetime at safaribudget.com You have come to the right place to get the best value and the right price for you. 
  We are great at what we do and you are the reason why we are in this business. Don’t let the wrong websites or companies bombard you with tons of information that do nothing to help you make a smarter decision. We use reliable methodology to identify the right partners have done our home work to research our partners whom we connect you with because they have the state of the art facilities and manpower to take care of you from start to finish. You will be glad you have called us. 

  0 0


  0 0


  0 0

   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiangalia bidhaa mbali mbali wakati alipotembelea masoko ya Mkoa wa Mjini Magharibi kuangalia upatikanaji wa bidhaa hizo zinazotumika zaidi katika mwezi mtukufu wa Ramadhan.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiangalia bidhaa mbali mbali wakati alipotembelea masoko ya Mkoa wa Mjini Magharibi kuangalia upatikanaji wa bidhaa hizo zinazotumika zaidi katika mwezi mtukufu wa Ramadhan. 
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiangalia bidhaa mbali mbali wakati alipotembelea masoko ya Mkoa wa Mjini Magharibi kuangalia upatikanaji wa bidhaa hizo zinazotumika zaidi katika mwezi mtukufu wa Ramadhan.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiulizia bei ya samaki aina ya vibua katika soko la Mombasa ambapo fungu moja linauzwa shilingi elfu tano.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiangalia bidhaa za viatu na vitambaa katika eneo la biashara Saateni, alipotembelea eneo hilo kuangalia hali ya upatikanaji wa bidhaa hizo. 
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiangalia bidhaa za viatu na vitambaa katika eneo la biashara Saateni, alipotembelea eneo hilo kuangalia hali ya upatikanaji wa bidhaa hizo.
  Picha na Salmin Said, OMKR

  0 0

  Hii ndio ratiba ya Bongo Star Search 2015 ... Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es Salaam. Follow BSS2015 Twitter @BstarSearch | Instagram @BongoStarSearch | Facebook www.facebook.com/BongoStarSearch kwa maelezo zaidi

  #JukwaaNiLako #KuwaOriginal

  0 0

   Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha Mustafa Panju akiongea na vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake ,akitangaza rasmi kuwania kiti cha ubunge jimbo la Arusha mjini kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM
   Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha Mustafa Panju akiongea na vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake ,akitangaza rasmi kuwania kiti cha ubunge jimbo la Arusha mjini kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM kushoto ni mke wake
   Kassim Mamboleo ambaye ni katibu wa kamati ya ushindi ya mgombea Mustafa Panju akitoa utambulisho kwa vyombo vya habari
  Taswira katika mkutano huo na waandishi wa habari

  Na Pamela Mollel, Arusha
  JIMBO la Arusha ni moja ya jimbo ambalo linaonekana kuwa  ni jimbo lenye siasa komavu, kutokana na hali hiyo limeonekana kuongoza kwa vurugu na uvunjifu wa amani , ambapo kupitia kwa Mtangaza nia wa ubunge jimbo la Arusha mjini  Mustafa Panju amewahakikishia wananchi
  kurudisha amani hiyo.

  Jimbo hilo ambalo linashikiliwa na Mbunge wa Arusha mjini kupitia 
  chadema ,Godbless Lema ambaye hivi sasa ametangaza tena kulitaka jimbo 
  , ambapo hadi hivi sasa jumla ya wagombea 18 kupitia chama cha
  mapinduzi wamejitokeza kumg’oa mbunge huyo.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana  wakati akitangaza nia ya 
  kuwania ubunge kupitia chama cha mapinduzi , Panju alisema kuwa ipo 
  sababu ya kurudisha jimbo hilo mikononi mwa CCM kwa kuwa CCM ni chama
  kinachopenda amani na kinachodumisha amani.

  ‘kila mmoja anatambua jinsi ambavyo jiji la Arusha hivi sasa halina 
  amani kabisa na hakuna mtu anayedhubutu hata kutembea usiku , ila 
  nitahakikisha linakuwa jiji la amani na utulivu na kuwawezesha 
  wananchi wake kufanya shughuli zao bila hofu yoyote’alisema Panju.
  Alifafanua zaidi kuwa,mbali na kurejesha amani jijini Arusha
  atahakikisha anaondoa makundi mbalimbali yaliyopo miongoni mwa 
  wananchi kwa kuwafanya wawe wamoja na wenye ushirikiano ili kuleta 
  mabadiliko katika jimbo la Arusha kwa ujumla.
  Pia alisema kuwa,wagombea wote wa nafasi ya ubunge katika chama ni 
  wajibu wao kujenga Undugu,Upendo, na urafiki wakati wote ili kuepuka 
  kujenga makundi ndani ya chama kwa misingi mbalimbali ya ukabila, 
  udini na hata urangi.
  Panju alisema kuwa, swala la kuwepo kwa makundi na vikundi katika 
  vyama na kwa wananchi linapaswa kuangaliwa kwa umakini kwani 
  likiendelea kuwepo linajenga uhasama ndani ya chama  na pia uhasama
  unaoleta ubaguzi ndani ya nchi kwa ujumla 

  0 0
 • 06/21/15--01:27: Kibonzo cha leo
 • 0 0

   Kampuni na taasisi zinazotoa huduma katika bandari ya Dar es Salaam zimeshauriwa kuanza kufikiria kuhamia katika jengo jipya la kisasa la Mamlaka ya Bandari Tanzania (kushoto) kama moja ya kuimarisha huduma za bandari. 
  Akizungumza na timu ya wahariri waliotembelea bandari hiyo hivi karibuni, Kaimu Meneja wa bandari ya Dar es Salaam, Bw. Hebel Mhanga alisema mbali na kuwa makao makuu ya TPA, jengo hilo litakapokamilika litakuwa na kampuni na taasisi mbalimbali zinazohudumia bandari. 
  “Hiki kitakuwa ni kituo kimoja cha kutolea huduma za bandari...tunakaribisha maombi ya nafasi toka kwa wadau wetu mbalimbali,” alisema. 
  Jengo hilo la ghorofa 35 litakuwa kati ya majengo marefu kabisa jijini. Tayari baadhi ya taasisi kama Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Ofisi ya Mkemia Mkuu na wakala wa Mizani na Vipimo tayari zina madawati yao TPA. 
  Meneja huyo alisema kuwa kama kampuni na taasisi nyingine zitafanya hivyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha huduma za bandari na kuifanya kuwa shindani. “Ujenzi wa jengo hili ni moja ya hatua za serikali kuimarisha huduma za bandari hii,” alisema. 
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kimataifa cha Makasha (TICTS), Bw. Paul Wallace alisema wanazidi kununua vifaa vya kunyanyulia mizigo vya kisasa zaidi kuhudumia shehena ya mizigo inayozidi kuongezeka siku hadi siku. 
  “Tumejipanga kuhudumia kwa wakati na ufanisi na hivyo kuchangia kuimarisha bandari hii,” alifafanua. 
  Alisema bandari hiyo inahitaji kuwa na kina kirefu ili kuwezesha meli kubwa zaidi kutia nanga na pia kuwa na mtandao mzuri wa barabara na reli unaounganisha Tanzania na nchi jirani. 
  “Majukumu haya ni ya serikali na wadau wengine kwa ujumla,” alieleza. Alisema TICTS inaendelea kuimarisha huduma zake ili kuifanya bandari kuwa kimbilio katika eneo hili la Africa. 
  “Bandari inaimarika kwa haraka...kuna kila sababu ya sisi kuwekeza zaidi hapa,” aliongeza.
   Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Hebel Mhanga (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kitengo cha Kimataifa cha Makasha (TICTS), Bw. Paul Wallace wakati wa ziara ya wahariri wa vyombo vya habari katika bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni.  Wahariri hao walitembelea maeneo mbalimbali katika bandari hiyo.
  Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Hebel Mhanga (kulia) akiwaelezea jambo wahariri wa vyombo vya habari katika bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni.  Wahariri hao walitembelea maeneo mbalimbali katika bandari hiyo.

  0 0

  Chuo Kikuu Mzumbe kimeanza rasmi awamu ya pili ya mchakato wa kuhuisha mtaala unaotumika katika Skuli yake ya Biashara ili kuendana na hali hasi ya mabadiliko yanayotokea haraka nchini na duniani katika nyanja za siasa, uchumi, jamii na teknolojia. 
  Inatarajiwa kuwa mabadiliko hayo yatasaidia pia kuwajengea zaidi uwezo wahitimu wa chuo hicho kujiajiri na kuajiriwa kwa urahisi zaidi. 
  Kaimu Naibu Makamu mkuu wa Chuo hicho, Taaluma, Profesa George Shumbusho aliwaambia waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mjini hapa kuwa mabadiliko hayo yanalenga kutoa wahitimu watakaokuwa na uwezo wa kushindana kitaifa na kimataifa katika nyanja za biashara, manunuzi, na ujasiriamali. 
  Uongozi na wataalamu wa chuo hicho ulikutana na wadau mbalimbali kutoka sekta ya umma na binafsi kupitia rasimu ya mapendekezo ya mabadiliko ya mtaala wa skuli ya chuo hicho. “Ni utaratibu wa chuo chetu kuhakikisha kuwa tunapitia mitaala kila baada ya miaka mitatu ili kuihuisha,”alisema Prof. Shumbusho. 
  Alisema mwanzo skuli hiyo iliwaomba wadau wa chuo wakiwemo waajiri, wazazi na taasisi mbalimbali kutoa mawazo yao kuhusu hitaji la kuwa na mtaala mpya unaoendana na mabadiliko yanayojitokeza hapa nchini na ulimwengu kwa ujumla. 
  Maoni hayo yalichukuliwa na kuingizwa katika rasimu ya mtaala iliyopendekezwa na kupitiwa na walimu na wanafunzi ambao waliandaa rasimu ya pili ambayo ndio ilikuwa inajadiliwa tena na wadau hao. 
  Profesa Shumbusho alisema baada ya kupata maoni ya wadau hao tena, watatoa rasimu ya mwisho ambayo itajadiliwa na seneti ya chuo hicho na kupelekwa Tume ya Vyuo vikuu (TCU). 
  Inatarajiwa kuwa mtaala huo utaanza kutumika mwezi Octoba 2015. Mkuu wa Skuli ya Biashara, Dkt. Hawa Tundui alisema skuli hiyo imedhamiria kutoa elimu iliyo bora na kuwa shindani hapa nchini na katika eneo hili la Afrika. “Tunataka kuleta manufaa zaidi kwa wahitimu, jamii, na nchi kwa ujumla,” alisema. Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Dkt. Clemence Tesha alisema mitaala ni lazima iendane na mageuzi yanayojitokeza la sivyo vyuo vitakuwa vinafundisha vitu vilivyopitwa na wakati. 
  “Katika vyuo hili ni jambo la lazima ili kuiwezesha nchi kuwa na wasomi wanaoendana na wakati,”alisema. 
  Alisema wao kama wadau wametoa maoni yao kwa mambo ya msingi yanayohitajika kufanyika ili taifa liweze kuwenda sambambana na mahitaji ya soko na nchi. 
  Baadhi ya wadau walioshiriki katika kujadili rasimu hiyo ni pamoja na Wizara ya Maji, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), PSPTB, Mamlaka ya Manunuzi nchini (PPRA), Mamlaka ya Usimamzi na Udhibiti wa Huduma za Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), benki ya CRDB, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu, Kampuni za Ukaguzi, na wajasilimali mbalimbali.
   Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Taaluma, Profesa George Shumbusho (kulia) akiwasilisha mada wakati wa kongamano la majadiliano ya rasimu ya mtaala wa Chuo Kikuu Mzumbe, Skuli ya Biashara, hivi mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Kongamano hilo lilihusisha wadau mbalimbali kutoka sekta ya umma na binafsi.
  Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Taaluma, Profesa George Shumbusho (kulia) akijadiliana jambo na Mkuu wa Skuli ya Biashara ya chuo hicho, Dr. Hawa Tundui (kushoto) wakati wa kongamano la majadiliano ya rasimu ya mtaala wa Skuli hiyo ya Biashara mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Kongamano hilo lilihusisha wadau mbalimbali kutoka sekta ya umma na binafsi.

older | 1 | .... | 877 | 878 | (Page 879) | 880 | 881 | .... | 3278 | newer