Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110108 articles
Browse latest View live

Viongozi Waanzilishi TAPSEA Walalamikia Uchaguzi wa Chama Chao

$
0
0
Viongozi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA) walioko madarakani sasa ambao wanaolalamikiwa kuingia madarakani kinyume na katiba ya chama hicho wakizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mjini Dodoma kuzungumzia mkutano wao mkuu unaoanza leo mjini Dodoma. Viongozi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA) walioko madarakani sasa ambao wanaolalamikiwa kuingia madarakani kinyume na katiba ya chama hicho wakizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mjini Dodoma kuzungumzia mkutano wao mkuu unaoanza leo mjini Dodoma.Viongozi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA) walioko madarakani sasa ambao wanaolalamikiwa kuingia madarakani kinyume na katiba ya chama hicho wakizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mjini Dodoma kuzungumzia mkutano wao mkuu unaoanza leo mjini Dodoma. Viongozi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA) walioko madarakani sasa ambao wanaolalamikiwa kuingia madarakani kinyume na katiba ya chama hicho wakizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mjini Dodoma kuzungumzia mkutano wao mkuu unaoanza leo mjini Dodoma.

MGOGORO wa uongozi ndani ya Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA) umeingia katika hatua tata baada ya viongozi waanzilishi wa chama hicho kulalamikia uchaguzi uliopangwa kufanyika Mei 30, 2015 mjini Dodoma ilhali kuna mgogoro wa uongozi ndani ya chama hicho ukiendelea. 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa niaba ya viongozi wenzake Mwenyekiti wa TAPSEA, Pili Mpenda ambaye pia ni miongoni mwa waanzilishi wa chama hicho jana jijini Dar es Salaam alisema anasikitishwa na kitendo cha viongozi walioingia kinyume na katiba ya chama hicho kujipanga kufanya uchaguzi ilhali kuna kesi ya msingi ipo mahakamani kulalamikia wao kuondolewa madarakani. 

Alisema viongozi waliopo madarakani sasa wameingia kwa nguvu za Msajili wa Vyama vya Siasa nchini baada ya kushinikiza uchaguzi kinyume na maelekezo ya Mkutano Mkuu wa kwanza wa TAPSEA uliofanyika Arusha Mai 18, 2013 wa chama hicho ambao ulielekeza maboresho ya katiba ya chama kabla ya chochote kufanyika. 

 Alisema mkutano mkuu wa pili uliofanyika mkoani Mwanza 2014 uliitishwa ili kuwaeleza wananchama juu ya shinikizo la msajili na wanachama wachache (7) kufanyika uchaguzi na kuwaeleza mwenendo wa marekebisho ya katiba ya TAPSEA lakini Ofisa msajili alishinikiza ufanyike uchaguzi ambao uliwagawa wanachama na wengine kususia uchaguzi huo kutokana na mvutano. 

Bi. Mpenda alisema uchaguzi uliofanyika haukuwa halali kwani mbali na kufanyika kinyume na katiba ya TAPSEA na maelekezo ya Mkutano Mkuu wa kwanza haukushirikisha wanachama wote. Aliongeza kuwa kati ya wanachama halali 815 waliokuwa wamejisajili ni wanachama 200 tu ndio walioshiriki katika uchaguzi huo. 

"...Uchaguzi huu ni kinyume na katiba ya TAPSEA na kinyume na maelekezo ya Mkutano Mkuu wa kwanza na ulifanyika kwa shinikizo la Msajili wa Vyama vya Siasa...sisi hatujui alitumia kifungu gani kuja kushinikiza uchaguzi na kuusimamia kinyume na katiba yetu," alisema Bi Mpenda katika mazungumzo.

 Aidha alisema tayari viongozi waliopinduliwa wameenda mahakamani kupinga kitendo hicho na msajili anafahamu lakini wanashangaa kuona viongozi wanaolalamikia wamejipanga kufanya uchaguzi mpya wa chama hicho Mai 30, 2015 mjini Dodoma. Hata hivyo taarifa kutoka kwa viongozi waliopo madarakani kwa sasa wamekiri kujiandaa na uchaguzi mkuu mpya kwa nafasi za juu za chama hicho pamoja na wajumbe 9 wa Kamati ya Utendaji. 

Akizungumza leo mjini Dodoma na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa TAPSEA aliyepo madarakani kwa sasa, Festo Emmanuel amesema chama hicho kinaendelea na mkutano mkuu unaoanza leo mjini hapo na wamesajili upya wanachama ambapo imefikia jumla ya wanachama 1500. Na alikiri watafanya uchaguzi katika nafasi za juu za chama hicho. Viongozi wa TAPSEA walioko madarakani sasa ambao wanaolalamikiwa kuingia madarakani kinyume na katiba ya chama hicho wakizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mjini Dodoma kuzungumzia mkutano wao mkuu unaoanza leo mjini Dodoma.

ATCL yaongeza safari zake visiwa vya Comoro.

$
0
0
  Abiria wakishuka kwenye  Ndege ya Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) aina ya CRJ 100. Picha ya Maktaba

SHIRIKA la ndege la taifa (ATCL) limetangaza  uamuzi wake wa kuongeza idadi ya safari zake kuelekea visiwa vya Comoro hatua inayolenga kuendana  na ongezeko la mahitaji ya huduma za shirika hilo hususani katika kuelekea kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kwa sasa shirika hilo linatoa huduma zake kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma na Mtwara kila siku. Sambamba na kutoa huduma hizo hapa nchini, shirika hilo lina mpango mpya utakaoanza rasmi tarehe mosi ya mwezi Juni mwaka huu kwa kuongeza safari zake kuelekea visiwa vya Comoro hadi kufikia mara nane kwa wiki ikiwemo mara mbili siku za Alhamisi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Bw. Johnson Mfinanga alisema shirika hilo ndilo pekee linalotoa huduma ya safari za anga kati ya Tanzania na Visiwa vya Comoro huku akibainisha fursa za kibiashara zilizopo kati ya nchi hizi mbili jambo linalosababisha uwepo wa ongezeko la mahitaji ya huduma za ATCL.

Pia amewaasa watanzania hususan wakazi wa mtwara kuchangamkia fursa hizo kwa kuwa shirika hilo kwa sasa linatoa huduma zake kati ya Mtwara na visiwa vya Comoro kwa siku za Jumatano na Ijumaa kila wiki.
“Siku zote tumekuwa tukihakikisha kwamba tunabadilika kuendana na mahitaji ya wateja wetu.

 Ni dhahiri kwamba katika kipindi hiki kuna hitaji kubwa la usafiri wa anga kuelekea visiwa vya Comoro kwa sababu za  kibiashara, mapumziko na sherehe mbalimbali, hivyo ATCL imejipanga kuchangamkia fursa hiyo,’’ alibainisha.

Akizungumzia ufanisi wa shirika hilo katika safari nyingine ikiwemo zile za Kigoma na Mtwara, Bw. Mfinanga alisema wamekuwa wakihudumia idadi kubwa ya abiria kutokana na ndege za shirika hilo kusafiri kwa mwendo kasi wa kuridhisha sambamba na huduma nzuri zinazotolewa kwa wateja wakati wa safari.

“Zaidi tunaamini kwamba huduma tunazozitoa kati ya Tanzania na Comoro zimekuwa zikichangia kuongeza ushirikiano baina ya nchi hizi mbili na tunaamini kuwa hata hili ongezeko la safari zetu kwenye mataifa haya mawili zitatoa fursa kwa wateja wetu kufaidi fursa zinazopatikana ndani ya nchi hizi,’’ aliongeza Bw. Mfinanga.

Kuhusu mpango wa shirika hilo kujipanua zaidi kihuduma, Bw. Mfinanga alisema:  “Ndege yetu aina ya De-Havilland Dash 8 Q300 kwa sasa inafanyiwa marekebisho makubwa kwenye karakana yetu iliyopo kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa  wa Julius Nyerere (JNIA) na itakapokamilika tutaendelea na huduma zetu katika mikoa ya Mwanza, Tabora, Kilimanjaro na Mbeya,’’

Bw. Mfinanga aliongeza kuwa kwa kufanya safari zake kuelekea visiwa hivyo shirika hilo limekuwa likiwezesha wateja wake kunufaika na fursa zilizopo kwenye visiwa hivyo huku pia akitoa wito kwa watanzania wengine kujitokeza kushiriki katika kuchangamkia fursa hizo.

MAZISHI YA SHEKHE OMARY ALHAD, KATIBU WA MSIKITI WA KICHANGANI MAGOMENI JIJINI DAR

MAKALA YA SHERIA:USIKAMATWE NA ASKARI KWA AMRI YA MAHAKAMA BILA KUONESHWA HATI HII.

$
0
0
Na  Bashir  Yakub.

Kifungu  cha  112 ( 1 )  na  ( 2 ) cha Sheria  ya Mwenendo  wa  Kesi  za  Jinai   kinaeleza  kwa  urefu  kuhusu  hati  ya  kumkamata  raia ( warrant  of arrest ) ambayo  hutolewa  na  mahakama. Kifungu  hiki  kimeeleza  namna  hati  hii  inavyopaswa kuwa  na  maudhui  yanayopaswa kuwa  ndani ya  hati  hiyo.   

Lengo  ni  kumfanya raia  ajue anakamatwa  na  nani , kwanini  na anapelekwa  wapi. Ni  hati ambayo  imebeba  taarifa  zinazolenga kusimamia  na   kulinda  haki  za  mtuhumiwa . Yumkini  mengi   yaliyo  katika  hati  hii  huwa  hayatekelezwi  na  wahusika.  Raia  wajue  kuwa amri  ya  kukamatwa  kwa mtu  inapotolewa  na  mahakama ni  lazima  askari  anayekuja  kukamata  awe  na  hati  hii.  

 Asije  askari  kukukamata  kwa maelezo  kuwa  ametumwa  na  mahakama  wakati akiwa  hana  hati  hii. Nisisitize tena kuwa  amri  ya  kumkamata  raia inapotolewa  na  mahakama mkamataji  askari  lazima  aje  na hati  hii  kwa ajili  ya  kutekeleza  kazi  hiyo.   Na  ili  hati  iwe  halali  lazima  iwe  na  taarifa  zifuatazo  kama  tutakavyoona  hapa  chini.

1.      HATI  LAZIMA  IWE  NA  TARIFA  HIZI.

( A ) LAZIMA   HATI  YA  KUKAMATA   IANDIKWE  NA  JAJI  AU  HAKIMU.
Upo  utaratibu  ambao  umezoeleka  ambapo  makarani  wa  mahakama  huandika hizi hati.  Hili  ni  kosa  kubwa  kwani  kifungu  hichohicho  cha  112  cha Sheria ya  Mwenendo  wa  Kesi  za  Jinai  kimeweka  wazi  kuwa  hati  ya kukamata  ni  lazima  iandaliwe  na  hakimu  au  jaji. 

 Afisa  yeyote  wa  mahakama  ambaye si  hakimu  au  jaji    hana  kabisa  mamlaka  ya kuandaa  hati  hiyo.  Basi  kama  ndio  hivyo  ieleweke  kuwa  hati  yoyote ambayo  haikuandaliwa  na  hakimu  au  jaji  ndio hati  batili na  ukamataji  unaotokana  na  hati  hiyo   ni  ukamataji  haramu. 

Nimeeleza  katika  makala  zilizopita  kuwa  sheria  inamruhusu  raia  kugomea  ukamataji  ambao  ni  haramu  kama  huo.  Hivyo  niseme tena  kuwa  ikiwa  hati  ya  kukamata  haikuandaliwa  na hakimu au  jaji  basi   raia  anayo  haki  ya  kugomea  kukamatwa.

(  B )  LAZIMA  HATI  YA  KUKAMATA  IWE  NA  MUHURI  WA  JAJI  AU  HAKIMU . 

Kawaida   kila  mahakama  ina  muhuri  wake  ambao  huwa  na  utambulisho  wa  Mahakama  husika.  Muhuri  huo  huwa  nao  jaji au  hakimu wa  mahakama  husika.  Muhuri  huo  ndio  unaotakiwa  kuwa  katika   hati  ya  kukamata. Kama   ni  hati  imetolewa  na  mahakama  kuu  muhuri  uoneshe  kuwa  ni wa mahakama  kuu  halikadhalika  mahakama  nyinginezo  kama za  wilaya  na  mwanzo.

(  C  ) HATI  YA  KUKAMATA  LAZIMA  IONESHE  KOSA  LA  MTUHUMIWA  KWA  UFUPI.

Mpaka  hati  inatolewa  kunakuwa  na  kosa  ambalo  tayari  raia  ametuhumiwa  nalo.  Hati  hii  haiwezi  kutolewa  iwapo  hakuna  kosa  ambalo   limeanzishwa. Kutokana  na  hilo  ni  lazima  kosa  hilo  lioneshwe ndani ya  hati  hiyo  ili  mtuhumiwa  ajue  anakamatwa  kwa  ajili  ya  nini  ili  naye  ajue anaandaa  nini  na  nini  kuhusu  kosa  hilo. Kwa  mfano kosa  liandikwe hivi, KUUA  KWA  KUKUSUDIA  KINYUME  NA KIFUNGU 196  CHA  KANUNI ZA  ADHABU. 

( D ) LAZIMA  HATI  IONESHE  JINA   LA  MTUHUMIWA  AU  WASIFU  WAKE.
Isiwe  hati  imetolewa kwa  ajili  ya  JOHN  ikatumika  kumkamata  CLEMENT.  Aliyeandikwa  kwenye  hati  ndiye  huyohuyo  anayepaswa  kukamatwa. Hii  ndio  sababu  ya  hati  hiyo  kuwa  na  jina. Kama  haina  jina  basi  iwe  inachambua  wasifu  wa  mlengwa  kwa  namna  hivyo hivyo  alivyo. Kama  haina  jina  au  wasifu    wa  mlengwa  basi  hati hiyo  sio  halali  na  mtuhumiwa anaweza  kuigomea.

( E ) LAZIMA  ITAJE  JINA  LA  ASKARI/AFISA   ALIYETUMWA  KUKAMATA .

Si  kila  askari  anamkamata  anayemtaka. Hati  ya  kukamatwa  hueleza  askari/afisa  maalum  aliyepewa  wajibu  wa  kukamata  mhusika.  Itamtaja  kwa  jina   kuwa  huyu  ndiye  aliyepewa  mamlaka  ya  kumkamata  fulani.

Haya  yote  ni  kwa  mujibu  wa  kifungu cha  112 ( 1 ) ( 2 )   cha  Sheria  ya  Mwenendo  wa Kesi  za  Jinai. ACHA  KUNYANYASWA, CHUKUA  HATUA.
MWANDISHI   WA   MAKALA  HAYA   NI   MWANASHERIA  NA  MSHAURI   WA  SHERIA  KUPITIA  GAZETI  LA  SERIKALI   LA   HABARI   LEO  KILA  JUMANNE  , GAZETI  JAMHURI   KILA  JUMANNE  NA  GAZETI  NIPASHE  KILA  JUMATANO.    0784482959,        0714047241              bashiryakub@ymail.com

KUSOMA  ZAIDI  LINKS goes  to  sheriayakub.blogspot.com.
              

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MAGARI YA UKUSANYAJI TAKA YA KAMPUNI YA GREEN WASTE PRO LTD YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 1.6

$
0
0
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa magari ya kufanyia usafi yanayomilikiwa na Kampuni ya Green Waste Pro ltd.
Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum (kushoto) akikabidhiwa risala na Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw.Abdallah Mbena iliyosomwa wakati wa uzinduzi wa magari ya kufanyia usafi katika manispaa ya Ilala jijini Dar.
Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo (katikati) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi wakiwa kwenye zoezi la kuweka uchafu kwenye moja ya gari la kufanyia usafi lililozinduliwa na Mwenge wa Uhuru.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

INTRODUCING:Tytus - Uzuri wako official video

JARIDA LA WIKI LA NISHATI NA MADINI TOLEO LA 69

Become a Graphic Designer


Tanzania yaadhimisha siku ya hedhi duniani

$
0
0
Tanzania imeadhimisha siku ya hedhi duniani, ambapo wizara ya elimu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamekubaliana kuandaa na kusimamia sera inayoondoa vikwazo kwa watoto wa kike katika masomo yao.

Akizungumza katika maadhimisho hayo jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Elimu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Madina Kemilembe, alisema kukosekana kwa miundombinu rafiki mashuleni kunasababisha wanafunzi kutohudhuria masomo.

Alisema ukosefu wa mazingira bora kama vyoo, maji safi na salama pamoja na vyumba mahsusi vya kubadilishia nguo , hasa kwa watoto wa kike wanapokua katika hedhi mashuleni kunachangia utoro. 

“Nawashukuru wadau Water Aid, Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV), Kasole Secrets pamoja na wengine kwa kuisaidia serikali kuandaa mazingira rafiki kwa watoto wetu kwa kuwajengea vyumba vya kubadilishia na kuhakikisha upatikanaji wa pedi kwa baadhi ya shule,” alisema Kemilembe.

Alisisitiza juu ya utoaji wa elimu kwa wazazi na wanafunzi wa jinsia zote ili kuondoa unyanyapaa ili kuboresha mazingira ya kusoma kwa mtoto wa kike. Naye Mkurugenzi wa Water Aid, Ibrahim Kabole, alisema kuna uelewa mdogo pamoja na mila potofu zinazofanya jambo la hedhi kuonekana ni la aibu.
 Afisa Elimu Mkuu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi Madina Juma, akihutubia wakati wa maadhimisho ya siku ya hedhi duniani yaliyofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya mnazi mmoja. Kauli Mbiu ya mwaka huu inaeleza "Usisite kuzungumzia hedhi".
 Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye maandamano ya kuadhimisha siku ya hedhi duniani yaliyofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania jana jijini Dar es Salaam.Kauli Mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inaeleza "Usisite kuzungumzia hedhi".

MBUNGE LUCY OWENYA AKABIDHI JEZI KWA TIMU ZILIZOFUZU ROBO FAINALI YA LUCY OWENYA CUP 2015

$
0
0
Dkt Fidelis Owenya akikabidhi jezi kwa vilabu nane vilivyo fuzu kucheza hatua ya robo fainali katika mashindano ya kombe la Mbunge lijulikanalo kama Lucy Owenya Cup 2015 yanayofanyika katika jimbo la Moshi vijijini.
Baadhi ya iongozi wa timu zilizofuzu hatua ya robo fainali wakifunga jezi zao mara baada ya kukabidhiwa kwa ajili ya hatua ya robo fainali. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

MWANAHARAKATI BI RITHI HAJI ALI AWATAKA WANAWAKE WENZAKE KUGOMBANIA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI

$
0
0
Na Maryam Kidiko-MaelezoZanzibar  
     
Mwanaharakati  wa  Masuala ya Wanawake wa Jimbo la Mwana kwerekwe  Bi Rihi Haji Ali amewataka Wanawake wenzake  kujitokeza kwa wingi kugombania nafasi mbali mbali za Uongozi ili kuweza kutetea haki zao .

Hayo ameyasema  huko Mwanakwerekwe wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika suala zima la wanawake kuacha woga na kujitokeza kwa wingi kugombania  ili waweze  kujisemea wenyewe na kupata haki zao za kimsingi. 

Hata hivyo amesema wakati umefika kwa Wanawake kujisemea wenyewe na kuacha tabia ya kusemewa matatizo yao jambo ambalo linarudisha nyuma na kuchelewa kupata haki zao za msingi wanazokusudia. 

Amesema kuwa Wanawake  watapojitokeza kwa wingi  na kuwa na ushirikiano mkubwa wataweza kutetea haki zao za msingi hasa katika suala zima la udhalilishaji  unaojitokeza  hapa Nchini kwa wanawake hao.

Vile vile amesema indapo watajitokeza Wanawake kugombani nafasi hizo watatoa ushirikiano mkubwa wa kumpigia kura ili kuwapa hamasa wanaume na wao waweze kuwaunga mkono katika kugombania nafasi hizo.

“Mwanamke yoyote akijitokeza  kugombania Uongozi  tutatoa ushirikiano mkubwa na kuhakikisha anapita katika ushindani huo”Amesema mwanaharakati huyo. Amefafanuwa kuwa wanajitahidi kutoa Elimu sehemu mbali mbali na kuwaelimisha Wanawake jinsi ya kugombea na kuacha imani potofu zinazosemwa Katika Jamii. 

Hata hivyo amesema wataunda Kamati Ndogo ndogo ili kuhakikisha kila Mwanamke aliyekuwa na vigezo vya kugombania nafasi yoyote ya uongozi kuweza kupata nafasi hiyo.

Mwanaharakati huyo ameishukuru Jumuiya   ya Waandishi wa habari Wanawake  Tanzania (TAMWA) pamoja na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kwakuweza kuwatetea Wanawake na kuhakikisha wanapata haki zao za msingi.

Sambamba na hayo amevitaka Vyombo vinavyotoa  Elimu kuhusu masuala ya Wanawake na kuzidi kutoa Elimu kwa Wanawake na kuwataka Wanawake kutoa mashirikiano pamoja na kupendana ili kutimiza lengo walilokusudia.
                                                             
                                 IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

TAARIFA YA ZIARA YA RAIS MSTAAFU ALHAJJ DR ALI HASSAN MWINYI KATIKA JAMHURI YA KIISLAMU YA IRAN

$
0
0


 Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Ali Hassan Mwinyi amefanya ziara ya siku tatu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ziara hiyo ya Rais Mstaafu inafuatia mwaliko wa Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran uliomuomba kuwa mgeni mashuhuri katika sherehe za kuadhimisha miaka hamsini na mbili (52) ya Afrika.

 Siku ya Afrika huadhimishwa tarehe 25 Mei na mataifa ya Afrika pamoja na Mabalozi na Wawakilishi wa mataifa hayo duniani kote, ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kuasisiwa kwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) tarehe 25 Mei 1963.

Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina desturi ya kuungana na Waafrika pamoja na wadau wengine wanaounga mkono hatua za ukombozi na kupinga ubeberu katika maadhimisho ya siku hii muhimu.

Katika sherehe hizo, Rais Mstaafu Mwinyi alihutubia hadhira iliyoongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Dkt Muhammad Javad Zariff na kuhudhuriwa na Mabalozi na Wawakilishi waliopo Iran, Viongozi na Maafisa waandamizi wa Serikali ya Iran, na wadau wengine muhimu ikiwemo wanataaluma, wawakilishi wa sekta binafsi na wanahabari.

Aidha, Rais Mstaafu Mwinyi alipata nafasi ya kukutana na Mkuu wa Kamisheni ya Usuluhishi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye pia ni Rais Mstaafu wa taifa hilo Ayatollah Hashemi Rafsanjani. 

Ayatollah Rafsanjani alikuwa Rais wa Iran wakati Ali Hassan Mwinyi akiwa Rais wa Tanzania na wawili hao waliimarisha uhusiano wa kidiplomasia wa mataifa haya mawili ambapo kila mmoja alizuru nchi ya mwenziwe. Rais Mstaafu Mwinyi aliupokea mwaliko wa taifa hilo kwa lengo la kuzidi kuimarisha uhusiano wa kidugu baina ya Tanzania na Iran. Katika ziara hiyo, Rais Mstaafu Mwinyi aliongozana na Mke wake, Mama Khadija Mwinyi.

MABALOZI WA TANZANIA NJE YA NCHI WATEMBELEA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

$
0
0

Pichani ni Mabalozi wa Tanzania Nje ya Nchi Waliotembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wa kwanza kushoto ni Balozi wa Tanzania Ubeligiji, Luxembourg na Jumuiya ya Ulaya Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala.

MH.ROSEMARY KIRIGINI AITETEA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI

$
0
0

Mh. Rose Kirigini mbunge wa viti maalumu wa CCM na mkuu wa wilaya ya Maswa wakati akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya ujenzi amemuumbua Mh.Mkosamali aliyesema kuwa ilani ya CCM haijatekeleza  ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami inayotoka Mwigumbi - Maswa - Bariadi - Lamadi, Kolandoto - Lalago na Meatu Mjini. 

Alisema kwamba mkandarasi yuko site na tayari ameanza kazi za ujenzi sehemu ya Mwigumbi  - Maswa na   Ujenzi unaendelea kwa Bariadi – Lamadi (km 71.8) . Aidha Barabara ya Kolandoto – Lalago – Mwanhuzi – Matala – Oldeani Jct (km 328), Mkataba umesainiwa na kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina imeanza Julai, 2014 na zinatarajiwa kukamilika Machi, 2016.

NHIF YATOA MSAADA VIFAA TIBA HOSPITALI YA RUFAA BABATI

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera (kushoto) akipokea msaada wa mashuka 150 yatakayotumika jana mjini Babati kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa huo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) Michael Mhando.
 Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) Michael Mhando (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera kifaa tiba cha mama mjamzito jana mjini Babati ili kitumiwe na wanawake watakaopata huduma ya matibabu kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera akionyesha dawa zilizotolewa na Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) Michael Mhando jana mjini Babati, ambapo NHIF ilitoa msaada wa vifaa tiba na dawa zenye thamani ya shilingi milioni 5.5.

SHULE YA SEKONDARI KINYEREZI TABATA JIJINI DAR ES SALAAM YAUNGANISHIWA VIFAA MAALUM VYA KUJIFUNZIA MASOMO KUPITIA KOMPYUTA

$
0
0
 Mkuu wa taasisi ya Vodacom Foundation, Renatus Rwehikiza (kushoto) akishirikiana na wasimamizi wa mradi wa kompyuta mashuleni Meelis Kuuskler (katikati) pamoja na Julius Giabe kuunganisha kifaa cha kujifunzia masomo  kupitia kompyuta  katika shule ya sekondari Kinyerezi  ya Tabata jijini Dar es Salaam.  Mradi huo unaendeshwa na Learning In Sync  chini ya Vodacom Foundation.
 Msimamizi wa mradi wa kompyuta mashuleni, Meelis Kuuskler (katikati)akiwafafanulia jambo Mkuu wa taasisi ya Vodacom Foundation, Renatus Rwehikiza (kushoto) na Julius Giabe kuhusu kifaa cha kujifunzia masomo  kupitia kompyuta  kilichokuwa kinaunganishwa katika shule ya sekondari Kinyerezi  ya Tabata jijini Dar es Salaam. Mradi huo unaendeshwa na Learning In Sync chini ya Vodacom Foundation.
 Msimamizi wa mradi wa kompyuta mashuleni, Meelis Kuuskler akiunganisha kifaa maalum cha kuchajia kompyuta katika shule ya sekondari Kinyerezi  ya Tabata jijini Dar es Salaam.  Mradi huo unaendeshwa na Learning In Sync chini ya Vodacom Foundation utakabidhiwa hivi punde.

Tanzania kukabiliana na Uharibifu wa Mazingira - Waziri Mahenge

$
0
0


Na Victor Mariki - Ofisi ya Makamu wa Rais

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais ( Mazingira), Dk. Binilith Mahenge amesema kuwa Serikali inaendelea  kukabiliana na changamoto za uharibifu  wa mazingira kwa kuhamasisha utekelezaji  wa mipango  ya kitaifa ya kuhifadhi mazingira pamoja na miongozo yake.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa maandalizi ya  maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo hufanyika  tarehe 5 Juni kila mwaka ambapo mwaka huu maadhimisho hayo yatafanyika jiji la Milani nchini Italia kimataifa na kitaifa yatafanyika mkoa wa Tanga.

Aidha Waziri Mahenge, alibainisha baadhi ya sababu za kuichagua Tanga kuwa sehemu ya maadhimisho hayo  ni kutokana na changamoto za mazingira zinazoukabili mkoa huo ikiwemo uvuvi haramu, uharibifu vyanzo vya maji, mmomonyoko wa fukwe pamoja na  kuzama kwa visiwa vya  Maziwe kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Aliongeza kuwa ujumbe wa  maadhimisho ya siku hiyo mwaka huu unasema " Ndoto Bilioni Saba. Dunia Moja. Tumia Rasimali kwa Ungalifu." ambapo alifafanua kuwa ujumbe huo unahimiza jamii katika umuhimu wa utumiaj endelevu wa rasimali kwa faida zao na kwa kizazi kijacho kwa kuzingatia ongezo la watu duniani lilofikia bilioni saba kwa sasa.

Sanjari na hayo Waziri Mahenge alitoa wito kwa kila mkoa kutekeleza shughuli za kuhamasisha uhifadhi wa mazingira kwa kudhibiti uvunaji miti, kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala ya kuni na mkaa, kupanda miti inayofaa kwenye vyanzo vya maji na kuvitaka viwanda vizingatie uzalishaji bora utakaopunguza  gesijoto na kuwa na mifumo mizuri ya majitaka.

Major finals, plus Copa America and more, in SuperSport’s never-ending football offering

$
0
0


As the football season nears its conclusion, SuperSport viewers will find themselves in the unique position of having the luxury of watching three major finals - the FA Cup, the German Cup and Copa del Rey - this weekend. No other broadcaster in the world can rival this feast of football.

Arsenal, playing a record 19th FA Cup final, will be looking to successfully defend their title when they take on Aston Villa at the iconic Wembley Stadium (live on SS3 HD from 5.30pm).

Borussia Dortmund face Wolfsburg in the German Cup final (live on SS7 HD from 7.55pm) determined to put behind them a forgettable 2014-15 season, which saw them flirt with relegation at one point, by winning the cup which could also be a parting gift to coach Jurgen Klopp. He is leaving after an eight-year stay.

With one out of the three titles they are bidding for already in the bag, Barcelona renew their Copa del Rey final rivalry with Athletic Bilbao. It’s their eighth final meeting and they are seeking the dream double. The match is live on SS3 HD from 9.30pm.

The curtain officially comes down on the football season next weekend when Juventus battle it out with Barcelona for club football’s ultimate prize, the Champions League title. The winner could be a treble champion.

SuperSport’s extensive coverage of the final includes an hour-long pitch-side build-up with Carol Tshabalala and Benni McCarthy. Despite the Champions League final signaling a close, the season never ends on the World of Champions. 

Just five days later South America’s finest footballers will kick up a major storm as they battle it out for continental glory in the 44th edition of the COPA America. The June 11–July 4 tournament, hosted by Chile, will be broadcast exclusively live and in HD on SuperSport.

“South America continues to be the biggest exporter of football talent to the world and the Copa America is the ground where star players like Neymar, Sergio Aguero, Alexis Sanchez, Edinson Cavani, Phillipe Coutinho and others announce themselves before moving on to some of the biggest clubs across the world. We are ecstatic at being able to bring such a prestigious tournament to our viewers,” said a beaming Brandon Foot, Acting Chief Executive of SuperSport. 

Article 4

StarTimes – SmartCodes Campagn on Mobile Application fosters Digital Solutions on Digital Broadcasting

$
0
0
 Since December 31, 2012 Tanzania started migrating from analogue to digital broadcasting. The implementation has been successful by 100% which makes Tanzania the first country in the East African Community (EAC) and Southern Africa Development Community (SADC) to meet the deadline imposed by the International Telecommunication Unity (ITU). In fostering this process StarTimes in partnership with SmartCodes is now running a campaign which offers an added value to digital broadcasting.  

Digital broadcasting which allows the consumers to choose from multiple methods of receiving television signals has given innovators at SmartCodes and Startimes the opportunity to make TV more private and personalized. Tenbre a mobile application that can be downloaded for free allows the user to access StarTimes guide wherever they are and share it.

With this mobile application the user can; find out what are showing in the next 7 days; sort all channels according to countries, regions, genres and bouquets; create their own favorite channel list; search shows or channels by the title; see what shows are on air; see the ranking order of the coming shows; see recommended shows and channels; set reminders for any show they like; view their wallet; receive their tasks and gain coins; alert setting; view their reminders and favorites; invite friends and get free coupon for recharging; access user friendly chat room; top post in each chat room for easy viewing of up-to-date information; support long press to copy text in chat room; support directing web links by clicking on the link; view number of people currently online in each chat room hence the number of people who are watching particular TV at that particular moment. All this has been made possible on the hand of the consumer.

It is of great honor that SmartCodes and StarTimes have pioneered in digitizing Tanzania. The big idea here is merging tradition with modern which is what SmartCodes envision. SmartCodes believes that if the government of the United Republic of Tanzania continues to support such initiatives by making them more accessible and affordable by year 2020 Tanzania will be the hub of technological innovation in Africa.  As we say in SmartCodes technology is for everyone and so it ought to be.

SmartCodes is the awards winning Tanzanian full service digital agency. SmartCodes is a single stop for all digital pursuits. Over the past 5 years, the commitment of the innovative minds you could find in the industry has contributed to the dynamic growth of Digital Industry not only in Tanzania but Africa. SmartCodes has contributed immensely on the exponential growth of digital products consumption in Tanzania. 

Currently Tanzania has about 31.86million mobile phone users and of that about 40% uses smartphones. With that rapid growth SmartCodes is now servicing a vast portfolio of clients across the sub-Saharan Africa. Quality, on time delivery and on budget has been their strongest reputation.

Viewing all 110108 articles
Browse latest View live




Latest Images