Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

MKUGENZI MKUU MSTAAFU WA TTCL ADOLAR MAPUNDA AFARIKI DUNIA

$
0
0


HABARI ZILIZOTUFIKIA ASUHII HII NI KWAMBA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA SIMU NCHINI ADOLAR BARNABAS MAPUNDA AMEFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA LEO KATIKA HOSPITALI YA HINDU MANDAL JIJINI DAR ES SALAAM ALIKOKUWA AMELAZWA. MIPANGO YA MAZISHI INAFANYIKA NYUMBANI KWAKE TEGETA. 


MAREHEMU MAPUNDA ALIWAHI PIA KUWA MWENYEKITI WA BODI KADHAA NCHINI IKIWEMO YA WADHAMINI YA MUHIMBILI NA TANZANIA STANDARD NEWSPAPERS, WACHAPISHAJI WA MAGAZETI YA SERIKALI YA DAILY NEWS, SUNDAY NEWS NA HABARI LEO. MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI- AMINA

TUTAENDELEA KUWAFAHAMISHA MAENDELEO YA MSIBA KILA TUTAPOPWEWA TAARIFA



WALIOHUSIKA NA UJENZI WA JENGO LILILOPOEROMOKA LEO KUWAJIBISHWA

$
0
0
 Jengo lililo pembeni mwa msikiti wa Shia Ithnaasheri mtaa wa Indira Ghandi katikati ya jiji la Dar es salaam linavyoonekana baada ya kuporomoka asubuhi hii. Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es salaam Suleiman Kova kawaambia wanahabari kuwa kila aliyehusika na ujenzi, usimamizi na hata utoaji vibali atawajibishwa endapo kutaonekana kumekuwepo uzembe upande wake
 Taharuki kila mahali katika eneo la tukio
 Jengo limetapakaa barabarani
 wananchi wakishuhuria kwa huzuni
 Bango la wakandarasi

 Hassan Mhelela wa BBC alikuwa miongoni mwa wanahabari wa kwanza kufika eneo la tukio
 Moja ya magari kadhaa yaliyodondokewa na kifusi
 Gari ingine ambayo inasemekana ndani yake mna watu
 Ulinzi wa kutosha kila pembe
Bila vifaa vizito kazi inakuwa ngumu

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

RAIS JAKAYA KIKWETE, MAKAMU WAKE DKT. BILAL, WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA WASHIRIKI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MBUNGE WA CUF DAR LEO

$
0
0
Rais Jakaya Kikwete, akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani CUF, Salim Hemed Khamis, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa baada ya kuuguaa ghafla wakati akiwa katika Kikao cha Kamati ya Bunge cha Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam juzi. Marehemu mefariki kwa ugonjwa wa shinikizo la damu.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri Mstaafu, Edward Lowasa, na viongozi wengine wakishiriki shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia CUF, aliyefariki jana mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zimefanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Machi 29, 2013. 
Katibu wa Bunge la Jamhuri, John Joel, akisalimiana na Samuel Sitta, katika Ukumbi wa Karimjee wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia CUF, aliyefariki jana mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zimefanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Machi 29, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya ndugu wa marehemu wakati viongozi wakiondoka kwenye ukumbi wa Karimjee baada ya kushiriki katika shughuli za kuaga mwili wa marehemu, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba, Salim Hemed Khamis (CUF), aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Adam Malima, wakizungumza nje ya ukumbi wa Karimjee, baada ya kushiriki shughuli ya kuaga mwili wa marehemu,Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia Chama cha CUF, aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu,Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia Chama cha CUF, aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakiingiza kwenye gari tayari kuelekea uwanja wa ndege kwa safari ya kuelekea Pemba kwa maziko, yatakayofanyika leo. Picha na OMR.

VIDEO YA TUKUO LA UOKOAJI KATIKA JENGO LILILOPOROMOKA LEO JIJINI DAR

video SHOWING SCENE OF A 15-STOREY BUILDING THAT COLLAPSED AND KILLED SEVERAL I N DAR ES SALAAM TODAY MARCH 29, 2013

HALI ILIVYO KATIKA JENGO LILILOPROMOKA DAR ES SALAAM

RAIS KIKWETE ATEMBELEA JENGO LILILOPOROMOKA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Bw. Suleiman Kova na Mkuu wa Mkoa huo Mhe saidi Meck Sadiki katika eneo la jengo lililoporomoka mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.

RAMBI RAMBI KUTOKA UJERUMANI KUFUATIA KUANGUKA KWA JENGO DAR

$
0
0
Umoja wa Watanzania Ujerumani umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kuanguka kwa jengo mjini Dar es Salaam. tunawapa pole nyingi ndugu na jamaa wa waliopoteza maisha, Umoja Wa Watanzania Ujerumani unaungana na watanzania wote pamoja wafiwa katika maombolezi ya msiba huu mkubwa.

Tunawaombea marehemu wote mungu awaweke mahala pema peponi AMIN

KUMBUKUMBU

$
0
0
Marehemu Mzee John P Sunga 

Ilikuwa kama ndoto lakini ni kweli yalitimia, tunaamini kimwili hauko nasi lakini kiroho u nasi. Tunakukumbuka daima mpendwa wetu. Upendo na ucheshi wako kwa familia hautasahaulika kamwe.

Ni mwaka mmoja sasa umepita tangu ulipotutoka mpendwa wetu Mzee John P Sunga. Unakumbukwa kipekee na mke wako Mama Sunga, watoto wako Dora, James, Calorine, Alan, Clement,Ngasa na wajukuu zako wote, ndugu jamaa na marafiki zako wote.

Raha ya milele umpe e bwana na mwanga wa milele umuangazie na apumzike kwa amani. Amina

SIKU YA TAIFA YA KUPANDA MITI 2013 KUADHIMISHWA KITAIFA MKOANIMOROGORO

BREAKING NYUZZZZZ.......: MTUHUMIWA WA MAUAJI YA PADRI EVALIST MUSHI AKAMATWA ZANZIBAR

$
0
0
MTU ANAESADIKIWA KUWA NDIE MUUAJI WA PADRI EVARIST MUSHI WA KANISA KATOLIKI VISIWANI ZANZIBAR AMEKAMATWA ALASIRI HII MAENEO YA KARIAKOO, ZANZIBAR.

JESHI LA POLISI LIMETHIBITISHA KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA HUYO,NA KWENDA NAYE KITUONI KWA AJILI YA MAHOJIANO ZAIDI.


PADRI MUSHI ALIUWAWA KWA KUPIGWA RISASI MWEZI ULIOPITA WAKATI AKIWA KWENYE GARI LAKE KUELEKEA KANISANI KWENYE IBADA YA JUMAPILI. IFUATAYO NI SEHEMU YA TAARIFA YA KAMISHNA WA POLISI ZANZIBA AFANDE MUSA A.MUSSA ALIYOITOA KWA WANAHABARI LEO,

Taswira ya kuchora ya mtuhumiwa

TAARIFA YA MSIBA

$
0
0
Wanangwa Mtawali


(Born Feb 1962 – Died Mar 28, 2013)


Familia ya Marehemu Clement na Marehemu Mwalimu Margareth Mtawali, wa zamani Chuo cha Ushirika Moshi, wanasikitika kutoa taarifa ya msiba wa Wanangwa ‘McTwist’ Mtawali aliyefariki ghafla alfajiri ya 28 March 2013. 

 MISA YA MAREHEMU ITAANZA SAA TANO ASUBUHI, KESHO JUMAMOSI  30/3/13, PALE NYUMBANI KWA MAREHEMU MTAA WA KAGERA NA KIMAMBA, KARIBU NA MSIKITI WA UNDANI, NA MAZISHI YATAKUWA SAA TISA KAMILI MAKABURI YA KINONDONI (NDANI YA UKUTA) DAR ES SALAAM.

Ndugu na marafiki tutashukuru kujumuika kwenu ki hali na mali katika kipindi hiki cha maombolezo hadi mazishi; waweza kuwasilisha kujikimu kwako kwa Michael Mtawali au kupitia MPesa namba 0754710334.



Kuishi ni Kristo, na kufa ni faida

IN LOVING MEMORY

$
0
0

Dada Grace Simtaji Ngowi


Our  beautiful Sister, our beautiful Mother, today 29.03.2013  is exactly one year since you passed away and left us with sorrow, tears and confusion. We thank God for the time we spent together the joy, laughter and words of encouragement from you.

We take this opportunity to thank all friends and family for comforting words and your help on regular basis.
 
You will always be in our hearts and you are remembered by your son Emmanuel, your husband Joseph, your sister Anna, your brothers Bahati, Kotto & Baraka, other members of the family and friends.
  ‘’...the Lord gave and the Lord has taken away may the name of the Lord be praised’’
Job 1:21

Guess what...KFC to hit Dar soon!

$
0
0
KFC to open shop in Dar es salaam soon! That is at Mikocheni, along Mwai Kibaki Road (formerly Old Bagamoyo Road) on the way to Butiama, next door to the Arcade...yummy!

Mechi za Kirafiki Mpira wa Miguu na Mikono timu za Ikulu Dar na ZNZ.

$
0
0
  Mchezaji wa Timu ya Netball ya Ikulu ya Dar es Salaam Haika Masoud (kulia) akimzuia Beshuu Abdalla wa Ikulu ya Zanzibar wakati wa mchezo wa Kirafiki katika michezo ya Sherehe za Pasaka katika viwanja vya Amani Nje. Ikulu ya zanzibar iliifunga Ikulu ya Dar es Salaam kwa vikapu 26-14
Mchezaji wa Timu ya Ikulu ya Zanzibar Mpira wa miguu Ali Mwinyi (kulia) akijaribu kumcheza Shaaban Kasanga wa Timu ya Ikulu Dar es Salaam,katika mchezo wa Kirafiki katika kusherehekea wiki ya Pasaka  leo katika Uwanja wa Amaan Studium. Ikulu Zanzibar ilitoka kifua mbele kwa mabao 4-2. Picha na Ramadhan Othman wa Ikulu, Zanzibar

Mhe James Mbatia aonesha uzalendo wa hali ya juu katika kuweka mambo sawa kwenye jengo lililopromoka Dar es salaam

$
0
0
Mbunge na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mhe James Mbatia ni mmoja wa mashujaa wasioimbwa (Unsung Heroes) waliofanya makubwa wakati wa zoezi la uokoaji katika jengo lililopromoka leo katika mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam. 
Baada ya kutoka kuaga mwili wa Mbunge wa Chama Cha Wananchi (CUF) Jimbo la Chambani, Salim Hemed Khamis, katika ukumbi wa Karimjee, sio tu alijumuika na wabunge wenzie katika kusaidia kuwatoa katika kifusi watu waliofunikwa baada ya jengo hilo kuporomoka. 
Akiwa mtaalamu wa kushughulikia dharura (Crisis Management expert), Mhe Mbatia alisimama kidete kuhakikisha kuwa shughuli za uokoaji zinakwenda inavyotakikana baada ya kukakamaa na kuamuru askari polisi na walinzi wengine kuondoa umati wa watu uliotapakaa sehemu ya tukio ili kutoa nafasi kwa wahusika kufanya kazi yao kwa ufanisi.
 Globu ya Jamii ilimshuhudia Mhe Mbatia akihaha huku na kule kuweka mambo sawa, na hata kutumia kipaza sauti kuamuru wasiohusika waondolewe eneo la tukio ili kupisha waokoaji wafanye kazi yao. 
Laiti kama asingekuwepo na kuchukua hatua hiyo kazi ingekuwa ngumu maradufu. Mhe Mbatia, bila kujali vurugu na vumbi lililokuwa likitimka, alitumia muda mrefu kuelekeza nini kifanyike, ikiwa ni pamoja na kuamuru uzio uliozunguka msikiti wa Shia Ithnaasheri uliokuwa jirani na jumba lililopromoka kuvunjwa na kupisha vikosi vya uokoaji viwajibike bila shida. Kwa kifupi kuwepo kwake kulifanikisha kazi iliyokuwepo.
Globu ya Jamii inatoa pongezi na shukrani kwa Mhe James Mbatia kwa ushujaa wa hali ya juu aliouonesha, pamoja na wabunge wote waliojitokeza kushirikiana bega kwa began na waokoaji katika dhahma hiyo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mhe James Mbatia
 Mhe James Mbatia akitoa maelekezo kwa Bw Zully Dewji ya nini kifanyike ili kufanikisha kazi
 Mhe James Mbatia, Kamanda Kova na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadik
 Mhe James Mbatia akitoa maelekezo

Ngoma Azipendazo Ankal

$
0
0
Wakubwa wamelalamika kuwa tumewasahau kabisa katika safu hii. Basi nawapa hii ya Aretha Franklin iitwayo 'Respect' ya mwaka 1967

ALBINUS AWA MFALME WA UZITO WA UNYOYA WA DUNIA KWA VIJANA

$
0
0
Albini Felesianu wa Namibia akipambana na Herbert Quartey wa Ghana jijini Windhoek
Rais wa IBF Africa Onesmo Ngowi (kulia) akimpongeza Albinu Felesianu 
Bondia Albinu Felesianu wa Namibia  ameudhihirishia ulimwengu kuwa yeye kweli ndiye Mfalme wa uzito wa unyoya duniani kwa vijana baada ya kumgalagaza bondia Herbert Quartey wa Ghana katika mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa Windhoek Country Club Resort  and Casino leo tarehe 29, March 2013.

Umati wa watu wasiopungua elfu 20 walijazana katika ukumbi huo wa burudani wakimshangilia kwa nderemo na vifijo bondia wao Albinus wakati alipokuwa anafanya vitu vyake kwenye ulingo.
 Baada ya mtangazaji wa ulingo kutamka kuwa “Na sasa bingwa mpya wa uzito wa unyoya duniani kwa vijana ni Albinus Felesianu”mayowe ya wapenzi wa ngumi waliojazana katika ukumbi huo yaliweza kusikika kilometa tatu mpaka katikati ya jiji la Windhoek.
Hata hivyo, haikuwa kazi rahisi kwa Albinus kuunyakua mkanda wa ubingwa wa dunia kwa vijana kwani Mghana Herbert Quartey naye alikuwa mbogo kwani alirusha kila aina ya masumbwi yaliyomo kwenye kitabu.
Wawili hao walichapana makonde mazito kama watu wenye uzito mkubwa na kama sio uwezo na ujuzi wa referii Deon Dwarte wa Afrika ya Kusini kazi ingekuwa ngumu sana kwani kila bondia alijaribu kumpata mwenzake katika sehemu zinazoumiza ili kuumaliza mpambano mapema lakini ujuzi na ubishi wa kila mmoja ulifanya kusiweko na knockout yoyote!
Hii ni mara ya kwanza kwa nchi ya Namibia kuweza kuandaa mpambano wa ubingwa wa dunia wa IBF na wakali hao waliweza kuufanya umati wote uliohudhuria kulipuka kwa makelele ya kushangilia kila wakati.
Alikuweko Harry Simon, ambaye ndiye Mnamibia aliyeweza kuufanya mchezo wa ngumi kupendwa na kuwa maarufu sana nchini humu. Uwezo na utukutu wa Harry Simon ulingoni umeufanya mchezo wa ngumi kupendwa karibu na kila Mnamibia.
Walikuweko pia wageni wengine wengi lakini kampuni ya simu ya Telecom ambayo ndio waliokuwa wadhamini wa mpambano huo imejikusanya kila aina ya sifa na upendo kutoka kwa wananchi wa Namibia jinsi inavyo dhamini mchezo wa ngumi!
Mpambano huu uliandaliwa na Kinda Nangolo wa kampuni ya Kinda Boxing Promotions ambayo ndio waandaaji wa mpambano ujao wa mwezi wa Mei wa bingwa wa IBF Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati katika uzito wa unyoya bondia Gottlieb Ndokosho. Mpambano wa IBF wa Kimataifa wa bondia Harry Simon nao utafanyika mwezi wa Juni.
Aidha, Immanuel “Prince’ Naidjala”wa Namibia na Lesley Sekotswe wa Botswana watarudiana tena mwezi wa July kumpata bingwa wa kimataifa wa uzito wa bantam baada ya kutoka sare walipokitana wiki iliyopota nchini Namibia.
Imetolewa na
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
Benjamin William Mkapa Pension Towers
Tower B, Mezzanine Floor, Azikiwe Street
Dar-Es-Salaam - Tanzania

Article 22

NENO KUTOKA KWA ERIC SHIGONGO

$
0
0
“Kama zilivyo alama za mikono yetu, hakuna mtu anayefanana na wewe.  Umejaa vipaji lukuki ndani yako, tatizo huamini kama unaweza  na kwa sababu watu walikuambia hivyo,  ndiyo sababu hiyo watu wengi wamekufa bila kugundua walikuja duniani kufanya nini.
AMKA LEO, JIAMINI, TENDA UONE MAAJABU YA AKILI YAKO.”
ERIC SHIGONGO.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images