Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 844 | 845 | (Page 846) | 847 | 848 | .... | 3285 | newer

  0 0


  Na Faustine Ruta,Bukoba

  Katika kutengeneza ajira kwa vijana na kuuendeleza mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kutoka sehemu mbalimbali na ndani ya mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa Bw. Nassor Mnabila aliamua kuanzisha timu ya mpira ya mkoa wa Kagera. 

  Madhumuni ya kuanzisha timu hiyo ni kuuleta mkoa wa Kagera pamoja, kutoa ajira kwa vijana wenye vipaji vya michezo aidha kuutangaza mkoa nje na ndani ya nchi kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana ndani ya mkoa wetu wa Kagera. 


  Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Nassor Mnambila mara baada ya kuanzisha timu hiyo ambayo kwa sasa inajulikana kama RAS Kagera Football Club na kuiwezesha kushiriki ligi daraja la nne na daraja la tatu na kufuzu kushiriki ligi daraja la pili ngazi ya Kanda katika kituo cha Mbulu mkoani Manyara . 
  Kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa mkoa wa Mkoa wa Kagera hasa wapenda michezo na maendeleo ya mkoa wa wameweza kuichangia timu hiyo ili kushiriki ligi daraja la pili ngazi ya Kanda na kama ikifuzu itaweza kushiriki ligi daraja la pili ngazi ya taifa. 


  Ushiriki wa timu hiyo unahitaji michango ya wadau kwani ni timu ya mkoa inayouwakilisha mkoa wa Kagera wadau walioweza kuichangia timu hiyo ni pamoja na Wadau wa maendeleo toka Dar es Salaam pamoja na Wadau wa maendeleo waliopo mkoani hapa. 

  Aidha wanasiasa hawakubaki nyuma ambapo Mbunge wa Bukoba Vijiji Mhe. Jasson Rweikiza naye ameichangia kiasi cha shilingi 300,000/- na Mbunge wa Meleba Kaskazini Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Charles Mwijage leo tarehe 20/05/2015 ameichangia timu hiyo shilingi 1,000,000/- 
  Wadau wote wa maendeleo wa mkoa wa Kagera mnaombwa kumuunga mkono Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera ili kufanikisha adhima yake ya kuuendeleza mkoa huu hasa katika sekta ya michezo. Aidha kwa wote wenye nia na mapenzi mema ya kuichangia timu hiyo wananweza kuonana na Mwenyekiti wa kamati ya muda Bw. Seif Hssein Katibu Tawala Msaidizi upande wa Miundombinu Ofisi ya Mkuu wa mkoa Kagera.

  0 0

  Mkuu wa Kitengo na Uhusiano na Uhamasishaji cha Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati mamlaka hiyo, ilipokuwa ikitoa ufafanuzi kuhusu kanuni No. 13 ya mafao ya wastaafu. Kulia ni Ofisa Mwandamizi Tafiti, Tathmini na Sera wa SSRA, Joseph Mutashubilwa. 
  Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ngabo Ibrahim, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati mamlaka hiyo, ilipokuwa ikitoa ufafanuzi kuhusu kanuni No. 13 ya mafao ya wastaafu. Katikati ni Mkuu wa Kitengo na Uhusiano na Uhamasishaji SSRA, Sarah Kibonde na kulia ni Ofisa Mwandamizi Tafiti, Tathmini na Sera wa SSRA, Joseph Mutashubilwa.
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria kwenye mkutano huo, wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo na Uhusiano na Uhamasishaji cha Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde, alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu kanuni No. 13 ya mafao ya wastaafu jijini leo.


  0 0

  Na Mwandishi Maalum, New York 
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe.Charles Kitwanga ( Mb), ni miongoni mwa mawaziri kutoka mataifa mbalimbali duniani wanaohudhuria mkutano wa kila mwaka kuhusu Nishati Endelevu kwa Wote (SE4All) 
  Mkutano huu unafanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, ambao siku ya jumatano mawaziri wameanza kujadili na kubadilisha uzefu kuhusu eneo hilo la nishati ambalo linaelezwa kuwa ni muhimu kwa maendeleo endelevu kijamii, kiuchumi na mazingira . 
  Mhe. Kitwanga ambaye anatarajiwa kuelezea msimamo wa Tanzania katika eneo hili la nishati endelevu siku ya alhamisi ( leo). Ameambatana na Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Ngosi Mwihava pamoja na wataalamu mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Madini. 
  Akifungua mkutano wa Mawaziri, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson, amesema mkutano huo wa mawaziri na ambao ulitanguliwa na mijadala mbalimbali iliyofanyika nje na Makao Makuu, kuwa Mawaziri hao wanakutana katika wakati muafaka na hasa kwa kuzingatia kwamba mwaka huu wa 2015 ni muhimu sana kwa Umoja wa Mataifa na Nchi wanachama. 
   Akasema , viongozi wa dunia wametambua kwamba, njia sahihi ya kufikia mafanikio ya pamoja sasa na baadaye ni kuwa na uwiano uliosawa kiuchumi, kijamii na kimazingira. Naibu Katibu Mkuu, ameongeza kuwa kwa muda mrefu, jumuiya ya kimataifa imekuwa ikifuata njia za ukuaji wa pamoja pasipo kuheshimu mipaka baina ya mazingira ya dunia na haja ya kuishi kwa kuzingatia uwiano bora na viumbe wengine. 
   Na kwa sababu hiyo, Bw. Jan Eliasson amewaeleza Mawaziri hao na wadau wengine wanaoshiriki mkutano huu kuwa, mwaka huu Jumuiya ya Kimataifa itakuwa na mikutano mitatu muhimu na ambayo itatoa mwelekeo mpya na ajenda mpya kuhusu maendeleo endelevu kwa wote. Ameitaja mkutano hiyo mitatu na muhimu kuwa ni  Mkutano utakaofanyika mwezi Julai Addis Ababa, Ethiopia, mkutano ambao dhumuni lake kuu litakuwa ni kujadili na kukubaliana kuhusu mfumo wa fedha kwaajili ya utekelezaji wa maendeleo endelevu. Mkutano wa pili ambao ameutaja ni ule utakofanyika mwezi Septemba hapa New York, mkutano ambao Wakuu wa Nchi na Serikali watapitisha ajenda na malengo ya Maendeleo Endelevu baada ya 2015. 
  Aidha mkutano wa tatu ni ule utakaofanyika Jijini Paris, Ufaransa mwezi Desemba, ambapo makubaliano yanatarajiwa kufikia kuhusu mabadiliko ya Tabia Nchi. 
  Akizungumzia kuhusu nishati endelevu, Naibu Katibu Mkuu, ameeleza kwamba Nishati endelevu ndio msingi mkuu wa maendeleo na mageuzi katika sekta zote ziwe za viwanda, kilimo au ustawi wa jamiii na kuongeza kuwa katika dunia ya sasa ambayo inakabiliwa na changamoto nyingi, ufumbuzi wa changamoto hizo unahitaji ushirikiano wa pamoja baina ya serikali, sekta binfasi na makundi mengine ya kijamii 
  Akasisitiza kuwa mpango kuhusu nishati endelevu kwa wote, umeonyesha kwamba ushirikiano miongoni wa wadau mbalimbali umeweza kusaidia kusukuma mbele ajenda hiyo ya nishati endelevu kwa wote. Ameongeza kuwa kizazi kijacho kitakichangaa kizazi cha sasa kwa kutoweka mipango madhubuti kwaajili yao. 
  Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Taifa akabainisha pia kwamba, Nchi zaidi ya 80 zinazoendelea zimejiunga mpango huo wa nishati endelevu kwa wote. Na kwamba Ahadi zenye thamani ya mabilioni ya dola tayari zimepatikana. Ripoti kuhusu kuhusu mchakato wa kuelekea nishati endelevu ambayo ilitolewa kwa washiriki wa mkutano huo Mei 18, inaonyesha kwamba watu 1.1 bilioni duniani kote wanaishi bila nishati ya umeme. 
   Huku karibu wengine 3 bilioni wakiendelea kupika kwa kutumia nishati ambazo si salama kwao na mazingira, nishati hizo ni pamoja na mkaa, kuni, mafuta ya taa na samadi.
  Nembo ya nishati endelevu kwa wote
  Naibu Waziri wa Nishati  na Madini, Mhe. Charles Kitwanga akiwa katika Ukumbi wa Mikutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, unapofanyika mkutano wa Mawaziri wa Nishati kutoka  mataifa mbalimbali duniani, mkutano ambao pia unawashirikisha wadau na wataalamu    wanaohusika  sekta ya  nishati.
  Sehemu  ya Wajumbe wa Mkutano wa Mawaziri kuhusu nishati,  mkutano ambao ulifunguliwa na   Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw.  Jan Eliasson. 

  0 0

  SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limeahidi kusaidia mapambano dhidi ya unyanyasaji na dhuluma zinazofanywa jamii dhidi ya watu wenye albinism. 
   Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Kiongozi wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues wakati akizungumza na mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo. 
   Mwakilishi huyo wa Unesco amesema hayo alipomtembelea Mkuu wa mkoa kumsalimia na kumweleza hatua zinazochukuliwana Unesco katika kukabiliana na ukatili dhidi ya watu wenye albinism. 
   Akifafanua zaidi alisema kwamba UNESCO haijatenga fedha zitakazotumika kuendesha kampeni mahsusi bali itatumia uwezo wa kiufundi uliopo kwa wataalamu walionao na kwamba wanakusudia kuona kwamba miaka 15 ijayo watoto wanaozaliwa nchini Tanzania wanakuwa huru pasipo na viashiria vya kuhatarisha maisha vinavyosababishwa na mauaji ya watu wenye albinism. Akimkaribisha Bi Zulmira ofisini kwake, Mkuu wa mkoa Magesa Mulongo alisema kwamba ingawa kuna utulivu katika kipindi hiki mkoani Mwanza, bado mkoa wake unaendelea kukabiliana na viashiria vinavyosababisha ukatili kwa watu wenye albinism na wazee. 
   Bwana Magesa alisema imani potofu zilizopo zinazosadikika kufanikisha biashara za uvuvi wa samaki, uchimbaji wa madini na wanasiasa kuendelea na madaraka ni miongoni mwa sababu kubwa za mauaji hayo yaliyoitia doa jeusi jamii ya kitanzania nje ya mipaka. Alisema kwamba jitihada zinafanywa kukabiliana na imani hizo potofu kwa kuihamasisha jamii kutoziamini na kwamba madaraka na utajiri unatokana na juhudi, kufanya kazi kwa bidii na si vinginevyo. 
   Aidha amesema mkoa wake umekuwa ukihakikisha kwamba makundi yanayotumika kuua watu wengine kwa kushirikisha jamii yanavunjwa na pia kuwachukulia hatua kali wote wanaobainika kushiriki kwa njia moja au nyingine. 
   Hata hivyo mwakilishi wa umoja wa mataifa alisema kwamba hali ya amani itatawala pale tu watu watakapobaini kwamba kuua ni ukiukwaji wa haki za binadamu na ni kosa la jinai. 
   Alisema pindi binadamu watakapokiri kwamba binadamu wote ni sawa na kuishi na albinism sio ‘mzimu’ watabadili mwelekeo mzima wa fikra potofu kimaisha na kuishi kwa amani na kuthaminiana. 
   Bi Zulmira alimwambia mkuu wa mkoa kwamba UNESCO kwa kushirikiana na wadau wengine wataendesha makongamano yenye lengo la kushirikisha jamii katika kuandaa na kutekeleza mikakati itakayo changia kuzuia na kutokomeza unyanyasaji na dhuluma zinazofanya dhidi ya watu wenye albinism.
  DSC_0369
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo akiendelea na maongezi na ugeni huo ofisini kwake jijini Mwanza.
  DSC_0377
  Kiongozi wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (kulia), akielezea nia ya Shirika lake kusaidia mapambano dhidi ya unyanyasaji na dhuluma zinazofanywa jamii dhidi ya watu wenye albinism nchini alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo ofisini kwake jijini Mwanza.

  0 0


  Na Faustine Ruta,
  Bukoba
  Katika kutengeneza ajira kwa vijana na kuuendeleza mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kutoka sehemu mbalimbali na ndani ya mkoa Katibu Tawala wa Mkoa Bw. Nassor Mnabila aliamua kuanzisha timu ya mpira ya mkoa wa Kagera. 
  Madhumuni ya kuanzisha timu hiyo ni kuuleta mkoa wa Kagera pamoja, kutoa ajira kwa vijana wenye vipaji vya michezo aidha kuutangaza mkoa nje na ndani ya nchi kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana ndani ya mkoa wetu wa Kagera. 
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Nassor Mnambila mara baada ya kuanzisha timu hiyo ambayo kwa sasa inajulikana kama RAS Kagera Football Club na kuiwezesha kushiriki ligi daraja la nne na daraja la tatu na kufuzu kushiriki ligi daraja la pili ngazi ya Kanda katika kituo cha Mbulu mkoani Manyara . 
  Kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa mkoa wa Mkoa wa Kagera hasa wapenda michezo na maendeleo ya mkoa wa wameweza kuichangia timu hiyo ili kushiriki ligi daraja la pili ngazi ya Kanda na kama ikifuzu itaweza kushiriki ligi daraja la pili ngazi ya taifa. 

  Ushiriki wa timu hiyo unahitaji michango ya wadau kwani ni timu ya mkoa inayouwakilisha mkoa wa Kagera wadau walioweza kuichangia timu hiyo ni pamoja na Wadau wa maendeleo toka Dar es Salaam pamoja na Wadau wa maendeleo waliopo mkoani hapa. 

  Aidha wanasiasa hawakubaki nyuma ambapo Mbunge wa Bukoba Vijiji Mhe. Jasson Rweikiza naye ameichangia kiasi cha shilingi 300,000/- na Mbunge wa Meleba Kaskazini Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Charles Mwijage leo tarehe 20/05/2015 ameichangia timu hiyo shilingi 1,000,000/- 
  Wadau wote wa maendeleo wa mkoa wa Kagera mnaombwa kumuunga mkono Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera ili kufanikisha adhima yake ya kuuendeleza mkoa huu hasa katika sekta ya michezo. Aidha kwa wote wenye nia na mapenzi mema ya kuichangia timu hiyo wananweza kuonana na Mwenyekiti wa kamati ya muda Bw. Seif Hssein Katibu Tawala Msaidizi upande wa Miundombinu Ofisi ya Mkuu wa mkoa Kagera.

  0 0

  Kama tangazo linavyojieleza, ni onyesho la kukata na shoka kati ya mfalme wa taarab Mzee Yussuf na malkia wa masauti Isha Mashauzi Juni 11 ndani ya jiji la Mwanza.


  Patakuwa hapatoshi ndani ya Villa Park pale wakali hao wanaokimbiza soko la taarab watakapoumana katika usiku wa Baba na Mwana.


  0 0

  Na Hassan Hamad, OMKR 
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ametoa wito kwa Watanzania kuwa waangalifu na kuendeleza amani iliyopo, ili Tanzania isije ikatumbukia katika migogoro na machafuko kama inavyojitokeza kwa baadhi ya nchi za Afrika. 
  Akifunga mkutano wa siku mbili wa mashauriano kuhusu amani na utulivu wa nchi huko ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Maalim Seif ambaye pia alikua mshiriki wa mkutano huo amesema Tanzania inahitaji mkakati wa pamoja katika kulinda amani iliyopo. Amesema Tanzania itazidi kung’ara katika ramani ya dunia, iwapo viashiria vya uvunjifu wa amani kuelekea uchaguzi mkuu vitadhibitiwa na kuifanya kuendelea kuwa nchi ya amani na ya kupigiwa mfano barani Afrika.
  Amewashauri washiriki wa mkutano huo ambao ni pamoja na viongozi wastaafu, viongozi wa taasisi za dini, vyama vya siasa na wazee, kuwa mabalozi wa kuyatangaza maazimio ya mkutano huo kwa wengine, ili jamii ielewe dhamira ya viongozi hao katika kuendeleza amani nchini. 
  Akisoma maazimio ya mkutano huo ulioandaliwa na taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Joseph Butiku amesema viongozi na wananchi wanapaswa kuelewa kuwa msingi mkuu wa amani unatokana na kuwepo kwa haki na usawa katika jamii. 
  Ameshauri kuwa ni vyema Serikali na taasisi za umma kuzingatia misingi ya demokrasia na utawala bora, na kutaka hatua zichukuliwe kwa wale watakaokiuka misingi hiyo. 
  Mapema akitoa maelezo ya mkutano huo kwa washiriki na vyombo vya habari, Butiku alitaja baadhi ya viashiria vya kuvunjika kwa amani kuwa ni pamoja na kutotendewa haki kwa wananchi katika utoaji wa vitambulisho vya ukaazi, kupuuza au kuikataa misingi ya usawa, migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji pamoja na tabia ya kutokutana kwa viongozi wakuu kujadili viashiria hivyo. 
  Viashiria vyengine ni pamoja na serikali kujiingiza kwenye mambo ya kidini, tabia ya viongozi kutozungumza matatizo ya Muungano kwa uwazi na kuyatafutia majibu na tabia ya baadhi ya vyama vya siasa kutovumiliana. Akitoa shukrani kwa niaba ya viongozi wa vyama vya siasa, Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Wilbroad Slaa, ameshauri kuchukuliwa hatua ziwezekanazo katika kuzuia machafuko yanayoweza kujitokeza. 
  Amesema Tanzania ni ya Watanzania wote, hivyo kila mmoja ana wajibu wa kushiriki na kuhakikisha kuwa Tanzania inabakia kuwa nchi ya amani wakati wote. 
  Awali washiriki wa mkutano huo walitahadharisha kuwa kutoweka kwa amani ni jambo rahisi lakini kuiresha baada ya kutoweka ni kazi ngumu inayoweza kuigharimu serikali katika Nyanja zote. 
  Hata hivyo baadhi ya viongozi hawakuweza kushiriki kwenye mkutano huo kutokana na dharura mbali mbali wakiwemo Marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Amani Karume, pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akifunga mkutano wa siku mbili wa mashauriano kuhusu amani na utulivu katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Bw, Joseph Butiku akizungumza katika mkutano wa mashauriano kuhusu amani na utulivu uliofanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya washiriki wa mkutano wa mashauriano kuhusu amani na utulivu, wakifuatilia mkutano huo.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiagana na Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania Mhe. Pius Msekwa, baada ya kumalizika kwa mkutano wa mashauriano kuhusu amani na utulivu jijini Dar es Salaam. Picha na Salmin Said, OMKR

  0 0

  1.USHAHIDI  WA  KUAMBIWA  NI NINI?

  Ushahidi  wa  kuambiwa  ni  ushahidi  unaotolewa  na  mtu  ambaye  hakuona  tukio  likitendeka,  hakusikia  tukio  likitendeka,  hakuhisi  wala  kuonja,  wala  kunusa  jambo  lililo mbele  ya  mahakama  kama  kosa  isipokuwa   aliambiwa    na  mtu  mwingine aliyeona,  kusikia, kuhisi, kunusa  au  kuonja.  
  Hapa  kuna  watu  wawili,  kwanza  aliyeona au kusikia , na  pili  yule  aliyeambiwa  na  huyu   aliyeona   au  kusikia .   Kwahiyo   katika maana  yetu    huyu   wa  pili  aliyeambiwa  na  wa  kwanza  aliyeona  au  kusikia   ndiye  mwenye  ushahidi  wa  kuambiwa.  Ni  kwa  maana  hii tunasema  huyu  wa  pili  aliyeambiwa  akienda  kutoa  ushahidi  wake  mahakamani    utaitwa  ushahidi  wa  kuambiwa.  Kwa  mfano  “A”  amemuona “ B”  akimuua  “C”.  “ A”  baada  ya  kuona  tukio  lile  akamwambia  rafiki  yake  “D”.  Ina  maana  “D”  hakuona  lolote  isipokuwa  ameambiwa  na  rafiki  yake  “A”  aliyeona. Kwa  maana  hii  ushahidi  wa  “D” ni  ushahidi  wa  kuambiwa.  Ameambiwa  na  nani,  ameambiwa  na  “A”  aliyeona  tukio.  Hii  ndio  maana  ya  ushahidi  wa  kuambiwa.  Kwa  jina  la  kitaalam  ushahidi  huu  huitwa “hearsay  evidence” .  Na  kwa  jina  jingine  la  mtaani  huitwa “ ushahidi  wa  nilimsikia  akisema”. 

  0 0


  0 0

   Hivi ndivyo hali ilivyo katika hili ni Daraja lilalounganisha eneo la Tandale na Mwananyamala jijini Dar es Salaam, ambapo wananchi wanaokaa maeneo ya jirani na Daraja hilo waliamua kukusanya viroba vilivyosheheni taka ngumu na kuwevilundika kwenye kingo za Daraja hilo ili kudhibiti maji yasiendelee kuchimba njia hiyo. Hali hii imekuja kutokana na mafuriko ya maji yaliyotokea hivi karibuni katika maeneo mengi hapa jijini kutokana na Mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha.

  Hali ilivyo katika mfereji unaopitisha maji katika eneo hilo baada ya kupitiwa na Mafuriko hivi karibuni.


  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu Mhe. Bahame Nyanduga akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya uchunguzi wa tuhuma dhidi ya Jeshi la Polisi za kuwapiga na kuwazalilisha Viongozi na Wafuasi wa CUF huko Mtoni Mtongani Temeke, Dar es sa Salaam.Picha na Eliphace Marwa-MAELEZO
  ---
  Na PIUS YALULA - MAELEZO
  TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imelaani vitendo vya uzalilishaji vilivyofanywa kwa Viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) Januari 27 mwaka huu (2015) wakati wa maandamano ya Chama hicho Mtoni Mtongani Wilaya ya Temeke.
  Akizungumza na waandishi wa habari leo (Mei 20, 2015) Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Bahame Nanduga, alisema uchunguzi wa tukio hilo umekamilika kwa kuzingatia kifungu cha 130[1][c],[f] na [g] cha katiba ya jamhuri ya Aidha aliongeza kuwa sheria nyingine zilizotumika kuchunguza tukio hilo ni pamoja na kifungu cha 6[1][c]na [g] vifungu 15[1][a] na 28[1][a],[b] na f vya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Na.7 ya mwaka 2001, sheria ya polisi na polisi wasaidizi, sura 322, na sheria ya vyama vya siasa, sura 258


  Nyanduga alisema Tume yake imebaini ukikwaji mkubwa wa haki za binadamu waliofanyiwa viongozi na wanachama chama cha wananchi CUF katika maandamano yao ya shughuli za kichama, hivyo Tume ilibaini kuwa jeshi la polisi lilitumia nguvu kupita kiasi, ukiukwaji wa misingi ya utawala bora na udhalilishaji wa wanachama wawili wa kike wa CUF.


  “Tume imetoa mapendekezo kwa jeshi la polisi  kuzingatia kanuni, sheria, haki za binadamu na misingi ya utawala bora katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku na kuhakikisha maafisa wake wanajipanga vyema katika kuratibu na kusimamia utekelezaji wa operesheni zake” alisema Nyanduga

  Kwa mujibu wa Nyanduga tume hiyo pia imewataka Viongozi na wanachama wa CUF kutafuta namna ya kuboresha mahusiano na jeshi la polisi, ili kuondoa mivutano isiyo na tija.Tume imepanga kuitisha mafunzo na mikutano mbalimbali kwa kushirikiana na vyama vya siasa,Tume ya Taifa ya Uchaguzi [NEC], pamoja na vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Polisi na Magereza, msajili wa vyama vya siasa, na asasi za kiraia ili kupanga taratibu zote katika kujua haki za binadamu na utawala bora.

  0 0

   Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akitoa maelezo ya taarifa zake muhimu wakati wa kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa Afisa Mwandikishaji Msaidizi Shaibu Chitala kwenye shule ya msingi Mbagala  Majengo B,jimbo la Mtama mkoani Lindi.
   Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitia saini wakati wa kukamilisha taratibu za kuandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ,Mtama mkoani Lindi.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akionyesha kadi yake mpya ya kupiga kura mara baada ya kumaliza kujiandikisha kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura Majengo B, Mtama mkoani Lindi.
  Picha na Adam Mzee.


  0 0  0 0


  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015

    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akielezea jambo wakati akifungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015


    Mkurudenzi Mtendaji wa taasisi ya Twaweza Bw. Brian Eyakuze akimkaribisha  Rais Jakaya Mrisho Kikwete kupokea tuzo maalumu ya taasisi zisizo za kiserikali kwake kwa kuwa kiongozi aliyetekeleza kwa vitendo masuala ya Serikali ya Uwazi na Ushirikiano. Hii ni wakati wa ufunguzi wa mkutano wa  siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
     Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Twaweza Bw. Brian Eyakuze akimkabidhi  Rais Jakaya Mrisho Kikwete  tuzo maalumu ya Asasi za Kijamii kwake kwa kuwa kiongozi aliyetekeleza kwa vitendo masuala ya Serikali ya Uwazi na Ushirikiano. Hii ni wakati wa ufunguzi wa mkutano wa  siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
  Kusoma hotuba ya JK BOFYA HAPA  0 0
 • 05/21/15--07:29: LOADING........

 • 0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ( Utawala Bora) Mh Kapt. (mstaafu), George Mkuchika akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa uwazi na kusikilizana kati ya Serikali na taasisi zisizo za kiserikali barani Afrika mkutano uliofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
    Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO, Assah Mwambene akichangia  kwa upande wa serikali kuwa serikali ya Tanzania ni sikivu, wakati wa mkutano wa Uwazi na usikivu katika mambo ya uchumi serikalini pamoja na taasisi zisizo za kiserikali  katika bara la Afrika.
   Mkurugezi wa kampuni ya Compass Communications Ltd,  Maria Sarungi akizungumza katika mkutano wa Uwazi na Usikivu  uliowakutanisha wadau mbalimbali kutoka bara la Afrika, mkutano hup umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
   Mkurugeni Mkuu wa TWAWEZA Aidani Eyakuza akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika kufunga mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali kutoka Bara la Afrika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
  Baadhi ya Wadau wa mkutano kutoka nchi mbalimbali  za Barani Afrika walihudhuria  mkutano uliofanyika  katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.

  Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

  Serikali na Taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali  Barani Afrika zimetakiwa kubadili maudhui yake kwa kuweka mipango ya  uendeshaji wa mambo yake kwa uwazi hasa kwenye sekta za uchumi.

   Hayo yamesemwa na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ( Utawala Bora) Mh Kapt. (mstaafu),George Mkuchika wakati akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali Barani  Afrika  kutoka serikalini na Taasisi zisizo za kiserikali,mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijijini Dar es Salaam leo.

  Mkuchika amesema kuwa,mkutano huo utasaidia sana endapo yaliyozungumzwa kwa siku mbili katika mkutano huo yatafuatwa na wananchi wataweza kujua mambo mbalimbali katika nchi zao, pia kila mwananchi ashiriki vyema kufanikisha malengo ya nchi.

  Pia kwa upande wa serikali amesema kuwa  serikali ikiweka mambo yake kwa uwazi pia inaweza kukosolewa, sio kila jambo inalofanya ni sahihi inahitaji kukosolewa ili kuleta maendeleo, pia wananchi waweze kufahamu nini kinaendelea katika nchi husika.

  0 0

  Kituo cha kuchakata na kuzalisha umeme kwa njia ya gesi cha Kinyezi I kimekamilika kwa asilimia 88 na kinatarajiwa kuzalisha umeme kuanzia Septemba mwaka huu.

  Hayo yalisemwa na Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima akiwatembeza katika kituo hicho wanajopo la ukaguzi wa miradi kutoka Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango walipotembelea mradi huo.   

  “Kazi zinazoendelea kwa sasa ni ufungaji wa mifumo katika mitambo; na njia za kusafirisha umeme msongo wa kV 220 kutoka Kinyerezi hadi Kimara na kV 132 Kinyerezi hadi eneo la viwanda la Gongolamboto, alisema Mhandisi Jilima.

  Tayari nguzo za kusafirishia umeme kutoka Kinyerezi mpaka Kimara zimeshasimikwa vivyo hivyo kwa upande wa Gongolamboto.

  Naibu Katibu Mtendaji  Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango,  Bibi. Florence Mwanri, alisema iwapo mradi huu utakamilika na kuanza kuingiza umeme wake katika gridi ya taifa ni dhahiri kuwa gharama za uendeshaji wa viwanda na uzalishaji wa bidhaa zitashuka, na pia kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje.

  “Katika miaka mitano ijayo mpango wetu wa maendeleo umejikita zaidi katika uchumi wa viwanda hivyo ni  vema ujenzi huu ukamilika kwa wakati ili kutoleta changamoto katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa mwaka 2016/17-2020/21” alisisitiza Bibi. Mwanri.

  Ili kuongeza uzalishaji wa nishati hiyo tayari Tanesco wameshanunua mitambo mingine mine ambayo itazalisha umeme kiasi cha kV 180.
  Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima (kulia) akitoa maelezo kuhusu hali ya maendeleo ya mradi kwa wanajopo la ukaguzi kutoka Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango, pichani ni Bibi. Florence Mwanri (Katikati), Ndg, Robert Masatu na Ndg. Aloce Shayo, kwa mfuatano.
  Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Jilima akimwonyesha Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango, Bibi. Florence Mwanri, eneo likatalojengwa kituo cha Kinyerezi II mara baada ya Kinyerezi I kukamilika.


  0 0

  Na Ali Issa - Maelezo Zanzibar 

  Jumla ya Shl. Milioni 370 za kitanzania, zinahitajika kwa ajili ya Ukarabati wa Jengo la Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi ulipo Wete Kisiwani Pemba.

  Kupatikana kwa Pesa hizo kutaiwezesha Serikali kuweka Samani na Vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuendeleza Shughuli za Baraza la Wawakilishi Kisiwani Pemba kama ilivyokuwa mwanzoni.

  Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud wakati akijibu Swali la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi Saleh Nassor Juma katika Kikao cha Bajeti kinachoendelea Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

  Amesema miaka ya nyuma kulikuwa na utaratibu wa kufanyika Vikao vya Baraza la Wawakilishi kwa mpangilio maalum baina ya Kisiwa cha Unguja na Pemba lakini kwa sasa utaratibu huo umeondoka.
  Amesema kukosekana kwa Vikao vya Baraza la Wawakilishi Pemba kumetokana na Ukumbi wa Baraza hilo uliopo Pemba kukosa Viwango vinavyohitajika.

  Hata hivyo Waziri Aboud amesema nchi nyingi Duniani Vikao vya Baraza au Bunge huwa vinafanyika pahala pamoja tu jambo ambalo ni tofauti na Zanzibar.

  Amesema licha ya tofauti hiyo bado Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaona ni vyema kuendeleza utamaduni wa kufanya Vikao vyake Unguja na Pemba hasa pale Ukumbi huo Utakapomaliza matengenezo yake.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meki Sadiki akiweka jiwe la msingi kwaajili ya uzinduzi rasmi wa tawi jipya na la kisasa la NMB Oysterplaza lililopo Oysterplaza jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NMB – Tom Borghols huku meneja wa tawi hilo Donatus Richard akishuhudia. Tawi la NMB Oysterplaza ni maalumu kwa wateja wakubwa na wa kati.Kufunguliwa kwa tawi hilo kunafanya mkoa wa Dar es salaam kufikisha matawi 26 ya NMB.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meki Sadiki akikata utepe kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa tawi jipya na la kisasa la NMB Oysterplaza lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NMB – Tom Borghols na kushoto ni Meneja wa tawi hilo - Donatus Richard na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam – Salie Mlay. Tawi la NMB Oysterplaza ni maalumu kwa wateja wakubwa na wa kati. Kufunguliwa kwa tawi hilo kunafanya mkoa wa Dar es salaam kufikisha matawi 26 ya NMB.
  Meneja NMB Kanda ya Dar es Salaam – Salie Mlay akiongea na wateja.


older | 1 | .... | 844 | 845 | (Page 846) | 847 | 848 | .... | 3285 | newer