Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live

MWANAHABARI DEOGRATIAS MONGELA ALIVYO UKACHA UKAPERA

$
0
0
 Deogratias Mongela akiwa na mke wake Elizabeth Sanga wakati wa hafla ya ndoa yao iliyofanyika Hoteli ya Atriums iliyopo Sinza Afrikasana baada ya kufunga ndoa Katika Kanisa la Katoliki, Parokia ya Mbezi Luis Dar es Salaam jana.
 Maharusi hao (katikati) wakiwa na wapambe wao kwenye hafla hiyo. Kushoto ni Cobson Nzige na mke wake Subira Nzige (kulia), 'hakika wamependeza si mnawaona'.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo akimpongeza bwana harusi Deogratias Momgela baada ya kuoa. Wengine ni wafanyakazi wa kampuni hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo (katikati), akijumuika na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo. Kushoto ni Mhariri, Amrani Kaima na Oscar Ndauka wa kampuni hiyo.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

TRENI YA DELUXE ILIYOPANGWA KUONDOKA LEO SAA 2 USIKU IMEAHIRISHWA HADI KESHO JUMATATU SAA MBILI USIKU!

$
0
0
UONGOZI WA KAMPUNI YA RELI TANZANIA UNASIKITIKA KUWATAARIFU ABIRIA WA TRENI YA DELUXE YA KWENDA KIGOMA LEO JUMAPILI MEI 31, 2015, KUWA SAFARI HIYO IMEAHIRISHWA HADI KESHO JUMATATU SAA MBILI USIKU! 

TAARIFA HIYO IMEELEZA KUWA SABABU ZA KUAHIRISHWA SAFARI HIYO NI AJALI YA TRENI YA MIZIGO ILIYOTOKEA JANA SAA 2 USIKU KATIKA STESHENI YA SARANDA AMBAPO MABEHEWA 4 YAMEPINDUKA ! TAYARI WAHANDISI NA MAFUNDI WA TRL WANAELEKEA ENEO LA KWA KAZI YA KUYAINUA NA PIA KUKARABATI  NJIA!

ATAYESOMA TAARIFA HII AMUARIFU NA MWENZAKE!
UONGOZI WA TRL UNASIKITIKA KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA!

IMETOLEWA NA AFISI YA UHUSIANO KWA NIABA YA KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI MHANDISI ELIAS MSHANA 
DAR ES SALAAM 
MEI  31 , 2015

NSSF YAENDESHA ZOEZI LA UPIMAJI AFYA WAKAZI WA MANISPAA YA MOSHI

$
0
0


Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii(NSSF) limeendelea na zoezi la upimaji afya kwa wananchi, Zoezi hili lililoanzia mkoani Tanga limeendelea kwenye manispaa ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
Zoezi lililofanyika kwa siku tatu mfululizo limekuwa la mafanikio kwa kuweza kuwafikia watu zaidi ya 900 .
Huduma zilizo kuwa zikitolewa kwenye zoezi ni pamoja na:
Upimaji wa Shinikizo la damu
Upimaji wa sukari kwenye damu- Kisukari
Upimaji wa hali ya lishe (Uwiano wa Urefu kwa uzito)
Ushauri wa kitaalam kwa watakaokutwa na Matatizo 
Ushauri nasaha  na upimaji hiari wa VVU (UKIMWI)
Kutoa vipeperushi vya Maelezo ya uboreshaji wa Afya.
Uchangiaji wa damu kwa Hiari.

Huduma  zote hizi zitatolewa na NSSF, BURE.
NSSF inaendelea kuwasii na kuwahimiza wakazi wa Manispaa ya Moshi kuwa waendelee kujiandikisha kwenye NSSF HIARI Scheme. NSSF HIARI Scheme ni kwa ajili ya wajasiriamali wadogo, wachimbaji wadogo, Wavuvi,  Ushirika wa Bodaboda , Ushirika wa Wakulima pamoja na wanachama wa Mifuko mingine ya hifadhi ya jamii.
Jiunge na NSSF HIARI Scheme ili uweze kujipatia mafao bora ya NSSF yakiwemo Bima ya Afya BURE kwa familia nzima (SHIB), mikopo nafuu ya SACCOS,  pamoja na Mafao bora mengineyo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji NSSF Bw. Crescentius Magori akipima sukari wakati wa zoezi la upima Afya katika Viwanja vya Memorial, Manispaa ya Moshi.
Wakazi wa manispaa ya Moshi wakipima VVU kwa Hiari Kwenye zoezi la Upimaji Afya linaloendeshwa na NSSF.
Daktari Aisha wa NSSF akimpima shinikizo la damu mkazi wa manispaa ya Moshi kwenye zoezi la upimaji Afya bure kwa wakazi wa manispaa ya Moshi.
Dkt. Zakia kutoka NSSF akimpima mkazi wa manispaa ya Moshi Shinikizo la Damu wakati wa zoezi la upimaji Afya bure lililoandaliwa na NSSF.
Wakazi wa Manispaa ya Moshi wakiwa wamejitokeza kwa wingi ili wapime Afya zao na kujua hali zao za Lishe kwenye zoezi lililoandaliwa na NSSF.

INTRODUCING: Chief Maker - Nenda Kamwambie official video

HOTUBA YA MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA (Mb) KWENYE MKUTANO WAKUTANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa ahutubia wananchi kwenye Mkutano wa hadhara, wakati akitangaza nia yake ya kuwania Urais wa Awamu wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM.

RAIS WASTAAFU MWINYI NA MKAPA WALIPOFUNGUA NA KUFUNGA MKUTANO WA BODI YA MAKANDARASI NCHINI (CRB) MWENYEJI WAO AKIWA DKT. MAGUFULI

Wananchi waishukuru serikali kuwajengea uwezo wa kupunguza athari za maafa ya ukame

$
0
0
Na. Mwandishi Maalum

Wananchi wa Wilayani  Same katika  kata ya Hedaru, Makanya na Vunta wameishukuru serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya uratibu maafa, kwa kuwajengea uwezo wa kuzuia, kupunguza na kukabiliana na maafa yanayotokana na ukame ambao umekuwa ukizisumbua kata hizo Kutokana na mabadiliko ya Tabia Nchi.

Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Mradi wa kujengea jamii uwezo wa kukabili maafa ya ukame imefanikiwa kujenga uwezo huo kupitia vikundi vya maendeleo vya wilayani humo, ikiwa vikundi kumi (10) kutoka kata tatu za wilaya hiyo vimepatiwa  Mbuzi 40, kuku 50, mbegu za mihogo, viazi, mtama, mboga mboga pamoja na kutoa miche ya miti kwa shule moja kila kata na vifaa vya kutunza bustani.  
Akiongea wakati Idara hiyo ilipokuwa ikifuatilia utekelezaji wa mradi huo hivi karibuni,  wilayani humo katika kata ya Makanya,  kijijini  Mgwasi, Mwenyekiti wa kikundi cha Kavangere, Stephano Hamisi, alieleza kuwa wananchi wa kata hiyo kupitia ufadhili wa mradi huo wameweza  kulima na kufuga hali inayowajengea uwezo wa  kupunguza na kukabiliana na maafa yanayotokana na ukame. 

TBL yadhamini Bonanza la Michezo jijini Dar

$
0
0

 Meneja Matukio wa TBL mkoa wa Dar es salaam, Zozimick Kimati (kushoto) akikabidhi sehemu ya jezi kwa Bw. Hamis Mwango, zilizotumiwa na timu mbali mbali zilizoshiriki kwenye Bonanza la Michezo lililodhaminiwa na TBL, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza michezo nchini.
  Meneja Matukio wa TBL mkoa wa Dar es salaam, Zozimick Kimati (kati) akizungumza jambo na uongozi wa Timu ya Mshikamano Veterans kabla ya kuingia uwanjani kukipiga na timu ya Uhuru veterans.
 Kikosi cha Makabe Veterans wakiwa kwenye picha ya pamoja tayari kwa mtanange wa Bonanza la michezo lililodhaminiwa na TBL, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza michezo nchini.
 Kikosi cha Mshikamano Veterans kikiwa kwenye picha ya pamoja tayari kwa mtanange wa Bonanza la michezo lililodhaminiwa na TBL, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza michezo nchini.
Kikosi cha Uhuru Veterans.

HIVI NDIVYO HALI ILIVYOKUWA JIJINI ARUSHA WAKATI MH. LOWASSA ALIPOKUWA AKIELEKEA KWENYE UWANJA WA SHEIKH AMRI ABEID KUTANGAZA NIA YA URAIS

$
0
0
 Sehemu ya Waendesha Bodaboda wa Jijini Arusha wakiusubiria msafara wa Mh. Lowassa, maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Arusha.
 Abiria kwenye basi pia hawakua nyuma kuchua Taswira zako pale walipomuona Mh. Lowassa akiwa kwenye gari lake.
 Sehemu ya wakazi wa Arusha wakimshangilia Mh. Lowassa alipokuwa akipita katika barabara ya Sokoine, Jijini Arusha wakati alielekea kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kutangaza nia.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

UHAMIAJI YASHIRIKI KATIKA MAONYESHO YA KARIBU TRAVEL MARKET FAIR, JIJINI ARUSHA

$
0
0
Waziri wa Utalii na Mali Asili, Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb.) akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Afisa Uhamiaji, Rosemarry Mkandala wakati alipotembelea Banda la Idara ya Uhamiaji mara baada ya kufungua rasmi Maonesho ya Utalii “Karibu Travel Market Fair” mnamo tarehe 29.05.2015 yaliyofanyika katika viwanja vya Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha.
Waziri wa Utalii na Mali Asili, Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb.) akipokea machapisho mbali mbali yanayolenga kuelimisha jamii taratibu za Utoaji wa Huduma za Uhamiaji nchini, mapambano dhidi ya Uhamiaji Haramu na makosa mengineyo ya Kiuhamiaji, wakati alipotembelea Banda la Idara ya Uhamiaji kwenye Maonesho ya Utalii “Karibu Travel Market Fair” yaliyofanyika katika viwanja vya Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha.
Maafisa wa Uhamiaji wakitoa Elimu juu ya masuala mbali mbali ya Kiuhamiaji nchini kwa wananchi na wadau mbali mbali walipotembelea Banda la Idara ya Uhamiaji wakati wa Maonesho ya Utalii “Karibu Travel Market Fair” yaliyofanyika katika viwanja vya Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha jana.

Rais Kikwete aongoza Mkutano wa Pili wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa EAC kuhusu Burundi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa kwanza kulia) kwa pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museven (wa pili kulia), Rais wa Afrika Kusini, Mhe Jacob Zuma (wa tatu kutoka kulia), Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Mhe. Alain Nyamitwe (wa tatu kushoto) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Richard Sezibera (wa pili kushoto), wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kabla ya kuanza rasmi kwa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili hali ya siasa na usalama nchini Burundi. Mkutano huo ulifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 31 Mei, 2015. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (wa pili kutoka kulia) akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Joyce Mapunjo na  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje (kulia)  nao wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Dkt. Richard Sezibera akisoma maazimio yaliyofikiwa mara baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kumalizika.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

KUMBUKUMBU

$
0
0
Mpendwa wetu imekua masaa, siku, juma, miezi na sasa ni mwaka tangu ulipokwenda kwa bwana siku Ya jumamosi Tarehe 31 mwezi wa Tano mwaka 2014 saa 7 mchana.

Tunaamini ulipigana vita vilivyo vizuri (2 Timothy 4:7) bado tunakupenda sana na tunakuhitaji lakini Mungu alikupenda zaidi na kukuita kwake. 

Tunaamini upo pamoja na Yesu na unatuombea zaidi. Unakumbukwa na Mke wako Maria,watoto wako Billy,Albert,Siya na Beatrice.Wajukuu Lynn na Lysette,dada,kaka na ndugu wote 

RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE APUMZIKE KWA AMAN.

VIJANA WA KAWE WASHIRIKI JOGGING

$
0
0
 Vijana wa Kawe wakishiriki Jogging.
 Gabriel Munasa (mwenye kaptura ya pink) akishiriki jogging pamoja na vijana wa Kawe,kushoto kwake ni Elias Nawera.
 Bendera ya Taifa ikiwa juu kuashiria kuhitimisha kwa mchakamchaka huo ambao mgeni rasmi alikuwa Gabriel Munasa.

MH.Mwigulu alivyotangaza nia ya kuwania urais mkoani Dodoma jioni ya leo.

$
0
0
  Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akiwapungia mkono baadhi ya wafuasi wake waliojitokeza kwa wingi,kumsikiliza wakati akitamka kutangania nia ya kugombea kiti cha uraui kupitia CCM


  Baadhi ya wakazi wa Dodoma wakimsikiliza kwa makini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alipokuwa akitangaza nia yake ya kugombea kiti cha Urais kupitia chama cha CCM
 Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akizungumza mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Dodom mapema jioni ya leo katika moja ya ukumbi wa chuo cha Mipango
Baadhi ya wakazi wa Dodoma wakimsikiliza kwa makini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alipokuwa akitangaza nia yake ya kugombea kiti cha Urais kupitia chama cha CCM

WAZIRI MEMBE AWASIHI WATANZANIA KUTOCHAGUA VIONGOZI WANAOSAKA UONGOZI KWA KUTOA RUSHWA

$
0
0
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akimkabidhi Bi. Shamim Khan tuzo ya heshima ya kujishughulisha na kazi za kijamii hapa Tanzania,katika tamasha la kwanza la Qaswida
lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa na kudhaminiwa na Kampuni ya Dira ya Mtanzania. PICHA NA MICHUZI JR.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akipokea tuzo maalumu kutoka kwa Sheikh Ismail Mohamed wakati wa tamasha la kwanza la Kaswida lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa na kudhaminiwa na Kampuni ya Dira ya Mtanzania.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulamaa Qaswida Promotions ambao ndio waandaji wa tamasha la kwanza la Qaswida,Ustaadh Jumanne Ligopora akimkaribisha mgeni rasmi  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh.Bernard Membe
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe  akizungumza katika tamasha hilo la kwanza Qaswida, lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa,Mh Membe amewataka Watanzania kusubiri kwa hamu siku ya kutangaza nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu,

Alisema siku hiyo ya Juni 6, wananchi wasikilize nini anataka kuifanya nchi iweze kuondoka ilipo ikiwemo kuendelea kudumisha amani na utulivu uliopo. “Mkae tayari siku hiyo, naamini uongozi mzuri wa nchi ni ule wa kudumisha amani na utulivu na ili nchi iweze kusonga mbele, maadili kwa viongozi ni muhimu,” alisema Waziri Membe.

Membe alitumia nafasi hiyo kuwasihi Watanzania kuacha kuchagua viongozi ambao kwa nje, wanajinadi  wana dini, lakini matendo hayaendani na maadili ya  dini zao. Alisema ili mtu aweze kuaminika kuwa ana dini, jamii ifuatilie katika madhehebu yao, hivyo amewasihi wasichague viongozi wanaosaka uongozi kwa kutoa rushwa.

“Msikubali kuwa na viongozi ambao kwa nje, wanaojinadi kuwa na dini kinyume na matendo yao, lazima mchague wenye hofu ya Mungu ambayo husisitizwa na dini zote,” Alisema uongozi wa heshima ni ule unaochukia rushwa ambayo ni adui wa haki, hivyo amewataka wananchi kuwaogopa wapenda rushwa kama ukoma. 
Baadhi ya Washiriki waliohudhuria tamasha hilo.
Baadhi ya Washiriki waliofika kwenye tamasha hilo la kwanza la Qaswida.

Article 14

TAMASHA LA KOMAA CONCERT LILIVYOFANA NDANI YA KIOTA CHA MARAHA CHA DAR LIVE JIJINI DAR.

$
0
0
 Uongozi pamoja na Wafanyakazi wa kituo cha radio ya EFM 93.7 kwa pamoja wakikata keki kusherehekea kutimiza mwaka mmoja wa kituo hicho ambacho kwa sasa kinakuja kwa kasi jijini Dar na kwingineko,hafla hiyo ilikwenda sambamba na kuadhimisha miaka 16 ya msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Juma Nature,katika tamasha lililoitwa  KOMAA CONCERT,ambalo lilifanyika ndani ya kiota cha maraha cha Dar Live,Mbagala jijini Dar mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na maelfu ya mashabiki na wapenzi wa muziki . 

Lengo la kuwaburudisha Mashabiki wa Juma Nature na wasikiliazaji wa 93.7 EFM  ilikuwa pia ni sehemu ya kuwashukuru mashabiki kwa ushirikiano wao kwa miaka kumi na sita ya muziki tangu kuanza msanii huyo Juma Nature aingie kwenye game ya Muziki nchini Tanzania.

Baadhi ya Wasanii walioshiriki kulinogesha tamasha hilo ni pamoja na Profesa Jay, Shetta, Snura, Makomando, Msagasumu na wengine wengi. Katika tamasha hilo lililowavutia wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake,kiingilio kilipangwa kuwa ni shilingi 7,000 tu. 

Meneja Mwasiliano na mambo ya Sheria wa EFM 93.7 Deniss ssebo alisema kuwa wanaamini Msanii Juma nature ni msanii mwenye kipaji kikubwa na aliyewahamasisha wasanii kibao kuingia katika muziki huu wa kizazi kipya hivyo anastahili kupewa heshima kubwa kwa mchango wake mkubwa katika kukuza muziki wa kizazi kipya,alisema na kuongeza kuwa lakini kwa Efm huyo ni msanii wa Kwanza tu na itaendelea kufanya hivyo kwa wasanii wengine kwa kuwa wanaaamini Muziki unaongea. 
Mkurugenzi wa Efm Dj Majay akiongoza jopo la wafanyakazi wenzake kukata keki 
Pichani kulia ni Meneja Mwasiliano na mambo ya Sheria wa EFM 93.7 Deniss Ssebo akizungumza jambo mbele ya mwashabiki na wapenzi wa muziki na pia wasikilizaji wakubwa wa kituo hicho kuhusiana na utaratibu mzima wa sherehe hiyo,kulia ni Mkurugenzi wa Efm Dj Majay akigawa keki kwa mashabiki waliofika kushuhudia tukio hilo ndani ya Dar Live. 
 Msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Juma Nature akitumbuiza jukwaani mbele ya mashabiki wake,pia akiwashukuru kumpa sapoti ya kutosha tangu ameanza muziki na sasa anatimiza miaka 16 katika tasnia hiyo adhimu.
Wakongwe pamoja  Juma Nature na Prof.Jay wakishoo love kwa mashabiki wao.
Msanii Snura na Madansa wake wakilishambulia jukwaa la KOMAA CONCERT.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Shetta akitumbuiza mbele ya mashabiki kibao waliofika kwenye tamasha la KOMAA CONCERT.
 Mashabiki walikuwa kibao. 
 Burudani ilipangwa sawa bin sawia huku Ma -Mc wakinogesha shughuli
  Mashabiki na mandhari ya Dar Live kwa usiku huo ndani ya jicho la samaki
 Dar Live palinoga usiku huo wa KOMAA CONCERT .

PICHA NA MICHUZI JR.

TAARIFA YA MAKUSANYO UJENZI YA MSIKITI

$
0
0
Kwa Jina la M/Mungu nina anza Andika , Nawashukuru Ndugu zangu WA TANZANIA ,KENYA na wasio kuwa hao kwa Upamoja wao wa Michango yao ya hali na Mali katika Kuimarisha UJENZI WA MSIKITI UNAONA KATIKA PICHA .

Nakushukuru BLOGS ZOTE ZA TANZANIA shukran za Pekee kwa Brother Mroki Mroki wa Father Kidevu Blog kwa kuwa Balozi Mzuri wa kulitangaza Jambo hili kwa Jamii pamoja na Blogs nyingi Marafiki wa Father Kidevu Blog. Leo Tarehe 30/5/2015 NAOMBA NIULETE MREJESHO HUU KWENU WA MAKUSANYO TOKA TAREHE 19/5 mpaka Tarehe 29/5/2015.


Na niwaombe Wadau kurudi tena kuleta mrejesho kama huu M/Mungu akipenda Tarehe 15/6/2015 .

UFUATAO NI MREJESHO WA MICHANGO YA UJENZI WA MSIKITI ULIOPO MKOA WA PWANI , WILAYA YA  MKURANGA , KIJIJI CHA MLAMLENI , KITONGOJI CHA KIMBANGULILE .

Naomba Nianze Ijumaa , Tarehe 29/5/2015 . TUMEPATA KIASI CHA TSHS 238,700/=
  1. CASH :- Tshs 96,700/= Nimezipokea Western Union.
  2. Tigo -Pesa Tshs 142,000/= Jumla ya Pesa zote unapata Tshs 238,700.
  3. TULIZOKUSANYA TSHS 1,373,500/= tukijumlisha na Siku ya Ijumaa Tarehe 29/5 tunapata TSHS 1,612,200/=
  4. Katika hiZo Pesa Taslimu ni Tshs 1,470,200/= na Tigo -Pesa 142,200/=
JUMLA YA MAKUSANYO YOTE Tshs 1,612,200/=

Balozi wetu wa KENYA Ali Bajiy Nasor update zake zitawajia atakapo kusanya Ahadi alizopewa Mpaka sasa amekusanya KSHS 4300/= ambae anakusanya kupitia M-PESA NAMBA +254725113783. ( Usajili ALI HAMIS ) .

Balozi wetu kwa waliopo Uingereza Tafadhali wawasiliane kwa Namba hii muwasilishe Michango yenu +447460340624.

Tanzania CHANGIA KUPITIA TIGO PESA 0715800772 (Brother ALI )

Mawasiliano zaidi Tuwasiliane Whatsapp : +255689604780 au Tembelea Facebook ID yetu :- Kijana Wa Kiislam Dsm
NAWASHUKURU WOTE MLIO CHANGIA NA MTAKAO ENDELEA KUCHANGIA KWA HALI NA MALI , kwa Pamoja TUIJENGE NYUMBA YA IBADA MALIPO YAKE AKHERA NI MAKUBWA ZAIDI NA DUNIANI PIA UNAPATA .


Daima Jamii ya watu huwa Nzuri zaidi na ikishikamana na IBADA na KUMTAMBUA MUUMBA kama Ni hivyo basi kwa PAMOJA TUUJENGE MSIKITI HUU tupate kuwa na Jamii Njema.

Wabillahi Taufiqh.

Wako katika Usimamizi wa hili .
GHALIB NASSOR MONERO.

KAMPENI YA UELEWA KUHUSU TATIZO LA USONJI YAZINDULIWA JIJINI DAR

$
0
0
Kampenii dhidi ya ugonjwa wa usonji yazinduliwa • 
Familia nyingi Tanzania hazina ufahamu wa hali hii
Kliniki ya Lotus kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, zimeanzisha kampeni mpya inayolenga kuelimisha uma kuhusu ugonjwa wa usonji (autism), ambao watanzania wengi hawaufahamu.Ugomjwa huu sasa unatishia familia nyingi kwani dalili zake huanza utotoni na zinaweza kuendelea hadi ukubwani.
Akizugumza wakati wa uzinduzi huo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Kuhudumia watu wenye Usonji Tanzania, Dk. Stella Rwezaula ambaye pia ni mtaalamu wa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na pia ana mtoto mwenye ugonjwa huo, aliishukuru Kliniki ya Lotus kwakuwa katika mstari wa mbele kuanzisha kampeni hiyo ili kuwaelimisha watanzania kuhusu ugonjwa huo.
“Ni vyema ugonjwa huu ukigundulika mapema na kutibiwa ili aliyeathirika aweze kupona na kuishi maisha ya kawaida hapo baadaye kulingana na athari aliyoipata. Mtoto kuanzia miaka 0-6 anawezakutibiwa vizuri na kusaidia kubadilisha maisha yake,” alisema.
Alisema watoto wenye hali hii wana shida katika kuwasiliana na tabia zao ni kurudia rudia mambo anayofanya mara kwa mara na pia watuwengi wenye ugonjwa huu wananamna yao ya kujifunza, kusikiliza na kuitika.
“Mfano wa hali hii ni kwamba katikahali ya kawaida, mtoto wa mwaka mmoja hutabasamu au kuwa na furaha kila wakati, huiga mambo mbalimbali anayoona na kufuatilia vitu anavyoviona vikisogea, lakini mtoto mwenye ugonjwa huu hafanyi vitu hivi,”alisema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kliniki ya Lotus, Dialla Kassam alisemamuelewa bado ni mdogo nchini Tanzania na watoto wengi huathiriwa na kuja kujukilana wakati hali imeshakuwa mbaya zaidi.
“Kukosa uelewa wa hali hii ya watoto wenye mahitaji huwafanya walimu na wazazi kudhani watoto ni watundu, wavivu au wanakera na wakati mwingine huadhibiwa kwa sababu hiyo wakati kwamba watoto hawa wanahitaji uangalizi wa karibu, kupendwa na kupata msaada kutoka kwa
walimu na wenzao,” alisema.
Alisisitiza umuhimu wa kuwafundisha walimu na wazazi kuhusu watoto hawa wenye mahitaji maalumu ili waweze kuwasaidia kuishi na kukubalika katika jamii.Alisema kliniki yake inahudumia watoto wenye mahitaji ya aina hii jijini Dar es Salaam na kuwa timu yake ina wataalamu mbalimbali wanaofanya kazi pamoja ili kutoa elimu kuhusu watoto wenye matatizo haya.
“Hii inafanyika kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa kwa kutoa elimu kwa wadau mbalimbali wakiwemo walimu na wazazi kupitia warsha,mafunzo mbalimbali, kutafuta wafanyakazi wa kujitolea na kutoa rasilimali kwa taasisi mbalimbali kama Shule ya Mbuyuni ya watu wenye ugonjwa huu,” alisema. 
Alisema kliniki mbalimbali kuhusu ugonjwa huo hufanyika katika Hospitall ya Taifa ya Muhimbili kila Alhamisi na kwamba Chama Cha Watu Wenye Usonji-Tanzania (NAPA-T) kimekuwa kikisaidia.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Lotus Clinic, Dialla Kassam (katikati), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya kueneza uelewa kuhusu tatizo la usonji ‘Autism’ nchini Tanzania iliyondaliwa na Lotus Medical Clinic kwa
kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na taasisi ya Autism Education Trust ya Uingereza. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Kuhudumia watu wenye Usonji Tanzania, Dk. Stella Rwezaula na Daktari wa kufundisha kuongea, Nazreem Sumar.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Lotus Clinic, Dialla Kassam (katikati), akitoa utambulisho kwa meza kuu mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana katika uzinduzi huo. Kushoto ni Mtaalam wa Afya kutoka taasisi ya Autism Education Trust ya Uingereza, Kevin Baskerville, Mwenyekiti wa Chama cha Kuhudumia watu wenye Usonji Tanzania, Dk. Stella Rwezaula (wa pili kushoto), Daktari wa kufundisha kuongea wa Lotus, Nazreem Sumar (wa pili kulia) na Daktari Fathema Hasham.
 

Heri ya Kuzaliwa Mdau Josephat Lukaza.

$
0
0
Mwanakijiji Josephat Lukaza.
Tunapenda Kuchukua nafasi hii kukupongeza kwa kufikisha Miaka kadhaa ya kuzaliwa kwako na ukiwa sehemu ya wanakijiji wa digitali hapa duniani.
Tunachukua nafasi hii kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kukulinda na kukubariki kwa kukuongezea maisha marefu na yenye heri hapa duniani ili vizazi vingine viweze kufaidi baraka na neema za mwenyezi Mungu kupitia Wewe.
Leo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa Kwako iwe chachu na siku ya kufikiria ulipotoka, Ulipo na uendapo ili kuweza kutimiza Malengo yako huku Jamii inayokuzunguka Ikitegemea Mazuri mengi kutoka Kwako.
Ni ngumu kuyatimiza pekee yako lakini tunakuombea kwa Mungu akujalie wepesi katika kutimiza yaliyo mema mbele zake na Jamii inayokuzunguka Umekuwa Mtu ambae ni wa kipekee sana na mwenye kupenda kushirikiana na watu wote pale ambapo unaombwa msaada bila kujali huyu ni nani Mungu Akujalie uendelee na moyo huo huo na mazuri hayo hayo .
Tunakuombea Kwa Mwenyezi Mungu azidi kukupa maisha marefu na yenye Baraka na fanaka tele hapa duniani.
Ukiwa kama Mwanakijiji Mwenzetu tunapenda kukutakia Heri ya Kumbukumbu ya Siku yako ya Kuzaliwa kwa kihispania wanasema 
"Feliz cumpleaños Josephat Lukaza"
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live




Latest Images