Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live

martin kadinda apigwa kabali na 93.7 efm


INTERNATIONAL CONVENTION OF LIONS IN DAR ES SALAAM

0
0
International Director Raju Manwani decorates the International President's lapel pin on Chairman of the Convention Lion Dr. T.M. Jafferji. Standing in the centre is Past International Director Lion Dr. Manoj Shah.
District Governor of Uganda, Tanzania and South Sudan Lion Night Ndyarugahi addresses convention delegates at the last Cabinet Meeting.
The latest additional country, South Sudan joined Sub District 411B . The other two countries areTanzania and Uganda. The Sub District 411A comprises Kenya, Ethiopia and Seychelles.

Immediate Past District Governor Lion Wilson Ndesanjo (4th right) being awarded Appreciation Certificate of International President jointly by Chief Guest International Director Raju Manwani and PID Dr. Manoj Shah. Third from right is Governor Night Ndyarugahi, the first lady to become a Governor in Sub District 411B.

UCHAGUZI MKUU 2015 UKO PALE PALE - TUME YA UCHAGUZI

NEC KUTANGAZA MAJIMBO MAPYA YA UCHAGUZI MKUU 2015, JUNI 31

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MAJIMBO mapya ya uchaguzi kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) mwishoni mwa Juni, ili kuweza majimbo hayo kupata wabunge watakaowakilisha wananchi hao.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ,Kailima Ramadhani amesema ugawaji huo utakuwa umezingatia idadi ya watu,jiografia ya eneo husika pamoja mawasiliano na uchumi ili kuweza kuwalishwa na bunge katika maendeleo ya jimbo.

Ramadhan amesema katika Wilaya mpya zote zinaingia katika jimbo la uchaguzi kinachobaki ni kupata maombi ya majimbo mengine kutoka kwa Makatibu Tawala wa Mikoa (RAC).

Amesema kuwa baada ya maombi hayo tume ya Uchaguzi ya Taifa itapitia mipaka pamoja na kugawa kata kutokana na kata moha haiwezi ikawa katika majimbo mawili.

“Tunachotaka ni makatibu Tawala wa Mikoa kuleta maombi yao mapema na kuweza kuyapitia na katika mipaka pamoja na vigezo vilivyoanishwa na NEC”amesema Ramadhan.
 Kaimu Mkurugenzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kailima Ramadhan akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC), juu ya ugawaji wa majimbo mapya ya uchaguzi jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari hawapo pichani walipokutana leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya   wanahabari wakifuatilia katika mkutano wa NEC uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII)

WAKALA WA MISITU WAHAMASISHA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA NYUKI.

0
0
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
WAKALA wa Huduma  za Misitu Nchini (TFS),wamewataka wawekezaji wawekeze kwenye sekta  ya ufugaji nyuki  ili kutoa matokeo mazuri katika sekta hiyo.
 Hayo yamezungumzwa na Afisa ufugaji nyuki  mkuu  wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Mwanahamisi Mapolu wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo.
 Mapolu amesema kuwa  wawekezaji wajikite zaidi katika usimamiaji wa viwanda  vitakavyozalisha vifaa vya kufugia nyuki,visigina asali na mavazi ya kujikinga  wakati wa kulina asali.
Pia wawekezaji wajikite zaidi katika usimamiaji wa  viwanda vitakavyo zalisha bidhaa zitokanazo na nta kama mishumaa , rangi za viatu, vilainisho pamoja na vipodozi.
Mapolu amesisitiza kuwa  sera ya ufugaji nyuki nchini inahimiza ushirikishwaji wa wananchi katika shughuri za nyuki, uhifadhi mazingira na uzallishaji wa mazao ya nyuki yanayokidhi mahitaji ya soko.
Pia sera ya  Taifa ya  ufugaji nyuki nchini inasema kuwa ili kuhakikisha kuwa kuna mfumo thabiti wa biashara ya mazao ya nyuki, udhibiti wa ubora wa mazao hayo ukaguzi na utaimarishwa. Biashara ya mazao ya nyuki itahimizwa kwa kuimarisha huduma za kuaminika za udhibiti wa ubora  na ukaguzi wa mazao hayo.
Afisa Ufugaji Nyuki  Mkuu  wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)Mwanahamisi Mapolu akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari Maelezo jijini Dar es Salaam leo, kushoto ni Afisa Nyuki Masoko na Leseni, Nuru Tengeza na kulia ni Afisa Ufugaji Nyuki Mkuu,Magori Nyachari.
Afisa Nyuki Masoko na Leseni, Nuru Tengeza akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na Wakala wa Huduma  za Misitu Nchini (TFS) katika ukumbi wa  Idara ya habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo,Afisa Ufugaji Nyuki  Mkuu  wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)Mwanahamisi Mapolu.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika  mkutano  wa Wakala wa Huduma  za Misitu Nchini (TFS), leo jijini Dar es Salaam.Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

Mwana Habari Luqman Maloto azindua kitabu cha wagombea Urais

0
0
Mwandishi wa habari mzoefu, Luqman Maloto akikitambulisha kitabu chake kijulikanacho kwa jina la “The Special One 2015 Nani Ajaye?” wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Mwandishi wa habari mzoefu, Luqman Maloto akimkabidhi mwandishi wa habari wa televisheni ya TBC, Angella Msangi kitabu chake kijulikanacho kwa jina la “The Special One 2015 Nani Ajaye?”.
Mwandishi wa habari mzoefu, Luqman Maloto akimkabidhi mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima, Tatu Mohamed kitabu chake kijulikanacho kwa jina la “The Special One 2015 Nani Ajaye?”.
Mwandishi wa habari mzoefu, Luqman Maloto akimkabidhi mwandishi wa habari wa televisheni ya Azam, Temeluge Kasuga kitabu chake kijulikanacho kwa jina la “The Special One 2015 Nani Ajaye?”

Na Mwandishi wetu
Mwanahabari mzoefu nchini, Luqman Maloto amezindua kitabu kinachoelezea wasifu wa wagombea Urais wa uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba kijulikanacho kwa jina la ‘The Special One 2015 Nani Ajaye?’ ambacho kwa sasa kipo mitaani.

Akizungumza jijini, Maloto amesema kuwa ameamua kuandika kitabu hicho kutokana na kutambua wajibu wake na kutoa mchango kwa nchi yake kama raia hasa kwa kutumia taaluma yake ya uandishi wa habari ili kuwawezesha wapiga kura kumchagua kiongozi bora.

UMUHIMU WA USHIRIKIANO KWENYE VITA DHIDI YA UHALIFU MTANDAO

0
0
Nianze mada hii kwa kurudia pongezi kwa rafiki yangu Bwana Joe, Kwa kuongezewa nguvu na Nchi yake ya Marekani. Tayari taarifa rasmi ya hili nimeiandikia, na inaweza kusomeka zaidi kwa “KUBOFYA HAPA”. Bwana Joe amekua na imani inayofanana sana na yangu kwa muda mrefu ya kua uhalifu mtandao ni mbio za sakafuni endapo hapatakua na ushirikiano thabiti.

Kume kua na hoja nyingi kutoka mataifa mbali mbali juu ya kusua sua katika ushirikiano unao vuka mipaka huku uhalifu mtandao kutotambua mipaka iliyopo katika mataifa yetu. Uhalifu mtandao umeendelea kufanyika huku ukivuka mipaka na athari kuendelea kushika kasi ya aina yake hivi sasa.

Nategemewa kuangazia changamoto kadhaa tulizo nazo katika bara la Afrika na nini kifanyike katika hotuba yangu kwa wataalam mbali mbali wa usalama mitandao baadae mwezi huu jijini Johannesburg ambapo changamoto kubwa iliyoafikiwa na wanausalama kutokea maeneo yote duniani ni kukosekana kwa ushirikiano wa dhati na endelevu katika kupambana na uhalifu mtandao.

Hili limekua ni tatizo zaidi nchini Tanzania kwani hata ushirikiano wa ndani umekua ukiyumba sana baina ya vitengo mbali mbali vinavyo husiana na usalama mitandao nchini licha ya kua na malengo yananyofanana ya kutokomeza uhalifu mitandao. Kuna kila haja ya kujiangalia zaidi kwenye hili hasa kwa sasa tunapo hitaji zaidi kua na mipango pamoja na mikakati madhubuti ya kuweza kufikia malengo ainishwa.

SHULE YA SEKONDARI MTAKUJA YA KUNDUCHI BEACH JIJINI DAR ES SALAAM YAPOKEA MSAADA WA KOPYUTA TOKA VODACOM FOUNDATION

0
0
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mtakuja iliyopo Kunduchi beach jijini Dar es Salaam,wakishusha vifaa vya kompyuta mpakato kwa kushirikiana na maofisa wa Vodacom Tanzania,Jumla ya kompyuta(25) pamoja na vifaa vingine vimetole msaada na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Samsung na vitafungwa hivi karibuni kwa ajili ya kufundishia somo la kompyuta shuleni hapo.
Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation,Renatus Rwehikiza akiwapa maelezo wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mtakuja iliyopo Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam juu ya utumiaji wa kifaa maalumu cha kuhifadhia na kuchajia kompyuta mpakato. Jumla ya kompyuta(25) pamoja na vifaa vingine vimetole msaada na mfuko huo kwa kushirikiana na Samsung na vinategema kufungwa kwa ajili ya kufundishia somo la kompyuta shuleni hapo.
Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu katika shule ya sekondari ya Mtakuja ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam,Elizabeth Claud akibofya komputa mpakato wakati Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation,Renatus Rwehikiza alipokuwa akiwaonyesha kompyuta hizo. Jumla ya kompyuta(25) pamoja na vifaa vingine vimetole msaada na mfuko huo kwa kushirikiana na Samsung na vinategema kufungwa hivi karibuni kwa ajili ya kufundishia somo la kompyuta shuleni hapo.
Kompyuta mpakato 25 zilizotolewa msaada na Vodacom Foundation kwa ushirikiano na Kampuni ya Samsung katika shule ya sekondari ya Mtakuja iliyopo Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam zikiwa zimehifadhiwa katika kifaa maalumu cha kuhifadhia na kuchajia Kompyuta hizo.

MH. PINDA AKUTANA NA WAWEKEZAJI TOKA POLAND

0
0
Waziri mkuu,Miengo Pinda akizungumza na wawekezaji na watalaamu wa kujenga vihenge vya kisasa na vyenye uwezo wa kuhifadhi tani nyingi za nafaka hasa mahindi ambao wanatarajia kujenga vihenge hivyo hapa nchini. Watalaamu na wakezaji hao kutoka Poland ambao wakulikutana na Waziri Mkuu mjini Dodoma leo. Kutoka kushoto ni Honorta Maslowsk, Witold Karczewski ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Poland na Aleksandar Zingman. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

HUDUMA YA TRENI YA DELUXE KUSIMAMA KATIKA KITUO CHA NGURUKA KUANZIA TRENI ITAKAYOANDOKA DAR JUMAPILI IJAYO MEI 17, 2015

0
0
Uongozi wa Kampuni  ya Reli Tanzania  –TRL unachukua  fursa hii kuwataarifu wateja wetu wote na Watanzania kwa ujumla na hasa maeneo ya kituo cha Reli cha Nguruka mkoani Kigoma, kuwa treni yetu maarufu ya Deluxe itasimama kituoni hapo kuteremsha na kupakia  abiria.

Kwa taarifa hii ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na Wakazi wa maeneo yanayozunguka kituo cha  Nguruka, shime  wajitokeze kwa wingi kukata tiketi za safari kwa mujibu wa mahitaji yao . 
Halikadhalika safari za deluxe zitakuwa wiki mara moja siku za Jumapili itaondoka Stesheni ya Dar es Salaam saa 2 usiku ikiwa na mabehewa yasiozidi  15, Daraja la kawaida 10 (abiria 80 kila moja) daraja la pili la kukaa 3 (kila moja abiria 60) na daraja la pili kulala 2( kila moja abiria 36). 
Kwa sasa    itasimama  katika vituo 18 ambavyo ni pamoja na Morogoro, Kilosa, Dodoma, Makutopora, Saranda, Manyoni, Aghondi, Itigi, Tabora, Urambo, Kaliua, Nguruka, Uvinza, Kigoma. Vituo vingine ni Isaka, Shinyanga, Malampaka na Mwanza. Wiki moja ikienda Kigoma wiki inayofuatia itaenda Mwanza.

Kwa wasafiri wa Dodoma na Tabora hawa watatumia huo usafiri wakati wote isipokuwa wale  wanaoishia Kigoma  na Mwanza. Kuhusu mapendekezo ya safari za deluxe zianze saa 2 asubuhi, Uongozi wa TRL unalifanyia kazi pendekezo hilo na muda sio mrefu litapatiwa majibu.

NAULI ZA TRENI YA DELUXE  KWA MUHTASARI  KUTOKA  DAR KWENDA KIGOMA/MWANZA NI KAMA IFUATAVYO:

Dar -Dodoma  daraja la kawaida  TZS 18,500, Daraja 2 Kukaa TZS 24, 700 na Kulala: 41,200
Dar -Tabora kawaida 25,400, Daraja la 2 Kukaa 33,900 na Kulala 56,500;
Dar – Nguruka kawaida 31,200 Daraja la 2 kukaa 41,600 na kulala 69,300
Dar - Kigoma kawaida 35,700, Daraja la 2 Kukaa 47,600 na Kulala 79,400 na 
Dar - Mwanza ;kawaida : 35,000, Daraja la 2 kukaa 46,700 na Kulala 77,800.

Aidha pia tunapenda kutoa wito wa ushirikiano wa wananchi na   wadau wote kutunza vitendea kazi na kwamba kila mmoja awe mlinzi wa mwenziwe. Tujiepushe na vitendo vya makusudi kuharibu mabehewa haya mazuri ndani na nje . Kuna msemo : KITUNZE KIDUMU’! Tukitunza vitendea kazi  vitaweza kutoa huduma kwa muda mrefu na hivyo kuongeza tija na kupunguza matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi.  

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya TRL kwa Niaba ya 
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ,
Mhandisi  Elias Mshana
Dar es Salaam – Mei  12,  2015

INSPEKTA WA POLISI AANZA KUTOA USHAHIDI KESI YA ALBINO MWANZA

0
0
Na Daniel Mbega, Mwanza
SHAHIDI wa sita katika kesi ya mauaji ya Aaron Nongo mwenye ulemavu wa ngozi (albino), Mkaguzi wa Polisi (Inspector) David Mhanaya, ameanza kutoa ushahidi wake leo hii katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.
Mbele ya Jaji Robert Makaramba anayesikiliza Shauri hilo namba 213 la mwaka 2014, shahidi huyo ametumia siku nzima kutoa ushahidi wake akiongozwa na mawakili wa serikali Emil Kiria, Esther Majaliwa na Robert Kilando.
Hata hivyo, Jaji Makaramba aliahirisha kesi hiyo hadi keshokutwa Mei 14, 2015 baada ya kutokea mgongano wa kisheria katika masuala ya vidhibiti kufuatia pingamizi la Wakili Makwega wa upande wa utetezi, hivyo siku hiyo atatoa uamuzi kuhusiana na pingamizi hilo.
Washtakiwa katika kesi hiyo ni Chacha Jeremia, Mathew Jeremia Mlimi, Paschal Lugoye Mashiku na Alex Joseph maarufu kama Bugwema Silola Jangalu.
Marehemu Nongo aliuawa Juni 26, 2009 majira ya saa tatu usiku akiwa nyumbani kwake Ibanda Relini, jijini Mwanza ambapo wauaji hao walimkata usoni na kisha kumkata miguu yake yote miwili na kutoweka nayo pamoja na meno mawili ya mbele.

MKURENZI WA UTAWALA WA UTUMISHI WA UMMA TANZANIA ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA UBELIGIJI

0
0
Mkurugenzi wa Utawala wa Utumishi wa Umma Mhe. Nyakimura Muhoji (wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Ubalozi wa Tanzania Ubeligiji baada ya kumaliza kikao nao Brussels Ubeligiji. Wa pili kutoka kushoto Ni Bwana Festo Kipate Afisa Mhandamizi kutoka Wizara ya Fedha na wa tatu kutoka kushoto ni Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala, Balozi wa Tanzania Ubeligiji, Luxembourg na Jumuiya ya Ulaya.

Minister for East African Cooperation Hon. Dr. Harrison G. Mwakyembe holds bilateral discussions with Rwanda Counterpart Amb. Valentine Rugwabiza

0
0
The Tanzania Minister for East African Cooperation Hon. Dr. Harrison G. Mwakyembe today held bilateral discussions with his Counterpart Hon. Ambassador Valentine Rugwabiza, Minister for East African Community from Rwanda, on the sideline of the on going Extra-Ordinary Meeting of the EAC Council of Ministers taking place in Dar es Salaam. 
 The two Ministers held fruitful discussions on measures to further boost bilateral trade relations between the two Countries. 
The Ministers resolved to work closely in tackling specific impediments that affect traders from the two Countries. Sixty (60) percent of cargo imported into Rwanda pass through the Port of Dar es Salaam because it is currently more efficient and the distance is shorter compared to the distance from Mombasa Port to Kigali. 
 The Meeting was also attended by Tanzanian Ambassador to Rwanda Hon. Ali Siwa and Rwandan Ambassador to Tanzania Hon. Eugene Segore Kayihura.
 Hon. Ambassador Valentine Rugwabiza, Minister for East African Community from Rwanda(right) making a point during her meeting with Tanzanian Minister for East African Cooperation Hon. Dr Harrison G. Mwakyembe (Left) today in Dar es Salaam. On the right hand of Minister Rugwabiza is the Rwandan Ambassador to Tanzania  Eugene Segore Kayihura.
 The Minister for East Africa Cooperation Hon. Dr. Harrison G. Mwakyembe (far left) leading the Tanzania delegation during the bilateral discussions with Rwandan Minister for East African Community Hon.Ambassador Valentine Rugwabiza today in Dar es Salaam. Others from left are: Permanent Secretary Ministry of East African Cooperation Ms Joyce Mapunjo, Deputy Permanet Secretary Mr Amantius Msole, Tanzanian Ambassador to Rwanda Ali Siwa, Director of Politics, Defense and Security Affairs from Ministry Mr. Stephen Mbundi
 The Minister for East Africa Cooperation Hon. Dr. Harrison G. Mwakyembe (second right) in a group photograph after a bilateral meeting held today at the ministry's conference hall in Dar es Salaam. Others are Ambassadors from Tanzania Mr. Ali Siwa (left) and Rwanda Eugene Segore Kayihura (right). 

ngoma azipendazo ankal - special request from Ras Makunja wa Ngoma Afrika band, Ujerumani

0
0

Simba Wanyika - Halleluja

TANZANIA, JAPAN KUSHIRIKIANA SEKTA YA NISHATI

0
0
Na Veronica Simba 
 Wizara ya Nishati na Madini inapanga kushirikiana na Kampuni ya Mitsubishi Hitachi Power System ya Japan katika kuendeleza sekta ya nishati nchini. Kamishna Msaidizi wa Umeme wa Wizara, Mhandisi Innocent Luoga aliyasema hayo mapema leo baada ya kukutana na uongozi wa juu wa kampuni hiyo, Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam. 
Mhandisi Luoga alisema katika kikao hicho, Ujumbe wa kampuni ya Mitsubishi Hitachi Power Systems Ltd uliwasilisha mapendekezo ya matumizi ya teknolojia ya kisasa ya kufua umeme kutokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo makaa ya mawe, jotoardhi na gesi. 
“Sisi kama Serikali, kupitia taasisi zetu tumeona ni vema tushirikiane na Kampuni hii ambayo inajishughulisha na kutengeneza mitambo ya kufua umeme wa gesi, makaa ya mawe na jotoardhi kwa kutumia teknojia ya kisasa. Hii ni kutokana na vyanzo vipya vya umeme tulivyonavyo hususan makaa ya mawe na jotoardhi, ambavyo hatujaanza rasmi kuvitumia kuzalisha umeme,” alisema Kamishna Luoga. 
Aliongeza kuwa, lengo la Serikali ni kuhakikisha umeme wa kutosha, wa uhakika na wa bei nafuu unazalishwa na kusambazwa nchini ili kuwaletea wananchi maendeleo na hivyo kuinua pato la Taifa kwa ujumla. 
 Alisema kuwa, Kampuni hiyo ilishafanya majadiliano kuhusu ushirikiano katika sekta ya nishati na taasisi zilizo chini ya Wizara ambazo ni Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) pamoja na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO). 
Akizungumzia kuhusu faida za matumizi ya teknolojia hiyo ya kisasa inayotumika kufua umeme, Kamishna Luoga alizitaja kuwa ni pamoja na kuwa rafiki wa mazingira, kuwezesha uhakika wa kufua umeme kwa bei nafuu pamoja na kufua umeme kwa ufanisi mkubwa. 
Awali, katika kikao hicho baina ya Wizara na Kampuni hiyo, Rais wa Kampuni, Takato Nishizawa alisema kampuni yake iko tayari kutoa mafunzo ya namna ya kutumia mitambo yao inayotumia teknolojia hiyo ya kisasa kwa Wahandisi wa kitanzania. 
Aidha, Nishizawa alitoa mwaliko kwa wataalamu hao kutoka Tanzania, kutembelea mitambo hiyo huko Japan kwa lengo la kujifunza zaidi. Katika hatua nyingine, ilielezwa kuwa Kampuni ya Mitsubishi Hitachi Power System Ltd, tayari imeingia mkataba na Kampuni ya Sumitomo ambayo inatekeleza Mradi wa Kufua Umeme wa gesi wa Kinyerezi II unaofikia kiasi cha Megawati 240, kwa kazi ya kufunga mitambo ya kufua umeme (gas turbines) aina ya Hitachi.
 Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini (Kushoto) wakiwa katika Kikao na Wataalamu wa Kampuni ya Mitsubishi Hitachi Power System Ltd (Kulia). Kikao kilijadili kuhusu ushirikiano katika sekta ya nishati na kilifanyika Mei 12, 2015 Makao Makuu ya Wizara, Dar es Salaam.

 Rais wa Kampuni ya Mitsubishi Hitachi Power System Ltd, Takato Nishizawa (Kulia), akitoa ufafanuzi kuhusu shughuli zinazofanywa na Kampuni yake kwa Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini (Kushoto), wakati wa Kikao kilichokutanisha pande hizo mbili Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam, Mei 12, 2015 kwa lengo la kujadili ushirikiano katika sekta ya nishati.

Makamu Rais wa Kampuni ya Mitsubishi Hitachi Power System Ltd, Satoshi Uchida (Kulia), akifafanua jambo kwa Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini, wakati wa kikao baina yao kilichojadili ushirikiano katika sekta ya nishati. Kikao kilifanyika Mei 12, 2015 Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam.

Rais wa Kampuni ya Mitsubishi Hitachi Power System Ltd, Takato Nishizawa (Kushoto) na Kamishna Msaidizi wa Umeme wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Innocent Luoga (Kulia) – (Walioshikana mikono), wakiwa katika picha ya pamoja na Maofisa kutoka Kampuni hiyo na Wataalamu wa Wizara, mara baada ya kikao baina yao kilichojadili ushirikiano katika sekta ya nishati nchini. Kikao kilifanyika Mei 12, 2015 Makao Makuu ya Wizara, jijini Dar es Salaam.


HARAMBEE YA Jumuiya ya Wazanzibari waishio nchini Canada (ZANCANA) YAFANA

0
0
Jumuiya ya Wazanzibari waishio nchini Canada (ZANCANA), imechangisha zaidi ya Dola 1500 za Canada kwa ajili ya waathirika wa hali ya hewa nchini Tanzania.
Wanajumuiya ya ZANCANA wakipata picha ya pamoja baada ya ibada ya dua maalum ya kuwaombea walioathirika na mvua za masika, nchini Tanzania
Katika taarifa yake ambayo Swahilivilla imeipata nakala yake, Zancana imesema kwamba mnamo tarehe 9 Mei, 2015, jumuiya hiyo iliandaa mkutano maalum wa wanachama wake katika jiji la Toronto nchini Canada.
Mkusanyika huo uliofanyika katika ukumbi wa Zancana, ulifunguliwa kwa ibada maalum ya kuwaombea na kuwakumbuka ndugu jamaa na marafiki waliokumbwa na maafa ya hali ya hewa katika maeneo ya Pemba, Unguja na Dar-es -Salaam.
Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa, baada ya ibada, mawaidha na dua, kilifuatia chakula maalum kilichoandaliwa kwa ajili ya uchangishaji wa fedha kwa lengo la kuwasaidia wahanga wa mvua za masika katika maeneo ya Unguja na Dar, na waathirika wa kimbunga katika eneo la Kisiwapanza kisiwani Pemba.
Taarifa ya Zancana imemalizia kwa kusema kuwa, bado michango inaendelea kupokelewa, na kuwaomba wale wote wenye moyo na uwezo kuchangia kwa kupitia accounti inayopatikana katika tovuti yao ya www.zancana.org

KERO YA MAJI MACHAFU MTAA WA NZASA ZAMANI UMOJA STREET MWENGE

0
0
 Huu si Mto lakini ni Maji Machafu ambayo yamefumuka kwenye Chemba baada ya Mvua kunyesha Katika mtaa wa Nzasa zamani Umoja Street Mwenge ambao pia unajulikana kama mtaa wa Kinyesi
 Haya ni maji machafu ambayo yanatoka katika Chemba za maji taka ambapo yanapita kando ya makazi ya watu na kusababisha Kero ya Harufu mbaya na wasiwasi wa Mlipuko wa Magonjwa.
  Hii ni Moja ya Chemba ikiwa inafuka Maji Machafu ambayo yamejitengenezea Njia katika Makazi ya watu
Na hii pia ni Chemba ambayo imefumuka na Kusababisha matatizo katika mtaa wa Nzasa Mwenge

HOTUBA YA WAZIRI MKUU, MHESHIMIWA MIZENGO PETER PINDA (MB), KUHUSU MAPITIO NA MWELEKEO WA KAZI ZA SERIKALI NA MAKADIRIO YA MATUMIZI YA FEDHA YA OFISI YA WAZIRI MKUU NA OFISI YA BUNGE KWA MWAKA 2015/2016

0
0
WAZIRI MKUU MHE. MIZENGO  PETER  PINDA
                                                                                         

UTANGULIZI


1.            Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba kutokana na Taarifa iliyowasilishwa ndani ya Bunge lako Tukufu na Wenyeviti wa Kamati za Katiba, Sheria na Utawala; Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa; Uchumi, Viwanda na Biashara na Kamati ya Masuala ya UKIMWI zilizochambua Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge lako sasa lipokee na kujadili Taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa mwaka 2014/2015 na Mwelekeo kwa Mwaka 2015/2016. 
Aidha, naliomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha Makadirio ya Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Bunge, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Mafungu ya Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambazo ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya na Msajili wa Vyama vya Siasa kwa mwaka 2015/2016.

Rais Kikwete amteua Kamishna wa Polisi (CP) Diwani Athumani Msuya, kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai, pia amteua Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Valentino Mlowola kuongoza Idara ya Intelijensia ya Jinai

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Diwani  Athumani Msuya (pichani kushoto) , kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai (Director of Criminal Investigation).

Kabla ya uteuzi huu CP Msuya alikuwa Kaimu Kamishna wa kamisheni ya Intelijensia ya Jinai. CP Msuya anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Robert S. Manumba ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria.

Rais Kikwete pia amemteua Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Valentino Mlowola (kulia) kuongoza Idara ya Intelijensia ya Jinai, kujaza nafasi inayoachwa na Kamishna Msuya.

Kabla ya Uteuzi huu, DCP Mlowola alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza.

Uteuzi huu umeanza tarehe 3 Mei, 2015

Imetolewa na; 

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
12 Mei, 2015.

MHE.FREEMAN MBOWE AMSHUKURU MAGUFULI NA SERIKALI YA CCM KWA KAZI NZURI

Viewing all 109595 articles
Browse latest View live




Latest Images