Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 828 | 829 | (Page 830) | 831 | 832 | .... | 3285 | newer

  0 0

  This month, every day is Africa Day on DStv as we celebrate our dynamic and beautiful continent with an exciting array of local talent and vibrant, informative and entertaining homegrown programming.

  The Africa Magic channels will continue to deliver original, homegrown content in entertainment, lifestyle, drama series, reality television and film. The channels are home to an array of entertaining African content to highly rated shows such as: Star Gist which airs weekdays at 20:00 CAT, 53 Extra on Mondays at 19:30 CAT, Jara every Wednesday at 21:00 CAT and the high rating soapies Hotel Majestic weekdays at 21:00 CAT, and Tinsel on weekdays at 20:30 CAT. Not only will viewers be treated to these all-time favourite shows, but they’ll  also get an hour-long dose of their favourite musicians every day as Africa Magic World flexes its music muscle with Africa Magic Music (Weekdays at 14:00 and 23:55 CAT). 

  Africa Magic Family will also introduce a one hour music block which may increase to three or more hours in subsequent months. The channel also bring popular shows like Tyme out with Tee A on Wednesdays at 23:00 CAT, Star Superfan every at Thursday at 20:00 CAT, and Airtel Changing Lives on Wednesdays at 21:00 CAT. For more African talent, be sure to catch the new kid on the TV block, the local adaptation of the multiple award-winning ABC television drama hit series, Desperate Housewives Africa as it takes over your screens on EbonyLife TV. 


  0 0

  WAJUMBE wa Sekreatrieti ya Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya (NEC) ya CCM, jana walitembelea maeneno yaliyofikwa na mafuriko ya Mkoa wa Mjini Magharibi kwa lengo la kuangalia na kuwafariji wananchi walioathirika na mkasa huo.


  Wakiongozwa na Mwenyekiti wao, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Vuai Ali Vuai, wajumbe hao wa Sekreatrieti walitembelea maeneo mbali mbali mkoani humo ikiwemo Mpendae kwa Binti Amrani, Tomondo na Mwanakwerekwe, ambayo yalikumbwa na kadhia hiyo.
  Walitumia nafasi hiyo kuwafariji baadhi ya wananchi waliathirika na mafuriko hayo, ambapo baadhi nyumba zimejaa maji na nyengine kuanguka kuta zake, na kusabababisha hasara kubwa.

  Wajumbe hao wamewataka wale wote waliokumbwa na janga hilo, kuwa na moyo wa subra na kuiachia Serikali kupitia kitengo cha maafa kutafakari na kuona nini la kufanya. Aidha, wametoa wito na haja kwa jamii nzima ya Wazanzibari kuchukua tahadhari hasa wakati huu wa mvua za masika zinazoendelea kunyesha.

  Mvua hiyo kubwa iliyonyesha kwa muda wa masaa matatu mfululizo, kuanzia saa 3:30, iliwafanya wananchi wa Manispaa ya Zanzibar na vVitongoji vyake kushindwa kutekeleza shughuli zao za kimaendeleo.  0 0

  Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

  Madereva wamepewa kipaumbele  kwenye tume itakayokuwaikisimamia usafirishaji,kwani tume hiyo itakuwa na wajumbe watano  kutoka  Umoja wa madereva tuu na kutoka sekta nyingine watakuwa wajumbe watatu .


  Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda  wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake  jijini Dar es Salaam leo.


  Makonda amesema kuwa kamati hiyo haitaundwa na serikali, wajumbe watatokana na  uchaguzi wa madereva wenyewe pia  na wajumbe wengine watatoka  Mamlaka ya usafirishaji (SUMATRA), TABOA , TATOA, Wizara ya Ajira, wizara ya na mambo ya ndani.


  Makonda ameongezea kuwa Mgomo wa madereva hautakuwepo tena milele, madereva wachague wajumbe  ambao wanaweza kuhakikisha haki zao kinasimamiwa vizuri na kutatua matatizo yao.


  Tume hiyo itaanza kufanya  vikao vyake ijumaa ya wiki hii.
   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na wandishi wa habari hawapo pichani  ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wandishi wa habari waliohudhulia katika mkutano wa wandhi wa habari na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda jijini Dar es Salaam leo.(Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.)

  0 0

  Ernest and Young (EY), Country Managing Partner, Joseph Sheffu, presents EY 2014 report on Acacia Mining Investment and Economic Contribution in Tanzania, at a News Conference in Dar es Salaam’s Serena Hotel, Wednesday May 6, 2015. Among other things, in 2014, Acacia Mining purchased TZS 795bn of goods and services from suppliers located in Tanzania.
  Acacia’s Chief Executive Officer, (CEO), Brad Gordon, makes his remarks on the report.
  Acacia’s Vice President (Corporate Affairs), Deo Mwanyika, responds to the questions from Members of the media, regarding the report.
  Acacia’s Chief Executive Officer, (CEO), Brad Gordon, (C), with Ernest Young’s country Managing Partner, Joseph Sheffu, (L), and EY Partner, Tax International Tax East Africa, Silke Mattern, shortly after the EY unveil a report of Acacia economic and fiscal contribution to Tanzania in 2014.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Na Avila kakingo,Globu ya Jamii.
   CHAMA cha wafugaji Tanzania (CCWT),kimewataka wafugaji wote nchini kufanya shughuli zao kwa kufuata sheria, pia hawataki kuona wafugaji wakifanya uonevu wa aina yoyote kwa watu wengine.
  Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT),Magembe Makoye wakati akizungumza na wandishi wa habari katika ukumbi wa Habari MAELEZO leo jijini Da es Salaam.
  Makoye Amesema kuwa wafugaji watambue kuwa kunakutegemeana na watu wengine katika kuendesha shughuli zao  bila kuathiri  watu wengine katika jamii.
  Pia Makoye amesisitiza kuwa  chama cha wafugaji Tanzania hakitavumilia kuona wafugaji wanakuwa chanzo cha migogoro katika jamii,aidha chama hicho kimetoa wito kwa wafugaji wote Tanzania  kujihadhali  na  watu wanaopita kwao na  kujitambulisha kuwa wao ni viongozi wa chama cha wafugaji Tanzania.
  Chama hicho  kimeitaka Serikali itenge  ardhi kwa ajili ya  wafugaji ili kuepuka mwingiliano uliopo sasa wa watu kutokujua mipaka yao na hatimaye kusababisha mapigano na uhasama  miongoni mwa makundi hayo,
  suluhu ya migogoro mbalimbali iliyopo kati ya wafugaji na watumiaji wa ardhi katika jamii.
  Katibu Mkuu wa Chama cha Wafugaji Tanzania,Magembe Makoye akizungumza na wandishi wa habari  kushusiana na wafugaji kufanya shughuli zao kwa kufuata sheria za nchi katika ukumbi wa Habari MAELEZO leo jijini Dar es Salaam kulia ni Mkurugezi Msaidizi wa Idara ya HABARI MAELEZO Tiganya Vincent .
  Baadhi ya waandishi wa habari (PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII)

  0 0

   Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Mahadhi Juma Maalim akimkabidhi Waziri wa Afya wa Zanzibar Rashid Seif Suleiman msaada wa  Vyandarua kwa ajili ya kumaliza maradhi ya malaria  Zanzibar katika hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja.
   Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman akitoa neno la shukrani baada ya kupokea  msaada wa vyandarua ambao utatumika katika Hospital nane zinazolaza wagonjwa  Unguja na Pemba.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Mahadhi Juma Maalim akimuaga Waziri wa Afya wa Zanzibar Rashid Seif Suleiman baada ya makabidhiano ya vyandarua yaliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Unguja.

  0 0
 • 05/06/15--09:10: MREMA ALIA NA ARDHI YA VUNJO
 •  Mbunge wa jimbo la Vunjo, Augustino Mrema akitetea uchukuliwaji wa kiwanja kilicho chukuliwa na wawekezaji badala ya kutumika kama ilivyopangwa na mmiriki wa kiwanja kilichopo katika kijiji cha Himo eneo la Mieresini,Jimboni Vunjo, katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa habari MAELEZO  jijini Dar es Salaam leo na kulia ni  Mkurugezi Msaidizi wa IDARA YA HABARI MAELEZO Tiganya Vincent.
     Mwakilishi wa familia ya mzee Lekule, Denis Lekule  akizungumza na wandishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na jinsi walivyo chukuliwa eneo lao na wawekezaji, badala ya kuwa kama ilivyo pangwa na wazazi wao kuwa eneo la shule ya msingi na shule ya sekondari katika kijiji cha Himo eneo la Mieresini,Jimboni Vunjo, na kulia ni  Mbunge wa jimbo la Vunjo, Augustino Mrema.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mbunge wa jimbo la Vunjo Augustino Mrema leo jijini Dar es Salaam.(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII)

  0 0

   Wasanii wawili wanaotamba Bongo hivi sasa Shilole na Nuh Mziwanda wametua leo nchini Ubelgiji tayari kwa show yao ya nguvu siku ya Jumamosi nchini Ubelgiji.Wakiwa na nyuso za furaha hotelini walipofikia wameahidi kufanya bonge la  show kwa pamoja.Wameomba wapenzi wao wajitokeze kwa wingi kuja kushuhudia burudani ya uhakika toka Bongo.
  Nuh Mziwanda kushoto akiwa na Shilole a.k.a Shishi Baby wakiwa tayari kuwapagawisha wapenzi wao jumamosi hii hapo Antwerpen. Picha na Maganga One Blog

  0 0


  Mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2014- 2015, Yanga wakishangilia ubingwa wao huo mara baada ya kumalizika kwa mtanange wao dhidi ya Azam FC, uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo.Mtanange huo ulimalizika kwa Azam kushinda Bao 2-1.

  Mgeni Rasmi katika Mchezo huo, Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, Mh. Dkt. Fenella Mukangara akimkabidhi Nahodha wa Timu ya Yanga, Nadir Haroub cheti cha pongezi kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Soka Duniani, Sepp Blatter kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara 2014 - 2015.Kushoto ni Rais wa TFF, Jamal Malinzi na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji.
  Hongera Yanga SC kwa kutwaa Ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2014- 2015.


  0 0

  Mwakilishi Maalum wa  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya  Kongo ( DRC) Bw. Martin Kobler akiwafariji  walinzi wa amani  kutoka  Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) wanaohudumu katika Misheni ya MONUSCO ( DRC)  kufuatia shambulio  lililotokea siku ya  Jumanne huko Ben,i Magharibi ya Jimbo la Kivu. Katika shambulio hilo na ambalo limelaaniwa vikali na  Katibu Mkuu, Ban  Ki Moon, walinzi wawili wamepoteza maisha na wengine 13 wamejeruhiwa.
  -----------------------------------------------------
  Na Mwandishi Maalum

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban  Ki Moon,  amelaani vikali kuuawa kwa walinzi  wawili wa amani kutoka  Tanzania wanaohudumu katika Misheni ya Kulinda Amani katika Jamhuri ya   Kidemokrasia ya  Kongo ( MONUSCO).

  Walinzi hao wamepoteza maisha  baada ya kushambuliwa na kundi la   waasi linalosadikiwa kuwa ni  la  Allied Democratic Forces ( ADF), shambulio hilo limetokea siku ya   jumanne katika  eneo la Beni,  Magharibi ya  Jimbo la  Kivu ambapo walinda Amani wengine 13 wamejeruhiwa.

  Shambulio hilo  limetokea wakati kikosi hicho cha  walinzi wa Amani kutoka JWTZ wakielekea kutoa ulinzi  kwa wananchi na ndipo waliposhambuliwa.

   Walinzi  wa Amani waliopoteza maisha  ni  Private Juma Ally Khamis na Koplo John Leonard Mkude.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na  msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  jumanne jioni,  inaelezea  masikitiko makubwa ya  Katibu Mkuu, Ban ki Moon,  kufuatia tukio hilo la kusikitisha na ametoa pole kwa   serikali ya  Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania na familia  za marehemu.

  Ban Ki Moon katika salamu zake  amesema,  walinzi hao wamepoteza maisha yao wakati wakielekea kutoa ulinzi  kwa raia kwa mujibu wa mamlaka waliyokabidhiwa na Umoja wa Mataifa, na kusisitiza kwamba suala la kuwalinda raia litaendelea kupewa muhimu kama ilivyoainisha kupitia azimio  namba  2211(2015) la Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa.

  Aidha taarifa ambazo Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, imezipata kutoka Idara ya Ulinzi wa Amani ya Umoja wa Mataifa ( DPKO) zimetaarifu kwamba walinzi  wengine wanne ambao walikuwa hawajulikani walipo wamepatikana wakiwa hai.

  Wakati huo  huo,  Mshauri wa Masuala ya Kijeshi katika Umoja wa Mataifa,  Luteni General Magsood Ahmed  naye ametoa salamu zake za pole kwa Serikali  na familia ya  marehemu kufuatia shambulio hilo.

  Katika  salamu zake kupitia kwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Lt. General Ahmed pamoja na kulaani shambuli hilo amesifu na kupongeza  namna  wanajeshi wa Tanzania wanaolinda Amani  kupitia  Misheni hiyo ya MONUSCO wanavyotekeleza majukumu yao ya ulinzi kwa weledi mkubwa.


  Katika  hatua nyingine,  Mwakilishi  Maalum wa Katibu MKuu katika DRC. Bw. Martin Kobler naye ameelezea kusikitishwa kwake kufuatia shambulio hilo.  Na kwamba hatavumilia kuona matukio ya kushambuliwa kwa walinzi wa Amani katika eneo hilo ya Beni yakiendelea.
  0 0


  0 0


  0 0

  Mwenyekiti Mtendaji wa Michuzi Media Group  (MMG) Ankal Muhidin Issa Michuzi (kulia) na Meneja Maslahi na Sheria wa Kituo cha redio cha 93.7 E-Fm Bw. Denis Ssebo  wakipeana mikono baada ya  kusaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano  kwenye hafla fupi zilizofanyika Jumatano Mei 6, 2015 kwenye ofisi za kituo hicho cha redio Mikocheni jijini Dar es salaam.

  Pamoja na mambo mengine MMG na Kituo cha redio cha 93.7 E-FM kuanzia sasa watashirikiana katika mambo ya habari, matangazo na shughuli zingine za kijamii ikiwa ni pamoja na michezo, muziki na utamaduni.

  “Hii ni siku ya kihistoria katika tasnia ya habari nchini Tanzania kwa makubaliano haya ya kwanza ya aina yake ambapo kituo chetu cha 93.7 E-FM kilicho mstari wa mbele kukuza tasnia za michezo, muziki na utamaduni wa Tanzania na MMG inayoendesha na kuongoza katika tasnia ya habari mtandanoni nchini ya Michuzi Blog pamoja na Michuzi online TV kukubaliana kufanya kazi pamoja.

  “Hii ni baada ya kila upande kugundua  kwamba ina wapenzi lukuki ndani na nje ya Tanzania kuliko vyombo takriban vyote vya habari Tanzania, na pia kwa pamoja kuona haja ya kuenzi na kukuza tasnia za michezo, muziki na utamaduni wa Tanzania ambavyo pamoja na umuhimu wake vyombo vingi vya habari havijazipa tasnia hizo msukumo wa kutosha.

  “Hivyo sisi kwa pamoja tumeamua kuungana na kufanya mabadiliko makubwa kwenye kuendeleza tasnia za michezo, muziki na utamaduni kwa nguvu zetu zote”, alisema Bw. Ssebo.

  Kwa pande wake, Ankal, ambaye anaamini katika vitendo zaidi ya kuongea, alisema MMG inayoendesha Michuzi Blog a.k.a Globu ya Jamii, pamoja na Michuzi TV online, watafanya kile ambacho wengi hawafanyi ama kama wanafanya inakuwa kijuu juu tu.

  “93.7 E-FM radio station imedhihirisha ndani ya mwaka mmoja tu kwamba michezo, utamaduni na jamii ya Tanzania vinaweza kupendwa na kuthaminiwa na kila mtu ndani nan je ya Tanzania…
  “Kwa kuwa Ubunifu, kujituma na juu ya yote kuwapa wananchi kile roho zao zinapenda ni dira ya MMG na kituo hiki cha redio kinachokuja juu kwa kasi ya ajabu na kustua, wadau wetu wakae mkao wa kula kila siku kwani maneno hayavunji mfupa”alisema Ankal, ambaye blog yake pendwa kuliko zote nchini ya Michuzi Blog mwaka huu inatimiza miaka 10  ya kuanzishwa kwake.


  Kituo cha redio cha 93.7 E-FM kina mwaka mmoja tu toka kuanzishwa kwake lakini kimetokea kuwa kituo pendwa nchini Tanzania kwa kuenzi tasnia za michezo, muziki na utamaduni, wakati Globu ya Jamii inatajwa kuwa ndiyo Blog ya Kiswahili inayosomwa zaidi duniani.

  0 0

  Msikilize mkubwa Fella akila kabali 
  kwa kubofya mshale mweupe hapo...

  0 0

  Na Pamela Mollel, Arusha
  Kufuatia anguko la shilingi ya Tanzania dhidi ya dola wafanyabiashara nchini wametakiwa kuona kuwa ni fursa ya wao kijiinua kiuchumi katika biashara zao ndani na nje ya nchi na kuachana na propaganda za wanasiasa ambapo wanalalamikia anguko hilo.
  Ambapo hali hiyo imesababisha kupanda kwa bidhaa mbalimbali nchini hali inayotajwa kuongeza ugumu wa maisha ya wananchi sambamba na wafanyabiashara nchini ambao wananunua na kuagiza bizaa kutika nje ya nchi. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei wakati akiongea na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya mkutano mkuu wa ishirini wa wanahisa wa Benki ya Crdb unatarajia kufanyika kesho jijini Arusha katika kituo cha mikutano cha Kimataifa AICC.
  Hata hivyo alisema kuwa hivi sasa Benki hiyo imeweza kupata faida ya shilingi bilioni 95.6 sawa na asilimia 14 kwa mwaka 2014 ambapo limekuwa ni ongezeko kubwa zaidi kutokea ambapo faida hiyo itawasaidia kuweza kupatia wanahisa hao gawio la shilingi 15 kwa kila hisa na idadi ya wanachama hao. Ambapo mizania imeongezeka kwa asilimia 17 katika lengo lao katika mwaka huu ingawa soko limekuwa gumu kutokana na mfumuko wa bei uliopo sasa.
  Dk. Kimei aliongeza kuwa kutakuwepo na ajenda mbalimbali katika mkutano huo mkuu ambapo moja ya ajenda ni kuangalia namna ya kukua zaidi na kuongeza mtaji wao na kuboresha mfumo mzima wa Tehama ili kuweza kukabiliana na wizi wa kupitia mtandao ili kuweza kuwahakikishia usalama wa pesa za wateja wao.
  Aidha Banki hiyo inamkakati wa kuongeza mtaji wao ambapo wanatarajia kuongeza zaidi ya billion 100 ili kuongeza aman za banki na mtaji wao ili kuboresha huduma hizo na kukuza rasilimali za banki hiyo.
  Dk. Kimei aliongeza kuwa wanamkakati wa kupanua huduma zao katika nchi ya Burundi na nchi jirani ili kuweza kuwarahishishia wateja wao pindi wanapotoka na kutembelea nchi hiyo na kupata huduma ya miamala ya fedha.
  Benki hiyo hivi sasa wanamawakala zaidi ya 575 ya fahari huduma na wanamashine ya zaidi ya 375 za kutolea pesa katika mikoa yote nchini ili kuwarahisishia wateja wao kupata huduma za kibenki.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiongea na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari jijini Arusha akitoa taarifa ya mkutano mkuu wa ishirini  wa wanahisa wa Benki ya CRDB  unaotarajia kufanyika May 8  jijini Arusha.
  SAM_2456Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Mtambuka Benki ya CRDB Bi.Esther Kitoka na kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uendeshaji na Huduma kwa Wateja Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay
  SAM_2443Baadhi ya waandishi wa habari kutoka jijini Arusha wakiwa katika mkutano huo.
  SAM_2437Meneja Mahusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyo akiwa katika mkutano huo.
  SAM_2432Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa akiongea katika mkutano na waandishi wa habari katika maandalizi ya mkutano mkuu wa ishirini wa wanahisa wa Benki ya CRDB.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0  0 0

  On 29th April 2015, Ambassador/Judge James Kateka celebrated his 70th birthday. A dinner party was held at the Serena hotel in Dar es salaam.
  The guest of honour, former President Benjamin W Mkapa is flanked on his right by Ambassador/Judge James Kateka, former PM Judge Joseph S Warioba and Mme Evelyn Warioba. On the left is Dr Adolphine Kateka, Mama  Anna Mkapa and Prof Rwekaza Mukandala. Standing at extreme right is Advocate Kahabuka Kateka and in the middle in red is Ms Kahumbya Kateka

  0 0

  Mhe. Pierre Nkurunziza, Rais wa Jamhuri ya Burundi akiwa kwenye mazungumzo na Ujumbe ulioongozwa na  Mhe. Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania. Mawaziri wengine katika picha ni Mhe. Louise Mushikiwabo (kulia kwa Waziri Membe), Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda na Mhe. Amina Mohamed (mwenye skafu nyekundu), Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Mhe. Bernard K. Membe jana aliongoza Jopo la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Burundi kwa lengo la kupata hali ya maendeleo ya kisiasa nchini humo.

   Wakiwa nchini humo, mawaziri hao walikutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Pierre Nkurunziza, Rais wa Jamhuri ya Burundi, viongozi na wawakilishi wa vyama arobaini na tano vya siasa vya upinzani nchini humo, ambapo walitoa salamu za Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
   Kwa mujibu wa Waziri Membe, kwenye mazungumzo yao na Rais Nkurunziza yaliyodumu takriban saa moja na nusu, mawaziri hao walifikisha mwaliko kutoka kwa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, kuhudhuria Mkutano wa dharura wa Wakuu wa Nchi ambao umepangwa kufanyika Dar es Salaam Mei 13, 2015.
   Kwenye jopo hilo la mawaziri liliongozwa na Mhe. Bernard Membe wa Tanzania, walikuwepo pia Mhe. Balozi Amina Mohamed, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya na Mhe. Louise Mushikiwabo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, ambapo Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda aliwakilishwa na Rtd Brig. Matayo Kyaligonza Balozi wa Jamhuri ya Uganda nchini Burundi.
   “Lengo kuu la mkutano huo utakaofanyika jijini Dar es salaam ni kujadili hali ya amani wakati wa kuelekea kipindi cha uchaguzi nchini Burundi” Waziri Membe aliwaeleza waandishi wa habari waliokuwa wakimsikiliza baada ya mazungumzo hayo.
   Kwenye mazungumzo hayo ya Burundi Waziri Membe alimuomba Rais Nkurunziza na viongozi wa vyama vya siasa nchini humo kutoa maelezo, na maoni yao kwa jopo hilo kwa uwazi na kupendekeza namna ambavyo viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki watakavyoweza kuisadia Burundi.

  Pande zote mbili zilizoshiriki kwenye mazungumzo hayo na jopo la mawaziri kwa nyakati tofauti walielezea kufurahishwa kwao na hatua ya Rais Kikwete kuitisha kikao hicho cha Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili suala la Burundi kwa wakati muafaka.

  Hadi wakati mazungumzo hayo, wakimbizi wapatao ishirini na nane elfu wameikimbia nchi hiyo kwenda Rwanda na Tanzania ambapo wengi wao wameingia nchini Rwanda.

   “Hili ni janga la kibinadamu ambalo ni lazima jumuiya yetu chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete kulipatia ufumbuzi kwa haraka” alimalizia Waziri Membe.
   Kwenye safari hiyo, Waziri Membe aliongozana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama (NUU) pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Leticia Mageni Nyerere (Mb.). 
  IMETOLEWA NA:

  KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI KWA UMMA,

  WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,


  07 MEI 2015


  0 0

   Tunawataarifu waislamu wote kuwa tutakuwa na shughuli Haulia ya kisomo cha maulid ya kumsalia mtume Muhammad (s.w.a) katika Msikiti wa masjid Kubah na Madrasat Rahman ,Segerea mwisho,Tabata Dar-es-salaam tarehe  9 na 10 Mei 2015

  Ratiba ya shughuli kuanzia asubuhi ya Jumamosi 9 Mei 2015 kisomo cha kinamama (wanawake) mchana kutakuwa na madrasa na kisomo cha wanafunzi  jioni hadi siku ya 10 Mai 2015 Kisomo cha haulia na Maulidi mnakaribishwa wote na madrsa wanazotaka kushiriki tafadhali pigeni simu na. 0767617961 au 0712840960 pia 0777000036 karibu sana. Ungana nasi at https://www.facebook.com/profile.php?id=100006405199429   0 0


  Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya
  Tanzania (Taifa Stars), Mart Nooij
  Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mart Nooij leo ametangaza kikosi cha wachezaji 28 watakaoingia kambini katika hoteli ya Tansoma iliyo eneo la Gerezani jijini Dar es salaam, kujiandaa na michuano ya kombe la COSAFA na kuwania kufuzu kwa AFCON na CHAN mwezi Juni mwaka huu.
   Akiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF amesema, wachezaji 28 aliowaita, amewaona kwa macho yake wakicheza, na katika wachezaji aliowaita amechanganya wanaochipukia (damu changa) na wenye uzoefu wa michuano ya kimataifa. 
  Nooij amesema katika orodha hiyo ya wachezaji 28 watakaoripoti kambini jumatatu mchana, watapimwa afya zao na madakatari wa timu ya Taifa, na kisha watakaokuwa fit atachagua wachezaji 20 watakaokwenda kwenye michuano ya COSAFA nchini Afrika kusini. 
  Aidha Nooij ameongeza wachezaji 8 watakaobakia nchini wanapaswa kuwa tayari wakati wowote wanaweza jumuishwa katika kikosi kutokana na Taifa Stars kukabiliwa na michuano mbalimbali ambayo pia inahitaji kuwa na wigo mpana wa wachezaji. 
  Wachezaji walioitwa na kocha Nooij ni magolikipa: Deogratius Munish (Yanga), Aishi Manula, Mwadini Ali (Azam), walinzi: Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Erasto Nyoni (Azam), Nadir Haroub, Oscar Joshua, Kelvin Yondani (Yanga), Abdi Banda, Hassan Isihaka (Simba), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Haji Mwinyi (KMKM). 
  Wengine ni viungo: Amri Kiemba, Salum Abubakar, Frank Domayo (Azam), Said Juma, Salum Telela, Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba), Haroun Chanongo (Stand United) na Mwinyi Kazimoto (Al Markhira). Washambuliaji ni Ibrahim Ajib (Simba), Mrisho Ngasa, Saimon Msuva (Yanga), John Bocco, Kelvin Friday (Azam) na Juma Luizio (Zeco United). 
  Taifa Stars inatarajiwa kuondoka nchini siku ya jumatano, Mei 13 saa 1 jioni kwa shirika la ndege la Fastjet kuelekea nchini Afrika Kusini katika mji wa Rusterburg - North West Province ambapo ndipo michuano ya COSAFA CUP itafanyika kuanzia Mei 17 mpaka Mei 31 mwaka huu. 
  Mchezo wa kwanza wa Taifa Stars iliyopo katika kundi B katika michuano ya COSAFA, itacheza dhidi ya Swaziland Mei 18, Mei 20 (Madagascar Vs Tanzania) na Mei 22 ( Tanzania vs Lesotho), mshindi wa kundi B atacheza robo fainali dhidi ya timu ya Taifa kutoka Ghana. 
  Mara baada ya kumalizika kwa michuano hiyo, Taifa Stars itarejea nchini kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa AFCON 2017, dhidi ya Misri utakaopigwa Juni 13 nchini Misri, kisha kurejea nchini kucheza na Uganda Juni 21 kuwania kufuzu kwa fainali za wachezaji wa ndani CHAN. 
  Mart Nooj amesema ataitumia michuano ya COSAFA kama sehemu ya maandalizi ya michezo ya kuwania kufuzu kwa AFCON na CHAN. 

  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA 
  MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


older | 1 | .... | 828 | 829 | (Page 830) | 831 | 832 | .... | 3285 | newer