Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 839 | 840 | (Page 841) | 842 | 843 | .... | 3270 | newer

  0 0

  MKUTANO Mkuu wa Dharura wa Wanachama wa Klabu ya Coastal Union unatarajiwa kufanyika kesho Mei 17 mwaka huu kwenye ukumbi wa Bwalo la Polisi mjini  Tanga.

  Sababu za Mkutano huo kufanyika katika Ukumbi la Polisi Mesi ni

  kutokana na makao makuu ya klabu ya Coastal Union kuendelea mchakato wa uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa na upigaji picha wananchikwa ajili ya vitambulisho hivyo.

  Akizungumza leo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga  alisema maandalizi ya mkutano huo yanaendelea vizuri na unafanyika kufuatia vikao vya maridhiano ya Uhakikiwa wanachama wa Klabu ya Coastal Union ulioongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la soka nchini (TFF) Ahmed Iddi Mgoyi.

  Ambapo alisema  baada ya kumalizika vikao hivyo,Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine aliiandikia barua Klabu ya Coastal Union akiiagizklabu hiyo kuitisha mkutano mkuu wa dharura wa wanachama tarehe 17 Meimwaka 2015.

  Alisema kuwa matokeo  ya maamuzi haya yamepatikana baada ya kikao chausuluhishi cha amani kilichoongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji yaTFF, Ahmed Iddi Mgoi aliyekuwa ameongozana na Makamu Mkurugenzi waSheria na Uanachama shirikisho la soka nchini (TFF) Eliud Peter Mvella kilichofanyika April 13 mjini hapa.

  Aidha alisema kuwa tayari shirikisho la soka nchini (TFF) ilishatuma

  orodha tatu za majina Wanachama stahiki,Wanachama waliobainika kuwawanadosari na inabidi wathibitishwe na wanachama stahiki.

  Orodha nyengine ni waombaji wapya wa  wa uanachama watakaohakikiwa nawanachama stahiki ambapo utaratibu huo ndio ulioagizwa kutumika .Hata hivyo alisema kuwa orodha zote zimekwisha kubandikwa kwenye ubao waMatangazo wa Klabu ya Coastal Union tayari kwa ajili ya mkutano huo wa kesho.

  Imetolewa na Kitengo cha

   Mawasiliano Coastal Union.

  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, limesema taarifa iliyoandikwa na Gazeti moja la tarehe 15, Mei 2015 yenye kichwa cha habari “Nkurunziza ameweka picha mbaya katika soka” haina uhusiano na TFF. 
   Katika taarifa hiyo katibu wa chama cha makocha nchini (TAFCA), Michael Bundala amenukuliwa akihusisha masuala ya mpira na hali ya kisiasa nchini Burundi. 
   TFF imesikitishwa na kauli hii na inajitenga nayo. Kwa kua aliyetoa kauli hii ni mwanafamilia ya mpira wa miguu nchini, uongozi wa TFF unafuatilia ili kujua ni hatua gani zichukuliwe.
   Jukumu la TFF ni kuendeleza na kusimamia maendeleo ya mpira wa miguu na si vinginevyo. 
   TFF inawatakia wananchi wa Burundi hususani familia ya mpira, amani, utulivu na baraka katika nchi yao. 

   IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA 
  MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0

  AutoSueco (VOLVO) Commercial Manager, Mr. Alen Nkya (right) clarifies a point regarding construction equipment, trucks and power generators to former President of Tanzania, Hon. Benjamin Mkapa (centre), Minister of Works, Dr. John Magufuli (left) and other delegates during Contractors International Conference in Dar es Salaam over the weekend.

  0 0

   Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi akisoma hotuba yake kabla ya kufunga rasmi mkutano wa Wadau wa Sekta ya ujenzi nchini uliondaliwa na Bodi ya Wakandarasi nchini CRB ikishirikiana na Bodi ya Wahandisi ERB pamoja na Bodi ya AQRB.
   Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akizungummza katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi (CRB) Eng. Consolata Ngimbwa akimkabidi zawadi mgeni rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi kama ishara ya kutambua mchango wake katika maendeleo ya sekta ya ujenzi nchini
   Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi akimkabidhi cheti cha ushiriki kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe kabla ya kufunga mkutano huo.
   Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Ujenzi
  Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na viongozi wengine akiangaalia moja ya vifaa vya ujenzi katika maonesho ya wadau wa sekta ya ujenzi nchini.


  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP)  Ernest Mangu, mara baada ya kuwasili katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano ya Dharura cha Polisi, iliyofanyika katika viwanja vya Kituo cha Kati cha Polisi,jijini Dar es salaam ambapo alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo. Katikati (mwenye tai) ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa ambaye pia alihudhuria hafla hiyo.kULIA NI Kamishna wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Suleiman Kova,
   

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (kulia), akiteta jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Ernest Mangu, katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano ya Dharura cha Polisi iliyofanyika katika viwanja vya Kituo cha Kati cha Polisi,jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe, akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano ya Dharura cha Polisi iliyofanyika katika viwanja vya Kituo cha Kati cha Polisi,jijini Dar es salaam. Waziri Chikawe alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.
   Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini(IGP),  Ernest Mangu, akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe, mara baada ya kufungua kituo  cha Mawasiliano ya Dharula cha Polisi iliyofanyika katika viwanja vya kituo cha kati cha Polisi,jijini Dar es salaam.Waziri Chikawe alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (wa nne kutoka kulia mstari wa kwanza), akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kutoka kulia – mstari wa mbele), viongozi mbalimbali wa jeshi la Polisi wakiongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu( watano kutoka kulia) na Wawakilishi mbalimbali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), mara baada ya uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano ya Dharura cha Polisi uliofanyika katika viwanja vya Kituo cha Kati cha Polisi,jijini Dar es salaam.


  0 0

   Mashimozz katika barabara hii ya Migombani, inayotokea DriveIn (makao makuu ya Zantel) kuelekea Victoria (Kairuki Hospitali) mpaka Makumbusho jijini Dar es salaam, yamekuwa ni kero kwa watumiaji wa njia hiyo, hasa kutokana na ukubwa wa mashimozz yaliyopo kwenye barabara hiyo. huo mpishano wa vyombo vya usafiri hapo pichani, si kwamba unatokana na mbwembwe za madereva, la hasha ni kutokana na namna ya kuyakwepa mashimozz hayo yaliyosheheni katika barabara hiyo.
   Hivi ndivyo hali ilivyo katika barabara hiyo hizi sasa, na hii ni kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni. maana kabla ya hapo mambo yalikuwa mswano kabisa.
   Hapa ni mwendo wa staili ya kinyonga, maana wenye kwenda mbio huku hakuwafai kabisa.
   Hii gari imekwama baada ya kunasa kwenye shimo la Chemba iliyofumuka kutokana na kuzidiwa na maji, hivyo hapo kuna shimo kubwa sana ambalo liko wazi.hivyo watumiaji wa njia hii kuweni makini sana na hapo maana haijulikani ni lini mkandarasi atapita na kuja kufanya mambo.


  0 0

  Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa akizungumza na wananchi wa Kata ya Msongola, Kijiji cha Mbondole katika uzinduzi wa Ujenzi wa Zahanati katika Kijiji hicho jijini Dar es Salaam.
  Diwani wa Kata ya Msongola, Angelina Makembeka akimshukuru Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa kwa kutembelea kijiji cha Mbondole jijini Dar es Salaam.


  0 0

  SAM_2715
  Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwapungia mikono wafuasi wake waliofika katika uwanja wa msikiti mkuu katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee hiyo.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
  SAM_2723Umati mkubwa wa wananchi wa Arusha wakiwa wanampungia mkono Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwapungia mikono wafuasi wake waliofika katika uwanja wa msikiti mkuu katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee 
  SAM_2688
  Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli,Edward Lowasa akiwa sheikh mkuu wa Bakwata mkoani  Arusha,Shaaban Juma wakifurahia jambo katika hafla ya harambe ya ujenzi wa  msikiti wa Patandi iliyofanyika jana katika uwanja wa msikiti mkuu wa mkoa Arusha,jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana.


  0 0

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akifafanua jambo mbele ya waandishi wa Habari leo (hawapo pichani) ,jijini Dar es Salaam, kuhusiana na kubadilika kwa tarehe ya mkutano wao kufuatia kuingiliana na Mkutano wa Baraza la Wawakilishi.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye Akizungumza na waandishi wa Habari leo ,jijini Dar es Salaam, kuhusiana na kubadilika kwa tarehe ya mkutano wao kufuatia kuingiliana na Mkutano wa Baraza la Wawakilishi.
  =========  ========  ======= 
  Na Chaalila Kibuda,Globu ya Jamii.

  KAMATI kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inatarajia kukutana Mei 23 mjini Dodoma na kujadili ajenda mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu .

  Akizungumza na waandishi wa Habari leo ,jijini Dar es Salaam,Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye amesema kuwa kubadilika kwa siku ya mkutano imetokana na kuingiliana na Mkutano wa Baraza la Wawakilishi.

  Nape amesema kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) kitafanyika Mei 22 ambapo ajenda mbalimbali zitatolewa ikiwa ni pamoja na maoni ya Ilani ya CCM 2015-2020 ambayo itawasilishwa na Kamati iliyoundwa kwa kazi hiyo.

  Amesema kutakuwa na vikao vya kawaida Mei 21 hadi 22 ambavyo vitakuwa vinafanyika mkoani Dodoma na Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wa Kamati kuu  ya CC na Halmashauri Kuu (NEC).

  Nape amesema vikao hivyo vitaongozwa na Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya  Kikwete katika kujadili masuala mbalimbali ikiwemo hali ya siasa ya chama hicho.

  Wakati huo huo Nape amesema kuwa wanachama sita  waliofungiwa  bado hatma yake kutokana na suala hilo linashughulikiwa na kamati mbili ambazo ndizo zinaweza kusema kifungo kinaendelea ama la,amesema na kuongeza kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM)  kinaongozwa na kanuni ambazo yeye mwenyewe amezikuta hivyo ni lazima wanachama na makada wazifuate kanuni na miongozo ya chama.

  Amesema wanachama kutangaza nia ya kugombea sio tatizo lakini mazingira yanayoendana baada ya kutangaza nia hiyo ndipo kanuni na miongozo ya chama inaanza kutumika,amesema kanuni na miongozo ya CCM zinasema mtu ambaye yuko kwenye kifungo katika chama haruhusiwi kugombea nafasi yeyote ndani ya chama ambazo zipo wazi.

  Amesema mikutano hiyo itajadili jinsi gani watu watapochukua fomu,urudishaji wa fomu pamoja na njia ambazo zitatumika katika utangazaji nia kwa wagombea kutokana na mazingira yaliyopo.

  0 0

  Mjumbe wa Kamati ya Mapokezi ya Rais wa Msumbiji Maalim Vuai Khamis kutoka Taasisi ya Elimu akikagua Gwaride la Jeshi la Wananchi wa Tanzania {JWTZ } ikiwa ni maandalizi ya mwisho ya ujio wa Kiongozi huyo wa Jamhuri ya Msumbiji Bwana Philipe Jacinto Nyusi anayetarajiwa kufanya ziara ya siku Moja Zanzibar.
  Kamanda Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jenerali Cyrill Ivor Mhaiki akibadilishana mawazo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika uwanja wa Ndege wa Zanzibar kuangalia matayarisho ya mwisho ya ujio wa Rais wa Msumbiji hapa Zanzibar.
  Balozi Seif akisisitiza jambo wakati alipokagua matayarisho ya mwisho ya Gwaride la kumpokea Rais wa Msumbiji atakapowasili Zanzibar mapema wiki ijayo. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar Balozi Silima Kombo, Mshauri wa Rais wa Zanzibar katika masuala ya Kiuchumi na Uhusiano wa Kimataifa Balozi Moh’d Ramia, Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jenerali Cyrill Ivor Mhaiki na Mjumbe wa Kamati ya Sherehe na maadhimisho ya Kitaifa kutoka JWTZ Kanali Shaaban Lissu.
  Balozi Seif akikiendesha Kikao cha Kamati ya Mapokezi ya Ujio wa Rais wa Msumbiji Bwana Philipe Nyusi hapo katika jengo la watu mashuhuri { VIP } Kongwe katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar.
  Rais wa Jamuhuri ya Msumbiji Bwana Philipe Jacinto Nyusi.

  0 0

  MKURUGENZI wa Kampuni ya Msama Promotions ambayo ndio inaandaa matamasha ya Pasaka na Krismasi, Alex Msama amekemea waimbaji wa muziki wa Injili Tanzania kufanya kazi ya Mungu na kuachana na siasa ambazo zinawaondoa kwenye uinjilishaji. 

  Msama ameyasema hayo wakati tukielekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na urais unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

  Msama anasema karipio hilo linawahusu pia viongozi wa dini wakiwamo Wachungaji na Maaskofu  ambao wanaonesha nia ya kutaka kuwania uongozi wa kisiasa katika nafasi hizo tatu.Sababu za Msama kukemea waimbaji wa Injili kujihusisha na Wanasiasa wakiwemo wagombea urais, kuna baadhi ya waimbaji wametunga nyimbo za ‘kuwatukuza’ wagombea urais wakati wao wanatakiwa muda wote kumtukuza Mungu na si binaadam wenzao.

  “Waimbaji tunatoka katika mstari, kwani Mungu anawategemea kufikisha ujembe wake kwa lengo la kuachana na machukizo ambazo yanapoteza mwelekeo wa jamii mbalimbali ambazo zinahitaji maono ya Wainjilisti,” alisema Msama na kuongeza. “Waimbaji ambao ninashirikiana nao katika kufikisha huduma ya neno la Mungu, nashangaa wanatoka katika mstari nawaomba wamrudie Mungu kwani wanapotea wakiwatumikia mabwana wengine.”  Alisema.
   

  0 0

   Muonekano wa ndani wa ukumbi mpya wa mikutano uliojengwa na CCM mjini Dodoma ambao uko katika hatua za mwisho kukamilika kabla ya kuanza kutumika.Ukumbi huu upo karibu na jengo la  Benki Kuu, njia ya kuelekea Chuo Kikuu cha Dodoma - UDOM.

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ujenzi wa Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Dodoma unaojengwa na  CCM.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ujenzi wa Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Dodoma unaojengwa na  CCM. Kulia ni makamu mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na makandarasi wanaojenga ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa Dodoma unaojengwa na  CCM, leo.Ukumbi huu upo karibu na Benki Kuu, njia ya kuelekea Chuo Kikuu cha Dodoma.

  Muonekano wa ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Dodoma. Picha na Freddy Maro.

  0 0

  Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi anatarajiwa kuwasili nchini kesho tarehe 17 Mei, 2015 kwa ziara ya Kitaifa ya siku tatu nchini kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
  Mhe. Rais Nyussi atapokelewa na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Mhe. Rais Nyusi atakagua Gwaride la Heshima na kupigiwa mizinga 21.

  Baada ya mapokezi hayo, Mhe. Nyusi atafanya mazungumzo ya faragha na Rais Kikwete yakifuatiwa na mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Msumbiji.

  Baadaye siku hiyo ya Mei 17, Mhe. Rais Nyusi atakutana kwa mazungumzo na Mabalozi kutoka Nchi za Afrika waliopo hapa nchini mkutano utakaofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es Salaam na kushiriki Dhifa ya Kitaifa itakayoandaliwa na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete, Ikulu.

  Mhe. Rais Nyusi ambaye ataongozana na Viongozi Waandamizi kutoka Serikali ya Msumbiji atahutubia Kongamano la Biashara litakalowakutanisha Wafanyabiashara wa nchi hizi mbili ambalo litafanyika tarehe 18 Mei, 2015 kwenye Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.

  Aidha, siku hiyo ya tarehe 18 Mei, Mhe. Nyusi atapata fursa ya kukitembelea Chuo cha Diplomasia kinachotambulika kama “Tanzania-Mozambique Centre for Foreign Relations” kilichopo Kurasini ambacho kilianzishwa mwaka 1978 kama mradi wa ubia ili kuendeleza mahusiano ya kindugu ya muda mrefu kwa lengo la kutoa mafunzo ya diplomasia na masuala ya kimataifa kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizi mbili.

  Mhe. Nyusi atakutana na Raia wa Msumbiji waishio hapa nchini kabla ya kuelekea Zanzibar ambako atafanya mazungumzo rasmi na Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na pia kuzungumza na raia wa Msumbiji waliopo Zanzibar.

  Akiendelea na ziara yake hapa nchini, Mhe. Rais Nyusi ataondoka Zanzibar tarehe 19 Mei, 2015 kuelekea Dodoma. 
  Akiwa Mkoani humo atatembelea Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuzungumza na Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, Mhe. Rais Nyusi atalihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadaye kutembelea Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

  Mhe. Rais Nyusi anatarajiwa kumaliza ziara yake hapa nchini tarehe 19 Mei, 2015 na kuondokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kurejea Msumbiji.


  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,

  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,

  Dar es Salaam.

  16 Mei, 2015


  0 0

  Na: Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma

  Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia mtu mmoja aliyekamatwa huko katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Yarabi Salama (Yarabi Salama guest house) katika Manispaa ya Dodoma. 

  Aliyekamatwa anafahamika kwa jina la MASAGARA S/O MESO, Mwenye miaka 40, Kabila Mzanaki wa Butiama, akiwa na funguo bandia 19, Master key 2, Bisibisi 2, Kisu kimoja, Tupa moja, Mikasi mitatu mikubwa ya kukatia vyuma, Msumeno ya kukatia vyuma mitano, Mitalimbo ya kuvunjia miwili, Adjustable spanner 1, Kipande cha bomba, Biti za kutobolea vyuma na mbao 8, Simu mbili aina ya Tecno na Nokia, Simu ya bandia ya Nokia, Pochi za mfukoni mbili, Hati ya dharura ya kusafiria, Betri ya simu moja, Nyenzo moja ya mbao, Nguo za kubadilisha, Madawa mbalimbali ya kienyeji, Kipande cha nondo kimoja na Irizi moja aliyokuwa amefunga sehemu ya juu ya mkono wa kushoto akiwa amehifadhi kwenye begi lake kwa maandalizi ya kufungua vyumba vya wapangaji wengine na kuvunja mita ili aibe.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema baada ya mahojiano na mtuhumiwa huyo, amekiri kufanya uhalifu wa kuvunja nyumba mbalimbali za kulala wageni na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu huko Mikoa ya Mwanza, Geita, Shinyanga, Tabora na hapa Dodoma. Uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini watuhumiwa wengine anaoshirikiana nao pamoja na matukio aliyofanya.

  Kamanda MISIME amesema nimuhimu kwa wenye nyumba za kulala wageni kuwa makini na wageni wanaowapokea kwani baadhi yao wanapanga vyumba kwa lengo la kufanya uhalifu wa kuwaibia wateja wengine au vifaa vya hoteli kama TV, DVD Player, Ving’amuzi n.k na wakati mwengine hufanya vitendo vya wizi mitaani.

  Pia Kamanda MISIME amesema katika hatua nyingine Jeshi hilo linamshikilia ONESMO S/O LUPILI YEYO Mwenye miaka 22, Muha, Mwenyeji wa Mkoa wa mwanza ambaye alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Kitivo cha Sayansi ya Jamii mwenye namba za usajli T/UDOM/2013/01760 kozi ya Uhasibu mwaka wa kwanza ambaye alisimamishwa masomo baada ya kukosa sifa ya kuendelea na masomo chuoni hapo. Baada ya wanafunzi kulalamika mara kwa mara kuibiwa mali zao ndipo tulipofanikiwa kumkamata.

  Mtuhumiwa huyo baada ya kuhojiwa alikiri kufanya uhalifu wa uvunjaji na wizi wa laptop na simu, alieleza kuwa mpaka anakamatwa na kuhojiwa alikuwa ameshaiba laptop zaidi ya 40 pamoja na simu zaidi ya 80 chuoni hapo.

  Kamanda MISIME ameendelea kusema kuwa baada ya ufuatiliaji katika kumbukumbu za Polisi, jumla ya matukio 30 yameripotiwa katika kituo cha Polisi UDOM na jumla ya Laptop zinazokadiriwa kuwa zaidi ya 60 zimeibiwa katika vitivo mbalimbali ndani ya chuo hicho ikiwemo kitivo cha Sayansi ya Jamii na Elimu.

  Mtuhumiwa huyo alipohojiwa zaidi alikwenda kuonyesha kwa mtu aliyemuuzia vitu hivyo baada ya kuiba, mtu huyo alibainika kuwa ni ISSACK S/O LEMA Mwenye miaka 29, Mkazi wa Airport ambaye ni fundi wa kutengeneza komputa maeneo ya Mtendeni Street Dodoma pembeni ya jingo la Bima.

  Polisi walifika kwa mtu huyo na alipohojiwa alikiri kupokea Laptop zaidi ya 19 kutoka kwa mtuhumiwa ONESMO na imebainika fundi huyu mara baada ya kuletewa laptop na mtuhumiwa anazifungua na kuuza kifaa kimoja kimoja.

  Kamanda MISIME ametoa wito kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbli kuwa makini na baadhi ya wanafunzi waliosimamishwa na kufukuzwa chuo kwani imebainika ndio wanaoshikiana na wahalifu wengine kuiba vitu mbalimbali katika vyuo, pia wananchi nao wasinunue vitu bila ya kupewa risiti au kuandikishiana kwa mujibu wa sheria ili kujenga uaminifu kwa anayenunua na anayeuza mali la sivyo unaweza kushitakiwa kwa kukutwa au kupokea mali ya wizi.

  0 0

  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga wastaafu wa shirika hilo kutoka ofisi ya mkoa wa Temeke.
  Meneja Kiongozi mpya wa Ofisi ya NSSF Mkoa wa Temeke, Chedrick Komba akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga wastaafu wa NSSF.
   Mstaafu wa NSSF, Brahan Newa kutoka Kitengo cha Takwimu akisalimiana na mstaafu mwenzake, aliyekuwa Meneja Kiongozi, Ofisi ya NSSF mkoa wa Temeke, Yahya Mhamali wakati wa hafla ya kuwaaga iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  11231914_1144808635544922_2269725808570836614_o..Wadau wa mwambao kukutana kila jumapili kwenye kiotaa hicho kipya

  Na Mwandishi Wetu
  Ule usiku wa Old is Gold Taarab na Bendi yenye ubora katika muziki wa mwambao ya GUSA GUSA Min Band, Jumapili hii ya Mei 17 na Jumapili nyingine kila wiki watatoa burudani ya nguvu na ya aina yake kwenye ‘kiota’ kipya ndani ya Hugo House, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

  Shoo hiyo inatarajia kuanza kuanzia majira ya saa mbili usiku na kuendelea, ni ya aina yake kwa wadau na wapenzi wa taarab nchini huku kiingilio kikiwa sh 5,000 tu kwa mlangoni.
  Kwa mujibu wa waandaji wa usiku huo, Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, alieleza kuwa bendi ya Gusa Gusa kwa sasa hipo juu baada ya kurejea kutoka katika ziara ya nchini Uingereza waliopiga kwenye miji kadhaa na sasa wamerejea nyumbani kwa makali zaidi.

  “Wadau wa usiku wa Old Is Gold karibuni sana ukumbi wa Hugo House ulipo Kinondoni, mkabala na TX Market. GUSA GUSA Min Band imejipanga kila idara uje uishuhudie” alieleza Asia Idarous.

  Asia Idarous amewasihi wapenzi na wadau kujitokeza kwa wingi kushuhudia bendi hiyo pamoja na kukumbushana yale ya zamani na kubadilishana mawazo.

  0 0


  0 0

  Last  Friday (  May 15) Ambassador Liberata Mulamula delivered  a  Keynote address at the School of Diplomacy's 2015 Graduation Commencement and Hooding Ceremony.

   The event took place at the Seton Hall University in New Jersey City. In her address which was  extremely well received by the audience,   Ambassador  Mulamula, who is also  the School's Board Member of Overseers,  touched upon some challenges facing the  international community at a time where the United Nations Commemorates her 70th  Anniversary of the   adoption of the  Charter


  0 0
 • 05/16/15--21:27: African imaginations
 • By Claude Grunitzky


   Africa is a special continent, rich in traditions and taboos. Only someone steeped in those traditions and taboos can hope to understand the challenges and opportunities before African citizens. 
  And yet, the West seems incapable of trusting Africans to analyse their own lives. Take, for instance, the American economist Jeffrey Sachs. An advocate for more aid to African nations, Mr Sachs is one of three editors of  The World Happiness Report 2015. 
  Happiness and prosperity are often (if not always) correlated. The first paragraph of the first chapter of this year’s report mentions that “happiness is increasingly considered a proper measure of social progress and a goal of public policy.” The 2015 rankings show my home country Togo as being, again this year, dead last, rock bottom in this odd geography of happiness. 

  Sachs and his team have derived a set of measures that supposedly extrapolate positive and negative experiences. These measures were educed by analyzing data from the Gallup World Poll. Here, ‘positivity’ is characterized by smiling and laughter, whilst ‘negativity’ is defined by experiences related to stress and depression. 


  0 0

  We are excited to share with you that our MD & CEO Mr. Moustafa H. Khataw was nominated as one of the 5 Top Franchise Owner of the Year (FOTY) at the UNIGLOBE Rendezvous    in London in the UNIGLOBE system worldwide. 

  Making the announcement above is the President & COO of Uniglobe Travel International, Mr. Martin Charlwood at the Global Rendezvous held on Saturday May 9th, 2015 at the London Lancaster Hotel.

  We thank all of you for your continued patronage.

  Management,
  Uniglobe Skylink Travel & Tours Ltd.

older | 1 | .... | 839 | 840 | (Page 841) | 842 | 843 | .... | 3270 | newer