Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live

RAIS WA MSUMBIJI FILIPE JACINTO NYUSI APATA MAPOKEZI MAKUBWA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais Kikwete akimpokea Rais Filipe Jacinto Nyusi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam . Rais huyo anayefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama rais wa Msumbiji yuko katika ziara rasmi ya siku tatu.
Rais Filipe Jacinto Nyusi akipokea shada la maua baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam . Rais huyo anayefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama rais wa Msumbiji yuko katika ziara rasmi ya siku tatu.
Rais Filipe Jacinto Nyusi akikagua gwaride la heshima baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam . Rais huyo anayefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama rais wa Msumbiji yuko katika ziara rasmi ya siku tatu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgteni wake Rais Filipe Jacinto Nyusi wakiangalia ngoma baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam . Rais huyo anayefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama rais wa Msumbiji yuko katika ziara rasmi ya siku tatu. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Video bofya mshale hapo

MZEE ALI MWINYI AISHUKURU WIZARA YA UJENZI NA WAZIRI MAGUFULI

Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) chatakiwa kuimarishwa kiushindani

$
0
0
Uongozi wa Mamlaka za Viwanja vya Ndege Tanzania wameshauriwa kuwa makini katika ujenzi unaoendelea wa jengo la kutua na kupaa ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyere (JNIA).

Ujenzi huo unaotarajiwa kuongeza uwezo wa uwanja wa mara tatu zaidi umejikita katika sehemu za maegesho ya magari, sehemu ya abiria kupumzika, sehemu za abiria kupandia na kushuka kwenye ndege, ofisi za uhamiaji na huduma zingine muhimu.

Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Suleiman S. Suleiman amesema kiwanja cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) hapo awali kilikuwa na uwezo wa kuruhusu ndege sita tu kutua kwa saa lakini kwa sasa unaweza kuruhusu ndege hadi 30. Tunatarajia kuongeza ndege zaidi na hivyo kuufanya kiwanja hiki kuhimili 2500 tofauti na abira 700 wa awali pindi ujenzi huu utakamilaka.
Mshauri Mkaazi wa ujenzi wa jengo la kufikia abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere akimwonyesha Naibu Katibu Mtendaji- Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Bibi. Florance Mwanri (Kulia) maendeleo mradi huo.

Kwa sasa ujenzi umefikia asilimia 85, katika awamu ya kwanza ambayo inategemewa kukamilika Juni mwaka 2016 na itakiwezesha JNIA kuhudumia abiria milioni tatu na nusu kwa mwaka. Iwapo ujenzi wa awamu ya pili utakamilika mwaka 2017 JNIA kitakuwa na uwezo wa kuhudumia jumla ya abiria milioni sita kwa mwaka.

Alipokuwa akitembelea mradi huo, Naibu Katibu Mtendaji- Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Bibi. Florance Mwanri, aliuambia uongozi wa Mamlaka hiyo kuzingatia wazo la kuwa na huduma zote za msingi katika kiwanja cha Julius Nyerere ili kuweza kushindana viwanja vya nchi jirani na barani Afrika kwa ujumla.
Mwonekano wa jengo la kushushia na kupandiashia abiria linaloendelea kujengwa katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

“Ni vema kuwa kiwanja chetu cha ndege kinapanuliwa ili kiweze kuhudumia watu wengi zaidi, lakini nimegundua kuna vitu muhimu vimesahaulika katika usanifu wa upanuzi huu, kuna vitu kama hoteli, jengo la hospitali, sehemu za kupata huduma za kibenki na pia namna nzuri ya kuwapatia abiria watuao usafiri wa kwenda mjini na sehemu nyinginezo, nadhani haya pia yazingatiwe, alisema Bibi. Mwanri.

MKUU WA MKOA WA NJOMBE AFUNGUA KIKAO KAZI CHA BIASHARA YA KILIMO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mh. Dk. Rehema Nchimbi akifungua kikao kazi cha biashara ya kilimo kwa kongani ya Ihemi iliyoandaliwa na SAGCOT (Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania) kwa ushirikiano na UONGOZI Institute (Taasisi ya Uongozi Afrika kwa Maendeleo Endelevu) mapema leo Iringa mjini. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Kilimo wa TCCIA Bi. Magadalena Mkocha, Mwenyikiti wa Bodi ya Agricultural Council of Tanzania Dk. Sinare Y. Sinare, DC wa Iringa Mh. Angeline Mabula, DC wa Mufindi Mh. Mboni Mhita na Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Philemon Luhanjo.
Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu, Philemon Luhanjo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa bodi ya UONGOZI Institute akitoa salaam kwa niaba ya taasisi hiyo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha biashara ya kilimo kwa kongani ya Ihemi inayoendelea Iringa mjini. UONGOZI Institute imeshiriki katika kuwezesha kikao kazi hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT, Bw. Geoffrey Kirenga akitoa utangulizi wa mada ya biashara ya kilimo kwa nyanda za juu kusini. Mkutano huu wa siku mbili unakutanisha viongozi wa serikalini, sekta binafsi, mashirika ya kimataifa pamoja na wakulima kwa ajili ya kujadili kuhusu kuboresha biashara ya kilimo nchini kwa nyanda za juu kusini.
Picha ya pamoja ya wageni waalikwa na washiriki wa kikao kazi cha biashara ya kilimo inayoendelea Iringa mjini. Mada zinazojadiliwa ni pamoja na wajibu wa viongozi katika kuleta mageuzi katika kilimo.

Kumbukumbu

Butiku Kufanya Mkutano na Viongozi Wakuu wakitaifa Kujadilia Amani na Umoja wa Taifa

$
0
0
Na Anitha Jonas – MAELEZO.

Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation imeandaa  mkutano wa mashauriano  unaotarajia kufanyika tarehe Mei 19-20 mwaka huu, ambapo watajadili mambo mbalimbali kuhusu amani na utulivu wanchi ya Tanzania.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi  Mtendaji wa  Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation Bw.Joseph Butiku alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es  Salaam kuhusu maandalizi ya mkutano  huo na agenda za  mkutano huo.

“Mkutano huu utahusisha viongozi wakuu wa Serikali  ikiwemo walioko madarakani na waliokwisha kustaafu,viongozi wakuu wa  Siasa na viongozi wa wakuu wa Dini na lengo kuu la kushirikisha viongozi  hao ni kutafakari na kujadili hali ya amani,umoja,na utulivu wanchi yetu kwa kuzingatia kuwa viongozi hao ndiyo wenye jukumu na wajibu wa kwanza wa kusimamia amani na umoja”,alisema Bw.Butiku.

Mbali na hayo Bw.Butiku aliendelea kusema mkutano huo utajadili hoja mbalimbali  ikiwemo masuala ya ukosefu ya ajira kwa vijana,kutoa ufafanuzi wa kuhusu Muungano,muongozo wa elimu kwa taifa letu pamoja na uanzishwaji wa vikundi vya ulinzi ndani ya vyama vya siasa.

Aidha hoja hizo ziliwasilishwa kwa wadau hao watakaoshiriki mkutano huo kwa ajili ya kutoa mapendekezo yao juu ya  hoja hizo na zaidi ya washiriki kumi na nne wametoa mapendekezo yao katika hoja hizo na zitakazojadiliwa
.
Kwa upande mwingine Bw.Butiku alisema muasisi  ya Mwalimu Nyerere  Foundation  Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alianzisha taasisi hiyo kwa lengo la kusimamia mwenendo wa amani na umoja kwa taifa na hivyo ndiyo maana wameandaa mkutano huo ilikujadili hatma ya taifa baada ya kuona uwepo kwa viashiria vinavyotishia amani na umoja. 

Hata hivyo mkutano huo unatarajiwa kuwahudhiriwa na viongozi mbalimbali wakisiasa na wadini akiwemo Bw.Ibrahimu Lipumba (CUF),Bw.Wilbroad Slaa (CHADEMA),Bw.James Mbatia (NCCR) na Katibu wa Chama cha Mapinduzi Taifa Bw.Abraham Kinana,Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Bw.Philip Mangula,Katibu Mwenezi (CCM) Bw.Nape Nauye na viongozi wa dini ni uongozi.

TPDC YAANZA UTAFITI TANGA

$
0
0
Mkurungezi wa Utafiti Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, Dkt. Emma Msaky, akizungumza na wataalam wanao endelea na uchimbaji wa visima vifupi katika Mradi Ujulikanao kama MP 10 GOMBERO DRILLING PROJECT kwa ajili wa utafiti wa mafuta na gesi kijiji cha Jihirini, wilayni Mkinga mkoani Tanga.
Mkurungezi wa Utafiti Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, Dkt. Emma Msaky, akionyesha sampuli za utafiti mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Mradi wa utafiti wa mafuta na gesi Ujulikanao kama MP 10 GOMBERO DRILLING PROJECT kijiji cha Jihirini, wilayni Mkinga mkoani Tanga.
Meneja wa Mradi wa MP 10 GOMBERO DRILLING PROJECT, Dkt. Amina Karega, akionyesha sampuli za utafiti mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kijiji cha Jihirini, wilayni Mkinga mkoani Tanga.

Na. Augustino Kasale - Kitengo Cha Mawasiliano-TPDC

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania limeanza utafiti wa mafuta na gesi eneo la Gombero, Wilayani Mkinga, Mkoani Tanga.

Mkurugezi wa Utafiti kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, Dkt. Emma Msaky, mwishoni mwa wiki alitembelea kujionea shughuli inayo fanya na Shirika hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari alioambatana naye Dkt. Msaky alisema kuwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), limeanza Mradi wa uchorongaji wa visima vifupi kumi (10) vya utafiti wa kijiolojia wa utafutaji mafuta na gesi katika vijiji mbalimbali mkoani Tanga ujulikanao kama MP 10 GOMBERO DRILLING PROJECT.  

MO AKUTANA NA RAIS FILIPE NYUSI WA MOZAMBIQUE JIJINI DAR

$
0
0
IMG-20150518-WA0054
CEO wa Makampuni ya MeTL Group na Mbunge wa Jimbo la Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji (kulia) katika picha ya pamoja na Rais wa Mozambique, Mh. Filipe Nyusi walipokutana jijini Dar es Salaam. Rais huyo anayefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama Rais wa Msumbiji yuko katika ziara rasmi ya siku tatu nchini Tanzania.

Mafuriko Dar es Salaam ni ushahidi wa athari za mabadiliko ya tabianchi

$
0
0
Mvua zinazoendelea kunyesha nakusababisha mafuriko na hasara kubwa jijini Dar es Salaam na maeneo mengine nchini zimetajwa kuwa ni moja ya ushahidi wa udhaifu wa miundombinu ya kweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ambayo ni janga kubwa duniani kwa sasa. Haya yalisemwa na FORUMCC; shirika linalijihusisha na masuala ya mabadiliko ya Tabianchi.

Watu zaidi ya 12 wameripotiwa kupoteza maisha mpaka sasa kutokana mafururiko hayo ambayo yameibua hisia na maswali mengi kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali wa mazingira wengi wakihoji nani wa kulaumiwa kutokana na mafuriko hayo.

Afisa Miradi, Fazal Issa kutoka shirika la ForumCC ameitaka serikali na watu binafsi kuchukua hatua thabiti katika kukabiliana na mafuriko haya ambayo yanasababishwa na mabadiliko ya tabianchi.

Alisema kuwa serikali na taasisi zake imekuwa na kawaida ya kuchukua hatua mara baada ya madhara kutokea badala ya kuweka mikakati ya muda mrefu ya kukabiliana na viashiria vya athari za mabadiliko ya tabianchi.

“Taasisi zenye majuku ya kutoa tahadhari na kushughulikia majanga hasa ya mafuriko, mamlaka zinazohusika na ujenzi wa miundombinu katika jiji la Dar es Salaam, ukusanyaji na utoaji wa taka zinapaswa kufanyakazi kwa kushirikiana ili kutafuta suluhisho la kukomesha maafa haya kabla hayajaleta athari kwa watu” alisema Issa.

Alisema hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwani utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini unaonyesha kuwa mvua kubwa zitaendelea kunyesha hadi Mei 20 mwaka huu, hivyo kuwataka wananchi kutotupa taka hovyo na kufanyia usafi mifereji katika maeneo yao.

“Badala ya kulalamika na kuhoji nani wa kulaumiwa kutokana na mafuriko yanayojirudia jiji la Dar es Salaam, ni jambo la busara sasa kwa kila mwananchi kuwajibika katika nafasi yake katika kuzuia au kupunguza kutokea kwa mafuriko hayo” alisema Issa.  

Kwa upande wake Afisa Habari wa ForumCC, Tajiel Urioh Aliwataka Watanzania kutambua kuwa mvua na mafuriko makubwa yanayoendelea kutokea Dar es salaam na maeneo mengine yanamahusiano mkubwa na ongezeko la Joto duniani.

“Watu wanapuuza na kuchukulia mzaha mabadiliko ya tabianchi lakini wanapaswa kujifunza kutokana na mafuriko haya ambayo mbali na kusababisha vifo pia yameharibu miundombinu ya barabara, nyumba, madaraja” alisema Urioh 

Tafiti zinaonyesha kuwa joto limeongezeka kwa 0.850C duniani huku kwa Tanzania Joto likiongezeka kwa 10C tangu mwaka 1961 jambo ambalo linasababisha baadhi ya maeneo kupata mvua zinazozidi kiwango na kuwa na majanga kama vile mafuriko, vimbunga na ukame. 

Hata hivyo, repoti ya Jopo la wanasayansi duniani (IPCC 2007) inaonyesha, ili kukabiliana na uharibifu unaosababishwa na mafuriko, inategemea sana na mipango thabiti ya mipango miji, jinsi ya kutumia ardhi, ubora wa kuweza kutabiri kutokea kwa mafuriko, utoaji taarifa na jinsi ya kuchukua hatua.

Mafuriko ya namna hii yaliyoleta athari kubwa ni yale yaliyotokea mwaka 2011 katika Jiji la Dar es Salaam na kusababisha vifo vya watu  arobaini (40) huku yakiharibu vibaya miundo mbinu ya barabara, madaraja na makzi ya watu.

Ushahidi wa upande wa Utetezi wa mshtakiwa wa pili, Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona kuendelea kusikilizwa na kesho

$
0
0
Ushahidi wa upande wa Utetezi wa mshtakiwa wa pili, Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona kuendelea kusikilizwa na kesho na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya leo mwenyekiti wa jopo la mahakimu wanaosikiliza kesi hiyo, Jaji John Utamwa kuwa udhudu wa kikazi.

Jaji Utamwa na Jaji Samu Rumanyika  walianza kusikiliza kesi hiyo wakiwa Mahakimu Wakazi Wakuu kabla ya kupanda na kuwa Majaji wa Mahakama Kuu Tanzania, ambao kwa sasa wako, Kanda ya Tabora.

Kesi hiyo iliahirishwa leo na jopo la mahakimu wawili Rumanyika na Hakimu Mkazi Mkuu, Saul Kinemela.

Pande zote mbili ziliridhia sababu hiyo na kesi hiyo itaendelea kusikilizwa utetezi wa Mshtakiwa wa pili Yona, hapo kesho.

Washtakiwa wengine ni,  Waziri wa zamani wa Fedha, Basil Mramba na Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja wote wanakabiliwa na kosa la matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7  kwa kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni tanzu ya Alex Stewart ( ASSAYERS) Government Business Corporation.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa kuwa, kati ya Agosti mwaka 2002 na Juni 14 mwaka 2004 jijini Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa umma kama mawaziri na katibu mkuu walitumia vibaya madaraka.

Ilidaiwa kuwa kwa kupitia kampuni ya Alex Stewart (ASSAYERS) ya Uingereza iliyoingia mkataba wa ukaguzi wa madini ambapo kwa kupitia kampuni tanzu ya Alex Stewart ( ASSAYERS) Government Business Corporation  waliingia mkataba kukagua kiwango cha uzalishaji wa madini ya dhahabu kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma.

NCCR-MAGEUZI WASHAMBULIA JIMBO LA VUNJO

$
0
0
Mwenyekiti wa kitengo cha kina mama Jimbo la unjo na Katibu wa Chama cha NCCR Mageuzi kata ya Kilema, Leah Mudy akizungmza wakati wa mkutano uliofanyika katika eneo la Lyamombikatika jimbo la Vunjo.
Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi jimbo la Vunjo ,Dauson Lyimo akizungumza katika mkutano huo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

RAIS WA MSUMBIJI AWASILI ZANZIBAR LEO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Msumbiji Mhe,Filipe Jacinto Nyusi alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume akiwa nchini kwa ziara ya kikazi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimtambulisha Rais wa Msumbiji Mhe,Filipe Jacinto Nyusi alipokuwa akisalimiana na Mawaziri wa Zanzibar mara alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume akiwa nchini kwa ziara ya kikazi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitambulishwa na Rais wa Msumbiji Mhe,Filipe Jacinto Nyusi aliposalimiana na Mawaziri mbali mbali wa Serikali ya Msumbiji walioungana na Rais Filipe mara baada ya mapokezi walipowasili katika uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume kwa ziara ya kikazi Nchini.

Maofisa wanane wa Benki Kuu Tanzania (BOT) kizimbani kwa mashitaka 14 ya kufoji vyeti vya kidato cha nne

$
0
0
Habari na Mwene Said 
wa Globu ya Jamii 
 Maofisa wanane wa Benki Kuu Tanzania (BOT) wamekutwa na kesi ya kujibu na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salam, dhidi ya mashitaka 14 ya kughushi na kuwasilisha vyeti vya kidato cha nne vilivyoghushiwa. 
 Uamuzi huo ulitolewa na Hakimu Mkazi Nyigulila Mwaseba baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi wao, dhidi ya washtakiwa Justina Mungai, Christina Ntemi, Siamini Kombakono, Janeth Mahengena Beatha Masawe, Jacquiline Juma, Philimina Mutagurwa na Amina Mwinchumu. 
 Hakimu Mwaseba alisema baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi wa Jamhuri bila kuacha shaka washtakiwa wana kesi ya kujibu na kwamba wanatakiwa kupanda kizimbani kujitetea dhidi ya mashitaka yao. 
Hakimu alisema kesi hiyo itaanza kusikilizwa utetezi wao Juni 16 hadi 17, mwaka huu. Watumishi hao wa Benki Kuu wanadaiwa kuwa katika kitengo cha kuhesabu fedha vya BoT. Mapema Septemba 19, mwaka 2008, upande wa Jamhuri uliwasomea washtakiwa hao mashitaka yao . 
Ilidaiwa kuwa siku isiyofahamika mwaka 2001, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Mungai alighushi cheti cha kidato cha nne, chenye namba S.342/43 kilichotolewa Februari 26, 1980. 
Aidha, ilidaiwa kuwa cheti hicho kilitolewa na Baraza la Mitihani la Taifa. 
Katika shtaka la pili, mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa siku isiyofahamika mwaka 2001, jijini, aliwasilisha cheti hicho huku akijua ni cha kughushi. 
Katika shtaka la tatu na nne, ilidaiwa kuwa siku isiyofahamika mwaka 2002 jijini, mshtakiwa wa pili alighushi cheti cha kidato cha nne chenye namba za usajili S.0222/42 kikionyesha kimetolewa Novemba 26, mwaka 1999 na kwamba aliwasilisha Benki Kuu. 
Katika shtaka la tano na sita, ilidaiwa kuwa siku isiyofahamika mwaka 2001 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Komakono, alighushi cheti cha kidato cha nne chenye namba za usajili S.238-0076 kilichotolewa Machi 14, mwaka 1997 akionyesha kuwa kimetolewa na Baraza la Taifa ambapo walikiwasilisha Benki Kuu. 
Upande huo wa Jamhuri uliendelea kudai kuwa katika shtaka la saba na nane, mshtakiwa wa Mahenge, anadaiwa kuwa alighushi cheti cha kidao cha nne, chenye namba za usajiliS.311/0071 kikionyesha kimetolewa Machi 14, mwaka 1997, na Baraza la Taifa ambapo aliwasilisha benki kuu. 
Aidha, shtaka la tisa na kumi, ilidaiwa kuwa siku isiyofahamika jijini, mshtakiwa Massawe, anadaiwa kuwa 2001 benki kuu, alighushi cheti cha kidato cha nne, chenye namba za usajili S.331/0071 kikionyesha kimetolewa Aprili 22, mwaka 2000, na Baraza la Taifa ambapo alikiwasilisha Benki Kuu. 
Ilidaiwa kuwa, shtaka la 11 na 12, mshtakiwa Juma, anadaiwa kuwa siku isiyofahamika mwaka 2000 jijini, alighushi cheti cha kidato cha nne chenye namba za usajili S.375/020 kikionyesha kimetolewa Machi 14, mwaka 1999 na Baraza la Taifa ambapo alikisilisha Benki Kuu. 
Pia, shtaka la 13 na 14, mshtakiwa Mutagurwa anadaiwa kuwa siku isiyofahamika mwaka 2002, alighushi cheti cha kidato cha nne, chenye namba za usajili S.0764/0012 kikionyesha kimetolewa Machi 14, mwaka 1997 na Baraza la Taifa ambapo alikiwasilisha Benki Kuu. Katika shtaka la 15 na 16, mshtakiwa Mwanchungu anadaiwa kuwa siku isiyofahamika, 2001 jijini, alighushi cheti cha kidato cha nne, chenye namba za usajili S.0307-004 kikionyesha kimetolewa Machi 28, mwaka 1991 na Baraza na Taifa, ambapo aliwasilisha Benki Kuu. Washtakiwa wote walikana mashtaka yao na wako nje kwa dhamana.

Burundi's President Pierre Nkurunziza makes first appearance since coup attempt - al Jazeera

Mapokezi ya Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi jijini Dar es salaam


SALAMU ZA SHUKRANI TOKA WAFANYE WATABASAMU

salsa in dar es salaam

$
0
0
Hi, thank you all who came to the opening it was great to see so many people interested in dance and exercise.
We are open to suggestions for our times please drop us an email :) 

Dance courses:
Salsa,  Belly dance, Bollywood,  Capoeira 
Are all 2 days a week courses for 15+ age, Price: 50$ a month
Modern African dance is with live drums, for 15+ age
 only drop in, Price:15,000tsh

Kidz hip hop, Kidz Capoeira (Brazilian Martial Arts) and Kidz Fusion ( a mixture of dance technique: Ballet, Jazz and contemporary with rotating cultural dances like african, latin, indian, etc.)
All are 2 day a week, according to age. Price 50$ a month
Exercise courses:
Power Yoga, Pilates, Kick boxing and Zumba 
Can be 2 days a week: Price 50$ a month
Can be 3 days a week: Price 80$ a month
Transform you is a holistic weight loss program that includes:
-Daily exercise (different type every day)
-Nutrition advice
-Diet coaching
Price 100$ a month (only exercise) or 250$ (for 2 months with coaching and nutrition advice)

TAARIFA MUHIMU - PASI YA KUSAFIRIA (TANZANIA PASSPORT)

$
0
0


Jumuiya inapenda kuwatangazia watanzania wa eneo la 'Washington State' na maeneo ya Idaho, Oregon, kujiandikisha kwa wingi wale wote wenye kuhitaji kuomba PASSPORT MPYA YA TANZANIA kama ifuatavyo:

Siku ya mwisho kujiandikisha ni Tarehe 5/6/2015 (June 5th, 2015)
Siku ya kuonana na Ofisa wa Uhamiaji kutoka Ubalozi wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania kwa ajili ya maombi hayo ni Tarehe 26/6/2015 - Taarifa ya pahala itatolewa rasmi..

Tafadhali wasiliana na wafuatao kujiandikisha rasmi:
Emil Muta - Mwenyekiti Tanzaseattle - simu - 206 291 8835
Haji Rajab Haji - Katibu Tanzaseattle - 206 302 9404

Au
Unaweza kutuma barua pepe (email) - Tanzaseattle @gmail.com
-
Ahsanteni sana.
Mkuu wa Kitengo cha Habari - Tanzaseattle.
A. DOLA - aka (Mayor of Seattle) - 206 422 3050.

WADAU WATAKA SERIKALI ZISIMAMIE UFUATILIAJI NA TATHMINI YA SDGs

$
0
0
Na Mwandishi Maalum, 
New York 
Mchakato wa ukamilishaji wa Malengo Mapya ya Maendeleo endelevu baada ya 2015 ( SDGs) umeingia katika hatua nyingine muhimu ambapo, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wanakutana hapa makao makuu ya UM wakijadiliana kuhusu mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya malengo hayo. 
Mkutano huo unaojadili aina ya mfumo wa ufuatiliaji na tathmini, utafanyika kwa siku nne na umeanza siku ya jumatatu kwa wajumbe kutoa mchango wa maoni na mawazo yao kwa kuzingatia rasimu iliyowasilishwa na wenyeviti- wenza wa mchakato wa majadiliano juu ya ajenda na malengo ya maendeleoe endelevu baada ya 2015. 
 Karibu wajumbe wote waliozungumza katika siku ya kwanza ya majadiliano haya, wametoa mapendekezo yao yanayotaka mfumo huo wa ufuatiliaji na tathmini uwe wa nama gani. Akizungumza kwa niaba ya Kundi la Nchi 77 na China ( G77&China) Mwakilishi wa Afrika ya Kusini amesema nchi zinazounda kundi hilo wangependa kuona kwamba mambo yafuatayo pamoja na mengine mengi yanazingatiwa katika eneo hilo la ufuatiliaji na tathmini. 
Baadhi ya mapendekezo ya G77na China ni mfumo wa ufuatiliani na tathimin uwe na upeo mpana na umilikiwe na nchi husika kwa kuzingatia mazingira yake, mahitaji yake na vipaumbele vyake. Kundi hilo limetaka pia ufuatiliaji na tathmini, eneo ambalo ni muhimu katika utekelezaji wa SDGs lazima uongozwe na kusimamiwa na serikali na uwe wa hiari uzishikisha Wizara mbalimbali na wadau wengine ambao wataonekana kuwa ni muhimu. 
Vile vile kundi la G77 na China limesisitiza haja na umuhimu wa kuhakikisha kuwa mfumo wa ufuatiliaji na tathmini unapaswa uwe ujumuishi na wenye uwiano ukizingatia pia ajenda namba 17 na malengo yote 169. 
 Kundi hilo la 77 na China pia limeleza kwamba ni kwa kupitia mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ndipo ambapo Umoja wa Mataifa utakuwa katika nafasi nzuri kutathmini utekelezaji wa ajenda za maendeleo baada ya 2015 ili kuhakikisha kwamba lengo kuu la malengo hayo ambalo ni kuondoka umaskini linafikiwa. 
Wachangiaji wengine wamesisitiza umuhimu wa uwazi, ushirikishwaji na uwajibikaji wa makundi yote zikiwamo Taasisi na mashirika ya Umoja wa Mataifa. Baadhi ya wazugumzaji wameeleza umuhimu wa matumizi sahihi ya takwimu, uwezeshwaji katika ukusanyaji wa takwimu hizo ikiwa ni pamoja na umuhimu wa ushiriki wa Asasi zisizo za kiserikali katika mchakato huo wa ufuatiliaji na tathmini. Wachangiaji wengine wamekwenda mbali zaidi kwa kutaka ushiriki na ujumuishi wa wananchi katika eneo hilo kwa kile wanachosema ili utekelezaji wa malengo hayo uwe wenye tija wananchi wanapashwa kuwa sehemu ya kufanya tathmini na kufuatilia kwa kuwa eneo kubwa la SDGs linahusu wananchi. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inashiriki kikamilifu katika majadiliano yote muhimu ya mchakato mzima maandalizi ya SDGs ambapo wawakilishi wa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Tume ya Mipango Tanzania Bara na Visiwani na Wawakilishi kutoka Asasi zisizo za Kiserikali wamekuwa wakihudhuria mijadala hiyo ikiwa ni pamoja na kusimamia maslahi ya Tanzania na Bara la Afrika katika ujumla wake. 
Aidha Tanzania Kupitia Mwakilishi wake wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi ni kiongozi wa majadiliano ( lead negotiator) kuhusu SDGs kwa Kundi la Afrika.
Sehemu ya Wawakilishi wa Nchi Wanachama wa Umoja wa  Mataifa katika siku yao ya kwanza ya mkutano wa siku nne unaojadili juu ya mfumo wa ufuatiliaji  na tathmini ya utekelezaji wa Maendeleo  Endelevu ya   Maendeleo baada ya 2015. Majadiliano  hayo ni  moja ya eneo muhimu kueleleka ukamilishaji wa  Mchakato wa  Ajenda na Malengo SDGs.  Mkutano huu unafanyika  hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Afisa Mkuu wa uwakilishi wa Kudumu wa  Tanzania  katika Umoja wa Mataifa, Bw. Songelael Shilla,  akizungumza wakati wa Mkutano wa pembezoni ( Side-Event) ulioandaliwa  kwa ushirikiano  kati  ya Uwakilishi na Asasi za Kimataifa,   kwaajili ya kubadilishana mawazo kuhusu nafasi za  Ki Kanda  na  Kitaifa katika  mfumo wa ufuatiliaji na  udhibiti,  fursa na  changamoto za  Malengo  ya Maendeleo  Endelevu baada ya 2015 kwa upande wa Afrika.

Sehemu wa Washiriki wa mkutano huo wa pembezoni ambapo washiriki  pamoja na mambo mengine walisisitiza haja na umuhimu wa wananchi kushirikishwa kikamilifu  katika eneo hilo la ufanyaji wa tathmini na  ufuatiliaji kwa kile walichosema malengo hayo ya  maendeleo endelevu yanawahusu wananchi  hiyo ushiriki wako ni muhimu
Sehemu wa Washiriki wa mkutano huo wa pembezoni ambapo washiriki 

UNESCO WATOA MAFUNZO YA TEHAMA KWA WALIMU WA VYUO VYA UALIMU

$
0
0
Godfrey Haongo mkufunzi kutoka Open University nchini Tanzania akitoa elimu ya njia ya mtandao.
 
 
Baadhi ya walimu wanaoshiriki mafunzo hayo.

Na Geofrey Adroph, 
Pamoja blog
UNESCO imeaandaa mafunzo ya uboreshaji wa elimu kwa walimu hususani katika somo la Tehama kwa vyuo mbalimbali vya hapa nchini vinavyotoa elimu ya ualimu. Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania yamefanyika  katika chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) ili kuweza kuwapa fursa hiyo waalimu wa vyuo mbalimbali katika ufundishaji na uelimishaji namna ya matumizi ya Tehama.
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live




Latest Images