Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live

DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI


MAWAZIRI WA FEDHA WA NCHI ZA UKANDA WA AFRIKA WAJADILI MAENDELEO

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali wa Dkt. Servacius Likwelile akiwa pamoja na Kamishina wa Fedha za Nje Bw. Ngosha Magonya wakati mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mjini Abidjan.

Akizungumza na vyombo vya habari mchana huu DKt.Likwelile ambaye ni amemuwakilisha Waziri wa Fedha na katika Mkutano wa Benki ya Dunia amesema kuwa,”Mkurungezi wa Kanda ametoa ripoti ya mwaka, ameelezea ni namna gani ukanda huu wa Afrika ulivyokuwa ukifanya kazi za maendeleo, ameelezea ripoti hiyo kuwa inagusa nchi zote sita za Afrika. Nchi hizo ni pamoja na Rwanda, Tanzania,Uganda, Kenya, Ethiophia na Visiwa vya Shelisheli, Aidha nchi hizo zimefanya kazi vizuri. Alisisitiza Likwelile.

Likwelile amefanafua kuwa, “Mkurugenzi wa ukanda wanchi za Afrika ameelezea jinsi uchumi unavyokua kwa kasi kubwa kwani umekua kwa asilimia sita mpaka saba na ukuaji huu wa uchumi unawanufaisha watu wote wa nchi hizo.

Ni Muhimu kuwekeza kwenye reli hii itawapunguzia wananchi usumbufu wanaoupata kwenye masuala ya usafiri na usafirishaji wa mizigo.Aliongeza Likwelile.

Pia Likwelile amezungumzia kuhusu kuendeleza kilimo hasa kilimo chenye tija. alisema kuwa kilimo cha biashara humuongezea kipato mwananchi wa chini na kumfanya kujikwamua kwenye hali ya kimasikini.

Aidha mwenyikiti amezungumzia suala nishati hasa nishati ya umeme ili tuweze kuendelea ni muhimu kusimamia suala la umeme kwa kikanda. Hii itapelekea nchi zote za Afrika kunufaika na masuala ya maendeleo kiujumla kwa nchi hizo za kikanda.

“ Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu wa rais, Aidha ukanda wa nchi za Afrika unapenda kumshukuru raisi aliyepita Dkt. Kaberuka kwa kazi nzuri aliyoifanya kwani ameziacha nchi katika hali nzuri sana” Alisisitiza Likwelile.

Mwisho Likwelile alifafanua kuwa, “Benki ya Maendeleo ya Afrika imetambua umuhimu wa kazi na mchango mkubwa alioutoa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na ndio maana imemualika katika Mkutano huu wa mwaka kutokana na kazi zuri aliyoifanya.

WORLD LUNG FOUNDATION YAZINDUA KAMPENI YA KUHAMASISHA UZAZI WA MPANGO MKOANI KIGOMA

0
0
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Cosmas Swai, akizindua kampeni mpya ya kuhamasisha Faida na Matumizi ya Uzazi wa Mpango jijini Dar es Salaam jana, kampeni itakayotekelezwa mkoani Kigoma. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la, World Lung Foundation (WLF), Nduke Mwakatundu (mwenye tai) na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dk.Leonard Subi (watatu kulia) na baadhi ya wafanyakazi wa (WLF).
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la World Lung Foundation (WLF), Nduke Mwakatundu, akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya kuhamasisha faida na matumizi ya uzazi wa mpango jijini Dar es Salaam jana, mpango utakaotekelezwa mkoani Kigoma. Kushoto ni Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya, Dk.Cosmas Swai na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dk.Leonard Subi.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dk. Leonard Subi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa kampeni mpya ya kuhamasisha faida na matumizi ya uzazi wa mpango jijini Dar es Salaam jana, mpango utakaotekelezwa mkoani Kigoma chini ya Shirika la World Lung Foundation (WLF).

TASWIRA ZA AWALI ZA TAMASHA KUBWA LA BURUDANI 'JEMBEKA FESTIVAL 2015

0
0
Mmoja wa wasanii washindani wa Mkali Jembeka akionesha ufundi wake katika hip hop kwenye fainali ndani ya Tamasha kubwa la burudani 'JEMBEKA FESTIVAL' lililozinduliwa Jumamosi ya tarehe 23/05/2015 uwanja wa CCM Kirmba jijini Mwanza na kuhudhuriwa na maelfu ya watu.  
Shengwe za wananchi kwa tamasha lililopigwa tangu saa 7 mpaka asubuhi siku iliyofuata na hapa ni mapema kabisa ngoma saa tisa huku burudani zikiwa tayari zimeshika kasi.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

PROPOSED REHABILITATION OF MNAZI MMOJA HOSPITAL PARK AND THE BUS (DALADALA) TERMINAL

NSSF YAENDESHA ZOEZI LA UPIMAJI AFYA BURE KWA WAKAZI WA TANGA

0
0
Meneja wa Mafao ya Matibabu( SHIB) Dk. Ali Mtulia akizungumza na waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali juu ya lengo la kambi ya upimaji Afya kwa wakazi wa Tanga ambayo inaendelea Mkoani Tanga kwenye Viwanja vya Tangamano.
Dk. Ali Mtulia (wa tatu kushoto ) na Dk. Limu (kushoto) wakipima uzito na Urefu wa Mkazi wa Tanga ili kuweza kujua na kumshauri juu ya uwiano wa Urefu na Uzito wake.
Daktari bingwa wa Siku nyingi Dk. Ali Mzige akimshauri mkazi wa Tanga juu ya afya yake na lishe bora.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

MH. PINDA AJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA

0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijiandikisha katika kituo cha kuandikisha wapiga kura cha Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kibaoni wilayani Mlele Mei 25, 2015. Kushoto ni Mwandikishaji wapiga kura, Auxilia Gaspar.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akionyesho kitambulisho chake cha mpiga kura baada ya kujiandikisha katika kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kibaoni wilayani Mlelele Machi 25,2015. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Katavi, Dkt Ibrahim Msengi na Kushoyo ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Julius Malaba.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akichuliwa alama za vidole wakati alipojiandikisha katika kituo cha kuandikisha wapiga kura cha Shule ya Msingii Kakuni katika kijiji cha Kibaoni wilayani Mlele Mei 25, 2015. Kulia ni Mwandikishaji wapiga kura, Happiness Isaya. 
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akichuliwa alama za vidole wakati alipojiandikisha katika kituo cha kuandikisha wapiga kura cha Shule ya Msingii Kakuni katika kijiji cha Kibaoniwilayani Mlele Mei 25, 2015. Kulia ni Mwandikishaji wapiga kura, Anna Gale.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania akutana na wateja wa benki hiyo jijini Mwanza

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania Edward Marks, akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo wa jijini Mwanza hivi karibuni katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo ili kufahaminiana na mkurugenzi huyo aliyejiunga na NBC hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania Edward Marks (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya wateja wao wa Jiji la Mwanza katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo ili kufahaminiana na mkurugenzi huyo aliyejiunga na benki hiyo hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania Edward Marks (wa pili kulia) akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo wa jijini Mwanza kuhusu jinsi NBC ilivyojipanga kuhakikisha wateja wao wanapata huduma bora na za uhakika.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania Edward Marks (kushoto) akimsikiliza mmoja wa wateja wa benki hiyo jijini Mwanza katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo ili kufahaminiana na mkurugenzi huyo aliyejiunga na NBC hivi karibuni akitokea Benki ya Barclays nchini Misri.

NANI KUTWAA KOMBE LA EURO LEAGUE 2015/16????

AKI NA UKWA WA BONGO WAELEZEA MAFANIKIO YAO KWENYE TASNIA YA FILAMU

0
0
Kushoto ni Meya Shabani a.k.a Aki akiwa na Mwenzake Nicholaus Ngoda a.k.a Ukwa nje ya ofisi yao.

Wasanii wa vichekesho maarufu kama Aki na Ukwa wa Bongo Muvi wameelezea mafaniko yao kwenye tasnia ya filamu za vichekesho nchini kwa mara ya kwanza tangu wajiingize kwenye filamu mwaka 2010.

Wakizungumza na Komedi Zone, Meya Shabani ambaye ni 'Aki' na Nicholaus Ngoda 'Ukwa' wamesema kuwa moja ya mafanikio waliyoyapata mpaka sasa ni kufanya kazi chini ya kampuni yao ya International Film Angels iliyopo Mwananyamala Visiwani jijini Dar na kuigiza muvi nzuri za vichekesho ambazo zina hadhi ya kipekee kimwonekano na hata simulizi zake tofauti na muvi nyingi za komedi ambazo hukosa ubora unaostahiki.
 Hapa wakionesha upande mwengine wa ofisi yao ya International Film Angels
Baadhi ya muvi zao za komedi walizozifanya ni kama vile; Sometimes Yes Sometimes No, Zero Brain, Lost Sons, Crazy in Hospital, Ayubu wa Leo na Pastor Miyamba's Trial huku wakisema kuwa kuna utitiri wa muvi kali zaidi zipo katika matengenezo.

Mbali na muvi hizo wasanii hao wa Komedi waliongeza kuwa kupitia sanaa wameweza kujiendeleza kimasomo katika kozi za kuongoza filamu, kuedit na kuigiza huku muvi zao zikiwatambulisha vyema kiasi cha kufahamika na watu wengi na kupata dili mbalimbali za kuelimisha jamii kupitia kuigiza na kuimba.

"Kwa sasa tunajiita kama 'Edutainmenter' tukiwa na maana ya kuwa ni waburudishaji na waelimishaji kutokana na uwezo wetu wa kuimba na kuigiza hivyo hayo yote kwetu ni mafanikio japo malengo yetu bado ni kufika mbali zaidi," walisema mastaa hao.

Pia kupata taarifa zaidi za wasanii wa Komedi Tanzania  tembelea mtandao wao wa www.komedizonetz.blogspot.com

Wiki ya Ukombozi wa Afrika na Uzinduzi Mradi Uhifadhi Urithi Nyaraka Tanzania

0
0
Profesa Issa Shivji akichokoza mada katika mjadala wa Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Afrika inayofanyika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Profesa Issa Shivji akichokoza mada katika mjadala wa Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Afrika inayofanyika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Silima akisoma hotuba ya uzinduzi akimuwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe kwenye Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Afrika inayofanyika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Silima akisoma hotuba ya uzinduzi akimuwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe kwenye Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Afrika inayofanyika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.Ofisa Mkuu na Mwakilishi Mkazi wa UNESCO nchini Tanzania, Mzulmira Rodrigues akizungumza katika Maadhimisho ya Wiki ya Ukombozi wa Afrika inayofanyika kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Ofisa Mkuu na Mwakilishi Mkazi wa UNESCO nchini Tanzania, Mzulmira Rodrigues akizungumza katika Maadhimisho ya Wiki ya Ukombozi wa Afrika inayofanyika kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi akizungumza katika Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Afrika inayofanyika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi akizungumza katika Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Afrika inayofanyika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

TASWIRA KATIKA BODABODA

0
0
Watalii wakiwa wamepanda bodaboda kwa mtindo wa mshkaki bila kujali sheria za usalama barabarani maeneo ya sinza Afrikasana, jijini Dar leo mchana.
Mama huyu ambaye jinalake halijapatikana akiwa amepanda bodaboda yeye mtoto wake na mzigo bila ya kujali maisha yatakuwaje endapo watadondoka, huku derevawao akiwa anaendesha pembeni ya barabara maeneo ya Kimara Temboni, jijini Dar leo jioni.  picha zote na Chris Mfinanga

BENKI YA CRDB YAKABIDHI HUNDI YA SH. MILIONI 20 KWA MEYA WA KINONDONI

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimkabidhi hundi ya sh. milioni 20 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda zilizotolewa na benki hiyo baada ya  meya huyo kupata tuzo ya Meya Bora Afrika iliyotolewa na Rais Jose Eduardo do Santos wa Angola. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
 Meya wa Kinondoni Yusuf Mwenda akitoa shukrani zake kwa uongozi wa Benki ya CRDB kwa kutambua juhudi wanazofanya katika utendaji kazi na masuala ya usafi na ukusanyaji wa mapato.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles kimei akizungumza katika hafla hiyo.

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MSIBA WA MTANGAZAJI WA ZAMANI WA RADIO TANZANIA MSHINDO MKEYENGE

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha aliyekuwa mtangazaji mashuhuri na maarufu wa iliyokuwa Redio Tanzania (sasa TBC Taifa), Ndugu Mshindo Mukeyenge ambaye alifariki dunia mwishoni mwa wiki na kuzikwa jana, Jumatatu, Mei 25, 2015.

Katika salamu alizomtumia Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mkoa wa Dar Es Salaam, Mheshimiwa Sofia Mjema leo, Jumanne, Mei 26, 2015, Rais Kikwete amesema kuwa kifo cha Mzee Mukeyenge kimelinyang’anya “taifa letu hakina kubwa ya uzoefu wa utangazaji katika kipindi ambapo vijana wanaochipukia katika tasnia ya habari, na hasa utangazaji, walikuwa wanahitaji sana malezi, ushauri na uongozi wake.”

Rais Kikwete amemwelezea Mzee Mukeyenge kama Mtanzania aliyetoa mchango mkubwa katika ujenzi wa taifa letu kupitia kipaji chake cha utangazaji na kuwa mchango wake utaendelea kukumbukwa kwa miaka mingi ijayo.

“Aidha, tutaendelea kumkumbuka Ndugu Mshindo Mukeyenge kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya michezo hapa nchini, na hasa mchezo wa soka, ambako alichangia kwa kulihabarisha taifa letu kupitia utangazaji wa mechi nyingi za soka za kitaifa ama kimataifa,” amesema Rais Kikwete.

Amemwambia Mkuu huyo wa Wilaya, “Kwa hakika nimepokea kwa huzuni taarifa za kifo cha Ndugu Mshindo Mukeyenge. Napenda kuungana nawe na wana-Temeke wote katika kuomboleza kifo cha mwenzetu. Aidha, napenda kukuomba unifikishie salamu zangu za rambirambi kwa wanafamilia na wote ambao wamepotelewa na mhimili wao. Wajulishe kuwa naungana nao katika machungu yao na katika kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke pema peponi roho ya Marehemu Mshindo Mukeyenge. Amina”.

Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
26 Mei, 2015

MAANDALIZI YA UZINDUZI WA MANJANO FOUNDATION YAKAMILIKA

0
0
Wasichana waliochaguliwa kunufaika na Mpango hup wakiwa Katika Picha ya Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama  Shekha Nasser .

Shear Illusions inasherehekea mwongo mmoja wa urembo nchini Tanzania kwa kuzindua vipodozi vyake ijulikanayo kama LuvTouch Manjano!
Uzinduzi huu utafanyika tarehe 31 Mei 2015 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee VIP Hall. Shamrashamra hizi pia itatoa fursa kwa kuendeleza mtandao wa kibiashara kwa kina mama na pia mada mbali mbali ya jinsi ya kujikwamua kimaisha itatolewa. Bila ya kusahau mafunzo ya jinsi ya kutumia vipodozi.



Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda na mtoa mada mkuu atakuwa ni Balozi Mwanaidi Majaar.

Shear Illusions, imeweza kutambulisha urembo na muonekano wa mwanamke wa kitanzania kwa Zaidi ya miaka kumi. Wamebaisha urembo kuanzia kujipodoa, nywele, vipodozi na vito hadi blog na jarida inayoelezea masuala ya urembo. Baada ya kuuza bidhaa mbali mbali ya urembo toka nchi mbali mbali, Shear Illusions inazindua rasmi bidhaa yake ya LuvTouch Manjano.


LuvTouch Manjano ni maalum kwa ajili ya kumpendezesha mwanamke wa kitanzania. Kuna aina kumi ya vipodozi msingi kuanzia Mwanzi na Mpodo hadi kahawa na ardhi. Bidhaa hizi zimezingatia hali ya hewa ya joto. Vipodozi hivi vinalengo la kuongeza muonekano wako kwa hali yoyote.

Shear Illusions inazishukuru kampuni zifuatazo waliojitokeza kusaidia hafla hii ya kuwawezesha wanawake; NSSF, TCRA, Clouds Media, Maxcom, A1 Outdoor, Mr. Price, Cassandra Lingerie, Amina Design, Maznat Bridal, Advertising Dar, Beauty Point, Hugo Domingo, I-View Media, FAIDIKA, Benchmark Productions, Fasta Fasta, TENSHI, Jardin Modeling Agency na mashirika mbali mbali hapa Dar es Salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama  Shekha Nasser Katikati  akiongea na Vyombo vya Habari leo wakati akelezea Mandalizi ya Uzinduzi wa Manjano Foundation Ambao ni Mpango unaolenga kuwawezesha Kutoa Mafunzo ya Ujasiriamali kwa Wasichana wa Kitanzania.Mpango Uzinduzi huu utafanyika tarehe 31 Mei 2015 kuanzia saa 6 mchana kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee VIP Hall. Utatoa fursa kwa kuendeleza mtandao wa kibiashara kwa kina mama na pia mada mbali mbali ya jinsi ya kujikwamua kimaisha itatolewa. Bila ya kusahau mafunzo ya jinsi ya kutumia vipodozi..Mgeni Rasmi anategemewa Kuwa Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda.


Article 17

Bayport: Wa mikoani nao wanaweza kukopa viwanja vya Kibaha

0
0
TAASISI ya Kifedha ya Bayaport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo,imesema hata Watanzania wanaoishi mikoani wanaweza kutumia fursa ya kukopeshwa viwanja katika mradi wa Vikuruti, uliopo Kibaha, mkoani Pwani. Unaweza kuptata fomu hapa.
Afisa Mipango wa Wilaya ya Kibaha, Obed Katonge, akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya mikopo ya viwanja, uliyofanyika mwishoni mwa wiki, katika hoteli ya Serena.

Bonyeza hapa kupata fomu ya mkopo wa viwanja kutoka Bayport Financial Services http://www.kopabayport.co.tz/RESERVATION%20FORM.pdf

Kauli hiyo imetolewa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa taasisi hiyo, Ngula Cheyo, ikiwa ni siku chache baada ya kuzindua huduma ya mikopo ya viwanja katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, huku akisisitiza kwamba si lazima mkopaji wa viwanja hivyyo atoke Dar es Salaam au Kibaha.
Kicheko cha furaha. Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport Financial Services, John Mbaga, kulia akifurahia jambo na Meneja Masoko na Mawasiliaano wa Bayport Financial Services, jijini Dar es Salaam.

Habari; Watanzania wengi wanaoishi mikoani wamekuwa wakiulizia kama nao wana weza kukopeshwa viwanja hivyo,hivyo Bayport imeona itowe ufafanuzi huu. Kwamba ni ruhusa. Kilaa mtu anaweza kukopa.

Cheyo alisema kwamba huduma hiyo ni ya Watanzania wote, ndio maana wamesambaza fomu za kuomba mkopo wa viwanja katika matawi yao mbalimbali, bila kusahau wale wanaoweza kukopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz.

“Nafasi ni chache, maana maombi yetu yanafanyika kwa siku (20), kuanzia ile Mei 22 hadi Juni 10, huku fomu za maombi zikipatikana katika matawi yao yote ya Bayport Financial Services, bila kusahau kupitia bank of Africa (BOA), ambapo malilipo ya awali yakianzia Sh 150,000 na yatakuwa yakilipwa kwa akaunti yao ya Bayport iliyopo BOA.

“Fomu ya maombi na nakala ya malipo ya awali yarejeshwe katika matawi BOA au ofisi za taasisi yetu ya Bayport zilizoenea nchi nzima, huku baada ya Juni 10, mteja akitakiwa kulipia kiwanja kwa fedha taslimu au mkopo kutoka Bayport, ambapo watumishi wa umma na wa kampuni wanaweza kukopeshwa kiwanja na wakikabidhiwa hati miliki ndani ya siku (90), baada ya kukamilisha mkopo wake kwa wateja wa fedha taslimu na wengineo wakipewa baada ya kumaliza mkopo wao,” alisema Cheyo.

Kwa mujibu wa Cheyo, huduma ya mikopo ya viwanja ni maalum kwa ajili ya kuwakomboa Watanzania wote waliokuwa wakitatizwa na suala zima la makazi, hususan kutokana na ugumu wa maisha unaowakumba Watanzania wengi nchini.

Ngula alisema kukaa mikoani si sababu ya kushindwa kukopa kiwanja kwa sababu wamefungua matawi katika wilaya na mikoa mbalimbali, hivyo ni jukumu la mjasiriamali, mtumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi wanatumia nafasi hiyo kujiendeleza kwa kupata viwanja hivyo.

Naye Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, aliliambia gazeti hili kuwa ukubwa wa viwanja hivyo unaanzia hatua 15 kwa 16, huku thamani yake ikianzia Sh 1,400,000 bila riba (mortgage), ambapo pia fomu zao zimejieleza na kujifafanua vizuri kwa ajili ya kutoa urahisi wa kuwahudumia Watanzania wote.

Mndeme alimaliza kwa kuwataka wateja wao na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kuchangamkia viwanja hivyo vinavyokadiliwa kuwa 1878 vilivyokuwa katika eneo zuri, kilomita 50 kutoka Kisutu, jijini Dar es Salaam na kilomita 6.5 kutoka barabara Kuu ya Morogoro.

WAZIRI LUKUVI AFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOANI TABORA

0
0
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akisisitiza jambo wakati alipozungumza na Wakuu wa sekta mbalimbali mkoani Tabora leo kuhusiana na masuala yanayohusu sekta ya ardhi mkoani humo katika ukumbni wa mikutano wa Isike. Kulia ni mkuu wa Wilaya ya Tabora Mh Suleiman Kumchaya  na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Bi Kudra Mwinyimvua. 
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akizungumza na Wananchi wa Eneo la Malabi katika Manispaa ya Tabora, kuhusiana na mgogoro wa Ardhi unaowakabili wananchi hao ambao unaotokana na Manisapaa kutowalipa fidia ya maeneo yao.
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mh Suleiman Kumchaya akijadiliana jambo wakati Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvu alipotembelea eneo la Malabi katika Manispaa ya Tabora kusikiliza matatizo ya Ardhi yanayo wakabili wananchi wa eneo hilo leo.  
Picha/Clarence Nanyaro

RAIS KIKWETE AFUNGUA RASMI MKUTANO WA NNE WA MABALOZI

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati akifungua rasmi Mkutano wa Nne wa Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi. Mkutano huo umefanyika katika Hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam ukiwa umebeba Kaulimbiu isemayo "Diplomasia ya Tanzania Kuelekea Dira ya Taifa 2025".
Mhe. Rais Kikwete akizungumza huku Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula wakimsikiliza.
Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia hotuba ya ufunguzi ya Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani).
Wajumbe wengine wakiwemo Wakuu wa Vitengo katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifutilia hotuba ya Mhe. Rais Kikwete ambaye haonekani pichani.Picha na Reginald Philip.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MAOMBI YA MCHANGO WA UJENZI WA MSIKITI

0
0
Katika Maisha yetu Wanaadamu Ibada ni Jambo Muhimu saana. 
Uzuri , Usafi wa sehemu ya kuabudu ni Moja katika mambo mazuri yenye kupendeza katika kila Nafsi ya Binaadamu.

Katika Nyumba (Msikiti)  huu , Ndugu zetu wanafanya Ibada ya Swala 5 kwa siku , Msikiti huu upo Mkoa wa Pwani , Wilaya ya Mkuranga , Kijiji cha Mlamleni Kitongoji cha Kimbangulile. 

Wenzetu wameanza kwa Nguvu zao  Ujenzi wa Msikiti kama Mnavyo uona.
Jitihada nyengine wameweza kuwa na Matofali yasiyo pungua 300 kwa Ajili ya kuanza Ujenzi Mpya. 

Ukiwa Umeguswa na hili tunaomba kutoka kwako MCHANGO WAKO WA VIFAA VYA UJENZI.

Kwa Mwanzo Tunahitaji 
1.Cement 
2.Tofali
3.mchanga
4.Vifaa vya Kuchimbia Majembe, Panga , chepe N.k

Maazimio yetu tuanze Ujenzi pale tu tutakapo pata uwezo wa kulifanya hili.

Tunawakaribisha mtembelee eneo la tukio kwa wale ambao Mtakuwa na  Na Muda wa kufanya hivyo.

Michango yenu tunaomba muwasilishe kwa Namba ya Simu.
0715800772( Tigo Pesa ) GHALIB MONERO.

Kwa wale waliopo Nje ya Tanzania : WESTERN UNION : GHALIB NASSOR MONERO 

Waliopo KENYA tafadhali wasiliana ALI BAJIY NASOR no' 0725113783 M-PESA.

More Update kuhusu Michango ya Msikiti huu Tafadhali Tutembelee : facebook : Kijana wa Kiislam Dsm or Whatssap Number : +255689604780

Au Piga Simu : +255715800772

Tunawashukuru kwa Michango yenu na Ubalozi wenu Mzuri wa kuitangaza kheri hii . 

WABILLAHI TAUFIQ WENU KATIKA UTUMISHI WA DINI KATIKA JAMII.
GHALIB N MONERO.
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live




Latest Images