Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 871 | 872 | (Page 873) | 874 | 875 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Ikungi, Bwana Muhammad Nkya akiongea na wataalamu waelekezi wa masuala ya mazingira na jinsia, kutoka kampuni ya CH2M HILL ya Marekani Bi. Cinamon Vann na Bwana Piercarlo Smith (kushoto) walipokuwa mkoani Singida kwa ajili ya upembuzi yakinifu wa miradi ya umeme inayotarajiwa kufadhiliwa na shirika la changamoto za millennia (MCC), makubaliano ya ufadhili wa utekelezaji wa miradi hiyo kwa Tanzania yanatarajiwa kufanyika mwezi Septemba 2015.
  Mshauri mwelekezi wa masuala ya jinsia ,kutoka kampuni ya CH2M HILL ya Marekani, Bi. Cinamon Vann (wa pili kulia waliosimama), akiongea na wanawake wa jamii ya kihadzabe na kimang'ati katika kijiji cha kipamba wilaya ya Mkalama mkoani Singida walikokwenda kukusanya taarifa mbalimbali kwa ajili ya upembuzi yakinifu wa miradi ya umeme inayotarajiwa kufadhiliwa na Shirika la Changamoto za Millenia (MCC). Makubaliano ya ufadhili wa utekelezaji wa miradi hiyo awamu ya pili kwa Tanzania yanatarajiwa kufanyika mwezi Septemba 2015.
  Mshauri mwelekezi wa masuala ya jamii na mazingira ,kutoka kampuni ya CH2M HILL ya Marekani, Bw. Piercarlo Smith (wa pili kushoto), akiongea na baadhi ya wadau wa mazingira wa halmashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida walikokwenda kukusanya taarifa mbalimbali kwa ajili ya upembuzi yakinifu wa miradi ya umeme inayotarajiwa kufadhiliwa na Shirika la Changamoto za Millenia (MCC). Makubaliano ya ufadhili wa utekelezaji wa awamu ya pili wa miradi hiyo kwa Taanzania yanatarajiwa kufanyika mwezi Septemba 2015.

  0 0

  Christian Bella akijimwaga jukwaani.
  Masaa machache baada ya kukosa kitatanishi tunzo ya wimbo bora wa mwaka katika Kili Music Awards Christian Bela (King of melodies) alipagawisha wapenzi wa muziki mjini Tabora alipoporomosha bonge la show akiwa na kundi zima la Malaika Band. Christian Bela alitarajiwa na  wadau wa muziki nchini kuwa angebeba tunzo hiyo bila ushindani mkubwa kutokana na wimbo wake wa Nani kama mama ambao aliomshirikisha Ommy Dimpoz kutamba sana katika vituo vyote vya redio na Runinga hapa nchini, lakini kama kawaida ya tunzo hizo zinazosimamiwa na BASATA na kudhaminiwa na kampuni ya utengenezaji bia ya Tanzania TBL zimekuwa zikilalamikiwa kila mwaka huku waanadaaji wakioneka kuweka pamba mbichi masikioni. Tunzo hiyo ya wimbo bora wa mwaka ilienda kwa wimbo wa Mwana wa msanii Ali Kiba. Onesho hilo lilifanyika katika viwanja vya Bwalo la Polisi Tabora.
  Bella akifanya yake jukwaani.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mwanahabari Mkongwe hapa nchini, Aboubakary Liongo (shoto) akiwa pamoja na Beki kisiki wa zamani aliyewahi kuzicheza na kutamba sana katika timu za Balimi na RTC Kagera, Hussein Kaitaba wakati walipokutana leo.

  0 0

  Baadhi ya wananchi wakiangalia ramani katika mradi wa viwanja unaoendeshwa na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, katika eneo la Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani mwishoni mwa wiki na kusimamiwa na Meneja Mauzo wa Taasisi hiyo Nasra Sudi. Picha zote na Mpigapicha Wetu.
  Wananchi waliokwenda kuonyeshwa viwanja hivyo wakipata somo la mradi huo wa vianja vya Vikuruti unaoendeshwa na Taasisi ya Bayport Financial Services.


  0 0

  Karibu kutazama ripoti hii fupi kuhusu matembezi ya SUSAN G. KOMEN RACE FOR THE CURE mwaka 2015 hapa Washington DC


  0 0


  Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, Akifurahia mara baada ya kutua Bukoba na tayari kuwahutubia wakazi wa mji wa Bukoba leo wakati wa mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mashujaa/Uhuru Platform Bukoba leo Jumatatu tarehe 15 june, 2015. Kiongozi huyu ambaye amefuatana na viongozi wenzake wa juu wa chama hicho, yuko kwenye ziara ya kukitangaza chama na sera mpya ya azimio la arusha lenye usasa. 

  Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akiongea na wakazi wa Mji wa Bukoba leo Jioni jumatatu ya juni 15, 2015. 
  Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Anna Mghira, akiwahutubia wakazi wa mji wa Bukoba leo wakati wa mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Uhuru Platform leo Jumatatu juni 15, 2015.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaji Aliko Dangote, akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia alipowasili kwenye uwanja wa Ndege mjini Mtwara jana kwa ajili ya kutembelea kiwanda chake cha Cementi kilichoko Msijute, mkoani Mtwara.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Hawa Ghasia akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaji Aliko Dangote, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara leo kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha Cementi cha Dangote. Katikati ni Balozi wa Nigeria Nchini Tanzania, Ishaya Manjanbu.
   Mkurugenzi wa Makampuni ya Dangote, Alhaj Aliko Dangote (kulia), akijadiliana jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, walipokutana mjini Mtwara jana kuangalia uwezekano wa kujenga kituo cha kusafirisha saruji katika eneo la Bandari ya Mtwara.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaji Aliko Dangote, akizungumza na waandishi wa habari baada kuwasili mjini Mtwara jana na kutembelea kiwanda chake cha Cementi, kilichoko Msijute, mkoani Mtwara.
   

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndg Kinana akisisitiza jambo mbele ya Wananchi (hawapo pichani),kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika viwanja vya stendi ya mabasi mjini humo.
  Umati wa wakazi wa Chato mjini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia kwenye uwanja wa stendi ya Zamani.Katibu Mkuu wa CCM aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali inabidi ifute kodi kandamizi zinazowazuia wananchi kurahisisha maisha yao.
   Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati akihutubia wakazi wa Chato mjini ikiwa siku ya kwanza ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mkoani Geita.

   Umati wa wakazi wa Chato mjini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu  Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia kwenye uwanja wa stendi ya Zamani.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na  Mkuu wa wilaya ya Chato Ndugu Rodrick Mpogole, viongozi wa CCM wilaya ya Chato pamoja na mafundi wa Tanesco akishiriki kutandaza waya za umeme katika mradi wa umeme vijijini REA katika kijiji cha Mkungo,wilayani Chato mkoani Geita.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi mara baada ya kuwasha mtambo wa maji uliojengwa Chato Mlimani kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji utakaohudumia wakazi wa mji huo leo, wakati wa ziara yake katika mkoa wa Geita .

  Kinana anaendelea na ziara hiyo ya kikazi mkoani humo baada ya kumaliza ziara kama hiyo mkoani Kagera jana, Kinana anaendelea  na ziara hiyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza uhai wa chama, kukosoa na kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili wananchi kwa maisha na maendeleo yao kwa ujumla akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa nyumba ya daktari katika kijiji cha Ihanga wilayani Chato.

  PICHA NA MICHUZI JR-CHATO


  0 0

  Kutoka kushoto juu ni Raymond Nyamwihula, Zainab Chondo, Rehema Salim, Nurdin Suleiman, Fatma Almasi Nyangasa, Baruan Muhuza, Ivone Kamuntu na baba lao Charles Hilary Nkwa'anga. Katika kunogesha usomaji wa habari sasa Azam TV inakuwa na watangazaji wawili wawili kila kipindi...

  0 0


  0 0


  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA, Bi. Marion Moore (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya bidhaa mpya ya mkopo maarufu kama ‘Executive Loan’, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Pamoja naye, kushoto ni Meneja Mauzo Kanda Bw. Haule Stephen na Mshauri Mkuu wa masoko Bw. Andrew Omusambayi.

  TAASISI ya kifedha, Faidika imezindua bidhaa mpya ya mkopo maarufu kama ‘Executive’ inayolenga kuwezesha upatikanaji rahisi wa mkopo usiokuwa na dhamana kwa wafanyakazi wa serikalini wa mpaka shilingi milioni 30. 

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Afisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA, Bi. Marion Moore alisema mkopo huo mpya ni moja kati ya bidhaa ya kipekee nchini yenye lengo la kurahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wafanyakazi toka serikalini.

  “Bidhaa yetu ya mkopo wa Executive, ni bidhaa itolewayo haraka, yenye ubunifu na rahisi katika upatikanaji wake na ya kipekee katika soko la Tanzania. Ni mkopo ambao utawawezesha wafanyakazi wengi toka serikalini kupata fedha na kuweza kuinua viwango vyao vya maisha kwa kujihusisha na miradi mikubwa mbali mbali.   Viwango vya mikopo hii ni kuanzia shilingi milioni kumi mpaka thelathini ambapo marejesho yake yananzia miezi sita mpaka miezi sitini,” alisema Moore. 

  “Bidhaa ya mkopo ya ‘Executive’ ni bidhaa ya kipekee kwa soko la Tanzania, kutokana na kwamba mteja atakiwi kutoa dhamana yoyote ili kupatiwa mkopo. Inachukua masaa 48 tu kwa mteja kupatiwa fedha za mkopo,” aliongeza.

  Naye Meneja Masoko wa Kanda wa FAIDIKA, Bw. Haule Stephen alisema kuwa muombaji anatakiwa kutoa stakabadhi mbili za mishahara ya miezi miwili iliyopita, taarifa ya kibenki ya akaunti kuanzia miezi miwili na kuendelea, Kitambulisho cha kazi na picha moja ya pasipoti, ili kujipatia mkopo huo. Na kuongeza kuwa viwango vya mikopo ya FAIDIKA vimekua kutoka kuanzia shilingi milioni kumi na kufikia shilingi milioni ishirini.  

  “Dhumuni letu ni kuona viwango vya maisha vya watanzania vinakua kupitia upatikanaji rahisi wa huduma za kifedha,” alisema Bw. Stephen. 

  0 0

   Makamu wa Rais,Dk.Mohamed Gharib Bilal akiwasili katika Msikiti wa Kinondoni  kwa ajili ya ibada  kuswalia mwili wa aliyekuwa Mufti Alhaj  Sheikh Shaaban Issa Bin Simba iliyofanyika katika Msikiti wa Kinondoni leo jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya waislaam wakiwa katika msikiti wa kinondoni katika ibada ya kuswalia mwili wa aliyekuwa Mufti Alhaj  Sheikh Shaaban Issa Bin Simba iliyofanyika katika Msikiti wa Kinondoni leo jijini Dar es Salaam.
   Sehemu ya waombolezaji katika msiba wa aliyekuwa Mufti Alhaj  Sheikh Shaaban Issa Bin Simba wakiwa katika majonzi  katika ofisi ya Makao Makuu ya Bakwata,Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.
   Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,Freeman Mbowe akimpa pole Mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu kufuatia na msiba aliyekuwa Mufti Alhaj  Sheikh Shaaban Issa Bin Simba katika msikiti wa Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.
  (PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.)  0 0

   Reminder: 8pm @ Paparazzi club (Slipway) 17th June. Tickets are still available today and tomorrow at the venue. Spread the word! #TWAJIACHIA


  0 0

  Mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Lydia Bukumbi akiaga mwili wa Robert Tillya.
  Mwandishi wa Global Publishers, Mayasa Mariwata akiuaga mwili wa mfanyakazi mwenzake kwa simanzi.
  Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (wa kwanza kulia), Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global, Oscar Ndauka (wa tatu kulia) na Ofisa Utawala wa Global, Soud Kivea (wa pili kushoto) wakiwa na simanzi wakati wa zoezi la kuaga mwili wa Robert Tillya.
  Elvan Stambuli akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Global Publishers Ltd. Kwa picha zaidi na habari kamili BOFYA HAPA

  0 0

  Mkuu  wa wilaya ya  Mufindi mkoani Iringa Bi Mboni Mhita  kushoto  akiwa na wajumbe wa kamati ya  ulinzi na usalama wilaya hiyo ya  Mufindi  katika  kuwatembelea wagonjwa katika Hospitali ya  wilaya ya  Mufindi
  Baadhi ya  ndugu  wakichukua mwili wa ndugu  yao baada ya  kuutambua

  Mkuu  wa wilaya ya  Mufindi Bi Mboni Mhita (kushoto)  akimfariji  mmoja kati ya  majeruhi wa ajali ya  basi la Another G na lori  iliyoua 23 na kujeruhi 34 jana  ,wengine pichani ni wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya  Mufindi. Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wea Monduli, Mh. Edward Lowassa, akitoa hotuba ya shukrani kwenye makao makuu ya CCM mkoa wa Sin gida, baada ya kupata wadhamini kufuatia kucvhukua fomu za kuomba kuteuliwa na chama hicho kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa, ameweka rekodi mpya baada ya kupata wadhamini 22, 758. Tangu aanze kutafuta wadhamini mapema mwezi huu
   Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia  wana CCM na wakazi wa Manispaa ya Singida, waklati akiondoka makao makuu ya CCM mkoani Singida, Juni 16, 2015, baada ya kupata wadhamini.
   Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akiwapungia mkono wana CCM na wakazi wa Manispaa ya Singida, waklati akiondoka makao makuu ya CCM mkoani Singida, Juni 16, 2015, baada ya kupata wadhamini.Picha na K-VISD MEDIA

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0


  Baadhi ya Wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Water Front wakitoa misaada katika kituo cha kulelea watoto wa chini ya miaka minne(4) yatima katika kituo cha Msimbazi Chidrens Home kilichopo Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam leo.

  Crediti manaja wa Benki ya CRDB, tawi la Water front, Isaya Lyimo akimpa maelekezo Sista wa kituo cha watoto yatima cha Msimbazi Chidrens Home kilichopo Msimbazi Centre, Sista Anna Marandu mara baada ya wafanykazi wa tawi hilo kutoa msaada wa vitu mbalimbali jijini Dar es Salaam leo. kulia ni Meneja wa Tawi la Water Front Donath Shirima
  0 0

  Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli (shoto) akizungumza jambo na Washindi wa Promosheni za Kilimanjaro kutoka mikoani walikuja Dar kula Bata wakati wa hafla ya Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2015, Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  Washindi wa Promosheni za Kilimanjaro kutoka mikoani walikula Bata jijini Dar es Salaam kushuhudia Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2015, Mlimani City jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na Mwandishi wetu

  Vijana wameridhishwa na mswada uliopitishwa bungeni wa kuanzishwa baraza la vijana la Taifa na kudai kuwa hiyo ndio njia mojawapo vijana wanaweza kuendeleza shughuli zao za maendeleo .

  Wamedai kuwa katika mswada huo vijana wanangazi zao za uongozi kutoka vijijini hadi kitaifa na hali hiyo inakuwa ni rahisi vijana kuwa na uwezo wa kuelezea changamoto zinazowakabili .

  Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na shirika la Restless Development Tanzania – ICS) linalojishughulisha na kuwaweka vijana kuwa mstari wa mbele katika kufikia maendeleo mara baada ya kumalizika kwa sherehe ya kutoa vyeti kwa vijana wakujitoea ambao wanasoma katika vyuo vikuu .

  Mkurugenzi wa ICS bibi Margareth Mriwa alisema wamefurahishwa na mswada wa baraza la vijana kupitishwa bungeni na kudai kuwa wanaamini kwamba katika muswada huo kuna mikakati inayofaa kabisa ya kuwaelekeza vijana kufikia maendeleo .
  ‘’ Kwasasa hivi waliowengi nchini Tanzania ni vijana na wanauwezo wa kuchangia maendeleo na tunaomba wapewe fursa hiyo katika ngazi mbali mbali za maendeleo . Jambo la kwanza ni kwamba vijana wamejitenga kidogo katika jamii zao na hawapati nafasi wanazopenda kuchaguliwa ‘’ alisema bibi Margareth .


older | 1 | .... | 871 | 872 | (Page 873) | 874 | 875 | .... | 3270 | newer