Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 864 | 865 | (Page 866) | 867 | 868 | .... | 3272 | newer

  0 0


  0 0

  TIMU ya wataalam wa biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara na wafanyabiashara wengine wa nchini Tanzania wanatarajiwa kutembelea China baadaye Julai mwaka huu, ikiwa ni katika jitihada za kutafuta fursa za ki biashara ambazo zinaweza kutumika kuleta maendeleo nchini.

  Hatua hiyo inakuja miezi michache baada ya ziara ya Rais Jakaya Kikwete nchini ambapo serikali ya China ilikubali kusaidia Tanzania katika maendeleo na uendeshaji wa Viwanda nchini.

  Akizungumza wakati wa sherehe ya kuadhimisha miaka 50 ya ziara Waziri Mkuu wa China Zhou Enlai nchini Tanzania iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dk Abdallah Kigoda alisema kuwa kuna faida kubwa sana katika uchumi wa viwanda na jopo la watalaam hao wanaotarajiwa kutembelea nchi hiyo iliyopo Mashariki ya Mbali, litasaidia kutoa utaalam juu ya fursa za kibiashara ambazo zinaweza kutumiwa na Watanzania.

  "Tutahakikisha kuwa mahusiano yetu haya kati ya China na Tanzania yanakuwa na manufaa pande zote mbili. Tumeendelea kukuza uhusiano mkubwa kati ya nchi hizi mbili na China, ambayo kwa sasa ipo kwenye safu ya nchi zenye nguvu zaidi kiuchumi duniani, imekubali ombi letu kutusaidia katika ukuaji  wa sekta ya viwanda," alisema Dk. Kigoda.

  Dk Kigoda alisema uendeshaji mzuri katika sekta ya viwanda utasaidia kuinua uchumi wa watu nchini, ikiwa ukuaji wa biashara mpya na viwanda utajenga maelfu ya ajira mpya na kutoa fursa kwa watu wenye kipato cha chini kujiinua kiuchumi.

  On hotuba yake, katika hafla hiyo, Balozi wa China nchini Tanzania Dk Lu Youqing alisema China imekuwa muwekezaji wa kigeni wa pili kwa ukubwa nchini Tanzania ikiwa imefikisha uwekezaji wa jumla ya dola za Kimarekani  bilioni 4 mwishoni mwa mwaka 2014.

  "China pia ni mbia mkubwa wa biashara nchini Tanzania ikiwa na jumla ya biashara zenye thamani ya zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 4.3,” Balozi Dk. Youqing alisema.

  Alibainisha kuwa Tanzania ni moja ya nchi tatu zilizopo kwenye mpango wa  China-Afrika wa ukuzaji wa Uwezo wa Ushirikiano katika Sekta ya Viwanda, huku Tanzania ni chachu ya kuonyesha mfano wa ushirikiano huo wa kirafiki wa China na Afrika.

  "Kama rafiki wa kweli na mbia wa kuaminika wa Tanzania, China itazingatia nguzo za ushirikiano wa China-Afrika za ukweli, matokeo halisi, mshikamano na nia njema ambazo zilianzishwa na Rais Xi Jinping," alibainisha.

  Balozi Dk Youqing alisema kuwa kutakuwa na uwekezaji zaidi wa China nchini Tanzania katika siku za  usoni hasa katika nyanja za miundombinu, mwanga/umeme na viwanda vikubwa na pamoja na habari na mawasiliano ya kisasa.

  "Uwekezaji wa China nchini utazidi kuwa na manufaa makubwa kwa serikali ya Tanzania na watu wake kwa kulipa kodi na kutengeneza idadi kubwa ya ajira za wazawa," alisema.
  Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dk Abdallah Kigoda (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa sherehe ya kuadhimisha miaka 50 ya ziara Waziri Mkuu wa China Zhou Enlai nchini Tanzania zilizofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wa Kwanza kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa Serikali ya Zanzibar, Mhe. Ali Juma Shamhuna, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Janet Mbene (wa pili kulia) na Balozi wa China nchini Tanzania Dk Lu Youqing (kulia).

  0 0

  UnaambiwanKama una sticker ya 97.3 EFM ya mwaka jana….wese la bure la kumwaga. Jana tuligawa wese Kinondoni…TSN Bamaga, Jumatano  tupo Ilala, TSN TABATA...Ushindwe wewe tu...!
  Wadau wa 97.3 EFM wakipata wese la bure katika kituo cha mafuta cha TSN Bamaga jijini Dar es salaam baada ya kukutwa na sticker ya mwaka jana ya 97.3 EFM
  Foleni katika kituo cha mafuta cha TSN Bamaga jijini Dar es salaam baada ya wadau kukutwa na sticker ya mwaka jana ya 97.3 EFM
  Wese mbele kwa mbele
  Mtangazaji wa Gardner G. Habash akiwa na wadau katika kituo cha mafuta cha TSN Bamaga jijini Dar es salaam ambao walikutwa na sticker ya mwaka jana ya 97.3 EFM na kuadhibiwa kwa kujaziwa wese full tank

  0 0

  Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa,(katikati), akipungia mkono maelfu ya wana CCM na wananchi wengine waliofika kwenye ofisi za CCM wilayani Geita Juni 8, 2015, kwa nia ya kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015; (Picha na K-VIS MEDIA)
  Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akipokea fomu za udhamini za CCM baada ya kujazwa na wananchama wa CCM wilaya ya Geita, kwenye ukumbi wa CCM wilayani humo Juni 8, 2015. Mheshimiwa Lowassa, amedhaminiwa na jumla ya wanachama 3,000 wilayuani hapo.
  Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Losassa, akiwaaga wananchi na wana CCM waliofika kumdhamini kwenye ofisi za CCM wilaya ya Chato Juni 8, 2015.


  0 0

  Na  Bashir  Yakub.

  Kisheria yapo  mazingira  ambapo  mtu  aliyeuza  ardhi  anaweza  kuidai tena  ardhi  ileile  aliyouza kutoka kwa mnunuzi na  akaipata. Na  hapa  haijalishi  kama  mnunuzi  ameiendeleza  ardhi  kwa  kiasi  gani au  amebadilisha hati na kuingia  jina  lake  na  vitu  vingine  kama  hivyo.  

  Sheria  imetoa  haki  hii  kwa  muuzaji  hasa  iwapo  masharti  katika   mkataba  wa  mauziano  yamevunjwa. Kwa  kawaida  kila  mkataba  wa  mauziano  ya  ardhi  huwa  na  masharti  ambayo  hupaswa  kutekelezwa na  kila  upande. Masharti  haya  huwa  ni  ya  msingi  na  hupaswa  kutekelezwa  vilevile  kama  ilivyokubaliwa. 

  Kuvunjwa/kukiukwa  kwake  hutoa  haki  kwa  muuzaji  kuchukua  tena  kilicho  chake yaani  kujirejeshea  umiliki  wa  ardhi. Na  hii  mara nyingi  husababishwa  na  kuingia  mikataba  kiholela  bila  kupata  ushauri  au  kusimamiwa  na  wanasheria ambao hupanga masharti  haya  kwa ufundi  usio na madhara. Hapa  chini tutaona  jambo  hilio hufanyikaje  kisheria.

  1.MUUZAJI  KUJIMILIKISHA  TENA  ARDHI  BAADA  YA  KUUZA.

  Sehemu  ndogo  ya  tatu,  kifungu  cha 73 – 76 cha  Sheria  ya Ardhi   ndivyo  vifungu  katika sheria  ya  ardhi  vinavyoeleza  kwa  urefu  namna  ya  kujimilikisha  tena  ardhi  baada  ya  kuiuza. 

   Kifungu  cha  73  kinaanza  kwa  kusema  kuwa.   mkataba  wa  mauziano  ya  ardhi  unapokuwa  umekamilika   na  mnunuzi  ameshakuwa  mmiliki  wa  ardhi  aliyonunua,  muuzaji  anaweza  kujitoa  katika  mkataba  huo   pale  ambapo  mnunuzi  atakiuka  au  kwenda  kinyume  na  masharti  au  makubaliano  katika  mkataba  huo. Maana  iliyo katika  kifungu hiki  ni  kuwa  tayari mkataba  umekamilika,  na mnunuzi  amemiliki  lile  eneo iwe  nyumba, shamba  au  kiwanja . 

  Na  amemiliki  kwa  kiwango  kuwa  mpaka hati/leseni  ya  makazi/ofa n.k   tayari  ina  jina  lake,  lakini  kuna  mambo  aliahidiana  na yule  aliyemuuzia  na  bado  hajayatekeleza  mpaka  sasa. Basi  huyu  aliyemuuzia  ana  haki ya  kudai  umiliki  au  kuchukua  tena  ile  ardhi. Anachukuaje  ile  ardhi  tutaona  hapa  chini.

  2.  SABABU  ZA  KUJIREJESHEA  UMILIKI  BAADA  YA  KUUZA.

  Sababu  kubwa za  kisheria  za  muuzaji  kujitoa  katika  mkataba  na  kujirejeshea  umiliki  ni  kutokufuatwa  kwa  masharti  au  makubaliano  yaliyo  katika  mkataba  wa  mauzo( sale  agreement).  

  Kwa  mfano  kutomaliziwa  kwa hela . Unakuta  mnunuzi  ameahidi  kuwa  atamalizia  kiwango  cha  hela  kilichobaki  ndani  ya  miezi  mitatu  tangu  siku  ya  kusainiwa  kwa  mkataba. Muda  huo  unafika  mpaka  unapita mnunuzi  hataki  kulipa  hela  na  tayari  anamiliki  eneo. Au  ni  ardhi  ya kijiji  na  ameahidi  kuiendeleza  ndani  ya muda  fulani  lakini  bado  hajafanya  hivyo na  muda  umepita sasa.  Haya  ndio  mazingira na kwa  ufupi  hii  huhusisha  kutotekelezwa  kwa yale  aliyoahidi  mnunuzi   katika  mkataba  wa mauzo si  lazima  yawe hayo  tu  niliyotaja.


  0 0
 • 06/08/15--14:35: DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI

 • 0 0

   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe leo June 8, 2015 amechukua fomu za kuomba ridhaa ya kugombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma baada ya kutangaza nia hiyo jana (Jumapili). 
  Waziri Membe akipokelewa fomu na Mkewe Dorcas mara baada ya kukabidhiwa fomu mjini Dodoma. 
  alipokelewa na makada na wafuasi wa chama hicho mjini Dodoma baada ya kukabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Oganaizesheni, Seif Khatib ambapo baada ya kupokea fomu hiyo Membe alisema; “Ninafurahi kukabidhiwa fomu hii na nina hakika kutokana na kujipima na kujiona ninafiti nafasi hii kulinganisha na waombaji wengine ni lazima tubadilishe nchi yetu kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.”

  0 0

  Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Watanzania waishio Uholanzi waliojitokeza kumlaki wakati akiwasili jijini The Hague, Uholanzi, leo Jumatatu Juni 8, 2015.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo na muhtasari wa ziara yake toka kwa Balozi wa Tanzania nchini Uholani Mhe Wilson Masilingi baada ya kuwasili The Hague leo Jumatatu Juni 8, 2015.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ICC Jaji Silvia Alejandra Fernandes de Gurmendi alipotembelea makao makuu ya mahakama hiyo jijini The Hague leo Jumatatu Juni 8, 2015.
  Rais Jakaya Kikwete akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi Mhe. Bert Koenders jijini The Hague leo Jumatatu Juni 8, 2015.  Watanzania wanaoishi nje ya Nchi wangependa serikali ijayo iendeleze na kudumisha juhudi za kuimarisha uchumi kuanzia pale ambapo Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameishia katika utawala wake.

  Jumuiya ya Watanzanzia wanaoishi nchini Uholanzi (TANE) wamemueleza Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika risala yao iliyosomwa na Makamu Mwenyekiti wa Mpito Bwana Johannes Rwanzo, ambapo Rais amepata fursa ya kuzungumza na Watanzania hao jioni ya tarehe 8 Juni2015, katika Hoteli ya Crowne Plaza, mjini The Hague .

  "Tunaomba serikali ijayo iendeleze pale utakapoishia". Amesema Bw. Rwanzo. “Tunajua kuna mambo mengi ambayo labda muda wa awamu mbili hautoshi kuyakamilisha, basi tungeomba mambo haya uweze kuyakabidhi kwenye utawala unaofuata ili waendeleze pale utakapokuwa umefikia" ameongeza.

  Bw. Rwanzo ameyataja baadhi ya mambo ambayo yanahitajika kuendelezwa na awamu ijayo kuwa ni pamoja na juhudi za kupambana na umaskini nchini na  ujenzi wa miundombinu.

  Watanzania hao pia wamemuomba Rais Kikwete kuwa, pamoja na kustaafu, bado wangependa aendelee kutoa msaada kwa wananchi wa Tanzania kwani "Kustaafu sio mwisho wa kusaidia jamii".

  Tangu kuingia madarakani, Rais Kikwete amekuwa na utaratibu wa kukutana na Watanzania wanaoishi nje ya Nchi kila anapofanya ziara katika Nchi mbalimbali na kuwaeleza maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

  Watanzania hao nao wamekuwa na jadi ya kumsomea risala, kumuuliza maswali kwa nia ya kupata  ufafanuzi wa masuala muhimu na kumpa Zawadi za aina mbalimbali.

  Rais Kikwete yuko katika ziara ya kikazi  ya  kuishukuru Nchi ya Uholanzi kwa misaada ya kimaendeleo na pia kuiomba iendelee kuisaidia Tanzania ili iweze kukamilisha na kuendeleza juhudi za kujenga na kuimarisha uchumi kwa nia ya kuleta maendeleo Tanzania.

  Rais Kikwete amepata fursa ya kuwaeleza Watanzania kuhusu uchaguzi Mkuu ujao ambao ameahidi kuwa utasimamiwa vizuri ili Watanzania wapate nafasi ya kuchagua viongozi wanaowataka.

  Rais pia  amewaeleza Watanzania kuhusu juhudi mbalimbali za maendeleo ambazo amezifanya katika kipindi cha utawala wake  ambazo zimechangia kukua kwa uchumi na Nchi kujijengea  uwezo na  kujiletea maendeleo.

  Rais ametumia fursa hiyo kuelezea jitihada zilizofanyika katika ujenzi wa barabara,  elimu, afya,  maji  na maendeleo katika teknolojia. Rais Kikwete amemaliza ziara yake katika Nchi za Finland, Sweden na Uholanzi na anatarajia kuondoka Uholanzi tarehe  9 Juni,2015 asubuhi na kuwasili Dar es Salaam jioni.

  Imetolewa na;
  Premi Kibanga,
  Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
  The Haque – Uholanzi.
  9 Juni, 2015

  0 0

  MKUU WA MKOA WA LINDI MWANTUMU MAHIZA AKIWASISITIZA WASHIRIKI WA KONGAMANO LA WANAWAKE LILILOWAKUTANISHA TAKRIBANI WASHIRIKI WANAWAKE 360 KUTOKA WILAYA 6 ZA ,KUTUMIA MAFUNZO HAYO KUJIKWAMUA KIUCHUMI KWANI MIONGONI MWA WALIYOFUNDISHWA,UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI,KILIMO CHA MWANI NA MENGINEYO AMBAPO PIA KWA KUONYESHA DHAMIRA YA DHATI YA KUMKOMBOA MWANAMKE KIFIKRA NA KIUCHUMI ALIWATAKA KUHAKIKISHA WANAJIUNGA CHF ILI WAWEZE KUPATA HUDUMA ZA MATIBABU KWA GHARAMA NAFUU,KAULI MBIU YA MAFUNZO HAYO IKIWA..MWANAMKE ANAWEZA KAMATIA FURSA..KONGAMANO HILO LILIFANYIKA HIVI KARIBUNI KWENYE SEKONDARI YA ILULU WILAYANI KILWA.
  WASHIRIKI WAKIFUATILIA KWA MAKINI RAI YA MKUU WA MKOA WA LINDI MWANTUMU MAHIZA KWENYE KONGAMANO HILO.
  MENEJA MWANDAMIZI WA MFUKO WA BIMA YA AFYA GRACE LOBULU AKITOA ELIMU YA MPANGO WA KIKOA UNAOWAHUSU ZAIDI WANAVIKUNDI WALIOSAJILIWA KAMA VILE VIKOBA,WAJASIRIAMALI NA SACCOS,KUCHANGIA HUDUMA ZA MATIBABU KWA GHARAMA NAFUU YA SHS.76800 MARA MOJA KWA MWAKA MZIMA,KWENYE KONGAMANO LA WANAWAKE WA MKOA WA LINDI LILILOKUWA NA LENGO LA KUWAJENGEA UWEZO WA KUJIKWAMUA KIUCHUMI KUTOKANA NA FURSA ZILIZOPO MKOANI HUMO,PIA ALIWASISITIZA KUWA MABALOZI WA MFUKO KATIKA KUFIKISHA ELIMU HIYO KWA WANAWAKE WENZAO. 


  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini.Prof Anna Tibaijuka pamoja na mkuu wa mkoa wa Kagera,John Mongella wakishiriki katika kazi ya utandazaji wa umeme wa REA katika shule ya sekondari ya Nyakatanga,jimbo la Muleba Kaskazini mkoani Kagera wakati wa ziara ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010 pamoja kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi
   Umeme wa REA umesambazwa kwa kasi katika jimbo la Muleba Kaskazini,kama uonekanvyo katika nyumba hii katika kijiji cha Nshamba,wilayani Muleba mkoani Kagera.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana (haonekani pichani) akikagua na kupata maelezo kuhusiana na maendeleo ya mradi wa maji katika kata ya Nshamba wilayani Muleba mkoani Kagera.
  katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo na Diwani wa CHADEMA wa kata ya Mushabago,Respikius Feruz,baada ya kuhudhuria mkutano wa hadhara katika kijiji cha Rushwa,Diwani huyo alionekana kuvutiwa mno na maneno ya Ndugu Kinana na pia alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini,Mh.Charles Mwijage kwa kazi nzuri anayoifanya jimboni mwake.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman  Kinana akikabidhi basikeli kwa ajili ya Makatibu wa CCM kata zilizopo jimbo la Muleba Kaskazini, baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara. Baiskeli hizo zimetolewa na Mbunge wa jimbo hilo Charles Mwijage (kulia).
   Katibu Mkuu wa CCM akikabidhiwa na Mbunge wa Muleba Kaskazini Mh.Charles Mwijage generata, kwa ajili ya kina mama wanaofanya shughuli za kilimo cha umwagiliaji.
    Vijana wanaofanya kazi katika mradi wa mabwawa ya kufugia samaki wa Ruhanga, katika Kijiji cha Izigo mkoani Kagera, wakiwa kazini leo .

   Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage akimpa maelezo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuhusu mradi wa mabwawa ya ufugaji samaki ya wajasiliamali, alipokagua mradi huo.
   Wananchi wa kijiji cha Izigo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa hadhara.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akisisitiza jambo alipokuwa akiwahubia wananchi wa kijiji cha Izigo,Wilayani Muleba katika mkutano wa hadhara.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahubia wananchi wa kijiji cha Izigo,Wilayani Muleba katika mkutano wa hadhara.
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kulia) wakati akimtambulisha kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana, Mhariri wa zamani wa Tanzania Daima Asbert Ngurumo, ambaye alifika kwenye mkutano wa Katibu Mkuu huyo wa CCM  uliofanyika katika kijiji cha Izigo, wilayani Muleba.

  PICHA NA MICHUZI JR-MULEBA 


  0 0

  Jumamosi ya 6 Juni 2015 inasemekana haikuwa nzuri katika kambi ya FFU -ughaibuni baada ya msimu wa joto kuanza nchini ujerumani, kikosi maalumu cha kuangalia wanyama kiliungana na Kamanda ras Makunja kumsaka Bundi wa mkuu huyo wa Ngoma Africa Band, Bundi maarufu kwa jina la udi udi alichomoka katika banda maalumu katika makao ya Ras Makunja marufu kama himaya ya Anunnaki Alien.

   Kutoroka kwa Bundi huyo kumesababishwa na mbwa wa kamanda aitwae Kopro Dogi Domobaya, mbwa huyo anashutumiwa kwa kuwa mzembe na kuupiga kikumbo mlango wa banda la Bundi na kumfanya bundi kutoroka, kamanda Ras Makunja aliwambia kikosi cha kuangalia wanyama kuwa "huyu mbwa si mlinzi mzuri siku hizi amekuwa na utoto sana ! mbwa huyu tangu ampewe zawadi ya mpira na watoto wa jirani yeye kazi yake ni kucheza na mpira mpaka kavunja banda la Bundi.

   Ras Makunja akilalamika na kudai kuwa huyu mbwa akiendelea na uzembe atamfuta kazi,Pia inasemekana midudu hiyo imetengewa eneo maalumu katika himaya ya FFU-ughaibuni, Bundi huyo baadaye alirudi mwenyewe baada ya kutoweka kwa masaa kadha.
  Kamanda ras Makunja akiwa nje ya himaya yake.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk.Ali Mohamed Shein na ujumbe waliofuatana katika ziara ya kikazi Mjini Berlin wakiwa wamesimama wakiimbiwa wimbo maalum na Wanafunzi wa Skuli ya Bruno H-Burgel Schule ya Postdam walipotembelea Skuli hiyo ambayo inaushirikiano na Skuli ya Mwanakwerekwe ya Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na ujumbe wake wakiwaangalia wanafunzi wa Skuli ya Bruno H-Burgel Schule ya Postdam wakati walipokuwa wakijibu masuala wakiwa katika moja ya madarasa skulini hapo wakiwa katika ziara Mjini Berlin nchini Ujerumani.
  Rais wa wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na ujumbe wake wakipata maelezo kutoka kwa Dr.Christoph Hauser Naibu Mkurugenzi Mkuu Idara ya Ushikiano wa Kimataifa wa Sayansi walipokuwa wakiangalia kukumbu mbali mbali walipotembelea Makumbusho ya Mjini Berlin Nchini Ujerumani wakiwa katika ziara ya kikazi.
  Rais wa wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na ujumbe wake wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Idara ya Sayansi katika Historia halisia Mjini Berlin Nchini Ujerumani wakati walipotembelea makumbusho katika Mji huo wakiwa katika ziara ya kikazi.


  0 0

  ILE Filamu kubwa iliyoshirikisha wasanii mahiri kutoka Tanzania movie Talent Top Ten 2014 (TMT) ipo tayari na inatarajia kuonyeshwa katika jumba la sinema la Mlimani City Cinema Tarehe 12.June. 2015 ni siku ya Ijumaa na itarfuka kwa siku tatu Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.

  Sinema hiyo ambayo imeshirikisha wasanii wakali wenye elimu ya uigizaji kutoka kwa wakufunzi kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam imerekodiwa katika viwango vya kimataifa ndio maana inaanza kurushwa katika majumba ya sinema na kuingia sokoni katika Dvd siku ya Jumatatu tarehe 8.June 2015.

  Filamu ya Mpango Mbaya ilitengenezwa baada ya shindano la kuibua vipaji kutoka mikoa mbalimbali kumalizika na kubaki na wasanii Bora 10 ambao walipata ofa ya kurekodi sinema hiyo ambayo imekidhi vigezo vya kimataifa ikiwa ni kampeni ya kampuni ya Proin Promotios kujenga mazingira wasanii kufika kimataifa.

  Wasanii wanaofanya sinema hiyo kuwa ni ya kipekee ni Mwanaafa Mwinzago mshindi wa milioni 50, Isarito Isaya, Aneth Peter, Tishi Abdalah, Macdolnard Mapunda, Chiki Mchoma, Kaparata Mtawana wasanii wakali kibao wanaofanya vinzuri katika tasnia ya filamu Swahilihood.

  Filamu ya Mpango mbaya kutoka kampuni ya Kizalendo ya Proin Promotions Ltd, imetayarishwa na Staford Kihore, na kuongozwa na Muongozaji mahiri wa kimataifa Karabani muandishi wa Muswada ni Novatus Nago Mugurusi ni kazi iliyojaa ujuzi wa kutukuka.

  Sinema ya Mpango Mbaya itaingia rasmi katika soko katika mfumo wa Dvd na kusambazwa na kampuni ya usambazaji ya Proin Promotions ya jijini Dar es salaam, ambaye ndio mtayarishaji mkuu, kampuni iliyojitoa kuibuka nyota wapya kutoka popote walipo Tanzania.

  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima aliwaalika Mabalozi wa nchi mbali mbali kuja kutembelea Tanzania hivi karibuni.

  Mabalozi hao kutoka Kuala Lumpur Malaysia walitembelea mbuga za wanayama za Serengeti, Ngorongoro na walifanya ziara mjini Zanzibar.

  Mabalozi hao ni Waheshimiwa Viorica na Constantin Nistor (Romania), Stephen Mubiru (Uganda), Dkt. Aziz Ponary Mlima(Tanzania), Isabela Mhlanga( Afrika Kusini), na Bwana Rogatius Shao (Naibu Balozi-Tanzania).
  Mabalozi walipowasili Kibo Palace Hotel, Arusha na kupokelewa na Naibu Waziri wa Maliasili.na Utalii Mheshimiwa Mahmud Mgimwa, Bwana Alan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA na Bwana Pascal Shelutete Meneja wa Mawasiliano na Masoko wa TANAPA.
  Sehemu ya wanyama katika Mbuga ya Serengeti, wakati walipotembelea hifadhi hiyo.
  Wakiwa kwenye uwanja wa Ndege wa JK Nyerere Walikutana na Mabalozi wengine ambao ni Balozi Thami Mseleku Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania na Balozi Chabaka Kilumanga na Mkewe walipokutana VIP Lounge kabla ya kuondoka na kurejea Kuala Lumpur.

  0 0

  Pretoria - A 27-year-old trainee pilot has died in a plane crash in north Pretoria, after apparently losing control of his microlight aircraft.

  Dawie du Toit, an instructor at the flight school Rosslyn Micro Flyers in Pretoria, was in the air on Sunday morning scouring the landscape for a missing plane, Netwerk24 reported on Monday.

  It was his colleague, Marthinus Nel, who noticed the crash scene of one of his students from the air.

  "It started burning on impact," said Du Toit.

  Adam Khatibu Makhanya, 27, was a Tanzanian student who was earning his flying hours at the flight school.

  According to Nel, who communicated with Makhanya via radio moments before the crash, the plane became uncontrollable.

  "These accidents happen very rarely. We can only speculate about what could have happened," said Nel.

  "Adam had training in Tanzania and had experience with much larger aircraft. He flew alone, because I knew he could do it. I would not have sent him out alone if I did not have full confidence in him."

  According to Conraad Naudé of the Hercules community policing forum, a security guard from Fidelity said he had seen an aircraft which looked as if it was in trouble on Saturday night.

  "We called the police and searched all night and all [of Sunday] morning," he said.

  Makhanya had joined the flight school in February.

  He wanted to get his pilot's licence, which he would have use to work on a game farm back home in Tanzania.

  SOURCE: HERE

  0 0

  Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) Tanzania, wameandaa warsha ya kuhamasisha na kujenga uwezo kwa watumishi wa Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu kujumuisha masuala ya vijana katika mipango ya Mkoa na wilaya.

  Warsha hiyo inafanyika katika vituo vya Mwanza na Musoma. Katika kituo cha Mwanza warsha inafanyika tarehe 8 na 9 Juni 2015, kituo ambacho kinajumuisha Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Geita.

  Washiriki wa warsha hii ni Makatibu Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya.
  Mgeni Rasmi Bw. Ibrahim D. Kalengo, Mtakwimu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ambae anamwakilisha Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, akitoa neno la ufunguzi kwa ajili ya warsha hiyo kuanza rasmi.
  Washiriki wa warsha kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Geita ambao ni Makatibu Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo ya siku mbili inayofanyika katika Hotel ya Gold Crest jijini Mwanza.
  Washiriki wa warsha kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Geita ambao ni Makatibu Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya wakimsiliza kwa makini mwezeshaji.


  0 0

  Na Andrew Chimisela

  Mkoa wa Morogoro umeanza maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi Mkuu wa Wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba mwaka huu.

  Maandalizi hayo yameanza jana kwa semina ya siku mbili inayotolewa kwa waratibu wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika ngazi ya Mkoa na Wilaya za Mkoa wa Morogoro.
  Semina hiyo inalenga kutoa Elimu itakayowawezesha kutekeleza jukumu hilo katika kufanikisha zoezi hilo muhimu. Mafunzo hayo yatahusisha ujazaji wa fomu zitakazotumika kwenye zoezi zima la uboreshaji la wapiga kura. 

  Aidha, yatatolewa mafunzo kwa vitendo yatakayohusu jinsi ya kutumia kifaa cha kisasa yaani Biometric Voters Registration (BVR) kinachochukua alama mbalimbali za mpiga kura kwa lengo la kuondoa uwezekano wa mtu kujiandikisha zaidi ya mara mbili.

  Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro  Dkt. Rajabu Rutengwe kupitia hotuba iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa  Mhe. John Henjewele,  aliwataka wanasemina kujifunza kwa bidii na kuhakikisha wanajua utaratibu unaotakiwa kutumika katika kuboresha daftari hilo la kudumu la wapiga kura.

  Dkt. Rutengwe alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wa Mkoa wa Morogoro kujiandikisha katika vituo vyao mara muda utakapowadia wa kufanya hivyo. “Naomba kutoa wito kwa wananchi walio na sifa ya kuwa wapiga kura Mkoani hapa waweze kujitokeza ili wajiandikishe”. Alisema.
  “Aidha, napenda kuwahakikishia kwamba Serikali Mkoani hapa imedhamiria kuhakikisha zoezi hili linafanyika kwa ufanisi mkubwa na kufanikiwa” Dkt. Rutengwe aliongeza.

  Naye Bi. Sajira Mbaga, Afisa kutoka Tume ya Uchaguzi alisema, zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa Mkoa wa Morogoro, linatarajiwa kuanza kufanyika Juni 14 mwaka huu na kuongeza kuwa Tume hiyo inaendelea na jitihada za kuondoa changamoto zilizojitokeza kwenye zoezi hili katika Mikoa mingine ambapo zoezi hili limekwisha fanyika.
  Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. John Henjewele akifungua mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura yaliyofanyika Juni 5, 2015 Katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Kulia, ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Bi Azimina Mbilinyi.
  Baadhi ya wajumbe wa mafunzo hayo wakila kiapo cha uaminifu katika utekelezaji wa zoezi ambalo liko mbele yao. Kushoto ni Hakimu Mkazi Bi. Agnes Ringo.
  Bi. Sajira Mbaga ambaye ni Afisa kutoka tume ya Taifa ya Uchaguzi, akihojiwa nawaandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
  Baadhi ya vifaa vilivyowasili Mkoani Morogoro kwa ajili ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura. Picha na Andrew Chimesela

  0 0

  Mwenyekiti wa klabu ya Gymkhana Dioniz Malinzi akipiga mpira wakati wa ufunguzi wa mchezo wa gofu kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa maktaba na vifaa vya kompyuta vya Shule ya Sekondari ya Mtakuja.

  Na Beatrice Lyimo- Maelezo

  Bahari Rotary Klabu ikishirikiana na HANSA GROUP wamefanya harambee ya tano kwa ajili ya kuchangia Shule ya Sekondari Mtakuja iliyopo Kunduchi jijini Dar es Salaam.

  Harambee hiyo iliyofanyika katika Viwanja vya Gymkhana kwa kuwa shindanisha washiriki kucheza mchezo wa Gofu kwa lengo la kukusanya kiasi cha Shilingi Milioni 40 za kitanzania kwa ajili ya kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo ikiwemo Maktaba ya shule na Maabara.

  Akizungumza na waandishi wa habari Rais wa Klabu hiyo Bw. Ally Abdallah alisema kuwa Shule ya Sekondari Mtakuja ina wanafunzi 1,141 na inakabiliwa na ukosefu wa Maabara ya mafunzo kwa vitendo, vitendea kazi, viti, meza, pamoja na madawati.

  “Tumeona changamoto nyingi zinazoikabili shule hiyo na jamii inayowazunguka hivyo tumejitolea kukabiliana nazo kwani dhima ya Bahari Rotary Club ni kubadilisha jamii kwa ujumla haswa kwa changamoto zinazojitokeza kwa wanafunzi,”

  “Mwaka huu tumejitoa kwa ajili ya Shule ya Sekondari Mtakuja ili kuwatengenezea mazingira mazuri ya kusoma kwani watoto hawa ni Viongozi wa kesho hivyo ni wajibu wetu kuwaanda” aliongeza Bw. Abdallah.

  Awali Bahari Rotary Club ilichangisha kiasi cha shilingi Milioni 20 za kitanzania kwa ajili ya ukarabati wa shule hiyo ikiwemo Uzio wa ukuta na Geti, kununua Matanki ya Maji na kuimarisha mfumo mzima wa usambazaji wa maji shuleni hapo aliongeza Bw. Abdallah

  Kwa upande wa Meneja Masoko wa HANSA GROUP Bw. Reuben Richard alifafanua kuwa Bahari Rotary Club imefanikiwa kusambaza maji safi na salama katika shule tofauti jijini Dar es salaam na kugundua kuwa shule nyingi jijini zinauhitaji maji safi na salama.

  Fuchs Oil, Eco bank, Hansa Group, Oryx Oil, Tanzania Distilleries LTD, Satuguru Travel, Car and General, R.K. Chudasama, NAS Tyres Services Ltd, Tecnowares, Scania Tanzania Limited, Spice Net, Oilcom, Minex Logistics, Bank of India and SBS (T) Ltd ni baadhi wa wadhamini waliojitokeza kudhamini mashindano hayo.

  0 0

  Tanzania National Parks has signed a Memorandum of Understanding with the Sino-Africa Joint Research Centre, Chinese Academy of Sciences whereby the duo have agreed to work together for the mutual benefit of conservation sector in the country and particularly in National Parks.

  Speaking during the official signing event, the Director General of TANAPA Allan Kijazi said that the MoU would boost and enhance higher education training through research, training, innovation, technological development and capacity building in areas of mutual interest.

  Kijazi further mentioned that the two parties would exchange experience and resources in areas such as biodiversity conservation, effective utilization of bio- resource, water pollution control, and strategies for solving conflicts with communities, tourism and environmental protection.

  On his part, the Executive Director of Sino-Africa Joint Research Centre, CAS Professor Qing Feng Wang commended the decision by TANAPA to enter into Mou with his institution believing that the move will assist TANAPA in managing better the National Parks.

  Sino-Africa Joint Research Centre had already sponsored three staff from TANAPA to attend a short course on ecology in China last year and they have also offered three Masters degree Scholarships for TANAPA staff to be implemented soon.
  Some of the TANAPA Management team posed in a group picture with a delegation from the Chinese Academy of Sciences after the official signing of the MoU between the two institutions.
  Director General of Tanzania National Parks Allan Kijazi (right) and Executive Director of Sino-Africa Joint Research Centre, Chinese Academy of Sciences Professor Qing-Feng Wang signing Memorandum of Understanding between their institutions in Arusha yesterday.

  0 0

  Recently Kaymu Tanzania had the opportunity to partner with the University of Dar-es-Salaam, in The 2015 UDBS Marketing Forum. The Forum was held on, Saturday, 6th June 2015, where potential marketers (marketing oriented students) met with the corporate practitioners.

  Kaymu Tanzania was amongst the many companies that were there on Saturday, to showcase and educate about their business. Kaymu had the opportunity to introduce its organization to students, academic staff and the general public who could in turn be potential clients as well as employees.

  Kaymu’s Country manager Erfaan Mojgani, was a special guest and speaker. He shared his experience and inspired the participants at this year’s Forum in the area of “E-COMMERCE”. He explains that, “E- commerce is the turning point to any business there is today; make use of the internet access to actually make an income for you. There a lot of platforms on the internet that you can log on and sell all your products for free.”

  Students from Institute of Finance Management (IFM), College of Business Education(CBE), University of Dodoma(UDOM), Tumaini University, St. Augustine University(SAUT), Moshi University college of Business(MUCOBS), Ruaha College, Tanzania Institute of Accounting (TIA), Kampala International University (KIU), Mzumbe University, Institute of Social Work (ISW) DSM, Open University of Tanzania (OUT), and St John’s University, DSM were present at the Forum.

  Junior Madebe, a student from the College of Business education told us with a very big smile, "This event was amazing. The speakers were brilliant and I could really connect to each and every one of them. I really hope they can make this happen at least twice a year."

  He adds, “The speech on E-commerce really appealed to me mostly because though I am an accounting major, I am also an upcoming entrepreneur. I am fascinated by the internet and countless opportunities it presents to us young entrepreneurs. If we understand it, we can really use it to develop ourselves in many ways”.
  Kaymu Tanzania's Country Manager, Erfaan Mojgani (Right), recently speaking to students at the University of Dar-es-Salaam Business School Marketing Forum held at Yombo Hall.

older | 1 | .... | 864 | 865 | (Page 866) | 867 | 868 | .... | 3272 | newer