Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 826 | 827 | (Page 828) | 829 | 830 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Dear invited quests.On Thursday 14 May 2015. The Vijana Vipaji Foundation is going to have an opening of a painting exhibition by Paul Ndunguru and Mac Saway. On the same day Vipaji Gallery will be turning one year old and the Vijana Vipaji is kindly welcoming you to celebrate the art, the culture and the creative mind of the Tanzanian Artists. See the attached invitation card and the flier for the inter time of exhibition. Best regards, Emmanuel Mathias VVF Project Coordinator.
  0 0


  Makadam na Prasad wakiwajibika
  Wapenzi wakipigishwa mpumwende.

  Baada ya ziara ya mafanikio ya mwezi mmoja mjini Addis Ababa, bendi ya Swahili Blues chini ya uongozi wa Leo Mkanyia imefanya ziara nyingine mjini Nairobi.

  Bendi hiyo yenye maskani yake katika hoteli ya nyota tano ya Serena iliyo katikati ya mji wa Dar es Salaam ilianza ziara yake katika klabu maarufu inayojulikana kama Choices iliyopo katika barabara ya Baricho kwenye kitongoji cha Industrial Area. Shoo hiyo kabambe ilifanyika siku ya tarehe 23 April 2015 chini ya usimamizi wa kampuni maarufu ya Roots International katika mradi maalumu uliojulikana kama Thursday Nite Live @Choices kwa udhamini wa Tusker Malt Lager.
  Shoo hii ilifana vilivyo na wapenzi lukuki waliohudhuria walikunwa kisawasawa na mirindimo kabambe toka kwa Swahili Blues Band. Wapenzi hao pamoja na kukunwa ipasavyo na umahiri wa Leo vilevile walifurahishwa sana na mwimbaji pamoja na mpiga ngoma Juma Setumbi. Kwa habari zaidi juu ya shoo hii tafadhali tembelea tovauti hiiwww.facebook.com/thursdaynitelive.

  Siku ya tarehe 24 April, bendi ilifanya shoo yake ya pili katika ukumbi ujulikanao kama "At The Elephant" uliopo barabara ya Kanjata maeneo ya Lavington. Siku hiyo bendi ilipiga kabla ya mwanamuziki maarufu wa Kenya anayeitwa Dan 'Chizi' Aceda. Shoo hii nyingine kabambe iliandaliwa na mwanamuziki na mmiliki wa klabu hii aitwaye Eric Wainaina.Ilikuwa ni onyesho nyingine kabambe kweli kweli ambapo Leo, Henry Mkanyia na Felix Kijana walioonyesha umahiri mkubwa wa kusakata sindimba wakati walipo yaacha magitaa yao pembeni na kuanza kunengua ipasavyo. Mpumwende huu ulidhaminiwa na Nederburg pamoja na Culture Connect.

  Siku ya Jumamosi ya tarehe 25 April bendi ilihamia katika ukumbi maarufu wa wasanii ujulikanao kama " The GoDown Arts Centre". Huo ulikuwa ni mpango maalumu wa kituo hicho kualika bendi mbalimbali kutoka Afrika Mashariki ambapo siku hiyo Nyota Ndogo na Kidum walibambisha sana tu. Ilikuwa ni jioni njema iliyojaa vionjo mbalimbali ambapo Kidum alipagawisha na miondoko yake iliyompatia umaarufu katika ukanda wote huu wa Afrika Mashariki. Nyota Ndogo naye akatupia nyimbo zake maarufu kama vile Nibebe na Watu na Viatu zenye miondoko ya pwani.

  Hii ilikuwa ni fursa nyingine kwa Wakenya kupata mpumwende kutoka mirindimo ya makabila ya Kitanzania kama vile Wagogo, Wayao, Wamakonde na Wazaramo kupitia nyimbo kama Afrika, Che Maria, Shikandambwe, Mdundiko na Aichelelo. Hakika ilikuwa ni nafasi nyingine kwa utamaduni halisi wa Mtanzania kutangazwa bila ya aibu nje ya nchi yetu.

  Shoo iliyofuata ilifanyika siku ya Ijumaa ya tarehe 1 May katika ukumbi mpya na wa kisasa ujulikanao kama Roof Top SunDowner uliopo maeneo yanayo karibiana na Ikulu hukoo Hullingham. Katika onyesho hili Leo alishirikiana vilivyo na wanamuziki maarufu wa Kenya wanaopiga vyombo kama vile Makadem ambayo anaimba na kupiga chombo cha asili kiitwacho Nyatiti. Vilevile alikuwepo mwanamuziki mkongwe Prasad ambaye anakung'uta ngoma za kiasili kutoka Bara Hindi zinazojulikana kama tabla. Ulikuwa ni mchanganyiko maalumu ambao wapenzi walifaidi kiingilio chao kikubwa walicho lipa ili kuona onyesha hilo kabambe na maalumu kabisa.

  Katika mahojiano na Leo yaliyofanyika baada ya shoo hii, alieleza kuwa ziara hii imekuwa ni ya ya mafanikio ya hali ya juu sana na ameridhika na matokeo ya ziara hii.
  "Matokeo ya ziara hii ni mazuri na makubwa sana. Mathalani, katika ziara hii nimeongeza wigo wa kufahamiana na wadau mbali mbali kutoka mataifa mengi zaidi. Faida nyingine ni kuweza kushirikiana na wanamuziki wengi zaidi wenye hadhi ya kimaitafa na nina shukuru kwa wao pia kupenda kazi yangu." alieleza Leo.


  0 0


  OTTU Jazz Band Kilio Cha Mtu Mzima

  0 0


  TAREHE 5 - MEI - 2015, UMETIMIZA MIAKA MITANO TANGU MWENYEZI MUNGU ALIPOKUTWAA TOKA HAPA DUNIANI.  PAMOJA NA KWAMBA KIMWILI HAUPO NASI, KIROHO TUNAKUKUMBUKA DAIMA.

  UNAKUMBUKWA DAIMA NA WATOTO WAKO FLORIDA, ILLUMINATA, LIBERATA, DUNSTAN, JOYCE NA EDWIN PAMOJA NA WAKWE, WAJUKUU, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI.


  IBADA YA MISA YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU MWALIMU RUTAGERUKA ITAADHIMISHWA SIKU YA JUMANNE TAREHE  5 - MEI - 2015, KATIKA KANISA LA MTAKATIFU JOSEPH, DAR-ES-SALAAM, SAA 11.30 JIONI.


  BWANA ALITOA, BWANA ALITWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE. AMINA


  0 0
  0 0


  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Mhe. Dkt. Aziz Ponary Mlima akiwa  na mkewe Mama Mkola Mlima pamoja na Wafanyakazi wa Ubalozi wakiwapokea wageni waalikwa kwenye maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Ubalozi wa Tanzania nchini humo uliandaa sherehe fupi kuuenzi Muungano.
  Balozi Mlima akitoa hotuba fupi wakati  wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
  Balozi Mlima akikata keki kuadhimisha miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Anayeshuhudia ni Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo ambaye ni Naibu Waziri wa Biashara ya Kimataifa na Viwanda wa Malaysia, Seneta Deto' Lee Chee Leong.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Askari wakisaidia kushusha kwenye gari mabati yaliyotolewa msaada na Kampuni ya Konyagi ya  Tanzania Distilleries Limited (TDL), kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi Chang’ombe, kitengo cha upelelezi. Hafla ya utoaji wa vifaa vya ujenzi vikiwemo pia saruji, misumari na fedha ya mafundi vilikabidhiwa jana katika kituo hicho kilichopo Temeke, Dar es Salaam.
   Askari wakisaidia kushusha kwenye gari mabati yaliyotolewa msaada na Kampuni ya Konyagi ya  Tanzania Distilleries Limited (TDL), kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi Chang’ombe, kitengo cha upelelezi. Hafla ya utoaji wa vifaa vya ujenzi vikiwemo pia saruji, misumari na fedha ya mafundi vilikabidhiwa jana katika kituo hicho kilichopo Temeke, Dar es Salaam.
   Inspekta John Mkweru (kushoto) akiangalia msaada wa misumari uliotolewa na Konyagi kwa kituo hicho.


  0 0  0 0

  TAARIFA KWA UMMA

  UFAFANUZI KUHUSU TUHUMA ZA UBADILISHAJI WA MATOKEO YA MITIHANI

  Utangulizi:

  Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa zilizoenea katika mitandao ya kijamii hususan Facebook na WhatsApp zilizoainishwa kama “Tuhuma Nzito katika Tasnia ya Sheria”. Kwa ufupi, tuhuma hizo zinadai kuwa baadhi ya Wahadhiri na Watumishi wa Taasisi hii wanafanya “biashara haramu”  ya kufelisha wanafunzi kwa makusudi sambamba na ubadilishaji wa matokeo ya mitihani, hususan Somo la Mirathi (Probate, Administration of Estates and Trusts).

  Ufafanuzi:

  Tunapenda kuufahamisha Umma kuwa tuhuma hizo si za kweli. Kumbukumbu zetu zinaonyesha kuwa wanafunzi wote waliofanya mitihani wametendewa haki. Wale waliofaulu wamefaulu kihalali na hakuna aliyefelishwa kwa makusudi. Katika utendaji kazi wa Taasisi watumishi wote wanafanya kazi kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo.

  Kwa nafasi hii, tunapenda kueleza juu ya utaratibu wa utayarishaji na utoaji wa matokeo ya mitihani kama ifuatavyo:-

  1.  Baada ya mtihani kusahihishwa na jopo la Wahadhiri wa somo husika (Internal Examiners), majibu ya wanafunzi (answer books) hupelekwa kwa Mtahini wa Nje ya Taasisi (External Examiner) kwa ajili ya uhakiki wa usahihishaji na alama za ufaulu zilizowekwa.

  2.  Baada ya kupokewa kutoka kwa Watahini wa Nje na kuandaliwa, matokeo huwasilishwa katika kikao cha ndani cha Wahadhiri/Watahini wa Ndani (Panel of Internal Examiners) kwa ajili kujadiliwa na kutolewa mapendekezo ya kuwasilishwa katika Kamati ya Mafunzo kwa Vitendo na Mitihani (Practical Legal Training and Examinations Committee).

  3.  Baada ya kupokelewa, kujadiliwa na kupitishwa na Kamati ya Mafunzo kwa Vitendo na Mitihani, Taasisi hutangaza Matokeo ya Awali (Provisional Results) kupitia Tovuti ya Taasisi ambayo inaruhusu mwanafunzi husika kuona matokeo yake baada ya kuingiza nambari yake ya usajili.

  4.  Katika hatua ya mwisho, Matokeo ya Awali huwasilishwa kwenye Bodi ya Uendeshaji wa Taasisi (Governing Board) kwa ajili ya kujadiliwa na kuthibitishwa kuwa matokeo rasmi (Final Results).

  Baada ya matokeo ya awali kutangazwa, mwanafunzi ambaye hajaridhika na matokeo yake ana haki na fursa ya kuomba uhakiki wa matokeo yake (verification) au kukata rufaa (appeal) au vyote kwa pamoja. Uhakiki humwezesha mwanafunzi husika kuthibitisha usahihi wa matokeo yake.

  Hivyo, Taasisi inatoa rai kwa mwanafunzi ye yote ambaye ana shaka na matokeo yake kuwa afuate taratibu zilizoelezwa hapo juu.

  Mwisho, Taasisi inatoa rai kwa wahusika waliotoa taarifa hizo za uzushi kuepuka tabia ya kutoa tuhuma bila ushahidi. Tuhuma zilizotolewa zimeleta usumbufu mkubwa sio tu kwa wahadhiri, wafanyakazi na wanafunzi wa Taasisi bali pia kwa wazazi/walezi wa wanafunzi na wadau wengine katika tasnia ya Sheria.

  IMETOLEWA NA:

  MKUU WA TAASISI TAASISI YA MAFUNZO YA UANASHERIA KWA VITENDO TANZANIA

  (THE LAW SCHOOL OF TANZANIA)

  5 Mei, 2015

  0 0

  Katibu wa Bunge Dkt. Thomas kashililah akisisitiza jambo wakati alipokutana na ujumbe kutoka taasisi inayojishughulisha na masuala ya kibunge ya Parliamentarians for Global Action Ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana. Ujumbe huo upo kwenye ziara yao ya kikazi kutembelea kila Bunge Duniani na kueleza malengo na mipango yao hususani kuangalia namna wanavyoweza kushirikiana na wabunge kutatua baadhi ya masuala yahusuyo haki za Binadamu. Kulia ni Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge Ndg. John Joel, na kushoto ni Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Jossey Mwakasyuka na Msaidizi wa Katibu Ndg. Emmanuel Mpanda.
  Katibu Mtendaji wa taasisi ya Parliamentarians for Global Action yenye makao makuu yake Mjini New York Marekani Dkt. David Donat Cattin akielezea baadhi ya shughuli za taasisi yake alipokutana na Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah (hayupo pichani) Ofisini kwake jana Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Kimataifa la Taasisi hiyo Duniani Mhe. Pindi Chana.
  Katibu Mtendaji wa taasisi ya Parliamentarians for Global Action yenye makao makuu yake Mjini New York Marekani Dkt. David Donat Cattin akielezea baadhi ya shughuli za taasisi yake alipokutana na Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah (hayupo pichani) Ofisini kwake jana Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Kimataifa la Taasisi hiyo Duniani Mhe. Pindi Chana.


  0 0

  Mratibu wa utamaduni wa Ubalozi wa Uswisi Kwame Mchuru akizungumza na wandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa nyimbo mpya leo katika ukumbi wa Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam, kulia ni Mwimbaji wa Bendi ya Mlimani Park Hassani Bichuka.
  Mwimbaji wa Bendi ya Mlimani Park Abdala Hemba akifafanua juuya wimbo mpya ambao umezinduliwa hii leo jijini Dar es Salaam,kulia ni Mpiga gita la bezi wa Bendi ya Mlimani Park Karama Tony na kushoto ni Mwimbaji wa Bendi ya Mlimani Park Hassani Bichuka.
  Baadhi ya vijana wa Bendi ya Mlimani Parkw wakitumbuiza wakati wa uzinduzi wa wimbo mpya katika ukumbi wa habari MAELEZO leo jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhulia katika uzinduzi wa wimbo mpya wa Bendi ya Mlimani Parkleo jijini Dar es Salaam. (PICHA NA EMMANUEL MASSAKA)

  0 0

  +
  Ni stori ambazo tumekua nazo mtaani 
  kwa kipindi kidogo ila mpaka zimefika 
  hapa ujue tumepata kauli sahihi 
  ambayo itasema ukweli.


  Babu Tale (pichani) ni meneja wa Diamond 
  Platnumz, amekutana kwenye hii Exclusive na dstv.com 
  na kukubali kuizungumzia hiyo na ishu nyingine zote.


  Kama wataka muziki ya kukupendeza basi 
  jiburudishe na kipindi ya Official African Chart 
  kila Jumanne saa 21:00 kwenye MTV Base.  0 0


  0 0


  Na Bakari Issa Majeshi
  Mgomo wa Madereva uliodumu  kwa takriban siku moja na ushee, hatimaye umepata muafaka baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul Makonda (pichani) kufanikiwa kuusuluhisha kwa kusaini makubaliano na Uongozi wa Chama cha Madereva.
  Makubaliano hayo yaliitaka Serikali kuboresha  Mikataba kwa Madereva, malipo kwa madereva hao, pamoja na tatizo la ukaguzi wa magari ili kuondoa usumbufu kwa madereva hao, na kuiomba Serikali kufanya ukaguzi huo kwa siku moja tu.
  Akizungumza na Madereva hao, Mhe, Makonda amewataka Madereva hao kuachana na mgomo huo  na kuwaahidi Madereva hao kuyafanyika kazi madai yao katika muda ambao wamekubaliana usiozidi saa 4 asubuhi kesho.

  Aidha, Mhe Makonda amesema katika madai hayo imeundwa Tume ambayo itashughulikia madai hayo pamoja na kuwahakikishia Madereva hao kuwepo na mwakilishi katika Tume hiyo iliyoundwa, ambayo itajadili masuala ya Mkataba, malipo, matibabu pamoja na suala la kusoma kwa Madereva hao.
  Pia Makonda amelitaka Jeshi la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni kuwaachia Madereva ambao tayari walikua wamekamatwa kutokana na kuonekana kufanya fujo katika mgomo huo katika Soko la Urafiki jijini Dar es Salaam. 
  Kwa Upande wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Madereva, Bw. Rashidi Salehe amemuomba Mkuu wa Wilaya kutatua madai ya Madereva hao ili kuondoa mgomo ambao unakwamisha usafirishaji wa abiria.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZA HALI ILIVYOKUWA 

  0 0
 • 05/05/15--08:19: Isha mashauzi apigwa kabali
 • Isha  Mashauzi akipigwa kabali na 93.7 EFM. Bofya mshale mwekundu umsikie mwenyewe anavyojibu mapigo...

  0 0

  Waziri mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya wanawake waliofika kwenye viwanja vya mukendo mjini Musoma kuhudhuria Maadhimisho ya ya siku ya wakunga dunia yaliyofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Mukendo, Musoma Mei 6, 2015.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akishuhudia wakati muuguzi, Naomi Sarali alipompima mapigo ya moyo, Mwajuma Juma ikiwa ni moja ya madhimisho ya siku ya wakunga duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mukendo mjiniMusoma Mei 5, 2015.Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Zilote Stephen.
  Msanii Magesa Julius wakikundi cha sanaa cha Egumba cha mkoani Mara akiongoza kundi hilo kutumbuiza katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wakunga duniani zilizofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Mukendo mjini Musoma, Mei 5, 2015.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakunga waliozawadiwa zawadi mbalimbali kutokana na mchango wao katika kuwahudumia wajawazito wanaojifungua katika meneo mbalimbali nchini. Mheshimiwa Pinda alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wakunga duniani zillizofanyika kitaifa kwenye viwanjavya Mukendo mjini Musoma Mei 5, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Baadhi ya wananchi wakitafuta maeneo ya hifadhi
  Na Abou Shatry wa Swahili Villa

  Familia zisizopungua 200 zimeachwa bila makaazi baada ya makaazi yao kuharibiwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyoikumba manispaa ya mji wa Unguja na vitongoji vyake.
  Akizungumza na Swahilivilla kwa njia ya simu, mkaazi wa Mwanakwerekwe Sokoni, mjini Unguja ndugu Mussa Makame alisema kuwa mvua hizo zilizoendelea kwa muda wa siku mbili mfululizo, zimepelekea maafa makubwa katika miundombinu mjini humo.
  "Hali ya hewa ya Zanzibar kwa siku ya pili leo imekuwa na utata wa hali ya mvua na maafa mengi yametokea", alisema Ndugu Mussa, na kuongeza kuwa kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa za watu wawili kupoteza maisha kutokana na maafa hayo, na kwamba vyombo rasmi vinavyohusika vitatoa taarifa sahihi kuhusu tetesi hizo katika wakati muafaka.
  Aliendelea kusema kuwa wananchi wamekuwa wakishirikiana katika juhudi za kusaidia waathikika wa janga hili, na kwamba serikali imetenga makaazi ya muda katika mashule na kujenga mahema kwa ajili ya kuzihifadhi familia zilizoathirika vibaya. 
  Aliyataja maeneo yaliyoathirika zaidi kuwa ni Mwanankwerekwe, Jang'ombe, Chumbuni na Tomondo. Aliutaja ujenzi holela na miundombinu duni kuwa ni miongoni mwa sababu zilizopelekea watu wengi kuathirika na mafuriko hayo.
  Mbali na athari za kijamii, mvua hizo pia zimekuwa na athari za kiuchumi kwa vile barabara kuu inayounganisha mji wa Zanzibar na Mkoa wa Kusini Unguja zimekuwa hazipitiki. Hali hii imepelekea usumbufu kwa wafanyabiashara kutoka maeneo ya kisiwa cha Unguja kufika katika maeneo ya Mjini ambako ndiko kwenye harakati nyingi za kiuchumi.
  Katika mahojiano hayo na Bwana Abou Shatry wa Swahilivilla, Ndugu Mussa amewataka Wazanzibari kuacha tofauti zao za kisiasa na kuwa kitu kimoja katika kukabiliana na maafa hayo. "Mvua ni kudura ya Mwenyezi Mungu, hakuna wa kulaumiwa, na wale wanaoingiza siasa waache kufanya hivyo", alisema Ndugu Mussa, na kuongeza kwamba tayari kuna watu wameanza kuingiza maslahi binafsi ya kisiasa katika swala hili.
  Mafuriko haya yanakuja wakati Zanzibar ikiwa bado inaendelea kuuguza jeraha la kimbunga kilicholikumba eneo la Kisiwapanza, kisiwani Pemba wiki chache zilizopita.
  Ungana nasi kusikiliza Mahojiano yetu na Ndugu Mussa Makame.

  0 0

  The European Commission is releasing EUR 1.5 million to meet the immediate needs for assistance and protection of Burundi refugees in neighbouring countries. The funding is part of the EUR 47 million of total humanitarian aid foreseen for the Great Lakes region for 2015, and follows the increase in number of refugees from the country in the last weeks.
  "Such sudden and massive displacement is a humanitarian tragedy and a serious challenge to neighbouring countries' capacities to accommodate refugees.  It is a serious concern in an already fragile region"said EU Commissioner for Humanitarian Aid and Crisis Management, Christos Stylianides.
  Rwanda, the Democratic Republic of Congo and Tanzania are experiencing flows of refugees from Burundi, who cite intimidation, threats, or fear of violence as reasons for fleeing. Over 30,000 people, the majority of whom women and children, are estimated to have fled already, with more feared to follow suit. More than 24,700 new refugees were reported by 3 May in Rwanda alone.
  The surge follows last week's clashes in Burundi's capital Bujumbura between police and opposition to President Nkurunziza, after he announced his candidacy for a third term as president at the upcoming elections in June.
  The European Commission is closely monitoring the situation and has expressed its concern at the increasing number of refugees.

  0 0

  The Chairman of the High Level Panel on The Global Response to Health Crisis President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete, The Un Secretary General Ban Ki Moon(Third Left) pose fro a group Photo with other panel members at the UN Headquarters in New York this afternoon. Other panel members in the picture from left are, Marty Natalegawa(Indonesia), Micheline Calmy Rey(Switzeland) fourth left,Celso Amorim from Brazil(second right) and Rajiv Shah(right). On April this year the UN Secretary General Ban Ki Moon appointed a six member High Level panel to make recommendations to strengthen national and international systems to prevent and manage future Health Crises taking into account lessons learnt from the response to the outbreak of Ebola Virus disease.(photo by Freddy Maro)

older | 1 | .... | 826 | 827 | (Page 828) | 829 | 830 | .... | 3278 | newer