Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

MAHAFALI YA TATU YA SHULE YA AWALI YA CHEKECHEA YA OJAYS KIDDIES ZONE YAFANYIKA LEO JIJINI DAR

$
0
0
 Wahitimu wa shule ya Chekechea ya Ojays Kiddies Zone wakiwa kwenye picha ya pamoja
 Mkurugenzi wa Shule ya Chekechea ya Ojays Kiddies Zone, Bi Usia Nkoma Ledama akizungumza jambo wakati wa mahafali ya tatu ya shule hiyo
 Mwalimu Debby Ndulla(wa kwanza kushoto) akiwatambulisha walimu wa Shule ya Chekechea ya Ojays Kiddies Zone ambao ni Mwalimu Tatu(wa pili kutoka kushoto) akifuatiwa na Mwalimu Revina(katikati), Mwalimu Doroth(wa pili kutoka kulia) pamoja na Mwalimu Aika(kulia).

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

BOHARI YA DAWA (MSD) YASHIRIKI MAONYESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Ofisa Uhusiano wa MSD, Benjamin Massangya (kulia), akimuelekeza jambo mwananchi aliyetembelea banda la MSD katika maonyesho hayo yaliyoyoanza leo na kufikia tamati baada ya wiki moja
Ofisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka (kulia), akimuelekeza jambo Mwanahabari aliyetembelea banda la MSD katika maonyesho hayo. Katikati ni Ofisa Udhibiti Viwango na Ubora wa MSD, Betia Kaema.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

SIKU YA MTOTO WA AFRIKA LEO JUNI 16, 2015 YAFANA BUKOBA IKIBEBA UJUMBE "TOKOMEZA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI - PAMOJA TUNAWEZA"

$
0
0
WADAU na wanaharakati wa maendeleo ya watoto leo wanaungana na jamii ya kimataifa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Afrika kwa kuwahimiza wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kuingiza ajenda ya mtoto katika kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa Juni 16 kila mwaka tangu mwaka 1991 kwa lengo la kuhamasisha jamii kujadili, kutathmini na kuweka mikakati ya kuboresha maisha ya mtoto wa kiafrika kama msingi wa kujenga taifa bora.

Siku ya mtoto wa Afrika ilianzishwa na Jumuiya ya Umoja wa Afrika (OAU) na kuadhimishwa kwa mara ya kwanza Juni 16, 1991 ili kuwahimiza viongozi kujenga utashi wa kisiasa wa kushughulikia matatizo yanayowakabili watoto wa Kiafrika kwa kuweka sheria za kuwalinda pamoja na kuwajengea mazingira bora ya kuishi.

Maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika sanjari na maadhimisho ya miaka 25 ya Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto kwa kutumia kaulimbiu isemayo,” Tuunganishe juhudi zetu kutokomeza ndoa za utotoni Afrika.

Wanaharakati na wadau wa maendeleo na haki za watoto wametumia maadhimisho ya mwaka huu kujadili na kutathmini hotuba za wanasiasa waliojitokeza hivi karibuni kutangaza nia ya kugombea urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kubaini kuwa hakuna mgombea aliyeweka bayana jinsi atakavyotetea haki za watoto.
Wagombea zaidi ya 30 kutoka Chama Cha Mapinduzi ambao wamejitokeza na kuchukua fomu za kugombea nafasi kupeperusha bendera ya CCM katika kinyang’anyiro cha kugombea urais. 

MAKAMU WA RAIS WA ZAMANI WA SUDANI YA KUSINI AMWOMBA JK AENDELEE KUSIMAMIA MAZUNGUMZO YA AMANI KATI YA MAKUNDI YANAYOPINGANA YA NCHI HIYO

JUST IN: Rais Kikwete aongoza maelfu ya Waombolezaji kwenye Mazishi ya Mufti Mkuu wa Tanzania MArehemu Sheikh Issa Shaaban bin Simba Mkoani Shinyanga leo

$
0
0



Jeneza lenye mwili wa Marehemu, Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban bin Simba, likitolewa nyumbani kwake, tayari kwa safari ya kwenda msikitini kuswaliwa na baadae kwenye mazishi, yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Waislam, Nguzo Nane Mkoani Shinyanga.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka ugongo kwenye Kaburi la Marehemu Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban bin Simba, aliezikwa leo Juni 16, 2015 kwenye Makaburi ya Waislam, Nguzo Nane Mkoani Shinyanga.
Masheikh kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini wakimzika Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Issa Shaaban bin Simba, aliezikwa leo Juni 16, 2015 kwenye Makaburi ya Waislam, Nguzo Nane Mkoani Shinyanga.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye akiweka ugongo kwenye Kaburi la Marehemu Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban bin Simba, aliezikwa leo Juni 16, 2015 kwenye Makaburi ya Waislam, Nguzo Nane Mkoani Shinyanga.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiweka ugongo kwenye Kaburi la Marehemu Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban bin Simba, aliezikwa leo Juni 16, 2015 kwenye Makaburi ya Waislam, Nguzo Nane Mkoani Shinyanga.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa Mazishi ya Marehemu, Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban bin Simba, Mbaraka Simba wakati kwenye Makaburi ya Waislam ya Nguzo Nane, Mkoani Shinyanga leo Juni 16, 2015.

KUONA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

MATUKIO MBALIMBLI KATIKA MSIBA WA MUFTI MKUU WA TANZANIA

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akitoa neno kwa umati wa waombolezaji katika msiba wa Mufti mkuu Issa Shaban Bin Simba nyumbani katika Mtaa wa Majengo mjini Shinyanga, baada ya mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Nguzo Nane mjini humo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa aliyekuwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Marehemu Shaaban Issa Bin Simba, Bi Makaje Goso, wakati alipofika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam, leo Juni 16, 2015 kwa ajili ya kuifariji familia hiyo kabla ya kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea nyumbani kwake Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya maziko Katikati ni Mke wa Makamu wa Rais, Mama Zakia Bilal. 
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakia Bilal, akimfariji mke wa aliyekuwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Marehemu Shaaban Issa Bin Simba, Bi Makaje Goso, wakati alipofika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam, leo Juni 16, 2015 kwa ajili ya kuifariji familia hiyo kabla ya kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea nyumbani kwake Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya maziko yanayotarajia kufanyika leo jioni. Kushoto ni Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal

Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akimpa pole Mjane wa Marehemu, Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban bin Simba, nyumbani kwake Majengo, Mkoani Shinyanga leo Juni 16, 2015. Mufti Simba alifariki dunia Juni 15, 2015 kwenye hospitali ya TMJ Mikocheni Jijini Dar es salaam.
Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mh. Fredrick Sumaye



RAIS KIKWETE AWAAPISHA RASMI MAJAJI WATEULE WAWILI WA MAHAKAMA YA RUFANI TANZANIA

$
0
0
Mhe. Augustine Mwarija- Jaji Mteule wa Mahakama ya Rufani,Ikulu jijini Dar es salaam Juni 16, 2015. Kabla ya Uteuzi wake Mhe. Mwarija alikuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu- Divisheni ya Biashara, anayeshuhudia pembeni ni Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania.
Mhe. Augustine Mwarija, Jaji Mteule wa Mahakama ya Rufani akitia sahihi hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa rasmi na Mhe. Rais kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe. Stella Mugasha- Jaji Mteule wa Mahakama ya Rufani, Ikulu jijini Dar es salaam Juni 16, 2015. Kabla ya uteuzi wake Mhe. Jaji Mugasha alikuwa Jaji Mfawidhi Mahakama kuu- Kanda ya Dar es Salaam.
Mhe. Jaji Mugasha akitia sahihi hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa rasmi na Mhe. Rais mapema leo.
Wakiongea na Waandishi wa Habari waheshimiwa Majaji hao wateule wameahidi kufanya kazi kwa bidii na kusaidia katika kuendeleza mapambano ya kumaliza mashauri ya muda mrefu. (Picha na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania).

MTWARA WAJITOKEZA KWA WINGI KUMDHAMNINI DKT. MAGUFULI

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhiwa fomu yenye orodha ya Wadhamini waliojitokeza kumdhamini katika  mbio za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mtwara.


 Mchakato wa udhamini ukiendelea kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Mtwara mjini.

 Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhiwa fomu yenye orodha ya Wadhamini kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara.

 CCM Oyeee…Ndivyo wanachama wa CCM Wilayani Masasi walivyokuwa wakisikika mara baada ya kumdhamini Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli katika Mchakato wa Kuwania nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea wa Urais kupitia CCM.

 Wanachama wa CCM Wilayani Masasi wakimsalimia Dkt. Magufuli


NHIF WASHIRIKI MAONYESHO YA UTUMISHI WA UMMA JIJINI DAR

$
0
0
 Afisa Mtafiti wa shughuli za mfuko wa Taifa wa bima ya Afya, Shani Mussa akitoa maelekezo katika maonyesho ya utumishi wa umma yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya madaktari wakitoa maelezo  kwa wananchi waliojitokeza katika maonyesho ya utumishi wa umma  yaliyofanyika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII)

VYAMA VYA WAONGOZA WATALII NA WAPAGAZI TANZANIA WATOA SIKU 30 KWA SERIKALI KUSHUGHULIKIA MADAI YAO

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha waongoza watalii mkoa wa Kilimanjaro (KGA) Respicius Baitwa akizungumza katika mkutano wa vyama vinayofanya shughuli za Utalii katika hifadhi za taifa juu ya kusudio la kutaka kusitisha kutoa huduma katika hifadhi kutokana na malalamiko yao kutofanyiwa kazi hadi sasa.
Baadhi ya wajumbe walioshiriki mkutano huo uliofanyika katika Hotel ya Uhuru mjini Moshi.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MADAKTARI WA CHINA WAAGA KWA RAIS WA ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Madaktari wa Kichina waliopo Zanzibar waliofika kumuaga Rais baada ya kumaliza muda wao wa kazi katika Hospitali mbali mbali Unguja na Pemba (wa pili kulia) Balozi Mdogo wa China Nchini Tanzania anyefanyia kazi Zanzibar Mhe,Xie Yunliang.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiwa katika mazungumzo na Balozi Mdogo wa China Nchini Tanzania anyefanyia kazi Zanzibar Mhe,Xie Yunliang wakati akiongoza ujumbe wa Madaktari wa Kichina waliopo Zanzibar waliofika kumuaga Rais (hawapo pichani) baada ya kumaliza muda wao wa kazi katika Hospitali mbali mbali Unguja na Pemba,[Picha na Ikulu]

WAZIRI MKUU APATA WADHAMINI 9,141 KATAVI

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapungia wanaCCM waliofika kwenye Ofisi ya CCM ya kata ya Kibaoni kumdhamini katika nia yake ya kuwania uteuzi wa CCM katika kugombea nafasi ya urais Juni 15, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimian na baadhi ya wananchi wa Mpanda waliofika kwenye ofisi ya CCM ya Wilaya ya Mpanda kushuhudia na kumdhamini ilia pate sifa za kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Juni 15, 2015.

BASATA LAWATAKA WASANII KUWA TAYARI KUKOSOLEWA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu 

 Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetoa wito kwa wasanii kuacha tabia ya kulewa umaarufu na kuchukia pale wanapokosolewa kwani kazi yoyote ya Sanaa lazima ikosolewe ili iwe bora na yenye kuvutia. 

 Wito huo umetolewa mapema wiki hii na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Godfrey Lebejo Mngereza wakati akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA linalofanyika kwa mwezi mara mbili siku ya Jumatatu kwenye Ukumbi wa Baraza hilo ulioko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.

 Alisema kuwa wasanii wafurahie wanapokosolewa kwani msanii yeyote duniani lazima atenge muda wa kuiwasilisha kazi yake kwa hadhira kwa ajili ya kusikilizwa au kuangaliwa na hatimaye kukosolewa na kutolewa mawazo ya wadau kabla haijaenda sokoni rasmi. “Kukosolewa kwa msanii ni sehemu ya kazi. 

Wasanii wengine hulipa fedha nyingi kwa ajili ya kukosolewa na kuboreshewa kazi zao. Hapa kwetu wasanii wanakosolewa bure, wanakasirika, wanamwona adui anayewakosoa” aliongeza Lebejo.

 Awali wakiwasilisha mada iliyohusu Umuhimu wa msanii kutumia umaarufu kukuza pato kwa nyakati tofauti kwenye Jukwaa hilo, mbunifu wa mavazi maarufu nchini Asia Idarous and mwanamitindo Jokate Mwegelo kwa pamoja walisisitiza umuhimu wa wasanii kuwa na malengo, bidii, uaminifu na kutengeneza kazi zenye ubora. 

 Jokate alisema kwamba amefika hapo alipo kutokana na kuzingatia uhusiano mwema katika kazi, kujitangaza, kujituma, kujiwekea akiba na kujenga mtandao mzuri wa kikazi na wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi pia kujenga umaarufu mzuri usiyo na maadili mabovu. 

 “Kupata umaarufu si kwa mteremko. Si kila umaarufu ni mzuri. Wasanii lazima wabuni kazi nzuri na zenye maadili ili zionekane na kupendwa. Tusibuni vitu vibaya au sisi wenyewe kujinadi kwa vitu vibaya” alisisitiza Jokate. Alizidi kueleza kwamba hakuna kitu cha muhimu kwa msanii kama uvumilivu , kuepuka makundi yasiyo na tija na zaidi kuwa karibu na watu wenye mafanikio katika kazi zao ili kuiga yale yaliyo bora kwa ajili ya kukuza uchumi na pato.
Msanii na mwanamitindo Jokate Mwegelo (Kushoto) akiongea na wadau wa Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa-BASATA (hawako pichani) mapema wiki hii kwenye ukumbi wa Baraza hilo ulioko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kulia ni Mbunifu wa mavazi maarufu nchini Asia Idarous na Katibu wa Chama cha Waandishi wa habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz), Hassan Bumbuli.
Mbunifu wa mavazi maarufu nchini Asia Idarous (Kulia) akisisitiza jambo mapema wiki hii wakati akiwasilisha mada kwenye Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) katika Ukumbi wa Baraza hilo ulioko Ilala Sharf Shamba jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mwanamitindo Jokate Mwegelo na Katibu wa CAJAtz Hassan Bumbuli.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Lebejo akipiga marimba ya kigogo mapema wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA linalofanyika kila Jumatatu mara mbili kwa mwezi kwenye ukumbi wa Baraza hilo ulioko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia kushoto kwake ni Mwanamitindo Jokate Mwegelo, Katibu wa CAJAtz Hassan Bumbuli na mbunifu mavazi Asia Idaorus.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

DIRA YA DUNIA YA IDHAA YA KISWAHILI YA BBC, LONDON

JOTO LA ASUBUHI LA 93.7 EFM KUANZIA SAA 12 HADI SAA 3 ASUBUHI KILA SIKU


RAIS MSTAAFU MHE. BENJAMIN WILLIAM MKAPA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA BAKWATA KUFUATIA KIFO CHA MUFTI ISSA BIN SHAABAN SIMBA

$
0
0
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa atuma salamu za Rambirambi kwa BAKWATA kufuatia kifo
cha Mufti Issa Bin Shaaban Simba.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin Mkapa, amemtumia Kaimu Mufti wa Tanzania, salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mufti Issa Bin Shaaban Simba kilichotokea Jumatatu katika hospitali ya TMJ.
Katika salamu zake Mhe. Mkapa ameelezea kushtushwa kwake na kifo cha Mufti Simba ambae amemuelea kama kiongozi “aliyekuwa muadilivu, mpenda amani, mwenye busara na mbobevu mkubwa wa masuala yanayohusu dini ya kiislamu”. Kwenye salaamu zake Mhe, Mkapa amemuelezea Marehemu Mufti Simba kuwa alikuwa “kiungo muhimu sio tu kwa waislamu bali hata kwa serikali na jumuiya za dini mbali mbali”.
Ametoa pole zake kwa BAKWATA, familia ya Marehemu Mufti Simba, waislamu wote na watanzania kwa ujumla kwa msiba huu; na amewaombea kwa mungu “awape subira, imani na busara kwenye kipindi hiki kizito”. Aidha, amewaombea BAKWATA mungu awape “busara na hekima zaidi za kuweza kuendelea kuijenga taasisi hiyo kama ambavyo Marehemu Mufti Simba alifanya ili iendelee kuwa nguzo muhimu ya amani na utulivu nchini mwetu” hasa katika kipindi hiki ambapo nchi inapita katika  mitihani kadhaa.
Inna lillahi wa Inna Ilayhi Rajiuun
Imetolewa na:
Ofisi ya Rais Mstaafu,
Mhe. Benjamin William Mkapa.

WAZAZI WAMEASWA KUWAPOKEA VIJANA WAO WALIOAMUA KUACHA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
 Na mwandishi wetu.
Wazazi wameaswa kuwa tayari kuwapokea Vijana au watoto wao walioamua kuacha matumizi ya dawa za kulevya ili kuwalinda na vishawishi vinavyoweza kutoa nafasi ya kuwarejesha tena kwenye matumizi ya Dawa hizo pamoja pombe haramu.

Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi ametoa wosia huo wakati wa kuwapokea Vijana Sita wa Kijiji cha Fujoni walioamua kuacha kutumia Dawa za kulevya na kupata mafunzo watakayoyatumia kuwasomesha wenzao kuachana na Dawa hizo hapo katika Skuli ya Fujoni Wilaya ya Kaskazini “ B “.

Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema wapo Wazazi na Familia  Nchini ambao bado wanaendelea  na tabia ya kuwatenga Vijana wao walioathirika na Dawa za kulevya kwa kuchelea kufanyiwa matendo ya maudhi kama wizi.

Alisema tabia hiyo inafaa kuachwa kwa vile kama haikutafutiwa ufumbuzi  inaweza kuzalisha zaidi Vijana wanaotumbukia katika matumizi ya Dawa za kulevya na hatimae kuwa na kundi kubwa la  walevi ndani ya Jamii ambao ni nguvu kazi ya Taifa.

Balozi Seif alionyesha furaha yake kutokana na ujasiri  mkubwa ulioonyeshwa na vijana hao wa kuamuwa kuacha matumizi ya Dawa za kulevya na kujitolea kuwa mfano kwa wenzao wenye tabia hiyo.

Wakati huo huo Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope Balozi Seif ameukabidhi Uongozi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } shilingi Milioni 5,000,000/-  kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kibanda cha Maji katika Kijiji cha Kinduni. 

Ujenzi wa Kibanda hicho una lengo la kuimarisha miundo mbinu ya upatikanaji wa huduma za Maji safi na Salama ndani ya Kijiji hicho chenye changamaoto ya upatikanaji wa huduma hiyo muhimu.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

 Mbunge wa Jimbo la Kitope ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisalimiana na mmoja kati ya Vijana sita walioamua kuachana na matumizi ya Dawa za Kulevya katika Kijiji cha Fujano hapo katika Viunga vya vya Skuli ya Fujoni. Kati kati yao ni Mwakilishi wa Umoja wa kusaidia mapambano dhidi ya matumizi ya Dawa za kulevya na Pombe Tanzania Bwana  Abdulrahman Mohammed Abdulla.
  Mwakilishi wa Umoja wa kusaidia mapambano dhidi ya matumizi ya Dawa za kulevya na Pombe Tanzania Bwana  Abdulrahman Mohammed Abdulla akielezea mikakati ya taasisi yake katika mapambano dhidi ya Dawa za kulevya hapa Nchini.
Balozi Seif akizungumza na baadhi ya Wananchi mara ya kukabidhiwa Vijana Sita walioamua kuachana na matumizi ya Dawa za kulevya waliokuwa wakipata mafunzo kwenye Kituo cha Mombasa nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Sheha wa Shehia ya Fujoni Bwana Said Mgeni Bakari na wa kwanza kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kaskazini “ B “ Nd. Hilika Khamis na Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kitope Mama Asha Suleiman Iddi.
Kijana Ayoub Hussein Ayoub Mmoja kati ya Vijana sita walioamua mkuachana na matumizi ya Dawa za kulevya akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake kuushukuru uongozi wa Jimbo la Kitope kwa kusaidia mbinu na uwezeshaji uliowachangia wao kuacha dawa hizo.
Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi shilingi Milioni 5,000,000/- Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } Dr. Mustafa Gharu hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kwa ajili ya uendelezaji wa ujenzi wa kibanda cha maji katika kijiji cha Kinduni.

WIZARA YA HABARI YAKAMILISHA UBORESHAJI TOVUTI YA WANANCHI, SASA IKO HEWANI

$
0
0

WIZARA ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Idara ya Habari- MAELEZO, imekamilisha kazi ya kuboresha Tovuti ya Wananchi na sasa iko hewani.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Wizara hiyo, Mkurugenzi wa MAELEZO Assah Mwambene,(Pichani) aliwataka wananchi kuitumia tovuti hiyo kupitia anuani ya www.wananchi.go.tz kuwasilisha hoja zao Serikalini ili ziweze kupatiwa majibu .
“Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Idara ya Habari- MAELEZO, imekamilisha kufanya  maboresho ya tovuti ijulikanayo kwa jina la Tovuti ya Wananchi” alisema Mwambene na kuongeza:
“Lengo letu sasa ni kutaka wananchi badala ya kuhangaika sana, akiwa sehemu yoyote ya nchi hii anaweza kuuliza swali kupitia mtandao wa intaneti kwa anuani ya www.wananchi.go.tz
Alisema mwananchi akiingia kwenye tovuti hiyo atakutana na sehemu ya kuweka hoja yake kuuliza swali, kutoa maoni, kutoa pongezi, kuwasilisha malalamiko yake na moja kwa moja yatapokelewa na MAELEZO na kufanyiwa kazi. 
“Mwananchi anaweza kuandika swali moja kwa moja kwenye taasisi anayotaka swali lile liende, kwa mfano kama anataka swali lile liende Wizara ya Ardhi anaweza akaandika” alisema Mwambene na kuongeza:
“Sisi tutapata taarifa kwamba ameleta swali na tutalipeleka kwenye taasisi husika na tutaangalia na kuona je swali hilo limejibiwa ama halijajibiwa”.
Mwambene alifafanua kuwa kila siku MAELEZO itajua ni wizara gani ama taasisi gani ya Serikali imepelekewa swali gani na swali hilo limejibiwa au la.
Alisema tovuti hiyo ni chombo muhimu katika mabadiliko ya sayansi na teknolojia na itamfanya mwananchi asilazimike kutembea kutoka kwenda wizara moja hadi nyingne ama taasisi ya Serikali kushughulikia malalamiko yake.
Alitoa mfano kuwa hata mwananchi akitaka kujua jinsi ya kupata viza au huduma nyingine inayotolewa na Serikali ataweza kupatiwa majibu ndani ya muda mfupi sana kupitia tovuti hiyo ya Wananchi.
“Baadaye kuna jambo lingine ambalo bado tunalifanyia tathimini, ni suala la kwamba wanaanchi wanaweza kutumia simu zao za mkononi kutuma maswali na kupokea majibu” alisema Mwambene.
Alibainisha kuwa tathimini hiyo ikikamilika hivi karibuni, watatoa namba ambayo mwananchi anaweza kutumia ujumbe mfupi wa simu ya mokononi kutuma hoja yake Serikalini na kupatiwa majibu kupitia njia hiyo.
“Ni tovuti ambayo tunapenda wananchi waitumie ili kupunguza gharama na muda mwingi sana kwa mfano mtu kusafiri, kupanda gari kwenda wizarani au taasisi ya umma kufuatilia shida yake.Hivyo anaweza kutumia simu yake ya mkononi” alisema Mwambene na kuongeza:
“Lengo letu ni kwamba wananchi waone kama hiyo ni fursa muhimu ya mawasiliano na waone kuwa sasa hivi wanaweza kutuandikia ujumbe kuuliza swali au malalamiko na yatatufikia na kufanyiwa kazi”.
Mwambene alisema Wizara imejipanga vya kutosha kuhakikisha kwamba Serikali inawasiliana na wananchi wake kwa kusikiliza shida zao na kuzipatia majibu.
“Hii ni Serikali ya wananchi na lazima tuwasiliane na wananchi kwa njia yoyote ambayo ni rahisi kuwafikia na Serikali imeona hii ni njia rahisi zaidi kuwafikia kupitia mtandao huu wa Tovuti ya Wananchi” alisema.
Tovuti ya Wananchi imewahi kufanya kazi katika miaka iliyopita na baadaye ilisimama lakini  sasa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imeifanyia marekebisho makubwa na iko hewani.

RAIS - ZIARA YA INDIA

$
0
0
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone:255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’ SOFFICE,
    STATE HOUSE,
           1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete yuko njiani kwenda India ambako atafanya ziara rasmi ya Kiserikali ya siku nne katika Jamhuri ya India kwa mwaliko wa Rais wa India, Mheshimiwa Pranab Mukherjee. Ziara hiyo, inaanza rasmi jioni ya leo, Jumatano, Juni 17, 2015.
Wakati wa ziara yake, Rais Kikwete ambaye anafuatana na Mama Salma Kikwete, mbali na kukutana na Rais Mukherjee kwa mazungumzo rasmi ya Kiserikali, atakutana kwa mazungumzo na Makamu wa Rais, Mheshimiwa Mohammad Hamid Ansari na Waziri Mkuu Narendra Damordadas Modi, ambaye aliingia madarakani rasmi Mei 26, mwaka jana, 2014 akiwa Waziri wa 15 wa Jamhuri ya India baada ya chama chake cha Bharatiya Janata Party (BJP) kushinda uchaguzi mkuu.
Ziara hii itakuwa ya pili kwa Rais Kikwete kutembelea India katika miaka 10 ya uongozi wake. Mwaka 2008, Rais Kikwete, akiwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), alitembelea India ambako alikuwa Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Afrika na India (India-Africa Forum) uliofanyika mjini New Delhi, mji mkuu wa India pamoja na Waziri Mkuu wa India wakati huo, Mheshimiwa Manmohan Singh.
Wakati wa ziara yake, Rais Kikwete atatembelea miji ya New Delhi na Jaypur (Pink City of India) na miongoni mwa shughuli zake ni kukutana na Watanzania ambao wanaishi India, kukutana na wafanyabiashara wakubwa wa India wenye kutaka kuwekeza Tanzania na na kufungua Mkutano wa Kwanza wa Wafanyabiashara wa Tanzania na India (1st Indian-Tanzania Business Forum).
Mbali na wafanyabiashara, kiasi cha wanafunzi 2,500 wa Kitanzania wanasoma katika vyuo vikuu vya India kwa ufadhili wa Serikali za Tanzania na India. Hawa ni mbali na maelfu ya wanafunzi ambao wanajisomesha wenyewe katika vyuo vikuu vya nchi hiyo.
Rais pia atakutana kwa mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la India, Air India, kwa nia ya kulishawishi shirika hilo kuanzisha tena safari za ndege kati ya nchi hizo mbili, atakutana na Mtendaji Mkuu wa Benki ya ICICI, benki kubwa binafsi kuliko zote katika India, ambayo inataka kuingia ubia na Benki ya Posta Tanzania, atakutana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Infrastructure Leasing and Financial Services ambayo inataka kujenga barabara ya kisasa kabisa kati ya Dar es Salaam na Chalinze na miradi mikubwa ya maji.
Aidha, Rais Kikwete atakutana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Kundi la Makampuni ya Hospitali za Apollo ambayo inataka kujenga hospitali kubwa na ya kisasa Kigamboni, Dar Es Salaam.
Rais Kikwete pia atatembelea kiwanda cha kutengeneza matrekta cha Fiat New Holland ambacho kimekuwa kinashirikiana kwa karibu na Kampuni ya Biashara ya Jeshi la Kujenga Taifa ya SUMA JKT na baadaye kutembelea Shirika la Taifa la Viwanda Vidogo la India.
Rais Kikwete ataungana na Waziri Mkuu Modi kushuhudia utiaji saini wa mikataba minne kati ya Tanzania na India katika maeneo ya utalii, maji na miundombinu.
Ziara ya Rais Kikwete katika India inatoa nafasi ya kuimarisha uhusiano wa kihistoria, wa karibu na wa kirafiki ambao una historia ndefu na ya karne nyingi  na ambao uliimarishwa zaidi na uhusiano rasmi ambao ulianzishwa miaka 54 iliyopita. Kimsingi uhusiano huo umejengwa katika misingi ya biashara na mahusiano ya watu kwa watu.
India ndiyo nchi inayofanya biashara kubwa zaidi duniani na Tanzania. Mwaka 2013-14, biashara hiyo ilikadiriwa kufikia dola za Marekani bilioni nne. Mbali na uhusiano wa biashara, Watanzania wengi wamekuwa wanasaka huduma za afya na elimu katika India. Inakadiriwa kuwa tokea mwaka 1999 kiasi cha Watanzania 4,100 wamepata huduma za afya katika hospitali za Apollo pekee.
Inakadiriwa kuwa kuna wananchi kati ya 50,000 na 60,000 wenye asili ya India (PIO’s) ambao wanaishi na kufanya kazi katika Tanzania.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
17 Juni, 2015.

BENKI YA NBC YASHINDA TUZO YA SUPERBRAND AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Edward Marks (kulia) akipokea tuzo ya ubora ya Superbrand ya Afrika Mashariki  kutoka kwa Mkurugenzi Mradi wa Taasisi ya Superbrands Ukanda wa Afrika, Jawad Jaffer katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Rukia Mtingwa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Edward Marks akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Edward Marks (wa pili  kulia) wakiwa na baadhi ya washindi wengine wa tuzo za Superbrands katika hafla hiyo.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images