Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 842 | 843 | (Page 844) | 845 | 846 | .... | 3283 | newer

  0 0
 • 05/18/15--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Christian Bella & Malaika Band - Nakuhitaji

  0 0

  Maisha Lab ya Uganda wametangaza kuwa warsha yao nyingine itafanyika Zanzibar wakati wa ZIFF 2015 mwezi Julai kuanzia tarehe 18 hadi 25. Maombi toka kwa wanaotaka kushiriki katika warsha hii yameanza kupokewa na mwisho wa maombi ni tarehe 13 Juni.

  Warsha za Maisha Lab zimekuza vipaji vya waandishi wa filamu na wakurugenzi wa filamu wengi hapa Afrika Mashariki. Tayari warsha hizo zimefundisha zaidi ya watu 1000 tangu Maisha Lab ianzishwe.

  Mkurugenzi wa Maisha Lab aliyeko Kampala Uganda alisema kuwa wanataraji kutoa skolaship 60 kwa wanafunzi kwa mwaka kwa washiriki toka nchi zote za Afrika Mashariki.

  “Katika warsha zetu watu 60 (15 toka kila nchi) watachaguliwa kuhudhuria mafunzo hayo yatakayoongozwa na wakufunzi waliobobea katika fani za uandishi wa filamu. Nia ni kuongeza  ujuzi na kupanuwa wigo wa biashara ya utengenezaji filamu hapa Afrika Mashariki.” Alisema Fibby Kioria Mkurugenzi wa Maisha lab.

  Katika kila Warsha script zitashindanishwa na mshindi atapatiwa $5000 ili kumwezesha kutengeneza filamu fupi katika mwaka unaofuata. Mwaka jana Nassir Qassim wa Tanzania ndiye aliyeibuka mshindi.

  Hii ni warsha ya 3 itakayofanyika Zanzibar na ZIFF ndio mdhamini wake ili kuwapa washiriki nafasi ya kushiriki katika tamasha na hivyo kuweza kukutana na watengeneza filamu wengine toka nje wanaokuja kwa ZIFF. Pia wanapata nafasi ya kuangalia filamu tele zinazoonyeshwa wakati wa Tamasha.

  Lakini Mkurugenzi wa ZIFF aliharakisha kusema kuwa anasikitishwa sana kuona kuwa washiriki toka Zanzibar huwa wachache kila mwaka. “Tunajuwa kuwa waandishi wa filamu toka zanzibar wanahitaji sana mafunzo haya maana yanawapa ujuzi na pia nafasi ya kujuana na watengeneza filamu wengine wa kimataifa”, alisema Mkurugenzi huyo

  Tasnia ya filamu ya Bongo Movies imesemwa sana kwa kuwa na hadithi dhaifu kimataifa. Kwa kutumia warsha kama hizi wadau wanaweza kukuza vipaji vyao na kufikia hadhi ya kimataifa.

  ZIFF mwaka huu imejitolea kuwasaidia wale wote ambao wangependa kutuma maombi yao ili kuwasaidia kufuata malekezo ya usaili, kuwapa miongozo ya uandishi wa skripti na kuwaongezea nafasi za kuchaguliwa kuhudhuria warsha hii muhimu. Wanaotaka kusaidiwa katika hili wanatakiwa kufika ZIFF, Ngme Kongwe Zanzibar, au kutuma maombi yao ya kusaidiwa kwa barua pepe workshop@ziff.or.tz


  Wanaotaka kujua zaidi kuhusu warsha hii waingie kwenye tovuti hii: www.maishafilmlab.org   au wawasiliane na fibby@maishafilmlab.org


  0 0


  0 0

  Familia ya  Bw. Uwesu Y.Mssumi wa Mbezi Beach Dar es Salaam inatoa shukurani za dhati kwa ndugu, jamaa, majirani na marafiki kwa   misaada ya hali na mali wakati  na maobolezo na  hatimaye mazishi ya mke wake mpendwa  Mwalimu  Hidaya U. Mssumi  ( mama ya Fatuma, Mwanana, Bibie na Mariam) kilichotokea  tarehe 27 April na kuzikwa tarehe 28 April, 2015.

  Shukurani za pekee ziwafikie wanajumuiya wa masjid Akram, Taqwa, Noor  na Fauz  Mbezi Beach, masjid Maamur- Upanga, Dr. Halid Gongoro, Ofisi za CCM Mkoa wa Pwani na  wilaya ya Rufiji,  Menejiment za kampuni ya Export Trading Group,  Mgodi wa Acacia North Mara, Chuo Kikuu Dodoma na Takukuru Mkoa Manyara bila kuwasahau wanafunzi waliomaliza shule ya msingi Muhimbili mwaka 1988.

  Haitakuwa rahisi kuwataja wote waliotusaidia na kushirikiana nasi ila kwa ujumla wenu tunawashukuru sana kwa  kutupa faraja wakati wa kipindi hiki kigumu.

  Tunawakaribisha na tunaomba tushirikiane nanyi katika arobanini ( Duah) ya kumwombea marehemu itakayofanyika tarehe 6 Juni, 2015 baada ya swala ya Adhururi ( saa saba mchana) . Duah hii itafanyika nyumbani Mbezi Beach kitalu J   plot na 229/30 mtaa wa Mufindi  (off Mwai Kibaki Road)  
  Inna Lilah waina Lilah Rajuhun.

  0 0


  0 0

   Kituo maarufu cha afya cha AAR Healthcare sasa kimehamia ghorofa ya pili katika jengo la Tropical Centre lililopo barabara ya New Bagamoyo road na Uporoto Street maeneo ya Victoria jijini Dar es salaam, kutoka mtaa wa Chato, na kinaendelea kutoa huduma zake bora kwa wananchi katika mazingira ya kisasa zaidi kila siku kwa kuanzia saa moja unusu asubuhi hadi saa mbili usiku.

   Muonekano wa jengo la Tropical Centre barabara ya Bagamoyo maeneo ya Victoria jijini Dar es salaam ambapo kituo cha AAR Healthcare kinapatikana hivi sasa katika ghorofa ya pili 
   Sehemu za ndani za kituo kipya cha AAR


  0 0

  Karibu kwenye sehemu ya kwanza kati ya mbili za mahojiano yetu na Katibu Uenezi na Itikadi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania. Ameeleza mengi akianza na Hali ya chama hivi sasa.KARIBU

  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akishirikiana na Wapigakura wake kushusha rola la Nyaya za umeme kwenye kijiji cha Luhana kata ya Luana wilayani Ludewa  jana kwa ajili ya mradi wa umeme  vijijini ambapo kijiji hicho pia kinatarajiwa kupata umeme  hivi karibuni.
   Mbunge jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akishirikiana na wapiga kura wake kushusha Transfoma jana kwa ajili ya kufungwa kwenye mradi wa umeme unaotekelezwa kwenye  kijiji cha Luana wilayani Ludewa mkoani Njombe. 


  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB,Bw.Edmund Mkwawa akipokea cheti cha kutambulika katika mafunzo ya Ukurugenzi wa benki hiyo. 
   Meneja Masoko wa benki ya DCB,Boyd Mwaisame(kulia) akipokea cheti cha utumishi wa muda mrefu na maendeleo ya benki ya DCB kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Mhe.Raymond Mushi.
   Baadhi ya wadau na wafanyakazi wa benki ya DCB wakiserebuka kwa pamoja katika hafla ya kukabidhi zawadi ya Mwenyekiti wa Bodi ya DCB kwa Tawi lililofanya vizuri kwa mwezi Julai hadi Desemba mwaka 2014.
    
  Na Bakari Issa.

  Wanahisa na wadau mbalimbali wametakiwa kuitumia kikamilifu benki ya DCB ili kuiwezesha kutimiza malengo ya kuanzishwa kwa benki hiyo.

  Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Mhe.Raymond Mushi katika hafla ya kukabidhi zawadi ya Mwenyekiti wa Bodi ya DCB kwa Tawi lililofanya vizuri kwa mwezi Julai hadi Desemba mwaka 2014.

  Katika hafla hiyo,Mhe.Mushi ameisifu benki hiyo ya DCB kutoa huduma zake kwa njia ya kisasa(Mtandao wa Intaneti) na kusema kuwa ni benki ambayo huduma zake ndiyo silaha kubwa katika ushindani wa mabenki.

  Pia,amewahimiza wafanyakazi na matawi ya benki hiyo kufanya kazi kwa ari na nguvu mpya ili waweze kufanya vizuri ili baadae wapate zawadi kama wafanyakazi wa tawi la Ukonga walioshika nafasi ya kwanza kwa asilimia 80 kwa mwaka 2014.

  Kwa upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo,Bw.Edmund Mkwawa amesema benki imepata faida ya Sh.3.7Bilioni kwa mwaka 2013 kutokana na ongezeko la matawi kama tawi la Kariakoo,Mabibo na Chanika.

  Hata hivyo,Mkwawa ameyataja matarajio ya benki hiyo kwa mwaka 2015,kuwa ni kuongeza amana kwa (33%),kuongeza mikopo kwa wateja pamoja na kutoa huduma bora naza haraka zaidi kwa wateja.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Selcom Tanzania, Sameer Hirji akimuonyesha mashine ya POS ya Selcom Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Mchechu. Mashine hizo zitatumika katika ulipaji wa kodi za majengo ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Selcom Tanzania, Sameer Hirji akielezea kwa waandishi wa habari jinsi huduma ya ulipaji kodi kwa njia ya Simu na akaunti za Benki inavyofanya kazi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Selcom Tanzania, Sameer Hirji akimuonyesha risiti za malipo ya pango za nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa malipo kwa njia ya mtandao wa Selcom.

  0 0


  0 0

  Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

  Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limesogeza mbele siku ya kufanya uchaguzi  wa Chama cha Mchezo wa Vinyoya Tanzania (TBA) ambapo unatarajiwa kufanyika Juni 10
  mwaka huu katika ukumbi wa Baraza hilo.

  Hayo yamesemwa na  Afisa habari Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Najaha Bakari wakati akizungumza na Mwandishi wetu kwa Njia ya simu.

   Pia Najaha amesema kuwa Baraza hilo linaongeza muda wa kuchukua na kurudisha fomu za Uchaguzi wa Viongozi wa Chama cha Mchezo wa Vinyoya Tanzania   (TBA) hadi  Juni 5 mwaka huu.

  Amesema kuwa Fomu zinapatikana ofisi za Baraza la Michezo na kwenye tovuti ya Baraza, gharama ya  fomu ni shilingi elfu 10,000/=,Amesema kuwa nafasi ya Mwenyekiti nafasi 1,Makamu Mwenyekiti nafasi 1,Katibu Mkuu nafasi 1,Katibu Mkuu Msaidizi nafasi 1,Mweka Hazina nafasi 1,Mweka Hazina Msaidizi nafasi 1na Wajumbe nafasi tano  wakuchaguliwa.

  0 0

  Mwenyekiti wa wasaidizi wa kisheria wilaya ya Monduli Mkoani Arusha, Ibramih Melita akizungumza na wafugaji wa kijiji cha Nanja kwenye mafunzo ya kujengewa uwezo wa kisheria yaliyotolewa na Chama cha wanawake wanasheria nchini (TAWLA) jana.
   Askari wa dawati la jinsia na watoto wa Mkoa wa Arusha, Baltazar Kitiku akizungumza na jamii ya wafugaji wa Kijiji Cha Nanja, Kata ya Lepruko Wilayani Monduli Mkoani humo, kuhusiana na kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia kwenye mafunzo yaliyotolewa na Chama cha wanawake wanasheria nchini (TAWLA) kwenye maadhimisho yao ya miaka 25.
   Jamii ya wafugaji wa Kijiji cha Nanja Kata ya Lepruko Wilayani Monduli Mkoani Arusha, wakiwasikiliza wanasheria wa Chama cha wanawake wanasheria nchini (TAWLA) Tawi la Arusha, ambao wameadhimisha miaka 25 ya kuanzishwa kwa chama hicho kwa kutoa elimu na ushauri wa kisheria jana kwenye vijiji vya Nanja na Meserani (Duka bovu) Wilayani Monduli.
  Baadhi ya jamii  ya wafugaji wa Kijiji cha Nanja, Kata ya Lepruko Wilayani Monduli Mkoani Arusha, wakiwasikiliza wanasheria wa Chama cha wanawake wanasheria nchini (TAWLA), ambao jana walitoa elimu na ushauri wa kisheria kwenye kijiji hicho.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku akizungumza katika Mkutano wakujadili Amani hapa nchini ulioandaliwa na Tasisi ya Mwalimu Nyerere leo jijjini Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu Mstaafu, Dk Salim Ahmed Salim akizungumza katika Mkutano wa Amani ulioandaliwa na Tasisi ya Mwalimu Nyerere leo jijjini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa akiteta jambo na Mwenyekiti wa chama cha Wananchi  Taifa (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi Taifa, James Mbatia wakiwa kwenye mkutano wa Amani ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu nyerere leo jijini Dar es Salaam.Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Katika jitihada za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuboresha huduma kwa wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja, leo Shirika la Nyumba la Taifa linazindua huduma mbili, ambazo ni kituo cha huduma kwa wateja na pili ni mfumo wa kulipa kodi za nyumba kwa kutumia simu ya kiganjani. 

  Kituo cha huduma kwa wateja kwa njia ya simu kitatumika kuhudumia wateja wetu wote kwa kupiga simu pale wanapohitaji kufahamu juu ya huduma zetu na bidhaa mbalimbali pamoja na kutoa taarifa mbalimbali za shirika zinazohusu huduma kwenye makazi yao. 

  Wateja wataweza kupata huduma hii kupitia nambari +255 784 105 200 na + 255 222 162 800. Kupitia kituo hiki Shirika linawaahidi kwamba maulizo na taarifa zozote zitakazoripotiwa zitapewa kipaumbele kwa kupatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

  Katika kuendelea kuboresha mfumo wa ukusanyaji kodi kutoka kwa wapangaji wetu, Shirika limeanzisha mfumo wa kulipa kodi kupitia simu za kiganjani ili wapangaji waweze kufanya malipo ya kodi zao bila ya usumbufu wowote kupitia tigopesa, mpesa na airtel money. 

  Kupitia mfumo huu, wapangaji wataweza kufanya malipo kwa kutumia simu zao na wataweza kuhamisha fedha kutoka kwenye benki akaunti zao na kwenda Shirika la Nyumba mahali popote walipo na kwa muda wowote ambao ni muafaka kwao bila ya kufika katika vituo vyetu vya makusanyo ya kodi.
  Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo cha huduma kwa wateja cha Shirika hilo uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo hicho kilichopo Makao makuu ya Shirika barabara ya Ufukoni na Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es salaam, Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari.
  Pichani ni baadhi ya waandishi wa habari wanaoshuhudia tukio hilo .
  Maofisa wa Shirika la Nyumba wanaokiendesha kituo hicho kipya cha huduma kwa Wateja wakiwa kazini mara baada ya kuzinduliwa, timu ya kituo hicho inaongozwa na mwanahabari Mzoefu Domina Rwemanyila.

  0 0

  AT1
  Mkuu wa mkoa wa Dar es slaam,Saidi Meck Sadiki(katikati) akiangalia athari ya maji yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni jijini Dar es slaam akiwa ameambatana na wakazi wa eneo hilo la Kunduchi Ununio.Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na DAWASA inaendelea na zoezi la kuyaondoa maji hayo pamoja na ujenzi wa mfereji mkubwa kuelekea baharini utakaokusanya maji kutoka Bunju na Kunduchi na kuyapeleka bahari ya Hindi.AT2
  Kazi ya ujenzi wa mfereji huo mkubwa wenye urefu wa kilometa 2.1 ikiendelea katika eneo la Kunduchi Ununio.AT3
  Maji yaliyotuama yakiwa bado yamezingira nyumba na makazi ya watu eneo la Boko jijini Dar es salaam ambayo harakati za kuyaoondoa zinaendelea kufanywa na manispaa ya Kinondoni.AT4
  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiki ( katikati ) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni Musa Nati wakati akikagua utekelezaji wa zoezi la kuondoa maji katika makazi ya watu eneo la Basihayo Tegeta.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  UKITAKA SHEREHE AMA SHUGHULI YAKO IPENDEZE BASI FANYA KAZI NA MC WA KISASA NA PIA HUDUMA ZA KISASA ZA USHEREHERESHAJI KWA UHAKIKA NA UFANISI WA HALI YA JUU MC KESSY NI MTU PEKEE AMBAE UKUMBINI ANASIMAMA YEYE NA PIA KWA UPANDE WA CAMERA NA MAMBO KADHA WA KADHA.
  ALIYOWEKA HAPO NI MOJA KWA MOJA UNAYAKUTA OFISINI KWAKE NA KUPEWA HAATA USHAURI WA BURE KUHUSU SHEREHE/TAMASHA AMA SHUGHULI YAKO KWA UTAALAMU WA KISASA NA WWA HALI YA JUU KABISA. 
   KARIBU UFANYE KAZI NA WAFANYAKAZI NA SIO KUFANYA KAZI NA WINGI WA WAFANYAKAZI BALI VYOMBO VYA KISASA NA UTAPENDA HUDUMA HIZI ZAIDI. WASILIANA NA MC MOJA KWA MOJA KWA HUDUMA HIZI


  0 0

  Na   Bashir    Yakub.

  Mara  nyingi  unapounda  kampuni   huwa  ni  lazima  kueleza  katika  zile  Memorandum  kuhusu  ukurugenzi  na  wakurugenzi.  Huwezi kusajili   kampuni  ikiwa  memorandum  zako  hazioneshi  lolote  kuhusu    hilo. 

  Kimsingi  nitaeleza  machache  japo  yapo   mengi kuhusu  ukurugenzi  na wakurugenzi  katika  kampuni.  Kwa  kampuni  zetu  ndogo ndogo  za  kijasiriamali  mara  zote  wakurugenzi  ndio  hao hao  wamiliki  na  ndio hao  hao  wana  hisa.  Niseme  mapema  tu kuwa si kosa  kuwa  hivyo  isipokuwa  yatupasa  kufahamu   kuwa  kuna  tofauti  kati  ya  wakurugenzi, wanahisa,  na  wamiliki.  

  Wakurugenzi  wanaweza  kuwa  watu  wa  kuajiriwa    na  wasiwe na  uhusiano  wowote  katika  umiliki.  Unakuta mtu ameajiriwa   tu  kama  mkurugenzi  kwa  ajili ya  kuendesha  kampuni  pengine  kutokana  na  elimu  yake,  uwezo  wake,  uzoefu  n.k.  Mwanahisa  naye anaweza  kuwa  mwanahisa  tu   na asiwe mkurugenzi  na  mmiliki  anaweza  kuwa   mmiliki tu  na asiwe  mkurugenzi.   Isipokuwa  tu mmiliki  lazima  awe  mwanahisa  kwasababu  hakuna  namna  ya  kufikia  kuwa  mmiliki  wa kampuni  bila  kuwa  mwanahisa. 

  Hivi  ni  vitu ambavyo  huwezi  kuvitenganisha. Mara  nyingi wanaotenganisha umiliki, ukurugenzi  na  uanahisa  ni  wenye  makampuni  makubwa.  Makampuni  yetu    madogo  ya  kufuga  kuku   mkurugenzi  ndiye  mmiliki  na  ndiye  mwanahisa.  Tutaona  baadhi  ya mambo   hapa   chini  kuhusu   ukurugenzi  wa  kampuni.

  1.NINI  MAANA  YA   MKURUGENZI.

  Sheria  ya  Makampuni  tunayotumia  hapa  nchini  imetoa  tafsiri  nyepesi  ya  maana ya  mkurugenzi  kwa  kusema kuwa mkurugenzi    ni  mtu  yeyote  ambaye   amepewa  nafasi  ya  ukurugenzi.  Sheria  hiyo  inasema  hivyo  kwa  kumaanisha kuwa  ili  umwite   mtu  mkurugenzi  au  hapana  itategemea  na    na  majukumu  anayotekeleza  katika  kampuni.  Ni  majukumu  tu  ndio  yatamtambulisha  mtu  kama  mkurugenzi.  

  Hii  ina  maana  yawezekana  mtu   akawa  anaitwa  mkurugenzi  lakini  hana  majukumu  ya  kiukurugenzi.  Kwa  tafsiri  hii  huyu   kisheria  sio  mkurugenzi.  Mwingine  yaweza   kuwa  anaitwa  mwenyekiti  lakini  akitekeleza  majukumu  ya  kiukurugenzi.  Huyu  kisheria  atatambulika  kama  mkurugenzi. Kwa  hiyo  kwa  kujibu  wa  tafsiri  hii  kumbe tunaona  kuwa   ukurugenzi  ni  majukumu  wala  sio  jina. 

  Pamoja  na hayo baadhi  ya  Mahakama   huko Wingereza  zimekuwa  zikitoa  tafsiri  mbalimbali  kuhusu  maana ya  ukurugenzi  ambapo  tafsiri  iliyokubalika  sana  ni ile  inayosema kuwa mkurugenzi  ni mtu  ambaye  ana  mamlaka  ya  kimwongozo,  kimaadili  na  kiutawala  katika  shughuli  zote  na  za  kila  siku  za  kampuni. 


  0 0

   Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya kimataifa la Ujerumani(GIZ)inayosaidia kujenga uwezo wa taasisi za Uongozi na Utawala bara la Afrika,Dk Iris Breutz akizungumza wakati wa semina ya siku nne ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutoka nchi za Afrika Mashariki namna Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu(AfCPHR) inavyofanya kazi zake leo jijini Arusha,kushoto ni Jenerali Ulimwengu ambaye ni mwezeshaji na Mkuu wa Mawasiliano wa AfCPHR,Chatbar Sukhdev.
   Mkuu wa Mawasiliano wa AfCPHR,Chatbar Sukhdev akitoa nasaha zake kwenye semina hiyo itakayowapa waandishi wa habari uelewa mpana wa Mahakama hiyo yenye makao yake jijini Arusha.
   Baadhi ya waandishi wa habari wakijifunza mambo mbalimbali yanayohusu kulinda Haki za Binadamu barani Afrika.
  Wawezeshaji wa semina hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari . 

  0 0

   SHEHA wa shehia ya Kipangani Ali Said Hamad akifungua mkutano wa kuelimisha katiba inayopendekezwa, ulioandaliwa na Kituo cha Hudma za Sheria Zanzibar ZLSC, tawi la Pemba, kulia ni Hakimu wa Mahakama ya Ardhi mkoa kusini Pemba Salim Hassan Bakar na kushoto ni Mratibu wa ZLSC Fatma Khamis Hemed
   MWANASHERIA wa serikali Albaghir Yakout Juma, akitoa ufafanuzi wa Katiba inayopendekezwa mbele ya wananchi wa wilaya ya wete Pemba, mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, ambao uliofanyika Jamhuri Hall wete Pemba
  MMOJA wa wananchi wa wilaya ya Wete akitaka ufafanuzi wa Ibara ya 97 juu ya ‘Bunge kumshitaki rais’ kwenye katiba inyopendekezwa, wakati Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC walipofika kutoa elimu ya katiba hiyo kwa wananchi gazi ya wilaya. Picha na Haji Nassor, Pemba

older | 1 | .... | 842 | 843 | (Page 844) | 845 | 846 | .... | 3283 | newer