Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 838 | 839 | (Page 840) | 841 | 842 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Siku 8 zimebaki kufikia kilele cha tuzo za filamu mwaka 2015.

  Ikiwa zimebaki siku chache kufikia kilele cha tuzo za filamu kwa mwaka huu ambapo Tuzo za Filamu Tanzania (TAFA) zinafanyika kwa mara ya kwanza nchini Mei 23, 2015 Mwalimu Nyerere International Conference Center jijini Dar es Salaam. 

  Haya ni mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu nchini kwani ni kuonesha mafanikio. Ni vipengele mbalimbali vilivyopo katika kinyang’anyiro cha tuzo za filamu mwaka huu 2015. Tuzo hizo ambazo ni kubwa na zenye hadhi ya juu zimeandaliwa na Shirikisho la Filamu Tanzania na washirika mbalimbali .

   “Kazi kubwa ya Shirikisho la Filamu Tanzania ni kusaidia kukuza tasnia ya filamu na kuunga mkono jitihada za wasanii kwa namna mbalimbali. Mbali na hilo pia ni daraja linalowaunganisha wasanii wa tasnia ya filamu na Bodi ya Filamu nchini hivyo kurahisisha utendaji wa kazi zao. 

  Ninayo kamati ya maandalizi iliyo imara na thabiti ambayo imefanya kazi katika mazingira magumu usiku na mchana kuhakikisha tunapata halfa nzuri na ya namna yake ambayo haijawahi kutokea”, Alisema Simon Mwakifwamba, Raisi wa Shirikisho la Filamu Tanzania.

  Aliongeza kwa kusema kuwa tasnia ya filamu nchini bado ina safari ndefu ukilinganisha na Hollywood ambao wameshapiga hatua kubwa. Tuzo hizi sasa ni jambo wanapaswa kujivunia kwa wasanii na watengeneza filamu kujivunia. 

  Imeripotiwa kuwa tasnia ya filamu imechangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa pato la taifa hili linathibitishwa na taarifa ya mapato nchini ya hivi karibuni, na hili linadhihirisha kuwa tasnia ya filamu inafanya kazi kubwa ya kupunguza tatizo la ajira nchini ambalo limekua ni tatizo kwa vijana wengi hapa nchini.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   
  JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
  KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

  Simu ya Upepo   : “N G O M E”          Makao Makuu ya Jeshi,
  Simu ya Mdomo : DSM  22150463      Sanduku la Posta 9203,
  Telex                     : 41051                       DAR ES SALAAM,    15, May 2015
  Tele Fax                : 2153426
  Barua pepe       : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
  Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz
                    
  Taarifa kwa Vyombo vya Habari

  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linasikitishwa na  taarifa za uvumi zilizotolewa  kuenea kwenye mitandao ya kijamii face book, whatsapp na twitter zikieleza kuwa JWTZ inafanya usaili leo tarehe           15 May 2015 katika Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) kwa wale waliosoma fani ya Computer science, IT, Electronics na Mechanical Enginering.

  JWTZ linapenda kuwajulisha wananchi pamoja na watumiaji wa mitandao hiyo kuwa taarifa hizo si za kweli ni uvumi, JWTZ lina utaratibu wake wa kuandikisha Jeshini ambapo hutoa taarifa katika vyombo vya habari kwa utaratibu ulio sahihi.

     Aidha, Jeshi linaendelea kusisitiza wananchi kuwa halina akaunti za mitandao hiyo na ni kinyume cha sheria kusambaza ujumbe kwa kutumia jina au nembo ya JWTZ watakao bainika watachukuliwa hatua za kisheria dhidi yao.
     
  Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano
  Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
  S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.
  Kwa Mawasiliano zaidi: 0783-309963.


  0 0

  NCC staff members in a collective picture during CRB Annual Consultative Meeting held at Mlimani City Hall in Dar es Salaam, 14th May 2015".

  0 0

  Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeendelea na mazoezi katika uwanja wa Olympia Park kujiandaa na mchezo wa fungua dimba dhidi ya timu ya Taifa ya Swaziland.

  Kocha mkuu wa timu ya Taifa Stars Mart Nooij amesema vijana wake wanaendelea vizuri na mazoezi, ikiwa leo ni siku ya pili kufanya mazoezi baada ya kufanya mazoezi ya kwanza jana jioni.

  Nooii amesema japokuwa kuna hali ya hewa ya baridi katika mji wa Rustenburg, wachezaji wake wameanza kuizoea na kusema kwa kuwa bado kuna zaidi ya masaa 72 kabla ya mchezo wa awali watakua wameshaizoea hali ya hewa.

  Kuhusu uwanja wa mazoezi, kocha Nooij amesema hali ya uwanja ni nzuri, uwanja una nyasi nzuri hali inayopelekea kikosi chake kufanya mazoezi katika mazingira mazuri.

  Akiongelea mchezo wake wa kwanza wa ufunguzi dhidi ya timu ya Taifa ya Swaziland utakaochezwa siku ya jumatatu, amesema anawajua Swaziland ni timu nzuri, mara ya mwisho katika mchezo wa kirafiki walitoka nao sare, hivyo anawaanda vijana wake kupata ushindi katika mchezo huo.
  Kikosi cha Swaziland kina wachezaji mchanganyiko wakiwemo wanaocheza ligi yao ya nyumbani na baadhi wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini.

  Taifa Stars itacheza mchezo wa kwanza dhidi ya Swaziland katika Uwanja wa Olympia Park siku ya jumatatu saa 1.30 usiku kwa saa za huku, sawa na saa 2.30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

  NB: Picha za mazoezi za Taifa Stars zimeambatanishwa

  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


  0 0

  kombe 2
  Baadhi ya wachezaji wa klabu ya Zamzam FC wakimwangalia mlinda mlango wao ,Seleman Casillas mara baada ya kuanguka na kulalamika kuua mguuni juzi katika mechi baina yao na Parrot katika kombe la Ng"ombe iliyochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni jijini Arusha,klabu ya Zamzam ilifanikiwa kutinga fainali katika mchezo huo ambapo itakutana na Nyota siku ya jumapili.
  kombe 3
  Mfadhili wa michuano ya kombe la Ng'ombe  ambaye pia mkurugenzi wa kampuni ya  East Link Tanzania Ltd,Kim Fute wapili kutoka kushoto akibadilishana mawazo na baadhi ya vijana waliofika kushuhudia michuano hiyo ,michuano hiyo itahitimishwa mapema siku ya jumapili wiki hiii katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni ambapo Timu ya Zamzam na Nyota watachuana.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog).
  kombe na view meru mlimaTaswira ya muonekano wa mlima Meru unavyoonekana pichani,hii ilikuwa juzi katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni jijini Arusha.

  Soka  ni mchezo wa ajabu embu sikia hii mlango wa klabu ya Parot FC,Sacrifice Adam juzi  alijikuta akiangua kilio uwanjani mara baada ya kushuhudiwa timu yake ikitolewa katika michuano ya kombe la ng’ombe linaloendelea  kuwaka moto katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni jijini Arusha.

  Adam,aliangua kilio wakati alipokuwa akishuhudia timu  yake ikiondolewa na klabu ya Zamzam FC juzi katika viwanja hivyo katika hatua ya matuta baada ya timu yake kuchapwa kwa jumla ya penati 5 kwa 4.

  Hatahivyo,hapo awali Adam alifanikiwa kuokoa mipira mingi ya hatari iliyokuwa ikipigwa na washambuliaji wa klabu ya Zamzam hususani wakati timu hizom zinakkwenda kumalizia kipindi cha pili.

  Kwa hatua hiyo klabu ya Zamzam sasa imefanikiwa kukata tiketi ya kuingia katika hatua ya fainali ambapo itakutana na Nyota siku ya kesho (jumapili) katika viwanja hivyo ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mdau wa michezo jijini Arusha na  mkurugenzi wa kampuni ya  East Link Tanzania Ltd,Kim Fute.

  Hatahivyo,jambo la kuvutia katika mechi hiyo ni pale paliposhuhudiwa watu wa kada zote wanafunzi,wanawake,wazee pamoja na watoto wadogo walipokusanyika kwa pamoja kushuhudia mchezo huo jambo lililoashiria kwamba mchezo wa soka bado unachukua nafasi ya kupendwa kwa kiasi kikubwa kupendwa tofauti na michezo mingine.

  0 0

  pichaaaaa
  Na Pamela Mollel wa jamiiblog.
  Wasanii wawili wa kizazi kipya nchini Nurdin Billal maarufu kama Shetta na Abdulwaheed Sykes” Dully Sykes” kesho jumamosi  wanataraji kunogesha katika onyesho la kundi la marafiki wa waziri mkuu mstaafu,Edward Lowasa lililopewa jina la “ Usiku wa marafiki wa Lowasa” .

  Onyesho hilo limeandaliwa na kundi la marafiki hao wa Lowasaa chini ya umoja wao unaojulikana kama “4 U Movement” linataraji kufanyika katika ukumbi wa burudani wa Triple A uliopo jijini Arusha ambapo mbali na wasanii hao pia wasanii wengine wachanga wanataraji kulisindikiza .

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mratibu wa onyesho hilo,Jonathan Kassano alisema kuwa lengo kuu ni kuwakutanisha marafiki wote wa kiongozi huyo anayetajwa kuwania mbio za urais mwaka huu kufahamiana, kubadilishana mawazo pamoja na kubalishana ujuzi .

  Mratibu huyo alisema kuwa onyesho hilo litaenea katika mikoa mbalimbali nchini ambapo mnamo Mei 20 mwaka huu kuanzia majira ya saa 4;00 usiku litafanyika  pia katika mkoa wa Dodoma na kisha kuelekea jijini Mwanza kabla ya kusambaa kote nchini.

  Alisema kuwa kufanyika kwa onyesho hilo katika mikoa mbalimbali nchini kutawapa fursa marafiki wa kiongozi huyo ambaye  pia ni mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha kutawapa fursa marafiki hao kukutana na kufahamiana pia.

  0 0

  Na Takdir Ali –Maelezo Zanzibar.

  Viongozi wa vyama vya siasa na Dini wametakiwa kuwashajiisha wafuasi wao kushiriki katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kuweza kujikinga na matatizo mbali mbali yanayoweza kujitokeza ikiwemo kokosa haki zao. Amesema Daftari la kudumu la wapiga kura lipo kisheria si kwa matakwa ya kisiasa hivyo viongozi hao wanapaswa kutumia nafasi zao kuwaelimisha wafuasi wao kushiriki kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura linaloendelea kuboreshwa.

  Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B Ayub Mohd Mahmoud wakati alipokuwa akifungua semina ya kutoa elimu ya uandikishaji na uendelezaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa vijana wa Wilaya ya Magharib A na B hapa Mwera Wilaya ya Magharibi B.

  Amewaaleza vijana kuwa mara baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992,hali ya siasa Zanzibar haikuwa nzuri lakini juhudi za viongozi walizochukuwa zimepelekea hali hiyo kutulia, kwa hiyo si vizuri kwa wazee kuwaachia watoto wao au wajukuu zao Zanzibar isiokuwa na amani na utulivu.

  “Tumerithi nchi yetu kutoka kwa wazazi wetu ikiwa katika hali ya amani na utulivu sivizuri hata kidogo kuwaachia watoto na wajukuu zetu wakiwa katika nchi isiyokuwa na amani na utulivu,” alisema Ayub. Aliongeza kuwa vijana kutoyajua yaliyopita na kujua yaliopo hivi sasa yanapelekea kukosa nafasi ya kufikiri zaidi katika kutoa maamuzi jambo ambalo amesema wanaweza kutoa maamuzi yasiyo sahihi.

  Mapema akitoa maelezo Afisa uandiskishaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura Wilaya ya Magharibi Maalim Khamis Mussa amesema ili kufanikisha Daftari hilo linaboreka zaidi mashirikiano ya pamoja ya wadau mbali mbali ikiwemo vyama vya siasa, vyama vya hiari na Wananchi wenyewe.

  Mwalimu Khamis amesema kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa kuna baadhi ya majina ya watu waliofariki ambao majina yao hayajaondolewa katika Daftari la kudumu na kusema Tume ya Uchaguzi haina uwezo wa kuwaondoa waliokosa sifa katika daftari hilo bila ya wananchi kuenda kutoa vielelezo muhimu .

  Wakichangia katika semina hiyo washiriki wameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Tume ya Uchaguzi kuandaa mazingira mazuri ya kuwawezesha wananchi kushiriki katika daftari la kudumu la wapiga kura bila vikwazo vyovyote sambamba na kuweka wazi kuwa watakuwa mabalozi wazuri kwa wenzao ambao hawakupatata fursa hiyo muhimu ya kushiriki.

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akisisitiza jambo kwa wadau mbalimbali wa habari toka nchi za ukanda wa Afrika Mashariki mapema hii leo wakati akifunga kongamano la siku mbili la wadau wa habari liloandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki lenye lengo la kuangalia mchango wa vyombo vya habari katika kukuza demokrasia katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki.
   Mhariri wa gazeti la Hoja toka nchini Tanzania Bw. Yassin Sadik  akichangia mada wakati wa kufunga kongamano la siku mbili la wadau wa habari liloandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki lenye lengo la kuangalia mchango wa vyombo vya habari katika kukuza demokrasia katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Bw. Kajubi Mukajanga akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe kufunga kongamano la siku lilowashirikisha wadau mbalimbali wa habari toka nchi za ukanda wa Afrika Mashariki mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wadau wa habari toka nchi mbalimbali za ukanda wa Afrika Mashariki wakiimba kwa pamoja wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa kufunga kongamano la siku mbili la wadau wa habari liloandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki lenye lengo la kuangalia mchango wa vyombo vya habari katika kukuza demokrasia katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Eliphace Marwa - MAELEZO

  0 0

  Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akizungumza na wadau wa filamu waliofika katika Ofisi za Wizara hiyo kuwasilisha taarifa ya maandalizi ya Tuzo za TAFA nchini itakayofanyika tarehe 23 Mei mwaka huu. Kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za TAFA Bibi. Caroline Gachara Gul (kulia) akiwasilisha taarifa ya maandalizi ya Tuzo za TAFA nchini kwa Uongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na watendaji kutoka Bodi ya Filamu nchini leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa kamati hiyo Bibi. Siima Rubibira.
  Wajumbe kutoka Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za TAFA pamoja na maafisa wanaosimamia Filamu nchini kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakimsikiliza kwa makini mjumbe aliyekua akichangia (hayupo pichani) wakati wa kuwasilisha taarifa ya maandalizi ya Tuzo hizo kwa uongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Meneja wa Utekelezaji na Maendeleo wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Mhandisi Keneth Haule (Kulia) akiukaribisha ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Mamlaka, Mabibo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kiongozi wa Msafara huo, Bibi Florence Mwanri. Wengine pichani ni Bw. Abel Shirima (Kushoto), Bw. Aloyce Andrea (Wapili Kushoto), na Bw. Omary Abdallah (Wapili Kulia).
  Kiongozi wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Mipango wa EPZA, Bw. Lamau Mpolo (Katikati) wakati walipotembelea kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam. Anayewasikilizia ni Meneja wa Utekelezaji na Maendeleo wa Mamlaka, Mhandisi Keneth Haule (Kulia).


  0 0

   Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Dkt.Shukuru Kawambwa akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma  kuongoza sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa Mei 15,2015. 
   Balozi wa Chini nchini Tanzania,Lu Youging akizungumza jambo na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma  kuongoza sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa Mei 15,2015,kulia ni Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mh.Anne Kilango Mallecela. 
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi mwanafunzi Agatha Julius Ninga kutoka Shule ya sekondari ya wasichana ya Tabora akiwa ni miongoni mwa wanafunzi sita waliofaulu vizuri katika mitihani ya sayansi ya kidato cha nne mwaka jana 2014.Agatha alifanya vizuri katika somo la Biolojia.Rais Kikwete alitoa zawadi kwa wanafunzi, shule,halmashauri na mikoa iliyofanya vizuri na kuongeza ufaulu katika mitihani ya Taifa kumaliza Elimu ya msingi na elimu ya sekondari.Tuzo na zawadi hizo zilitolewa leo katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya elimu nchini.
  Waziri wa Elimu Dkt.Shukuru Kawambwa akitoa tuzo maalum kwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza na kuboresha elimu nchini wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya elimu yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma leo.


  0 0


  0 0
 • 05/15/15--15:16: NYALANDU: NASARI MZUSHI
 • Na Mwandishi wetu
  WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amesema kauli zilizotolewa Bungeni na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, ni za kutapatapa na zimejaa ukosefu wa busara na uzushi.
  Amesema mbunge kusimama bungeni na kutoa kashfa badala ya kueleza masuala ya kisera au kiutendaji ni kupungukiwa busara na jamii haina budi kumpuuza.

  Akichangia hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu bungeni juzi, Nassari alisema Nyalandu kazi yake kubwa ni kuzunguka katika mapori ya akiba na kupiga picha na askari pamoja na kushangaa mbwa wa kizungu na kupokea ndege, helkopta za msaada. Alisema utendaji huo na mawaziri wengine unaweza ukawa ni ishara ya serikali iliyochoka.


  Hata hivyo, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Nyalandu alisema Nassari anapaswa kuwakilisha na kutetea wapigakura wake kwa hoja badala ya kuropoka masuala ambayo hayana tija.

  Alisema kauli zinazotolewa na wapinzani bungeni akiwemo Nassari kuishutumu serikali kuwa imechoka na kujaribu kuichonganisha na wananchi, kamwe hakuwezi kuikatisha tamaa kwa kuwa uzushi kwa upinzani ni jambo la kawaida.


  0 0

  Uncle mimi Hobidan Ackim Mwaijulu wa Kunduchi Mtongani. Nimepotelew na wallet yangu usiku huu Tarehe 15/05/2015.Kwenye daladala Nikitokea Makumbusho kwenda Kunduchi Mtongani Majira ya saa mbili usiku. Wallet ilikuwa na kadi ?(4) nne za Bank mbili za exim bank,moja ya foreign currency na nyingine ya tshilings. 

  Nyingine ni ya CRDB bank (master card). kadi nyingine ambayo ni muhimu sana ni Kadi ya Nje Bank ya HSBC pamoja na Token access yake ambayo ina muonekano wake ni mfano wa calculate ndogo. Pia kulikuwa na kitambulisho cha mpiga kura. 

  Kadi nyingine ni ya Nssf na baadhi ya business cards. Pesa hazikuwemo kwenye wallet. Tafadhali uncle naomba uaambie kuwa kwa yeyote atakaye vipata au kuviokota kupeleka kituo chechote cha polisi au anaweza kuwasiliana nami kwa simu zifuatazo 0756 841417 na 0787455678. 

  Asante sana uncle Michuzi pamoja na Grobuya Jamii kwa msaada wenu

  0 0


  0 0

  Ten years have passed since you left us for eternal glory.

  You may be physically gone, but you are forever treasured in our hearts and memories.

  As we remember you today; we keep on thanking the Almighty God for the life we shared with you.

  Always remembered and deeply missed by your father Mzee CD Msuya; wife Mary; sons Ngazo and Rumisha; sisters Joyce and Naanjela; brothers George, John, and Job; mother-in-law, sisters-in-law; brothers-in-law, nieces, nephews, relatives, and friends.

  MAY YOUR SOUL REST IN ETERNAL PEACE. AMEN!

  0 0
 • 05/15/15--21:50: kamusi ya juma nature


 • 0 0

   Wajumbe wa Kamati Kuu wa Baraza la Watoto wakijadili baadhi ya mambo yanayowahusu watoto pamoja na changamoto zinazo wakabili katika kikao cha Kamati Kuu ya Baraza la Watoto kilichofunguliwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dk. Pindi H. Chana mjini Dodoma.

   Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dk. Pindi H. Chana na viongozi wengine akimsikiliza  Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Ameir Haji Khamis
   
   Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dk. Pindi H. Chana akihutubia kikao hicho
   
   Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dk. Pindi H. Chana (Mb) (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Ameir Haji Khamis (kushoto) na Muweka Hazina wa Baraza hilo Haitham Juma (kulia) pamoja na Wajumbe wa Kamati Kuu wa Baraza la Watoto na Baadhi ya Walezi.


  0 0

  Just one goat can make a difference! Through your support, the Dar es Salaam Charity Goat Races has raised over 1 billion shillings for Tanzanian charities and local organizations. In our biggest year yet, here are some of the charities we will be supporting in 2015. For more information visit our website www.goatraces.com


  0 0
 • 05/16/15--00:06: Kutoka bungeni dodoma
 •  Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akizungumza na wabunge wa Viti Maalum, Mhe. Christawaja Mtinda (kushoto) na Mhe. Christina Lissu  Mughwai a(katikati) kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma
   Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudencia Kabaka kwenye viwanaj vya Bunge mjini Dodoma
  Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akijadili jambo na Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Jaji Francis Mutungi kwenye viwanja vya Bunge 

older | 1 | .... | 838 | 839 | (Page 840) | 841 | 842 | .... | 3272 | newer