Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

Banda la Wizara ya Mambo ya Nje lazidi kung'ara kwenye maonesho ya Utumishi wa Umma

0
0
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bw. Mkumbwa Ally akizungumzia ushiriki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye maonyesho ya ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam
Afisa Mwandamizi wa Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje  na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Mashaka Chikoli akielezea utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje  na mafanikio ya Wizara  kwa  Mtayarishaji wa Vipindi vya Televisheni, Bw. Paschal Mayala.
Mkufunzi wa Chuo cha Diplomasia, Bw. Ali Masabo akielezea Kozi mbalimbali zinazotolewa na Chuo hicho ikiwemo kozi mpya ya Shahada ya Mahusiano ya Kimataifa na Diplomasia wakati akihojiwa na Bw. Mayala. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MATHIAS CHIKAWE ATOA RISALA YA SIKU YA WAKIMBIZI DUNIANI

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AUNGURUMA WILAYANI BUSANDA NA MJI MDOGO WA KATORO MKOANI GEITA LEO.

0
0


 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Mji Mdogo wa Katoro, wakati wa ziara Jimbo la Busanda, wilayani Geita, Mkoa wa Geita, ambapo aliwaahidi wachimbaji wadogo wadogo kulitafutia ufumbuzi wa kuwapatia vitalu vya machimbo eneo la Nyarugusu linalomilikiwa na Stamico, wilayani Geita.

Ndugu Kinana ambaye ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, yupo mkoani Geita kwa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kupokea kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. eneo la Nyarugusu. 
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Katoro waliojitokeza kwa wingi ,Katika mkutano huo Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi aliwaambia wakazi hao vyama vingi vya siasa vimeshindwa kuendelea kutokana na kukosa sera,kushindwa kusimamia mambo pamoja na kuwa na viongozi wasiokubali mabadiliko na kung'ang'ania madaraka.
Wakazi wa Katoro waliojitokeza kwa wingi ,Katika mkutano huo Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi aliwaambia wakazi hao vyama vingi vya siasa vimeshindwa kuendelea kutokana na kukosa sera,kushindwa kusimamia mambo pamoja na kuwa na viongozi wasiokubali mabadiliko na kung'ang'ania madaraka.
  Sehemu ya umati wa watu waliofurika katika mkutano wa hdhara uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana katika Mji Mdogo wa Katoro, Jimbo la Busanda, mkoani Geita leo.


Mbunge wa Jimbo la Busanda Mhe.Mh Lolensia Bukwimba akihutubia wakazi wa Katoro kwenye mkutano wa hadhara ambao mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
PICHA NA MICHUZI JR-BUSANDA,GEITA

wimbo maalumu wa kumkaribisha JK Stockholm, Sweden

0
0
TZK tulifurahi sana kupata nafasi ya kutengeneza wimbo wa kumkaribisha Mh Dr. Jakaya Mrisho Kikwete 2015.

Tino Mhina - Producer
Zoelina Mårsen - Singer and song  writer.
Kennedy Mmbando - Singer and song writer/Fine artst

MUSLIM ARUDISHA FOMU YA UBUNGE, MAKUNGU AJIUNGA NA CHADEMA

0
0
Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Muslim Hassanali akirudisha fomu  kwa Mratibu wa Kanda ya Pwani, Casimir Juma Mabina  za kuomba kuteuliwa kuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya chadema katika uchaguzi mkuu ujao. Kulia ni Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema, Mabere Marando. (Picha na Francis Dande)
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  Mabere Marando (kushoto) akimkabidhi kadi ya Chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM tawi la Kigamboni Wilaya ya Mafia, Mohamed Makungu ambaye amekiama chama chake na kujiunga na Chadema. Hafla hiyo ilifanyika katika Ofisi za Kanda ya Pwani jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mwenyekiti Bodi ya Wadhamini wa chama hicho, Arcado Ntagazwa.

AFRICAN BUSINESS ROUNDTABLE AND GLOBAL AFRICAN DIASPORA TOURISM INITIATIVES

0
0
 Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bibi Lily Munanka wa pili kulia pichani pamoja na mabalozi wengine walipotembelea bandari ya Philadelphia ambayo inapokea bidhaa nyingi kutoka Afrika hasa mazao ya kilimo.
 Bibi Munanka akizungumzia kuhusu Tanzania na fursa zilizopo kwenye mkutano wa African Business Roundtable.
 Bibi Munanka akijadiliana jambo na mwakilishi kutoka ubalozi wa Afrika Kusini kwenye mkutano wa The Global African Diaspora Tourism.

Mwakilishi wa Ubalozi, wa kwanza kushoto pichani Bibi Munanka pamoja na baadhi ya mabalozi wakisikiliza kwa makini mada inayowasilishwa na mmoja wa mabalozi kutoka nchi za Afrika kwenye mkutano wa Global African Diaspora Tourism Initiatives uliofanyika jijini Philadelphia.

                          PICHA ZOTE KWA HISANI YA UBALOZI.

DIRA YA DUNIA YA IDHAA YA KISWAHILI YA BBC, LONDON LEO IJUMAA

MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2015 VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM.


Tanzania na India Zasaini Mikataba kadhaa ya Ushirikiano

0
0
 The Deputy Minister for Foreign Affairs and International Cooperation Dr.  Mahadhi Juma Maalim exchange documents with his counterparts India’s Secretary in The Ministry of Defence Shri Mohan Kumar on Memorandum of Understanding in the Field of Hydrography between India and Tanzania
 The permanent Secretary in The Ministry of Natural Resources and Tourism Dr.Adelhelm  Meru  exchange documents with India’s Administrative Secretary in the Ministry of Tourism  after signing an MOU on cooperation in the field of Tourism
 The Deputy Permanent Secretary in the Ministry of Finance Ms.Dorothy Mwanyika exchanges documents with the chairman of the EXIM Bank Mr. Yaduvendra Mathur after signing a loan agreement between Exim Bank and Government of Tanzania for US$268.35 million for extension of Lake Victoria pipeline project.
 The Head of East Africa Statistical Training Center(EASTC) Professor Innocent Ngalinda exchange documents with his Indian counterpart Mr.T.V Raman after signing an MOU between his institute and the India’s National Statistical System Training Academy(NSSTA) on establishing a collaborative program in official statistics.
.During the same occasion India’s Chief Hydrographer Vice admiral SK Jha handed over Navigational charts for the ports of Zanzibar and Dar es Salaam, harbor to Defense Advisor in the Tanzania High Commission to India Major General Issa Nassor, for which survey was conducted by Indian Navy. Photos by Freddy Maro.

PRESIDENT KIKWETE WITH INDIA PRIME MINISTER NARENDRA MODI HOLD JOINT PRESS CONFERENCE IN NEW DELHI

WIMBO MPYA: KADJA NITO - SINA MARINGO

0
0
Msanii wa Bongo Fleva, Kadja Nito.

MSIBA NEW YORK NA TANZANIA. MAZIKO YANATARAJIWA KUWA JUMAPILI JUNE 28,NEW JERSEY,TUTAUAGA MWILI BRONX,NEW YORK. RATIBA HII ITATEGEMEA NA UKAMILIFU WA MICHANGO YETU TAFADHALI CHANGIA ILI TUKAMILISHE JUKUMU HILI KWA PAMOJA.

0
0
MAREHEMU MZEE ALFRED MAGEGE.

Jumuiya ya Watanzania New York,New Jersey,Connecticut na Pennsylvania inaungana na Familia ya Magege kwa masikitiko kutangaza kifo cha marehemu Mzee Alfred Magege kilichotokea jumamosi June 13,2015. Marehemu Alfred Magege alisumbuliwa na Saratani ya mifupa kwa zaidi ya miaka kumi.Marehemu ameacha Mke na watoto watatu. Kama kawaida yetu tunaombwa watanzania tujitokeze ili kuwafariji wafiwa.Ili tukamilishe Msiba huu kiasi cha $10,000 kinahitajika.Watanzania tuungane,tujitolee kwa hali na Mali tusaidiane kumzika Mtanzania mwenzetu.Michango yenu inahitajika. Tuchangie kupitia www.gofundme.com/wyfewd5 
Msiba utakuwa 
2939 Wilson Avenue,Bronx,NY,10469. 
Kwa taarifa zaidi tuwasiliane na wafuatao.
 Hajji Khamis:3476238965 
Miriam Abu:9143162814 
Seif Tunaomba msaada wenu wanagroup mwili uko Funeral home na michango inahitajika ili tukamilishe. Tuchangie tuwezavyo kwani katika hali inayoweza kumkuta kila mmoja kati yetu.

MKUTANO WA CHADEMA MJINI MOSHI MKOANI KILIMANJARO.

0
0
Mwenyekiti wa Chama Taifa Freeman Mbowe akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Reli, Kata ya Njoro, Manispaa ya Moshi mjini jana.
Baadhi ya Wakazi wa  Kata ya Njoro,Manispaa ya Moshi mjini wakiwa kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa reli wakimsikiliza Mwenyekiti wa CHADEMA-Taifa ,Mh Freeman Mbowe.

WASANII MAARUFU WA VICHEKESHO WATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

0
0
000000
 Msanii maarufu wa vichekesho nchini wa Kundi la Kashi-Kashi anayeshiriki katika kipindi cha Mizengwe cha Kituo cha ITV, Habib Mrisho (Sumaku) akisaini kitabu cha wageni katika banda la Jeshi la Magereza wakati msanii huyo na mwenzake Jesca Kindole kwa jina maarufu la uigizaji (Safina -kulia) walipotembelea mabanda ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kulia ni maafisa wa Jeshi hilo.
00000
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Bulimba (kulia) akiwapa maelezo wasanii maarufu wa vichekesho wa Kundi la Kashi-Kashi wanaoshiriki katika kipindi cha Mizengwe cha Kituo cha ITV, kuhusu taarifa mbalimbali zinazoandaliwa na Jeshi hilo, katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Jesca Kindole (Safina) na Habib Mrisho (Sumaku).0000
 Wasanii maarufu wa vichekesho nchini wa Kundi la Kashi-Kashi wanaoshiriki katika kipindi cha Mizengwe cha Kituo cha ITV, wakipewa maelezo na Koplo wa Jeshi la Polisi, Sylvester Mganga, kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Jeshi hilo, katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Habib Mrisho (Sumaku), Jesca Kindole (Safina) na Rashid Costa (Maringo 7).000
2. “UTII WA SHERIA BILA SHURUTI” Msanii maarufu wa vichekesho nchini wa Kundi la Kashi-Kashi anayeshiriki katika kipindi cha Mizengwe cha Kituo cha ITV, Jesca Kindole (Safina) akilipigia saluti sanamu la askari wa Jeshi la Polisi wa kipindi cha kikoloni, wakati msanii huyo na wenzake walipotembelea mabanda ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.00
Wasanii maarufu wa vichekesho nchini wa Kundi la Kashi-Kashi wanaoshiriki katika kipindi cha Mizengwe kinachorushwa na Kituo cha ITV, wakichukua vipeperushi vya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi toka kwa Afisa wa Idara ya Probesheni na Huduma kwa Jamii, Pendo Mtama (kulia) wakati wasanii hao walipotembelea mabanda ya Wizara hiyo, katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Habib Mrisho (Sumaku) na Jesca Kindole (Safina).Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kipindi Kipya ' Nyumbani Na Diaspora'


KIONGOZI WA CHAMA CHA ACT WAZALENDO, ZITTO KABWE, AWAHUTUBI WAKAZI WA MJI WA MPANDA

0
0
001
Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, akiwahutubi wakazi wa mji wa Mpanda mkoani Katavi jana, ambapo chama hicho kinaendelea na ziara za kutambulisha viongozi wake. 002mail.google.com
Mwanaharakati na Mshauri wa chama cha ACT Wazalendo, Mama Terry, akiwahutubia wakazi wa mji wa Mpanda mkoani Katavi jana, ambapo chama hicho kinaendelea  na ziara ya kutambulisha viongozi wake.003

MHANDISI EDWIN NGONYANI ATEMBELEA MABANDA YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI KWENYE MAONESHO YA UTUMISHI WA UMMA

0
0
????????????????????????????????????
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la  Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi  Edwin Ngonyani (kushoto) akisaini kitabu  cha wageni kwenye banda la Wizara ya Nishati na Madini.
????????????????????????????????????Mtaalam kutoka Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC), Jumanne  Shimba ( wa kwanza kulia) akimwonesha Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la  Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi  Edwin Ngonyani (katikati)  moja ya  bidhaa zinazotengenezwa na  kituo hicho, kwenye  banda la Wizara ya Nishati na Madini
????????????????????????????????????Afisa Uhusiano kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA), Yisambi Shiwa (kulia) akieleza shughuli zinazofanywa na  wakala huo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la  Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi  Edwin Ngonyani (Kushoto) mara alipotembelea banda la wakala huo. Katikati ni Omari Rwakyaya kutoka wakala  huo.
????????????????????????????????????Kaimu Afisa Masoko Mkuu kutoka makao makuu ya Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) (Katikati), Monica Massawe akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la  Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi  Edwin Ngonyani (Kushoto) mara alipotembelea banda la TANESCO. Kulia ni Afisa Uhusiano Wateja –TANESCO  Mkoa wa Illala, Lucas Kusare.
????????????????????????????????????Mtaalam kutoka Idara ya Nishati – Wizara  ya Nishati na Madini, Jacob Mayala (Kulia) akimweleza Abdul Naseka (Kushoto) majukumu  ya Idara ya Nishati kwenye maonesho ya  Wiki ya Utumishi wa Umma  yanayoendelea katika  viwanja  vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam.
????????????????????????????????????Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi Edwin Ngonyani (katikati aliyevaa suti) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kutoka Wizara ya Nishati na Madini.

MKUTANO MKUU WA MWAKA WA 27 Ecobank Group jijini Dar es Salaam

0
0
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 27 wa Ecobank wakiwa kwenye mkutano huo, katika  Ukumbi wa Julius Nyerere Convention Centre uliofanyika jijini Dar es Salaam leo, 19 June 2015. 
Meza kuu
Wakurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya ECOBANK wakishiriki Mkutano Mkuu wa mwaka wa benki hiyo, uliofanyika ukumbi wa Julius Nyerere Convention Centre jijini Dar es Salaam leo, 19 June 2015.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Emmanuel Ikazoboh (kulia), akiendesha Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Ecobank Group, jijini Dar es Salaam leo.
Wajumbe wa mkutano huo wa 27 wa mwaka wa Ecobank, wakifuatilia taarifa mbalimbali wakati wa mkutano huo jijini Dar es Salaam.

MH.WAZIRI WA FEDHA SAADA M.SALUM AFANYA UKAGUZI WA MATUMIZI WA MASHINE ZA EFD KATIKA MADUKA MKOANI DODOMA.

0
0
1
Mh.Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum(MB) akitoa maelekezo kwa Meneja wa TRA mkoani Dodoma (mwenye miwani) na wakala wa TRA kutoka Yono Action Mart kulifunga duka la Salome Furniture baada ya kukutwa akifanya biashara bila ya kutumia risiti za mashine ya EFD.2
Mh.Waziri wa Fedha Mhe. Saada M.Salum(MB) akimsikiliza msimamizi wa duka la Salome Furniture wakati akijitetea baada ya kukutwa anafanya biashara bila ya kutumia mashine ya EFD.3
Waziri wa Fedha Mh. Saada M.Salum(MB) akiwa katika mgahawa wa Dodoma Carnival alipotembelea kukagua matumizi ya mashine za EFD. Mh.Waziri aliagiza mgahawa huo ufungwe mpaka hapo watakaponunua mashine hizo. Kushoto kwa Mh.Waziri ni meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma na mwenye shati jekundu ni msimamizi wa mgahawa huo.4
Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum (MB) akiwa na Mh.Rukia Kassim Ahmed Mbunge wa viti maalum kupitia chama cha wananchi CUF wakitoka kwenye duka ambalo lilikutwa mmiliki wake akifanya biashara bila ya kutoa risiti za mashine ya EFD. (Picha zote na Ramadhani Omary).5
Mh.Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (MB) akijadiliana jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha Bi.Ingiahedi Mduma mara baada ya kufanya ukaguzi wa matumizi ya mashine za EFD katika duka mojawapo Mkoani  Dodoma
.……………………………………….
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum amefanya ukaguzi wa ghafla katika baadhi ya maduka Mkoani Dodoma ili kuona kama maelekezo ya Serikali kuhusu matumizi ya mashine za EFD yanatekelezwa ipasavyo.
Katika ukaguzi huo ambao ulihusisha maduka ya kuuza thamani za majumbani,nguo na maduka ya kuuza bidhaa mchanganyiko (Mini supermarket).
Mh.Waziri akiongozana na Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania aliagiza kufungwa kwa maduka yote ambayo yamekaidi agizo la Serikali la matumizi ya mashine EFD mpaka pale watakaponunua na kuzitumia ipasavyo mashine hizo.
Aidha Mh.Waziri amewataka wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kuisaidia Serikali kuwafichua wafanyabiashara wasio waaminifu na ambao wanapelekea kuikosesha Serikali mapato ambayo yangetumika katika kuboresha huduma za kijamii.

Imetolewa na Msemaji Mkuu,
Wizara ya Fedha
Dodoma

WAZIRI BERNARD MEMBE APATA MAPOKEZI MAKUBWA BUKOBA, AZOA WADHAMINI LUKUKI

0
0
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi waliofurika nje ya Ofisi ya CCM Mkoa wa Kagera mjini Bukoba Juni 20.2015, alipokwenda kwa ajili ya kutafuta wadhamini wa kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 500 mkoani humo.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi waliofurika nje ya Ofisi ya CCM Mkoa wa Kagera mjini Bukoba Juni 20.2015, alipokwenda kwa ajili ya kutafuta wadhamini wa kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 500 mkoani humo.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (mbele mwenye miwani) akiongoza umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba mkoani Kagera Juni 20.2015 na kufanya matembezi kutoka uwanjani hapo hadi katika Ofisi ya CCM Mkoa, alipokwenda kutafuta wadhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 500 mkoani humo. Kushoto kwake Ini Katibu mstaafu wa CCM mkoa Kagera, Faustine Kamaleki.
 Msafara wa bodaboda ukiongozi msafara wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (hayupo pichani) baada ya kuwasili mjini Bukoba mkoani Kagera Juni 20.2015,kwa ajili ya kutafuta wadhamini wa kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 500 mkoani humo. Picha na John Badi
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images