Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 85 | 86 | (Page 87) | 88 | 89 | .... | 3272 | newer

  0 0


  Ankal,

  picha hizi mbili moja ni mkate wa kawaida (chini) na juu ni mkate kwa  yai  la jicho la ng'ombe. Ni viitafunwa safi kabisa wakati huu wa mapumziko ya Pasaka, HAPPY EASTER!
  Chef Issa

  Kwa haya na mengine mengi yahusuyo uandaaji wa mapochopocho baabkubwa  tembelea libeneke la Che Issa 

  0 0

   Waziri wa Viwanda na Biashara,Dkt. Abdallah Kigoda (wa pili kulia) akikagua shughuli za Ujenzi wa kiwanda hicho huku akipewa maelezo na Meneja wa Mradi huo.kazi za ujenzi wa kiwanda hicho cha Cementi inaendelea kwa kasi sana.
  Waziri wa Viwanda na biashara,Abdallah Kigoda akipata taarifa fupi ya kazi za ujenzi wa kiwanda cha Simenti toka kwa Mkurugenzi wa Meis Industries,Merey Ally Saleh. 
  kazi za ujenzi zinaendelea katika kiwanda hicho kinachotarajiwa kuanza uzalishaji April mwakani.

  Na Abdulaziz,Lindi

  Zaidi ya dola milioni 30 zinatarajia kutumika kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha Lindi simenti ambacho kimeanza ujenzi wake mapema mwenzi feb na kinatarajia kumamilika baada ya miezi 14 kuanzi sasa.

  Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mtendaji wa Meis Industries company Ltd,, Merey Ally Saleh alipokuwa anazungumza na waziri wa viwanda na biashara Abdala Kigoda wakati alipotembelea kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho .

  Meley alisema kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda hicho kutasaidia kuajiri watu zaidi ya 1000 na kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 600 hadi 700 za sement kwa siku ambayo Itasaidia wakazi wake kupata bidhaa hiyo kwa bei nafuu kuliko hivyo sasa.

  Alisema kiwanda pia kitatumia raslimali zinazopatikana hapa nchini kwa asilimia 95 na asilimia tano bidhaa za kutoka nje ambazo ni kemikali za kuumulia udongo na kufanya kuwa sementi.

  Kwa upande wake waziri wa viwanda Abdalah Kigoda ameipongeza kampuni ya Meis kwa kitendo cha kufikiria kujenga kiwanda hicho na kueleza kuwa kitakuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo kwa mikoa ya kusini Lindi na Mtwara na kupunguza tatizo la ajira lililopo.

  Kigoda alisema kiwanda hicho kitakuwa cha nne kwa ukubwa ambacho kinatumia raslimali za ndani kwa asilimia kubwa kama vile viwanda vya Twiga sementi, Tanga sementi na Lindi Sementi.

  Alisema serikali inaona juhudi za wawekezaji na hivyo basi iko katika utaratibu wa kuondoa changamoto cha ukosefu wa umeme ambao umekuwa kero kubwa kwa wawekezaji wa viwanda hapa nchi kwa kuharakisha miradi ya uvunaji wa gesi kwa ajili ya nishati hiyo

  0 0

   ABIRIA wapatao 45 waliokuwa wakisafiri na basi la kampuni ya Sai baba,kutoka Jijini Dar es salaam kwenda Masasi,mkoani Mtwara,wamenusulika kifo,kufuatia gari yao kuacha njia na kuingia vichakani.

  Tukio la ajali hiyo limetokea maeneo ya kijiji na kata ya Mbanja,iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi,Katika ajali hiyo watu watano akiwemo dereva na kondakta ndiyo waliokuwa wameumia na kukimbizwa Hospitali ya mkoa wa Lindi, Sokoine kwa matibabu.

  Waliojeruhiwa ni,Juma Mtoi (Dereva),Said Mkumbwa (Kondakta) wakazi wa Jijini Dar es salaam,na kwa upande wa abiria ni John Kasawala (21),mkazi wa kijiji cha Nangamba,wilaya ya Nanyumbu,mkoani Mtwara,Noel Akui (35) mkaazi wa wilaya ya Masasi,mkoani Mtwara na Kuruthumu Ally (25) wakazi wa mji wa Lindi.

  Said Mkumbwa ambaye ni kondakta wa basi hilo, amesema kwamba chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa tairi la mbele upande wa kulia kwa dreva, ambapo liliacha njia na kutumbukia mtoni chini ya daraja la Mbanja.

  Akasema basi lake lililokuwa limebeba abiria 45 lilikuwa likitoka Jijini Dar es salaam kuelekea wilaya ya Masasi,mkoani Mtwara,kufuatana na ruti zake.


  “Tulikuwa tikitokea Dar es salaam kwenda Masasi,kwani ndiyo ruti yetu ilivyo, na ndipo tulipofika eneo hilo mpira wa tairi ya mbele upande wa dereva likapasuka na kukosa mwelekeo kisha likagonga kingo ndogo ya daraja na kutumbukia mtoni,,,,,,,,,tunachoshukuru ni kwamba wote tumetoka tukiwa hao hakuna aliyepoteza maisha”Alisema Mkumbwa.


  Kuruthumu Ally ambaye amepata michubuko kiasi usoni na mabegani na John Kasawala aliyeumia kichwani,kwa nyakati tafauti walisema wao walikuwa wamekaa sehemu ya mbele walisema wakiwa wanaendelea na safari yao hiyo,ghafla walisikia mlio mkubwa kasha basi lao kuyumba na kutumbukia chini ya daraja.


  Akizungumza kwa niaba ya kaimu mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo,Dkt,Edgar Mlawa amesema majeruhi hao wameumia sehemu mbalimbali ya miili yao,ikiwemo vichwani na hali zao zinaendelea vizuri na kuna mategemeo ya kuweza kuendelea na safari zao kama kawaida.


  “Hapa Hospitalini wamefikishwa majeruhi watano tu,akiwemo dereva,kondakta wake na abiria watatu,mmoja wao ni mwanamke, ambapo wote hao hakuna aliyekuwa sirias kwa kuumia licha ya kupata majeraha sehemu mbalimbali ya miili yao.ikiwa ni pamoja na vichwani”Alisema Dkt,Mlawa.

  0 0

  Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukiwa katika picha ya Pamoja, muda mfupi kabla ya Iran, Syria na Korea ya Kaskazini kukaza buti na kukataa kata kata kuunga mkono kupitishwa kwa Taarifa ya Mwisho ya Mkutano wa mwisho wa Mkataba wa Biashara ya Silaha ya Biashara (ATT( , taarifa iliyokuwa na kiambatisho cha Mkataba. Ujumbe huu wa Tanzania ulioongozwa na Naibu Mwakilishi wa Kudumu, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi na ulishiriki kikamilifu katika mijidala yote iliyofanyika mchana na usiku kuhakikisha kwamba maslahi ya Tanzania yalikuwa yanazingatiwa katika Mkataba huu. Moja ya Hoja kuu ya msingi iliyosimamiwa kidete na ujumbe wa Tanzania katika majadiliano hayo ilikuwa ni kuhakikisha kwamba silaha ndogo na risasi zilikuwa zinaingizwa na kwenye mkataba huo. Juhudi hizo zilifanikisha kuingizwa kwa silaha ndogo na rasasi ingawa Mkataba huo haukupitishwa kama ilivyotarajiwa.
  Hizi ni baadhi ya silaha ambazo zinapashwa kudhibitiwa kupitia Mkataba wa Kimataifa wa Kudhibiti Biashara ya Silaha, Mkataba ambao licha ya kusubiriwa kwa hamu kubwa ulishindwa kupatikana mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya Iran, Syria na Korea ya Kaskazini, kutia ngumu na kudai kwamba Mkataba huo ambao Rais wa Mkutano wa mwisho wa Mkataba wa Kudhibiti Biashara ya Silaha ( ATT) Balozi Peter Woolcott kutaka upitishwe kwa kauli moja, haukuwa umezingatia hoja za nchi zao pamona na nchi nyingine na kwamba ulikuwa umekumbatia maslahi ya 'wakubwa' na kwa sababu hiyo walikuwa hawauungi mkono.


  0 0


  0 0

   Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar (SMZ), mama Asha Seif Idd akifungua mashindano ya tamasha la Pasaka kwa timu za netiboli yaliyofanyika katika uwanja wa Gymkhana mjini Zanzibar na kuzikutanisha timu za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Zanzibar (ZSSF)
    Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar (SMZ), mama Asha Seif Idd akifuatilia kwa makini mchezo wa netiboli wa tamasha la Pasaka kati ya ZSSF na NSSF uliofanyika kswenye uwanja wa Gymkhana mjini Zanzibar. Kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji ZSSF, Abdulwakili Haji Hfidh na Kulia ni Meneja Uwekezaji na Mipango NSSF, Abdallah Mseli na wa pili  kulia ni Mkurugenzi Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori .
   Barke Mohamed wa ZSSF (katika) akichuana na mchezaji wa NSSF Queens.
  Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Asha Seif Idd akimkabidhi ngao ya ubingwa wa michuano ya Tamasha la Pasaka, nahodha wa timu ya NSSF Queens, Pili Rashid Mogella baada ya kuifunga ZSSF 35-29.
  Naodha wa timu ya NSSF Queens, Pili Rashid Mogella akimkabidhi ngao ya ubingwa wa tamasha la Pasaka Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume baada ya kuifunga ZSSF magoli 35-29 katika mchezo uliofanyika katika viwanja vya Gymkana mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mkurugenzi Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori na Meneja Uwekezaji na Mipango NSSF, Abdallah Mseli.


  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakimpa pole Bw. Yusuf Abdallah ambaye ni mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25, katika wodi ya Sewa Haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam. kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Mhe. Hawa Ghasia.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Sewa haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Machi 31, 2013 wakimjulia hali na kumpa pole Bw. Selemani Saidi, mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25 Kushoto mwenye suti nyeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Raymond Mushi Kulia ni Daktari C.N. Mcharo wa taasisi ya Mifupa ya Moi.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Sewa haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Machi 31, 2013 wakimjulia hali na kumpa pole kijana Baqir Dhamji, mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25. Kulia ni Daktari C.N. Mcharo wa taasisi ya Mifupa ya MOI.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam wakimpa pole kijana Mohamed Ally Dhamji ambaye ni miongoni mwa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25.PICHA NA IKULU.

  0 0


  0 0  0 0
 • 03/31/13--07:12: TASWIRA TAMU
 • Ankal keshapiga taswira kibao ila ukimuuliza hivi karibuni kapata taswira ipi anayodhani ni tamu kwake atakurudisha Desemba 9 mwaka jana wakati wa sherehe za Uhuru katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam ambapo kulikuwa na burudani toka kundi la taifa la utamaduni toka Rwanda. Hizi ndizo taswira tatu tamu za Ankal za hivi karibuni. Unaruhusiwa ku-comment na kuzichambua
  0 0


  Habari Ankal,
  Napenda kuwafahamisha wadau  juu ya Blog mpya inayohusu mambo mbalimbali yanayoambatana na injili. Yakiwemo masomo mazuri ya kutujenga kiroho,nyimbo mpya za injili,video na shuhuda. 
  Tafadhali tembelea hata  mara moja kwa siku.
  HII NI KWA WOTE BILA KUJALI DINI WALA DHEHEBU

  0 0


  Ndugu Wanajumuiya wa TANROK na Watanzania wote, Kwa niaba ya uongozi - Jumuiya ya Watanzania Nchini Korea Kusini, Tunawatakieni Wanajumuiya na Watanzania wote kokote walipo, kheri, baraka, na fanaka tele kwa kusheherekea sikukuu hii ya Pasaka. Idumishe ishara ya upendo, amani na umoja, na ilete furaha kwa familia
  zenu, wapendwa wenu, ndugu zenu na jamaa wote. 
  Tafadhali pitia wavuti yetu

  HERI YA PASAKA!
  Emmanuel Lupilya.
  M/Kiti Jumuiya ya Watanzania - Korea.

  0 0

  Wasanii wa kundi la Vichekesho la Kinoko lenye maskani yake Kinondoni jijini Dar, wakiwakilisha wakati wa tamasha la utangulizi maalum kwa Uzinduzi wa huduma ya AIRTEL Yatosha lililofanyika mkoani Morogoro leo.
  Jukwaani ni mmoja wa wasanii chipukizi wa mkoni Morogoro akiwakilisha wakati Airtel wapolifanya tamasha maalum la uzinduzi wa huduma ya Airtel Yatosha mjini humo leo.
  Wakazi wa Morogoro waliendelea kujitokeza kwa wingi jukwaani kujiunga na huduma ya Airtel Yatosha kwa Kupiga  namba *149*99#,na kupokelewa vyema na wakazi wa mji huo jioni ya leo.
  Wakazi wa Morogoro walijitokeza kwa wingi jukwaani kujiunga na huduma ya Airtel yatosha kwa Kupiga  namba *149*99#.
  Sehemu ya umati wa watu waliojitokeza viawanja vya shule ya msingi Sabasaba kushuhudia shamra shamra za uzinduzi wa maalum wa huduma ya AIRTEL Yatosha mjini morogoro
  ========  =======  =======  ====
  TAMASHA LA UTANGULIZI LA AIRTEL YATOSHA LATIKISA MKOA WA MOROGORO LEO.
  Airtel yatosha yapokelewa kwa kishindo na umati wa wakazi wa morogoro waliojitokeza kwa wingi leo katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo mjini morogoro wakati Airtel ilipofanya tamasha la utangulizi leo na kutumbuizwa na wasanii wa kundi la COMEDY la KINOKO toka jijini Dar es salaam

  Akiongea wakati wa tamasha hilo la Utangulizi meneja uhusino wa Airtel Jackson Mmbando alisema “Airtel YATOSHA imefanikiwa  kupunguza gharama za mawasiliano nchini hivyo tumeamua kuingia Morogoro kwa kishindo kuanza matamasha yetu ya kutoa elimu kuhusu huduma hii ya Airtel yatosha ili wananchi waitumie na kufaidika zaidi" alisema.

   Zaidi zaidi pia tumejipanga kutoa burudani kwa wananchi kwa kufanya matamsha haya ambapo tutazunguka kila pande waliko wateja wetu ili pia kuendeleza ushkaji wetu na wateja wetu nchini Tanzania.

  0 0
 • 03/31/13--14:16: Diamond aiteka Bukoba

 • Mwananmuziki wa kizazi kipya ambae yupo juu kwa sasa katika gemu ya Bongo Flava, Diamond akipokelewa na mashabi wake mjini Bukoba baada ya kuwasili Jumamosi Marcha 30, 2013 kwa ziara yake inayoendelea kanda ya ziwa wiki hii ya Pasaka.
  Prezidah wa Bongo flava akisalimiana na mashabiki wake Mjini Bukoba wakati alipowasili akiwa njiani kuelekea Hotelini kwake ilibidi Polisi waingilie kati msafara wake kwa kusimamisha magari kuruhusu msafara wake upite na shughuli nyingine zilisimama kwa muda.

  0 0


  Leo tarehe 29 Machi 2013, mnamo saa mbili na nusu asubuhi jengo linalojengwa kwenye kiwanja namba 2032/73 Mtaa wa Indira Gandhi lilianguka kutokana na sababu ambazo bado hazijathibitishwa kitaalam na mamlaka husika. Shirika la Nyumba la Taifa linasikitika sana kutokana na kuanguka kwa jengo hilo pamoja na maafa yaliyotokana na tukio hilo la kusikitisha. Pia Shirika linatoa pole kwa wale wote waliofikwa na msiba uliotokana na ajali hii.

  Mradi huu wa ubia kati ya NHC na M/s Ladha Construction Limited ya Jijini Dar Es Salaam ulianza kutekelezwa tarehe 4 Februari 2008 ambapo Shirika la Nyumba litakuwa na hisa asilimia 25 na mbia ana asilimia 75 mara baada ya mradi kukamilika. Kwa mujibu wa sera ya ubia iliyoanza kutumika mwaka 1993 na kuhuishwa mwaka 1995 na 2005, Shirika la Nyumba la Taifa lilikuwa likitoa ardhi ambayo ilikuwa ikihesabika kama asilimia 25 ya mtaji wake kwenye jengo husika na mbia alikuwa akipata asilimia 75.

  Kwa mujibu wa mkataba huo mbia mwendelezaji M/s Ladha Contruction Limited kama walivyo wabia wengine, anapaswa kabla ya kuanza ujenzi kupata vibali kutoka kwenye mamlaka husika na kuwa na wataalam wa ujenzi na washauri waliokubalika na kuthibitishwa na mamlaka husika. Aidha, mbia huyu akishapata wataalam hao ndiye anayehusika kuingia nao mikataba ya kazi ya kujenga na kusimamia ubora wa jengo husika kwa mujibu wa sheria. Katika mradi huu mbia mwendelezaji aliajiri wataalamu wote waliosajiliwa na Mamlaka husika ambazo ni CRB, ERB, AQRB na Mansipaa husika na mamlaka nyinginezo. Kwa kuwa ujenzi ulikuwa bado haujakamilika, Shirika lilikuwa bado halijapata asilimia 25 ya umiliki wake.

  Pia tunapenda kuufahamisha Umma kuwa, Shirika la Nyumba la Taifa, lilisimamisha utoaji wa miradi mipya ya ubia mwaka 2010 ili kuweza kutathimini mafanikio na changamoto za utekelezaji wa miradi ya ubia na hivyo kuwezesha kutengeneza sera mpya. Kama sehemu ya zoezi hilo, shirika pia lilifuta jumla ya mikataba 64 ambayo ilikuwa imesainiwa lakini haijaanza ujenzi.

  Katika sera mpya ambayo utekelezaji wake utaanza hivi karibuni Shirika litahusika moja kwa moja katika kuteuwa mjenzi mtaalam (contractor), msimamizi mtaalam wa mradi husika (consultant) na kusimamia kikamilifu shughuli zote za ujenzi.

  Tunapenda kuufahamisha umma kuwa taarifa zaidi zitatolewa baada ya vyombo husika kuwasiliana na mjenzi wa mradi huu. Aidha, taarifa zinaweza kupatikana moja kwa moja kutoka M/s Ladha Construction Limited ambaye ndiye mbia mwendelezaji aliyekuwa anasimamia ujenzi huu.

  IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA JAMII
   
  S.L.P. 2977 Simu: 2851590 DAR ES SALAAM
  Telegrams : "NYUMBA" TANZANIA
  Fax 2851442


  0 0


  Kufuatia ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa 16 lililokuwa linajengwa katikati ya jiji la Dar es Salaam juzi siku ya Ijumaa Kuu tarehe 29 Machi, 2013 mpaka sasa maiti za watu 30 zimepatikana.

  Kwa mujibu wa taarifa rasmi,  watu 17 waliweza kuokolewa, wanne kati yao bado wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.  Wengine walitibiwa na kuruhusiwa.

  Kazi ya kufukua eneo la ajali inaendelea na sasa inakaribia kufikia ukingoni. 

   .

  0 0

  Promota Kinda Nangolo wa Namibia (kulia) akiagna na Rais wa IBF/Africa Onesmo Ngowi wakati akiondoka nchini humo kuelekea Botswana

  Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, Mtanzania Onesmo Ngowi amewasili katika jiji la Gaborone, Botswana kupromoti ubingwa wa IBF wa Kimataifa katika uzito wa Bantam.  
  Bondia wa Botswana Lesley Sekotswe na bondia mwenzake kutoka nchini Namibia Immanuel “Prince” Naidjala walitoka sare wakati wakishindania ubingwa huo katika pambano lililofanyika katika jiji la Windhoek, Namibia tarehe 20 Mei  mwaka huu.  
  Ujio wa Rais Ngowi ulikuwa unangojewa na wadau wengi wa ngumi katika nchi hii tangu aitembelee Botswana mwaka 2002 wakati wa mpambano kati ya bondia wa Botswana Thuso Kubamang na Peter Malinga kutoka nchini Afrika ya Kusini.  
  Rais Ngowi atakutana na viongozi wa serikali ya Botswana pamoja na wadau mbalimbali wa ngumi na safari yake itaanzia jiji kuu la Gaborone mpaka jiji la pili kwa ukubwa la Francistown ambako wadau wengi wa ngumi wanamsubiri kwa hamu.  
  Nchi ya Botswana ni nchi yenye msingi mzuri sana wa ngumi za ridhaa lakini tatizo kubwa limekuwa ni namna ya kuwaendelza wanapofikia kikomo kwenye ridhaa. Kikao cha Ngowi na viongozi wa serikali wa Botswana kitaweka msingi mzuri wa namna ya kuwaendeleza mabondia wa Botswana. 
  Botswana ni nchi inayopakana na Namibia kwa hiyo mpambano wa Sekotswe na Naidjala unategemewa kuwa na wapenzi wengi wa ngumi kutoka katika nchi hizi mbili.

  0 0
 • 03/31/13--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Ni Jumatatu ya Pasaka na Kwaya ya Kiinjilisti ya Kijitonyama wanasherehekea kwa 'Eeee Baba, kama si wewe ningekuwa wapi'.

  0 0

   Ankal na bendi yake aliyoipa jina la Orchestre les Libeneke akiwa mazoezini na vijana wake kwenye kambi ambayo kwa sasa jina kapuni kwa kuhofia wadaku. Tayari bendi hiyo ina nyimbo nne huku ikifanyia kazi mbili zaidi, kabla ya kuingia studio kurekodi. 

  Akiongea na mwandishi wetu wa maswala ya burudani kwa njia ya simu, Ankal amesema ameamua kujiingiza katika muziki kwani umo ndani ya damu yake ambapo kaka yake mkubwa Ismail ni mmoja wa waanzilishi na wanamuziki wa awali wa Dar International ya Marijani Rajabu. Pia Ankal anasema anafanya sana mazoezi na Wananjenje na hivi sasa anakaribia kuhitimu kupiga drums. 

  Hakupenda kuweka bayana bendi itazinduliwa lini na wapi, ila alisisitiza ni kabla ya SabaSaba mwaka huu. Hivi sasa anatafutwa producer mkali wa kurekodi nyimbo zao pamoja na video. Huenda wakamtumia tiketi Producer mkali Miika Mwamba aliko huko Sweden  aje ashurikiane na wakali wa nyumbani kufanya vituzzzz.
  Ankal akiwa na kijana wake Omary Makuka ambaye naye alipigia Dar International. Kwa sasa wanakamilisha nyimbo mbili za mwishio kabla ya kuingia studio. Katika hizo sita mbili ni 'Remix' ya ngoma za 
  Marijani Rajabu 'Mayasa' na 'Rosa Nenda Shule'


  0 0

  Hii ni sehemu ya kwanza kati ya mbili za mjadala kuhusu mustakabali wa Jumuiya mbalimbali za waTanzania katika DIASPORA baada ya kufunguliwa kwa matawi ya vyama mbalimbali vya siasa katika nchi husika
  Hii ni sehemu ya pili na ya mwisho ya mjadala kuhusu mustakabali wa Jumuiya mbalimbali za waTanzania katika DIASPORA baada ya kufunguliwa kwa matawi ya vyama mbalimbali vya siasa katika nchi husika.

older | 1 | .... | 85 | 86 | (Page 87) | 88 | 89 | .... | 3272 | newer