Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

BALOZI WA NIGERIA NCHINI ATEMBELEA MAHAKAMA YA AFRIKA KUAGA

$
0
0
 Jaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu(AfCPHR)Gerald Niyungeko(kushoto)akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Nigeria nchini Tanzania,Dk. Ishaya  Majanbu aliyefika katika Mahakama hiyo jijini Arusha kuaga baada ya kumaliza muda wake wa Ubalozi nchini.
 aji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu(AfCPHR)Gerald Niyungeko(katikati)akimkabidhi zawadi mgeni wake Balozi wa Nigeria nchini Tanzania,Dk. Ishaya  Majanbu aliyefika katika Mahakama hiyo jijini Arusha kuaga uongozi wa Mahakama hiyo baada ya kumaliza muda wake wa Ubalozi nchini,anayeshuhudia kushoto ni Naibu Msajili wa Mahakama hiyo,Nouhou Diallo.
Jaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu(AfCPHR)Gerald Niyungeko(katikati)akizungumza na wageni wake,kushoto ni wafanyanyakazi wa Mahakama hiyo

KAMPUNI YA ASAS DAIRIES LTD KWA MWAKA WA TATU MFULULIZO YASHIKILIA TUZO YA UBORA ,YAZIBWAGA KAMPUNI KONGWE TENA WAZIRI KAMANI APONGEZA

$
0
0
Afisa masoko wa kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd Bw Jimmy Kiwelu (kulia)  akiwa na   wafanyakazi  wenzake baada ya  kutwaa tuzo ya ubora ya Kitaifa katika  bidhaa za Asas Dairies Ltd 

Hii  ndio kampuni  iliyoweza  kushinda tuzo ya  ubora
Medali  ,vyeti na  tuzo  ya ushindi  ambayo kampuni ya Asas Dairies Ltd imeshinda  tena  mwaka huu katika maonyesho ya maziwa mkoani Mara.

SERIKALI YAPATA GAWIO LA FAIDA LA SHILINGI BILIONI 3 KUTOKA KAMPUNI YA PUMA ENERGY TANZANIA LIMITED

$
0
0
Waziri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya Salum (wa pili kulia) akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dr. Servacius Likwelile pamoja na Msajili wa Hazina, Nd. Lawrence Mafuru wakipokea hundi ya mfano ya shilingi Bilioni 3 kutoka Kampuni ya Puma Energy Tanzania Limited iliyokabidhiwa na Mkuu wa Puma Energy Tanzania Limited, Nd. Philippe Corsaletti.
Waziri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya Salum akiwashukuru watendaji wakuu wa Puma Energy Tanzania Limited kwa kuwasilisha kwa Serikali gawio la faida la shilingi Bilioni 3. Mawasilisho hayo yalifanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha,Mjini Dodoma. Kulia kwa Mh.Waziri ni Dr.Servacius Likwelile,Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali.

UNFPA-TANZANIA KWA KUSHIRIKIANA NA TUME YA MIPANGO YAENDESHA WARSHA MKOA WA MARA

$
0
0
Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, wameandaa warsha kwa ajili ya kuhamasisha na kuwajengea uwezo watumishi wa Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu kujumuisha masuala ya vijana katika mipango ya Mkoa na wilaya. 

 Warsha hiyo inafanyika katika vituo vya Mwanza na Musoma. Katika kituo cha Musoma warsha inafanyika katika ukumbi wa Afrilux Hotel tarehe 11 na 12 Juni 2015. Kituo hiki kinajumuisha Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za mkoa wa Mara na Simiyu. 

 Washiriki wa warsha ni Makatibu Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya.
Mgeni Rasmi Bw. Ibrahim D. Kalengo, Mtakwimu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ambae anamwakilisha Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, akitoa neno kwa ajili ya warsha hiyo kufunguliwa rasmi.
Mwezeshaji Dr. Deograsias P. Mushi ambae pia ni Mchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mtafiti wa Ecom Research Group akishusha nondo kwa wanawarsha juu ya mambo mbalimbali yanayohusu ujumuishaji wa masuala ya vijana katika mipango ya maendeleo ya mkoa na wilaya.

Zulia Jekundu na VOA Kiswahili - Arnold Schwarzneggar, Jackman,Depp &"I am Cait"

Usikose usiku wa ‘Stara Fashion Show’ leo ukumbi wa City garden jijini Dar es salaam

$
0
0
Ni usiku wa ‘Stara Fashion Show’ ambayo inategemea kufanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 13 June 2015. Hivyo hupaswi kukosa show hiyo kwani Mama wa mitindo alimaarufu kwa Jina la Asya Idorous Khamsin ataipamba Fashion Show hiyo kwa mitupia ya hatari, Itakuwa ni mapema sana kuanzia saa moja jioni Katika Ukumbi wa City Garden ni onyesho la kipekee lenye mavazi ya heshima tofauti na jinsi ambavyo umezoe kuona Fashion Show zingine.

Usiku huo umeandaliwa na Kampuni ya ‘Jast Tanzania Limited’ chini ya usimamizi wa mratibu wa Kampuni hiyo Juhu Mohammed Kessy wakishirikiana na Founder wa Kampuni hiyo Latifah Makau.
Wana kuletea raha zote na burudani nyingi kwa mtonyo wa buku 20000/= yaani elfu Ishirini tu! na kwa wale wa VIP ni elfu 40000/= tu. Usicheze mbali

KINANA AWASILI WILAYA YA KYERWA, ATAKA MIRADI YA MAENDELEO ISIMAMIWE NA HALMASHAURI SIYO SERIKALI.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitembelea shamba la ndizi na kahawa la  mkulima wa Kahawa na Ndizi Ndugu Eustace Kubalienda Kishunji katika kijiji cha Mabila,wilayani Kyerwa mkoani Kagera
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa mkulima wa Kahawa na Ndizi Ndugu Eustace Kubalienda Kishunji ambaye ni mmiliki wa shamba la Ndizi,, Amesema shamba hilo  lina  miche 345 ambayo huvuna magunia 25 na ana shamba la migomba ambalo humpatia mavuno ya  mikungu  kwa mwezi 45.

Mzee Kishunji ambaye anaishi katika kijiji cha Kikukuru kata ya Mabira ameweza kusomesha watoto wawili katika vyuo vikuu vya Dar es salaam na Dodoma na amejenga nyumba ya kisasa yenye thamani kubwa ya fedha kutokana na kilimo bora cha kisasa.

Katibu Mkuu Kinana yuko ziarani katika mikoa ya Kagera , Geita na Mwanza akikagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010, akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
 Mkulima bora wa migomba na kahawa katika Kijiji cha Mabira, Mzee Eustus kishunju Ntibalienda (kulia) akimpatia maelezo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kuhusu alivyoweza kufanikiwa katika kilimo cha mazao hayo, Katibu Mkuu alipomtembelea mkulima huyo,  akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera, leo. 
 Sehemu ya soko la biashara la kisasa na la kimataifa linalojengwa Kigorogoro,mpakani mwa Tanzania na Uganda.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (pichani kati) akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Mkuu wa mkoa wa Kagera Mh.John Mongella wakijadiliana jambo mara baada ya kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Kigorogoro, alipowasili katika kijiji hicho kukagua ujenzi wa soko la kisasa na la Kimataifa katika kijiji hicho leo.

Hhata hivyo Kinana ameonesha kusikitishwa baada ya kujulishwa kuwa ujenzi wa mradi huo, unaohitaji sh. bilioni 1.5 umesimama kutokana na serikali kuu kukosa fedha.

        Kutokana na hali hiyo, Katibu Mkuu wa CCM, amesema ni vema miradi muhimu ya maendeleo iwekwe chini ya usimamizi wa halmashauri ya eneo linalohusika badala ya serikali kuu. 

       Amesema, utaratibu wa kuifanya miradi ya aina hiyo kuwa chini ya usimamizi wa serikali, umekuwa ukileta matokeo mabaya ikiwemo kusimama kwa ujenzi wa miradi.

       Kinana amesema hayo leo, baada ya kukagua ujenzi wa kitu kikubwa cha biashara, katika Kata ya... wilayani Kerwa mkoa ni Kagera ambacho ujenzi wake umesimama tangu mwaka juzi kwa maelezo ya kukosekana fedha.

      "Jamani jengo kama hili lilitakiwa lisimamiwe na Halmashauri ya eneo hili, lakini kusimamiwa na wizara ni kupoteza muda, hivi kweli ni rahisi mkaguzi atoke Dar es Salaam, kuja hadi huku kukagua ujenzi tu wa jengo hili, hasa ikizingatiwa kuwa miradi kama hii ni mingi?" alihoji Kinana.
 Wananchi wa Kijiji cha Kigorogoro katika Kata ya Murongo wilayani Kyerwa mkoani Kagera wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCm, Abdulrahman Kinana akipowasili kuwahutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho leo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwahutubia Wananchi wa kijiji cha Kibingo Wilayani kyerwa mkoani Kagera.
 Wananchi wa kijiji cha Isingiro wakimshangilia Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,alipopanda jukwaani na kuwasalimia.
 Wananchi wa kijiji cha Isingiro wakimsikiliza Katibu Mku wa CCM,Ndgu Kinana alipokuwa akiwahutubia.

PICHA NA MICHUZI JR-KYERWA KAGERA.


DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI LEO


Rais Kikwete awasili Arusha kuongoza maadhimisho ya Siku ya Albino

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama Cha Albino Tanzania Bwana Ernest Kimaya akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) muda mfupi baada ya kuwasili jana  jioni.Rais Kikwete atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kimataifa wa Albino itakayofanyika leo katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid. Kushoto ni Bwana Godson Mollel mwenyekiti wa Chama cha Albino Mkoa wa Arusha. Picha na Freddy Maro

JK aongoza maadhimisho ya siku ya watu wenye Albinism Duniani leo jijini Arusha.

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na baadhi ya watoto wenye albinism mara baada ya kuwasili katika uwanja wa michezo wa Sheikh amri Abeid mjini Arusha leo ambapo aliongoza maadhimisho ya siku ya watu wenye Albinism Duniani leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na baadhi ya watoto wenye albism katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha wakati wa maadhimisho ya siku ya watu wenye albinism Duniani leo. Picha na Freddy Maro

MH. LOWASSA ATUA KIGOMA LEO, AKOMBA WADHAMINI 11,250

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiusalimia umati wa wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Kigoma, wakati alipowasili kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Kigoma, kusaka wadhamini wa kumsainia fomu za kupata ridhaa za Chama kuwania Urais wa Tanzania. Mh. Lowassa amedhaminiwa na wanaCCM 11,250 wa Mkoa wa Kigoma, leo Juni 13, 2015.

Umati wa WanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Kigoma, ukiwa umefurika kwenye Uwanja wa Ofisi Kuu ya CCM Mkoa wa Kigoma, kuja kumuona Mh. Edward Lowassa (anaeonekana kule mbele) wakati alipofika kuomba udhamini wa wanachama wa CCM, ili aweze kupata ridhaa ya Chama kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amepata udhaminiwa na wanaCCM 11,250 wa Mkoa wa Kigoma, leo Juni 13, 2015.
Katibu wa CCM Wilaya ya Kigoma Mjini, Noverty Kibaji akizungumza wakati akimuelezea Mh. Lowassa, idadi ya wanaCCM waliomdhani ili apate ridhaa ya Chama kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Katibu wa CCM Wilaya ya Kigoma Mjini, Noverty Kibaji (kushoto) akimkabidhi, Mh. Edward Lowassa, majina ya wanaCCM wa Kigoma Mjini waliomdhani ili apate ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dkt. Aman Kaborou, muda mfupi kabla ya kupokea idadi ya majina ya wanaCCM waliomdhani ili apate ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amedhaminiwa na wanaCCM 11,250 Mkoani Kigoma, leo Juni 13, 2015.

STARS YAWASILI BORG EL ARAB, KUWAVAA MISRI KESHO

$
0
0
Msafara wa timu ya Taifa ya Tanzania (taifa Stars) inayodhaminiwa na kampuni ya bia ya Kilimanjaro Premium Lager tayari umewasili salama katika eneo la Borg El Arab jijini Alexandria na kufikia katika hoteli ya Panacea tayari kwa mchezo wake wa kesho.

Taifa Stars ambayo ilikuwa kambini nchini Ethiopia kwa takribani wiki moja, iliondoka jana usiku Addis Ababa  na kuwasili uwanja wa ndege wa Cairo majira ya saa 8 usiku, kisha kuunganisha kwa usafiri wa basi mpaka Borg El Arab takribani masaa matatu.

Kocha mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij, atakiongoza kikosi chake katika mazoezi ya mwisho leo saa 1 usiku katika uwanja wa Borg El Arab kwa saa za Misri, sawa na saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Akiongelea mchezo wa kesho, Nooij amesema anashukuru kikosi kimefika salama nchini Misri na kipo katika hali nzuri, vijana wana ari na morali ya hali ya juu, anaamini kesho timu itfanya vizuri katika mchezo huo dhidi ya wenyeji Misri.

Nooij amesema mchezo wa kesho ni muhimu kwake, na kikosi chake kitacheza mpira wa kasi na pasi za haraka haraka, huku safu ya ushambuliaji ikihakikisha inatumia vizuri nafasi itakazozipata.

Aidha kuelekea katika mchezo huo wa kesho, kiungo Amri Kiemba ameungana na wachezaji wengine waliokuwa kambini Addis Ababa kuchukua nafasi ya Mrisho Ngasa ambaye alishindwa kuungana na timu kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo wake.

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia tayari amewasili jijini Alexandria kwa ajili ya kuipa sapoti Taifa Stars katika mchezo huo wa kesho.

Mchezo kati ya Misri na Tanzania utachezwa kesho saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki na kati katika uwanja wa jeshi la Misri (Borg El Arab) uliopo takribani kilometa 70 kutoka jijini Alexandria na kilometa 200 kutoka jiji la Cairo.

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA BARAZA KUU LA SHIRIKA LA HALI YA HEWA DUNIANI (WMO)

$
0
0
Ujumbe wa Tanzania unaendelea kushiriki katika kikao cha Mkutano Mkuu wa Kumi na saba wa Shirikia la Hali ya Hewa Duniani (WMO-Congress 17), mijini Geneva, nchini Uswisi. Ujumbe huo umeshiriki katika matukio mbalimbali ya mkutano huo ikiwa ni pamoja na Dkt. Agnes Kijazi kushiriki katika siku ya Jinsia ya WMO (WMO Gender Day), kutoa mada zilizotoa uzoefu wa Tanzania wa utekelezaji wa program za utekelezaji wa programu ya utoaji wa huduma bora za hali ya hewa kwa jamii “Global Framework for Climate Services (GFCS) na programu ya uendelezaji wa mitandao ya upimaji wa hali ya hewa na mawasiliano (WMO Integrated Observation System and WMO Information System-WIGOS/WIS). Kwa habari zaidi angalia picha za matukio mbalimbali ya Mkutano huo hapa.
Balozi wa Tanzania na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa, Uswiss, Balozi Modest Mero na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Dkt. Agnes Kijazi na Ujumbe wa Tanzania wakishiriki katika Mkutano Mkuu wa Kumi na Saba wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO- Congress-17), Geneva, Uswisi.

MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA UELIMISHAJI UMMA KUHUSU UALBINO

$
0
0
Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Dkt. Kevin Mandopi akizungumza na wadau mbalimbali wa masuala ya haki za binadamu katika mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelimishaji Umma Kuhusu Ualbino uliofanyika kwenye ofisi za Tume hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali Bibi. Neema Ringo na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bibi. Nkasori Sarakikya.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bibi. Mary Massay akitoa ufafanuzi kuhusu haki za watu wenye ualbino katika mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelimishaji Umma Kuhusu Ualbino uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bibi. Nkasori Sarakikya.
Mwakilishi wa UNESCO Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza kwenye mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelimishaji Umma Kuhusu Ualbino leo jijini Dar es Salaam ambapo ameishauri Serikali kuweka mikakati ya muda mrefu ili kukomesha ukatili na unyanyapaa dhidi ya watu wenye ualbino.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali Bibi. Neema Ringo (kushoto) akitoa rai kwa watanzania kutoa taarifa mapema za vitendo vya ukatili dhidi ya watu wenye ualbino katika mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelimishaji Umma Kuhusu Ualbino uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Dkt. Kevin Mandopi na Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bibi. Nkasori Sarakikya.
Baadhi ya waandishi wa habari na wadau wa masuala ya haki za binadamu wakifuatilia mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelimishaji Umma Kuhusu Ualbino uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA FATMA SALUM - MAELEZO

Wananchi watakiwa kuuchukia uhalifu kwa vitendo

$
0
0
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi
Wananchi wametakiwa kuuchukia uhalifu kwa vitendo pamoja na kuwa na kauli moja katika kupambana nao kwa kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kukomesha vitendo hivyo hapa nchini.

Hayo yalisemwa jana  na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki wakati alipokuwa akifungua semina ya siku moja katika ukumbi wa Nkurumah iliyokuwa na kauli mbiu ya Kataa uhalifu iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya Jeshi la Polisi na Shule kuu ya Sheria ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa lengo la kupambana na uhalifu hapa nchini, semina ambayo iliwashirikisha wahadhiri, maofisa wa Polisi na wanafunzi wa chuo hicho.
 Kaniki alisema wananchi wakiukataa uhalifu watawezesha jamii ya watanzania kuwa salama na kuondoa vikwazo katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kuwa uhalifu ndio kikwazo katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali.

Aidha aliwaomba wasomi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam hususani wanaosomea shahada ya sanaa katika utekelezaji wa sheria kufanya tafiti ambazo zitaweza kulisaidia Jeshi la Polisi katika kutatua kero za uhalifu hapa nchini.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Prof.Rwekaza Mukandala alisema jukumu la kupambana na uhalifu sio la jeshi la polisi pekee bali ni jukumu la watu wote.
 Aliongeza kuwa  kwakutambua hilo mwaka 2009 walianzisha shahada ya utekelezaji wa sheria ambayo asilimia kubwa ya wanafunzi wanatoka katika vyombo vya ulinzi na usalama na wakufunzi wa shahada hiyo ni maofisa  kutoka katika Jeshi la Polisi.

Naye Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) Diwani Athuman alisema kauli mbiu hiyo ya kataa uhalifu ilibuniwa na Shirikisho la Polisi wa Kimataifa (INTERPOL) ili kutimiza malengo yake ya kuwa na dunia iliyo salama  kwa binadamu ambapo kwa hapa nchini ilizinduliwa mwaka jana kwa kushirikisha wadau mbalimbali.
 Alisema katika semina hiyo wajumbe watapata fursa ya kujadili kwa pamoja makosa yaliyopo hapa nchini yakiwemo ya madawa ya kulevya, ujangili, mauaji ya albino, mauaji ya vikongwe, kujichukulia sheria mkononi , waham,iaji haramu pamoja na usafirishaji haramu wa binadamu.

WASIFU WA BERNARD KAMILIUS MEMBE

$
0
0
Bernard Kamilius Membe alizaliwa tarehe 9 Novemba, 1953, Rondo, Chiponda, katika Mkoa wa Lindi, akiwa ni mtoto wa pili kati wa watoto saba (7) waliozaliwa katika familia ya Mzee Kamillius Anthony Ntachile na Mama Cecilia John Membe. Kwa kabila, Bernard Membe ni Mmwera, na kama ilivyo desturi ya Wamwera, watoto hutumia jina la ukoo wa Mama. Hivyo watoto wote saba wa familia hii ya Mzee Kamillius wamekuwa wanatumia jina la upande wa mama yao, Cecilia, yaani Membe.

Elimu:
1962 – 1968: Elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Chiponda, Lindi.
1969 – 1972: Elimu ya Sekondari, (O-level) Namupa Seminary, Lindi
1973 – 1974: Kidato cha tano na sita (A-level) Itaga Seminary, Tabora
1975 – 1980: Aliajiriwa serikalini, ofisi ya rais
1981 – 1984: Alipata Shahada ya kwanza katika tasnia ya Sayansi katika maswala ya Siasa na mahusiano ya kimataifa (Bachelor Political Science and International Relations)
1985 – 1989: Aliendelea na ajira yake serikalini katika katika ofisi ya rais
1990 – 1992: Alipata Stashada ya Uchumi, Mahusiano ya Kimataifa na Sheria za Kimataifa (Masters- Economics, International Relations and International Law)
1993 – 1994: Alirudi serikalini kuendelea na kazi kama mchambuzi za mambo ya ulinzi na usalama

Mafunzo:
Kati ya mwaka 1975 na 1976 Ndugu Bernard Membe alijiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kambi ya Oljoro, Arusha. Hii ni kwa mujibu wa Sheria ambapo vijana wote waliohitimu kidato cha Sita walitakiwa kujiunga na mafunzo ya Jeshi kwa muda wa mwaka mmoja. Baada ya kuhitimu mafunzo hayo ya Jeshi, Ndugu Membe aliajiriwa katika Ofisi ya Rais, Utawala bora.

KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AMUAGA BALOZI WA BRAZIL ALIYEMALIZA MUDA WA KAZI NCHINI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula kwa pamoja na Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe. Juma Halfan Mpango wakimsikiliza kwa furaha Balozi wa Brazil aliyemaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Mhe.Francisco Suarez Luz (kushoto) kabla ya kuanza kwa hafla fupi ya chakula cha mchana iliyoandaliwa kwa ajili ya kumuaga Balozi Luz. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Juni, 2015.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mulamula kwa pamoja na Balozi Mpango wakiendelea kumsikiliza Balozi Luz mara baada ya kuketi tayari kwa kushiriki chakula cha mchana kwa heshima ya kumuaga Balozi Luz.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

HIVI NDIVYO HALI ILIVYOKUWA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

KINANA AITAKA SERIKALI KURAHISISHA UTOAJI WA LESENI KWA WAFANYABIASHARA,MADEREVA WA MAGARI NA BODABODA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua rasmi Chanjo ya  watoto kuzuia maambukizi ya magonjwa katika kata ya Nyakisasa kijiji cha Kashinga akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Ngara mkoani Kagera,lengo la ziara hiyo likiwani ni kukagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010 na kuhimiza uhai wa chama, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na ktibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na viongozi mbalimbali wa CCM  kutoka mkoa wa Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi mbalimbali za waliokuwa wanachama wa Chama cha CHADEMA mara baada ya kurejesha kwake na kujiunga na CCM katika mji wa Rulenge.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ngara Mama Constansia Buhie wakizikusanya kadi  mbalimbali za wafuasi wa upinzani na kuzikabidhi kwa viongozi hao wa CCM,ikiwa ni ishara ya kujiunga na chama hicho cha CCM
 Baadhi ya kadi zilizorejeshwa kwa Kinana na wananchi hao na kujiunga na CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na mhandisi wa kampuni ya kichina ya TKPE Bw.Ton Minyang wakati alipokagua ujenzi wa  Mtambo wa umeme  vijijini REA unaojengwa katika kijiji cha Djuruligwa kata ya Kabanga wilayani Ngara.
 Wananchi wa Ngara mjini wakishangilia jambo katika mkutano wa hadhara wa CCM
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Abdulrhaman Kinana akiwahutubia wananchi wa Ngara mjini,Kinana ameitaka Serikali kurahisisha utoaji wa leseni kwa wafanyabiashara , madereva wa magari na bodaboda badala ya kuacha watu wanasumbuka kutafuta leseni umbali mrefu tena kwa gharama kubwa.

Kinana amesema kuwa  moja ya ombi la wananchi hao ilikuwa ni kuomba kurahisishiwa kupata leseni ili kuondoa usumbufu wanaoupata sasa.Alisema Serikali lazima iweke mazingira mazuri ya kutoa leseni kwa wananchi wakiwamo wafanyabishara na madereva bodaboda huku akieleza hakuna sababu ya kutumia gharama kubwa kwa ajili ya leseni. 

 KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa mji wa Ngara Mjini kwenye mkutano wa hadara,Nape Nnauye alisema kuwa hakuna sababu ya Watanzania kuingia kwenye mpasuko kwa sababu ya mchakato wa katiba mpya na kuashauri ni vema mjadala ukafungwa kwenye nyumba za ibada. Amesema inasikitisha unapoona baadhi ya viongozi wa dini badala ya kuhubiri neno la Mungu na kuwaunganisha Watanzania wanatumia nafasi yao kuwagawa wananchi kwa sabababu ya Katiba mpya.

PICHA NA MICHUZI JR-NGARA


MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA MJI WA AVIC, 'AVIC TOWN' ULIOPO KIGAMBONI DAR

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lyu Youqing (kulia), Makamu wa Rais wa 'Avc International', Dkt. Cheng Baozhong (kushoto) kwa pamoja wakikata utepe kuzindua ramsi Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Avoc 'Avic Town', uliozinduliwa leo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lyu Youqing (kulia), kwa pamoja wakifunua kitambaa kuashiria kuweka jiwe la Msingi la uzinduzi ramsi wa Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Avoc 'Avic Town', uliozinduliwa leo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa Mradi wa Ujenzi wa Mki wa Avic, 'Avic Town', uliofanyika leo Juni 13, 2015 Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images