Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 843 | 844 | (Page 845) | 846 | 847 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini 'Tanzania Bloggers Network' - TBN kilichosajiliwa rasmi na Serikali Aprili 2015 na kupewa namba ya usajili; S. A 20008 kinapenda kuwajulisha wanaotaka kujiunga na chama hicho kuwa fomu za kujiunga zinatolewa. Wahusika ni wamiliki na waendeshaji wote wa mitandao ya kijamii (blogs na forums) Tanzania na Watanzania wanaofanya kazi kama hiyo nje ya nchi.

  Sifa kuu kwa mwanachama ni kuwa na blog ambayo ina umri wa miezi sita tangu ianze kuendeshwa mfululizo ambayo ipo hai. Kwa wakazi wa Dar es Salaam wenye sifa na wanataka kujiunga na TBN fomu zinapatikana kwenye Ofisi za Muda za Tanzania Bloggers Network (TBN) kwenye Jengo la Dar Free Market lililopo mkabala na Barabara ya Ally Hassan Mwinyi.

  Mwanachama muitaji wa kujiunga kabla ya fomu atatakiwa kutoa shs 25,000/- ikiwa ni Kiingilio cha mwanachama, shs 15,000/- yakiwa ni malipo ya ada ya miezi mitatu kwa mwanachama na shs 10,000/- ikiwa ni malipo ya kadi ya TBN kwa mwanachama (utambulisho). Jumla kuu kila mwanachama anatakiwa kulipa shs 50,000/- na kupewa risiti halali ya malipo ya TBN. Fomu zitatolewa siku za kazi kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni. Zoezi la utoaji fomu litasimamiwa na Mweka Hazina wa TBN, Shamim Mwasha (0767418941). Fomu pia zinapatikana Ofisi za Michuzi Media Group, mjini Jengo refu karibu na Hospitali ya Ocean Road ghorofa ya pili. 

  Kwa wanachama wa mikoani juu na namna ya kujiunga wasiliana nasi kwa barua pepe; mushijoa@gmail.com  au  piga namba; 0756469470. 

  Kwa wanaoitaji kujiunga mnaombwa kuchukua fomu mapema kabla ya zoezi la usaji lililoanza 22 Aprili, 2015 halijafungwa.

  NB;- Kwa watakaohitaji katiba ya TBN watapewa pia ofisini coppy, lakini coppy hiyo wataigharamia wenyewe. Hata hivyo utaratibu unafanywa wa kuichapa kwenye soft coppy katiba hiyo na itatumwa mikoani kwa gharama za TBN. 

  Imetolewa na:
  Joachim Mushi, 0756469470 
  Mwenyekiti wa Muda wa Tanzania Bloggers Network (TBN)

  0 0

   Rais Wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma huku Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Spika wa Bunge hilo Mh.Anna Makinda wakisikiliza.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi,Waziri Mkuu Mizengo Pinda,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi waandamizi katika serikali ya Msumbiji wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Rais wa Msumbiji kulihutubia Bunge lao mjini Dodoma.
   .Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwa Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi wakati Rais huyo wa Msumbiji alipowasili katika makao makuu ya CCM m.Jakayajini Dodoma na kuzungumza na viongozi waandamizi .Kushoto ni Naibu katibu Mkuu wa CCM Bwana Mwigulu Nchemba.
   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania Mh.Anna Makinda akimkaribisha Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma ambapo Rais huyo alilihutubia Bunge hilo.
   Rais Wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akipokea heshima muda mfupi baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma akisindikizwa na mwenyeji wake Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
   Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo huku Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Spika Mhe.Anna Makinda wakishuhudia
  (Picha na Freddy Maro)

  0 0


  0 0


  0 0


  0 0

  Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Tanzania, Rukia Mtingwa akikabidhi cheti kwa Eddah Francis (kulia), mmoja wa wahitimu wa mradi wa Kuendeleza Vijana Kiuchumi Dar es Salaam katika mahafali yao yalifanyika Chuo cha ufundi stadi cha Future World, Gongo la mboto, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam leo. Kulia kwa Rukia ni Mkuu wa Future World, Robert Mkolla na Meneja Huduma za Jamii wa NBC, Irene Peter. Mradi huo umefadhiliwa na NBC kwa kushirikiana na Shirika la Plan International.
  Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Tanzania, Rukia Mtingwa akikabidhi cheti kwa Rasuli Mikidadi (kulia), mmoja wa wahitimu wa mradi wa Kuendeleza Vijana Kiuchumi Dar es Salaam katika mahafali yao yalifanyika Chuo cha ufundi stadi cha Future World, Gongo la mboto, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam leo. Kulia kwa Rukia ni Mkuu wa Future World, Robert Mkolla na Meneja Huduma za Jamii wa NBC, Irene Peter. Mradi huo umefadhiliwa na NBC kwa kushirikiana na Shirika la Plan International.


  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya (mwenye koti) akipata maelezo ya njia ya kutembea kwa miguu kutoka Kagunga hadi Mkigo kutoka kwa mkazi wa kijiji hicho, Mahmud Ahmad wakati alipokagua njia hiyo ili itumike kuwasafirisha waomba hifadhi ya ukimbizi wa Burundi, tarehe 17 Mei, 2015, (mwenye Kaunda suti ) ni Mkurugenzi Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen, Mbazi Msuya.
  Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya (mwenye koti) akiwa katika kijiji cha Kilemba kwa ajili ya kuwapokea waomba hifadhi ya ukimbizi wa Burundi waliokuwa wanasafirishwa kwa kutembea kwa miguu kutoka kijiji cha kagunga hadi kijijini hapo ili wapelekwe kambini (mwenye Kaunda suti ) ni Mkurugenzi Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen, Mbazi Msuya, Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Wananchi 24 KJ Kigoma, Luteni Kanali Donald Msengi (katikati) na Kaimu Katibu tawala wa mkoa wa Kigoma, Salvatory Shauri tarehe 17 Mei, 2015.
  Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya akiongea na vijana ambao ni waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi mara baada ya kuwapokea vijana hao walipofika kijijini Kilemba ili wapelekwe kambini baada ya kusafirishwa kwa kutembea kwa miguu kutoka kijiji cha kagunga tarehe 17 Mei, 2015.
  Baadhi ya vijana takribani 36 ambao ni waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi wakiwa wamepunzika kijiini Kilemba kabla ya kusafirishwa na basi kwenda kwenye kambini mara baada ya kusafirishwa kwa kutembea kwa miguu kutoka kijiji cha kagunga tarehe 17 Mei, 2015.
  Mkurugenzi Idara ya uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig.Jen, Mbazi Msuya akiongea na mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la kusafirisha wakimbizi, Son Ha Dinh, mara baada ya kuwasafirisha vijana takribani 36 ambao ni waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi kutoka kijiji cha kagunga, tarehe 17 Mei, 2015.

  0 0
 • 05/20/15--00:46: MoFLAVA ALL WHITE PARTY
 • WADAU WA TANZANIA WAISHIO USA ILE TOUR YA "MoFLAVA ALL WHITE PARTY" FT. TANZANIAN BORN & #1 USA INT'L VERSATILE DJ  "DJ KAYCEE MoFLAVA" SASA IMEWADIA. KAA TAYARI KWANI HIVI KARIBUNI THE PARTY WILL BE IN YOU CITY.  TAREHE ZA TOUR NI HIZI HAPA CHINI AND MORE WILL BE ADDED SOON! SO SAVE THE DATE FOR YOUR CITY OR CITY NEAR YOU. LETS ENJOY TOGETHER THIS SUMMER!
  MORE DATES & CITIES FOR MoFLAVA "ALL WHITE" USA TOUR:
  06/06/2015 CINCINNATI OHIO 
  O6/20/2015 DALLAS TEXAS W/ 
  07/11/2015 HOUSTON TEXAS 
  07/18/2015 MINNEAPOLIS MN 
  07/30/2015 COLUMBUS OHIO 
  08/01/2015 WASHINGTON D.C
  08/22/2015 WICHITA KS 
  09/05/2015 ANTLANTA GA 
  MORE DATES COMING SOON. 4 BOOKING CALL OR TXT 2812365204
  To listen to DJ Kaycee Moflava Mixes go to www.hulkshare.com/djkaycee

  0 0

  Zaidi ya watumiaji milioni 13 wa mtandao wa simu za mkononi kuanzia leo wataweza kuperuzi internet inayofikia MB100 kwa masaa mawili bure kuanzia saa 12 alfajiri hadi saa 2 asubuhi kutokana na ofa inayojulikana kama”Good Morning Tanzania” inayotolewa na Vodacom Tanzania.

  Promosheni hii imeanzishwa kutokana na kuonenakana kuwepo kwa mahitaji makubwa ya matumizi ya data katika kupata  taarifa kupitia mtandao wa intaneti.Vodacom Tanzania siku zote imekuwa mstari wa mbele kubuni huduma zinazoendana na matakwa ya wateja wake na kuwarahisishia maisha katika nyanja ya elimu,afya,Kilimo,burudani,huduma za kibenki na huduma nyinginezo  za kurahisisha biashara mbalimbali.

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hii leo,Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Kampuni hiyo Kelvin Twissa amesema “Kupitia promosheni hii ya ”Good Morning Tanzania” Vodacom tutawaunganisha wateja wetu na sehemu nyingine za dunia bure kila siku.Ofa hii  inawawezesha wateja wetu kufanya shughuli zao mapema bure kupitia mtandao wa intaneti ikiwemo kuwasiliana na marafiki,kupata habari mbalimbali za kitaifa na kimataifa na matumizi mengineyo mengi yanayoweza kufanyika kupitia kwenye mtandao wa internet.

  Promosheni ya ”Good Morning Tanzania”imeadaliwa mahususi kukidhi matakwa ya wateja wa Vodacom ili kuwarahisishia maisha na watanzania wametakiwa kujiunga na familia ya Vodacom  waweze kutumia  fursa hii kupata wakipendacho kupitia teknolojia ya simu  za mkononi.

  Ili kupata huduma hii mteja anachotakiwa kufanya ni kupiga namba *149*01# ambapo atapata maelekezo zaidi na kuanza kupakua na kuperuzi intaneti na kuweza kupata kwa urahisi anachohitaji akiwa ametulia nyumbani kwake.

  0 0

  MWAKILISHI viti maalumu wanawake CUF wilaya ya Chake Chake, Mhe. Salma Mohamed Ali (kulia) akimkabidhi dawa na vifaa tiba,   Daktari dhamana wa hospitali ya Chake Chake, Dk. Yussufu Hamad Idd vilivyotolewa na mwakilishi wa Jimbo la Chake chake, Mhe. Omar Ali Shehe, Mei 3 mwaka huu, kabla ya baadhi ya vifaa na dawa hizo kugunduilika kupitiwa na muda wake wa matumizi.
  BAADHI ya dawa na vifaa tiba zilizotolewa hivi karibuni na Mwakilishi wa Jimbo la Chake Chake, Mhe. Omar Ali Shehe ambazo tayari zimeshapitiwa na muda wake wa matumizi, ambapo uongozi wa hospitali ya Chake chake umezigundua wakati wakitaka kuzitumia.
  MFAMASIA mkuu wa hospitali ya Chake Chake Pemba, Dk.  Kassim Zahir akionyesha vipamba vya kusafisa damu baada ya kung’olewa jino, ambavyo navyo ni miongoni mwa vifaa tiba vilivyogundulika kupitiwa na muda wake, ambavyo vilitolewa hivi karibuni na Mwakilishi wa Jimbo la Chake Chake, Mhe. Omar Ali Shehe, pamoja na dawa nyengine.
  DAKTARI dhamana wa hospital ya Chake Chake Pemba, Dk.  Yussuf Hamad Idd, akitoa maelezo jinsi watakavyomkabidhi dawa na vifaa tiba Mwakilishi wa Jimbo la Chake chake, Mhe. Omar Ali Shehe ambaye hivi karibuni alikabidhi dawa hizo ambazo zimegundulika kupitwa na muda wake wa matumizi.(Picha na Haji Nassor, Pemba).

  0 0  0 0

  BG Tanzania imetangaza  kutoa udhamini kwa wanafunzi 13 wa shahada ya uzamili  ya sayansi ya mafuta na gesi (MSc. in Petroleum Geology) itakayotolewa katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Idara ya  Jiolojia  kwa mwaka wa masomo 2014/2015. Udhamini huu utahusisha malipo ya gharama za ada,  vitabu, pesa ya kijikimu na utafiti kwa muda wa miezi 18.

  Katika hafla ya  uzinduzi huu, Mgeni rasimi alikuwa  Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.  Mizengo Kayanza Pinda. Wageni wengine walio alikwa na kufika ni Waheshimiwa Mabalozi wa nchi mbalimbali, akiwemo mkuu wa jumuia ya nchi za Ulaya,  Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar e salaam, viongozi wa makampuni ya gesi na mafuta na wa wakilishi kutoka taasisi mbalimbali za Serikali.

  Ushiriki wa BG Tanzania unazingatia mpango mkakati wake wa muda mrefu wa kufanya kazi na kusaidiana na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na taasisi  za elimu ya juu katika kujenga uwezo na kuongeza utaalam kwa Watanzania kwenye shahada za juu za sayansi ya mafuta na gesi (MSc. in Petroleum Geology) lengo kuu ikiwa ni kuongeza fursa za ajira na utaalamu kwenye sekita za gesi na mafuta. Pia BG Tanzania, tangu mwaka 2012 imekuwa inatoa udhamini kwa ajili ya shahada ya juu vyuo vya nje na ndani ya nchi, hasa Uingereza. Wanafunzi 10 wamekuwa wanafaidika kupitia mpango huu kila mwaka.
  Mkuu wa Kampuni ya BG ukanda wa Africa Mashariki,  Ndugu, Derek Hudson, alisisitiza kuwa, mpango wa muda mrefu wa kampuni ya BG ni  kufanya kazi na serikali  pamoja na wadau wengine kuhakikisha watanzania wanahusika kikamilifu kwenye  sekta ya nishati na gesi.   Aliongeza kusema, BG Tanzania tunafurahi kuwa washirika na chuo kikuu cha Dar es salaam, hususani idara ya Geology.   Ushirikiano wetu utajikita katika kujenga uwezo  ili idara iwe na wataalam wakutosha kwa ajili ya kufundisha na kufanya tafiti mbalimbali za kisayansi.
  Alisisitiza kwamba, ushirika huu wa BG na Chuo Kikuu cha Dar es salaam utadumu kwa muda wa miaka minne katika maeneo  makuu matatu, (i) Udhamini wa wafanya kazi wa idara ya  Geolojia kufanya shahada ya uzamivu (PhD) chuo cha Aberdeen - Uingereza,  (ii) Udhamini wa wanafunzi 13, wanaofanya  shahada ya uzamili  ( MSc) elimu ya miamba na petrol ( Petroleum Geology) na  kugharamikia wakufunzi ( Professors) kutoka chuo cha Aberdeen -   Uingereza kuja kufundisha chuo kikuu cha Dar es salaam- idara  ya Geology.  Takribani dola milion mbili na nusu ($ 2.2m) zitatumika kwa muda wa miaka 4  katika  utekelezaji wa hiyo miradi mitatu.
  ​K​atika hafla hii, Mh. Balozi wa serikali ya Uholanzi, akihutubia,  alisisitiza ushirikiano endelevu wa sekta binafsi, hususani makampuni ya gesi na mafuta  pamoja na chuo kikuu cha Dar es salaam.
  BG Tanzania itaendelea kusaidia jitihada mbalimbali zinazohusiana na kujenga uwezo kwa taasisi na Watanzania kwa ujumla, hii itahusisha kuendelea kudhamini watanzania kufanya  shada za juu ndani nan je ya nchi.


  0 0

  WADAU WA TANZANIA WAISHIO USA ILE TOUR YA "MoFLAVA ALL WHITE PARTY" FT. TANZANIAN BORN & #1 USA INT'L VERSATILE DJ  "DJ KAYCEE MoFLAVA" SASA IMEWADIA. KAA TAYARI KWANI HIVI KARIBUNI THE PARTY WILL BE IN YOU CITY.  TAREHE ZA TOUR NI HIZI HAPA CHINI AND MORE WILL BE ADDED SOON! SO SAVE THE DATE FOR YOUR CITY OR CITY NEAR YOU. LETS ENJOY TOGETHER THIS SUMMER!
  MORE DATES & CITIES FOR MoFLAVA "ALL WHITE" USA TOUR:
  06/06/2015 CINCINNATI OHIO 
  O6/20/2015 DALLAS TEXAS W/ 
  07/11/2015 HOUSTON TEXAS 
  07/18/2015 MINNEAPOLIS MN 
  07/30/2015 COLUMBUS OHIO 
  08/01/2015 WASHINGTON D.C
  08/22/2015 WICHITA KS 
  09/05/2015 ANTLANTA GA 
  MORE DATES COMING SOON. 4 BOOKING CALL OR TXT 2812365204
  To listen to DJ Kaycee Moflava Mixes go to www.hulkshare.com/djkaycee  0 0

  Na Mwandishi Maalum
  Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu imeupongeza mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa yanayowahudumia wakimbizi kwa ubunifu wanaoufanya wa kusafirisha waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi. 
  Kutokana na zoezi linaloendelea mjini Kigoma la upokeaji waomba hifadhi hao, tayari waomba hifadhi wapatao elfu 90 wameandikishwa kuingia nchini kupitia kijiji jirani na Burundi cha Kagunga. 
  Hadi tarehe 15, Mei tayari waomba hifadhi wapatao elfu 21 walikuwa wamesafirishwa kwa meli hadi Kigoma mjini na baadae kusafirishwa kwa basi hadi katika kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu. 
  Kutoka kijijini Kagunga hadi Kigoma mjini usafiri unaoaminika ni usafiri wa majini. Meli ya Mv. Liemba ambayo hutumika kubeba abiria inaouwezo wa kubeba abiria wapatao 600. Mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na mashirika ya Kimataifa wameweza kutumia meli ya kukodi ya Mv. Malagarasi kwa ajili ya kubeba abiria yenye uwezo wa kubeba abiria wapatao 300. 
  Aidha, kwa kuzingatia idadi kuwa kubwa ya waomba hifadhi dhidi ya vyombo vya usafri salama vya majini vinavyotumika, tayari njia nyingine imebuniwa ya kutumia njia ya kutembea umbali wa km 10 kwa vijana wenye nguvu , kutoka kagunga hadi Kilemba ambapo husafirishwa na mabasi hadi katika kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu. 
  Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya akiongea hivi karibuni mara baada ya kuwatembelea waomba hifadhi hao waliopo kijijini Kagunga na kushiriki zoezi la kuwapokea waomba hifadhi hao mjini Kigoma wapatao 600 waliowasili kwa meli ya Mv. Liemba na kuwapokea wengine kijijini Kilemba wapatao vijana 36 waliosafirishwa kwa kutembea kwa miguu kutoka Kagunga, alisema kuwa kutokana na idadi ya watu waliopo kijijini hapo na vyombo salama vya usafiri wa majini vilivyomo mkoani humo ubunifu wa namna ya kuwasafirisha waomba hifadhi hao hadi kambini ni vyema ukapongezwa. 
  “Takwimu za uhamiaji za Kagunga zinaonesha kuwa hadi hivi sasa watu wapatao watu elfu 90 wamejiandikisha kuingia nchini kupitia mpaka uliopo hapa kagunga na kati ya watu hao watoto ni wapatao elfu 75 , ile hali kwa mujibu wa mtendaji wa kijiji hiki kuna wakazi wapatao elfu 17, kwa mantiki hii idadi hii ya watu ni kubwa ukilinganisha na uwezo wa kijiji hivyo ubunifu wa kutumia njia ya kusafirisha vijana wenye nguvu kutembea mwendo wa km 10, hadi Kilemba utapunguza idadi ya watu waliopo hapa na hatimaye tutakuwa nauwezekano mkubwa wa kuepuka magonjwa ya mlipuko kijijini hapo” alisema Afande Msuya.
   Aliongeza kuwa palipo na watu wengi yakilipuka magonjwa ya mlipuko ni maafa makubwa. Hivyo idara ya uratibu wa maafa nchini inaupongeza uongozi wa mkoa wa Kigoma unavyofanya zoezi hilo kwa kushirikiana na serikali ya kijiji cha kagunga , halmashauri za wilaya pamoja na mashirika ya kimataifa yanayowahudumia wakimbizi na Taasisi za kitaifa zinazowahudumia wakimbizi kwa kuwapokea waomba hifadhi hawa kwa kuhakikisha wanakuwa salama. Vilevile alifafanua kuwa lengo ni kuepusha maafa kwa waomba hifadhi na jamii ya kitanzania hivyo tayari wameshajadiliana na uongozi wa mkoa juu ya njia nyingine mbadala za kuharakisha usafiriishaji wa waomba hifadhi hao ambapo kwa kuwa njia hizo zinashirikisha wadau tofauti wenye mamlaka mbalimbali baada ya kuwafikishia mawazo hayo njia hizo zitaanza kutekelezwa mara moja ili kuepusha maafa yanayo weza kutokana na idadi kubwa ya watu waliopo Kagunga. 
  Awali, akiongea mara baada ya kuwapokea vijana wapatao 36 ambao ni waomba hifadhi ya ukimbizi waliotembea kwa miguu umbali wa km 10 kutoka kijijini Kagunga hadi kijijini Kilemba Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu, Issa Machibya aliwataka waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi hao kutii na kufuata sheria na kanuni wanazo elezwa na uongozi husika pindi wanapokuwa katika kambi watakazo hifadhiwa hapa nchini.
   Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya (mwenye koti) akipata maelezo ya njia ya kutembea kwa miguu kutoka Kagunga hadi Mkigo kutoka kwa  mkazi wa kijiji hicho, Mahmud Ahmad wakati alipokagua njia hiyo ili itumike kuwasafirisha waomba hifadhi ya ukimbizi wa Burundi, tarehe 17 Mei, 2015, (mwenye Kaunda suti ) ni Mkurugenzi Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen, Mbazi Msuya.
   Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya (mwenye koti) akiwa katika kijiji cha Kilemba kwa ajili ya  kuwapokea waomba hifadhi ya ukimbizi wa Burundi waliokuwa wanasafirishwa kwa kutembea kwa miguu kutoka kijiji cha kagunga hadi  kijijini hapo ili wapelekwe kambini (mwenye Kaunda suti ) ni Mkurugenzi Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen, Mbazi Msuya, Mkuu wa Kikosi  cha Jeshi la Wananchi 24 KJ  Kigoma, Luteni Kanali Donald Msengi (katikati) na Kaimu Katibu tawala wa mkoa wa Kigoma, Salvatory Shauri
   Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya akiongea na  vijana ambao ni waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi mara baada ya kuwapokea vijana hao walipofika kijijini Kilemba ili wapelekwe kambini baada ya kusafirishwa kwa kutembea kwa  miguu kutoka kijiji cha kagunga
   Baadhi ya vijana takribani 36 ambao ni waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi wakiwa wamepunzika kijiini Kilemba kabla ya kusafirishwa na basi kwenda kwenye kambini mara baada ya  kusafirishwa kwa kutembea kwa  miguu kutoka kijiji cha kagung
  Mkurugenzi Idara ya uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig.Jen, Mbazi Msuya akiongea na mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la kusafirisha wakimbizi, Son Ha Dinh, mara baada ya kuwasafirisha vijana takribani 36 ambao ni waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi kutoka kijiji cha kagunga

  0 0


  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuzindua rasmi uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura kwa kutumia mfumo wa kielektroniki wa (Biometric Voters Registration BVR) mkoani Kagera katika Manispaa ya Bukoba kesho tarehe 21/05/2015 kuanzia asubuhi saa mbili. 
  Zoezi la uzinduzi litaongozwa na Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella katika mtaa wa Pwani eneo la uwanja wa ndege wa Bukoba kata ya Miembeni Manispaa ya Bukoba. Uzinduzi huo utafanyika katika Halmashauri zote za wilaya siku hiyo ya kesho Halhamisi na kuanza uandikishaji rasmi katika mkoa wetu wa kagera. 
  Kulingana na ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uandikishaji wa wananchi katika mkoa wa Kagera utafanyika kwa siku 29 kuanzia hiyo kesho Mei 21, 2015 hadi Juni 18, 2018 ambapo maoteo ya uandikishaji ni wananchi 1,217,388 kwa mkoa wa mzima. 
  Wananchi wanaotarajiwa katika Halmashauri hizo ni 92,000 Bukoba Manispaa, Bukoba 148,033, Biharamulo 150,000, Karagwe 130,000, Kyerwa 150,000, Missenyi 144,600, Muleba 198,600 na Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ni 128,000. 
  Aidha vituo vya uanduikishaji vilivyoainishwa katika mkoa mzima wa Kagera nia 1,676 ambapo Bukoba Manispaa ni vituo 75, Halmashauri ya Bukoa 250, Biharamulo 140, Karagwe 217, Kyerwa 207, Missenyi 174, Muleba 395, na Halmashauri ya Wilaya ya Ngara 218. 
  Wananchi wa Mkoa wa Kagera wote wanaokidhi vigezo pia wenye umri wa miaka 18 wanahamasishwa kujitokeza katika vituo vitakavyokuwa katika maeneo yao kujiandikisha ili waweze kupata haki ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao mwezi Oktoba mwaka huu.

  0 0

  The Dar Choral Society and Orchestra proudly presents to you a classical music night. It will be a mass of peace to emphasize the importance of peace during the upcoming General Elections, which will feature a special performance of Karl Jenkins the armed man.
  Limited number of seats available for the night at the Dar es Salaam Serena Hotel on 24th May 2015, from 06:00 PM.
  Tickets are available at Serena Hotel, Epidor, Black Tomato, Best Bite & A novel idea (Slipway). Karibuni sana.
  This Sunday - A Classical Music Night by Dar Choral Society and Orchestra

  0 0

   Tanzania College Music Star ni shindano la kutafuta vipaji vya kuimba muziki wa kizazi kipya kwa wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania, Tumeanza na huu mchakato tokea mwezi wa 12 mwaka jana tumefanya audition mara mbili na tukapata top 5 kutoka vyuo vyote jijini mbeya. 
  Finali itafanyika wiki hii tarehe 23/05/2015 VibeMaishaClub Mbeya na kutakuwa na special appearance kutoka kwa mtangazaji na mjasiliamali maarufu Tanzania Kutoka Born2shine a.k.a Bdozen 
   Nelson kutoka Mbeya university of science and technology (MUST)
   Dinax Kutoka Teofilo Kisanji University (TEKU)
  Kutoka Mzumbe University Mbeya campus

  0 0

  Situated just off Kawawa Road (Kanisani Bus stop), near Facebook Restaurant. New Building – perfect for an NGO or Law Firm - away from the City Centre hustles!
  Electric Fence, Electric Gate, Beautiful Finishing, World class! 
  Call Charles on 0713 464646 for an appointment.   

  0 0


  0 0

  Ankal akiwa nje ya ukumbi ambao Bw. David Letterman, mtangazaji maarufu wa CBS ambaye leo anastaafu kazi baada ya miaka 33 jijini New York, Marekani. Huyu bwana ameshahojiana na watu  maarufu karibu wote duniani na kipindi chake cha David Letterman Show hakijapata mfanowe hadi sasa kiasi hata viongozi wa CBS wanajiuliza wafanyeje kumpata mtu kama yeye!

older | 1 | .... | 843 | 844 | (Page 845) | 846 | 847 | .... | 3283 | newer