Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

RAMADHAN CONFERENCE


Cholera outbreak triggers UNICEF cross-border relief operation

$
0
0
Lake Tanganyika, Burundi-Tanzania border, May 20, 2015 – UNICEF has rushed relief supplies to Tanzania’s north-western border with Burundi, in response to a devastating cholera outbreak among 50,000 Burundian refugees gathered on the shores of Lake Tanganyika.

UNICEF has dispatched cholera treatment supplies, as well as WASH, health and nutrition items, shuttled in from Burundi and Tanzania to the affected area, and is working with partners on both sides of the border to help scale up the response.

Burundi’s current unrest has forced more than 110,000 people to flee to neighboring countries. Most are women and children, and a majority have arrived in Tanzania, where a cholera outbreak has so far claimed 27 lives.
“Children constitute more than half of the population on the move and are particularly vulnerable to cholera,” says Johannes Wedenig, UNICEF Representative in Burundi. “Concerted action by the two countries has fast tracked the dispatch of lifesaving commodities to stem the spread of the epidemic.”

The village of Kagunga has seen the highest number of arrivals, with around 50,000 camped out on its shores, in a remote and hard-to-reach part of Tanzania.

Overcrowding and poor sanitation have resulted in a surge of confirmed or suspected cases of cholera and acute watery diarrhea among the refugees, and without a cholera treatment centre on site in Kagunga, mortality rates may run extremely high.

In Burundi, 15 suspected cases of cholera have been brought to the district hospital of Nyanza Lac, where infection reportedly originated from people who recently tried to cross into Tanzania. The Burundian Ministry of Health and partners have now re-opened a cholera treatment center in the area, with support from UNICEF.

Relief supplies delivered by UNICEF include a cholera treatment kit for 100 cases, chlorine, soap, water purification tablets and plastic buckets. High-nutrition ready-to-eat food was also provided by UNICEF to cover up to 1,000 vulnerable children for one week.

Burundians have fled to three neighboring countries, Rwanda, DRC, and Tanzania, where UNICEF is on the ground working with partners to provide basic healthcare, nutrition, water, sanitation, child protection and education services.

Dr. Winnie Mpanju-Shumbusho kutoka Tanzania ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Geneva, Uswisi

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Dr. Margaret F. Chan amemteua Dr. Winnie  Mpanju-Shumbusho kutoka Tanzania kuwa Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Afya Duniani, upande wa masuala ya Ukimwi, Kifua Kikuu Malaria na Magonjwa yaliyosahaulika. Uteuzi huu umetangazwa rasmi na Dr. Chan wakati wa kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Shirika la Afya Duniani kilichoanza tarehe 14 mpaka tarehe 26 Mei 2015, Geneva, Uswisi.

Dr. Mpanju-Shumbusho ni mtaalamu na kiongozi mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 30 katika ngazi za juu za uongozi katika sekta ya Afya na Ushirikiano wa Kimataifa.

Kabla ya uteuzi huu, Dr. Mpanju-Shumbusho alikuwa Naibu wa Mkurugenzi Mkuu Msaidizi ndani ya Shirika la Afya Duniani upande wa Ukimwi, Kifua Kikuu, Malaria na Magonjwa yaliyosahaulika na akiwa na cheo cha Ukurugenzi wa Idara inayoshughulikia Ushirikiano wa Shirika la Afya Duniani na Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund to Fight AIDS, Tuberculosis na Malaria). Dr. Mpanju-Shumbusho pia ni mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani kwenye Bodi ya Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria na Bodi mbalimbali za kimataifa.

Hapo awali, Dr. Winnie Mpanju-Shumbusho alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya kudhibiti Ukimwi na magonjwa mengine husika katika ya Shirika la Afya Duniani (WHO), makao makuu Geneva, Uswisi.

Kabla ya kujiunga na Shirika la Afya Duniani, amewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa East, Central and Southern Africa Health Community Secretariat yenye makao makuu yake, Arusha, Tanzania. Vilevile, aliwahi kuwa Mkuu wa Idara na Mhadhiri Mwandamizi, Idara ya Afya ya Jamii na Mgonjwa ya Watoto, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (Muhimbili University of Health Science). Katika wadhifa huu, Dr. Winnie pia alikuwa mwanzilishi wa mipango mbalimbali ya Afya na taaluma na Mshauri Mkuu wa Wizara ya Afya, Tanzania upande wa Afya ya Jamii. Pia amewahi kuwa mjumbe wa Bodi mbalimbali za kimataifa.

Dr. Mpanju-Shumbusho ana Shahada ya Udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; vilevile ana Shahada ya Uzamili katika Afya ya Jamii kutoka Chuo Kikuu cha Tulane, Marekani na Shahada ya Uzamili katika Medicine (Paediatric and Child Health) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, vilevile ana Shahada ya Uzamifu na Shahada nyingine mbalimbali.

Akiwa Mkurugenzi na mtaalamu katika Shirika la Afya Duniani, amekuwa mstari wa mbele katika kuandaa, kuongoza na kutekeleza mipango mkakati ya Dunia ya kujenga na kuimarisha sekta ya Afya hususani katika nchi maskini na zile zinazoendelea. Mipango hii imezaa mafanikio makubwa ikiwemo kujenga uwezo wa nchi maskini kukabiliana na maradhi ikiwemo pia afya za kina mama na watoto. 

Sambamba na hilo, mipango hii pia ilifanikisha upatikanaji wa madawa ya gharama nafuu katika nchi maskini ili kuweza kumudu gharama za matibabu kwa watu maskini. Nchini kwetu, Dr. Mpanju-Shumbusho ameweza kufanikisha upatikanaji wa matibabu na huduma nasaha za kusaidia kudhibiti ugonjwa wa Ukimwi, Kifua Kikuu, Malaria na magonjwa yaliyosahaulika.

Dr. Shumbusho ameolewa na ana watoto wawili, wa kiume na kike.

MTEMVU ATATUA MGOGORO YA MIKATABA KWA WANANCHI WA MTA WA CHAUREMBO, KURASINI JIJINI DAR

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu akizungumza na wananchi wa kijiji Chawavuvi Mta wa Chaurembo uliyopo Kurasini baada ya kutokea mwekezaji na kuwa na sinto fahamu ya muda mrefu na kupelekea wananchi kufanya maandamano ya amani hadi Ofisi za Serikali ya Mta huo na kumlazimu Mbunge kuingilia kati mgogoro huo  Dar es Salaam leo (PICHA ZOTE  NA KHAMISI MUSSA)
  Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu  akipitia moja ya mkataba waliyoandikiwa wananchi hao na mwekezaji ambayo wananchi hao hawajaridhishwa, Muhandisi Msaidizi wa Bandari  na kiongozi wa kero za wananchi wa kijiji Chawavuvi Mta wa Chaurembo Kurasini David Mlassi akimweleza mambo fulani mbunge huyo (kushoto)
 Wananchi wa kijiji cha Wavuvi wa Mta wa  Chaurembo wakimsikiliza Mbunge huyo.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

BALOZI KAMALA AMSHUKURU MZEE NYAMTARA MUKOME KWA KAZI NZURI ALIYOFANYA UBALOZI WA TANZANIA UBELGIJI

$
0
0
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (kulia) akimkabidhi Mzee Nyamtara Mukome zawadi ya kumshukuru kwa kazi nzuri aliyofanya Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji alipokuwa Afisa wa Mambo ya Nje Ubalozi wa Tanzania Ubeligiji masuala ya Jumuiya ya Ulaya. Mhe. Nyamtara amestaafu na wiki ijayo anarejea Tanzania.

EXCLUSIVE: President Goodluck Jonathan's LEGACY with Zuriel Oduwole/ ELECTORAL REFORMS

TASWIRA KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akijibu maswali bugeni mjini Dodoma, Mei 21, 2015.
Waziri wa Katiba na Sheria,Dkt. Asha Rose Migiro akiwasilisha Makadirio ya Matumizi ya wizara hiyo , bungeni mjini Dodoma Mei 21, 2015.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri MkuuSera Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama akizungumza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, bungeni mjini Dodoma Mei 21, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

NAPE AHIMIZA MSHIKAMANO MTAMA

$
0
0
 Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa akisalimiana na Mzee Masoud Ali Chitende Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Mtama mara baada ya kuwasili kwenye kata ya Mtama ambapo alipata nafasi ya kuwasalimu wajumbe wa Halmashauri Kuu za Kata Mtama na Majengo, Mtama mkoani Lindi.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mtama Mzee Said H. Maluma,kushoto ni Mwenyekiti wa CCM kata ya Majengo Mzee Omari Mataka.
 Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu za Kata ya Mtama na Majengo wakimsikiliza Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye .


JARIDA LA WIKI LA NISHATI NA MADINI TOLEO LA 68

KUMBUKUMBU

$
0
0
MWL. ERNEST MWAMKAI KIONDO

Mpendwa Baba, tarehe 22 May 2015 umetimiza mwaka mmoja tangu ututoke hapa duniani kwa mapenzi yake Mwenyezi Mungu.

Tunakukumbuka sana kwa malezi, upendo na ushauri wako  ambao daima ndio dira yetu na kumbukumbu yetu.

Unakumbukwa sana na Wazazi wenza Mama Anna na Mama Agatha, Dada zako na sisi wanao, wakwe zako, wajukuu wote pamoja na ukoo wote wa Kiondo, Bendera, Mbaruku, Msangazi, Bila, Mjata na  Nyangasa.

Japo haupo tena pamoja nasi kimwili, lakini kiroho tuko pamoja nawe kila siku.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu aendelee kukuhifadhi  mahali pema peponi.

AMEN.

Kutakuwa na misa ya kumuombea Marehemu Mzee wetu Jumamosi  tarehe 6/6/2015 katika Kanisa la Mtakatifu Yohana  Krisostomo, Majani Mapana, Tanga.

Misa inategemewa kuanza saa 3 asubuhi na kabla ya hapo, Ijumaa tarehe 5/6/2015 kutakuwa na mkesha  nyumbani kwa Marehemu Kwaminchi Tanga, karibu na Uwanja wa saba saba.
Karibuni sana.

MPENDWA BABA TUTAKUKUMBUKA DAIMA

SIJAFUKUZWA UANACHAMA WA TLP-MREMA

$
0
0

Mwenyekiti   wa chama cha Tnzania Labour Part (TLP) Agustino Mrema akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo)   katika mkutano uiliofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari MELEZO kuhusu kukanusha  kuwa yeye amefukuzwa TLP,Kushoto Mkurugenzi wa Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo,Kulia ni Katibu Mkuu wa TLP,Nancy Mrikariya.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

MWENYEKITI wa Chama cha Tnzania Labour Party (TLP) Agustino Mrema,amesema hajafukuzwa unachama katika chama hicho.

Mrema aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana kuwa yeye ni mwenyekiti wa Chama hicho na hakuna mtu wa kumtoa kutokana na kuendesha chama hicho kwa kufuata katiba.

Amesema kikundi kinachofanya hivyo na kusambaza taarifa kuwa kimemtoa kutokana na kufanya vikao hakitambui na kuwataka wanachama kuwabeza watu hao. 

Mrema amesema yeye akiwa Mwenyekiti ataendelea kutetea jimbo lake la Vunjo,hivyo watu wanaosema amefukuzwa katika chama wapuuzwe.
Aidha amesema biashara ya Urais ameachana nayo ,sasa kazi yake ni Ubunge kupitia jimbo la Vunjo na ameweza kuleta maendeleo ya wananachi katika jimbo hilo.

vanessa mdee afiwa na dada yake mkubwa

$
0
0
Muimbaji mahiri Vanessa Mdee amefiwa na dada yake mkubwa Anna Mdee, ambaye amefariki katika hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam,  jana Jumatano alfajiri. Anna ambaye alikuwa mfanya kazi wa kampuni ya sigara ya TCC na alikuwa katika kituo cha Dodoma kwa muda mrefu alikuwa India akipatiwa matibabu.

Anna na Vanessa ni watoto wa marehemu Sammy Mdee, aliyekuwa mwandishi mkongwe aliyewahi kuongoza gazeti la Daily News, Katibu wa Mwalimu Nyerere na pia mkurugenzi wa kituo cha AICC. Mazishi ya Anna yatakuwa Same Jumamosi saa 8 mchana.

Mungu Amlaze Pema Anna Mdee

KADA WA CCM ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Dotto Mwaibale 
 KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Kawe jijini Dar es Salaam, Elias Nawera, ametangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo la Kawe katika uchaguzi mkuu unatorajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, kwa tiketi ya chama chake. 
 Akitangaza nia yake mbele ya wanachama na viongozi wa chama hicho jijini Dar es Salaam jana, Nawera ambaye ni Wakili wa kujitegemea alisema anayo nia ya kuwania ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM. 
 Alisema anaamini kuwa anatosha kuliongoza jimbo hilo kwakuwa amekuwa kada kwa muda mrefu na kwamba wakati wa kuwania nafasi hiyo ukifika atakuwa miongoni mwa watakaojitokeza kuchukua fomu ndani ya chama kwa lengo la kugombea kuchaguliwa ili kuwa miongoni mwa wawania ubunge jimboni humo. 
 "Nataka kulirudisha jimbo ili mikononi mwa Chama cha mapinduzi, hivyo ndugu zangu nimesimama mbele yenu kutangaza nia yangu ya dhati ya kutaka kuwania jimbo ili pale muda utakapofika na mimi nitakuwa miongoni wa nitakaoomba ridhaa kwa chama changu.
 "Ndugu zangu nitaomba ushirikiano wenu pale muda utakapofika na kwa pamoja tuhakikishe kuwa jimbo hili linarejea CCM kwa ushindi wa kishindo"alisema Nawera. 
 Kwa upande wake Meneja Kampeni wake Harold Maruma alisema kwamba anaamini kuwa wakati wa mchakato wa kugombea ndani ya chama utakapofika, Nawera atakuwa miongoni mwa watakaoomba ridhaa ya kuwa mgombea kwa tiketi ya chama hicho. 
 Alisema kwamba nia ni moja kuhakikisha kuwa CCM inapata ushindi wa kishindo na kwamba kwasasa kinachofanyika ni kuweka nia ukizingatia kuwa jimbo hilo linaongozwa na upinzani hivyo kwa CCM linahesabika kama lipo wazi. Imeandaliwa na mtandao wa http:www.habari za jamii.com
Wakili wa Kujitegemea, Elias Nawera.

Kada huyo, Elias Nawera (katikati), akizungumza na wanachama wa CCM na viongozi mbalimbali (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Tawi la Kawe Ukwamani, Chande Mbonde, Diwani mstaafu wa Kata ya Mikocheni (CCM), Harold Maruma ambaye ni kampeni Meneja wa Elias Nawera, Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kawe, Lilian Mkotani na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kawe, Athumani Athumani.
Diwani mstaafu wa Kata ya Mikocheni (CCM), Harold Maluma ambaye ni kampeni Meneja wa Elias Nawera akimtambulisha mgombea huyo mbele ya viongozi wa kata hiyo na waandishi wa habari (hawapo pichani)
Mjumbe wa Propaganda wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam ambaye alikuwa ni Mshereheshaji (MC), wa shughuli hiyo, Muhidini Mtengereka,  akitoa mada mbalimbali.

Makada wa CCM wa Kata ya Kawe 
wakiwa kwenye mkutano huo.


HAKUNA MAENDELEO BILA NISHATI YA UHAKIKA-MHE. KITWANGA

$
0
0
 Na Mwandishi Maalum, New York 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaamini kwamba, utekelezaji wa mipango na malengo ya mbalimbali ya maendeleo hayataweza kupatika au kufikiwa kwa haraka pasi na uwepo wa nishati endelevu na kwa wote. 
Ni kutokana na kulitambua hilo, Tanzania imejikita kikamilifu katika kukuza uwezeshaji wa matumizi ya teknolojia za kisasa na mbinu za kuongeza upatikanaji wa huduma za kisasa za nishati ikiwa ni pamoja na kuongeza maradufu kiwango cha uboreshaji na ufanisi wa nishati mbadala ili kuchagiza maendeleo. 
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Charles Kitwanga ( Mb), wakati akizungumza katika siku ya pili ya majadiliano ya mawaziri wanaohusika na sekta ya nishati ambapo kila waziri aliyehudhuria mkutano huo alipata fura ya kuelezea na kutoa ahadi ya namna inavyotekeleza mkakati wa nishati endelevu wa wote (SE4All). 
Mhe. Kitwanga na ujumbe wake unaowashirikisha wataalamu mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Madini akiwano Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Ngosi Mwihava wameshiriki kikamilifu katika mkutano huu ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ambapo tangu ulipoanza mapema wiki hii, washiriki wamekuwa wakijadili mada mbali mbali zinazohusiana na masuala ya nishati, uwekezaji na mchango wake katika eneo zima la utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu. 
“ Tanzania inaamini kwamba hakuna ajenda za maendeleo zinazoweza kufikiwa kwa ukamilifu pasipo uwepo wa nishati ya uhakika” akasema Naibu Waziri Na kuongeza kuwa, mkakati wa nishati endelevu kwa wote ni nyezo muhimu katika kurahisisha ukusanyaji na uwekezaji wa raslimali inayohitajika ili kufika malengo ya kitaifa ya nishati endelevu kwa wote kufikia mwaka 2034 kama inayoainishwa katika mkakati huo. 
Kwa mujibu wa Naibu Waziri, Charles Kitwanga, Tanzania ilipitisha mkakati wa SE4All mwaka 2012 na kufuatiwa na mchakato wa kufanya tathmini ili kubaini mapungufu ambayo yalipelekea kutoa taarifa ya tathmini mwaka 2013. 
 Baada ya tathmini hiyo ilifuatia misaada kutoka SE4All kwaajili ya Afrika iliyosaidia kuandaa rasimu ya Ripoti na nchi ( Country Action Agenda) kwa ufadhili wa Banki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB) na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ( UNDP). 
Kwa mujibu wa Mhe. Kitwanga, taarifa hiyo inatarajiwa kuwasilishwa kwa udhibitisho mwezi Agosti, 2015. Aidha maandalizi ya Mpango wa Uwezeshaji umeanza na utalenga katika kuangalia mahitaji ya haraka ili kuwezesha mpango huo kuanza kutekelezwa. Mkutano kuhusu Nishati Endelevu kwa wote (SE4All) umefungwa jana ( Alhamis).
 Mhe. Charles Kitwanga ( Mb) Naibu Waziri, Nishati na Madini akizungumzia namna  Tanzania  inavyotekeleza     Mkakati wa Nishati Endelevu kwa Wote  (SE4All) wakati wa  Mkutano wa siku Mbili wa  Mawaziri wa  Sekta ya Nishani,  uliofanyika  hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
 Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini ambao wamefuatana na  Naibu  Waziri  katika mkutano huu muhimu  uliojadili kwa kina  nafasi na umuhimu wa nishati endelevu kwa  wote  katika kusukuma mbele malengo ya maendeleo endelevu , ukuaji wa uchumi, maendeleo ya jamii na utunzaji  wa mazingira.
 Kaimu Katibu Mkuu,  Bw. Ngosi Mwihava akiwasilisha  Action Agenda of Tanzania  kuhusu SE4All  katika moja ya mikutano  iliyofanyika hapa jijini  New York.
 Kaimu    Katibu Mkuu,  Bw. Ngosi  Mwihava akiwa  na wataalamu wake na wataalamu washauri  wakibadilishana mawazo kuhusu Action Plan of  Tanzania.
Mhe. Kitwanga akiteta jambo na  Mwakilishi wa  Bank ya Maendeleo  kwaajili ya Afrika  AfDB muda mfupi  mara baada ya   Naibu    Waziri kuzungumza ,  mkutano huu wa SE4All,  pamoja na  Mawaziri wa sekta husika umewashirikisha pia wadau mbalimbali wakiwamo wakuu wa  vyombo   vya fedha kama  vile Bank ya Dunia,  AfDB na wataalamu wengine wakiwamo pia wanamziki  maarufu ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakichagiza na kuwekeza katika  nishati endelevu.

NANI KUJINYAKULIA TUZO ZA FILAMU 2015 KESHO JUMAMOSI!

$
0
0
Raisi wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba(katikati) akielezea jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati alipokutana nao katika ofisi zake kuelezea siku ya tuzo za filamu zitakazofanyika jumamosi hii jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Bwana Ezekiel kutoka Push Mobile na kushoto kwake ni Meneja Masoko wa EATV na EAR Happy Shame.
 Meneja Masoko kutoka EATV na EA Radio Happy Shame(kulia)akielezea jambo kwa Raisi wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba wakati wa mkutano na wana habari kuhusu Tuzo za Filamu Tanzania 2015 leo jijini Dar es Salaam ambapo EATV na EAR ni moja ya wadhamini wa tuzo hizo.

Mei 23, hapatoshi Mwalimu Nyerere Internnational Conference Center;

 Ni siku moja tu imebaki kufanyika kwa tuzo kubwa za filamu nchini ‘Tanzania Film Awards’ 2015(TAFA). Ni tuzo kubwa ambazo zitafanyika kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam tarehe 23 Mei 2015, Mwalimu Nyerere International Conference Center. Haya ni mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu nchini na kila mmoja ana shauku ya kushuhudia tuzo hizo zitakazo wapa wasanii wetu amsha amsha ya mafanikio katika tasnia yao.

Akiongea na wana habari katika ofisi zake raisi wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba alisema, “Maandalizi yote yapo tayari na tumejipanga kikamilifu kufanikisha tuzo hizi. Kutakuwa na burudani mbalimbali kusherehesha tuzo hizi zikiongozwa na mzee Kikii, Mwasiti na Barnaba, pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wana tasnia ya filamu watakaowakilisha vizuri kabisa tasnia yao kwa kutufanya tucheke na tufurahi. 

Yote hii ni kuwaburudisha wageni wetu watakaokuja kutuunga mkono katika siku hii muhimu kwa wana tasnia ya filamu.Tuna wageni mbalimbali ambao wameshafika kutoka nchi tofauti za Afrika ili kutuunga mkono katika hafla hii”.

 “Napenda kuwashukuru waisani mbalimbali waliojitolea kutuunga mkono Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, TRA, EATV na EAR, International Eye Hospital, Foreplan Clinic, R&R Associates, Simu Tv na Barazani Production. Kwa namna ya pekee nashukuru vyombo vyote vya habari kwa sapoti kubwa waliotupa kipindi chote cha mchakato wa tuzo hizi tangu wakati wa uzinduzi hadi sasa bado wapo nasi bega kwa bega.”

“Wito wangu kwa watanzania na wana Afrika Mashariki kwa ujumla kutuunga mkono kwa kununua tiketi za hafla hii ili waweze kufika kushuhudia tuzo hizi za kipekee zitakazo andika historia mpya katika tasnia ya filamu. 

Tiketi zinapatikana kwa bei ya 50,000/= kawaida na VIP ni 100,000/= katika vituo vifuatavyo;Shear Illussion - Mlimani City and Millenium Towers, Robby One Fashion- Kinondoni and Sinza Africasana, B&B Boutique- Dar Free Market duka namba 46 na Viva Towers duka namba 31, Secky Bureau de Change - Big Bon Sinza Mori,  Save Mart wholesalers - Mikocheni kwa Nyerere EATV na ITV.  Karibuni sana tufurahie na kuunga mkono kazi za wasanii wetu.” Alisisitiza Mwakifwamba.

Tuzo za Filamu Tanzania 2015 zitakua na ‘surprises’ za kutosha hasa kushuhudia mastaa kutoka nchi za Ghana na Nigeria na mengine kibao. Watanzania wajitokeze kwa wingi kuunga mkono kazi za wasanii wetu hii ni kuonesha uzalendo kwa kupenda kazi za wasanii wetu.

HAKUNA MAENDELEO BILA NISHATI ENDELEVU - KITWANGA

$
0
0
Mhe. Charles Kitwanga ( Mb) Naibu Waziri, Nishati na Madini akizungumzia namna Tanzania inavyotekeleza Mkakati wa Nishati Endelevu kwa Wote (SE4All) wakati wa Mkutano wa siku Mbili wa Mawaziri wa Sekta ya Nishani, uliofanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini ambao wamefuatana na Naibu Waziri katika mkutano huu muhimu uliojadili kwa kina nafasi na umuhimu wa nishati endelevu kwa wote katika kusukuma mbele malengo ya maendeleo endelevu , ukuaji wa uchumi, maendeleo ya jamii na utunzaji wa mazingira.
Mhe. Kitwanga akiteta jambo na Mwakilishi wa Bank ya Maendeleo kwaajili ya Afrika AfDB muda mfupi mara baada ya Naibu Waziri kuzungumza , mkutano huu wa SE4All, pamoja na Mawaziri wa sekta husika umewashirikisha pia wadau mbalimbali wakiwamo wakuu wa vyombo vya fedha kama vile Bank ya Dunia, AfDB na wataalamu wengine wakiwamo pia wanamziki maarufu ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakichagiza na kuwekeza katika nishati endelevu.

SHULE HATARINI KUANGUKA

$
0
0
Na John Gagarini, Globu ya Jamii - Chalinze

WANANCHI wa Kijiji cha Mkoko wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wameiomba Halmashauri kubomoa baadhi ya madarasa ya  shule ya Msingi Mkoko ambayo yananyufa na yako hatarini kuanguka hivyo kufanya wanafunzi kusoma kwa hofu.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo hivi karibuni Muhsin Mkumbi alisema kuwa majengo hayo yako kwenye hali mbaya na wakati wowote yanaweza kuanguka na kuleta madhara.

Mkumbi alisema kuwa madarasa hayo ni mabovu sana na hayastahili kutumika kutokana na ubovu wake hivyo ni vema Halmashauri ikayabomoa na kuyajenga upya ili kuepuka madhara ambayo yanaweza kutokea.

“Madarasa hayo yameharibika sana na yataanguka wakati wowote hivyo tunaiomba halmashauri iyabomoe kwani ni hatari kwa wanafunzi na walimu wanaofundisha shule hiyo, hali ni mbaya sana tunaomba hatua madhubuti zichukuliwe,” alisema Mkumbi.

Alisema kuwa hata baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakiogopa kwenda shule kutokana na hali hiyo ya ubovu wa madarasa hayo ambayo yamewekewa na miti kuyazuia ili yasianguke na tunawasiwasi kwani yakianguka yataleta tatizo.

Kwa upande wake ofisa elimu wa kata ya Msata Rajab Msakam alikiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa madarasa mengi yana nyufa kutokana na ardhi ya eneo hilo ujenzi wake kuwa mgumu kwani inapasuka na kusababisha nyufa.

Msakamali alisema kuwa talipeleka jambo hilo sehemu husika ili kuangalia namna ya kuikabili hali hiyo ambayo inahatarisha usalama wa wanafunzi pamoja na walimu wanaofundisha madarasa hayo yenye nyufa.

Naye Mbunge wa Jimbo hilo Ridhiwani Kikwete alisema kuwa tayari suala hilo limepelekwa halmashauri na kinachosubiriwa ni kibali kwa Kijiji kwa ajili ya kuvunja madarasa hayo ambayo yanahatarisha usalama wa wanafunzi na walimu.

Smart Codes Revamped website nominated for 2015 Awwwards again.

$
0
0
Smart Codes now a full service digital company has been nominated again in the 2015 Awwwards from awwwards.com as one the best website around the world.  www.smartcodes.co.tz  has been placed in a queue to appear as “Site of the Day”. If successful, it will also be included in Awwwards book "The Best 365 Websites Around The World" in 2015. The awwwards Team pointed out that, Smart Codes site will be fully checked and tested by their submission team, and then posted in their nominees section and will be evaluated over 7 days by their international jury and Awwwards’ users.  If the submission (Smart Codes site) is awarded a high score will be the best 365 website around the world in 2015.
Smart Codes team is thrilled by being given this honor for the second time. Being nominated again as the best site from Tanzania, we hope to present our country well in this prestigious award. At Smart Codes we believe that “Technology is for Everyone” and therefore we are excited by this and we will strive to make our tagline (Technology for Everyone) more so.

You can vote for Smart codes by clicking VOTE here: http://www.awwwards.com/best-websites/smart-codes-1/

MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU(AfCHPR) YASIKILIZA KESI YA WATUHUMIWA 10 WA UJAMBAZI MOSHI

$
0
0
Majaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu (AfCHPR) wakiingia Mahakamani kusikiliza kesi ujambazi iliyofunguliwa dhidi ya watuhumiwa 10 raia wa Kenya walioufanya mwaka 2006 mkoani Kilimanjaro.
Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu (AfCHPR), Jaji Augustino Ramadhani akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Arusha na kutoa wito kwa nchi zaidi kutoa tamko kwa Mahakama hiyo ili wananchi na asasi za kiraia kuitumia Mahakama hiyo, nchi saba pekee ikiwemo Tanzania zimetoa tamko hilo.
Wanafunzi wa Shule ya mchepuo wa kiingereza ya St Jude ya mkoani Arusha wakiwa katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu (AfCHPR)wakisikiliza mwenendo kesi ikiwa ni sehemu ya masomo yao.

Hotuba ya Rais Kikwete kwenye Mkutano wa Open Government Partnership

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images