Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109592 articles
Browse latest View live

LIVE: FATILIA HAPA USIKU WA TUZO ZA KTMA


MAMA MONICA MWAMNYANGE AZINDUA BARAZA LA USHAURI TCAA

0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Mama Monica Mwamyange akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Ushauri wa Watumiaji wa Huduma ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA-CCC) na semina ya wadau wa usafiri wa anga Dar es Salaam leo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Mama Monica Mwamyange akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Baraza  la Ushauri wa Watumiaji wa Huduma ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA-CCC), Shaban Mtambalike wakati wa uzinduzi wa baraza hilo la nne tangu kuanzishwa kwake.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri wa Watumiaji wa Huduma ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA-CCC), Hamza Johari akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi huo. 
 Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu-Wizara ya Uchukuzi, Monica Mwamnyange (walioketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza hilo na wadau wa Sekta ya usafiri wa Anga.

Na Father Kidevu Blog
USHINDANI mdogo katika utoaji wa huduma za usafiri wa anga kutokana na kuwepo kwa mashirika machache ya ndege yanayotoa huduma nchini.
Hayo yalibainishwa Dar es Salaam na  Katibu Mtendaji wa baraza la Ushauri wa Watumiaji wa Huduma ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA-CCC), Hamza Johari wakati wa uzinduzi wa baraza hilo na semina kwa wadau wa usafiri wa anga nchini.
Johari alisema endapo kama nchini kungekuwa na watoa huduma wengi wa usafiri wa anga basi kungepelekea kushuka kwa gharama za usafiri na kuwepo kwa huduma bora miongoni mwao.
“Siku zote tunaamiani kama ushindani wa kutosha gharama zinakwenda chini, huduma zinakuwa bora, na ni mdogo kwasababu soko na miundominu haijaweza kutandaa nchi nzima, ”alisema Johari.
Aidha Johari alisema pindi nchi itakapokuwa na miundombinu bora ya viwanja vya ndege, na utaratibu mzuri wa huduma za anga nchini anaamini huduma zitaboreka zaidi.
Mapema akifungua baraza hilo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Monica Mwamunyange amewataka kuwa karibu na wadau wa sekta ya usafiri wa anga nchini ili kuweza kutoa huduma bora na zenye ufanisi nchini.
Mwamunyange alisemwa ipo haja ya baraza kulifanyia kazi dhana ya ushirikishwaji na utoaji wa elimu kwa walaji kuwa ya vitendo zaidi.
“ Baraza linatakiwa kuwashirikisha wadau wake katika mambo mbalimbali yanayoendelea katika seklta nzima ya usafiri wa anga lakini pia wanapaswa kutoa elimu ya mara kwa mara ya haki na wajibu wa mlaji,”alisema Mwamunyange.
Baraza lina takiwa kuangalia maslahi ya mtumiaji wa huduma za usafiri wa anga na kutoa elimu ambayo itamfanya mlaji awe na uwelewa wa kutosha wa huduma za anga.
Aidha Mwamunyange amesema kwa sasa huduma za usafiri wa anga nchini zinakabiliwa na changamoto kutoka kwa walaji ambapo wanashindwa kutofautisha huduma zitolewazo na mashirika yatuayo huduma za gharama nafuu nay ale yaliyozoeleka.
Wadau wa usafiri wa anga pia walipata fursa ya kushiriki semina baada ya uzinduzi huo na mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwa ni pamoja na huduma kwa wateja, uwajibikaji wa mtoa huduma anaposababisha madhara, ndege za bei nafuu na masuala ya usalama.
Uzinduzi wa baraza hilo la nne la Ushauri wa Watumiaji wa Huduma ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA-CCC), baada ya kuteuliwa na Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta ambapo pia wajumbe wa Baraza lililopita waliagwa.

biashara matangazo...Design Mpya ya Tshirts za Kitaa wear zapatikana sasa

0
0
Design Mpya ya Tshirts Bei 25,000/= per peace 
Designer ; Mike Mwakatundu 
Shop ; Kitaa Wear 
Kwa Mawasiliano Email; mwakatundu.m@gmail.com 
+255 754 310 202 +255 713 292 212 
 NB Unaletewa mpaka Nyumbani/Ofisini 
 Kama upo interested na bidhaa nyingine zaidi hizo hapo chini tembelea blog yetu www.dukaletu.blogspot.com 
 Ili kuwajua watengenezaji waagizaji wa bidhaa mbalimbali, mahoteli, usafiri , address sahihi za watu mbalimbali maarufu hapa nchini tembelea blog yetu www.tanzaniasocialmedia.blogspot.com





DK. MALECELA ASAKA WADHAMINI KATIKA KUGOMBEA NAFASI YA URAIS

0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti Magonjwa ya Binadamu Dk. Mwale Malecela  pichani kabla ya kuingia  katika chumba cha habari katika Redio ya Mwambao iliyopo Tanga eneo la Kange ndani ya Kiwanda cha Tanga Fresh ambaye ni mtoto wa Makamu wa zamani wa Chama cha Mapinduzi (CCM)  John Malecela ni miongoni mwa wana CCM ambao wamejitosa kugombea urais kupitia CCM. Dk. Mwale katika maisha yake mengi kwa zaidi ya miaka20 amekua mtumishu katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)  ambako alianza kazi akiwa kijana na akapanda hadi kuwa mtafiti mkuu na baadaye akateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu, licha ya kukulia katika familia ya mwanasiasa. 
 Dk. Mwale Malecela akizungumza na wananchi kupitia kituo cha Mwambao Radio.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

RAIS KIKWETE AWASILI AFRIKA KUSINI KUHUDHURIA MKUTANO WA 25 WA UMOJA WA AFRIKA

0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na mkewe mama Salma Kikwete wakilakiwa mara walipowasili katika hoteli ya Sun Internatioal Maslow Hotel, Sandton, Johannesburg, Afrika ya Kusini kwa Mkutano wa 25 wa kawaidavwa Umojanwa Afrika.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na mkewe mama Salma Kikwete wakilakiwa na Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe. Sophia Simba mara walipowasili katika hoteli ya Sun Internatioal Maslow Hotel, Sandton, Johannesburg, Afrika ya Kusini kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 25 wa kawaidavwa Umojanwa Afrika.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na mkewe mama Salma Kikwete wakilakiwa na maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini mara walipowasili katika hoteli ya Sun Internatioal Maslow Hotel, Sandton, Johannesburg, Afrika ya Kusini kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 25 wa kawaidavwa Umojanwa Afrika. PICHA NA IKULU

MSIBA NEW YORK NA TANZANIA.

0
0
MAREHEMU MZEE ALFRED MAGEGE.


Jumuiya ya Watanzania New York,New Jersey,Connecticut na Pennsylvania inaungana na Familia ya Magege kwa masikitiko kutangaza kifo cha marehemu Mzee Alfred Magege kilichotokea jumamosi June 13,2015. Marehemu Alfred Magege alisumbuliwa na Saratani ya mifupa kwa zaidi ya miaka kumi.Marehemu ameacha Mke na watoto watatu. Kama kawaida yetu tunaombwa watanzania tujitokeze ili kuwafariji wafiwa.Ili tukamilishe Msiba huu kiasi cha $10,000 kinahitajika.Watanzania tuungane,tujitolee kwa hali na Mali tusaidiane kumzika Mtanzania mwenzetu.Michango yenu inahitajika kwaajili ya mazishi yatakayofanyika New York, Bwana ametoa na Bwana ametwaa. Tuchangie kupitia www.gofundme.com/wyfewd5

 Msiba utakuwa Address hii:
 2939 Wilson Avenue,Bronx,NY,10469.
 Kwa taarifa zaidi tuwasiliane na wafuatao. 
Hajji Khamis:3476238965
 Miriam Abu:9143162814
 Seif Akida:9175573195
 Buyamba Magege(Son):6469431104 
Geoffrey Ngullu:2675826276 
Amy Magege:5169467859 

Uongozi 
NY Tanzanian Community.

PROFESA MARK MWANDOSYA AENDELEA KUSAKA WADHAMINI MKOANI KILIMANJARO

0
0
Profesa Mwandosya akizungumza katika ukumbi huo.

Prof,Mwandosya akiteta jambo na RC Gama mara baada ya kukutana.


Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akimpatia kipaza sauti Prof Mwandosya asalimie wajumbe waliokuwa katika ukumbi huo.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.



TANZANIAN AGRICULTURAL DEVELOPMENT HAS A BRILLIANT FUTURE

0
0
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda akizungumza wakati wa kumbukumbu ya Kiongozi wa China  wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa BOT jijini Dar es Salaam
 Wajumbe wa mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda akizungumza mara baada ya kutoka katika mkutano wa kumbukumbu ya kiongozi wa nchini china, aliyeweka uhusiano mzuri kati ya watu wa Tanzania kipindi cha enzi za uhai wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Baadhi ya wajumbe wakiangalia picha iliyopigwa kipindi cha Mwalimu Nyerere.

CHADEMA WATOA SALAAM ZA POLE NA RAMBIRAMBI MSIBA WA MUFTI MKUU SHEIKH SIMBA

0
0

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
(CHADEMA)
SALAAM ZA POLE NA RAMBIRAMBI MSIBA WA MUFTI MKUU SHEIKH SIMBA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa taarifa za msiba wa Mufti Mkuu wa Tanzania Tanzania, Sheikh Issa Shaaban bin Simba, Kiongozi Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kilichotokea asubuhi ya leo kwa maradhi ya sukari na shinikizo la moyo.

Akitoa salaam za pole na rambirambi kwa waumini wa madhehebu ya Kiislamu na Watanzania wote kwa ujumla baada ya kupata taarifa za msiba huo, Mwenyekiti wa CHADEMA (T), Freeman Mbowe amesema kuwa Mufti Mkuu Simba atakumbukwa kwa namna aliyosimama kama kiongozi wa dini kupitia kauli zake mara kwa mara akisisitiza ushirikiano ndani ya jamii ya Watanzania bila kujali tofauti zao katika itikadi za dini.

“Mara kwa mara Mufti Mkuu Simba amesikika akiwaambia Watanzania, si Waislam pekee aliokuwa akiwaongoza kiroho, hata wale wanaoamini katika madhehebu tofauti, umuhimu wa kudumisha ushirikiano miongoni mwa dini mbalimbali na makundi mengine katika jamii ikiwa ni mojawapo ya misingi ya kuimarisha umoja wa taifa letu.”

“Naungana na Waislam wote nchini katika wakati huu wa kuomboleza kifo cha kiongozi huyu wa kiroho. Kwa niaba ya niaba ya uongozi wa CHADEMA, wanachama, wapenzi na wafuasi, natoa salaam za pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, BAKWATA, viongozi wa kiroho nchini na Watanzania wote ndani na nje ya nchi walioguswa na msiba huu mzito.”

“Mwenyezi Mungu awatie nguvu wote na kuwafanyia wepesi katika wakati huu mgumu wa majonzi ya msiba wa Mufti Mkuu Simba,” amesema Mbowe
Inna Lillahi wa inna ilaihi raji’un.

Imetolewa leo Jumatatu, Juni 15, 2015 na;
Idara ya Habari na Mawasiliano- CHADEMA.

MWILI WA MUFTI KUSAFIRISHWA KESHO KWENDA MKOANI SHINYANGA

0
0
Na Chalila Kibuda.
MWILI wa  Mufti ,Alhaj Sheikh Shaban Issa Bin Simba unataraji kusafirishwa kesho Jumanne Juni 16, kuelekea mkoani Shinyanga kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata), Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj  Mussa Salum, amesema mwili wa marehemu utaswaliwa kesho katika Msikiti wa Msilimu, viongozi mbalimbali wa dini na serikali watakuwepo.

Amesema marehemu amefikwa na umauti huo, baada ya  kusumbuliwa sana na sukari,Shinikizo la Damu (BP)  pamoja na Figo.

Hata hivyo amesema kuwa jana (Jumapili) Mufti alifanyiwa oparesheni ya figo katika Hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam.

Salum amesema marehem anatarajiwa kuzikwa Alhamis mkoani mkoani Shinyanga .
Mufti ,Alhaj Sheikh Shaban Issa Bin Simba enzi za uhai wake.
 Sehemu ya wanawake waliofika nyumbani kwa Marehemu  Mufti Alhaj Sheikh Shabaan Issa Bin Simba Mikocheni B jijini Dar es Salaam leo.
Sheikh Mkoa wa Dar es Salaam,Alhaj Sheikh Alhad Mussa Salum akibadilishana na mawazo na Sheikh wa Mkoa wa Kigoma Hassan Kiburwa walipofika nyumbani kwa Marehemu Mufti ,Mikocheni B leo jijini Dar es Salaam
Kulia ni Sheikh wa Mkowa Dar es Salaam,Alhaj Sheikh Alhad Mussa Salum akiwa na baadhi ya Masheikh waliofika Nyumbani kwa Marehen Mufti,Shabaan Issa Bin Simba Mikocheni B Jijini Dar es Salaam.(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA.)

MAMA SALMA AHUTUBIA MKUTANO WA WAKE WA MARAIS NA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA (OAFLA) NCHINI AFRIKA KUSINI

0
0
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akielekea kwenye ukumbi wa mkutano wa Sandton Internationa Center unakofanyika mkutano wa wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika huko Johannesburg nchini Afrika Kusini tarehe 15.6.2015. Aliyefuatana na Mama Salma ni Mwenyekiti wa OAFLA anayemaliza muda wake Mama Hinda Derby Itno.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia moja ya machapisho mbalimbali yanayohusiana na Mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika (OAFLA) unaofanyika nchini Afrika Kusini.
  Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano wao wa mwaka unaozungumzia uwezeshaji kwa wanawake na Maendeleo katika Bara hili.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake ya mwisho kwenye kikao cha Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika kinachofanyika kwenye Ukumbi wa Sandton jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini tarehe 15.6.2015.

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AMETUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA WAISLAMU WOTE NA BAKWATA KUFUATIA KIFO CHA SHEIKH MKUU WA TANZANIA MUFTI SHEIKH ISSA BIN SHAABAN SIMBA

0
0

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone:255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Waislamu wote nchini na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania  (BAKWATA)) kufuatia kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania  Mufti Sheikh  Issa Bin Shaaban Simba.

Marehemu Mufti amefariki  leo 15/6/2015 asubuhi katika hospitali ya TMJ – DSM alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa sukari na shinikizo la damu (pressure).

"Kifo kinaleta huzuni, hata hivyo Kifo hakizuiliki, hatuna budi kukikubali na ni wajibu wetu kumuombea Sheikh Mkuu kwa Mola wetu ampe mapumziko ya milele". Rais Kikwete ametuma salamu hizo za rambirambi kupitia kwa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum.

"Nawaombea subra wana familia, ndugu, jamaa, waislamu wote na wana jamii kwani Mufti alikua kiongozi katika Jamii yetu'Rais amesema na kueleza kuwa "Kamwe mchango wake hautasahaulika katika jamii yote kwa Ujumla na hakika sote tutamkumbuka"ameongeza.

Marehemu alijiunga na BAKWATA mwaka 1968 na amekuwa mwalimu wa chuo katika mikoa mbalimbali ya Mwanza, Bukoba na Mwaka 1970 alikuwa Shekhe wa Mkoa wa Shinyanga.

Rais amemuelezea Marehemu Mufti kama mwalimu katika jamii ambaye alikua na uzoefu wa hali ya juu na mwenye kupenda dini yake na kuitumia kwa manufaa ya jamii iliyomzunguka

"Amekua mwalimu imara na mtu wa kutumainiwa na kutegemewa katika uislamu na jamii kwa ujumla, hakika tutamkumbuka siku zote' Rais Kikwete ameongeza.

Shekhe Issa Bin Shaaban Simba alikuwa na uzoefu  mkubwa ndani ya BAKWATA na  aliwahi kukaimu nafasi ya mufti kwa siku 90, baada ya kifo cha Mufti Hemed mwaka 2002.

Baada ya hapo akasimamia mchakato wa uchaguzi wa Mufti Mkuu na baadaye 2003 akachaguliwa kuwa Mufti Mkuu wa Tanzania.

Mwenyezi Mungu ailaze roho yake pahali pema Peponi, Amina.

Imetolewa na :
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu-DSM
15 Juni, 2015

EWURA YAPATA TUZO MDHIBITI BORA WA NISHATI 2015

0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngamlagosi akizungumza na waandishi wa habari juu ya tuzo waliopata Dubai katika udhibiti wa Nishati iliofanyika Ofisi za EWURA,  leo  jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mhandisi wa Umeme EWURA, Anastas Mbawalla.
 Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi akionyesha kitabu cha kinachofafanua masuala ya mikataba katika sekta ya Nishati ambacho Mtaalam wa Mhandisi wa Umeme, Anastas Mbawalla (kushoto)alishiriki katika kuandika kitabu hicho.
Mhandisi wa Umeme wa EWURA, Anastas Mbawalla akizungumza na waandishi wa habari juu alivyoshiriki katika kuandika kitabu cha masuala ya mikataba ya nishati iliofanyika leo katika ofisi za EWURA jijini Dar es Salaam, Kulia ni Mkurugenzi Mkuu EWURA, Felix Ngamlagosi.(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA.GLOBU YA JAMII)

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),imeibuka mshindi wa mashindano ya Tuzo  ya Mdhibiti Bora wa mwaka wa Nishati 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mkuu wa EWURA,Felix Ngamlagosi amesema kuwa tuzo hiyo imetolewa Juni 8 mwaka huu kwenye uzinduzi wa sherehe za 17 za Mkutano Mkuu wa Kila mwaka wa Nishati wa Afrika  uliofanyika Dubai.

Ngamlagosi amesema kuibuka kwa  EWURA  katika Tuzo za Nishati inalenga kuwatambua wale wote ambao wametoa mchango kwa maendeleo ya soko la nishati barani Afrika.

“Ushindi wa Tuzo ya Udhibiti Bora wa mwaka wa nishati 2015 imetambua mchango wetu wa udhibiti kutokana na huduma tunayotoa kwenye malengo  ya kuboresha mazingira ya uwekezaji  katika sekta ya nishati kutokana na mahitaji”amesema Ngamlagosi.

Amesema tuzo hiyo inaifanya Tanzania sasa itambulike Kimataifa kwa kuwa na taasisi thabiti ya uhakika ya udhibiti wa sekta nishati na maji ,ambalo ni jambo la muhimu kwa nchi kuendelea kuimarisha imani ya wawekezaji ambayo inatakiwa sana katika kuvutia mitaji binafsi kwenye sekta ya nishati.

Niambie Live Show wiki hii (teaser)

NHC yakabidhiwa cheti cha Mwajiri Bora 2015

0
0
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga (wa kwanza kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), James Rhombo tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2014 mara baada ya Shirika hilo na mengine mawili kutangazwa kuwa mwajiri bora wa mwaka 2015 iliyotolewa na Chama Cha Wafanyakazi wa Migodini, Ujenzi, Nishati na Kazi nyingine (TAMICO). Katikati ni Mwenyekiti wa TAMICO Taifa, Mbaraka Igangula akishihudia. Katika tuzo hizo jumla ya waajiri 160 walishindanishwa na kupatikana watatu bora ambao ni NHC, Kampuni ya kuchimba madini ya Geita Gold Mining (GGM) na Wakala wa Ujenzi wa Barabara Tanzania (Tanroad).Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), James Rhombo (Kulia) Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC, Muungano Saguya na Meneja wa Mawasiliano kwa Umma wa NHC, Yahya Charahani wakiimba wimbo wa solidarity forever wakati wa hafla hiyo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Filamu ya Mpango Mbaya ina viwango vya Kimataifa - Wadau

0
0
Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Group, Bw Johnson Lukaza akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa filamu ya Mpango Mbaya iliyochezwa na washiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) mwaka 2014, uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa sinema wa century uliopo Mlimani City, Jijini Dar Es Salaam. Filamu hii ni moja ya filamu ambayo ina ubora wa hali ya juu huku wadau waliofanikiwa kuitazama filamu hiyo kuvutiwa nayo na kukubali kuwa ni filamu yenye viwango vya kimataifa na yenye utofauti mkubwa na filamu nyingine za Kitanzania.
Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Group, Bw Johnson Lukaza akifurahia jambo na mwenyekiti wa bodi ya filamu nchini, Mama Fisoo kabla ya uzinduzi wa filamu ya Mpango Mbaya kuanza, uzinduzi huo ulifanyika jana katika Ukumbi wa Sinema wa Century uliopo Mlimani city, Jijini Dar Es Salaam.

Bunge latoa Ufafanuzi kuhusu Vicoba

MASHINDANO YA MTEMVU CUP YAFIKIA TAMATI, KATA YA 14 YAIBUKA KIDEDEA

0
0
Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu (kushoto), akiwa na Waziri wa Habari  Vijana Utamaduni na Michezo, Dk.Fenellah Mukangala (kulia) aliyekuwa mgeni rasmi katika fainali za mashindano ya Mtemvu CUP yaliyofikia tamati viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam jana. Timu zilizoingia ingia fainali hiyo ni Miburani Kata ya 15 na Kata ya 14 ambayo iliibuka kidedea kwa ushindi wa bao 1-0.
Mchuano ukiendelea.
Hapa ni kazi tu kwa kwenda mbele.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

BREAKING NEWSSS MUFTI MKUU WA TANZANIA SHEIKH ISSA BIN SHAABAN SIMBA AFARIKI DUNIA

0
0
MUFTI  Mkuu wa Tanzania, 
Sheikh Issa Bin Shaaban Simba, 
enzi za uhai wake.

Habari zilizofika chumba chetu cha habari mapema asubuhi leo na kuthibitishwa na mamlaka husika zinasema Mufti Mkuu wa Tanzania,  Sheikh Issa Bin Shaaban Simba,  amefariki dunia alfajiri ya leo katika hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam. 


Habari hizo zinasema mwili wa marehemu umeondolewa hospitali hapo na kuhamishiwa hospitali kuu ya Jeshi ya Lugalo kungoja taratibu za mazishi.

  Kwamujibu Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum
 amesema kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo pamoja na presha.
Mwili wa marehemu utasafirishwa kesho mkoani Shinyanga  kwaajili ya maziko.
  Tutaendelea kuwaletea taarifa zaidi 
kwa kadri  zitapopatikana.


Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un 
إِنَّا للهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعونَ‎) 

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (Mb.) ametuma salamu za rambirambi kwa Baraza Kuu la Waislamu Nchini (BAKWATA) na Waislamu wote nchini kufuatia kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Bin Simba kilichotokea Jumatatu, tarehe Juni 15,2015 katika hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam alipokuwa anatibiwa.

Katika salamu hizo, Mhe. Mukangara amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kumpoteza kiongozi huyo ambaye bado Taifa lilikuwa likimuhitaji hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwezi  Oktoba mwaka huu. 
Waziri huyo ameongeza kuwa Mufti atakumbukwa kwa upole  , unyenyekevu wake na kutopenda makuu,wakati wa uhai wake marehemu alikuwa tayari kumsikiliza kila mtu bila kujali dini au kabila lake. 
“Nimepokea kwa huzuni nyingi taarifa ya kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Bin Simba ambaye alikuwa Kiongozi anayeshirikiana vizuri na viongozi wote wa serikali na vyama mbalimbali katika kuhakikisha Watanzania wanaendelea kuwa wamoja” amesema .

Amesema Waziri Mukangara: “Nakutumia salamu zangu za rambirambi wewe Katibu Mkuu, BAKWATA na waislamu wote nchini na naungana nanyi katika kuomboleza msiba huu mkubwa katika nchi yetu. 
Aidha, kupitia BAKWATA, natuma salamu za dhati ya moyo wangu kwa familia ya marehemu kwa kumpoteza mpendwa wao. Napenda wajue kuwa msiba wao ni msiba wangu. Pia, naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aiweke pema peponi roho ya marehemu … Amina.”
Imetolewa na;
Idara ya Habari(MAELEZO)

15 Juni,2015

MAKONDA AONGOZA MAMIA MAZISHI YA BABA YAKE MSANII STEVE NYERERE

0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Francis Festus Mengele, Baba wa Msanii, Steven "Nyerere" Mengele (kulia) .
 Shangazi wa Msanii, Steve Nyerere, Grace Mengele (katikati), akiwa na wadogo zake Steve Nyerere wakati akiwasili makaburi ya Kinondoni kwa mazishi ya mpendwa wao, Francis Mengele.
 Watoto wa marehemu na dada zake wakiwa kwenye ibada ya maziko makaburi ya Kinondoni.
 Ibada ya maziko ikiendelea.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
Viewing all 109592 articles
Browse latest View live




Latest Images