Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

DKT. SHEIN AFANYA ZIARA MAENEO YALIYOKUMBWA NA MAAFA YA MVUA, ZANZIBAR

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na wasaidizi wake alipofika Uwanja wa Farasi na Kwahani Mjini Zanzibar leo wakati alipofanya ziara ya hafla kutembelea wananchi wa sehemu hiyo waliopatwa na maafa ya kuingiliwa na maji ya mvua iliyonyesha juzi na kupelekea maafa yaliyosababisha kukosa makaazi bora.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wananchi wa Uwanja wa Farasi na Kwahani Mjini Zanzibar wakati alipofanya ziara ya hafla leo kutembelea wananchi wa sehemu hiyo waliopatwa na maafa ya kuingiliwa na maji ya mvua iliyonyesha juzi na kupelekea maafa yaliyosababisha kukosa makaazi bora.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Injinia Ramadhan China wa Idara ya Ujenzi wakati alipofanya ziara ya hafla leo kutembelea Maeneo ya Mwanakwerekwe Mjini Unguja kuangalia maafa mbali mbali yaliyowakumba wananchi wa sehemu hiyo kwa kuvunjikiwa na nyumba zao kutokana na mvua kubwa iliyonyesha juzi na kupelekea hasara mabali mbali.


Attorneys from Rex Attorneys join forces with ENSafrica in Tanzania

DC WA MISSENYI AWAPATIA MATIBABU YA BURE WATU WENYE UALBINO

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mh. Fadhil Nkurlu akimpatia mmoja wa walemavu wa ngozi kadi za afya zitakazowawezesha kupata matibabu bure wao pamoja na wategemezi wao katika vituo vya huduma za afya za serikali na zile binafsi vilivyosajiliwa na mfuko wa afya ya jamii (CHF).
Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mh. Fadhil Nkurlu (wa nne kutoka kulia walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na walemavu wa ngozi pamoja na viongozi wa dini na serikali za mitaa wilayani Missenyi.

MAKALA YA SHERIA: UNANUNUAJE NYUMBA/KIWANJA BILA KUJIRIDHISHA NA HATUA HII?

0
0
Na  Bashir  Yakub.
Mara  nyingi  nimeandika  kuhusu  ardhi  hususan   viwanja  na  nyumba.  Katika  kufanya  hivyo  mara  kadhaa  nimejaribu  kuwatahadharisha  watu namna  mbalimbali  ya  kisheria ya kuepuka   kuingia  katika  migogoro  ya  viwanja  na  nyumba  hasa  wakati  wa  kununua( wanunuzi). 

 Nimewahi  kueleza  namna  au  vitu  vya  msingi ambavyo  hutakiwa  kuwa  katika  mkataba  wa   ununuzi  wa  nyumba  au  kiwanja. Nikaeleza  umuhimu  wa  kila  kimoja   na nikasisitiza  kuwa  atayekuwa  amenunua  ardhi na  mkataba  wake  ukajaaliwa   kuwa  na  vitu  hivyo  basi  si  tu  atakuwa  amefanya  manunuzi  bora  lakini  pia  atakuwa  amefanya manunuzi  yanayokubalika  kisheria. 

Ifike  hatua  watu waelewe kuwa  migogoro  mingi  ya  ardhi  huanzia  na  kutokuwa makini kwenye  manunuzi. Kutokupata  ushauri  wa  kisheria   ikiwa  ni  pamoja  na  kutopitia  hatua   za  msingi za kisheria  kabla  ya  manunuzi,  kuandikiwa  mikataba ya  manunuzi  isiyokidhi  vigezo  vya  kisheria  ikiwemo  ile  ya  serikali  za  mitaa  ambayo  hairuhusiwi  kabisa kisheria  ni  kati  ya sababu chache  kati  ya  nyingi  zitakazokupelekea  uingie  katika  mgogoro.  Leo  nitaeleza  hatua  moja   ya  msingi  sana  ambayo  hutakiwi ufanye  manunuzi  ya  ardhi  bila  kuipitia.

 1.HATUA  TANO  ZA  KUFUATA   UNUNUAPO   NYUMBA/KIWANJA.  

Ziko  hatua  tano  muhimu  za  kupitia  pale  unapo kuwa  katika  mchakato  wa    kununua  ardhi. Umuhimu  wa  hatua  hizi  ni  kuwa  kwanza  kabisa  si  rahisi  kujikuta  katika  mgogoro  unapokuwa    umezipitia.  Lakini  pili  hata  bahati  mbaya   utokee  mgogoro   basi  wewe  uliyepitia  hatua  hizo  utakuwa  salama  na  kama  ni  kesi  basi  wewe  upo  katika  mazingira  mazuri  ya  kushinda.  Hatua  ya  kwanza  huitwa  hatua  kabla  ya  mkataba( pre contractual  stage).  

Hatua  hii inayo  mambo  yake  ya  msingi  na  ya  kisheria     ambayo  kuyafuata  kwako  kwaweza  kukuweka  mbali  na hatari  ya  kununua  ardhi  yenye  mgogoro  au  itayokuingiza  katika  mgogoro  . Hatua  hii  ndiyo  nitakayoeleza   kama  msingi  wa  makala  ya  leo  kama  tutakavyoona.  Kabla  ya  kueleza  hatua  hiyo  ni  vema  pia  nikazitaja  hatua  nyingine   japo  kwa  ufupi. Hatua  ya pili  huitwa  hatua  ya  mkataba( contractual  stage). Hii  ni  hatua  ya  kupitia  na  kujiridhisha  na  mkataba    wa  manunuzi  ikiwa  ni  pamoja  na  kuusaini. Hatua  ya  tatu  huitwa  “pre completion  stage”,  hatua  ya nne  huitwa  hatua  ya  kumalizia ( completion stage)  na  hatua  ya  tano  na  ya  mwisho  huitwa  hatua  baada  ya  kumalizia ( post  completion  stage). 

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay aanza kutekeleza ahadi

0
0
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay, Zefrin Lubuva (kushoto) akikabidhi fedha kwa Katibu wa Shina la CCM Morogoro Store, Ramadhan Abdallah, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya kutunisha mfuko na kukihimarisha chama kuelekea kwenye uchaguzi mkuu 2015.Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Shina la CCM Morogoro Store,Majibu Joseph.

ngoma azipendazo ankal special request by jane mihanji

0
0

Ottu Jazz Band - Asha Mwana Seif

Kiota Kipya cha maraha ndani ya Bunju, jijini Dar es salaam

0
0
Posto Bella Resort, Kiota Kipya cha maraha pande za  ya Bunju jijini  Dar es salaam.

Chimbo jipya kwa jina La Posto Bella Resort limefunguliwa nje kidogo ya mji wa Dar. Kwa wale wanaopenda maeneo private, utulivu na salama, hakuna haja ya kuumiza kichwa. 

Kama inavyoonekana kwenye picha, pana garden nzuri iliyotengenezwa kwenye miinuko ya Bunju A, 1.2km toka Bagamoyo road, njia ya kuingia DogoDogo Centre, ikipata upepo baridiii unaotokea bahari ya Hindi. 
Ni mazingira ya kiutu-uzima na kimahaba, hakuna kelele za aina yoyote isipokuwa ndege wanaoruka mitini tuu, hakuna boda boda wala honi za magari. Kwa mazingira ya chimbo hili, anayekutafuta lazima atumie GPS!
Ni muafaka kwa ajili ya watu wanaotafuta privacy kama wapendanao, mikusanyiko ya kifamilia (family gatherings), harusi za watu wachache, sherehe za kiofisi (corporate parties), birthdays, mitoko ya ki-group cha kazini, engagement parties, kitchen parties, na mengineyo mengi. Ukumbi (garden yetu) ni bure, hatutozi hela yoyote. Pia ni mahali muafaka kwa mitoko ya familia kwa ajili ya lunch na dinner siku za weekend.
Bei zetu za vinywaji na chakula ni za kawaida sana. Kwa maelezo zaidi tupigie 0652036191 or 0719222234 au email: postobellaresort@gmail.com

Picha zaidi tucheki kwenye facebook page yetu www.facebook.com/PostoBellaResort na kwenye Instagram: @posto_bella. Tafadhali tu-follow kwenye instagram uweze kupata habari za matukio mbali mbali kila mwezi.
Posto Bella is like Nowhere in Dar!
Kijani ya kupendeza yatawala eneo la kiota hicho.

MEYA MWENDA WA KINONDONI ASHINDA TUZO YA MEYA BORA AFRIKA

0
0
Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam

Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda ameshinda Tuzo ya Meya Bora katika Bara la Afrika katika kundi la Majiji ya Kati na kuyabwaga majiji mengine mbalimbali.

Tuzo hizo zilizoandaliwa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (The United Cities and Local Government of Africa- UCLGA) na kupewa jina la Rais wa Angola ‘President Jose Eduardo Dos Santos- Africa Mayors Award’ ni za mara ya kwanza kufanyika Barani Afrika.

Tofauti na Tuzo za Tanzania, Tuzo hizi za Afrika zinahusika na Mamlaka ya miji tu.

Tuzo hizi zilikuwa ni katika makundi matatu ambayo ni Tuzo za Majiji Makubwa (Large Size Cities), Tuzo za Majiji ya Kati (Medium Size Cities) na Tuzo za MajijiMadogo (Small Size Cities).

Tuzo za Majiji Makubwa (Large Size Cities) zimekwenda jijini Accra, Ghana wakati zile za Majiji madogo zimechukuliwa na Praia katika visiwa vya Cape Verde.

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ilishiriki mashindano ya Tuzo za Meya (Halmashauri Bora za Afrika baada ya kushinda Tuzo za Meya/ Halmashauri Bora Tanzania zilizoandaliwa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT).

Miradi iliyoshindanishwa kutoka Manispaa ya Kinondoni ni pamoja na ukusanyaji wa mapato na kituo cha Mabasi Sinza. Hata hivyo Manispaa ya Kinondoni ilipimwa katika vigezo vyote vilivyoanishwa na UCLGA.

Zawadi zilizotolewa ni kikombe, Cheti na Fedha tasilimu kiasi cha Dola za Kimarekani 100,000 ambazo sawa na shilingi milioni 200.

Majiji mengine yaliyoshinda yalipata Dola za Kimarekani 200,000 (Sawa na shilingi Milioni 400) kwa Miji Mikubwa na Dola za Kimarekani 50,000 (sawa na shilingi milioni 100 kwa Miji midogo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Hawa Ghasia akikabidhi Tuzo ya Meya/ Halmashauri Bora katika Bara la Afrika Kundi la Majiji ya Kati (Medium Size Cities) zilizotolewa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (UCLGA), kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Hawa Ghasia akikabidhi cheti cha Meya/ Halmashauri Bora katika Bara la Afrika Kundi la Majiji ya Kati (Medium Size Cities) kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda katika hafla iliyo zilizotolewa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (UCLGA), Dar es Salaam jana.


DC wa Kinondoni Mhe. Paul Makonda alivyohitimisha mgomo wa madereva Ubungo, Dar es salaam

TANZANIA PASSPORT RENEWAL IN THE US – 2015

0
0
Dates: May 9 – 10, 2015 (Saturday & Sunday)

Location: 591 N. Main Street Alpharetta GA 30009

Fees: $70 Money Order (Passport Fees & FedEx return)

Service Cost: $30/person.

All Tanzanians living GA, AL, SC, NC, TN, FL & nearby states are welcome.

For more information and requirements visit: http://tanzaniaembassy-us.org/?page_id=79


RSVP to guarantee spot: http://bit.ly/1JMQ5q1

Raia watatu wa kigeni watiwa mbaroni kwa wizi wa mitandao

WAKUNGA WAHIMIZWA KUSHIRIKIANA KUTENGENEZA TAIFA LA KESHO

0
0
DSC_0228
Rais wa chama cha wakunga nchini (TAMA), Feddy Mwanga akimkaribisha Ofisa Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wakunga duniani, Frances Ganges (kulia) kuzungumza na wakunga nchini waliokusanyika kwenye mdahalo wa siku moja kuelekea sherehe za kilele cha maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani ambapo kitaifa imefanyika mjini Musoma mkoani Mara. Kushoto ni Kaimu Muuguzi mkuu wa serikali kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Ama Kasangala. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na Mwandishi wetu, Musoma
Ofisa Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya wakunga duniani, Frances Ganges, ametoa wito wa wakunga na wauguzi kubadilisha uzoefu wa shughuli zao ili kuhakikisha taifa linaondokana na vifo vya wanawake wajawazito na watoto.

Akizungumza katika mdahalo kuelekea sherehe za kilele cha maadhimisho ya siku ya wakunga duniani, iliyofanyika kitaifa mkoani Mara, Ganges alisema kwamba ni wajibu wa wakunga kuhakikisha kwamba dunia ya kesho inakuwa bora na wanaweza kwa kushirikiana na kubadilishana uzoefu.

Alisema dunia inawategemea wauguzi kuendeleza kizazi cha binadamu na katika kufanya hivyo kuna changamoto nyingi zinazotokea changamoto ambazo zinaweza kumalizwa kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake katika eneo analofanyia kazi.

Aliutaja wajibu huo kama uongozi, uelimishaji na pia utendaji wa kazi wenye tija na busara.
Alisema nia ya siku ya wakunga ipo wazi ni kuleta ushirikiano kwa ajili ya kuleta dunia iliyo njema ya kesho.

Mtendaji huyo wa Shirikisho hilo lenye makao makuu yake nchini Uholanzi alisema kwamba wanafuraha kubwa kusikia mambo makubwa yanayofanywa na wakunga nchini Tanzania pamoja na changamoto zake zilizopo.
Alisema mafanikio yaliyopo ni matokeo ya ushirikiano na ufanyaji kazi wa pamoja.
DSC_0247
Ofisa Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wakunga duniani, Frances Ganges akizungumza na Wakunga nchini Tanzania waliohudhuria kwenye mdahalo wa siku moja uliofanyika kwenye ukumbi wa Mara ofisi za Mkuu wa mkoa wa Mara mjini Musoma kuelekea kilele cha sherehe za maadhimisho ya siku ya Wakunga duniani kujadili changamoto zinazowakabili Wakunga nchini. Katikati ni Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA), Feddy Mwanga na Kushoto ni Kaimu Muuguzi Mkuu wa Serikalim kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Ama Kasangala.

COSTECH in Partnership with US Embassy Dar es Salaam award winners of the Powering Africa Research Paper Competition

0
0
May 5th, 2015, The Tanzania Commission for Science and Technology (COSTECH) in partnership with the US Embassy Dar es Salam have awarded a total amount of 15,000 USD to the Winners of the Powering Africa Research Competition in a special ceremony at COSTECH Head quarters Kijitonyama Dar es Salaam

This is one of the measures towards realizing Power Africa initiative, the programme that was announced in 2013 by President of the US, Mr. Barrack Obama when he visited Tanzania.

Jury Chairperson of the Competition Prof Prosper Ngowi from Mzumbe University said the main objective of the competition was for the University students to address the potential impact of power availability, demand, supply as well as consumption in the selected regions as a reflection of economic and social development by 2025.

He said the Competition was for undergraduate students for the three selected regions and three Universities located in those regions.

Delivering a speech on behalf of the Permanent secretary in the Ministry of Communication, Science and Technology, the Director of Science and Technology in that Ministry Prof Evelyn Mbede said the US State Department –US Embassy of Dar es Salaam together with COSTECH have demonstrated an innovative way to address future scenarios using research.
The Guest of Honor, Director of Science and Technology from the Ministry of Communication Science and Technology, Prof Evelyn Mbede delivers a speech during the Award Ceremony at COSTECH.

She also said it was more common to solve current problems using research than looking into research to solve future challenges.

She maintained that youths should receive the correct guidance to take on the challenges and leverage opportunities of development and reminded about the role of higher learning institutions

“I urge all higher learning Institution in Tanzania to use student projects to analyze and research on the varied challenges that face the respective regions where they occur, the communities and nation as a whole.”She remarked.
The Guest of Honour, Director of Science and Technology from the Ministry of Communication Science and Technology, Prof Evelyn Mbede(Centre)Smiles when handing over a Cheque worth 1500 USD to Mr Cralence Nyanga(in a Black Suit) and Ms Labule Beatrice from St Augustine University of Tanzania. Looking on is a Power Africa Tanzania Inter-Agency Coordinator Ms. Sharon Pauling and Prof Ngowi from Mzumbe.

Marekani na Tanzania zazindua Program ya Mbwa Maalum wa kubaini Dawa za kulevya na Pembe za ndovu

0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii,.Mhe. Lazaro Nyalandu ( katikati) akiwa na Kamishna wa Idara ya Forodha na Ulinzi wa Mipaka ya Marekani R. Gil Kerlikowse( wa pili kushoto) pamoja na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Bi. Virginia Blaser ( wa kwanza kushoto) wakiwa katika uzinduzi wa Program ya Mbwa maalumu kubaini dawa za kulevya na pembe za ndovu uliofanyika katika Bandari ya Dares Salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Lazaro Nyalandu akizungumza katika uzinduzi wa Program ya Mbwa maalumu kubaini dawa za kulevya na pembe za ndovu, akiwa na Kamishna wa Idara ya Forodha na Ulinzi wa Mipaka ya Marekani R. Gil Kerlikowse( wa kwanza kulia). Wengine ni Kaimu Balozi wa Marekani nchini Bi. Virginia Blaser ( katikati) akiwa na Eng. Mathayo.
Kamishna wa Idara ya Forodha na Ulinzi wa Mipaka ya Marekani R. Gil Kerlikowse ( wa kwanza kulia). akizungumza wakati wa uzinduzi wa Program ya Mbwa maalumu kubaini dawa za kulevya na pembe za ndovu. akiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Lazaro Nyalandu ( wa pili kulia) . Wengine ni Kaimu Balozi wa Marekani nchini Bi. Virginia Blaser ( wa pili kushoto) akiwa na Eng. Mathayo.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Lazaro Nyalandu wakiwa katika picha ya pamoja na Kamishna wa Idara ya Forodha na Ulinzi wa Mipaka ya Marekani R. Gil Kerlikowse akiwa ameinama amemshika mbwa( wa tatu kulia ) pamoja na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Bi. Virginia Blaser ( wa tatu kushoto) w uzinduzi wa Program ya Mbwa maalumu kubaini dawa za kulevya na pembe za ndovu uliofanyika katika Bandari ya Dares Salaam.

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAKUNGA DUNIANI YALIVYOFANA MJINI MUSOMA

0
0
DSC_0056
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya uuguzi mkoani Mara wakijiaanda kuanza maandamano kutoka Hospitali Hospitali ya Rufaa mkoa wa Mara wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani ambapo kitaifa yamefanyika wilayani Musoma.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
DSC_0060
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya uuguzi wilayani Musoma wakiwa wamekusanyika nje ya Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara kwa ajili ya maandamano ya kuadhimisha Siku ya Wakunga Duniani ambapo kitaifa yamefanyika mjini Musoma kwenye viwanja vya Mkendo, mkoani Mara.
DSC_0086
baadhi ya Wakunga kutoka mikoa mbalimbali ya nchini wakijumuika na wenyeji wao kwenye maandamano ya maadhimisho hayo.
DSC_0103
Baadhi ya Wakunga wakijumuika na wakinama wa mjini Musoma njiani kuelekea kwenye viwanja vya Mkendo wakati maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga duniani burudani ya matarumbeta yaliyokuwa yakishereheshe maandamano hayo.


HAPA VIPI WADAU??

WANANCHI NA TAASISI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI WANAPOTAKA KUPIMA MAENEO YAO YA ARDHI KUEPUKA KUTAPELIWA

0
0
Mkurugenzi Msaidizi wa Upimaji na Ramani vijijini wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Huruma Lugalla (kushoto) akitoa maelekezo kwa wataalam wa Upimaji na Ramani wa wizara hiyo wakati wa uhakiki wa moja ya ramani ya eneo linalopaswa kuwa la makazi ya watu na taasisi nje kidogo ya mji wa Chalinze, Bagamoyo mkoani Pwani iliyopimwa na Kampuni ya Intergrated Property Consultancy and Services (IPCS) ya Morogoro na kubainika kuwa chini ya kiwango.
Wataalam wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakifanya uhakiki wa moja ya ramani ya eneo linalopaswa kuwa la makazi ya watu na taasisi nje kidogo ya mji wa Chalinze, Bagamoyo mkoani Pwani lililopimwa chini ya kiwango. Katikati (aliyesimama) ni Bw. Bernard Malugu, Mkurugenzi wa Kampuni ya Intergrated Property Consultancy and Services (IPCS) ya Morogoro iliyoifanya kazi hiyo chini ya kiwango.
Mkurugenzi Msaidizi wa Upimaji na Ramani vijijini wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Huruma Lugalla (kushoto) akifuatilia moja ya eneo ambalo lilitakiwa kuwa na alama ya mpaka ambalo halikuwa na alama yoyote wakati wa uhakiki wa moja ya ramani ya eneo linalopaswa kuwa la makazi ya watu na taasisi nje kidogo ya mji wa Chalinze, Bagamoyo mkoani Pwani iliyopimwa na Kampuni ya Intergrated Property Consultancy and Services (IPCS) ya Morogoro ambayo ilibainika kuwa chini ya kiwango. Kulia ni Bw.Allex Kachoka Mpima Ardhi wa wizara hiyo.

TFF yaiagiza Klabu ya Coastal Union kuitisha mkutano mkuu wa dharura wa wanachama

0
0
KUFUATIA vikao vya maridhiano ya Uhakiki wa wanachama wa Klabu ya Coastal Union ulioongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la soka nchini (TFF) Ahmed Iddi Mgoyi.

Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine ameiandikia barua Klabu ya Coastal Union akiiagiza klabu hiyo kuitisha mkutano mkuu wa dharura wa wanachama tarehe 17 Mei mwaka 2015.

Matokeo ya maamuzi haya yamepatikana baada ya kikao cha usuluhishi cha amani kilichoongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Ahmed Iddi Mgoi aliyekuwa ameongozana na Makamu Mkurugenzi wa Sheria na Uanachama shirikisho la soka nchini (TFF) Eliud Peter Mvella kilichofanyika April 13 mwaka huu katika hotel ya Tanga Beach Resort Tanga mjini.

TFF imehaidi kutuma orodha tatu za majina 
(A) Wanachama stahiki. 
(B) Wanachama waliobainika kuwa wanadosari na inabidi wathibitishwe na wanachama stahiki naa.
(C) Waombaji wapya wa wanachama watakaohakikiwa na wanachama stahiki.

Orodha hizi zinapaswa kubandikwa kwenye ubao wa Matangazo wa Klabu, katika kikao cha ufunguzi cha kuleta usuluhisho huo, mbali na kuhudhuriwa na kamati ya Utendaji ya Coastal Union chini ya Makamu wake Mwenyekiti Steven Mguto pia kilihudhuria na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF,Khalid Abdallah, Mwenyekiti wa Chama cha soka Mkoa wa Tanga,Said Soud.

Wengine waliohudhuria kikao hicho walikuwa ni Afisa Michezo wa Mkoa wa Tanga, Digna Tesha, Katibu wa Chama cha soka Mkoa wa Tanga, Beatrice Mgaya, Afisa Utamaduni Jiji la Tanga, Peter Semfuko na Katibu wa Chama cha soka wilaya ya Tanga (TDFA) Salim Carlos.

Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Coastal Union.
Oscar Assenga.

bei ya Madafu leo

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 06.05.2015

Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images