Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

Bonanza la Taswa kufanyika Aprili 6,TCC Club Chang'ombe

0
0

BONANZA la vyombo mbalimbali vya habari lililopangwa kufanyika Aprili 6 mwaka huu viwanja vya Leaders Klabu likiandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), sasa litafanyika viwanja vya Sigara (TCC), Chang’ombe pia Dar es Salaam.

Uamuzi wa kuhamisha bonanza hilo umechukuliwa na sekretarieti ya TASWA kutokana na maombi ya waandishi wengi wa michezo kwa vile siku hiyo kuna mechi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika kati ya timu ya soka ya Azam na Barrack Young Controllers ya Liberia  itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam siku hiyo.

Azam ni timu pekee ya Tanzania iliyobaki kwenye michuano ya Afrika kwa ngazi ya klabu baada ya Simba na Jamhuri ya Pemba kutolewa katika raundi ya awali.

Tunaamini kwa bonanza kufanyika Sigara itakuwa rahisi kwa wadau wetu kushiriki kwenye bonanza na wale wengine watakaohitaji kwenda uwanjani wafanye hivyo wakitokea Sigara kwa hakuna umbali mrefu na kisha warejee kujumuika na wenzao mpaka mwisho.

Tunawaomba radhi kwa mabadiliko hayo, lakini yakiwa na lengo la kujenga na kuwa pamoja na wenzetu wa Azam kuhakikisha tunashirikiana nao kwa namna mbalimbali siku hiyo.

Bonanza hili linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) likiwa na lengo la kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari bila kujali ni wa siasa, michezo, uchumi, afya na mambo mengine pamoja na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari ili kubadilishana mawazo na kufurahi pamoja.

Bonanza hilo ambalo litahusisha wadau 1,500 kutoka vyombo mbalimbali vya habari litaambatana na michezo mbalimbali itakayohusisha vyombo vyote vitakavyoshiriki na pia kutakuwa na burudani ya muziki kutoka katika moja ya bendi kubwa za muziki wa dansi hapa nchini, ambayo itatangazwa siku zijazo.

Nawasilisha

Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA

naibu spika mhe. job ndugai na ujumbe wake Uingereza

0
0
 Naibu Spika Mhe Job Ndugai ( wa nne toka kulia, mbele) akiwa na Watanzania waishio Uingereza alipokutana nao jijini London
 Naibu Spika akiongea  na Watanzania waishio Uingereza
Uumbe huo ukiwa ni toka shoto Saidi Yakubu, Mhe. Godfrey Zambi, Naibu Spika Job Ndugai Mhe. Salehe Pamba na Mhe. Beatrice M. Shellukindo

nani tena huyu??

0
0
Msaada tutani wadau. Nimekutana na huyu jamaa akipiga boksi ndani ya boti hadi nashuka alikua busy tu na mzigo. Anayeweza kumtambua msaada. - Na mdau Gerson Msigwa

Waziri Mkuu akutana na Wanachama wa chama cha wakulima wa zao la Embe kutoka AMAGRO

0
0
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda amepokea kitabu cha muongozo wa kilimo bora wa zao la Embe kutoka kwa wana chama wa kilimo cha Embe Tanzania (AMAGRO).kitabu hicho alikabidhiwa na mwenyekiti wa (magro) Bwana Burton Nsape.shughuli hiyo ya kukakabidhi imefanyika leo ofisini kwa Waziri kuu magogoni Dar es salaam.
Wanachama wa chama cha wakulima wa zao la Embe wakiwa katika mazungumzo na Waziri Mkuu muda mfupi baada ya kumkabidhi kitabu cha muongozo wa kilimo cha zao la Embe.Picha na Chris Mfinanga.

Wanafunzi wa Kozi ya Ukamanda na Unadhimu kutoka Jeshi la Ulinzi la Rwanda watembelea Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar

0
0
Wanafunzi wa Kozi ya Ukamanda na Unadhimu kutoka Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) walipotembelea Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini Dar es Salaam jana, kwa lengo la kupata maelezo kuhusu vyanzo vya nishati nchini na changamoto zake. Wizara ya Nishati na Madini kupitia Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Hosea Mbise, imesisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya Tanzania na Rwanda katika masuala ya nishati.


KIDUM LIVE ON STAGE...@ FULL MOON NJIRO COMPLEX ARUSHA

0
0

WHO IS KIDUM???
His real name is Jean Pierre a.k.a KIDUM. 
He was born on the 28th of October in the year 1974, in the Northern town of Bujumbura, Kinama location in Burundi.
He involved himself in the music industry as a drummer when he was only ten years old in 1984. 
Burundian master drummer, composer, arranger and singer Jean Pierre Nimbona, fondly known as Kidum, is a Nairobi-based artist whose infectious tunes have hooked legions of East African fans. In Burundi, Kidum is an icon of hope and reconciliation; in neighboring Rwanda, he is recognized as the ‘homeboy.’
His secular-but-spiritual songs range from rocking zouk to acoustic classics, all featuring his vocal prowess. This is absolutely cool music from a musician who is ahead of his contemporaries as a composer and singer.
This Easter, with BODABODA BAND, he decide to Mingle LIVE with the Good People from
ARUSHA.
Is This Friday 29th March 2013 @ FullMoon Lounge from 2100.
Don’t Miss The Night to remember.
ENTRANCE 20,000.
POWERED BY: Intelli Track,  Intelligence SECURICO,
SUNBRIGHT hotels ltd,  Red Bull,  TUSKER LITESKYY VODKA and Zoom  net Printers.

JAPAN YATOA BILIONI 1.28 KUSAMBAZA MAJI MKOANI TABORA

0
0
Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa (kushoto) akiongea na waandishi wa habari jana(leo) jijini Dar es salama mara baada Tanzania na Japan kusaini hati za mkataba wa Japan kusaidia shilingi bilioni 1.28 kwa ajili ya usambazaji wa maji safi na salama katika baadhi ya vijijini vya mkoa wa Tabora.Kulia ni Balozi wa Japan nchini Masaki Okada.
Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa (kushoto) na Balozi wa Japan nchini Masaki Okada (kulia) wakibadilishana hati za mkataba wa Japan kusaidia shilingi bilioni 1.28 kwa ajili ya usambazaji wa maji safi na salama katika baadhi ya vijijini vya mkoa wa Tabora.
Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa (kushoto) na Mwakilishi wa JICA nchini Yasunori Onishi (kulia) wakibadilishana hati za mkataba wa Japan kusaidia shilingi bilioni 1.28 kwa ajili ya usambazaji wa maji safi na salama katika baadhi ya vijijini vya mkoa wa Tabora.Picha na MAELEZO_ Dar es salaam.

MAMA SHUJAA WA CHAKULA ATWAA TUNZO YA MAFANIKIO YA MWANAMKE KUNDI LA KILIMO (2013)

0
0
Bi. Emiliana Aligaesha, Mama Shujaa wa Chakula aliyepata nafasi ya pili kitaifa mwaka jana 2012 chini ya mashindano ya MAISHA PLUS, MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2012, amenyakua tunzo ya Mafanikio ya Mwanamke 2013 katika kundi la kilimo.

Mama huyu ambaye ni mkulima kutoka Mkoani Kagera, Wilaya ya Karagwe, Kata ya Kituntu, Kijiji Katembe, Kitongoji cha Nyakabanga ametwaa tunzo hii kutokana na jitihada zake katika kukuza kilimo katika kijiji chake kwa kuwa na mashamba yanayotunzwa kwa kanuni bora za kilimo.

Bi. Aligaesha anasema shamba lake ameweza kulitunza kwa ustadi mkubwa pamoja na umri wa miaka karibu 70 aliyokuwa nayo. Mama huyu ambaye ni mjane kwa sasa, anasema amejitahidi kulima mazao ya migomba na kahawa kwa kufuata ushauri wa kitaalam na kanuni mbalimbali za kilimo.

Tunzo hii imeandaliwa na Tanzania Women Achievement Award (TWAA) ambayo Rais wake ni Bi. Irene Kiwia. TWAA hutoa tunzo hii kila baada ya miaka miwili ili kutambua mchango wa akina mama waliotoa michango yao katika jamii kupitia sekta mbalimbali za kijamii.

Fuatilia habari katika picha katika hafla iliyofanyika leo Serena Hotel, Jijini Dar Es Salaam.
Bi. Emiliana ALigaesha akipokea tunzo yake kutoka kwa waandaji
Mama akitoa shukrani kwa waandaji
Kutoka kulia ni; Bi. Irene John ambaye ni mka mwana wa Bi. Emiliana Aligaesha akifuatiwa na Bi. Irene Kiwia ambaye ni Rais wa TWAA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Marina Njelekela ambaye alipata tunzo ya TWAA mwaka 2011 akimpongeza Bi. Emiliana Aligaesha.
Kutoka kushoto: Dkt. Linda Ezekiel ambaye amepata Tunzo ya Mafanikio 2013 (Sekta ya Afya) aliyetoa mchango mkubwa katika kuanzishwa Kitengo cha Tiba ya Figo na Uchujaji Damu, akifuatiwa na mdau ambaye naye alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa.
Mwanamitindo na mmiliki wa blog matata hapa mjini Bi. Shamimu Mwasha akiwa amepozi katika picha na Bi. Emiliana Aligaesha.
Bw. & Bi. Aminiel Aligaesha katika picha ya pamoja na mama yao mpendwa.
WASHINDI WA TUNZO KATIKA PICHA YA PAMOJA

WAJUMBE WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA WIZARA YA UCHUKUZI WATEMEBELEA ENEO LA RELI LILIHARIBIKA KUTOKANA NA MVUA KUBWA ILIYONYESHA HIVI KARIBUNI KATIKA ENEO LA TABATA MWANANCHI

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania(TRL), Mhandisi Aman Kisamfu akitoa maelezo ya namna mvua zilivyoletaa uharibu katika eneo la tabata Mwananchi kwa Wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Uchukuzi leo mchana.Wajumbe wa Baraza hilo walitembelea eneo hilo na kuona uharibifu mkuwa uliofanywa na mvua zilizonyesha hivi karibuni.Kulia kwa Mkurugenzi Mkuu wa TRL ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,Mhandisi Omar Chambo(Mwenye Shati jeupe).
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Miliki ya Rasilimali za Reli(RAHCO), Mhandisi Benhadard Tito(aliyevaa miwani) akitoa maelezo ya namna RAHCO ilivyojipanga kuboresha njia za reli katika eneo lilioathirika na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wa Wizara ya Uchukuzi leo mchana walipotembelea eneo hilo kujionea namna mvua zilivyoathiri Njia za Reli ya USafiri wa Treni Dar es Salaam.
eneo lililoharibiwa na mvua zilizonyesha hivi karibuni na kuondoa kingo zilizo karibu na Reli katika eneo ya tabata Mwananchi. Wajumbe wa baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Uchukuzi wametembelea eneo hilo leo mchana kuona uharibifu uliofanywa na Mvua hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo, akitoa maelekezo kwa Mkurgenzi Mkuu wa Shirika la reli Tanzania(TRL) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Miliki ya Rasilimali za Reli(RAHCO), wakati wa Ziara iliyofanywa na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Uchukuzi katika eneo la Reli lililoharibiwa na mvua leo mchana.
Uharibifu uliofanywa na mvua zilizonyesha hivi karibuni na kuondoa kingo zilizo karibu na Reli katika eneo ya tabata Mwananchi. Wajumbe wa baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Uchukuzi wametembelea eneo hilo leo mchana kuona uharibifu uliofanywa na Mvua hizo.

TAASISI YA CATHERINE FOUNDATION DEVELOPMENT YATOA MISAADA YA KIJAMII KWA WAGONJWA NA WATOTO YATIMA ARUSHA LEO

0
0
Taasisi ya Maendeleo isiyo ya kiserikali ya Catherine Foundation ya jijini Arusha leo imetoa misaada mbalimbali ya vyakula kwa wagonjwa Hospitali ya Mt Meru na vituo viwili vya Yatima vya Faraja na Lohada Moshono vyopte vya jijini humo.

Catherine Foundation Develeppent inaongozwa na Mbunge wa Viti Maalum UVCCM Arusha, Catherine Magigie.

Misaada hiyo ya vyakula na sabuni pamoja na kuwatembelea wagonjwa kufanyika ikiwa ni sehemu ya kuwapa faraja wagonjwa na yatima hao waki huu wa kuelekea siku kuu ya Pasaka ili nawao wajisikie ni miongoni mwa jamii.
Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akimkabidhi  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru, Frida Mokit msaada wa mablang’eti ya kujifunikia wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo.
Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akiwajulia hali wagonjwa waliolazwa Hospitali ya Mt. Meru ya jijini Arusha na kuwapa zawadi mbalimbali.

CAR FOR SALE

0
0

TOYOTA CRESTA YEAR 1999, 
CC 1998, 
WORKING KLM 189,000
 PRICE TSH 6,700,000/= 
NEGOTIATIONS AVAILABLE. 
FOR INFORMATION CALL: 0652-430196:

DAR - ES - SALAAM (MWENGE).

kamuzi la FM academia ndani ya Kiota cha East 24 usiku huu

0
0
 Wanamuziki wa Bendi ya FM Academia Wazee wa Ngwasuma,chini ya Uongozi wake Prezidaa Nyoshi El Sadat (katikati) wakionyesha umahiri wao wa kuyarudi magoma wakati wa Onyesho lao la kutambulisha nyimbo zao mpya,lililofanyika usiku huu kwenye Kiota cha East 24,Mikocheni jijini Dar es Salaam.FM Academia wameangusha show babkubwa kwa wapenzi na Mashabiki wao walifika kwenye kiota hicho.Onyesho hili limedhaminiwa na Kampuni ya Mabibo kupitia bia yake ya Windhoek.
 Kiongozi wa Bendi ya FM Academia,Prezidaa Nyoshi El Sadat (kati) akiimba sambamba na wenzake wakati wa onyesho hilo.
 Madansa wa FM Academia wakionyesha manjonjo yao.
Rapa wa FM Academia,Kalala Junior akiwajibika.
Kila kazi na Manjonjo yake,hapa ni Mpiga tumba wa FM Academia akiruka juu huku akiendelea kujipiga ngoma,

Rais wa Zanzibar,Dk. Shein azindua Mradi wa Usajili wa Ardhi katika Mjini Zanzibar

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza na wananchi na masheha wa Wilaya Magharibi,wakati wa sherehe ya Uzinduzi wa Mradi wa usajili wa ardhi (Smole) uliofadhiliwa na serikali ya watu wa Finland,katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akipokea zawadi ya picha za visiwa vya unguja na pemba a kuchora kutoka kwa Balozi wa Finland Chini Tanzania Bibi Sinikka Antilia,wakati wa sherehe ya Uzinduzi wa Mradi wa usajili wa ardhi (Smole) uliofadhiliwa na serikali ya watu wa Finland,katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Zanzibar leo,Waziriri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban,(kushoto) na Katibu Mkuu Ali Halil Mirza.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimkabidhi zawadi ya mlango wa Zanzibar Balozi wa Finland Chini Tanzania Bibi Sinikka Antilia,wakati wa sherehe ya Uzinduzi wa Mradi wa usajili wa ardhi (Smole) uliofadhiliwa na serikali ya watu wa Finland,katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akimkabidhi hati ya Ardhi Marium khaidar Mohamed, wa Mji Mkongwe,wakati wa sherehe ya Uzinduzi wa usajili wa adrhi uliofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia)akimkabidhi hati ya Ardhi Abdulhamid Ismail wa Mji Mkongwe,wakati wa sherehe ya Uzinduzi wa usajili wa adrhi uliofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) na akizindua Mradi wa Usajili wa Ardhi, katika viiwanja vya Victoria garden ,Mjini Zanzibar leo,(smole)uliofadhiliwa na Serikali ya watu wa Finland,(kulia) balozi wa Finland Sinikka Antilia,na (kutoka Kushoto) katibu Mkuu na Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban,na Mrajis wa Ardhi Mwanamkaa A.Mohamed,(wa katikati).
Baadhi ya masheha wa Wilaya Magharibi,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi na masheha hao katika sherehe ya Uzinduzi wa Mradi wa usajili wa ardhi (Smole) uliofadhiliwa na serikali ya watu wa Finland,katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Zanzibar leo .(Picha na Ramadhan Othman,lkulu).

MAONYESHO YA UTALII YA OTTAWA (OUTDOOR ADENTURE SHOW) YAFANA

0
0
Katika mwendelezo wa kukuza Diplomasia ya Uchumi na kupanua wigo wa Utalii wa Tanzania, Ubalozi wa Tanzania nchini Canada ulishiriki Maonyesho ya Utalii ya Outdoor Adventure yaliyofanyika mjini Ottawa tarehe 16&17 Machi, 2013. Maonyesho hayo yalikuwa na mafanikio makubwa kwa kuitangaza Tanzania na vivutio vyake hususan Mlima Kilimanjaro. Wanaoonekana kwenye picha ni Mhe. Balozi Alex Massinda (Katikati), kutoka kulia ni Bw. Richard Masalu, Afisa Ubalozi Ottawa, anayefuata ni Bw. Paul Makelele, Afisa wa Ubalozi, anayefuata baada ya Mhe. Balozi kushoto ni Bw. Rashid Adam wa Kampuni ya Zara Tours iliyoko Toronto na wa mwisho ni Bw. Julio Sanchez wa Zara Tours.
Bw. Richard Masalu akitoa maelezo kwa mmoja wa wageni waliotembelea Banda la Ubalozi.

Ngoma Azipendazo Ankal

0
0

Five Stars na 'All fall down'

uzinduzi wa tawi la yanga marekani

0
0

TUNAPENDA KUWATANGAZIA RASMI MASHABIKI, WADAU NA WAPENZI WOTE WA TIMU YETU YA SOCCER YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB MLIOPO MAREKANI KUWA TUNAZINDUA RASMI TAWI LETU HAPA MAREKANI LITAKALO JULIKANA KAMA YOUNG AFRICANS FAMILY USA. TUNAOMBA UKIPATA TANGAZO HILI MWARIFU NA MWENZIO.

TAREHE: JUMAMOSI 03/30/2013 

MAHALI: KILIMANJARO PASSION RESTAURANT

ADDRESS: 2310 PRICE AVENUE, WHEATON,MD 20902

MUDA:  4:00 PM

KWA MAWASILIANO: 
ALEX KASSUWI : TEL :301 305 9685

YOUNG AFRICANS "DAIMA MBELE NYUMA MWIKO"

NEWS ALERT: BARAZA KUU LATOA RUKSA BRIGEDI MPYA KWENDA DRC NA KUTUMIA NGUVU KUWAKABILI WAASI

0
0

Na Mwandishi Maalum, New York

 Katika hali ambayo haijawahi kutokea  katika  Operesheni za Ulinzi wa Amani  za Umoja wa Mataifa. Baraza Kuu la Usalama  ,  jana (Ijumaa), kwa kauli moja,  limepitisha  azimio linaloidhinisha   kupelekwa kwa Brigedi mpya ( Intervention Brigade)   itakayokuwa na uwezo wa kutumia nguvu pale inapobidi kuyakabili, kuyadhibiti na kupokonya silaha  makundi ya wanamgambo yenye silaha katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo,

 Hii ni mara ya kwanza kwa Baraza Kuu kupitisha Azimo la namna hiyo na kutoa idhini ya utumiaji wa nguvu za ziada katika shughuli za  operesheni za ulinzi wa amani  ambazo kwa  muundo na  malengo yake  ya asili ni kulinda amani na si kupigana au kutumia nguvu za ziada.

Brigedi hiyo mpya inayokadiriwa kuwa na wanajeshi 3,069 inaundwa na wanajeshi kutoka  Tanzania, Afrika ya Kusini na Malawi na  inatarajiwa  wakati wowote mara baada ya kupitishwa kwa Azimio   hili lililopewa namba 2098 (2013) kwenda  DRC ambako  itaungana na  walinzi wengine wa amani  waliopo huko chini ya  Misheni Maalum ya  Kutuliza  Amani maarufu  kama MONUSCO.

Uwepo wa Brigedi hiyo mpya itaiongezea uwezo MONUSCO kwa kuongeza idadi ya walinzi kufikia  19,815

Makundi ya wanamgambo yanayotarajiwa kudhibitiwa na Brigedi hii maalum na ambayo yamenyoshwa  kidole   na Azimio hilo,  ni pamoja na  kundi la M23,   Jeshi la Kidemokrasia la Ukombozi wa Rwanda ( FDLR)  na makundi mengineyo ambayo yamekuwa yakihatarisha amani na usalama katika eneo la Mashariki ya Kongo.

 Kwa lugha nyepesi  Baraza Kuu    linatoa ruska kupitia Azimio hilo,  kwa  Brigedi hii maalum,  yenyewe kama ilivyo au kwa kushirikiana na Jeshi la Kitaifa la  DRC  kutumia  nguvu  kubwa na kwa uhodari  wa  hali ya juu    kuyakabili makundi ya waasi.

Upitishwaji wa Azimio hili na ambalo  pia limeungwa  mkono na Katibu  Mkuu  Ban Ki Moon,  linafungua  ukurasa mpya katika kushughulikia  hali tete ya  Mashariki wa DRC.Ulishuhudiwa na Waziri wa  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Mhe, Rymond Tshibanda N’tugamulongo ambaye pamoja na mambo mengine alilishukuru  Baraza kwa kupitish azimio hilo muhimu kwa usalama na amani ya nchi yake na watu wake.

Azimio hilo   pamoja na mambo mengine linaainisha wazi kabisa  vigezo na  mipaka  ya  uendeshaji na dhamana ya Brigedi hiyo  itakayokuwa na batalioni tatu ya askari wa miguu,  kikosi cha mizinga na kikosi maalum cha upelelezi itakayokuwa na makao yake makuu katika mji wa Goma. Na kwa ujumla  imerejea na wajibu na dhamana wa MONUSCO kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Azimio ingawa Brigedi hii inadhama pana na uwajibikaji mkubwa    itakuwa ikiwajibika   kwa   Kamanda  Mkuu  wa  Misheni (Force  Commander) ya  MONUSCO

Ingawa Azimio hilo ambalo kimsingi liliasisiwa na  Ufaransa,  limeungwa  mkono  na wanachama wote 15 wanaounda Baraza  wakiwamo P5, hata hivyo kuna  baadhi ya nchi ambazo  licha ya kuunga mkono zilielezea waziwazi hofu yao  juu hasa dhanana kubwa ya matumizi ya nguvu iliyopewa Brigedi.

  Hofu ya nchi hizo ni pamoja na kwamba uwepo wa Azimio hilo siyo tu kulikuwa kunatishia madhumuni asilia ya  operesheni za  ulinzi wa amani lakini pia kuna hatari kubwa  kwa walinzi wa amani kutoka nchi zao walioko DRC kujikuta wakilazimika kutumia nguvu na hivyo kuhatarisha maisha yao, jambo ambalo ni kinyume na dhamana ya awali iliyowapeleka huko.

Nchi hizo  Guatamala, Pakistani,  Argentina na Morocco zilisema kwamba  Azimio hilo lilihitaji muda zaidi wa kujadiliwa  ili hoja za pande zote ziweze kusikilizwa na kuzingatiwa.  Zikatahadharish kwamba uamuzi huu wa kupeleka Brigedi itakayokuwa na uwezo wa kutumia nguvu, usijechukuliwa kama mfano wa kuingwa katika maeneo mengine bali  uamzi huu umetokana na mazingira tofauti ya eneo husika.

heri ya pasaka toka ujerumani

0
0

Umoja wa watanzania waishio Ujerumani,
Unawatakia kila la heri ya Sikuu ya Pasaka
watanzania wote popote mlipo,
Upendo na Amani katika jamii
ndio msingi imra wa watanzania.
Pasaka Njema

Mfundo. P.Mfundo
Mwenyekiti (UTU) Ujerumani

salamu za pasaka toka kwa FFU Ughaibuni

0
0
Bendi  maarufu ya muziki wa dansi " Ngoma Africa Band" aka FFU yenye makao yake nchini Ujerumani, inawatakieni wadau wote popote pale mlipo " kila la heri na fanaka " katika sikukuu ya msimu wa Pasaka. bendi yenu "Ngoma Africa" inawambea amani na baraka.
Pia msikose kupata burudani kamili ya Pasaka kwa kusikiliza nyimbo aka (Virungu vya FFU) at
mawasiliano at contact@ngoma-africa.com.
Kamanda Ras Makunja wa FFU Ughaibuni akiwa katika patrol

BREAKING NYUZZZZZZ......: JENGO LA GHOROFA LAPOROMOKA ASUBUHI HII JIJINI DAR NA KUPELEKEA WATU KADHAA KUPOTEZA MAISHA

0
0

TAARIFA YA UHAKIKA KABISA ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII HIVI PUNDE INAELEZA KUWA JENGO MOJA LA GHOROFA 15 AMBALO NI SEHEMU YA MSIKITI WA SHIA ITHNAASHERI  KATIKA MTAA WA INDIRA GHANDI KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM LIMEPOROMOKA MUDA MFUPI ULIOPITA 

INAELEZWA KUWA MPAKA SASA WATU 17 WAMEOKOLEWA HUKU WAWILI WAKIWA WAMEPOTEZA MAISHA,NA JUHUDI ZA ZIADA ZINAENDELEA KUFANYWA ILI KUOKOA WENGINE WENGI WALIOFUKIWA NA KIFUSI HICHO.

MKUU WA MKOA WA JIJI LA DAR ES SALAAM,MH. SAID MECK SADICK PAMOJA NA VIONGOZI WENGINE MBALIMBALI WAPO ENEO LA TUKIO HIVI SASA AKISHIRIKIANA NA WADAU WENGINE WA VYOMBO MBALI MBALI VYA ULINZI NA USALAMA,KUHAKIKISHA UOKOAJI UNAFANYIKA KWA WAKATI.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI DKT EMMANUEL NCHIMBI AMEWASILI PUNDE ENEO LA TUKIO NA INATARAJIWA KWAMBA HATA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE ATATEMBELEA SEHEMU HIYO WAKATI WOWOTE KUANZIA SASA.

CHANZO CHA KUPOROMOKA KWA JENGO HILO HAKIJAFAHAMIKA MPAKA SASA,KWANI KILA MTU YUPO KWENYE HEKAHEKA ZA UOKOAJI.

PICHA NA VIDEO ZA TULIO HILO LA KUSIKITISHA ZITAWAJIA PUNDE TU. HIVYO TUVUTE SUBIRA KIDOGO.
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images