Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

Mkutano wa tano wa Jumuiya ya Vijana wasio na ajira Tanzania (TUWEPO) zanzibar

$
0
0
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wasio na ajira Tanzania (TUWEPO) Ussi Said Suleiman akitoa maelezo mafupi ya Jumuiya hiyo na kumkaribisha mgeni rasmi Mwakilishi wa jimbo la Rahaleo Mhe. Nassor Salim Ali kuzungumza na wanajumuiya.
 Watendaji wa wakuu wa Jumuiya ya TUWEPO wakimskiliza kwa makini Mwakilishi wa jimbo la Rahaleo Mhe. Nassor Salim Ali (hayupo pichani) alipokuwa akiwahutubia.
 Mwakilishi wa jimbo la Rahaleo Mhe. Nassor Salim Ali akiwahutubia vijana wa Jumuiya ya TUWEPO katika Mkutano wa tano wa Jumuiya hiyo, na kusifu jitihada zao za kuwakomboa vijana katika suala zima la kuwapa elemu. Mhe. Nassor ameahidi kuisaidia Jumuiya hiyo.
 Mhe. Nassor Salim Ali akikabidhi cheki ya laki tano kwa niaba ya Jumuiya ya TUWEPO kwa kikundi cha wajasiria mali wa jumuiya hiyo.
 Mgeni rasmin Mhe. Nassor Salim Ali (wa tatu kushoto waliokaa ) katika picha ya pamoja na viongozi wa TUWEPO , wa kwanza kushoto ni sheha wa rahaleo Mhe. Omar Said.
Mgeni rasmin Mhe. Nassor Salim Ali akiagana na vijana wa Jumuiya ya Vijana wasio na ajira Tanzania (TUEPO) katika Ukumbi wa Water Front Rahaleo Mjini Zanzibar. 
Picha na Makame Mshenga - Maelezo.

Usiku wa Tuzo za Filamu wafana jijini Dar, wengingi wapata tuzo

$
0
0
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala pamoja na viongozi mbalimbali wa meza kuu kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 wakipiga picha na baadhi ya washindi wa Tuzo za Filamu 2015 jana zilizofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala pamoja na viongozi mbalimbali wa meza kuu kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 wakipiga picha na baadhi ya washindi wa Tuzo za Filamu 2015 jana zilizofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala akitoa shukrani baada ya kupokea tuzo aliyopewa Rais Jakaya Kikwete na Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFA) kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala akitoa shukrani baada ya kupokea tuzo aliyopewa Rais Jakaya Kikwete na Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFA) kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015.Mama yake na Steven Kanumba akipeana mkono na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo ya mwanaye kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana.Mama yake na Steven Kanumba akipeana mkono na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo ya mwanaye kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

TANZIA: MAMA BISHANGA AFIWA NA KAKA YAKE MKUBWA CASIMU JAFFER MANJI "JALEJALE"

$
0
0
Tarehe 23/05/2015 asubuhi ya Tanzania nimefiwa na kaka yangu mkubwa Bw Casim Jaffer Manji (Jalejale) Kongowe kwa binti yetu Anna Kepha mtoto wa marehemu dada Mwl Cecilia Hatia, Napenda kutumia nafasi hii kumjulisha Abasi Manji na akina Manji wa DSM. Familia ya Jaffer Manji wa Bombey, wadogo zangu
 Dr Geofrey Hatia Nambira wa Namibia, Isaya Hatia wa Finland, na aunt Eva Mack Hatia wa Finland. Familia ya marehemu mzee Abdruhaman Bellim, familia ya mzee Abdala, mzee Jalabi, na shangazi Anna Mchauru wa Masasi ya zamani na Mkuti, ukoo wa che Mbungo wa Lukuledi Masasi, na ukoo wa Hatia wa Ndanda. Na Deo mwalujua na familia yake wa Columbus Ohio.

Kwa taarifa za mipango na ratiba ya mazishi wasiliana na:

Mwl Mack Hatia wa Azania sekondari 225 0754 290 013
Kilian kamota 225 653 0763 200
Constancia Hatia (Mrs Solmon) 225 0712 555 966
Musa Kamota 225 075 609 370 
Fidelis Mrope 225 0713 410 321 
Hendrich Nambira (Kenny) 225 0715 965 321
Joseph Hatia (Ndugu) 225 0713 987 173

Mungu amempenda Zaidi kaka yetu. Tushukuru kwa yote.

Mama Bishanga / Mrs Marolen

Ohio / USA

News alert: Watu sita akiwemo mwalimu wa shule ya msingi wakamatwa na mifupa ya albino Kahama

$
0
0
WATU sita, akiwemo Mwalimu wa Shule ya Msingi Katunguru iliyoko Kata ya Wendele, Tarafa ya Msalala wilayani Kahama, wamekamatwa mjini hapa wakiwa na vipande sita vya mifupa inayodhaniwa kuwa ya albino. 

 Taarifa zilizopatikana mjini Kahama zimeeleza kwamba, mwalimu huyo Bahati Kilungu Maziku (56), Msukuma na mkazi wa Mtaa wa Mbulu katika Halmashauri ya Mji wa Kahama, amekamatwa akiwa na watu watano, wakiwemo waganga wa jadi watatu, katika harakati za kuuziana mifupa hiyo.
Wengine waliokamatwa ni mganga wa jadi Bi. Elizabeth au Shija Makandi Sweya (42), mkazi wa Busongwahala, Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Bilia Masanja Mhalala (39), Msukuma, mkulima na mkazi wa Mogwa wilayani Nzega, mke wa Biria ambaye ni mganga wa jadi Regina au Tatu Kashinje Nhende (40), Msukuma na mkazi wa Mogwa. 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, SACP Justus Kamugisha, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo Mei 21, 2015 na kwamba watu hao walikamatwa saa 7:00 mchana katika nyumba moja ya kulala wageni inayofahamika kwa jina la Maji Hoteli iliyopo Phantom, Kata ya Nyasubi mjini Kahama baada ya Polisi kuweka mtego kufuatia taarifa za wasamaria wema. 
Taarifa ya Kamanda Kamugisha imesema kwamba, mnamo Mei 19, asubuhi, mkuu wa upelelezi wa Wilaya ya Nzega alipata taarifa kuwa kuna mtu anauza viungo vya albino, ndipo walipoweka mtego. Hata hivyo, alisema kuwa walishindwa kuwakamata na baadaye mtu huyo alihamishia biashara hiyo wilayani Kahama. 
 Aidha, watuhumiwa wengine waliokamatwa ni Muhoja John Shija (24), Mnyamwezi na mkazi wa Isagenhe wilayani Nzega pamoja na mganga wa jadi na mfanyabiashara Abubakar Ally Magazi (25), Mrundi na mkazi wa Nzega. Taarifa za uchunguzi wa awali zinaeleza kwamba, Mwalimu Bahati ndiye aliyesuka mpango mzima akishirikiana na waganga wa jadi Bi. Shija Makandi ambaye ndiye aliyeitafuta mifupa hiyo na Abubakar Magazi ambaye alikuwa apelekewe ili ‘kuibetua’ (kuitengeneza) na kuzalisha fedha. 
 Watuhumiwa watano wanadaiwa kwamba walifunga safari kutoka Nzega hadi Kahama kwa Mwalimu Bahati, ambaye kwa mujibu wa maelezo ya awali, ndiye aliyejua ni wapi ambako mifupa hiyo ingeuzwa, hivyo walikuwa wanakutana hapo kwa ajili ya kugawana fedha. 
 Mifupa hiyo inadawa kuhusishwa na tukio la kukatwa mkono wa kulia Bi. Muungu Masaga Gedi (35) mwenye albinism, mkazi wa Kitongoji cha Mkuyuni, Kijiji cha Buhekela, Kata ya Igoweko wilayani Igunga, ambalo lilitokea Mei 16, 2014 na kufunguliwa Jalada Namba IGU/IR/1070/2014. 
 Katika tukio hilo, mume wa majeruhi huyo, Mapambo Mashili, aliuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiofahamika wakati akipambana na watu hao wasimdhuru mkewe.  
 Hata hivyo, amesema, jeshi la polisi bado linaendelea na msako dhidi ya watu wengine wanaotajwa kwamba ndio walioitafuta mifupa hiyo, na kwa mujibu wa taarifa za awali, ndio waliohusika na mauaji pamoja na kumjeruhi mama huyo. Picha zote za watuhumiwa hao 
zimepigwa na Daniel Mbega, Kahama

Bilia Masanja Mhalala.


Mwalimu wa Shule ya Msingi Katunguru wilayani Kahama, Bahati Kilungu Maziku.


Abubakar Ally Magazi.


Elizabeth au Shija Makandi Sweya na Regina au Tatu Kashinje Nhende.

Muhoja John Shija

Makalla afunika Mvomero

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji na mbunge wa Mvomero, Amos makalla jana amehutubia maelfu ya wananchi wa mji Mdogo wa madizini na Vijiji vya jirani  huku akikabidhi Fedha taslimu shilingi milioni 10 kwa vikundi 12 na mabati 200 yenye thamani ya shilingi milioni Tatu kwa ajili ya kupaua Jengo la Tawi la CCM madizini bati 100, misikiti wa lusanga road bati 50 na kanisa la full salvation church bati 50.

Akihutubia maelfu ya wananchi hao aliwaeleza kuwa katika kipindi cha uongozi wake amekuwa ni mdau mkubwa wa kusaidia vikundi, makanisa, misikiti na shughuli nyingi za maendeleo na amewatadharisha wanaotamani jimbo la Mvomero wajipime kama wanaweza kwani kwa umati huu na matamko yanayotolewa na Makundi mbalimbali jimboni ni dhahiri wanaotaka jimbo la Mvomero ni sawa na mtu anayesubiri Ndege bandarini.
Naibu Waziri wa Maji na mbunge wa Mvomero, Amos Makalla akiwahutubia wananchi wa mji Mdogo wa madizini, Mvomero.

Akikabidhi misaada hiyo alisema ameamua kujibu barua za maombi ya vikundi vya ujasiriamali vya Vijana na akinamama vya vitongoji Sita vya madizini na vikundi viwili vya kijiji cha kichangani. Vikundi vilivyofaidika na msaada huo ni mji mpya,kibaite,mpingoni,Kkkt,barabarani,madizini B,kiwandani, Gezaulole, kazi kwanza,Vijana mpingoni , ushonaji kichangani na soko la ndizi kila kikundi kilipata shilingi laki tano.

Alivipongeza vikundi kwa shughuli wanazifanya na akawataka wengine kuiga mfano huo kwani umoja ni ushindi. Aliwaahidi ataendelea kuwaunga Mkono kwani katika kipindi chote cha uongozi wake amesaidia vikundi vingi jimboni.
Kuhusu kero ya kucheleweshewa malipo ya miwa na mishahara kwa wakulima na wafanyakazi wa kiwanda cha Mtibwa ameeleza hatua alizochukua ikiwemo kuipeleka Kamati ya viongozi wa wafanyakazi na wakulima kuonana na Waziri mkuu na jambo hilo linashughulikiwa na hata hivyo katika hatua ya awali amewajulisha ujio wa Waziri wa kilimo na Chakula, Steven Wasira atatembelea kiwanda na kuongea na menejimenti ya kiwanda, wafanyakazi, wakulima na wananchi jumatatu tarehe 25 mei.

Amewaomba wawe watulivu wakati huu ambao ofisi ya Waziri mkuu na wizara ya kilimo ikishughulikia tatizo hilo

Naibu Waziri wa Maji na mbunge wa Mvomero, Amos makalla akikabidhi mabati kwa viongozi wa Dini katika mji Mdogo wa madizini, Mvomero.

TAMASHA LA GOSPEL CONCERT & CONFERENCE MEMORIAL WEEKEND, COLUMBUS, OHIO

$
0
0

Mwimbaji mahili wa nyimbo za injili kutoka Tanzania Upendo Nkone akiimba moja ya nyimbo zilizowainua watu vitin kwenye tamasha la Gospel linaloendelea mjini Columbus tangia siku ya Ijumaa May 22 na kuhitimishwa leo siku ya Jumapili May 24. Tamasha lilihudhuriwa na watu kutoka mataifa mbalimbali wengine wakiwa wamesafiri kutoka majimbo ya mbali na Ohio.

Mwimbaji kutoka Jamhuri ya Congo akienda sambamba na mwimbaji mahili wa nyimbo za injili Upendo Nkone kwenye tamasha la Gospel lililofanyika siku ya Jumamosi May 23, 2015 6230 Busch Blvd suit 260, Columbus, OH 43229.

 Nnunu Nkone akitoa neno la Mungu na kuimba kwenye Tamasha la Gospel lililofanyika
Mchungaji Donis Nkone ambaye ni kaka ya mwimbaji Upendo Nkone akitoa ukifanya utambulisho kwa bendi iliyokuwa ikitumbuiza nyimbo za injili kwenye tamasha la Gospel lililofanyika siku ya Jumamosi May 23, 2015 mjini Columbus.

Mchungaji Donis Nkone na mkewe Nnunu Nkone wakifuatilia tamasha la Gospel. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kilivyoendelea mjini Dodoma leo

$
0
0

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa na viongozi wa ngazi ya juu wa Chama baada ya kuwasili ukumbini. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Wajumbe wakiwa wamesimamaukumbini kumlaki Kikwete alipoingia ukumbini kuendesha kikao hicho leo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, mjini Dodoma leo, May 24, 2015. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. (Picha na Bashir Nkoromo)
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, mjini Dodoma leo, May 24, 2015. Kuahoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara, Philip Mangula Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. (Picha na Bashir Nkoromo)aption
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akishauriana jambo na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kabla ya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kuanza leo, mjini Dodoma Nkoromo)
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiendelea kuongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, mjini Dodoma leo, May 24, 2015. Picha zote na Bashir Nkoromo

JK atoa Msaada kwa Timu ya Kilimani Sports Club mjini Dodoma

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiikabidhi timu ya soka ya Kilimani Sports Club jezi na mipira katika ikulu ndogo ya mjini Dodoma leo asubuhi.Rais Kikwete alitoa msaada kwa timu hiyo baada ya kuwakuta vijana hao wakifanya mazoezi bila zana bora katika uwanja wa mpira ulioko eneo la Kilimani karibu na Ikulu wakati Rais alipokuwa akifanya mazoezi ya kutembea katika eneo hilo.Wakiongea mara baada ya kupokea msaada huo vijana hao walimshukuru Rais Kwa moyo wake wa upendo na nia yake ya kukuza vipaji kwa vijana na kuahidi kufanya vyema katika ligi ya Wilaya ya Dodoma mjini. Picha na Freddy Maro

watatu wapoteza maisha katika ajali ya basi mkoani mbeya leo

$
0
0
Watu watatu wamepoteza maisha leo baada ya basi la abiria  liitwalo Super Feo linalofanya safari zake toka Mbeya Songea baaya ya kupata ajali maeneo ya Inyara mkoani Mbeya likiwa na abiria 20. 
Habari zinasema dereva wa basi hilo lenye uwezo  wa kubeba abiria 53 kutaka kulipita gari lingine  bila ya uangalifu ambapo akakutana na roli mbele yake hivyo katika kujiokoa akakimblia kulia zaidi ndipo basi likapinduka mara tatu na kufikia kwenye kalvati.
Waliotajwa kupoteza maisha ni Anastazia Ngonyani, Robert Lyman kutoka  Marekani na mwanaume ambaye bado hajafahamika jina.
Abiria 13  wako salama dereva wa basi anaitwa shafii ngaiyo ametoroka baada ya tukio.
Taarifa zinasema watu kadhaa wamejeruhiwa ikiwa ni pamoja na Patriki Mwimbila dereva msaidizi wa basi hilo ambaye amevunjika mguu. 
Majeruhi wengine waliotajwa na ambao wote wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya Mbeya ni Sakeni mwandanege, Fatuma nyambi na Feliciana mwalongo.

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

$
0
0
Leo jumapili tarehe 24, Mei 2015 Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF imeketi katika ukumbi uliopo makao makuu ya Shirikisho uwanja wa Karume.

Kamati ya Utendaji imepitia masuala mbalimbali na kutoa maamuzi yafuatayo:

CLUB LICENCING (Leseni za vilabu)
Kamati ya Utendaji imeiagiza sekretarieti ivisisitize vilabu vya Ligi Kuu umuhimu wa kukamilisha maombi yao ya ushiriki wa ligi kuu kwa msimu wa 2015/16 kwa kuwasilisha fomu za maombi ya Leseni za vilabu TFF. Klabu ambayo haitakamilisha mchakato huo haitaruhusiwa kushiriki ligi kuu ifikapo msimu wa 2015/16.

KOMPYUTA - Kutokana na maamuzi ya mkutano mkuu wa TFF uliofanyika Morogoro ambao uliagiza wanachama wake wapya wapewe kompyuta, agizo hilo limetekelezwa na kompyuta hizo watakabidhiwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanaotoka kanda hizo ili waziwakilishe maeneo husika. Mikoa hiyo ni Geita, Katavi, Manyara, Njombe na Simiyu.
MFUKO WA FDF - Kufuatia mkutano mkuu wa TFF kuingiza kipengele cha FDF katika katiba yake, kikao cha Kamati ya Utendaji wa mujibu wa katiba kimepitisha kanuni za uendeshaji wa mfuko huo.

     Aidha kikao hicho kimeteua wajumbe wafuatao wawe wajumbe wa      tume hiyo
     (i)Tido Mhando - Mwenyekiti, 
     (ii) Deogratius Lyatto - Makamu mwenyekiti
     (iii)Ephraim Mafuru - mjumbe,  
     (iv)Beatrice Singano - mjumbe, 
     (v)Joseph Kahama - mjumbe 
     (vi)Ayoub Chamshana - mjumbe.

Pia Henry Tandau ameteuliwa kuwa katibu mtendaji wa mfuko huo.

AJIRA
Kamati ya Utendaji ya TFF imemteua Boniface Wambura kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Bodi ya Ligi Kuu nchini kuanzia tarehe 01, Juni 2015. Wambura kabla ya uteuzi huo alikua mkurugenzi wa mashandano  TFF.TFF inampongeza Wambura kwa uteuzi na inaamini atatoa mchango mzuri katika kukuza na kuzitangaza ligi zetu. 
Kamati ya utendaji imemteau Martin Chacha (mratibu wa timu za Taifa) kukaimu nafasi ya mkurugenzi wa mashandano TFF.

TIMU ZA TAIFA
Kamati ya utendaji ya TFF imesikitishwa na mwenendo mbovu wa Taifa Stars Rais wa TFF, Jamal Malinzi kwa niaba ya kamati ya utendaji amewaomba radhi wapenzi wa mpira kwa matokeo mabaya ya Taifa Stars kwenye michuano ya  Cosafa.
Kikao cha kamati ya utendaji kilipokea taarifa juu ya mwenendo wa timu ya Taifa.Baada ya majadiliano ya kina, ilikubaliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa, Mart Nooij apewe changamoto maalumu ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN na asipofanikisha jambo hilo mkataba wake utasitishwa mara moja.
Maamuzi haya yamezingatia hali halisi ya timu ya Taifa ambayo inakabiliwa na michuano mbalimbali ya kimataifa ndani ya kipindi kifupi. Aidha katika kuliimarisha benchi la ufundi la timu ya Taifa, Leopald Tasso Mkebezi ameteuliwa kuwa meneja mpya wa timu ya Taifa.
Mkebezi amewahi kuwa meneja wa timu ya Taifa katika kipindi cha mwaka 2006 - 2012.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO 
LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

JK apiga tizi na kutoa msaada wa Jezi na mipira Dodoma

UNESCO YASISITIZA UPENDO KWA WATOTO WENYE ALBINISM

$
0
0
DSC_1073
Mdau Semeni Kingaru akimsimamia kula chakula cha mchana mtoto mdogo kuliko wote mwenye albinism aliyeonekana kukosa upendo wa wazazi wake kwa kipindi kirefu na kufarijiwa na ugeni huo uliofika shuleni hapo.
DSC_1101
Mbunge wa viti maalum CCM,anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir akibadilishana mawazo na mabinti wa shule ya msingi Mitindo alipowatembelea na Bi. Zulmira Rodrigues.
DSC_1106
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akisaidiana na Mdau Semeni Kingaru kugawa zawadi ya juisi kwa watoto wa shule ya msingi Mitindo.
DSC_1113
Mtaalamu wa Jinsia na Haki za Binadamu kutoka UNESCO, Bi. Annica Moore aliyeambatana na Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (hayupo pichani) akifurahi jambo wakati akigawa zawadi ya juisi mmoja watoto wenye albinism shuleni hapo. Picha zaidi BOFYA HAPA

Serikali yajipanga kuboresha mazingira rafiki ya hedhi Salama kwa wanafunzi

$
0
0
Mratibu wa huduma ya Maji, Afya na Usafi wa mazingira shuleni kutoka wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi Theresia Kuiwite (Katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya Hedhi Duniani yatakayofanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania tarehe 28 Mei, yatakayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 

Kauli mbiu ya mwaka huu Ikiwa "Usisite Kuzungumzia Hedhi". Wengine kushoto ni Mwandaaji wa maadhimisho hayo kutoka kampuni ya Kasole Secrets LTD, Bi. Hyasintha Ntuyeko na Bi Emmy Manyelezi (Kulia) ambae ni Mratibu wa mradi kutoka shirika la Water Aid Tanzania.

SERIKALI imetangaza programu maalumu inayolenga kuziwezesha shule za msingi na sekondari hapa nchini kuwa na vyumba maalumu tofauti na choo vitakavyo wawezesha wanafunzi wa kike kupata faragha za usafi wakati wa hedhi wakiwa shuleni.

Hatua hiyo ya serikali iliwekwa bayana na Mratibu wa huduma ya Maji, Afya na Usafi wa mazingira shuleni kutoka wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi Theresia Kuiwite alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya siku hedhi duniani yanayotarajiwa kuadhimishwa Mei 28 mwaka huu.

“Lengo ni kupunguza tatizo la mahudhirio hafifu miongoni mwa wanafunzi wa kike ambao wamekuwa wakishindwa kuhudhuria masomo wanapokuwa kwenye hedhi kutokana na ukosefu wa miundombinu rafiki inayoweza kuwapa faragha za wao kufanya usafi wanapokuwa kwenye hali hiyo,’’ alisema.

Kwa mujibu wa Bi. Kuiwite, mpango huo tayari umekwishaanza kutekelezwa katika baadhi ya maeneo hapa nchini ikiwemo wilaya ya Njombe huku akibainisha kuwa kwa sasa wanafunzi wengi wa kike wamekuwa wakishindwa kuhudhuria masomo yao kwa zaidi ya siku 3 hadi 5 kutokana na hedhi jambo linalozorotesha ufahulu wao darasani.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Kasole Secrets LTD, Bi. Hyasintha Ntuyeko ambae pia ni mdau na muandaaji wa  maadhimisho ya Siku ya Hedhi Duniani  alisema Kampuni yake kwa kushirikiana na wadau wengine wameamua kuitumia siku hiyo kuhamasisha mabadiliko ndani ya jamii hususani mila na desturi zinazosababisha suala la hedhi kwa mwanamke lionekane kama ni jambo la aibu kwa jamii.

“Ukweli upo wazi kwamba hata matatizo mengi ya wanawake kuhusiana na uzazi chimbuko lake ni kushindwa kwao kukabiliana na hedhi kwa njia salama haswa walipokuwa katika umri mdogo. Kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni ‘USISITE KUZUNGUMZIA HEDHI’“, alibainisha.

Kwa mujibu wa Bi. Hyasintha, maadhimisho hayo yataongozwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhe. Anna Kilango Malecela na yanatarajiwa kupambwa na matembezi ya hiari yatakayoanzia Wizara ya elimu saa 34:00 asubuhi - 06:00 mchana na kumalizikia katika viwanja vya Mnazi Mmoja siku ya tarehe 28,Mei, 2015.

Naye Bi Emmy Manyelezi ambae ni Mratibu wa mradi kutoka shirika la Water Aid Tanzania alitoa wito kwa wadau mbalimbali hususani sekta binafsi kuhakikisha wanaisaidia serikali katika kuhakikisha kuwa vifaa muhimu vinavyohusu masuala ya hedhi zikiwemo pedi za wanawake vinawafikia wananchi wote hususani waliopo vijijini na kwa bei nafuu.

Zaidi ilielezwa kuwa maadhimisho hayo pia yatatoa fursa kwa washiriki kubadilishana elimu juu ya usafi wa hedhi, uzoefu, changamoto na ufumbuzi endelevu kwa ajili ya wasichana wa mashuleni na wanawake kwa ujumla.

MWENYEKITI WA CHADEMA NA MBUNGE WA HAI FREEMAN MBOWE AZINDUA KITABU CHA UTEKELEZAJI AHADI ZA JIMBO LA KAWE

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akisalimiana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima wakati wa mkutano wa hadhara uliokwenda sambamba na uzinduzi wa kitabu cha utekelezaji wa ahadi za jimbo la Kawe.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe  akizindua kitabu cha ukekelezaji wa ahadi za jimbo la Kawe kulia ni Mbunge wa Kawe-Chadema Halima Mdee
 Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe akihutubia.
 Umati wa watu waliohudhuria mkutano huo.

Familia ya mtoto aliyegongwa na fuso na kukatwa miguu anaomba msaada wa kisheria

$
0
0
Naibu Kamanda wa UVCCM ,Innocent Melleck akiwa na mama mzazi wa mtoto Felista ,Beatrice Shirima mara baada ya kukabidhi kiti cha walemavu cha magurudumu kwa ajili ya kusaidia kutoka eneo moja hadi jingine.
Naibu kamanda wa UVCCM wilaya ya Moshi vijijini ,Innocent Melleck akikabidhi Pempers kwa mama wa mtoto Felista ,Beatrice Shirima kwa ajili ya kumsaidia mtoto huyo aliyepata ulemavu wa miguu miwli baada ya kugongwa na gari aina ya Fuso.(Na Dixon Busagaga).
Naibu kamanda wa UVCCM wilaya ya Moshi Vijijini ,Innocent Melleck akiwa amembeba mtoto Felista Shirima(3) aliyekatwa miguu yote miwili baada ya kugongwa na gari aina ya Fuso jirani na nyubani kwao.

Akizungumzia sakata la mtoto huyo Naibu kamanda huyo alisema kuwa ataumia kila aina ya uwezo na nguvu zake kwa kushirikiana na ofisi ya umoja wa vijana wa chama chama mapinduzi UVCCM ili kuhakikisha kuwa  haki ya mtoto huyo inapatikana.

Awali akizungumza mara baada ya kukabidhiwa msaada wa baiskeli  ya magurudumu matatu na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi laki saba na kamanda huyo, mama mzazi wa mtoto huyo Beatrice Kelvin,aliiomba serikali na wadau mbalimbali kujitokeza na kumsaida mwanae ili kuhakikisha haki inapatikana. 

Alisema kesi iliyokuwepo mahakama kwa ajili ya kudai haki za msingi za mwanae imeisha bila haki yake kupatikana licha ya kuhangaika sehemu mbalimba na kuomba vyombo husika vinavyo jishughulisaha na haki za binadamu kuingilia kati suala hilo hatua ambayo itasaida kupata haki.

KAMPUNI YA SHELTER AFRIQUE YATOA DOLA MILIONI 1 KUWEKEZA NDANI YA TMRC

$
0
0
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya mikopo ya nyumba ya Tanzania Mortgage Refinance (TMRC), Oscar Mgaya (kulia) akipokea jijini Dar es Salaam,  mfano wa hundi ya Dola za Kimarekani milioni moja kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SHELTER AFRIQUE, James Mugerwa (wa pili kushoto), baada ya kampuni hiyo kununua hisa asilimia 11.6 katika TMRC. Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Fedha Mkuu wa TMRC, Oswald Urassa na  Mkurugenzi wa Uendeshaji na Mfumo Habari wa taasisi hiyo, Shabani Mande.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya mikopo ya nyumba ya Tanzania Mortgage Refinance (TMRC), Oscar Mgaya (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SHELTER AFRIQUE, James Mugerwa (katikati) na Ofisa Fedha Mkuu wa TMRC, Oswald Urassa (kushoto) katika hafla hiyo. Taasisi ya TMRC ina wanahisa 14 ambao ni benki za Exim, NMB, CRDB, NBC, Azania, TIB, DCB, NIC, ABC, PBZ, BOA, I&M Bank, NHC na SHELTER AFRIQUE.  
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya mikopo ya nyumba ya Tanzania Mortgage Refinance (TMRC), Oscar Mgaya (wa sita kushoto) akizungumza kabla hajapokea  mfano wa hundi ya Dola za Kimarekani milioni moja kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SHELTER AFRIQUE, James Mugerwa (kulia kwake), baada ya kampuni hiyo kununua hisa asilimia 11.6 katika TMRC. Wengine ni maofisa wa TMRC.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 25.05.2015

TPSC yazindua jengo jipya jijini Mbeya

$
0
0
Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani akikata utepe kuzindua jengo jipya litakalotumiwa na TPSC tawi la Mbeya eneo la Soko Matola, jijini hapa, kulia ni Mkuu wa TPSC Said Hamis Nassor na kushoto ni Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga.
Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani akishusha pazia kuashiria uzinduzi wa jengo jipya litakalotumiwa na TPSC tawi la Mbeya eneo la Soko Matola, kulia ni Musa Zungira,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya. 
Sehemu ya wafanyakazi na wanafunzi wa TPSC tawi la Mbeya wakimsikiliza Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani.

bei ya Madafu leo

WANANCHI VIJIJINI KUNUFAIKA NA MAWASILIANO YA SIMU KUTOKA TTCL

$
0
0
Kampuni ya Simu Tanzania(TTCL) kuwapatia wananchi waishio vijijini zaidi ya Laki Moja mawasiliano ya Simu ifikapo mwaka 2016. Jumla USD 3.3 (sawa na Bilioni 6.8 Tsh) zitatumika kwa ajili ya kupeleka mawasiliano kwenye kata 41 zenye vijiji 41 kupitia ruzuku kutoka kwa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(UCSAF) ikiwa ni awamu ya 2B.

Kata hizo ni pamoja; Oljoro –Arusha, Olmotonyi- Arusha, Olorieni – Arusha, Chikola- Dodoma, Mpalanga- Dodoma, Farkwa-Dodoma, Iduo-Dodoma, Masagalu-Tanga, Mazinde- Tanga , Mpale-Tanga, Misalai-Tanga, Ivaeny- Tanga, Kashisha-Tanga, Kashisha-Tanga, Arri-Manyara, Ayasanda-Manyara, Sigino-Manyara, Lengatei-Manyara, Bashay- Manyara, Buhendangabo- Kagera, Nyakato-Kagera, Ihembe- Kagera, Mwandu- Mwanza, Kiloleli- Simiyu, Itinje-Simiyu, Isanzu-Tabora, Neruma- Mara, Rigicha- Mara, Bwanga-Geita, Kasenga-Geita, Lumuli-Iringa, Kihesa-Iringa, Namichiga- Lindi, Galula-Mbeya, Luwalaje- Mbeya, Mbangala-Mbeya,Namkukwe- Mbeya, Kajunjumele- Mbeya, Kapele- Mbeya Mdandu-Njombe, Liparamba-Ruvuma.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa akizungumza na wadau wa makampuni ya simu pamoja na wananchi waliohudhuria uwekaji wa saini wa kupeleka mawasiliano vijijini.
Katibu Mkuu wa Wizara wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Patrick Makungu akitoa hotuba katika hafla ya uwekaji wa mikataba ya kupeleka mawasiliano ya simu vijijini.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr. Kamugisha Kazaura akitoa neno la shukhurani kwa niaba ya Makampuni ya Simu, baada ya makampuni hayo kushinda zabuni ya kupeleka mawasiliano kwenye jumla ya kata 117.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI  
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images