Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

DUNIA YATAZAMA WAKIMBIZI NYARUGUSU, WA MTABILA WAREJEA TENA

$
0
0
DSC_0015
Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma, Sospeter Christopher Boyo (aliyesimama mwenye shati la kitenge) akisoma taarifa fupi ya Kambi ya Nyarugusu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (aliyeketi mwenye suti ya kijivu) aliyeambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez mara baada ya kuwasili kwenye kambi hiyo kujionea hali halisi ya mazingira na changamoto zinazowakabili Waomba hifadhi wa Burundi na Kongo. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog). 
DSC_0072
Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (wa pili kushoto) akizungumza jambo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) huku Mkuu wa kambi mpya inayotarajiwa kuanzishwa ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile (wa nne kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa tatu kushoto) mara tu baada ya kuwasili na kusomewa taarifa kwenye kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Wengine pichani ni baadhi ya viongozi wa ulinzi na usalama wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
DSC_0038
Mkuu wa kambi mpya inayotarajiwa kuanzishwa ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe wakati akitembelea na kukagua maeneo mbalimbali ya Kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
DSC_0143
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole wakikagua sehemu wanayolala Waomba hifadhi wanaoendelea kuwasili katika kambi ya Nyarugusu ambayo inaelemewa kutokana na wingi wa Waomba hifadhi hao wanaoendelea kumiminika mjini Kigoma.
DSC_0148
Muonekano wa moja ya chumba cha kulala familia za waomba hifadhi katika kambi ya Nyarugusu ambapo kifika muda wa kulala wanatandika mkeka chini katika vumbi hilo jekundu na kupata usingizi.



HOTEL YA DOUBLETREE BY HILTON YA JIJINI DAR YAFANYA USAFI WA MAZINGIRA YANAYOIZUNGUKA HOTEL HIYO

$
0
0

Mkurugenzi mkuu wa Hotel ya Double Tree by Hilton nchini Tanzania, Bw.Ian Mclachan (wa pili kutoka kushoto) akifanya usafi katika ufukwe wa Bahari inayoizunguka Hoteli ya Double Tree huku akishirikiana bega kwa bega na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Hoteli ya Double Tree By Hilton, Bw. Yehia Elmansoury (wa kwanza kushoto).
Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Double Tree by Hilton, Bw. Florenso Kirambata(kushoto) akifanya usafi wa mazingira katika fukwe inayoizunguka hoteli hiyo ya jijini Dar es Salaam huku akiwa pamoja na mmoja wa wafanyakazi wa hoteli hiyo.
Baadhi ya uchafu uliokuwa katoka fukwe ya Bahari inayoizunguka Hoteli ya Double Tree by Hilton ya jijini Dar.
Wafanyakazi wa hoteli ya Double Tree ya jijini Dar es Salaam wakifanya usafi maeneo yote yanayoizunguka hoteli hiyo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

NAIBU KATIBU MKUU CHADEMA,ZANZIBAR SALUM MWALIM ATUNUKU VYETI KWA WANACHAMA WA CHASO MKOA WA KILIMANJARO

$
0
0
Naibu Katibu mkuu wa Chadema Taifa upande wa Zanzibar Salum Mwalimu akizungumza wakati wa mahafali ya Chaso mkoa wa Kilimanjaro yaliyofanyika katika shule ya sekondari Majengo.

Naibu katibu mkuu Chadema Zanzibar,Salum Mwalimu akitunuku yeti kwa wanafunzi wana tarajia kumaliza elimu ya chuo kikuu ambao ni wanachama wa Chaso mkoa wa Kilimanjaro.
Baadhi ya wanachama wa Chaso  kutoka vyuo mbalimbali mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katimsikiliza Naibu katibu mkuu wa Chadema taifa,upande wa Zanzibar Salum Mwalimu wakati wa sherehe za umoja huo.
Wakili wa kujitegemea Elikunda Kipoko (katikati) akisikiliza kwa makini hotuba ya Naibu katibu mkuu Zanzibar ,Salum aliyoitoa wakati wa mahafali ya kuhitimu kwa wanafunzo wa vyuo vikuu ,wanachgama wa Chaso. 

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

MHE. Dkt. PINDI CHANA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA MAWAZIRI WA JINSIA NA MAENDELEO YA WANAWAKE WA NCHI ZA SADC, NCHINI HARARE, ZIMBABWE

$
0
0
 Mhe. Dkt. Pindi Chana, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto (kushoto) pamoja na mmoja wa wajumbe kutoka Tanzania,  Bi. Costansia Gabusa, Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Jinsia wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, wakati wa Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC wanaoshughulikia masuala ya Jinsia na Wanawake, Harare Zimbabwe.
 Mhe. Dkt. Pindi Chana, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto (kushoto) akiwa na mmoja wa wajumbe kutoka Tanzania,  Bi. Costansia Gabusa, Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Jinsia, katika Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC wanaoshughulikia masuala ya Jinsia na Wanawake, Harare Zimbabwe.
 Mhe. Dkt. Pindi Chana, akiwa pamoja na Mawaziri na viongozi mbalimbali kutoka nchi za SADC wakimpokea Makamu wa Rais wa Zimbabwe, Mhe. E.D. Mnangagwa alipowasili kwa ajili ya uzinduzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC wanaoshughulikia masuala ya Jinsia na Wanawake, Harare Zimbabwe
Mhe. Dkt. Pindi Chana, (mstari wa nyuma, katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri na viongozi mbalimbali kutoka nchi za SADC walio hudhuria  Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC wanaoshughulikia masuala ya Jinsia na Wanawake, Harare Zimbabwe.Mkutano huu ulifungwa na Makamu wa Rais wa Zimbabwe, Mhe. E.D. Mnangagwa (pichani mbele, watatu kushoto)

STARS KUINGIA KAMBINI LEO

$
0
0
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ambayo inadhaminiwa na kampuni ya bia ya Kilimanjaro, leo inaingia kambini katika hoteli ya Tansoma iliyopo eneo la Gerezani kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON).

Kikosi kitakachoingia kambini kinawajumuisha wachezaji waliocheza michuano ya Cosafa nchini Afrika Kusini mwishoni mwa mwezi Mei, wachezaji 20 walioanza kambi tangu wiki iliyopita na wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nchini Congo DR.

Taifa Stars inatarajiwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Gymkana na Uwanja wa Taifa kwa muda siku mbili kabla ya siku ya alhamis kusafiiri kuelekea Addis Ababa nchini Ethiopia ambapo itaweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri.

Wachezaji wanaotarajiwa kuingia kambini leo ni Deogratias Munish, Mwadini Ali, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Haji Mwinyi, Aggrey Morris, Salum Mbonde, Erasto Nyoni, Saimon Msuva, Hassan Dilunga, Joram Mgeveke, Juma Liuzio, Said Ndemla, Mwinyi Kazimoto, Abdi Banda, John Bocco, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, Ibrahim Hajibu, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta.

Wachezaji waliopo kambini tangu wiki iliyopita ni Nadir Haroub, Juma Abdul, Salum Telela, Peter Manyika jr, Jonas Mkude, Hassan Isihaka, Mohamed Hussein, Aishi Manula, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Kelvin Friday, Malimi Busungu, Bennedict Tinoco, Rashid Mandawa, Atupele Green, Haroun Chanongo, Emmanuel Simwanda, Said Mohamed, Andrew Vicent, Gadiel Michael, Deus Kaseke.

Msafara wa Taifa Stars unatarajiwa kuondoka nchini Alhamis Juni 4, 2015 kuelekea Ethiopia ukiwa na wachezaji 23,benchi la ufundi pamoja na viongozi .

Mechi kati ya Misri dhidi ya Tanzania inatarajiwa  kuchezwa Juni 14, 2015 katika uwanja wa Borg El Arab pembeni kidogo ya jiji la Alexandria.

Wakati huo huo Tanzania imepata mwaliko wa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Rwanda kati ya Juni 6, 7 mwaka huu jijini Kigali, kwenye kumbukumbu ya mauaji ya kimbali, Tanzania itapeleka kikosi cha vijana U23 katika mchezo huo utakaochezwa mwishoni mwa wiki.

Kufuatia kupata mwaliko huo kikosi cha U23 kitaondoka nchini ijumaa tarehe 5, Juni 2015 kuelekea nchini Rwanda kikiwa na wachezaji 18 chini ya kocha Salum Mayanga.

Kocha wa Mtibwa Sugar Mecky Maxime ameongezwa kwenye benchi la ufundi litakalokwenda Ethiopia kisha nchini  Misri kufuatia kocha Salum Mayanga kuwa na timu ya U23 nchini Rwanda.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

KAMPENI YA ZUIA AJALI SASA,TOA TAARIFA MAPEMA YATUA JIJINI MWANZA

$
0
0
  Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya ziwa Dominician Mkama akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(Hawapo pichani)wakati wa kuendeleza kampeni ya kuzuia ajali barabarani inayojulikana kama“Zuia Ajali Sasa,Toa Taarifa Mapema” kupitia namba 0800757575kwa watumiaji wote wa simu ikiwa nibure kwa wateja wa Vodacom.Kampeni hiyo inayoendeshwa na jeshi la polisi  kikosi cha Usalama barabarani,Vodacom Tanzania na vyombo vya habari vya ITV/Radio one ilifanyika  katika stendi ya mabasi ya Nyegezi jijini Mwanza.
 Mkuu wa jeshi la polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza Kamanda Mohamed Likwata akiwapatia maelezo baadhi ya abiria waliokuwa wakisafiri kutoka Mwanza kwenda Bukoba kuhusiana na  kampeni ya kuzuia ajali barabarani inayojulikana kama“Zuia Ajali Sasa,Toa Taarifa Mapema”kupitia namba 0800757575kwa watumiaji wote wa simu ikiwa nibure kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Kampeni hiyo inaendeshwa na jeshi la polisi  kikosi cha Usalama barabarani kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania  na Vyombo vya habari vya ITV/Radio one ilifanyika  katika stendi ya mabasi ya Nyegezi jijini Mwanza.
 Abiria Aaron Yuda Mkazi wa jijini Mwanza(kushoto)aliyekuwa akisubiria basi la kwenda Bukoba akimfafanulia jambo maofisa wa jeshi la polisi kikosi cha Usalama Barabarani mkoani humo wakati wa zoezi la kampeni ya kuzuia ajali barabarani inayojulikana kama“Zuia Ajali Sasa,Toa Taarifa Mapema”kupitia namba 0800757575kwa watumiaji wote wa simu ikiwa ni bure kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Kampeni hiyo inaendeshwa na jeshi la polisi  kikosi cha Usalama barabarani kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania  na Vyombo vya habari vya ITV/Radio one ilifanyika  katika stendi ya mabasi ya Nyegezi jijini humo.
 Baadhi ya abiria wakiwa tayari kwa safari yao ya kwenda Bukoba mkoa wa Kagera kutoka Jijini Mwanza baada ya kupatiwa elimu na jeshi la polisi  kikosi cha Usalama barabarani kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania  na Vyombo vya habari vya ITV/Radio one kuhusiana na kampeni ya kuzuia ajali barabarani inayojulikana kama“Zuia Ajali Sasa,Toa Taarifa Mapema”kupitia namba 0800757575kwa watumiaji wote wa simu ikiwa ni  bure kwa wateja wa Vodacom Tanzania.Kampeni hiyo ilifanyika katika stendi ya mabasi ya Nyegezi jijini humo.

EMERGENCY SUMMIT OF THE EAC HEADS OF STATE ON THE SITUATION IN BURUNDI

$
0
0

Theme:One People, One Destiny

  1. THE EAST AFRICAN COMMUNITY HEADS OF STATE, THEIR EXCELLENCIES PRESIDENT JAKAYA MRISHO KIKWETE OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, PRESIDENT YOWERI KAGUTA MUSEVENI OF THE REPUBLIC OF UGANDA, PRESIDENT UHURU KENYATTA OF THE REPUBLIC OF KENYA, HON. ALAIN NYAMITWE, MINISTER OF EXTERNAL AND INTERNATIONAL COOPERATION REPRESENTING THE REPUBLIC OF BURUNDI, HON. VALENTINE RUGWABIZA, MINISTER FOR EAST AFRICAN COMMUNITY, REPRESENTING THE REPUBLIC OF RWANDA, HELD AN EMERGENCY MEETING OF THE SUMMIT OF THE EAST AFRICAN COMMUNITY HEADS OF STATE ON THE SITUATION IN BURUNDI ON 31ST MAY, 2015 AT THE STATE HOUSE CONFERENCE HALL IN DAR ES SALAAM, TANZANIA.
     
  2. THE SUMMIT WAS ALSO ATTENDED BY H.E. JACOB ZUMA, PRESIDENT OF THE REPUBLIC OF SOUTH AFRICA AND H.E. NKOSAZANA DLAMINI ZUMA, CHAIRPERSON OF THE AFRICAN UNION COMMISSION. IN ATTENDANCE WERE H.E. SAIDI DJINNIT, UNITED NATIONS SECRETARY GENERAL'S SPECIAL ENVOY FOR THE GREAT LAKES REGION; HON. MINISTERS AND ATTORNEYS GENERAL OF THE EAC PARTNER STATES; THE SECRETARY GENERAL OF THE EAST AFRICAN COMMUNITY; THE EXECUTIVE SECRETARY OF THE INTERNATIONAL CONFERENCE ON GREAT LAKES REGION; AS WELL AS REPRESENTATIVES OF THE COOPERATING PARTNERS.
     
  3. THE HEADS OF STATE AND GOVERNMENT MET IN A WARM AND CORDIAL ATMOSPHERE.
  4. THE SUMMIT RECEIVED THE REPORT OF THE MINISTERS/CABINET SECRETARIES OF THE EAC PARTNER STATES ON THE SITUATION IN BURUNDI.
     
  5. THE SUMMIT RECEIVED AND CONSIDERED THE REPORT OF THE ATTORNEYS GENERAL/MINISTERS OF JUSTICE AND CONSTITUTIONAL AFFAIRS.
  6. THE SUMMIT RECEIVED A REPORT FROM HE SAIDI DJINNIT, UN SECRETARY GENERAL SPECIAL ENVOY FOR THE GREAT LAKES REGION. THE SUMMIT COMMENDED THE EFFORTS OF THE SPECIAL ENVOY WITH THE SUPPORT OF THE EAST AFRICAN COMMUNITY, INTERNATIONAL CONFERENCE ON GREAT LAKES REGION AND THE AFRICAN UNION TO PROMOTE DIALOGUE AND URGED HIM TO CONTINUE WITH THE INITIATIVE

Benki ya Exim yazindua kampeni kuhamasisha akaunti ya Amana ya malengo.

$
0
0
Benki ya Exim Tanzania imezindua kampeni maalum ya kuhamasisha wateja wake kufungua akaunti ya amana ya malengo (Fixed Deposit Account) ikiwa sehemu ya mpango wa benki hiyo kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba miongoni mwa watanzania.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma lililopita, Meneja Bidhaa wa Benki hiyo, Bw Aloyse Maro alisema lengo kuu la kampeni hiyo ni kukuza utamaduni wa kuweka akiba hapa nchini ili kuongeza tija kwenye maendeleo ya taifa.

"Kampeni hii ina lengo la kukuza utamaduni wa kuweka akiba hapa nchini.Viwango vya ushindani vinavyotolewa na benki yetu ndio chachu ya mafanikio kwenye kampeni yetu hii kwakuwa kupitia akaunti hii wateja wetu wataweza kunufaika zaidi kwa kupata kiasi kikubwa cha faida mrejesho kutoka kwenye akaunti zao,’’ alibainisha Bw. Maro.

Katika jitihada za kuonyesha dhamira ya benki hiyo katika kuhamasisha zaidi ufunguaji wa akaunti hiyo, Bw. Maro aliongeza kuwa kampeni hiyo itaambatana na zawadi za kila mwezi kwa wateja watakaokuwa wanafungua akaunti hiyo.

"Zawadi hizi za kila mwezi ni pamoja na simu aina ya iphone. Pia tunatarajia kutoa zawadi ya gari kama tuzo kuu '' alitangaza meneja huyo kwa majigambo.

Bw.  Maro alisisitiza zaidi kuwa Benki hiyo inadhamira ya dhati katika kuhakikisha kwamba wateja wake wanapata huduma na bidhaa bora zaidi za kibenki huku pia akitumia fursa hiyo kuwashawishi wateja wa benki hiyo kufika au kuwasiliana na matawi ya benki hiyo ili kupata maelezo zaidi kuhusu kampeni hiyo.

MISA YA KUMUAGA MZEE SAMUEL LUANGISA NEW YORK

$
0
0
Naibu balozi bi Maura Mwingira akitoa pole kwa watoto wa Mzee Luangisa, Bi Maura Mwingira kwa niaba ya balozi alipata nafasi ya kuongea machache mbele ya Watanzania waliojitokeza kwenye misa hiyo ya kumuombea marehemu mzee Luangisa pamoja na kuaga mwili wake tayari kwa safari ya kwenda nyumbani Bukoba Tanzania kwa mazishi.
Mtoto wa marehem Kwame akitoa wasifu wa mzee Luangisa wasifu huo uliwatoa machozi watu kutokana jinsi mzee Luagisa alivyokuwa mtu mwenye moyo wa kutoa kwakile alichonacho bila kuchagua wala kuhoji.
Mchungaji akiongoza misa mbele ya Watanzania wa New York na miji ya karibu na New York.
Watoto wa marehem wakiwa na sura za udhuni ya kuondokiwa na baba yao mpendwa ambae alikuwa nguzo ya familia hii pendwa.
Watu wakiaaga mwili wa mzee Luangisa pamoja na misa iliyofanyika jumamosi ya tarehe 30 mwezi wa 5. Kwa picha zaidi nenda soma Hapa.

CCM MOSHI VIJIJINI WAMPONGEZA MWENYEKITI MPYA WA MJI MDOGO WA HIMO HUSSEIN JAMAL.

$
0
0
Baaadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi waliofika katika sherehe ya pongezi kwa mwenyekiti wa mji mdogo wa Himo.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Moshi vijijini Miriam Kaaya akizungumza wakatio wa sherehe za kumpongeza mwenyekiti wa mji mdpgo wa Himo ,Hussein Jamal.
Mwenyekiti mpya wa mji mdogo wa Himo ,Hussein Jamal akizungumza na wananchi waliofika katika sherehe za pongezi zilizofanyika katika ukumbi wa King size uliopo mji mdogo wa Himo. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Rais Kikwete aanza ziara ya nchi tatu Ulaya

$
0
0



 THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone:255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Kikwete aanza ziara ya nchi tatu Ulaya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Juni Mosi, 2015 ameanza ziara rasmi ya wiki moja katika nchi tatu za Ulaya kwa mwaliko wa viongozi wa nchi hizo.

Rais Kikwete ambaye aliondoka nchini usiku wa jana, Jumapili, Mei 31, 2013 baada ya kumaliza kuendesha Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Burundi ameanzia ziara yake katika Finland ambako atakaa kwa siku tatu.               

Baadaye, Rais Kikwete atatembelea nchi za Sweden na Uholanzi kabla ya kurejea nyumbani.

Katika Finland, Rais Kikwete miongoni mwa mambo mengine kesho Jumanne, Juni 2, 2015, atafanya mazungumzo rasmi ya Kiserikali na Rais wa nchi hiyo na baadaye atatembelea Bunge la nchi hiyo ambako atafanya mazungumzo na Wabunge.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
1 Juni, 2015

DCB YASHIRIKI MAONYESHO YA KAMPUNI YA EAG GROUP KATIKA HUDUMA ZAKE ZA MIKOPO YA NYUMBA

$
0
0
Afisa Masoko wa Benki ya DCB,Hildergard Nehrab akimpa maelekezo mteja aliyefika katika banda la DCB,kuhusu huduma zake za mikopo ya nyumba,kwenye maonyesho nyumba yaliyoandaliwa Kampuni ya EAG Group yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini,Dar es Salaam.
Meneja Mikopo wa Benki ya DCB,Godwin Mngulu akimpa maelekezo mteja aliyefika katika banda la DCB  kuhusu huduma zake za mikopo ya nyumba katika maonyesho nyumba yaliyoandaliwa na Kampuni ya EAG Group yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini,Dar es Salaam.Benki ya DCB inatoa mikopo ya nyumba kupitia huduma zake za Mortagage loan na micro housing loan kwa wateja wa kipato cha chini na cha kati.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katikla maonyesho ya kampuni ya EAG group yanayofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.

ASKOFU WA KANISA LA GOOD NEWS FOR ALL GADI KUFANYA MAOMBI NCHINI INDIA.

$
0
0


 Askofu wa Kanisa la Good News for all Ministry,Charles Gadi akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani ,juu ya maandalizi ya mkutano wa maombi nchini India,katika ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo ,kushoto ni katibu wa Palemo Massawe wa Kanisa la Good News for all na kulia ni mjumbe wa wa Kanisa la Good News for all Fabiani Msimbe.


Mjumbe wa wa Kanisa la Good News for all Fabiani Msimbe, akifafanua jambo Mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) juu ya kuongezeka kwa joto Duniani na athari zake 


Waandishi wa habari wakimsikiliza Askofu wa Kanisa la Good News for all Ministry,Charles Gadi hayupo pichani juu ya maandalizi  ya mkutano wa  maombi nchini IndiaPICHA NA EMMENUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Eng. Felchesmi Mramba akizungumzia mkutano wa Wafanyakazi makao makuu jijini Dar.

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESC.Eng.Felchesmi Mramba akizungumzia mkutano wa Wafanyakazi wote wa jijini Dar na Pwani kupokea kombe la mshindi wa pili wa mpira wa miguu na mbio ndefu katika mashindano ya Mei mosi yaliyoyafanyika jijini Mwanza.Mkutano huo uliofanyika tarehe 29 Mei 2015 makao Makuu ya shirika hilo Ubungo Dar Es Salaam.

NHIF YAENDELEA NA MPANGO WAKE WA KUPELEKA MADAKTARI BINGWA KATIKA MIKOA YA PEMBEZONI

$
0
0
1 
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Fatma Ali akizungumza na wananchi kabla ya kuzindua mpango wa kupeleka madaktari Bingwa katika mikoa ya pembezoni ili kuwapunguzia wananchi mzigo wa kusafiri umbali mrefu kwenda kufuata huduma hizo katika hospitali kubwa,
2
2. Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bwana Raphael Mwamoto, akitoa maelezo kuhusu mpango wa Madaktari Bingwa wanaopelekwa mikoani na Mfuko huo.
3
Baadhi ya wakazi wa Mtwara wakisubiri huduma za madaktari Bingwa,
4
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Fatma Ali akiwa katika picha ya pamoja na madaktari Bingwa baada ya kuzindua rasmi huduma ya madaktari Bingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara,
..........................................................................................................
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF unaendelea na mpango wake wa kupeleka madaktari Bingwa katika mikoa ya pembezoni ili kuwapunguzia wananchi mzigo wa kusafiri umbali mrefu kwenda kufuata huduma hizo katika hospitali kubwa. 

 Mpango huo pia unalenga kuwajengea uwezo wa kiutendaji madaktari walioko katika hospitali za mikoani ambao watafanya kazi pamoja na madaktari bingwa hao.Madaktari waliokwenda Mtwara ni pamoja na wagonjwa ya akinamama,m magonjwa ya ndani, bingwa wa upasuaji na bingwa wa dawa za usingizi.Zoezi hilo litadumu kwa muda wa siku sita.

Akizindua zoezi hilo Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mtwara Bi. Fatma Ali amewahimiza wananchi wa mkoa wa Mtwara kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii CHF ili kuujengea uwezo zaidi Mfuko huo kupeleka huduma za kibingwa katika mikoa mingi zaidi.

JAJI ANTONY BAHATI KUZIKWA LEO MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR

$
0
0
Mwili wa marehemu ukiwasili nyumbani.
 Watoto wa marehemu wakiwa na huzuni mara baada ya mwili kuwasili nyumbani.
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa Jaji mstaafu, Antony Bahati nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam. Mazishi ya jaji Bahati yanafanyika leo Juni 2 katika makaburi ya Kinondoni. (Picha na Francis Dande)
 Baadhi ya waombolezaji.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

TAASISI YA UTT-PID CHINI YA WIZARA YA FEDHA YAPANUA BARABARA ENEO LA MRADI WA VIWANJA LINDI

$
0
0
 Muonekano wa viwanja vya Mabano vilivyopimwa na Taasisi ya UTT-PID kwa ushirikiano na Halmashauri vilivyopo Manispaa ya Lindi.

Baada ya kupima na kufanikiwa kuuza viwanja zaidi ya 2,500 katika fukwe za Mabano na Mmongo kwa ushirikiano na Manispaa ya Lindi, Mradi huo umeingia katika hatua ya upanuzi wa barabara kuu na za mitaa ndani ya mradi ambapo kwa ushirikiano huo zaidi ya Shilingi Billion 1 zinatarajiwa kutumika mpaka kukamilika kwake.

Mradi huo mkubwa zaidi nchini katika upimaji wa viwanja Manispaa ya Lindi ulifadhiliwa na Taasisi ya UTT-PID utekelezaji wake ulianza mapema mwaka 2013 na sasa uaandaji wa hati kwa wanunuzi upo katika hatua ya mwisho baada ya kila mteja wa kiwanja kufanikiwa kuweka saini kwa hati zao katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na Lindi kwenyewe.
 Uchongaji wa hatua za awali wa Barabara ukiendelea katika eneo la Mradi. Ujenzi wa barabara hizi unatarajia kukamilika kabla ya wanunuzi kuuanza ujenzi wa makazi yao katika eneo la mradi.
Uwekezaji huo ukiendelea pia Taasisi hiyo kwa ushirikiano huo na Halmashauri ya Lindi inatarajia kuingia katika awamu ya pili ya Mradi wa upimaji viwanja katika fukwe hizo ambapo zaidi ya viwanja elfu tano vitapimwa na kuuza kwa wananchi wote. Utekelezaji wa awamu ya pili bado upo kwenye hatua za awali na unatarajia kuuanza ndani ya mwaka huu 2015.
 Viwanja vya Mabano na Mmongo vipo katika fukwe nzuri na vikipata upepo mwanana kutoka bahari ya Hindi.

Toka kuanzishwa kwake Taasisi ya UTT-PID imejikita sana katika upimaji wa maeneno katika mikoa mbalimbali kwa kushirikiana na Halmashauri tofauti nchini. Miradi mikubwa kama ya Bukoba ambapo viwanja zaidi ya 5,000 vilipima kuuzwa, Halmashauri ya Sengerema kwa ushirikiano na Taasisi ilipima zaidi ya viwanja 1,200 na uuzaji pamoja na uwekezaji katika Miundombinu husika unaendelea kwa kasi. Pia Taasisi imewekeza katika miradi binafsi kama vile eneo la Mapinga katika wilaya ya Bagamoyo huku ikatarajia uwekezaji mkubwa zaidi katika mikoa ya Morogoro , Arusha, Dar es Salaam, Maswa, Pwani, Maswa na Ruvuma.
 Upanuzi huu wa barabara utafanyika mpaka kwenye fukwe kuwapa nafasi wakazi wa eneo husika kutembelea maeneo ya fukwe hizo
Zaidi ya viwanja 2,500 vilipimwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali kama vile Makazi, Biashara, Maeneo ya Umma na sehemu za kupumzika. (Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog).

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI WASHIRIKI KIKAO KAZI CHA UTAYARISHAJI WA MPANGO WA MANUNUZI WA WIZARA WA MWAKA 2015/2016 MJINI MOROGORO

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mwamini Malemi wa nne kutoka kulia  akiwa pamoja na Wakuu wa Taasisi zote za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi waliohudhuria Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Manunuzi wa wizara wa mwaka 2015/2016 kilichoanza leo katika hoteli ya Oasis mjini Morogoro, watatu kutoka kushoto ni Kamishna wa Lojistiki na Fedha wa Jeshi la Polisi Clodwig Mtweve, wa pili kushoto ni Kamishna wa Fedha wa Jeshi la Magereza Sanga, waliosimama nyuma ni baadhi ya Wakurugenzi Wasaidizi wa wizara, Maafisa Bajeti pamoja na Maafisa Ununuzi wa wizara .
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mwamini Malemi akisalimiana na Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Edwin Makene baada tu ya kupokelewa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi cha wizara hiyo Manyama Mapesi akielekea kufungua Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Manunuzi wa wizara wa mwaka 2015/2016 kilichoanza leo katika hoteli ya Oasis mjini Morogoro.
 Sehemu ya wajumbe wa Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Manunuzi wa Wizara ya Mambo  ya Ndani ya Nchi wa mwaka 2015/2016  kinachowahusisha Maafisa Bajeti, Manunuzi, Wakurugezi, Wakurugenzi Wasaidizi na Wakuu wa Taasisi zote za wizara hiyo kilichoanza leo katika hoteli ya Oasisi mjini Morogoro , wa kwanza kushoto  ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Usajili wa Vyama Marlin Komba, anayefuatia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Joyce Momburi na Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokaoji Maria Kulaya.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mwamini Malemi akisoma hotuba yake wakati akifungua Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Manunuzi wa Wizara ya Mambo  ya Ndani ya Nchi wa mwaka 2015/2016  kinachowahusisha Maafisa Bajeti, Manunuzi, Wakurugezi, Wakurugenzi Wasaidizi na Wakuu wa Taasisi zote za wizara hiyo kilichoanza leo katika hoteli ya Oasisi mjini Morogoro.
 Kamishna wa Lojistiki na Fedha wa Jeshi la Polisi Clodwig Mtweve akitoa Neno la Shukrani kwa niaba ya Wajumbe wote wa Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Manunuzi wa Wizara ya Mambo  ya Ndani ya Nchi wa mwaka 2015/2016 baada ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mwamini Malemi kufungua Kikao Kazi hizo katika hoteli ya Oasisi mjini Morogoro, wa kwanza kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Manunizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Manyama Mapesi.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mwamini Malemi wa nne kutoka kulia  akiwa pamoja na Wakuu wa Taasisi zote za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi waliohudhuria Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Manunuzi wa wizara wa mwaka 2015/2016 kilichoanza leo katika hoteli ya Oasis mjini Morogoro.

WANANCHI MANISPAA YA MOSHI WAALIKWA KUTOA MAONI JUU YA OMBI LA MUWSA KUBADILI BEI YA KUTOA HUDUMA YA MAJI.

$
0
0

Na Dixon Busagaga.Moshi.

MAMLAKA ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA) inakusudia kuongeza bei ya kutoa huduma za maji kwa watumiaji wake ,lengo likiwa ni kutaka kuendelea kufanya maboresho katika utolewaji wa huduma hiyo.

Kwa mujibu wa ombi Na,TR-W-15-008 kutoka Muwsa kwenda Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji(EWURA) Mamlaka ya maji safi na maji  taka mjini Moshi imetaka kuongeza beo ya huduma zake kwa mwaka 2015/2016 HADI 2017/2018.

Mabadiliko ya bei hiyo inayopendekezwa itawahusu makundi mbalimbali ya watumiaji wa huduma hiyo hususani wale wa majumbani,Taasisi,Biashara ,Viwanda na wale wa kwenye Vioski.

Mapendekezo mapya ya bei ya utolewaji wa huduma hiyo kutoka kiasi cha sh 495 kwa  Uniti moja ya ujazo wa maji ilivyo sasa hadi kufikia 710 katika kipindi cha mwaka 2015/2016 na kiasi cha sh  746 kipindi cha mwa 2016/2017 kwa wateja wa majumbani na taasisi.

Kwa upande wa Biashara ,Muwsa imependekeza bei ya huduma hiyo kuwa ni kiasi cha sh  839 kwa uniti moja kipindi cha 2015/2016,n ash 881 kipindi cha mwak 2016/2017 kutoka kiasi cha sh 585 katika ,kipindi cha mwa 2014/2015.

Eneo jingine ni kwa watumiaji wa viwandani ,ambao Muwsa imepndekeza bei ya huduma kuwa ni kiasi cha sh 947 katika kipindi cha mwaka 2015/2016 hadi kufikia kiasi cha sh 994 mwaka 2016/2017 kutoka 660 za sasa.

Nao wamiliki wa vioski  bei iliyopendekezwa ni kiasi cha sh 696 katika kipindi cha mwa 2015/2016 hadi kufikia 731 katika kipindi cha mwala 2016/2017 kutoka kiasi cha sh 485 bei ya sasa.

Kutokana na hali hiyo mamlaka ya udhibiti wa wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeandaa mkutano na wananchi wa manispaa ya Moshi ili kutoa maoni yao juu ya ongezeko la bei za huduma za maji .

Mkutano huo unatarajia kufanyika June 4 mwaka huu ,kuanzia majira ya saa 4 asubuhi , katika ukumbi wa Hindu Mandal uliopo jirani kabisa na kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani cha mjini Moshi.

Mgeni rasmi katika mkutano huo anatazamiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama.

ALI KIBA & ABDU KIBA KUWARUSHA LIVE WASHINGTON DC JUMAMOSI HII JUNI 6

$
0
0

KWA MARA YA KWANZA SHOW YA AINA YAKE KATI YA WANA NDUGU WAWILI ALI NA ABDU KIBA ITAFANYIKA WASHINGTON DMV,JUMAMOSI HII PALE FIRE STATION 1, 8131,GEORGIA AVENUE,DOWN TOWN SILVER SPRING,VIP PACKAGE ZINAPATIKANA,FREE PARKING
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images