Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live

ORGINAL KOMEDI WAKABIDHIWA MATREKTA KWA LENGO LA KUENDELEZA KILIMO


NEWS ALERT: SEPP BLATER ATETEA URAIS FIFA KWA KISHINDO LEO

JUST IN: NANA BY DIAMOND PLATNUMZ FT. MR. FLAVOUR

SHEREHE ZA KUFUNGA MAFUNZO YA AWALI YA JESHI LA MAGEREZA KOZI NA. 27 CHUO CHA MAGEREZA KIWIRA ZAFANA, JIJINI MBEYA

$
0
0
Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza wakipita kwa mwendo wa haraka mbele ya Mgeni rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil(hayupo pichani) leo Mei 29, 2015 katika Chuo cha Magereza, Kiwira Kilichopo Mkoani Mbeya.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza leo Mei 29, 2015 Chuo cha Magereza Kiwira, Mbeya.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil akipokea Salaam ya heshima akiwa jukwaan kabla ya kukagua Gwaride Maalum katika sherehe za kufunga Mafunzo ya Uaskari Magereza, Kiwira Mbeya(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Stanford Ntirundura.

CCM WASHINDA NAFASI YA UENYEKITI MJI MDOGO WA HIMO

$
0
0
Mwenyekiti  mpya wa mji mdogo wa Himo Hussein Jamal akizungumzamara baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo katika uchaguzi huo uliofanyika katika shule ya walemavu wa usikivu eneo la njia Panda.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Moris Makoi akisalimia mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza wakati wa kufunga kikao cha uchaguzi huo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MRATIBU MKAZI WA UN NCHINI NA WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI WATEMBELEA ENEO LA MAPOKEZI YA MUDA KWA WAKIMBIZI MJINI KIGOMA

$
0
0
IMG_0495
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) akiongozana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa tatu kushot0) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (katikati), Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (wa pili kulia), Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Kigoma, Amah Assiama-Hillgartner (kulia) mara tu baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Lake Tanganyika mjini Kigoma, eneo ambalo Wakimbizi wanapokelewa na kupewa huduma ya kwanza kabla ya kuelekea katika eneo maalum ya Nyarugusu, wilayani Kasulu mkoani Kigoma.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
IMG_0457
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akizungumza na wafanyakazi wa wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wanaoandikisha Wakimbizi wanaowasili kwenye uwanja wa Lake Tanganyika kabla ya kuelekea katika kambi ya Nyarugusu, iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
IMG_0468
Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Kigoma, Amah Assiama-Hillgartner (kushoto) akifafanua jambo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa tatu kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (wa pili kushoto) walipotembelea uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.

MH. LOWASSA KUANZA "SAFARI YA MATUMAINI" MCHANA WA LEO

$
0
0
Gari iliyombeba Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa ikipita nje ya uwanja wa Sheih Amri Abeid, jijini Arusha mapema leo asubuhi wakati akielekea kwenye Ofisi za CCM Mkoa. Mh. Lowassa anatarajia kulihutubia taifa mchana wa leo kwenye uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid, ikiwa ni sehmu ya kutangaza kwake nia yake ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na baadhi ya viongozi waliokuwepo kwenye ofisi ya CCM Mkoa wa Arusha.Kulia ni Mkewe Mama Regina Lowassa.
Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea ofisi ya CCM Mkoa wa Arusha. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole.
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole akizungumza machache mbele ya Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa alieambatana na Mkewe, Mama Regina Lowassa pamoja na wanaCCM wengine.
Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole (hayupo pichani).

PICHA ZAIDI ZITAWAJIA BAADAE KIDOGO

In Loving Memory of Mzee Felician Makwaia

$
0
0
In Loving Memory of Mzee Felician Makwaia 1944 - 2013

Beloved Dad!
It has been two years now
since you responded to your Almighty’s call,
If we only knew it would be the last time
that we see you walk out the door,
We would give you a hug and kisses,
and call you back for one more.

A million times we needed you,
A million times we cried,
If love alone would have saved you,
You would have never died.

In life we loved you dearly,
In death we love you still,
In our hearts you will forever hold a place,
No one can ever fill.

A light from our household is gone,
A voice from our love is stilled,
A place in our vacant home,
Which never can be filled.

Some may think you are forgotten,
Though on earth you are no more,
But in our memory you are with us,
As you always were before.

It broke our hearts to lose you,
But you did not go alone,
A part of us went with you,
The day God called you home.

Your precious memories are for keepsakes,
with which we never part,
God has you safely in his keeping,
But we have you in our hearts and your Legacy will forever live on!

Deeply missed by your Loving Wife Mama Makwaia, your Children Stella, Frank, Robert and Christopher, In-laws, Grand-children, Neighbours, Friends and Relatives.

May you Rest in Peace Dad! Amen.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera azindua zoezi la unywaji maziwa

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera akizindua zoezi la unywaji wa maziwa kwenye maadhimisho ya wiki ya 18 ya maziwa ambayo kitaifa ilizinduliwa jana mjini Babati, kwa kuwapa maziwa wanafunzi wa shule ya msingi Babati.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dk Joel Bendera akizinduzi wa wiki ya 18 ya maziwa, ambapo kitaifa inafanyika Mjini Babati, kwa kumpa maziwa mkazi wa mji huo Magdalena Joseph ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni ng'ombe wa maziwa ni fursa ya kiuchumi na lishe fuga kisasa.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dk Joel Bendera akizindua wiki ya 18 ya maziwa, ambapo kitaifa inafanyika Mjini Babati, kwa kumpa maziwa mkazi wa mji huo John Simon maziwa, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni ng'ombe wa maziwa ni fursa ya kiuchumi na lishe fuga kisasa.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Kwaraa ya Mjini Babati Mkoani Manyara, wakiimba jana kwenye uzinduzi wa wiki ya 18 ya maziwa ambayo kitaifa inafanyika mkoani humo, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni ng'ombe wa maziwa ni fursa ya kiuchumi na lishe fuga kisasa.
 Wasanii wa kizazi kipya wa wakawaje wa Mjini Babati Mkoani Manyara, wakicheza jana kwenye uzinduzi wa wiki ya 18 ya maziwa kitaifa inafanyika mkoani humo, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni ng'ombe wa maziwa ni fursa ya kiuchumi na lishe fuga kisasa.

MWANDISHI WA HABARI MWANDAMIZI ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UDIWANI KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA SONGEA MKOANI RUVUMA

$
0
0
Mwandishi wa Habari mwandamizi Bi. Celesencia Kapinga akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari ambao hawapo pichani wakata alipotangaza nia ya kugombea udiwani kata ya NDILIMALITEMBO Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM).
 Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma wakiwa pamoja na Mwandishi wa Habari wa gazeti la Majira ambaye ametangaza nia ya kugombea udiwani kata ya Ndilimalitembo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) . Habari na picha na Demasho.com.
..............................................................
WAKATI watu mbalimbali wameanza kujitokeza kutangaza nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kupitia vyama vya siasa mwandishi wa habari  Mwandamizi,  Mkoani  Cresensia Kapinga ametangaza nia ya kugombea udiwani kata ya Ndilima litembo manispaa ya Songea  Ruvuma.

Mwandishi huyo ametangaza nia yeke ya kuwania nafasi ya udiwani  mbele ya waandishi wa habari  kwenye ofisi za chama cha waandishi wa habari  Mkoa wa Ruvuma  zilizopo mtaa soko kuu mkoani  humo.
Amesema kuwa  kabla ya kutangaza nia amejipima na kujiona anaweza kuongoza kata baada ya kuwa  aligombea nafasi hiyo kupitia viti masalumu mwaka 2010 ambapo kura hazikutosha.

Akijibu masawali mbalimbali ya Waandishi wa habari amesema kuwa ameamua kugombea nafasi hiyo baaada ya kuona Changamoto mbalimbali zinazowakabaili Wananchi Katika Kata hiyo iliyokonje kidogo ya Manispaa  ya songea hazijafanyiwa kazi. 

‘Ziko Changamoto nyingi zinazowakabili Wananchi  wa Kata ya Ndilimalitembo bado hazijafanyiwa kazi,baadhi zikiwa ni Ukosefu wa Zahanati,Shule kukosa Vyoo na Wananchi kukosa soko la uhakika la kuuza mazao yao ambazo naamini  nikipata  nafasi ya kuwa Mwakilishi wao nitazishughulikia’anasema Bi. Cresensia Kapinga.

Anasema kuwa kuwa kutokana na  na taaluma yake ya uandishi wa habari ana uwezo wa kuingia Ofisi yoyote katika Manispaa ya Songea  na kuwasemea Wananchi wa  Kata hiyo hivyo anasema ni fursa  pekee ya Wananchi hao kumpa Fursa ya kuongoza Kata hiyo.
Kwa upande wa Waandishi wa habari amesema kuwa  kwa kuwa yeye ni Mwanahabari atajitahidi kuwasema kwenye Baraza la  Madiwani  akiamini yapo mambo mengi yanashindwa kushughulikiwa ikiwemo posho zao.

Kwa upande wao Waandishi wa Habari wamepongeza hatua hiyo  na kutaka Waandishi wengine wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwa kuwa Waandishi wamekuwa  wakinadi watu wengine wakati wapo baadhi yao wana uwezo wa kuongoza.

Mmmoja wa Waandishi hao Julius Konala anasema hatua hiyo ni ya kupongeza sana kwa kuwa imefunguia njia kwa Wanahabari wengine kugombea zaidi  na kuwata Wananchi  na Wanaccm kumuunga mkono  katika  azma yake ya kutaka kuwa  Diwani wa Kata ya Ndilimalitembo.

MKUU WA WILAYA KINONDONI PAUL MAKONDA AZINDUA MAONESHO YA 5 YA KAMPUNI YA EAG GROUP LEO JIJINI DAR.

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akikata utepe kuzindua maonyesho ya 5 ya Kampuni ya EAG Group Ltd yanayofanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam,kutoka kushoto ni Msanifu majengo wa wizara ya Ardhi Julius Ndege na Mkurugenzi mkuu wa EAG group Ltd Imani Kajula.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akipewa maelekezo alipotembelea banda la DEGE Eco Village na  Mkurugenzi  na Afisa Masoko wa DEGE Eco Villag,Ashar Malik katika maonyesho ya 5 ya EAG Group Ltd yanayofanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda Akimsikiliza Meneja masoko wa kampuni ya AVIC Internatinal Real Estate (T) Ltd, Linda Zhang alipotembelea maonyesho ya 5 ya kampuni  EAG Group Ltd yanayofanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akionyeshwa namna mbalimbali za kujenga nyumba kwa kutumia vyuma na Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya PIVOTECH,Eric Chonjo  alipotembelea banda la Kampuni ya PIVOTECH katika aonyesho ya 5 ya kampuni  EAG Group Ltd yanayofanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wananchi waliotembelea mabanda mbalimbali katika maonyesho ya 5 ya kampuni  EAG Group Ltd yanayofanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika maonyesho ya 5 ya kampuni  EAG Group Ltd yanayofanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.

LOWASSA ALITIKISA JIJI LA ARUSHA LEO

$
0
0
 Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
 Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Mh. Kangi Lugola akisalima umati wa watanzania uliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, kumsikiliza  Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa (kulia).
 Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa, kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo.
 Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akihutubia katika mkutano wa hadhawa wa kutangaza nia yake hiyo,  kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo.
Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru akihutubia kwenye mkutano huo.
Umati wa watu uliofurika kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha, kumsikiliza Mh. Edward Lowassa akitangaza nia yake ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

UMOJA WA MATAIFA WA WAENZI WALINDA WA AMANI WALIOPOTEZA MAISHA 2014

$
0
0
Na Mwandishi Maalum, New York 
 Mashujaa Private Ally Salum Jumanne, Private Mohamed John Mbizi, Private Vasco Adrian Msigala na Sajent Hamis Juma Nyange kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) ni miongoni mwa mashujaa 126 ambao siku ya Ijumaa, Umoja wa Mataifa uliwatunuku medali ya Dag Hammarskjold 
Ijumaa ya Mei 29 ya kila mwaka Umoja wa Mataifa umeitenga kama siku maalum ya kutambua na kuenzi mchango wa walinda Amani ambao wamepoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu ya ulinzi wa Amani kupitia operesheni za Umoja wa Mataifa. 
Katika adhimisho hilo na ambalo lilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa, Ban ki moon, Naibu wake Jan Eliasson, na Wakuu wa Idara za Ulinzi za Umoja wa Mataifa, jumla ya mashujaa 126 kutoka nchi 38 waliopoteza maisha mwaka jana (2014) walienziwa kwa kutunukiwa medali maalum ya DagHammarskjold. 
Adhimisho hilo lilitanguliwa na uwekaji wa shada la maua kwa heshima ya mashujaa hao, shada liliwekwa na katibu Mkuu Ban Ki Moon katika sehemu maalum ambayo imeandaliwa kwaajili ya kumbukumbu hiyo. 
Akizungumza kwa masikitiko makubwa wakati wa hafla hiyo, Katibu Mkuu, Ban Ki Moon, amesema, katika maadhimisho yote yanayofanyika katika Umoja wa Mataifa, hakuna adhimisho lenye kutia simanzi na ngumu kama hili la kuwakumbuka na kuwaenzi walinda amani ambao wamepoteza maisha yao wakati wakitoa ulinzi kwa watu wengine. 
“ Ninasikitika kusema kwamba, hii ni mara ya saba mfululizo ambapo zaidi ya walinda amani 100 wamepoteza maisha katika kipindi cha mwaka mmoja. Hatari wanayokumbana nayo walinda amani wetu inazidi kuongezeka kwa kasi kubwa, kutoka kushambuliwa na makundi ya wahafidhina na makundi ya wanamgambo wenye silaha mpaka hatari ya magonjwa ambukizi kama vile Ebola” amesema katibu Mkuu. 
Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa akaendelea kusema. “ Tumekusanyika hapa kuwaenzi mashujaa wetu waume kwa wake ambao wamepoteza maisha yao wakati wakiwalinda wananchi katika maeneo hatari duniani. Kujitoa kwao muhanga na namna walivyoyaishi maisha yao, wanatufanya sisi tujisikie fahari na kututia shime ya kufanya kazi kwa bidii zaidi ili kudhihirisha kwamba maisha yao hayakupotea bure. 
Ban Ki Moon, awaeleza wawakilishi kutoka nchi ambazo zimepoteza mashuja wake kwamba, operesheni za ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa zitaendelea kuwa zenye changamoto na hatari kubwa, na cha kusikitisha ni kwamba adhimisho lililofanyika ijumaa la kuwaenzi mashujaa hao halitakuwa la mwisho 
“ Walinda amani wetu wanabeba jukumu zito kwaajili yetu sote. Natoa heshima zangu kwa mashujaana salamu zangu za pole kwa familia za mashujaa hawa” akasisitiza Katibu Mkuu. 
Walinda amani hao 126 na raia 19 wamepoteza maisha wakati wakihudumua katika misheni zilizopo, Afghanistan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ivory Coast, Cyprus, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Haiti, Mali, Mashariki ya Kati, Liberia, Sudan na Sudan ya Kusini Pamoja na Tanzania 
Nchi nyingine ambazo zimepoteza mashujaa wake katika misheni mbalimbali za kulinda Amani katika mwaka uliopita ni Senegal, Afrika ya Kusini, Uhispania, Togo, Rwanda, Benin, Burkina Faso, Bangladesh,na Burundi. Nyingine ni Cambodia, Chad, El Salvador, Ethiopia, Fiji, France, Ghana, India, Indonesia, kenya , Malawi, Niger, Pakistan, Philippines, Tunisia na Zimbabwe. 
 Pamoja na mashujaa hao ambao ni wanajeshi, wapo pia raia 19 wakiwamo pia polisi, madaktari, watumishi na watoa misaada ya kibinadamu ambao wamepoteza maisha wakati wakitoa misaada kwa binadamu wenzao. 
Wakati Umoja wa Mataifa ukiwaenzi mashujaa hao waliopoteza maisha mwaka jana. Tayari mwaka huu wa 2015 mashujaa wapatao 49 wamekwisha poteza maisha wakitekeleza majukumu yao ya kuleta Amani , utulivu na ulinzi wa raia wasio na hatia katika nchi zenye migogoro. Kati ya mashujaa 49 hao wapo watanzania wawili. Jumla ya walinzi wa Amani 3,300 wamekwisha kupoteza maisha tangu kuanzishwa kwa Operesheni za Ulinzi wa Amani chini ya Umoja wa Mataifa mwaka 1948.
Bi. Maura  Mwingira, Charge d' affaires a.i wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  akipokea kutoka kwa  Mkuu wa Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani za  Umoja wa Mataifa ( DPKO ) Bw. Harves Ladsous,  Medali  Maalum ya  Dag Hammarskjold  ambazo wametunukiwa  Mashujaa wanne walinda Amani  kutoka JWTZ ambao walipoteza maisha mwaka  2014  wakati wakitekeleza majukumu yao. Umoja wa Mataifa umeitenga  Mei 29 kama siku ya  Kimataifa ya  kuwakumbuka na kuwaenzi walinda amani  ambao walipoteza maisha katika misheni mbalimbali za Umoja wa Mataifa. Jumla ya  walinda amani  126 walipoteza maisha mwaka jana . Medali hizo  zitawasilishwa kwa Familia za Mashujaa   hao.
Charge d' affaires Bi. Maura Mwingira wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akiandika katika kitabu maalum,  baada ya kupokea  kwa niaba ya  familia  za mashujaa  wanne wa JWTZ waliopoteza maisha wakati wakihudumu katika misheni za kulinda amani mwaka jana.  Medali hiyo  maalum  ya Dag  Hammarskjold  ilitokwa  siku ya  ijumaa kama  ishara ya kuwaenzi, kutambua na kuthamini mchango mkubwa wa mashujaa hao.
Katibu Mkuu Ban Ki Moon, akiwa na Naibu Katibu Mkuu, Jan  Eliasson, na  Viongozi wakuu wa  Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani ( DPKO) muda mfupi kabla ya utoaji wa medali maalum kwa mashujaa 126 walinda amani ambao walipoteza maisha mwaka jana. katika  salamu zake  Katibu Mkuu alieleza kwamba katika  maadhimisho yote yanayofanyika katika Umoja wa Mataifa,   adhimisho la kuwakumbuka na kuwaenzi walinda amani ni adhimisho lenye  kutia simanzi na gumu.
Mpiga  Buluji akiimba wimbo maalum wa  maombolezo kama ishara ya kuwakumbuka mashujaa 126 walinda amani waliopoteza maisha  mwaka jana. shughuli za utoaji wa medali  maalum zilitanguliwa na uwekaji wa  shada maalum la maua katika eneo ambalo limetengwa katika viunga vya Umoja wa Mataifa .   Pichani anaonekana Katibu Mkuu Ban Ki Moon akitoa salamu za heshima kwa wahanga hao anaonekana pia Naibu Katibu Mkuu  Jan Eliasson

MWANAMITINDO WA KIMATAIFA FLAVIANA MATATA AZIDI KUWIKA

$
0
0
MWANAMITINDO AFANYAYE KAZI ZAKE ZA UANAMITINDO ALOJIKITA MAREKANI FLAVIANA MATATA AMEKUWA AKIFANYA KAZI MBALI MBALI ZA KUONESHA MAVAZI JUKWAANI SAMBAMBA NA HIZI ZA MATANGAZO YA KIBIASHARA YA MATANGAZO YA MAVAZI NA SAFARI HII AMEFANYA NA KAMPUNI YA NEWYORK AND COMPANY KWA AJILI YA MAVAZI YA MAJIRA YA JOTO
FullSizeRenderIMG_6387IMG_6388IMG_6389

JAMBO LEO YAICHABANGA BODABODA FC TAMASHA LA BODABODA UKONGA

$
0
0
 Mlinda mlango Maganga Benjamin wa timu ya Bodaboda Wilaya ya Ilala, akiudaka mpira katikati ya wachezaji wa timu ya Jambo Leo 'Wagumu Stars' Zahoro Mlanzi (kushoto) na Ali Salum wakati wa Tamasha la Bodaboda lililofanyika kwenye Uwanja wa Ukonga Gerezani, Dar es Salaam. Mgeni rasmi katika tamasha hilo alikuwa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa. Jambo Leo ilishinda mabao 2-1.
 Moja ya kizazaa langoni mwa Bodaboda FC iliyosababishwa na washambuliaji wa Jambo Leo
 Mshambuliaji wa timu ya Gazeti la Jambo Leo, Ali Salum (katikati) akifunga bao la kwanza dhidi ya Bodaboda FC,wakati wa Tamasha la Bodaboda lililofanyika kwenye Uwanja wa Ukonga Gerezani, Dar es Salaam leo. Mgeni rasmi katika tamasha hilo alikuwa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa.Jambo Leo ilishinda mabao 2-1.
 Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akiwasalimia wachezaji wa timu hizo mbili


Tangazo la Msiba wa Ndg Sebastian Lukas Mgimba

$
0
0
Familia ya bwana Sebastian Lukas Mgimba ya sinza kumekucha inasikitika kutangaza kifo cha baba Yao mpendwa ndugu Sebastian Lukas Mgimba kilichotokea alhamis 28/5/2015 katika hospital ya kairuki mikocheni Dar es salaam. Mipango ya mazishi Inafanyikia nyumbani kwa marehemu sinza kumekucha. Mwili unatarajia kusafirishwa kwenda Lugarawa Ludewa Njombe jumatatu 1/6/2015. 
Habari ziwafikie Familia ya Malyatabu Mgimba iliyopo Lugarawa Ludewa familia ya Philipo Mshengeli Msuya ya shighatini Mwanga pamoja na ndugu jamaa na marafiki popote pale walipo.    
Misa takatifu pamoja na Kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu zitafanyikannyumbani kwa marehemu Sinza Kumekucha tarehe 1-06-2015 kuanzia saa Sita Mchana
Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe

KAMPENI YA KUTOKOMEZA MARADHI YA FISTULA YATUA WILAYA YA KIBONDO

$
0
0
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kumwamba iliyopo Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma walijumwika na wakazi wa wilaya hiyo katika viwanja vya Community Centre wakimsiliza Meneja Biashara wa Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Grace Lyon wakati alipokuwa akiwafafanulia jambo kuhusiana na maradhi ya Fistula. Wakati wa kampeni ya kutokomeza maradhi hayo inayoendelea kufanyika katika mikoa mitatu nchini,Kampeni hiyo inaendeshwa na Hospitali ya CCRBT kwa kushirikiana na Vodacom Foundation. Inakadiriwa wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo kwa mwaka wakati wa kujifungua.
Balozi wa maradhi ya Fistula nchini Msanii Mrisho Mpoto alimaarufu”Mjomba” akitoa elimu kwa wakazi wa Kibonda kuhusiana na maradhi ya fistula na kuwasihi wakina baba kuwaruhusu wake zao wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Alitoa elimu hiyo wakati wa kampeni inayoendeshwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na CCBRT ya kutokomeza maradhi hayo inayoendelea katika mikoa mitatu nchini. Inakadiriwa wastani wa wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo kwa mwaka wakati wanapojifungua.
Mkazi wa Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma Esther Batolomea akisoma kipeperushi chenye ujumbe wa maradhi ya Fistula wakati wa kampeni ya kutokomeza maradhi hayo iliyofanyika wilayani hapo. Hospitali ya CCBRT kwa kushirikiana na Vodacom Foundation zinatoa elimu kwa Umma kupitia kampeni inayozunguka mikoa mitatu nchini kuwasisitiza wanawake wajitokeze wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo kwa mwaka wakati wa kujifungua.

STARTIMES KUANZA KUONYESHA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA U20

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

WAPENZI  wa soka nchini sasa watafaidi kwa kutazama michuano ya kombe la dunia chini ya miaka 20 mwaka 2015 moja wa moja kwenye luninga zao kupitia ving’amuzi vya StarTimes pekee.

Michuano hiyo ambayo itaanza kutimua vumbi tarehe 30 mwezi Mei na kumalizika tarehe  20 mwezi Juni  mwaka huu moja kwa moja kutoka nchini New Zealand ambapo timu 24 za vijana kutoka mataifa mbalimbali duniani yatachuana kuwania ubingwa.


Akizungumza baada ya kupata haki miliki kutoka kwa FIFA za kutangaza michuano hiyo maarufu duniani ambayo hubeba mastaa wa baadae kwa timu zao za taifa, Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amesema kuwa wanafuraha kubwa kuonyesha michuano hiyo kwani soka ni mchezo unaopendwa zaidi duniani.


“Tunayofuraha kubwa kuwatangazia wateja wetu kuwa tumepata haki miliki kutoka FIFA za kuonyesha michuano ya kombe la dunia kwa vijana wa umri chini ya miaka 20 mwaka 2015 itakayofanyika nchini New Zealand. Soka ni mchezo unaopendwa zaidi nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla na tunaamini tutawapatia wateja wetu burudani ya matangazo yenye ubora wa hali ya juu kupitia ving’amuzi vya StarTimes.” Alisema Bi. Hanif

SOMA ZAIDI HAPA

Rais Kikwete akutana na Maalim Seif Ikulu jijini Dar es Salaam

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad aliemtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo. (picha na Freddy Maro)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad aliemtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam leo. 

CBA yasaidia wenye mahitaji maalumu kupitia mashindano ya mbuzi

$
0
0
Afisa mwandamizi wa Masoko wa Benki ya CBA, Solomon Kawiche akikabidhi mfano wa hundi ya sh laki sita kwa Sue Hurford ambaye mbuzi wao aliibuka kidedea wa shindano lililopewa jina la CBA ‘Sparkers’ lililodhaminiwa na benki hiyo wakati wa mashindano ya mwaka huu ya mbio za mbuzi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Fedha hiyo itapewa Hospitali ya CCBRT.
Mbuzi wakitimua mbio ili kumpata mshindi wa shindano katika mbio za mbuzi​lililopewa jina la 'CBA Sparkers’ lililodhaminiwa na benki ya CBA wakati wa mashindano ya mwaka huu ya mbio za mbuzi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Afisa mwandamizi wa Masoko wa Benki ya CBA, Solomon Kawiche akionyesha cheti alichokabidhiwa kutokana na benki ya CBA kudhamini mashindano hayo ya kuchangia fedha za kusaidia makundi mbalimbali yenye mahitaji maalum katika jamii wengine pichani ni wafanyakazi wenzake na waandaaji wa shindano hilo
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live




Latest Images