Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

JAHAZI WAFANYA MAKAMUZI YA NGUVU DAR LIVE USIKU WA KUAMKIA LEO

$
0
0
Mzee Yusuf 'Mfalme' akicheza kiduku na shabiki aliyepanda jukwaani.
Shabiki huyo akiwapagawisha mashabiki sambamba na wacheza shoo wa Jahazi.
Shabiki akiwapa raha wapenzi wa burudani.
...Akizidi kuonesha machejo stejini.
Mwimbaji wa Jahazi Modern Taarab, Rahma 'Machupa' akipagawisha mashabiki waliofurika ndani ya Dar Live.
Mwimbaji wa Jahazi akiwarusha roho mashabiki.
Nyomi ikiwa imepagawa na midundo ya Jahazi ndani ya Dar Live.
---
WAPENZI wa muziki wa mwambao usiku wa kuamkia leo walipata burudani ya aina yake ndani ya Dar Live wakati kundi la Jahazi Modern Taarab chini ya Mfalme Mzee Yusuf lililopokuwa likiporomosha burudani. Katika shoo hiyo, dada mmoja ambaye hakujulikana jina lake mara moja alikuwa kivutio ukumbini hapo kwa burudani aliyoitoa sambamba na wanamuziki wa Jahazi. Pichani juu ni baadhi ya matukio yaliyochukua nafasi ndani ya ukumbi huo wa maraha uliopo Mbagala Zakheem jijini Dar es Salaam.

RAIS KIKWETE AZINDUA TAARIFA YA UTAFITI WA VIASHIRIA VYA UKIMWI NA MALARIA MWAKA 2012

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata ukanda kuzindua rasmi taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwi na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiri Ukimwi (TACAIDS) Mama Fatma Mrisho na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Mhe William Lukuvi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akinyanyua juu baada ya taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwi na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda', Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiri Ukimwi (TACAIDS) Mama Fatma Mrisho.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa kuzindua rasmi taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwi na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Meza kuu ikimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiri Ukimwi (TACAIDS) Mama Fatma Mrisho akisoma taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwi na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipitia baada ya kuzindua rasmi taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwi na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda na kushoto kwake ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi, Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa.
Wadau kutoka sekta mbalimbali wakiangalia matangazo ya kupiga vita UKIMWI na Malaria wakati wa uzinduzi rasmi wa taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwi na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.PICHA NA IKULU.

EU TO SUPPORT TANZANIA IN PROTECTING ITS FOREST

$
0
0

THE Joint Research Centre of the European Union (Institute for the Environment and Sustainability) and the Tanzania Forest Services (TFS)Agency under the Ministry of Natural Resources and Tourism(MNRT) have today signed a collaboration agreement aimed to help to curb the alarming rate of deforestation in the country. 

THE CA is complementary to the on-going NAFORMA , the first ever National forest Assessment in Tanzania, initiate in 2009 and currently in its final stages.  Under the agreement, both sides have agreed to cooperate in mapping the land cover changes and forest degradation assessment in support to national readiness initiative for REDD+ (Reducing Emissions from Deforestation and forest Degradation).


The signing ceremony was held today Wednesday 27thdMarch at the headquarters of the Ministry of Natural Resources and Tourism in Dar es Saalam.

Introducing Nyamo's new track 'Mzuka Bado'

Balozi Kallaghe Atembelea Shughuli za Watanzania Leicester na Northampton - UK

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe mwishoni mwa wiki iliyopita (Jumamosi, 23 na Jumapili, 24 Machi 2013) alitembelea baadhi ya shughuli za miradi mbalimbali zinayofanywa na Watanzania waishio Leicester and Northampton kwa lengo la kufahamu mafanikio na changamoto zao.

Akisindikizwa na Afisa wa Ubalozi, Bw. Amos Msanjila, Balozi alipenda kufahamu nini mahitaji ya Watanzania hao ili kuweza kujenga mkakati muafaka wa kuwatia moyo na kuwashirikisha wananchi hao kujenga nchi.

Akiwa Leicester alipata fursa ya kutembelea kituo cha redio ya jamii ya mji huo na kufanyiwa mahojiano ya moja kwa moja kwa Kiswahili na Mtangazaji wa redio hiyo, Bw. Omar Hussein. Redio hiyo inasikika moja kwa moja katika maeneo yote ya Leicestershire na vitongoji vyake.

Aidha Balozi Kallaghe alitembelea kiwanda kidogo cha usindikaji wa vyakula na viungo kinachomilikiwa na mfanyabiashara mwenye asili ya Tanzania cha Jalpur Millers. Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho Bw. Deepen J. Pau alimwambia Balozi kwamba Kampuni yao ina mipango ya kuwekeza zaidi Tanzania.

Baadae Mheshimiwa alitembelea kituo cha kuratibu usafirishaji wa mizigo mbalimbali kwa makontena kwenda nchi za Afrika Mashariki na hasa Tanzania. Pamoja na kuonyeshwa shughuli mbalimbali zinazofanyika hapo, Balozi alipata pia fursa ya kuzungumza na wajasiliamali Bw. Abdul Nasser Hamed wa Zanzibar Driving School na Mussa Issa Mussa wa BMA Store and Shipping Agency.

Alipata pia fursa ya kutembelea mgahawa wa biriyani wa Maalim Hamis na kukutana na mpishi huyo maarufu kabla ya kukutana na Watanzania wachache, hasa viongozi wa Jumuiya ya Watanzania ya Leicester.

Siku ya Jumapili Balozi alitembelea Jambo Hair Salon na baadae kukutana na viongozi wa watanzania wachache kwenye Mgahawa wa Kass’s Grill unaomilikiwa na kijana wa kitanzania Kasongo Mohamed. Pamoja na kupata chakula cha mchana kwenye mgahawa huo, Mheshimiwa alifanya na mazungumzo na watanzania hao na kusisitiza umuhimu wa mshikamano na moyo wa kuunga mkono biashara za watanzania wenzao.

Mheshimiwa ataendelea kutembelea miji mbalimbali hapa Uingereza na kujionea shughuli zinazofanywa na Watanzania kila atakapopata fursa ya kufanya hivyo.




Kesi za mimba kwa wanafunzi zapungua Handeni

$
0
0
Na Joachim Mushi.

MATUKIO ya kesi za kuwatia mimba/kuwabaka wanafunzi yaliokuwa yameshamiri katika shule mbalimbali za msingi na sekondari wilayani Handeni sasa yameanza kupungua tofauti na ilivyokuwa awali. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Machi 2012 na Machi 2013 matukio ya mimba yanapungua.

Akizungumzia hali hiyo juzi Wilayani Handeni, Ofisa Elimu wa Wilaya, Mgaza Muchiwa alisema matukio ya mimba kwa wanafunzi yanapungua tofauti na miaka ya nyuma ambapo matukio ya utoro wa mimba kwa wanafunzi yalikuwa mengi. “Picha ya mwaka jana niliiona na tulikuwa tukifuatilia kwa karibu matukio ya kesi za mimba kwa wanafunzi…huwezi kufananisha na ilivyo sasa kunamabadiliko kwani matukio haya yamepungua,” alisema Muchiwa akizungumza na mwandishi ofisini kwake Handeni juzi.

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Handeni, Zuber Chembera alithibitisha pia kupungua kwa kesi za mimba zinazofikishwa katika vituo vya Polisi ukilinganisha na hapo nyuma. Akifafanua zaidi kupitia taarifa za Dawati la Jinsia na Watoto Kituo cha Handeni, alisema hadi Novemba 2012 walipokea kesi 66 za matukio hayo lakini tangu hapo hadi Machi mwaka huu kesi hizo zimepungua kwa kiasi kikubwa.

Uchunguzi uliofanywa na www.thehabari hivi karibuni katika shule za sekondari Komnyang’anyo, Kileleni na Kivesa zote za wilayani Handeni umeonesha kupungua kwa matukio ya mimba kwa wanafunzi, huku walimu wakidai hali hiyo imechangiwa na kampeni ya ‘Niache Nisome’ iliyoanzishwa na Mkuu wa Wilaya mpya, Muhingo Rweyemamu.

“Kweli kampeni ya ‘Niache Nisome’ iliyoanzishwa na Mkuu wa Wilaya mpya imesaidia sana maana watu wameanza kuogopa kuwarubuni wanafunzi…hata wazazi na wanafunzi nao wanaogopa kuhusishwa katika kesi hizo hii imesaidia kupunguza matukio ya mimba,” alisema Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Komnyang’anyo Nadhiru Kinyama.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Rweyemamu Agosti 2012 alianzisha kampeni ya kupambana na watu waliyokuwa wakiwakatisha masomo wanafunzi kwa kuwatia mimba na kuwaozesha kwa kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wanafunzi na jamii juu ya umuhimu wa elimu wilayani humo.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Handeni, Zuber Chembera akizungumza.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu.
Ofisa Elimu wa Wilaya ya Handeni, Mgaza Muchiwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi.

Article 3

SAFARI LAGER YASOGEZA MBELETAREHE YAKURUDISHA FOMU ZA PROGRAMU YA “SAFARI LAGER WEZESHWA”.

$
0
0
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akiwanyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) namna ya kupata fomu kwa njia ya mtandao wa www.wezeshwa.co.tz baada ya kusogeza mbele zoezi la kurudisha fomu za program ya Safari Lager Wezeshwa wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Jaji Mkuu wa Programu hiyo, Joseph Migunda.


HOTUBA YA RAIS KIKWETE ALIPOZINDUA RASMI MAFUNZO JKT NCHINI KATIKA KAMBI YA RUVU MKOA WA PWANI MACHI 26, 2013

MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA ILALA MH.JERRY SILAA AZINDUA RASMI ZIARA YA KUTEMBELEA MAKUMBUSHO YA KIHISTORIA KATIKA MANISPAA YA ILALA.

$
0
0

Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 wakiwa katika Picha ya Pamoja
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Muheshimiwa Jerry Silaa akiwakaribisha washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 katika Manispaa ya Ilala
Mmoja wa washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 , kutoka Kanda Maalum ya Zanzibar akitoa Shukurani kwa niaba ya Warembo wenzake
Muheshimiwa Jerry Silaa Akizungumza na Washiriki wa Miss Utalii Tanzania
kwa picha zaidi bofya read more
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania Taifa 2012/13 wakiwa katika Picha ya pamoja na Muheshimiwa Meya wa Manispaa Jerry Silaa

Matamasha ya Airtel Yatosha kufanyika Nchi Nzima

$
0
0

 kiongozi wa Tip Top connection Bwana Madee  moja ya kikundi kitakachotumbuiza katika Matamasha ya Airtel Yatosha akiongea wakati wa uzinduzi wa Matamasha hayo yaliyofanyika katika ofisi za Airtel morocco, Matamasha haya yatawashirikisha wasanii wengine wakiwemo Fid Q,   Juma Nature,   Ney wa Mitego  na Stamina.Kulia Meneja Mauzo Airtel  Kanda ya Pwani  Raphael Daudi
Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akiongea wakati akitangaza wa Airtel wa kufany Matamasha ya Airtel Yatosha katika mikoa mbalimbali ya Tanzania yenye lengo la kutoa burudani sambamba na kuelimisha Jamii na wateja  wake kuhusu huduma za Airtel ikiwemo kuitambulisha huduma mpya ya Airtel Yatosha. Kulia Meneja Mauzo Airtel  Kanda ya Pwani  Raphael Daudi
===========  ==========  =======
Matamasha ya Airtel Yatosha  kufanyika Nchi Nzima
·         Tamasha la kwanza litafanyika Morogoro siku ya Jumapili na Jumatatu
·         Zaidi ya mikoa 6 kupata burudani kutoka kwa Wasanii wa kizazi kipya nchini
Airtel Tanzania leo imetangaza mpango wake wa kufanya matamasha ya Airtel Yatosha yenye lengo la kutoa burudani na kuwaelimisha jamii na wateja wake  juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Airtel ikiwemo huduma mpya Airtel Yatosha inayomuwezesha mteja kupiga simu kwenda mtandao wowote kwa gharama nafuu zaidi.
Akiongea wakati wa kutambulisha matamasha hayo, meneja uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando alisema “Airtel tumeamua kutoa burudani wakati wa msimu huu wa sikukuu ikiwa ni pamoja na kuitambulisha huduma yetu ya Airtel yatosha kwa watanzania,  tunaamini kwa kupitia matamasha yatakayofanyika katika mikoa mbalimbali ya Tanzania wateja wetu na watanzania kwa ujumla watapata burudani na kupata nafasi ya kupata elimu juu ya huduma zetu Nyingi
“Safari yetu ya burudani za Airtel yatosha itaanza katika Mkoa wa Morogoro katika siku ya  Jumapili na Jumatatu ya Tarehe 31/3 na 01/04/2013,  Kuanzia Saa Tatu kamili Asubuhi mpaka saa Kumi na Mbili Jioni, pale katika viwanja vya Sabasaba.

Tutakuwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Fid Q,   Juma Nature,   Ney wa Mitego  na    Tip Top Connection. Kiingilio ni BURE , tunapenda kukukualika wewe na washikaji zako wote kuhudhuria katika tamasha hili la kwanza kabisa pale morogoro na utape burudani kabambe. Njoo na Kitambulisho chako ili uunganishwe na ufurahie ofa nyingi toka Airtel” aliongeza Mmbando

Naye kiongozi wa Tip Top connection Bwana Madee  alisema” kama kawaida tumejipanga kuwapa wateja wa Airtel na watanzania burudani ya Ukweli katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, tunaomba watanzania wajitokeze kwa wingi katika matamasha haya ya Airtel Yatosha. Mbali na sisi kutoa burudani itakuwa nafasi pia kwetu kuona vipaji mbalimbali vya mashabiki wetu ambao ndio wasanii nyota wa kesho hivyo tuwapa hamasa ya kujitokeza kwa wingi ili tuweze kuburudika pamoja.

Wasanii watakaoshiriki katika Matamasha maalumu ya Airtel yatosha watatumbuiza kwa vibao vyao mahiri kama vile Fid Q na kibao chake cha Sihitaji Marafiki na  Ney wa Mitego na kibao chake cha Nasema Nao huku Tip Top Connection wakiwakilisha na kibao chao cha Nani kamwaga pombe yangu
Airtel hivi karibuni imezindua huduma ya Airtel Yatosha inayomuwezesha  mtumiaji wa mtandao wa Airtel kupiga simu kwenda mitandao yote kwa gharama ya chini kabisa na hivyo kutokuwa na haja tena ya kubadilisha kadi ya simu pindi anapohitaji kuongea na mtu wa mtandao mwingine.  Mteja anajiunga kwenye huduma hii kwa kupiga *149*99# 

Launch of Mobile Environmental Laboratory Unit

$
0
0
The United Nations Industrial Development Organization (UNIDO) and the Cleaner Production Centre of Tanzania (CPCT) today joined hands in launching a Mobile Environmental Laboratory Unit. This event was officiated by Hon Dr. Terezya Huvisa, Minister of State, Vice President’s Office – Division of Environment. UNIDO has been working with various stakeholders in Tanzania, including the Vice President’s Office – Division of Environment, CPCT and other UN agencies in promoting the concept of Resource Efficient and Cleaner Production (RECP) in Tanzania’s industry.

Hon. Dr. Terezya Huvisa remarked, “The government has started taking a number of steps to implement measures for dealing with environmental degradation and pollution and will continue to support all initiatives which address climate change challenges. In this regard we are very glad that UNIDO and the CPCT have taken this initiative of launching the Mobile Environmental Monitoring Laboratory which will greatly enhance our efforts to closely monitor gaseous and liquid emission and allow for regular feedback to our productive sectors.”

The Mobile Monitoring Laboratory Unit is expected to give quick and precise on-the-spot measurements of liquid and gaseous effluents from industrial or productive operations. This is an initiative that is geared towards waste an increase of industrial productivity while using less energy, water and raw materials so as to significantly reduce waste.

“I am optimistic that with the introduction of this laboratory, our strategies and engagement with the private sector and other stakeholders will be better informed and responsive to the real challenges that impede the green industrial growth that we aspire to realize,” said Mr. Emmanuel Kalenzi, UNIDO Representative in Tanzania.

12 Tanzanians received specialized training on the use of the facility. Hon. Dr. Terezya Huvisa was quick to challenge the new trainees to ensure that their local environments are up to standard and challenged UNIDO and CPCT to look into more areas, including the mining industry, to ensure that there is minimal generation of waste and harmful emissions.

“For quite some time now we have been trying to have a mobile facility for environmental pollution monitoring and performing on-the-spot analysis of industrial effluents and air pollution… We would like to express our sincere gratitude to the UN through UNIDO for the gesture shown in supporting our endeavor to deliver timely and accurate qualitative and quantitative assessments,” said the Executive Director of CPCT, Prof. Cleophas Migiro.
Mobile Environmental Laboratory Unit.


EU Heads of Mission visit to mining operations and local authorities in Northern Tanzania March 26 and 27 2013

$
0
0
EU Ambassadors visited Northern Tanzania on 26 and 27 March. The Ambassadors of the EU, Belgium, Finland, France, Ireland, the Netherlands, Sweden, and the High Commissioner of the UK visited mining operations and local authorities in Kahama (Shinyanga) and North Mara (Mara) and met regional authorities and stakeholders in Mwanza.

The ambassadors had discussions on the business environment and socio-economic developments in the areas that they visited. In the attached picture from left are Steve Kisakye (Corporate Community Relations Manager of African Barrick Gold), Ambassadors Sinikka Antilla (Finland), Lennarth Hjelmaker(Sweden), Filiberto Cerinani Sebregondi (EU), Ad Koekkoek (Netherlands), Dianna Melrose (UK), Koen Adam (Belgium), Fionnuala Gilsenan (Ireland) and Marcel Escure (France) together with Deo Mwanyika (Vice President African Barrick Gold).

Airtel Tanzania YATOSHA

DR BILAL IMPRESSED BY COSTECH'S DTBI

$
0
0
 The Vice President listens to an entrepreneur on digitizing Swahili Science Books
 Eng. George Mulamula introduces the Vice-Chair of DTBi to the Vice President
 The Vice President of the United Republic of Tanzania, Dr. Mohamed G. Bilal  listening to Eng. George Mulamula, CEO of Dar Teknohama Business Incubator (DTBi)  explain the achievements of the Incubator. On his right is the Minister of Communication, Science & Technology, Prof Makame Mbarawa and on his left is the Director General of COSTECH, Dr. Hassan Mshinda
    DTBi Board Members Ms. Rosemary Mwakitwange & Mr. Mihayo Wilmore being introduced to the Vice President

 First Access explaining to the Vice President their programme that assists Micro Finance Institutions give loans to low income people without collateral but based on their phone usage
Vincent of Day One explain how his software application has helped Local Government Authorities in Dar es Salaam increase revenue collection by over 300% in about one year

 Young Innovator Godfrey Magila showing the Vice President how Technology can change how Politics and Parliament works by  fusing Social Media, Real Time Citizens Opinions, and Technology.Godfrey's company Magila Tech is a Member of the DTBi, who was one of the best young entrepreneurs at the recently held ITU exhibition in the Middle East

The Vice President, Dr. Mohamed Gharib Bilal giving a statement to the Press, saying he is impressed by what DTBi is doing and encourage more innovators to come out in plenty to capitalize on COSTECH's initiative.


Breaking Newzzzzzzzz:Mbunge wa Chambani Salim Hemed Khamis,afariki dunia mchana huu.

$
0
0
Pichani ni Baadhi ya Maofisa wa Ofisi Ndogo ya Bunge,wakimsaidia kwa kumbeba Mbunge wa Chambani,Bwa.SalimHemed Khamis,mara baada ya kuanguka ghafla hapo jana jijini Dar akiwa katika vikao vya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kukimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu ya haraka.
=======  ======  ======
Habari  zilizoifikia Globu ya Jamii hivi punde inaelezwa kuwa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Chambani-Pemba, Salim Hemed Khamis,ambaye hapo jana alianguka ghafla jijini Dar Es Salaam alipokuwa akihudhuria vikao vya kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kukimbizwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu, amefariki dunia muda mfupi uliopita katika Hospitali hiyo ya Taifa ya Muhimbili,aidha chanzo cha habari hizi kimeongeza kuwa taratibu za kuusafirisha mwili wa Marehemu kuelekea Pemba kwa mazishi zinafanyika.Tutazidi kuwafahamisha zaidi kadiri ya habari zitakavyokuwa zikiingia.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema Peponi-Amin 


MABADILIKO RATIBA YA KIFO CHA MBUNGE WA CHAMBANI

$
0
0

Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda, (Mb) anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Chambani, Pemba, Mhe. Salim Hemed Khamis (CUF) - pichani -kilichotokea leo mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Marehemu Khamis, alilazwa jana katika Hospitali hiyo baada ya kuanguka ghafla akishiriki vikao vya kamati za Bunge vinavyoendelea katika Ofisi Ndogo ya Bunge, Dar es Salaam.


Marehemu ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, alikimbizwa Hospitalini na kulazwa katika chumba cha wagonjwa Mahututi Muhimbili baada ya kubainika kuwa alikuwa amepata kiharusi kufutia shinikizo la damu lililopelekea kuanguka kwake ghafla akiwa katika majukumu yake katika Kamati za Bunge. Kutokana na Msiba huu, Shughuli zote za Kamati za Bunge zimearishwa hadi jumanne tarehe 2 Aprili, 2013.


Marehemu ataangwa kesho tarehe 29 Machi, 2013 saa mbili na Nusu Asubuhi katika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam na kusafirishwa kwa ndege kwenda Pemba Saa Nne Asubuhi ambapo Mazishi yatafanyika nyumbani kwake Chambani, Pemba Mchana. Mhe. Spika anatoa Pole kwa Familia ya Marehemu, wananchi wa Chambani, Wajumbe wa Kamati ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Wabunge wote na Watanzania wote kwa ujumla.


Mungu alilaze Roho ya Marehemu, Mahali Pema Peponi, Amina!


Imetolewa na

Idara ya Habari, Elimu Kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa

Ofisi ya Bunge

DAR ES SALAAM

28 Machi, 2013

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali akabidhi ripoti ya 2011-2012 leo

$
0
0
 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Bwana Ludovick Utouh akikabidhi Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2011-2012 kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo. Picha na Freddy Maro

IGP Mwema afungua Programu ya Mafunzo kazini kwa askari wote nchini

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema, wapili kutoka kushoto akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa Programu ya Mafunzo kazini kwa askari wote nchi nzima yaliyofanyika jijini Dar es salaam, akifuatiwa na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam DCP Suleiman Kova, Mkuu wa chuo cha Taaluma ya Polisi (DPA) ACP Ally Lugendo na kushoto ni Mkuu Kitengo cha wa Mafunzo SACP Alice Mapunda.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema akikagua program ya Mafunzo kazini kwa wakaguzi wa Polisi pamoja na askari, ukaguzi huo ulifanyika Makao makuu ya Polisi jiji Dar es salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema, akiwa na maofisa wa Polisi wakifuatilia kwa karibu uzinduzi wa program ya mafunzo kazini kwa kutumia mtandao, tukio hilo lilifanyika jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema akikagua Utekelezaji wa Programu ya mafunzo kazini kwa maofisa wa Polisi( kushoto ni Msemaji wa Jeshi la Polisi Advera Senso), ukaguzi huo ulifanyika Makao Makuu ya Jeshi Polisi ( picha na Frank Geofray- Jeshi la Polisi) .

Balozi mpya wa UAE Mhe.Abdulla Ibrahim Al Sowaidi awasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais Kikwete leo

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati za utambulisho kutoka kwa balozi mpya wa Muungano wa Falme za Kiarabu UAE,Mhe.Abdulla Ibrahim Al Sowaidi ikulu jijini Dar es Salaam leo.Katikati anayeshuhudia ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Juma Maharage.(picha na Freddy Maro).
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images