Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

SHUKRAN KWA WOTE KUTOKA KWA WAHUSIKA WA MAZIKO YA MAREHEMU MUNA YALIYOTOKEA MILTON KEYNES, UK

$
0
0
Assalaam alaykum Dear brothers & sisters, 
Once again l would like to give thanks to everyone in the community who offered their support to Br Muna’s family and friends in many ways so our dearest FRIEND & BROTHER can rest in peace, ameen.
I would like to give special thanks to the MKMA team who worked tirelessly to ensure everything went according to plan. 
I would also like to personally thank Brother Ami Salim who held our hands from the beginning to the end of the funeral process.  May Allah SWT grant you what you desire, ameen.
Many thanks to Masjid Rawdha for their support and  many thanks to Wolverton Masjid for Kindly letting us use their facilities.
Also a very heartfelt thanks to the Bedford sisters who raised £1000 for Brother Muna. 
The passing of Br Muna has brought everyone together and strengthened our community.  Long may it continue that we are always there for one another, ameen.
There are no words I can use to thank all of you but may Allah the Almighty reward all of your efforts. Jazak Allahu kheir. Eddy
Assalaam alaykum brothers, just up date tulichozungumza Leo regarding Sadaka ya Munawar Said, as group tume decided tuchangishana kila mtu kwaniaba ya uwezo wake, kiwango chamwanzo £50, na hii Sadaka itaendelea kwa yoyote yule or me ataendoka or fariki, first tutafanya kama tulivyomchangishia Marehamu kwenye kuzika na family  than. Sadaka yake iyakayoendelea inshaAllah, chochote mfano; kujengesha kisima, kutengeneza mskiti, or any jambo la kheri. Kwa hiyo atakae wafiq ajiweke tayari by one to one me or Eddy or same account  details ref : Muna Sadaka. But remember  sio lazima, hatutaki mtu ajikalif. Shukran.
Kwa habari zaidi wasiliana na:
Abdallah Mohammed 07716607908 (UK), Mohammed 079501307276 (UK).

Kwa niaba ya wafiwa: www.salamatrust.com

SIR GEORGE KAHAMA AMBARIKI MH. MEMBE KUWANIA URAIS WA TANZANIA

$
0
0
 Mwanasiasa mkongwe nchini, Sir. George Kahama akizungumza na wana CCM na wakazi wa Lindi katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana, wakati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (wa tatu kushoto waliokaa), alipotangaza nia ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba, katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana. Wengeni (kutoka kushoto) ni Katibu wa CCM Mkoa wa Lindi, Adelina Gefi na Mke wa Waziri Membe, mama Dorcas Membe.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto), akimpongeza Mwanasiasa mkongwe nchini, Sir. George Kahama baada ya Mzee Kahama kuhutubia umati wa  wana CCM na wakazi wa Lindi katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana, wakati Mheshimiwa Membe alipotangaza nia ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba.


Mama Dorcas Membe mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe, akimpongeza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Lindi, Mzee Ali Mtopa baada ya kuhutubia umati wa  wana CCM na wakazi wa Lindi katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoani humo jana, wakati Mheshimiwa Membe (katikati), alipotangaza nia ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba.

THE NEW TELECOM COMPANY GETS A LICENSE TO ENTER THE TANZANIAN MARKET

$
0
0

The Board Chairman, Mkulima African Telecom Company Limited , MTC-AMOTEL, Professor Robert Mabele (second right) in a group Photo with other MTC-AMOTEL staffs during the award licencing ceremony held at Head Office of TCRA, Mawasiliano Tower in Dar es Salaam on Friday. Right is the CEO of MTC-AMOTEL, Dr Sinda Hussein Sinda, National Marketing Manager, Mr Edward Shigula (centre), Head of Commercial, Elibariki Massawe and Director of Legal and Corporate Affairs, Maria Mkemwa.
Professor Robert Mabele- The Board Chairman, Mkulima African Telecom Company Limited, MTC-AMOTEL receives the certificate from Director General of TCRA, Prof. John Nkoma (centre) in Dar es Salaam on Friday. Looking is TCRA Director of Legal Affairs, Ms Elizabeth Nzagi.
The Board Chairman, Mkulima African Telecom Company Limited , MTC-AMOTEL, Professor Robert Mabele- speaks with reporters in during the award licencing ceremony held at Head Office of TCRA, Mawasiliano Tower in Dar es Salaam on Friday.
TCRA Communications Manager, Mr Innocent Mungy speaks to welcome guests for the ceremony.
Professor Robert Mabele- The Board Chairman, Mkulima African Telecom Company Limited, MTC-AMOTEL clarifies a point to reporters during the ceremony.

UDSM YAWATUNUKIA TUZO DR. MENGI, MILLARD AYO, SHERIA NGOWI, DIAMOND PLATINUMZ NA ZITO KABWE

$
0
0
Mwenyekiti wa chama cha wanafunzi wanaosoma kitivo cha masoko cha chuo kikuu UDSM ( DUMA ) ndg DOcta Uliwmengu akitoa hotuba fupi ya ufunguzi wa kongamano la wanafunzi wanaosoma kitivo cha masoko na biashara lilifofanyika Jumamosi tarehe 6  hapa chuoni  UDSM na kukutanisha wanataaluma wengi pia wajasiriamali waliofanikiwa na kuweza kukutanisha vyuo mbalimbali ikwemo UDSM , IFM, CBE, na TIA
Mlezi wa chama cha wanafunzi   wanaosoma masomo ya biashara na masoko kutoka chuo kikuu UDSM Ndg David Rweikiza akiwakaribisha wanafunzi na wageni waalikwa katika Kongamano hili lilifonyika jumamosi tarehe 6 katika viwanja vya UDSM
Umati wa wanafunzi kuttoka chuo ikuu cha Dar es salaam na vyuo vya jirani ukisikiliza aamada kwa makini kutoka kwa wachangiaji mahiri na wanataluma ya masoko kwa muda mrefu wakihamasiha vijana waweze kujiaili kwa kutumia fursa nyingi za mitandao ya kijamiii

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

USHAHIDI WAKWAMISHA KESI DHIDI YA UKATILI KWA ALBINO

$
0
0
image004 (8)
Mtaalamu wa masuala ya vyombo vya habari jamii na Mkufunzi Bi Rose Haji Mwalimu (aliyesimama) wakati wa ufunguzi kijiji cha Usagara, wilayani Misungwi mkoani Mwanza hivi karibuni.

Na Modewjiblog team, Mwanza
Tabia ya watu kukwepa kutoa ushahidi mahakamani ni sababu mojawapo ya wahalifu wa mauaji ya albino kutotiwa hatiani na kuachiwa huru.

Hayo yameelezwa katika warsha zilizoendeshwa mfululizo wilayani Misungwi, Kahama na Bariadi za ushirikishwaji wa jamii katika kuzuia na kutokomeza ukatili, unyanyasaji na unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) nchini.

Wakichangia mada kuhusu changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi, washiriki wamesema kwamba imekuwa ni kawaida kwa watu kutokuwa tayari kutoa ushahidi mara wanapoitwa mahakamani kwa sababu zisizokuwa na mashiko.

Sababu hizo ni kuogopa kuuawa na wahusika na shinikizo kutoka kwa wanafamilia.
“Mara nyingi tumeshuhudia watu wanaoitwa mahakamani kutoa ushahidi hawaendi siku kesi inaposikilizwa hata kama aliandikiwa na mahakama kufanya hivyo, wengine huamua kuhama kabisa eneo analoishi kwa kukwepa lawama kutoka kwa jamii au familia na kuogopa kuuawa baada ya kugundulika kuwa katoa ushahidi,” alisema mmoja wa washiriki.

Kuachiwa kwa watuhumiwa wanaodaiwa kuhusika na ukatili hususan kukatwa viungo na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi kumezua mjadala mkubwa katika jamii kwamba jeshi la polisi haliwajibiki kikamilifu au kuhisiwa kuwa na ushirikiano wa namna fulani na watuhumiwa hao.
DSC_0577
Afisa mtetezi na ushawishi kutoka shirika linaloshughulika na watu wenye Albinism la Under The Same Sun (UTSS), Kondo Seif akisisitiza jambo kwa washiriki katika warsha ya siku tatu iliyofanyika katika kijiji cha Nyakasungwa wilayani Sengerema mkoani Mwanza hivi karibuni.

INTRODUCING: MFANO ONGOV NA IMARA BY MONI FT WALTER CHILAMBO

UJUMBE WA BI. IRINA BOKOVA, MKURUGENZI MKUU WA UNESCO SIKU YA BAHARI DUNIANI

$
0
0
Irina_Bokova
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi Irina Bokova.

DUNIA endelevu haiwezi kuwapo kama hakutakuwepo na bahari yenye kuendeleza uhai.

Miezi michache kabla ya kufanyika kwa kongamano la kihistoria la COP21 (21st Conference of the Parties to the United Nations Framework Convention on Climate Change) la kutengeneza ajenda mpya ya maendeleo endelevu, ujumbe huu ulikuwa hauna tija.

Lakini sasa ujumbe huu una tija sana na muhimu sana.
Iwe nchi iko mbali na bahari au karibu, kila nchi na kila aina ya uhai hutegemea zaidi namna bahari inavyokuwa salama na yenye kutekeleza wajibu wake wa kulea uhai.

Kiukweli bahari ni kitu muhimu katika mfumo wa hali ya hewa duniani, ikiratibu kwa namna ya kipekee mabadiliko ya muda mrefu ya hali ya hewa na mfupi na pia uwepo wa hewa mbalimbali katika anga ikiwemo oksijeni tunayovuta.

MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA MOSHI ,JAFARY MICHAEL ATOA MSAADA WA KOMPYUTA KWA SHULE YA MSINGI PASUA MJINI MOSHI

$
0
0
Msathiki Meya wa manispaa ya Moshi ,Jafary Michael akizungumza wakati wa kikao cha wazazi wa watoto wanaosoma katika shule hiyo.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi Jafary Michael akimkabidhi mwenyekiti wa Shule ya msingi Pasua Shabani Machivya msaada wa Kompyuta kwa ajili ya shule hiyo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WANANCHI WATOA MAONI JUU YA MUWSA KUOMBA KUPANDISHA BEI YA UTOLEWAJI WA HUDUMA YA MAJI KATIKA MJI WA MOSHI

$
0
0
Viongozi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa mazingira mjini Moshi,MUWSA wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama (hayupo pichani) wakati wa utolewaji wa maoni juu ya bei mpya ya huduma ya maji.
Mkuu wa mkoa a Kilimanjaro,Leonidas Gama akizungumza katika mkutano huo ulioandaliwa na EWURA.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA) Sharry Raymond.
Baadhi ya wananchi waliohudhulia mkutano huo.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

18 WATAJWA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2015

$
0
0
Baada ya zoezi la kupokea na kusahihisha fomu za washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 kukamilika, takribani washiriki 18 kutoka mikoa tofauti nchini wamefanikiwa kupita katika mchujo wa kwanza kabla ya washiriki watatu kuyaaga mashindano hayo na kubakia 15 ambao ndiyo wataingia kijijini kwa ajili ya kumpata mshindi.

akizungumza na waandishi wa habari mmoja wa majaji waliohusika katika zoezi la kusahihisha fomu za washiriki, Zephania Mugittu alisema kuwa idadi ya washiriki waliowasilisha fomu zao ni 26,500 ambapo fomu zilizokidhi viwango zikiwa 2,317 tu.

Jaji huyo aliongeza kuwa fomu za washiriki 21 ndiyo zilizovuka alama zaidi ya asilimia hamsini huku vigezo vya umri, shughuli za kilimo cha mazao ya chakula, uvuvi na ufugaji vikiwabakiza washiriki 18 wenye alama za juu kutoka mikoa tofautitofauti.

Naye Ofisa Mahusiano ya Ushawishi  wa Oxfam Tanzania  Suhaila Thawer alimalizia kwa kusema washiriki 18 wote  watatembelewa maeneo waliyopo kuhakikisha kama wanafanya kazi hizo kweli na baadae kuanza rasmi mchakato wa kumpata Mama Shujaa wa Chakula 2015.

Washiriki hao 18 ni Getrude Bundala Deonatus(35) Ukerewe Mwanza, Winnie  L. Mallya (24) Kilimanjaro Moshi, Dina Samwel Sumari (62) Meru Arusha, Tatu Ramadhani Kilua (48) Lushoto Tanga, Edna Gabriel Kiogwe (40) Ilala Dar es salaam, Neema Hilonga (35) Hanang  Manyara,  Pili Kashinje Itamba (30) Kaskazini(U), Eva Mageni Daudi (31) Bagamoyo Pwani, Hawa Athumani  Mkata (56) Masasi Mtwara, Wandutha Daud Kitoelth (48) Mkalama Singida, Shida Daudi Mwedugo (35) Chamwino Dodoma, Hellen Materu (36) Iringa Mjini, Upendo Paulo Mhomisoli (35) Njombe, Savera  Xeveri Mutahyabarwa (65) Bukoba Mjini Kagera, Carolina Humphrey Chelele (48)  Kilombero Morogoro, Stella Fabian  Masulya (42) Ukerewe Mwanza,  Regina Kapili Stephano (19)  Mpanda  Katavi, Rehema Daniel  Lukali (46) Sumbawanga Rukwa.
Jopo la Majaji, Kutoka Kulia ni Zephaniah Muggitu wa Digital Consulting Ltd, Jairos Mahenge Mhifadhi Mwandamizi wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu, Dora Myinga Mkulima na Mjasiliamali, Mwandiwe Makame Mkulima na Mfugaji, Roselyn Kaihula kutoka Ekama Development
 Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi  Oxfam akikaribisha majaji kwa ajili ya kutaja majina ya washindi watakao ingia shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

ONESHO LA SAUTU YETU MAKUMBUSHO YA TAIFA

TASWIRA MBALI MBALI ZA ZIARA YA RAIS WA ZANZIBAR, DKT. SHEIN NCHINI UJERUMANI

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Mkuu wa Idara ya magonjwa ya Tropiki Prof.Dr.med.Augustin Stich baada ya Taasisi ya Tafiti mbali mbali yakiwemo magonjwa ya Binadamu, Chuo cha Afya katika Mji wa Wurzburg kimeweza kutoa mchango mkubwa katikakupambana na maradhi ya Ebola yaliyotokea Nchi za Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakipata maelezo kutoka kwa Mario Gerth (kulia) wakati waalipotembelea katika kituo cha maonesho ya picha Spitale katika Mji wa Wurzburg picha hizo zenye kuonesha Zanzibar na Ustaarabu wa Waswahili zilizotayarishwa chini ya nusimamizi wa Dr.Stefan Oschman Mkurugenzi wa Tamasha la Muziki wa Afrika.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Mama Mwanamwema Shein (wa pili kulia) akiwa na ujumbe wake wakiangalia magari ya aina mbali mbali baada ya kupata maelezo kutoka kwa Adam Nowak M.A.Afisa anehusika na Ufundi wakati walipotembelea katika Kampuni ya Magari ya Mercedes-Benz na kuangalia magari hayo yaliyotayari kwa kuingia sokoni Mjini Wurzburg nchini Ujerumani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Mama Mwanamwema Shein (wa pili kulia) pamoja na Viongozi waliofuatana nao katika ziara ya kikazi Nchini Ujerumani wakiwa na ujumbe wake wakiangalia mashine ya gari aina ya Mercedes -Benz na kupata maelezo kutoka kwa afisa anaehusika na ufundi Adam Nowak M.A katika kampuni hiyo.

WAZIRI MAGUFULI AZIDI KUPATA WADHAMINI WENGI KATIKA MIKOA YA MWANZA NA GEITA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhiwa fomu yenye orodha ya Wadhamini waliojitokeza kumdhamini katika mbio za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama hicho kutoka kwa Katibu wa CCM Wilayani Chato Mkoani Geita.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwa katika picha na baadhi ya Wadhamini wake katika Ofisi ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Chato Mkoani Geita.
Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhiwa fomu yenye orodha ya Wadhamini waliojitokeza kumdhamini katika mbio za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama hicho kutoka kwa Katibu wa CCM Wilayani Sengerema.

HUAWEI YAENDELEA KUWEKEZA KATIKA SECTA YA ICT NCHINI TANZANIA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI Tanzania Peter Zhang, akizungumza na waandishi wa habari juu ya uwekezaji katika Tekinolojia ya ICT nchini.Mazungumzo hayo yalifanyika Makao makuu ya HUAWEI Tanzania jijini Dar es Salaam.
Tarehe 18 na 19 Juni 2015, ndani ya ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) uliopo mkoani Dar es Salaam, kampuni ya Huawei Tanzania itashirikiana na Wizara ya mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kufanya kongamano la sekta ya Teknolojia ya IT. Kongamano hili litazungumzia teknolojia mpya ya IT ikiipa kipaumbele sekta mpya ya kuhifadhi data kwa kutumia njia ya mawingu/cloud storage.

Lengo na dhumuni ya kongamano hili ni kuendelea kuwawezesha Watanzania kwa njia moja au nyingine kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. kila mmoja wetu anaelewa kua kwenye karne hii ya mawasiliano; teknolojia ya habari na mawasiliano ni muhimu sana hususani katika shughuli zetu za kila siku ziwe za kibinafsi au za kibiashara .

Kwa kupitia teknolojia ya Habati na Mawasiliano, dunia inakua connected zaid na zaid huku viwanda vilivyopo vikihitaji revamp kuhakikisha biashara inaendeshwa efficiently and sustainability.

Teknolojia ya Habari na Mawasiliano imewezesha kwa kiasi kikubwa ukuaji wa sekta mbalimbali na kufanya ongezeko la uvumbuzi wa vitu mbalimbali na hivyo kupelekea kuongezeka kwa mahitaji ya employment hususani kwa upande wa vijana Huawei Technologies Tanzania co. Ltd, imekua katika kiini cha mzunguko wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ulimwenguni ; ikiendesha shughuli zake katika kila nchi mbalimbali duniani. Huawei imejizatiti huku kuhakikisha kua kiongozi kwenye uvumbuzi wa teknolojia mpya pamoja na ukuaji na ongezeko la maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya kilimo, viwanda, biashara, ...... n.k

Kampuni ya Huawei Tanzania imewekeza nchini Tanzania kwa kiasi kikubwa na has commited zaidi kwenye ukuaji wa maendeleo ya sekta ya Habari na Mawasiliano nchini. Katika sekta hii ya Habari na Mawasiliano, kampuni ya Huawei Tanzania imelenga Zaidi kwenye upande wa elimu na mawasiliano na imeahidi kuendelea kufanya hivo.

Mwaka 1998, Kampuni ya Huawei Tanzania ilianza shughuli zake nchini Tanzania na mpaka hadi leo ina wafanyakazi Zaidi ya 315 kupelekea kufanya idadi ya watanzania kua na Zaidi ya asilimia 75. Toka ianze shughuli zake za kukuza Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hapa nchini, Kampuni ya Huawei Tanzania imekua ikishikiriana na wadau wengine mbalimbali wa ICT ikiwemo mashirika binafsi, mashirika ya uma pamoja na Serikali ya Tanzania.

Kampuni ya Huawei Tanzania inaongoza katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini Tanzania na imekua ikishirikiana na wadau wengine wa mawasiliano kama Tigo, Vodacom, Airtel, Zantel na TTCL katika kuchangia ukuaji wa individuals kwenye hii sekta (ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano).

AAR CELEBRATES WORLD ENVIRONMENT DAY AT MSASANI

$
0
0
AAR Insurance Tanzania Ltd celebrates the world environment day by involving in several environmental actions, doing cleanness along Kimweri Road, cleaning sewage channels, and removing all the abounded trashes along the road.

Speaking during the event, AAR Insurance Public Relations Officer, Mrs. Amisa Juma said, “Being one of the leading companies in Health Insurance and major contributors in Health services in the country, it is our obligation and duty to show the society how environment is vital to the human health and life”.

Mrs. Juma added “We can say we have saved human life today because, the place was neglected with loaded sewage systems, trashes thrown along the road which could cause several diseases like Malaria and Diarrhea, we needed to show the community that, it is possible to make their place a better one instead of abandoning it and only take blame to the government”.

“However we can still urge the local government as well to take care of their areas and make sure the first and major thing to acknowledge before anything should be health of the people they are leading because without it poverty is inevitable”. Concluded Mrs. Juma.
Since 1972, World Environment Day has been celebrated annually on 5th of June and it has also been UN major action to ensure proper awareness of the environment and encourage political attention.
AAR Insurance Sales Manager Mrs Tabia Massudi elaborating to the Media the importance of environment in human life.
AAR Insurance staff heading to the cleaning area at Kimweri Msasani.
AAR staff Miss Salome cleaning Kimweri area at Msasani.


Ankal na Wadau wa Globu ya Jamii, The Hague, Uholanzi

$
0
0
Ankal (wa pili shoto) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Globu ya Jamii jijini The Hague, Uholanzi, leo. 

JANUARY MAKAMBA ALIPOTANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS

$
0
0
 MBUNGE wa jimbo la Bumbuli,mjumbe wa NEC na Naibu Waziri wa wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknologia, January Makamba akizungumza wakati akitangaza nia ya kugombea nafasi ya Urais leo katika ukumbi wa mikunano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa Mbunge wa jimbo la Bumbuli,Mjumbe wa NEC na Naibu Naziri wa wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknologia, January Makamba wakati akielezea vipaumbele vyake kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo.
 Mbunge wa jimbo la Bumbuli,Mjumbe wa NEC na Naibu waziri wa wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknologia, January Makamba akizungumza na wananchi waliojitokeza kumsikiliza wakati akitangaza nia ya kugombea nafasi ya Urais katika  mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo.
 Kutoka kulia ni Baba na Mama mzazi waMbunge wa jimbo la Bumbuli,Mjumbe wa NEC na Naibu waziri wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknologia, January Makamba wakiwamsikiliza January Makamba wakati akitangaza nia ya kugombea nafasi ya Urais katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam leo.
Mbunge wa jimbo la Bumbuli,Mjumbe wa NEC na Naibu Waziri wa wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknologia, January Makamba akisalimiana na wananchi katika mkutano wa kutangaza nia ya kugombea nafasi ya Urais leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Avila Kakingo.)

Kipindi cha The Avenue TBC1- mahojiano na Gnako

NSSF yaboresha huduma za wateja wake

$
0
0
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeboresha huduma kwa wateja wake kwa kubadilisha muonekano wa ofisi zake za jijini Dar es Salaam ili kupunguza urasimu wa kutoa huduma sanjari na utaratibu wa wateja kubonyeza kitufe maalum kwaajili ya maoni ya huduma zinazotolewa.

Aidha sekta isiyo rasmi na rasmi zimeaswa kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi kwani waliojiandikisha kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii ni wachache hali inayopelekea wazee kujiingiza katika ulinzi .

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha hivi karibuni.

Alisema lengo la kuboresha ofisi hizo ni kuhakikisha wateja wanapata kile wanachokihitaji sambamba na kuondoa msongamano wa kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na mfuko huo lakini pia wamekuja na huduma nyingine muhimu kwaajili ya kupima utendaji kazi kwa wafanyakazi wanaowahudumia wateja.

Alisema sababu nyingine ya kuboresha ofisi za Dar es salaam ni kutokana na kuwa na wachama wengi ambapo asilimia 7 ya wanachama wa Mfuko huo wapo huko.

“Lakini tukishamaliza huko tutaenda mikoa mingine kuboresha ofisi na mazingira ya ofisi yawe mazuri, ili wateja wapate huduma bora na za uhakika”.

Akizungumzia suala zima la sekta isiyo rasmi na rasmi ni vyema kujiunga katika mifuko hiyo ya jamii ili waweze kujiwekea akiba na baadaye kunufaika na mafao mbalimbali kwani vijana hivi sasa wanafariki na kuwaacha wazee hali inayopelekea wazee kukosa misaada kwa tegemezi wao na kusababisha kuingia katika sekta mbalimbali ili waweze kupata fedha za kijikimu na maisha.

“wazee hivi sasa ndio wanabaki na vijana ambao ni tegemezi wanakufa hivyo ni vyema sasa kuhakikisha watu wanajiunga na mifuko ya hifadhi za jamii na kuboreshwa maisha yao “.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea juu ya Shirika lilivyojipanga kuboresha huduma za wateja wake.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume akionyesha kifaa maalum cha  maoni ya Wateja wa NSSF juu ya huduma wanazozitoa.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA TAMASHA LA BULABO KABILA LA WASUKUMA MKOANI MWANZA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akihutubia Wananchi wa Kijiji cha kisesa Wilaya ya Magu,katika sherehe za Kimila ya wasukuma zilizofanyika Mkowani Mwanza jana tarehe 7/6/2015.
Makamu wa Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akipiga Ngoma ishara ya Kuzindua Sherehe za kimila za kabila la wasukuma zilizofanyika kwenye kijiji cha kisesaWilayani Magu Mkoa wa Mwanza jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Mwenyekiti wa Machifu wa Kisukuma Charles llago Kaphipa wakati wa sherehe za Kimila za wasukuma kwenye Tamasha la bulabo katika kituo cha bujoro Mkoani Mwanza Jana Tarehe 7/6/2015.

Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images