KIPINDI CHA DIRA YA DUNIA
↧
↧
CAF YAIPA TANZANIA UENYEJI FAINALI ZA U17
Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika -CAF leo hii limeipa Tanzania uenyeji wa fainali za michuano ya Afrika ya vijana umri chini ya miaka 17 mwaka 2019.
Uenyeji huu ni hatua muhimu sana kwa Tanzania katika kukuza soka la vijana na kwa hatua hii Tanzania itacheza moja kwa moja fainali hizi.
Katika kuandaa kikosi bora cha kushiriki fainali hizi Tanzania, mwezi Juni mwaka huu TFF itaandaa mashindano ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 13 na wachezaji bora wa mashindano haya wataunda kikosi cha mwanzo cha Taifa kuelekea fainali za mwaka 2019.
TFF inamshukuru sana Rais Jakaya Kikwete na Mh. Fennela Mukangara Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kufanikisha maamuzi haya, na inaamini ushirikiano huu wa Serikali na wadau wengine utafanikisha mashindano haya mwaka 2019.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF).
↧
MAKALA YA SHERIA; NI KOSA ASKARI KUONDOKA NA MTU MWINGINE BAADA YA KUMKOSA MTUHUMIWA NYUMBANI.
Na Bashir Yakub.
Malalamiko ya raia dhidi ya jeshi la polisi hayataishi kama polisi wenyewe hawatajirekebisha. Na ieleweke kuwa si kweli kwamba wanaolalamika ni wajinga au hawana sababu za msingi. Mara zote ukiangalia malalamiko ya raia huwa ni ya msingi na mzizi wake ni mmoja tu. Ni utamaduni wa askari wetu kutopenda kutenda hatua kwa hatua kama sheria inavyoagiza. Sheria imetoa maelezo mazuri tu ya namna ya kuyaendea mambo. Tatizo watekelezaji ndio hakuna.
Sheria husema kingine na watekelezaji hufanya kingine. Namna hii huwezi kuepuka chuki na migongano kati ya hawa watekelezaji askari na raia. Na migongano na kutokuelewana kunapokuwa kukubwa na usalama nao unayumba kwakuwa ili askari afanye kazi ya usalama vizuri anategemea msaada wa raia karibia kwa asilimia zaidi ya 80. '
Na raia huyu hatatoa ushirikiano wakati jana umempiga bila sababu, umemtukana na kumtolea maneno ya kebehi. Makala iliyopita nilizumgumzia namna sheria inavyomruhusu raia kukataa kukamatwa na polisi iwapo polisi huyo atakiuka taratibu katika ukamataji. Leo nazungumzia namna sheria inavyokataza kumchukua mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi wa kosa. Tutaona hili likoje.
1.ASKARI KUONDOKA NA MTU MWINGINE BAADA YA KUMKOSA MTUHUMIWA HALISI.
Hii ni tabia ambayo imezoeleka sana na ipo kwa muda mrefu. Yumkini kuzoeleka kwake na kuwepo kwake kwa muda mrefu hakuifanyi hata kwa sekunde moja tabia hii kuwa halali kisheria. Mara nyingi wanaokutwa sana na tabia hii ni watu wa vijijini hasa wa hali ya chini. Lakini hata mijini pia ipo sana. Nazungumzia tabia ya kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi. Kwa mfano askari wamekuja nyumbani kumtafuta JOHN kwa kosa analotuhumiwa nalo. Bahati mbaya au nzuri JOHN hayupo nyumbani.
Kutokana na hilo askari wanaamua kuondoka na mke wa JOHN au mtoto wake ili kumfanya JOHN aweze kutokea. Hiki ndicho ninachozungumzia. Na wanaokuwa wakichukuliwa mara kwa mara ni mke wa mtuhumiwa , mtoto au ndugu. Lengo eti ni kumfanya mtuhumiwa halisi aweze kujisalimisha.
SOMA HAPA ZAIDI
SOMA HAPA ZAIDI
↧
MKURUGENZI MTENDAJI WA TAASISI YA MOI DKT. OTHUMANI KILOLOMA AFUNGUA MKUTANO WA TATU WA MADAKTARI WA MIFUPA JIJINI DAR
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa,ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dokta Othman Kiloloma (kulia) akifungua Mkutano wa tatu wa Madaktari Bingwa wa Mifupa uliyofanyika katika Taasisi hiyo Dar es Salaa
Daktari Bingwa wa Mifupa wa Taasisi hiyo Dk. Edmund Ndalama (kulia) akizungumza na Makt. Bingwa tota Nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania na Marekani ambapo lengo ni kubadilishana ujuzi kwa Nadharia na Vitendo na unatarajia kumaliza 29-Mei 2015
↧
Waziri Mwandosya akutana na Pele
Akiwa njiani kwenda Hanoi, Vietnam, Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais ( Kazi Maalum),Profesa Mark Mwandosya, amekutana na Edson Arantes do Nascimento (Pelé) mwanamichezo maarufu sana duniani. Pelé atatimiza umri wa miaka 75 ifikapo tarahe 23 Oktoba,2015. Katika uhai wake, Pelé aliweza kuingiza magoli 1283 katika michezo ya ushindani wa mpira wa miguu.
Pelé aliichezea timu yake klabu ya Santos, Brazil kuanzia mwaka 1956 mpaka mwaka 1974.Baada ya kustaafu alijiunga na klabu ya New York Cosmos kwa muda mfupi kuanzia mwaka 1974 mpaka 1977. Pelé ametajwa kuwa mmoja wa watu maarufu zaidi duniani na hakika mwanasoka maarufu kuliko wote karne ya 20.
Waziri Mwandosya alimshukuru Pelé kwa kuwa mfano bora katika mwenendo, maisha, ubunifu,na uongozi katika tasnia ya michezo na alimtakia afya njema na maisha marefu. Amewahi kuwa Waziri wa Michezo,Brazil. Katika picha ni Waziri Mwandosya, kulia;Pelé,katikati;na Mama Lucy Mwandosya, kushoto.
↧
↧
PATAKUWA HAPATOSHI DAR LIVE SIKU HIYO.
↧
WAZIRI NYALANDU ASAINI MKATABA MSUMBIJI KULINDA SELOUS
Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akibadilishana hati za makubaliano ya kuhifadhi Pori la akiba la selous nchini Tanzania lililoungana na Hifadhi ya Nnyasa nchini Msumbiji na waziri wa Ardhi na Maendeleo vijijini Celso Coreia, ambapo mbali na uhifadhi watashirikiana kupambana na ujangili , utaalamu na vifaa, jana mjini Maputo Msumbiji.
Waziri wa maliasili na Utalii, lazaro Nyalandu akimsikiliza waziri wa Ardhi na Maendeleo vijijini, Celso Coreia jana mjini Maputo kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kuhifadhi Pori la akiba la selous nchini Tanzania lililoungana na Hifadhi ya Nnyasa nchini Msumbiji ambapo mbali na uhifadhi watashirikiana kupambana na ujangili , utaalamu na vifaa.
Waziri wa Maliasii na Utalii, Lazaro Nyalandu na waziri wa Ardhi na Maendeleo vijijini wa Msumbiji Celso Coreia wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kuhifadhi Pori la akiba la selous nchini Tanzania lililoungana na Hifadhi ya Nnyasa nchini Msumbiji ambapo mbali na uhifadhi watashirikiana kupambana na ujangili, utaalamu na vifaa.
↧
MKUTANO WA MAJADILIANO YA RIPOTI YA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA MAFANIKIO NCHI ZA AFRIKA WAFANYIKA MJINI ABIDJAN
Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile akiwaeleza Mawaziri wa Fedha kuhusu serikali ya Tanzania ilivyonufaika na fedha za Benki ya Maendeleo katika kutekeleza mipango yake hasa kwenye miundombinu. Kutoka kulia ni Waziri wa Fedha wa Rwanda Bw. Claver Gatete na kushoto kwake ni Mchumi Mkuu Rugwabiza Minega Leonard.
Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile akitoa ufafanuzi kuhusu Tanzania inavyoshirikiana na Benki ya Afrika kwa Mawaziri wa Fedha kutoka nchini Rwanda, Ethiophia, Kenya na Visiwa vya Shelisheli wakati wa uwasilishaji wa ripoti ya utekelezaji wa mazimio ambayo kila nchi imejiwekea.
Waziri wa Fedha wa Rwanda Mhe. Claver Gatete akitoa ufafanua wa masuala mbalimbali yanayohusu nchi za Afrika. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile ambaye amemwakilisha Waziri wa fedha na kulia kwake ni Waziri wa Fedha wa Ethiophia Mhe. Fisseha Aberra.
Kamishna wa Fedha za Nje Bwana Ngosha Manyoga akiwa katika majadiliano yanayohusu ya ripoti ya utekelezaji wa mpango wa mafanikio katika nchi za Africa.
Wajumbe waliohudhuria Mkutano wa Kanda ya Afrika wakimsikiliza na kufuatilia kwa makini Dkt. Mulu Ketsela ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Afrika alipokuwa akiwasilisha ripoti ya Benki hiyo.
↧
TAARIFA YA MSIBA WA MZEE MGAYA
Familia ya mzee Richard Azza Mgaya inasikitika kutangaza kifo cha baba yao Mzee Richard Mgaya kilichotokea hospitali ya Apollo - India. Mwili wa marehemu utawasili Kilimanjaro International Airport tarehe 28/05/2015 saa nane mchana, msiba uko nyumbani kwake Arusha no. 59 Themi Hill. Marehemu ataagwa Ijumaa tarehe 29/05/2015 saa 6mchana katika kanisa la waadventista wa sabato Njiro Arusha.Mazishi yatafanyika Jumamosi tarehe 30/05/2015 Mamba Miamba - Same Kilimanjaro.
↧
↧
WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI UTALII NA MICHEZO AKUTANA NA BALOZI WA MALAWI ZANZIBAR.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk akisalimiana na Balozi wa Malawi Nchini Tanzania Hawa O. Ndilowe wakati alipowasili Ofisini kwake kwaajili ya kujitambulisha pia na kuzungumzia masuala mbalimbali kuhusuUtalii Zanzibar.
Afisa Ubalozi anaeshughulikia masuala ya Uchumi Tanzania Chinvano Kapeleta akizungumzia masuala ya Uchumi na Utalii na Viongoizi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk akifafanua jambo katika mazungumzo na Balozi wa Malawi Nchini Tanzania Hawa O. Ndilowe wakati walipokutana Ofisini kwake Zanzibar.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk katikati akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Malawi Hawa O.Ndilowe kulia yake na baadhi ya viongozi waliofika Ofisini kwake Zanzibar.PICHA ZOTE NA MIZA OTHMAN-HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
↧
WAZIRI MKUU PINDA ATEMBELEWA NA MTOTO ALBERT
↧
tamthilia ya #Kitendawili sehemu ya tatu
↧
MOAT WAPINGA MUSWADA WA SHERIA YA VYOMBO VYA HABARI
↧
↧
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI KENYA, JOHN HAULE
↧
Rais Kikwete afungua Mkutano Mkuu wa Chama Cha Waalimu Tanzania (CWT)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa Chama Cha Waalimu TANZANIA( CWT) uliofanyika katika hoteli ya Ngurdoto nje kidogo ya mji wa Arusha jana.Wakati wa mkutano huo wanachama wa CWT ulitarajia kuwachagua viongozi wapya wa chama Hicho.Akizungumza katika mkutano huo Rais Kikwete ameahidi kutatua changamoto moto mbalimbali zinazowakabili waalimu nchini(picha na Freddy Maro).
↧
Tangazo la Kozi ya Masters
↧
JK ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA ZA MZEE RUANGISA
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone:255-22-2114512, 2116898 E-mail: ikulucommpress@googlemail.com Fax: 255-22-2113425 | PRESIDENT’S OFFICE, STATE HOUSE, 1 BARACK OBAMA ROAD, 11400 DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa masikitiko na huzuni nyingi taarifa ya kifo cha mwanasiasa mkongwe nchini na aliyepigania uhuru wa Tanganyika, Ndugu Samwel Ntambala Ruangisa, ambaye aliaga dunia mwanzoni mwa wiki hii nchini Marekani ambako alikuwa anatibiwa.
Katika salamu za rambirambi ambazo amempelekea Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mheshimiwa John Mongella kuomboleza kifo cha Mzee Ruangisa, ambaye pia alikuwa bado diwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Rais Kikwete amesema:
“Nimepokea taarifa za kifo cha Mzee Ruangisa kwa masikitiko na huzuni nyingi. Kwa zaidi ya nusu karne, Mzee Ruangisa amekuwa kiongozi wa kuigwa mfano katika nafasi zote ambazo zimepata kuzishikilia katika maisha yake kuanzia Ukuu wa Mkoa wa Ziwa Magharibi (sasa Kagera) na baadaye Mkoa wa Mara tu baada ya Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, Ubalozi, Uwaziri, Ubunge, Umeya na Udiwani. Katika kila nafasi aliyoishikilia, Mzee Ruangisa alionyesha uongozi wa kiwango cha juu. Kwa hakika, tumepoteza kisima cha uzoefu wa uongozi.”
Rais Kikwete ameongeza katika salamu zake za rambirambi: “Mkuu wa Mkoa nakutumia salamu zangu za rambirambi kuomboleza msiba huu na kupitia kwako naomba uwape pole wana-Kagera wote kwa kuondokewa na mzee wao wa siku nyingi.
Aidha, naomba unifikishe pole zangu nyingi kwa wanafamilia wote ambao wamepoteza baba, babu na mhimili wa familia. Wajulishe kuwa niko nao katika kipindi hiki kigumu. Waambie naelewa machungu yao kwa sababu machungu yao ni machungu yangu. Vile vile, naungana nao katika kumwomba Mwenyeji Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke peponi roho ya Marehemu Samwel Ntambala Ruangisa. Amina.”
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU,
DAR ES SALAAM.
27 Mei, 2015
↧
↧
MAADHIMISHO YA WIKI YA UKOMBOZI BARA LA AFRIKA,WANAWAKE WAELEZA NAMNA WALIVYOSHIRIKI KATIKA UKOMBOZI
Mwenyekiti wa Bodi ya AICC na Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya wiki ya Ukombozi wa Bara la Afrika, Balozi Christopher Liundi akikata utepe katika maadhimisho hayo ikiwa leo ni siku ya Kuona Mchango wa Wanawake katika Ukombozi wa Bara la Afrika, maadhimisho hayo yamefanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Profesa Ruth Meene akizungumza na baadhi ya wanafunzi na watu wengine waliohudhuria (hawapo pichani) ili kujua mchango wa wanawake katika ukombozi wa Bara la Afrika, wanawake hao ambao wamesaidia zaidi ni Mke wa Rais wa Mozambiq,Jocina Machel,Bi Ndaitwa wa Namibia,Winnie Mandela wa Afrika Kusini,Albetina Kisulu,Elizabeth Sebeko,Mariam Makeba wote wa Afrika kusini na hapa nchini ni Bibi Titi Mohamed,Lucy Maulid na Sophia Kawawa ambao walikuwa wakihamasisha wananchi Kisiasa katika kulikomboa Bara la Afrika.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Victoria waliohudhuria katika Mkutano wa kujua jinsi wanawake walivyoshiriki katika kulikomboa Bara la Afrika, katika Mkutano uliofanyika Makumbusho ya Taifa jijiji Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Bodi ya AICC na Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya wiki ya Ukombozi wa Bara la Afrika, Balozi Christopher Liundi akizungumza leo na waandishi wa habari mara baada ya kutoka katika kumbi zenye picha na vitu mbalimbali ndani ya jengo la Makumbusho ya Taifa vinavyoonyesha kumbukumbu ya matukio mbalimbali yalivyowahi kutokea hapa nchini.Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
↧
RAIS KIKWETE AWAAPISHA KATIBU MKUU, NAIBU KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE NA BALOZI WA TANZANIA SAUDIA
| ||
↧
DR. MENGI AZINDUA MPANGO WA AIRTEL FURSA 'TUNAKUWEZESHA' JIJINI DAR.
Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi (wa pilikulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania, Balozi Juma Mwapachu (wapili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso (kulia) na Menejawa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi wakiwa wameshika bango kamaishara ya uzinduzi wa mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’, katika haflailiyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi (wa pili kulia), akikabidhi zawadi ya pasi na meza yake kwa muuza mitumba RashidSeleman (wa pili kushoto), ambaye ni mmoja wa vijana waliowezeshwa na mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’ katika hafla ya uzinduzi wa mpango huo, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso, Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania, Balozi Juma Mwapachu (wa tatu kushoto) na Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi.
Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi (wa pili kulia), akikabidhi zawadi ya mashine ya kutengeneza juisi kwa Abdulkarim Ramadhan (wa tatu kushoto), ambaye ni mmoja wa vijana waliowezeshwa na mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’ katika hafla ya uzinduzi wa mpango huo, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka (kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso, Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania, Balozi Juma Mwapachu na Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
↧
More Pages to Explore .....