Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 84 | 85 | (Page 86) | 87 | 88 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Pichani kati ni Mwanamuziki nguli wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Sipho Makhabane alipowasili usiku wa jana kwenye  Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa ameambatana na baadhi ya wanamuziki wenzake (hawapo pichani),tayari kwa kutumbuiza tamasha la Pasaka litakalofanyika Uwanja wa Taifa Macho 31,kulia ni Mkurugenzi wa Msama Promotions ambao ndio waandaaji wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama.


  Mwanamuziki nguli wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Sipho Makhabane akizungumza na Wanahabari wa vyombo mbalimbali mara alipowasili usiku wa jana kwenye  Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa ameambatana na baadhi ya wanamuziki wenzake (hawapo pichani),tayari kwa kutumbuiza tamasha la Pasaka litakalofanyika Uwanja wa Taifa Macho 31
  Mwanamuziki Sipho Makhabane akibadilishana mawazo na Mwanamuziki mwenzake wa nyimbo za Kiroho hapa nchini,Upendo Kilahiro,mara baada ya kuwasilia usiku wa jana kwenye  Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 
  Baadhi ya Wanamuziki wa kiroho wa kwaya ya Ambassadors of Christ ‘Kwetu Pazuri’ la Kigali, Rwanda wakizungumza na baadhi ya Wanahabari wa vyombo mbalimbali mara walipowasili mapema jana jioni kwenye  Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,tayari kwa kutumbuiza tamasha la Pasaka  litakalofanyika Uwanja wa Taifa Macho 31,ambapo pia watazindua albamu yao mpya itakayoitwa Mtegemee Yesu yenye nyimbo kama vile  Kaeni Macho, Mungu Wangu, Tugireurukundo, Ewe Ndugu, Tuombeane, Umwamini Yesu, Msalaba, Twawona, Okuswala na Huruma.
  Baadhi ya Wanamuziki wa nyimbo za kiroho wa kwaya ya Ambassadors of Christ ‘Kwetu Pazuri’ la Kigali, Rwanda wakiwasili mapema jana jioni kwenye  Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,tayari kwa kutumbuiza tamasha la Pasaka  litakalofanyika Uwanja wa Taifa Macho 31
  Mwanamuziki Ephraim Sekeleti wa Zambia ambaye  pia aliwasili jana kwa ajili ya kutumbuiza tamasha la Pasaka.Tamasha la Pasaka litafanyika kwenye uwanja wa Taifa jijni Dar es Salaam kesho na litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. 

  0 0

  Jumla ya maiti 18 zimeopolewa katika kifusi cha jengo la ghorofa zaidi ya kumi lililopromoka jana asubuhi katika mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam, idadi hiyo ya watu waliopoteza maisha ikiwa ni ya kihistoria kwa majanga ya aina hii.

  Mwili mmoja umeopolewa muda mfupi uliopita, ikiwa ni masaa kadhaa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Saidi Meck Sadik kuthibitisha mapema asubuhi kwamba miili 17 ilikuwa imepatikana baada ya kazi za uokoaji ya usiku kucha na inayoendelea hivi sasa.

  Makampuni kadhaa ya ujenzi yamejiunga katika zoezi hilo toka usiku kusaidia kuinua vifusi na kuopoa miili ya marehemu. Uwezekano wa kukuta mtu aliye hai hadi sasa ni mdogo sana wakati waokoaji wakiwa ni pamoja ya wanajeshi na vijana wa JKT wakiendelea na kazi.

  Tutaendelea kuwapa Updates kila itapobidi.

  Mola aziweke roho za marehemu mahala pema peponi - AMIN

  0 0


  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Mh. Maalim Seif Shariff Hamad akiongea jambo na viongozi wengine wakati wa Mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Chambani Pemba, Marehemu Salim Hemed Khamis (CUF),aliefariki katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam juzi.
  Taratibu za Mazishi zikiendelea.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Mh. Maalim Seif Shariff Hamad akiweka udongo kaburini.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiweka udongo kaburini.


  0 0


   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei (kushoto) akiongozana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu na  Balozi wa China hapa nchini, Lü Youqing wakati wa hafla ya uzinduzi wa CRDB China Desk.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa CRDB China Desk
   Balozi wa China hapa nchini, Lü Youqing akizungumza wakati wa uzinduzi wa CRDB Chine Desk.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu akizungumza katika hafla hiyo.
   Baadhi ya wageni waalikwa.

  MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei, amewataka wajasiriamali na wawekezaji wanaofanya biashara zao kati ya Tanzania na China, kuchangamkia fursa pana ya ukuzaji mitaji yao na pato kwa kutumia huduma mpya ya CRDB China Desk.


  Dk Kimei aliyasema hayo jana wakati wa hafla ya uzinduzi wa China Desk, inayotolewa na CRDB, itakayo wahudumia wafanyabiashara, wajasiriamali na wawekezaji wanaofanyakazi zao baina ya mataifa hayo rafiki.  “China Desk, ni huduma yenye fursa inayoweza sio tu kusaidia kukuza mitaji na kutanua wigo wa maendeleo, bali kudumisha ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo baina ya China na Tanzania, ambao uliasisiwa karibia nusu karne iliyopita,” alisema Dk Kimei katika hafla hiyo.


  Aidha, akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu, aliiomba CRDB kuboresha utoaji wa mikopo ya riba nafuu kwa wajasiriamali wadogo na wa kati, ili kuharakisha ukuaji wa pato la Mtanzania na Taifa kwa ujumla.


  Dk Nagu alibainisha kuwa, taasisi za kipesa nchini zina mchango mkubwa kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wa kati kukuza pato lao, kama zitakuwa tayari kuwapa mikopo yenye masharti nafuu na riba ndogo, ili kusaidia harakati zao za kujikwamua na kukuza uchumi wa taifa.


  “CRDB mnastahili pongezi kwa huduma hii, inayokuja wakati ambao Tanzania kama Taifa, lilimpokea rais mpya wa China, Xi Jinping katika ziara ya kikazi. Taasisi nyingine za kifedha zitambue umuhimu wa ushirikiano baina ya mataifa haya na kubuni huduma kama hizi,” alisema Dk Nagu.


  Aliongeza kwamba, kwa kuwa harakati za kumkomboa Mtanzania zimeshika kasi, huku China ikijitoa kadri iwezavyo kuisaidia Tanzania, kuna haja huduma kama hizo za China Desk zikaambatana na mikakati endelevu ya kimandeleo, na taasisi nyingine nazo zinastahili kuiga.


  Kwa upande wake, Balozi wa China hapa nchini, Lü Youqing, aliipongeza CRDB kwa kufuata nyayo za waasisi wa China na Tanzania, kiasi cha kubuni na kuzindua China Desk – dawati litakalowanufaisha wajasiriamali na wafanyabiara wa kila upande.


  “Huduma hii ni harakati chanya inayofuata nyayo za waasisi wa ushirikiano baina ya China, Rais Mao Tse Tung na Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere. Vizazi na vizazi vitabaki kujivunia na kila mmoja atajisikia yu nyumbani anapokuwa katika moja ya nchi hizo,” alisisitiza Youqing. 

  0 0

   Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa,hali ya eneo hili ndio iko namna hii kama ilivyonaswa na Mdau wa Globu ya Jamii,huku akiuliza kwamba, hivi kama hali iko hivi huku kwa "wakubwa" je kwa "kina yakhe" itakuwaje? Kweli hii ni aibu kubwa kwetu sote wakaaji wa Dar.


  0 0

  WAZIRI WA MWASILIANO,SAYANSI NA TEKNOLOJIA PROF. MAKAME MBARAWA (KUSHOTO) AKIKABIDHI MFANO WA HUNDI YA SH MIL. 307,440,000/=KWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI,DR. EMMANUEL NCHIMBI (KULIA),IKIWA NI MCHANGO WA TAASISI YA COSTECH KWA JESHI LA POLISI.KATIKATI NI MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI IGP SAID MWEMA PAMOJA NA MKURUGENZI MKUU WA COSTECH.
  MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI IGP SAID MWEMA AKIZUNGUMZA NA WAANDIHI WA HABARI KUHUSU JITIHADA ZA COSTECH KUSAIDIA UTAFITI WA JESHI LA POLISI NCHINI NA TAFITI NYINGINE,PEMBENI YAKE NI AFISA UHUSIANO WA COSTECH,BW. THEOPHIL LAURIAN PIMA
  MKURUGENZI MKUU WA COSTECH DR HASSAN MSHINDA AKIZUNGUMZA NA WAANDIHI WA HABARI KUHUSU JITIHADA ZA COSTECH KUSAIDIA UTAFITI WA JESHI LA POLISI NCHINI NA TAFITI NYINGINE.
  PICHA YA PAMOJA

  0 0


   Eneo la tukio ambapo jengo la ghorofa zaidi ya 10 liliporomoka jana asubuhi na hadi kufikia saa sita mchana leo maiti 18 zilikuwa zimeopolewa na watu wanne wakiwemo wakandarasi waliokuwa wanajenga pamoja na wahandisi wa halmashauri ya wilaya ya Ilala wanashikiliwa na polisi, wakati wawili wanaendelea kusakwa ikiwa ni pamoja na mjenzi ambaye kapewa masaa 12 kujisalimisha. Kuna habari kwamba jengo hilo refu kulia pia linajengwa na mkararasi aliyejenga hili lililoporomoka na kila aliye sehemu hii analiangalia kwa jicho la wasiwasi.
   Rais Kikwete akiwa eneo la tukio tena leo, baada ya kutembelea jana,  akitoa maagizo kwa Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova kwamba kila aliyehusika na ujenzi wa jengo hilo kuanzia mchoraji, msimamizi na mjenzi wahojiwe na wawajibishwe wakipatikana na kosa 
   Rais Kikwete akiongea na viongozi wa msikiti wa Shia ithnaasheri wakati anaondoka eneo la tukio

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mchana wa jana, Ijumaa, Machi 29, 2013, ametembelea jengo  lililoporomoka na kusababisha vifo vya watu na majeruhi kwenye Mtaaa wa Indira Gandhi/Morogoro mjini Dar es Salaam na amesikitishwa na kuhuzunishwa na maafa yaliyotokana na kuporomoka kwa jengo hilo.

  Rais Kikwete anawapa pole nyingi wafiwa, anawapa pole nyingi walioumia na wanaoendelea kupatiwa matibabu baada ya kubanwa katika kifusi, wakiwamo watoto wadogo ambao walikuwa wanacheza chini ya jengo hilo la ghorofa 16 wakati lilipoporomoka asubuhi ya jana huku likiendelea kujengwa.

  Rais Kikwete amewapongeza na kuwashukuru wananchi wote walioshiriki na wanaendelea kushiriki katika zoezi la uokoaji pamoja na vyombo na taasisi za umma na Serikali zinazoshiriki katika zoezi na kazi hiyo ya uokoaji.

  Amewataka waendelee na jitihada hizo ili kama kuna watu ambao bado wamebanwa kwenye kifusi waweze kuokolewa ili wapatiwe matibabu, na kama watakuwa wamepoteza maisha basi miili yao ipatikane na iweze kupewa mazishi ya heshima yanayostahili mwanadamu.

  Wakati alipotembelea eneo la tukio hilo, Rais Kikwete ametoa maelekezo mahsusi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mheshimiwa Saidi Mecky Sadik pamoja na Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi ya Dar es Salaam, Kamanda Suleiman Kova.

  Rais amewataka kuhakikisha kuwa Mjenzi wa jengo hilo, Mhandisi Mshauri aliyekuwa anasimamia ujenzi wa jengo hilo, Mhandisi wa Jiji la Dar es Salaam  ambaye alitoa kibali cha ujenzi na ndiye Mkaguzi wa ujenzi pamoja na mwenye Jengo wanapatikana haraka na kuwajibishwa ipasavyo.

  Aidha, Rais Kikwete amezitaka taasisi za kitaaluma zinazohusina na shughuli za ujenzi – Wachoraji Majengo, Wakadiriaji Majengo, Wajenzi, Wakandarasi na Wahandisi nazo zichunguze tukio hilo kwa haraka na kwa karibu, ili zibaini yapi yalikuwa ni matatizo na zichukue hatua kwa mujibu madaraka na mamlaka ya taasisi hizo kwa sababu zinayo madaraka na mamlaka hayo.

  Rais pia amesema kuwa wakati umefika kwa taasisi hizo sasa kujihusisha kwa karibu zaidi na matatizo yanayojitokeza katika shughuli za ujenzi kwa sababu kila yanapoporoka majengo inakuwa heshima mbaya kwa taasisi hizo. 

  Hivyo ni muhimu kwa taasisi hizo kufanya uchunguzi wa kubaini nini chanzo cha kila tukio kuanzia na lile la jana – kama ilikuwa ni udhaifu katika uchoraji, kama ilikuwa ni udhaifu katika ukandarasi, kama ilikuwa udhaifu na Ushauri ili hatua stahiki zichukuliwe.

  0 0

  Naibu Mkurugenzi Mtendaji -Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB PLC,Bw. Saugata Bandyadhiyay akiongea na waandishi wa habari na baadhi ya wageni waalikwa waliofika katika halfa ya uzinduzi wa mpango wa ushirikiano baina ya Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, Benki ya CRDB PCL na Samsung. Mpango huo unalenga kuwawezesha wateja wa CRDB nchini kujipatia simu za Samsung Galax S3,Samsung Galax note2 na Samsung Galax note 10 katika duka lolote la Vodacom na kuzilipia kwa awamu kwa kati ya miezi 12 na 24.
  Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbawara akimsikiliza Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa, wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa ushirikiano baina ya Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, Benki ya CRDB PCL na Samsung. Mpango huo unalenga kuwawezesha wateja wa CRDB nchini kujipatia simu za Samsung Galax S3,Samsung Galax note2 na Samsung Galax note 10 katika duka lolote la Vodacom na kuzilipia kwa awamu kwa kati ya miezi 12 na 24,kushoto ni Mkuu wa Vifaa vya Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Bw.Mgopelinyi Kiwanga.
  Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Tenkolojia Profesa Makame Mbawara akihutubia wakati wa kampuni ya Vodacom,Tanzania, kampuni ya Samsung na Benki ya CRDB PLC walipokuwa wakizindua mpango wa ushirikiano wa kuwawezesha wateja wao kujipatia simu aina ya Samsung Galax S3,Samsung Galax note 2 na Samsung Galax note 10 kwa malipo ya awamu kati ya miaezi 12 hadi miezi 24 ambapo wateja wa benki ya CRDB PLC watajipatia huduma hiyo katika duka lolote la Vodacom nchini..Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.

  Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.
  Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto), akigonganisha glasi na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (wa tatu), Meneja Mwandamizi wa Kampuni ya Samsung, Afrika Mashariki, Simon Kariithi (kulia) na Naibu Mkurugenzi Mwendeshaji, Undeshaji na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay, mara baada ya kuuzindua mpango wa ushirikiano wao, Dar es Salaam juzi, ambapo utamwezesha mteja kununua simu za Sumsung kwa malipo ya awamu.
  Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa, wa pili kulia, akifafanua jambo kwa Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbawara, Dar es Salaam jana, wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa ushirikiano baina ya Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, Benki ya CRDB PCL na Samsung. Mpango huo unalenga kuwawezesha wateja wa CRDB nchini kujipatia simu za Samsung Galax S3,Samsung Galax note2 na Samsung Galax note 10 katika duka lolote la Vodacom na kuzilipia kwa awamu kwa kati ya miezi 12 na 24. Kulia ni Meneja wa huduma za kibenki wa CRDB, Farida Mbwana.

  0 0


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti Muzdalifa,Sheikh Abdalla Hadhal,alipoangalia maonesho ya picha mbali mbali wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto Yatima katika Ukumbi wa Salama Bwawani leo, maadhimisho hayo yamefanywa na Shirika la I.H.H la nchini Uturuki kwa ushirikiano na Jumuiya ya Muzidalifa ya hapa Zanzibar inayoshuhulika kna Mayatima.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea zawadi kutoka kwa Mtoto Hinaina Said Khalfan,wakati wa sherehe za siku ya Mtoto yatima zilizofanyika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel leo Mjini Zanzibar,shirika la misaada la I.H.H la Uturuki,kwa Ushirikiano na jumuiya ya Muzdalifa ya hapa Zanzibar kwa pamoja wamefanikisha kufanyika kwa sherehe hizo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa hutuba yake wakati wa Sherehe ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto Yatima katika ukumbi wa Salama bwawani Mjini Zanzibar leo,maadhimisho hayo yamesimamiwa na jumuiya ya Muzidalifa na Shikika la misaada la I.H.H la Nchini Uturuki,(kushoto) makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif,Balozi wa Uturuki Nchini Ali Daudi Gul,na Waziri wa Katiba na Sheria,Abubakar Khamis Bakary,(kulia).
  Watoto Yatima waliohudhuria katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Mtoto Yatima,wakiwa katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar,zilipofanyika sherehe hizo,kwa ushirikiano wa jumuiya ya Muzdalifa na shirika la misaada la I.H.H la Nchini Uturuki leo na kuhudhuriwa na wananchi na Viongozi mbalimbali.

  BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI

  0 0


  MAHAKAMA ya Juu Kabisa nchini Kenya imeamua leo kuwa Uhuru Kenyatta alichaguliwa katika uchaguzi uliokuwa huru na wa haki,  na kutupilia mbali pingamizi lililowekwa na mgombea Raila Odinga aliyedai kwamba kura zilichakachuliwa na mashine za uchaguzi zilijaa kwikwi.

  Uamuzi huo umesafisha njia kwa Uhuru Kenyatta kuingia Ikulu. Anatarajiwa kuapishwa wiki ijayo Aprili  9, 2013 uwanja wa michezo wa Moi.  Habari zimeingia sasa hivi zinasema aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Mhe Raila Odinga amekubali uamuzi wa mahakama kuu, na kukubali yaishe (shingo upande?) kuashiria kwamba sasa mambo ni tambarare, na sio kama ilivyohofiwa awali kuwa kutatokea vurugu kama za uchaguzi wa mwaka 2007.
  “Ni uamuzi wa mahakama hii kwamba walalamikiwa wa tatu na wa nee walichaguliwa kwa haki”, alisema Jaji Mkuu wa Kenya Willy Mutunga, wakati wa kutoa uamuzi hu, akimaanisha Kenyatta na mgombea mwena na Naibu Rais William Ruto wameshinda kihalali.


  Jaji Mkuu huyo alisema mahakama imetekeleza wajibu wake katika muda huo wa kihistoria. “Sasa ni juu ya Wakenya, viongozi wao, taasisi za kijamii, sekta binafsi na vyombo vya habari kutekeleza wajibu wao kuhakikisha umoja, amani, utaifa na maendeleo ya taifa vinahifadhiwa”, aliongezea.

  Rais mteule wa Kenya huyo alimshinda mpinzani wake kwa asilimia 50.07 dhidi ya asilimia 43,28 za Odinga.


  0 0


  Yanga ya Dar es Salaam, imetoka suluhu ya 0-0 na timu ya Polisi katika mchezo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.


  Simba nayo imetoka sare ya mabao 2-2 na Toto Afrika ya Mwanza katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Kirumba jijini Mwanza.

  Katika Ligi hiyo ya Vodacom, Azam imeibuka kidedea kwa kuifunga Ruvu Stars 1- 0 katika mechi iliyochewa Uwanja wa Mabatini mjini Kibaha, Pwani. Soma habari kamili hapo...  0 0


  Dear Sir,
  We are currently conducting an exciting research which investigates the possibility of introducing a remote electronic voting system for future presidential and parliamentary elections in Tanzania. This research is expected to provide guidance to our government on how to improve its electoral system through information and communication technology.
  As part of the initial stages of this process, we would like to open up the floor for sharing ideas.  Please take a few minutes to fill-out our online survey by clicking the link below:

  Regards

  S.Kimbi

  0 0

   FRONT VIEW
  FRONT VIEW_2
   BACK VIEW WITH WATER RESERVE TANKS
  SITTING ROOM
   CEILING FANS
  CORRIDOR
  KITCHEN
    PUBLIC TOILET

     MASTER TOILET_WASHING BASIN
   MASTER TOILET

  Nyumba inapangishwa, ipo Tabata Kimanga Uwanja wa Twiga. Ni ya vyumba vitatu, kimoja master, jiko na sebule. Iko sehemu nzuri, barabara nzuri hadi getini na gari inaingia mpaka ndani ya geti. Iko kwenye muinuko, hakuna mafuriko wala maji hayajai kwenye nyumba hata mvua inyeshe kwa masaa 24! Maji ya matumizi ya ndani yapo ya uhakika muda wote, kuna 'reserve water tanks' juu na chini ya nyumba, umeme ni wa uhakika pia. Inapangishwa na fanicha zake kwa bei nafuu. We unakuja na shuka na nguo zako tu.
  UNAHITAJI? PIGA SIMU FASTA: +255 0754 290167  0 0


  Ankal,
  Kumekuwa na malumbano ya lebo.
  Binafsi nashangaa kwani sio tu zipo suti natunza lebo, ila najua kuna watu wanaweka suit juu na jeans, wengine suti bila tai, na lebo sio ushamba kwani tunajua viatu,saa, miwani, kofia, magari nk vyote vina lebo..na yote ni kusema napendelea designer fulani. Sio bei, ila kupendela kama perfume nk.
  Niliwahi kuelea kuwa ukiagiza gari mpya na utake wasiweke lebo ya model, unalipa hela ya ziada. Binafsi niliona nishai (kubana matumizi) kulipa hela hiyo..nikaacha lebo.
  Pasaka njema
  Mdau wa Lebozzz

  0 0
 • 03/30/13--11:54: mambo ya gado leo
 • Uhuru & Ruto celebrating

  0 0

  Baadhi ya Magreda yaliopo kwenye eneo lililotokea janga la kuporomoka kwa jengo lenye urefu wa ghorofa 16,mtaa wa Indra ghand katikati ya jiji la Dar es Salaam,yakiendelea na kazi ya kuondoa kifusi cha jengo hilo ili kuweza kutoa miili ya watu waliopo chini ya kifusi hicho.ambapo usiku huu wameweza kutoa miili ya watu wanne na kufanya idadi kuwa ni watu ishirini na nne (24),kwani mpaka mchana wa leo walikuwa wameweza kutoa miili ishirini (20).zoezi la kutafuta miili mingine bado linaendelea hivi sasa.
   Baadhi askari wa Kikosi cha Zima moto kutoka Kampuni ya Ulinzi ya Night Support wakimwagia maji kifusi hilo ili kilainike na kufanya uraisi kwa Magreda kuweza kutoa udongo.
   Baadhi ya Mafundi wakiendelea na kazi ya kukata nondo zilizokuwepo kwenye jengo hilo ili kuwezesha urahisi wa kubeba.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TTCL Marehemu Adolar Mapunda huko Tegeta, Dar es salaam jana Machi 29, 2013. Marehemu Mapunda, ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Standard Newspapers na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kwa mujibu wa taarifa za familia ya Mapunda, Mazishi yatafanyika Jumatatu katika makaburi ya Kinondoni. Imeelezwa pia kwamba mwili wa marehemu utaletwa nyumbani kwake kesho Jumapili.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TTCL Marehemu Adolar Mapunda huko Tegeta, Dar es salaam jana Machi 29, 2013. Marehemu Mapunda, ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Standard Newspapers na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa marehemu Adolar Mapunda huko Tegeta, Dar es salaam jana Machi 29, 2013. Marehemu Mapunda, ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Standard Newspapers na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alifariki usiku wa kuamkia jana.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiifariji familia ya marehemu Adolar Mapunda huko Tegeta, Dar es salaam jana Machi 29, 2013. Marehemu Mapunda, ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Standard Newspapers na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alifariki usiku wa kuamkia jana.
  Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TTCL Marehemu Adolar Mapunda huko Tegeta, Dar es salaam jana Machi 29, 2013. Marehemu Mapunda, ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Standard Newspapers na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mtoto wa marehemu Adolar Mapunda huko Tegeta, Dar es salaam jana Machi 29, 2013. Marehemu Mapunda, ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Standard Newspapers na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alifariki usiku wa kuamkia jana.
  Picha ya Marehemu Adolar Barnabas Mapunda.PICHA NA IKULU

  0 0

   Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam,Seraphin Lusala (kulia) akipeana mkono na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba Mwekundu Kanda ya Dar es Salaam,Haiden Ricco wakati wa kukabidhi chakula kwa ajili ya wale wanaondelea na shughuli ya uokoji wa watu waliofukiwa na kifusi cha jengo lililoporomoka jana maeneo ya katikati ya jiji la Dar.Wa pili kushoto ni Meneja Mkuu Msaidizi wa Hoteli ya Serena,Daniel Sambai.
    Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam,Seraphin Lusala (katikati) akizungumza na baadhi ya wasaidizi wa huduma ya chakula katika Ukumbi wa Taasisi ya Agha Khan Ismailia uliopo Mtaa wa Mosque,mara baadha ya kukabidhi vyakula kutoka Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jioni ya leo.
   Chakula kikiendelea kuletwa kutoka Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
   baadhi ya wasaidizi wa huduma ya chakula katika Ukumbi wa Taasisi ya Agha Khan Ismailia uliopo Mtaa wa Mosque wakihadithia namna hali ilivyo katika zoezi zima la uokoaji wa watu waliofukiwa na kifusi.
  Picha ya pamoja.

  0 0
 • 03/30/13--20:00: Ngoma azipendazo Ankal
 • KC and the Sunshine band waliturusha sana na 'That's the way i like it.

  0 0

  Asalaam alaykhum wajina,
  Nimeinasa taswira hii leo jmosi wakati naangalia taarifa ya habari ya dunia toka CNN na kuona jamaa wanaripoti kuanguka kwa jengo Tanzania na kuainisha chanzo cha habari ni ISSAMICHUZI BLOG. Hongera sana wajina hawa jamaa wamerusha habari hii kwa kujiamini wakiwa na imani imetoka katika chanzo cha habari kinachoaminika na chenye kutoa habari fasta kuliko vyote nchini.


  BLOG YA JAMII ISONGE MBELE.

  Chef Issa

older | 1 | .... | 84 | 85 | (Page 86) | 87 | 88 | .... | 3272 | newer