Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110129 articles
Browse latest View live

NEWS ALERT: Wakimbizi toka Burundi wamiminika Tanzania kupitia Kigoma

$
0
0
Na Editha Karlo
Waomba hifadhi kutoka nchini Burundi wakiwasili nchini kwa boti hivi  maeneo ya Kibilizi, Mkoani Kigoma. Bado idadi yao haijafahamika kwani bado zoezi la kuwaandikisha linaelea katika eneo hilo. 
Ujio wa waomba hifadhi hawa unakuja kutokana na machafuko yanayoendelea nchini Burundi  ambayo yameshika kasi na kusababisha wananchi kuanza kukimbilia nchini Tanzania.
Burundi ilikumbwa na machafuko katika miaka ya nyuma na baadaye kuwa na amani lakini sasa inaingia katika mgogoro tena baada ya Rais wa sasa Pierre Nkurunzima kutaka kuwania urais kwa muhula mwingine.
Waomba hifadhi kutoka nchini Burundi wakijiandikisha mara baada ya kuwasili nchini Tanzania leo kwa boti.


SEMINA YA USAMBAZAJI WA MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2012 YAFANYIKA MKOANI MOROGORO

$
0
0
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu akitoa maelezo mafupi wakati wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo mjini Morogoro.
Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Hajjat Amina Mrisho Said akitoa maelezo mafupi ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro wakati wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo mjini Morogoro.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt. Rajab Rutengwe akiwahutubia washiriki wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo mjini Morogoro.
Baadhi ya washiriki wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo mjini Morogoro wakifuatilia kwa makini Semina hiyo.

Miradi ya umeme ya REA kutolipiwa fidia

$
0
0
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa sita kutoka kushoto, mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja Mameneja Tanesco wa mikoa na wilaya katika Nyanda za Juu Kusini Magharibi pamoja na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA ya usambazaji umeme vijijini, Awamu ya pili katika kanda hiyo, mara baada ya kumaliza kikao kilicholenga kujadili utekelezaji wa miradi husika. Kulia kwa Naibu Waziri ni Meneja Mwandamizi wa Tanesco Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi, Salome Nkondola na kushoto kwa Naibu Waziri ni Kaimu Meneja wa Tanesco katika mkoa wa Mbeya, Magwila Mbalamwezi.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa nne kutoka kushoto, mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja Mameneja Tanesco wa mikoa na wilaya katika Nyanda za Juu Kusini Magharibi mara baada ya kumaliza kikao kilicholenga kujadili utekelezaji wa miradi ya usambazaji umeme vijijini Awamu ya Pili katika kanda hiyo. Kulia kwa Naibu Waziri ni Meneja Mwandamizi wa Tanesco Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi, Salome Nkondola na kushoto kwa Naibu Waziri ni Kaimu Meneja wa Tanesco katika mkoa wa Mbeya, Magwila Mbalamwezi.

Na Teresia Mhagama, Mbeya

Serikali imesema kuwa haitolipa fidia kwa wananchi wanaopisha miradi ya usambazaji umeme vijijini inayotekelezwa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kwa kushirikiana na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Hayo yamesemwa mjini Mbeya na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage wakati wa kikao chake na mameneja Tanesco wa mikoa na wilaya katika Nyanda za Juu Kusini Magharibi pamoja na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA ya usambazaji umeme vijijini, Awamu ya pili katika kanda hiyo.

Mwijage amesema kuwa serikali imechukua hatua hiyo baada ya kubaini kuwa suala hilo limekuwa likichelewesha utekelezaji wa miradi ya usambazaji umeme vijijini pamoja na kuigharimu serikali fedha nyingi ambazo zinapaswa kutumika katika kuongeza kasi ya usambazaji umeme katika maeneo hayo.

Suala hilo la baadhi ya wananchi vijijini kukwamisha miradi ya umeme kwa kudai fidia lilielezwa pia na baadhi ya wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo vijijini ambapo limepelekea usitishaji wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji umeme katika sehemu zenye mapingamizi.

Naibu Waziri aliwaagiza wakandarasi hao kuhakikisha kuwa wanatoa taarifa kwa wananchi kabla ya kuanza kazi katika maeneo ya wananchi hao ili kujenga uelewa wa pamoja na hivyo kupunguza changamoto za kupinga miradi hiyo ya umeme.

Vilevile Naibu Waziri aliwataka wakandarasi hao kuongeza rasilimali watu katika maeneo waliyopangiwa kusambaza umeme ili miradi hiyo ikamilike mwezi Juni mwaka huu kama ambavyo makubaliano kati ya serikali na wakandarasi hao yanavyoelekeza.

"Ongezeni sub cotractors katika maeneo mnayofanyia kazi na kama mna changamoto yoyote wasilianeni na Wakala wa Nishati Vijijini ili changamoto hizo zitatuliwe na miradi hii ikamilike kwa wakati" alisema Mwijage. Alisema kuwa wakandarasi watakaozembea katika ukamilishaji wa miradi ya umeme, Awamu ya Pili, hawatapata nafasi ya kushindanishwa katika mchakato wa kuwapata wakandarasi watakaopewa kazi ya kusambaza umeme vijijini Awamu ya Tatu.

Vilevile Naibu Waziri amewapongeza wakandarasi wanaoendelea kutekeleza miradi ya usambazaji umeme vijijini licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali na kuwahakikishia kuwa Wizara ya Nishati na Madini inaendelea na jitihada za kuhakikisha kuwa malipo ya wakandarasi hao yanafanyika kwa wakati.

ROBO TATU YA VIFO VITOKANAVYO VYA UZAZI VIMEPUNGUZA

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

MALENGO ya Milenia ya Nne na Tano yamefikiwa kutokana na mkakati wa kupunguza vifo vya Mama na mtoto nchini vinavyotokana na uzazi kwa robo tatu na kuweza kufikia wakina mama 193 kwa vizazi hai 100,000.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid wakati akitangaza kuwepo kwa Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yatafanyika kesho katika viwanja Mkendo mkoani Mara.

Amesema tafiti zilizofanywa katika nchi 72 zimeonyesha kwamba upatikanaji wa huduma mwafaka za ukunga umewezesha kupunguza kiwango cha vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi kwa wastani wa asilimia tatu kwa mwaka kuanzia mwaka 1990, jambo ambalo linaridhisha umuhimu wa wakunga katika kuhakikisha kwamba hakuna mama mjamzito anapoteza maisha kutokana na sababu zinazoweza kuzuilika.

Katika Maadhimisho hayo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi ambapo watu wa maeneo ya karibu wametakiwa kushiriki na kuweka kazi za wakunga katika utoaji wa huduma za uzazi.

Dk. Seif amesema kwa mujibu wa Shirikisho la Vyama Vya Wakunga Duniani,Mkunga akitayarishwa vizuri kwa kufuata viwango vilivyowekwa na kuzingatia mahitaji ya nchi,mkunga huyu anaweza kutoa asilimia 87 ya huduma zote muhimu anazohitaji mama mjamzito na mtoto mchanga.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Wakunga kwa Maendeleo ya Kizazi kijacho" ikiwa inalenga kauli hiyo kutambua umuhimu wa wakunga katika kuokoa maisha ya kina mama na watoto wachanga .

Amesema kuwa kutokana na kutambua umuhimu wa wakunga wameongeza idadi ya vyuo kutoka 3,000 hadi 10,000 ikiwa lengo lake kupunguza vifo vya mama mjamzito na mtoto mchanga.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza maadhimisho ya siku ya wakunga duniani iliyofanyika leo katika ukumbi wa Wizara ya Afya na Ustawi Jamii jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Utawi wa Jamii,Dk.Donnan Mbando akimkaribisha Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dk.Seif Rashid kutangaza Maadhimisho ya Siku ya Wakunga iliyofanyika leo katika ukumbi wa Wizara ya Afya na Ustawi Jamii jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakifatilia taarifa ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dk.Seif Rashid ya Siku ya Wakunga Duniani iliyofanyika leo katika ukumbi wa Wizara ya Afya na Ustawi Jamii jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Emmanuel Massaka).

Taswira ya Ubungo jijini Dar es Salaam leo.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Madereva nchini, Rashid Saleh akizungumza na baadhi ya Madereva wenzake walioingia kwenye mgomo leo, kuishinikiza Serikali kuwatimizia matakwa yao waliyoyaomba kwa kipindi kirefu kilichopita.
Sehemu ya Umati wa Madereva hao ukimsikiliza kiongozi wao, mchana wa leo kwenye Stendi kuu ya Mabasi, Ubungo jijini Dar es salaam.
 Taswira ya kituo cha Simu 2000 Ubungo jijini Dar es Salaam leo baada ya mgomo wa madereva wa mabasi ya abiria.Picha zote na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
 Barabara ya Sam Nujoma eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam leo.
 Licha ya mgomo wa madareva Miundombinu ya maji machafu hakuna katika kituo cha Mabasi Yaendayo mikoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam.
Hakuna kukanyaga maji ni kuruka mawe tuu.
 Mabasi yakiwa yameegeshwa katika Stendi kuu ya Mabasi yaendayo mikoani-Ubungo jijini Dar es Salaam leo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Maalim Seif Sharif achangiwa fedha za kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya urais wa zanzibar wakati utakapofika

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad,akipokea fedha taslim kiasi cha shilingi milioni mbili na laki tano, kutoka kwa Mwenyekiti wa CUF zoni ya Mjini Unguja, Massoud Khamis, ili aweze kuchukua fomu ya kugombea urais wa Zanzibar wakati utakapofika.
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akionyesha fedha alizokabidhiwa kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea urais.
Mwenyekiti wa CUF zoni ya Mjini Unguja, Massoud Khamis, akimkabidhi Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, cheti cha heshima kutokana na uongozi wake.
Baadhi ya viongozi na wanachama wa CUF waliojitokeza katika hafla ya kumkabidhi fedha Maalim Seif iliyofanyika nyumbani kwake Mbweni. (Picha na Salmin Said, OMKR)

ADAM MZEE NA LILIAN WAMEREMETA

$
0
0
 Marafiki wakiwa katika picha ya pamoja na maharusi,waliosimama kutoka kushoto ni,Merry Geofrey,Sheila Simba,Hafidh Kido ,John Bukuku,Suleiman Mwenda,Micky, Said Mwishehe,Sharifa,Neema Mwangomo,Abdala Kiluke,Mringi Petro ,katika Harusi ya Adam Mzee iliyofanyika katika Ukumbi wa Kivukoni,Serena Hotel.

Adam Mzee ni mtumishi wa Chama Cha Mapinduzi Makao Makuu ,Idara ya Itikadi na Uenezi,na ni mmiliki wa  blog maarufu ya Kamerayangu na Lilian ni mtumishi wa NMB Makao Makuu.
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi,Ndugu Abdurahman Kinana wa pili kulia,na Katibu wa Nec,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wa tatu kutoka kushoto,wakiwa na Mr & Mrs Mzee.
 Maharusi wakituzwa na Ndugu na marafiki wakati wakutoa zawadi.
 Maharusi wakiwa na wapambe wao,katika picha ya pamoja na wanakamati walipoenda kutoa zawadi na kuwapogeza maharusi.
Mr & Mrs.Adam Mzee

MGOMO WA MADEREVA UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Chama cha Madereva Tanzania (CHAMAMATA),Rashid Salehe akizungumza na madereva (hawapo pichani) katika Kituo kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani Ubungo jijini Dar es Salaam, kuhusiana na mgomo wa mabasi yaendayo mikoani.
Makamu Mwenyekiti wa chama cha Madereva Tanzania (CHAMAMATA),akizungumza na Madereva wa mabasi yanayosafirisha abiri (hawapo hewani),waliogoma kusafirisha abiri kwa madai yao ya Mikataba ya kazi pamoja na Ajira za kudumu.
  Madereva wakiwa wameshika mabango katika mgomo wa Madereva leo katika Kituo kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani-Ubungo jijini Dar es Salaam.
Usalama nao haukuwa mbali na mikusanyiko ya  Madereva katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam. 
 Abiria wakisubiri usafiri wowote katika kituo cha mawasiliano-Ubungo jijini Dar es Salaam leo.
 Mabasi ya mikoani yakiwa yameegeshwa katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani-Ubungo jijini Dar es Salaam.
(Picha zote na Avila Kakingo,Globu ya Jamii)

NEWS ALERT: BALOZI MULAMULA ATEULIWA KUWA KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, BALOZI SIMBA NAIBU WAKE

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Balozi Liberata Rutageruka Mulamula (kulia) kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. 

Kwa sasa Balozi Mulamula ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico.


Rais Kikwete pia amemteua Balozi Hassan Simba Yahya (chini) kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo  ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.  


Kwa sasa Balozi Yahya ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Wizarani hapo.



Uteuzi huu umeanza tarehe 2 Mei, 2015


Imetolewa na;
Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu - Dar es Salaam.
4 Mei, 2015

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, asikitishwa na mtindo wa “Tegesha” unaofanywa na wananchi eneo la kuzunguka mgodi wa North Mara

$
0
0
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, akizungumza na mama huyu mkazi wa kijiji cha Nyakunguru, kilicho jirani na eeno la mgodi wa North Mara, huko Nyamongo wilayani Tarime mkoa wa Mara, wakati alipofanya ziara ya kutembelea maeneo yanayozunguka mgodi huo Jumatatu Mei 5, 2015 ili kufahamu jitihada za mgodi kuendeleza miradi ya kijamii na changamoto ambazo Jamii na Mgodi zinapata kutokana na shughuli za uchimbaji.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, (Wapili kushoto), akizungumza jambo wakati alipotembelea eneo la ujenzi wa nyumba moja kwa mtindo unaoitwa na wakazi wa Nyamongo “Tegesha”, mita chache kutoka uzio wa mgodi wa North Mara, ili kufahamu jitihada za mgodi kuendeleza miradi ya kijamii na changamoto ambazo Jamii na Mgodi zinapata kutokana na shughuli za uchimbaji. Naibu waziri amesikitishwa na mtindo huo ambapo wananchi hususan wanotoka nje ya eneo la Nyamongo, hujenga majengo haraka haraka eneo la kuzunguka mgodi huo kwa matarajio ya kujipatia malipo makubwa ya fidia kinyume na tathmini iliyofanywa awali.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, (kushoto), akisalimiana na Meneja Uendelezaji wa kampuni ya Acacia, Asa Mwaipopo, wakati alipofika kwenye kijiji cha Nyakunguru, kilicho jirani na mgodi wa North Mara, Mara ulioko Nyamongo, wilayani Tarime mkoa wa Mara Jumatatu Mei 4, 2015, ili kufahamu jitihada za mgodi kuendeleza miradi ya kijamii na changamoto ambazo Jamii na Mgodi zinapata kutokana na shughuli za uchimbaji  Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga,(Watatu kulia), Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi huo, Jimmy Ijumba, (Wapili kulia) na Mkuu wa Mahusiano ya Serikali wa kampuni ya Acacia, Alex Lugendo.
 Meneja Uendelezaji wa Mgodi wa dhahabu wa North Mara, Abel Yiga, (kushoto), akimpatia maelezo Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga wakati waziri huyo alipotembelea maeneo yanayozunguka mgodi huo ili kufahamu jitihada za mgodi kuendeleza miradi ya kijamii na changamoto ambazo Jamii na Mgodi zinapata kutokana na shughuli za uchimbaji. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga, (Watatu kulia), na kaimu kiongozi wa kitengo cha mahusiano ya kijamii ya mgodi wa North Mara, Zakayo Kalebo. (kushoto)
 Meneja Unedelezaji wa Kampuni ya Acacia, inayomiliki migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara, Asa Mwaipopo, (katikati), akimpatia maelezo Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, (kushoto), wakati wa ziara yake ya kutembelea mgodi wa North Mara ili kufahamu jitihada za mgodi kuendeleza miradi ya kijamii na changamoto ambazo Jamii na Mgodi zinapata kutokana na shughuli za uchimbaji. Kulia ni Mkuu wa Mahusiano ya Serikali wa kampuni ya Acacia, Alex Lugendo
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, (kushoto), akisalimiana na Meneja Uendelezaji wa kampuni ya Acacia, Asa Mwaipopo, wakati alipofika kwenye kijiji cha Nyakunguru, kilicho jirani na mgodi wa North Mara, Mara ulioko Nyamongo, wilayani Tarime mkoa wa Mara Jumatatu Mei 4, 2015, ili kufahamu jitihada za mgodi kuendeleza miradi ya kijamii na changamoto ambazo Jamii na Mgodi zinapata kutokana na shughuli za uchimbaji  Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga,(Watatu kulia), Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi huo, Jimmy Ijumba, (Wapili kulia) na Mkuu wa Mahusiano ya Serikali wa kampuni ya Acacia, Alex Lugendo.

Introducing Dkt Panjuan wa 93.7 EFM katika SPORTS HEAD QUARTERS

News Alert: membe akutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi jijini Dar es salaam leo

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Mhe. Laurent Kavakure jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro. 
Mhe. Kavakure aliwasili nchini tarehe 03 Mei 2015. Wakati huo huo, Mhe. Membe ataongoza ujumbe wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenda Burundi siku ya Jumatano tarehe 06 Mei 2015 kufanya mazungumzo na Serikali ya Burundi kuhusu hali ya kisiasa inayoendelea nchini humo.
Imetolewa na: Wizara ya Mambo ya Nje na 
Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es Salaam 
04 Mei 2015

Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akiwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Mhe. Laurent Kavakure jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro.


Ujumbe wa Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Kimataifa, wakifuatilia mazungumzo hayo kabla ya kupata chakula cha mchana kilichoandaliwa na Waziri Membe kwa heshima ya


mgeni wake.

BREAKING NYUZZZZZ.....: MOTO WATEKETEZA JENGO MOJA MTAA WA LIVINGSTONE NA NARUNG'OMBE, KARIAKOO HIVI SASA

$
0
0
Moto mkubwa ukiendelea kuteketeza moja ya jengo lililopo kwenye makutano ya Mtaa wa LivingStone na Narung'ombe, Kariakoo jijini Dar es salaam muda huu. Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika mpaka sasa.


Globu ya Jamii inafuatilia tukio hilo taarifa kamili na video ya tukio itawajia baadae kidogo.

MGOMO WA MABASI,,,,ABIRIA MJINI MOSHI WAKWAMA STENDI, WAIGEUZA UKUMBI WA SINEMA...

$
0
0
Hivi ndivyo kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi kilivyoonekana.
Baadhi ya abiria wakiwa wamekaa kitako katika maegesho ya magari huku wakitizama Big Screen iliyopo jirani na kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi.
Baadhi ya abiria wakitizama kwa mbali screen hiyo.
Screen kubwa kwa ajili ya matangazo ya biashara iliyoko jirani na kituo kikuu cha mabasi ikionesha picha ya mashindano ya magari ambayo ilikuwa burudani kwa abiria baada ya kukosa usafiri kutokana na mgomo wa madereva uliotikisa nchi nzima.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


introducing Tanzania's first online magazine Rozzie


3D cctv camera zinapatikana Dar es salam

$
0
0
3D cctv camera hizi Tuna-supply na ku-install hizo camera ambazo ni unique. Anayehitaji piga namba hizo chini 
- Uliza Bernard


News alert:mvua za masika zasababisha maafa, uharibifu wa nyumba na miundombinu leo

$
0
0
Michuzi Blog inatoa pole kwa wote waliofikwa na mafa na wote waliopoteza ama kuharibikiwa na mali zao na nyumba. Tunawaombea Mungu awape moyo wa Subira na nguvu kukabiliana na majanga haya - Ameen.
Na Abdulla Ali wa Maelezo, Zanzibar                                        

Mvua za masika zinazoendelea kunyesha Visiwani Zanzibar zimesababisha hasara kubwa ikiwemo upotevu mali na mifugo, uharibifu wa miundombinu pamoja na kusababisha vifo vya watu. 
Hadi sasa watu wawili  ambao ni Nd. Juma Hamad (25) mkaazi wa Mwanakwerekwe na mtoto mmoja  mkaazi wa Kinuni anaekisiwa kuwa na miaka 8 wamepoteza maisha. Wote wawili ni kutoka Wilaya ya Magharibi Unguja.
Hayo yamweelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud Mohamed wakati akitoa taarifa kwa wananchi kuhusiana na athari za mvua hizo katika ukumbi wa  Karume House, Mjini Zanzibar.

Amesema mvua hizo zimesababisha mafuriko katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mjini Magharibi na kupelekea athari kubwa katika maeneo hayo ikiwemo vifo vya watu, uharibifu wa nyumba za makaazi na upotevu wa mali na mifugo.

Aidha Waziri Aboud amesema kuwa maiti ya mtoto imeshapatikana na kuzikwa jana Tarehe 3/5/2015 na maiti ya Nd. Juma Hamad bado haijapatikana na juhudi za kumtafuta zinaendelea.

Amefahamisha kuwa maeneo yaliyoathirika zaidi na mvua hizo ni pamoja na Magomeni, Jang’ombe, Nyerere, Sebleni, Sogea, Mwanakwerekwe, Welezo, Kisauni, Tomondo, Mombasa, Kinuni, Mtopepo, Chumbuni, Kwahani, Mpendae, Bububu na Kwaalinato, ambapo maeneo yote hayo yanapatikana ndani ya Mkoa wa Mijini Magharibi.

Ametanabahisha kuwa, kwa vile mvua bado zinaendelea kunyesha ni vyema wananchi wakachukua tahadhari ili kujiepusha na athari zaidi zinazoweza kujitokeza, ikiwemo wazazi kuangalia watoto wao na kuhakikisha hawachezi karibu na maeneo yanayotuama maji, kwa wale wanaoishi mabondeni ni vyema wakahama sehemu hizo.

Waziri Aboud pia amewataka wananchi waliochimba mashimo katika maeneo ya makaazi wawe waangalifu kwa kuyafunika haraka iwezekanavyo , kuchemsha maji wanayoyatumia, kuhifadhi chakula ili kuepukana na maradhi ya miripuko pamoja na kufuata kanuni za afya ikiwemo usafi binafsi na maeneo yanayowazunguka.

Vilevile amewataka wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu kwani Serikali itaendelea kushirikiana nao ili kuhakikisha kuwa hali ya maisha kwa wananchi hao inarudi kama kawaida pamoja na kuwapa pole wale wote waliopoteza jamaa na mali zao.



IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.


Maji ya mvua yenye kasi yakitapakaa kila eneo la Zanzibar
Wananchi wakihangaika kwenye mafuriko kutokana na mvua 
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar nako kumefurika. Picha zaidi BOFYA HAPA

INTRODUCING DR. PANJUA INTERVIEWS VIA SPORTS HEAD QUARTERS 93.7 EFM

$
0
0
Globu ya Jamii kwa kushirikiana na EFM 93.7 kuanzia leo itakuletea baadhi ya vipindi ama mada motomoto zinazoifanya stesheni hiyo ya redio inayokuja juu kwa kasi izidi kuchana anga nchini Tanzania na nje ya nchi kupitia mtandaoni. Kukuonjesha tu leo tunakuandalia mahojiano ya mtangazaji hodari wa Sports Headquaters Dkt. Panjuan wakati akihojiana na wadau mbalimbali wa michezo.
BOFYA MSHALE MWEKUNDU TUANZE KAZI...

video ya moto ulivyoteketeza nyumba kariakoo jijini Dar es salaam

Video ya mgomo wa madereva wa mabasi ya abiria jijini Dar es salaam

Viewing all 110129 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>