Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

NHIF WAZINDUA MPANGO WA HUDUMA ZA MADAKTARI BINGWA MANYARA.

$
0
0
 Meneja wa NHIF Mkoa wa Manyara, Innocent Mauki akiwakaribisha viongozi wa NHIF makao makuu na uongozi wa Mkoa wa Manyara, kwenye uzinduzi wa mpango wa huduma za madaktari bingwa Mkoani Manyara. 

Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, wakishuhudia Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Nkaya akizindua mpango wa huduma za madaktari bingwa mkoani humo, zilizowezeshwa na NHIF
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Nkaya Bendera akizungumza asubhi ya leo kwa kuwa mkoa huo kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) kwenye uzinduzi wa mpango wa huduma za madaktari bingwa mkoani Manyara uliowezeshwa na NHIF.
 Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Nkaya Bendera (kushoto) akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Ally Uredi vifaa tiba na dawa zilizotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF) ambazo gharama zake ni shilingi milioni 5.5.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


LORI LAPIGA MWELEKA LIKIJARIBU KUKWEPA GARI NYINGINE KIJIJI CHA KITUMBI

$
0
0
 Lori la Mizigo lenye namba za usajili T 112 BAL lililokuwa na tela lenye namba za T 108 AVT likiwa halitamaniki baada ya kupata ajali alfajiri ya leo kwenye kijiji cha Kitumbi, Wilayani Handeni Mkoa wa Tanga. Kwa mujibu wa utingo wa lori hilo, aliefahamika kwa jina la Makeke Moses, amesema kuwa kutokea kwa ajali hiyo kulisababishwa na Lori lingine (halipo pichani) lililokuwa limeharibika na kusimama katikati ya barabara bila ya kuwa na ishara yeyote ya tahadhali, hali iliyompelea dereva wake kutumia maarifa yake ya kiudereza ili kulikwepa lori hilo, lakini maarifa hayo hayakuzaa matunda na kujikuta wakitoka kando ya barabara mpaka kufikia hapo. hakuna aliepoteza maisha katika ajali hiyo.
 Kichwa cha lori hilo kikiwa pembeni baada ya kutolewa.
 Zoezi la ufaulishaji mizigo likaanza na hapo barabara ikafungwa kwa muda ila kufanikisha zoezi hilo.
 Baadhi ya Matingo wa malori mengine wakimjulia hali Utingo mwenzao alienusurika ajalini.

IJUMAA HII @ RHAPSODY' S - DJ PETER MOE & GROOVEBACK TEAM

Tanzania yapata Mabilioni ya pesa kusaidia maendeleo

$
0
0
Gavana wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Servicus B.Likwelile ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Bw. Aly Abou- Sabaa wakisaini mkataba wa Tsh 137.5 Billion kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo kwa serikali ya Tanzania. Sherehe hiyo ilifanyika hapa Mjini Abidjan- Ivory coast.
Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Bw.Aly Abou – Sabaa na Gavana wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servicius Likwelile wakipongezana mara baada ya kusaini mkataba wa Tshs 137.5 Billoni wa kusaidia kwenye sekta ya umeme na nishati nchini Tanzania.
Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Bw. Aly Abou-Sabaa na Gavana wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servicius Likwelile pamoja na wajumbe waliohudhuria katika hafla ya kutia saini mkataba wq kiasi cha Tsh. 137.5 Billion kwa ajili ya kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo hasa umeme nchini Tanzania.

COKE STUDIO AFRIkA MSIMU WA TATU YAANZA

$
0
0
KUFUATIA mafanikio makubwa yaliyopatikana katika Msimu wa Pili wa Coke Studio Africa, Kampuni ya Coca-Cola kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Kenya, inayo furaha kutangaza kuanza tena msimu wa tatu wa burudani ya muziki maarufu kwa jila la Coke Studio Africa. msimu huu utajumuisha wanamuziki wakali 26 barani Afrika huku nyimbo mpya 52 kutumbuizwa ikiambatana na maonyesho 9 ya wanamuziki wanaotamba hapa duniani. 

Maonyesho hayo ya muziki ya Coke Studio Africa ni tofauti na mengine ya aina hiyo yanayolenga zaidi kupatikana mshindi. Badala yake, maonyesho haya yanalenga kujumuisha pamoja vipaji tofauti vya wanamuziki mbalimbali kutoka barani Afrika. Aidha, yanatoa fursa kwa wasanii wanaochipukia kufanya pamoja kazi zao na wanamuziki nguli wa ndani na wale wa ngazi za kimataifa.
Alikiba
Msimu huu unaozinduliwa utawakutanisha wanamuziki kutoka katika nchi za Tanzania, Msumbiji, Kenya, Uganda na Nigeria, na kwa mara ya kwanza wasanii hawa wataweza kukonga nyoyo za wapenzi wa muziki kwa kushirikiana katika staili ya kipekee ijulikanayo kama mash-ups – ambayo inatawala kwa sasa katika tasnia ya muziki duniani. “Kufurahia muziki wa Kiafrika” ikiwa ndiyo kiini kikuu cha burudani hiyo, msimu huu mpya wa Coke Studio Africa utawakutanisha wasanii maarufu ambao wameonyesha mafanikio makubwa katika kazi zao, na pia maonyesho hayo yatawaleta pamoja wasanii nyota wanaochipukia katika ulimwengu wa muziki.

Chini ya ushirikiano huo mpya na Kampuni ya Coca-Cola, Shirika la Ndege la Kenya kwa upande wake litawasafirisha wasanii wote na waandaaji wa muziki wanaoshiriki katika Msimu wa Tatu wa Coke Studio Africa. Mpango huo wa ushirikiano wa makampuni haya makubwa unatokana na imani ya kwamba hatua hiyo itajenga msingi wa ubia muhimu wa kufanya kazi kwa pamoja.
Vanessa Mdee

Akizungumzia juu ya Coke Studio Africa Msimu wa Tatu, Meneja Bidhaa wa Coca-Cola Tanzania, Maurice Njowoka alisema: “Lengo letu ni kuufanya na kuwezesha namna ambayo muziki unavyoweza kuchukua nafasi katika kukonga nyoyo za watu katika Bara letu. Coke Studio Msimu wa Tatu si kwa ajili ya kuwakutanisha tu wanamuziki wa Afrika, bali pia maonyesho haya yanatoa fursa ya pekee ya ushirikiano ambao ni imani yetu kuwa wateja wetu pamoja na umma kwa ujumla wangependa kuusikia.”

Donald Kaberuka of African Development Bank feted with the WWF Leaders for a Living Planet award

$
0
0
Abidjan, Wednesday 27 May 2015 – WWF awarded its prestigious Leaders for a Living Planet award to Donald Kaberuka, outgoing African Development Bank (AfDB) President, in recognition of his bold steps to mainstream sustainability concerns and champion the fight against illicit wildlife trade during his tenure at the African Development Bank. At a colorful luncheon on the sidelines of the AfDB’s Annual Meetings, Marco Lambertini, WWF Director General gave tribute to Mr Kaberuka‘s effort to stem the increasing large-scale illegal trade on the continent.

Donald Kaberuka is widely recognized for his call for urgent action to tackle the severe crimes of poaching and the illegal pillaging of the natural resources of the African continent. At the London Conference on the Illegal Wildlife Trade in February 2014, Mr Kaberuka said: “Our people, our natural resources and our very economic development are in danger. The illegal trade in wildlife is undermining the foundations of our development, its natural resources”.

At the Marrakesh AfDB Annual Meetings in 2013, AfDB called on governments, businesses and civil society to urgently mobilize in this fight to protect the biodiversity of Africa. “I call on all leaders in Africa and elsewhere to invest in the future of our region, by all possible means, to strengthen law enforcement and criminal justice for these crimes,” Kaberuka urged in Marrakesh. The AfDB President has repeatedly stressed how much this fight, going beyond governments, institutions and associations, concerns all Africans.

WWF’s Leaders for a Living Planet award aims to recognize the individuals who make a significant personal contribution to the conservation of the natural world and sustainable development. WWF publicly celebrates these individuals and their achievements to profile their environmental leadership and the inspiring example they show to others.

The award is symbolic. It enables WWF to congratulate individuals and their achievements, together with the government, company, community or organization they represent, and to encourage further action. Over 100 such awards have been made since 2000, recognizing a wide variety of initiatives. These range from local actions to protect wildlife to the leadership of government ministers to achieve specific conservation goals such as sustainable fisheries and new protected areas. Recent high-level recipients include Kofi Annan, the former UN Secretary-General, as well as the Minister of Fisheries of Norway, the Vice-Premier of China, and the Ministers of Water Affairs of France, Togo and Benin.

“The actions of individuals recognized as WWF Leaders for a Living Planet demonstrate visionary environmental leadership and personal responsibility to protect the planet, for a future where people and nature thrive. Donald Kaberuka is an extremely inspiring example – as a leader who is working to create a better world for current and future generations, leading the African Development Bank toward green growth and sustainable development,” said Marco Lambertini, Director General of WWF International.
Donald Kaberuka, President, African Development Bank receives the WWF Leader for a Living Planet award presented by Marco Lambertini, WWF Director General at the 2015 AfDB Annual Meetings in Abidjan, Cote d’Ivoire. Looking on is Hawa Sow, WWF Africa Institutional Partnerships Lead.

Rais Kikwete alipomuapisha Balozi Mulamula na Naibu wake pamoja na Balozi mmoja

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR AFUNGA MKUTANO WA MABALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA JIJINI DAR

$
0
0
Balozi Seif kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein akiufunga Mkutano wa Nne wa siku Tatu wa Mabalozi wa Tanzania uliokuwa ukifanyika katika Hoteli ya Ramada Mjini Dar es Salaam.Baadhi ya Mabalozi wa Tanzania katika Mataifa mbali mbali Duniani walioshiriki Mkutano wao wakifuatilia Hotuba ya Ufungaji wa Mkutano huo iliyosomwa na Balozi Seif kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. ASli Mohammed Shein.Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa Tanzania Nchi mbali mbali Duniani mara baada ya kufunga Mkutano wao wa Nne ulifanyika Ramada Hoteli Jijini Dar es Salaam. Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mh. Bernard Membe, Katibu Mkuu Mpya wa Wizara hiyo Balozi Lebereta Mula mula na kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh. Mhadhi Juma Maalim. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Jamuhuri ya Watu wa China Balozi Abrahaman Nyimbo mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Mabalozi wa Tanzania Mjini Dar es salaam. Picha na – OMPR – ZNZ.

ZAIDI SOMA HAPA


MANGO GARDEN NYEUPE WIKI HII, BURUDANI NI MOJA TU …YAMOTO BAND NA MASHAUZI LEO USIKU

$
0
0
Kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi, ukumbi wa Mango Garden Kinondoni unapitisha wikiendi bila burudani yoyote na badala yake onyesho la Yamoto Band na Mashauzi Classic leo usiku ndio show pekee wiki hii katika ukumbi huo. 

Kesho Ijumaa  Malaika Band ambao hupiga hapo Mango kila Ijumaa, watakuwa Arusha mjini. Twanga Pepeta ambao hupiga Mango Garden kila Jumamosi, Jumamosi hii watakuwa Wenge Garden Ukonga.

Bendi ya FM Academia ambayo huibuka Mango Garden na kufukia viraka vya bendi zilizopata dharura ya kuhama ukumbi, Ijumaa hii itakuwa Polisi Kilwa Road wakati Jumamosi itakuwa Leaders Club katika tamasha la nyama choma.

Yamoto Band watakwea jukwaa la Mango Garden Kinondoni leo usiku (Alhamisi, 28) kuonyeshana kazi na wenyeji wao Mashauzi Classic chini yake Isha Mashauzi.

Ni onyesho ambalo limeteka hisia za mashabiki wa muziki kutokana na ukweli kuwa vikundi hivyo viwili havijawahi kukutana katika katika onyesho la pamoja, ukiondoa yale matamasha yanayoshirikisha wasanii wengi.

MISA YA MAREHEMU MZEE SAMUEL LUANGISA KUFANYIKA JUMAMOSI MAY 30, 2015

$
0
0
MZEE SAMUEL NTAMBALA LUANGISA

Familia ya Marehemu Mzee Luangisa na New York Tanzania Community, inawakaribisha kwenye MISA ya kumuaga Marehemu Mzee wetu, Baba yetu na Kiongozi wetu Mzee Samuel Ntambala Luangisa (83), kabla ya kwenda Bukoba kwa mazishi Siku Jumamosi MAY 30th, 2015
kuanzia Saa: 1pm - 5pm

Address: LEE'S Funeral Home L.L.C
160 Fisher Avenue
White Plains, NY 10606

Baada ya Misa sote tutajumuika nyumbani kwa Wafia The Luangisa Residence: 

374 Hawthorne Terrace, 
Mt. Vernon, NY 10552

Mpe taarifa mwenzako wote karibuni. 

Kwa taarifa zaidi wasikiana na:

1. Prof. K. Lwiza 631-273-3859
2. Dr. Abas Byabusha 914-584-7502
3. Shabani Mseba 347-712-8539
4. Hajj Khamis 347-623-8965

Ukitaka kutoa rambirambi yako unaweza kutumia number hizi hapa chini.
Luangisa na Kwame Luangisa. Bank ni Bank of America. Account# 9504210977. Routing# 021000322. Swift code ni BOFAUS3N. 

Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake la Bwana litukuzwe. Amen!

TANZANIA KUTOA NAFASI ZAIDI KUWEZESHA WAKIMBIZI KUWA NA MAISHA YA KAWAIDA

$
0
0
DSC_0113
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akizungumza kwenye mkutano wa kupokea taarifa fupi ya hali ya wakimbizi katika mji wa Kigoma na changamoto wanazokabiliana nazo mbele ya wawakilishi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini.
DSC_0128
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumzia jitihada zilizofanywa na Umoja wa Mataifa kupitia Shirika lake la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na mashirika mengi katika kuhakikisha huduma zote muhimu zinapatikana kwa haraka zaidi ili wakimbizi nao wafarijike kama binadamu wengine sambamba na sheria za Umoja wa Mataifa zinavyotaka. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe na watatu kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole.
DSC_0134
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendelea na mazungumzo na viongozi mbalimbali wa ulinzi na usalama wa mkoa wa Kigoma.
DSC_0146
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole akizungumza katika mkutano huo ambapo ameipongeza serikali ya Tanzania kwa moyo wake wa upendo na kutenga maeneo maalum ya kuhifadhi Wakimbizi kutoka nchi za jirani.
DSC_0163
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe katika picha ya pamoja ya viongozi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na wa mkoa wa Kigoma sambamba wafanyakazi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yaliyopiga kambi mkoani Kigoma kuhudumia Wakimbizi.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

HOSPITALI YA POLISI KILWA ROAD YAPATA VIFAA VYA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI

$
0
0

Balozi wa Misri Nchini, Hossam Moharam (kulia), akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kushoto), kontena lenye vifaa vya chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Jeshi la Polisi Kilwa Road. Wa kwanza kushoto ni Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Abdulrahmani Kaniki.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kushoto), akiongozana na Balozi wa Misri Nchini, Hossam Moharam (kulia), kuelekea kwenye jengo litakalotumika kwa ajili ya kuhifadhia maiti  katika hospitali ya Jeshi la Polisi Kilwa Road jijini Dar es Salaam.

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akizungumza  wakati wa hafla ya makabidhiano ya kontena lenye vifaa vya chumba cha kuhifadhia maiti vilivyotolewa na Serikali ya Misri kwa Hospitali ya Jeshi la Polisi Kilwa Road Jijini Dar es Salaam.


 Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Abdulrahman Kaniki akizungumza  wakati wa hafla ya makabidhiano ya kontena lenye vifaa vya chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Jeshi la Polisi Kilwa Road jijini Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi nchini, Richard Malika akitoa maelezo kuhusu mchoro wa jengo la kuhifadhia maiti linalojengwa  katika Hospitali ya Jeshi la Polisi Kilwa Road jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi na Balozi wa Misri Nchini, Hossam Moharam wakimsikiliza.

Jivunie Utanzania na dot tz (.tz)

$
0
0
Kama utakuwa na kumbukubu nzuri kipindi cha nyuma kidogo ulikuwa ukiingia kwenye mtandao utakuta domain nyingi ziko kwa namna ya jinafulani.com alafu baada ya muda tukaanza kuona jinafulani.co.uk ila hapakuwa na jinafulani.co.tz. Hilo lime badilika na kwa takwimu za sasa kuna takribani domain 10,000 zinazoishia na .tz ambazo zimesajiliwa na tzNIC moja kwa moja au kupitia wakala wao. 

Tanzania Network Information Centre (tzNIC) ni msajili wa domain zinazo ishia na .tz. Hivyo pale unapo taka kusajili domain ambayo inaishia na .tz hawa ndio wahusika wakuu. tzNIC wanasimamia mfumo ambao una onyesha barua pepe yani email na servers zote zinazo ishia na .tz na zilipo. Tanzania Network Information Centre nishirika lisilo la kutafuta faida (nonprofit) ambalo lilianzishwa na kusajiliwa mwaka 2006 kwaajili ya kusimamia na kutekeleza shuguli zote zinazo husiana na Tanzania country code Top Level Domain (.tz ccTLD). 

tzNIC ni limited company (kwa dhamana) ambayo ina waanzilishi wawili ambao ni TCRA ambae ni mdhibiti mkuu wa maswala ya mitandao Tanzania na TISPA (Tanzania Internet Service Provider Association) ambae ni sehemu ya chama cha ISP (Internet Service Provers Association).

Lengo la tzNIC

Lengo kuu la tzNIC ni kukuza matumizi ya majina ya domain yanayo ishia na .tz pamoja na kulinda maslahi ya walio sajiliwa kwa kuwapa database ambayo ina ulinzi wa kutosha na unafuu. Kwa kufanya hivyo huwapa watumiaji fursa ya kuonekana dunia nzima, wana brand huduma yako na muonekano wa kitanzania, kuongeza ushindani wa biashara yako ndani na nje ya Tanzania, kuwezesha domain yako ulio sajili kupata watembeleaji wengi wa ndani ya nchi ya Tanzania, na kukuza utumiaji wa mtandao katika biashara.

Wako wapi
Head office za tzNIC (Tanzania Network Information Cetre) ziko Suite #4 Ground Floor, of LAPF Millenium Towers, at the New Bagamoyo Road, Dar es Salaam na namba zao za simu ni +255 22 2772659 fax: +255 22 2772660 na email address ni: info@tznic.or.tzhivyo pale unapo taka ku register domain yako au una tatizo linalo husiana na usajili wa domain usisite kuwasiliana nao au kuwatembelea.

Diamond Platinumz aibukia programu ya Mziiki

$
0
0
Nyota wa muziki wa bongo flava nchini Diamond Platinumz amewataka wasanii wa Tanzania kusambaza nyimbo zao kwa njia ya teknolojia kama vile Mziiki iliyozinduliwa hivi karibuni ili ziweze kuwafikia watu wengi na kwa wakati huohuo wanamuziki pia kunufaika na jasho lao.

Diamond anasema kuwa  ameamua kazi zake kuziingiza sokoni tofauti na kazi zake za nyuma ambapo baada ya  kushauriana na wadau anaoshirikiana nao kikazi ameamua aingie sokoni kwa njia ya kidigitali kupitia programu ya Mziiki iliyozinduliwa hivi karibuni ambayo pia yeye ni balozi anayeitangaza.

Anasema Tanzania ina wanamuziki wengi wenye vipaji lakini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikiwafanya wasifike mbali zaidi ya muziki wao kusikika hapa nchini na wengi wao kutamba kwa muda mfupi na kupotea katika ulimwengu wa muziki huku wakiwa hawajanufaika na kitu chochote kimaisha na kushauri kuwa  wasibaki nyuma kiteknolojia hasa wakati wa kupeleka kazi zao sokoni iwapo watataka kujikwamua.

WAZIRI KOMBANI AIPA SOMO MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII NCHINI.

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani ( kati kati) akisisitiza jambo.

 Katibu Mkuu wa TSSA, Meshack Bandawe ( kushoto ) akiwa na mwezeshaji wa mafunzi, Patrick Ngwila.

Na John Nditi, Morogoro

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani, ameitaka Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini kuelekeza nguvu zao vijijini kwenye idadi kubwa ya  wananchi na wazalishaji wa mali wanaohitaji huduma zao badala ya kung’ang’ania mijini pekee.

Kombani alitoa changamoto hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku nne yaliyoanza Mei 25 hadi kufikia 28, 2015 mjini Morogoro ya  kuwajengea uwezo na ufahamu wafanyakazi wanaunda Jumuiya ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA) kutoka katika mifuko ya Hifadhi ya jamii ya PPF,NSSF,LAPF,GEPF,NHIF na ZSSF.

Hata hivyo alisema,  mifuko hiyo imekuwa ikikimbilia kutafuta wanachama katika maeneo ya mijini na kushindwa kubuni mbinu mbadala za kuwafikia wananchi wengi wanaoishi vijijini.

Kwa mujibu wa Waziri huyo kuwa, dhana iliyojengeka kutoka kwa Mifuko hiyo kuwa vijijini hakuna watu wenye vipato sasa imepitwa na wakati kwa kuwa wananchi wanaishi vijijini  ni wakulima, wafugaji na  wafanyabiashara ndogo ndogo ambao  wanaouwezo mkubwa wa kuchangia mifuko hiyo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Article 2

Mkapa - Zero HIV and AIDS in Tanzania is Possible

$
0
0
 Dr. Fatma Mrisho, Executive Director for Tanzania Commissions for AIDS (TACAIDS), joined by Former President Hon. Benjamin Mkapa (centre) and The Managing Director of AngloGold Ashanti - Geita Gold Mine Mr. Terry Mulpeter and Mr. Simon Shayo Vice President of Sustainability and their colleagues during the launch of Kilimanjaro Challenge 2015 campaign in  Dar es Salaam. TACAIDS received a cheque worth two hundred million so as to facilitate the eradication of HIV and AIDS in Tanzania.
 DC of Geita, Hon. Manzie Mangochie receive TZS 100M on behalf of Geita District Hospital from the Former President Hon. Benjamin Mkapa and The Managing Director of AngloGold Ashanti - Geita Gold Mine Mr. Terry Mulpeter and Mr. Simon Shayo Vice President of Sustainability during the launch of Kilimanjaro Challenge 2015 campaign in Dar es Salaam. 
 The Former President Hon. Benjamin Mkapa and The Managing Director of AngloGold Ashanti - Geita Gold Mine Mr. Terry Mulpeter and Mr. Simon Shayo Vice President of Sustainability at AngloGold Ashanti - Geita Gold Mine during the launch of Kilimanjaro Challenge 2015 campaign in Dar es Salaam.
Some of the participants joined by the Former President Hon. Benjamin Mkapa and The Managing Director of AngloGold Ashanti - Geita Gold Mine Mr. Terry Mulpeter and Mr. Simon Shayo Vice President of Sustainability at AngloGold Ashanti - Geita Gold Mine during the launch of Kilimanjaro Challenge 2015 campaign in Dar es Salaam.

Kaymu Partners with the Nyama choma festival

$
0
0
Kaymu Partners with the Nyama choma Festival ticket sales.
28th May 2016 Dar-es-salaam, Tanzania- Kaymu, Tanzania’s number one online market place has partnered with the Nyama Choma festival to sell the events tickets online, of which the event will be held at the Leaders club on the 30th of May 2015. The tickets are available to anyone for a massive discount of only Tsh 5000, which is double the amount you will need to pay at the gate on the day of the event.

Kaymu Tanzania’s Head of Marketing, Angaza Nkurlu said; “We are very proud to announce this exciting partnership, this continues to prove that e-commerce is a fast growing digital lifestyle in Africa and many Tanzanians are taking advantage of it”

He continues; “This will help people pre-order discounted tickets to their favorite event online, this rewards those who plan ahead by helping them save money and avoid long queues at the event, any person can simply go on our website, search for the key words “Nyama Choma” and press “Buy now” and register themselves, after doing so they will receive a unique order number via sms and email of which they will have to show at the gate on the day of the event. After confirmation and payment the person will be allowed to enter the grounds.  

Additionally, anyone with a Tigo mobile wallet can also pre-pay through Kaymu’s safe pay; this will reduce the reliance on carrying sufficient cash everywhere at the event. Additionally, everyone who pre-orders through Kaymu will be automatically entered into a raffle where any random buyer can win him or herself a VVIP card. The VIP card consists of entrance to all Nyama choma festival events for a whole year (+one), reserved parking, hospitality tent treatment and so much more .The winner will be announced on Friday 29th May 2015.

That Advance ticket sales are available on Kaymu until Noon Friday May 29, 2015! Click hereto Order your 50% discounted advance Nyama Choma ticket!

SERIKALI YASHAURIWA KUONGEZA BAJETI WIZARA YA HABARI

$
0
0
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo leo bungeni mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Mhe. Said Mtanda akiwasilisha mapendekezo ya kamati yake kuhusu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa bajeti ya wizara hiyo leo mjini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na Naibu Katibu Mkuu Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kutoka kushoto) wakifuatilia kwa makini bajeti ya Wizara hiyo leo mjini Dodoma. 
Naibu Waziri wa  Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Juma Nkamia akimsikiliza Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi kwenye viwanja vya bunge leo mjini Dodoma. PICHA ZOTE NA FATMA SALUM - MAELEZO

TRADE MISSION TO THE US

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images